Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,658
- 4,866
Inasikitisha sana Nchi kama Tanzania inakuwa kikwazo cha ndoto za vijana wengi walioamua kuwa wagunduzi, wabunifu na waboreshaji wa vitu mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya Taifa. Kwenye majukwaa ya kisiasa, mitandao, kwenye TV na Radio. Utasikia serikali inasema tunainua vijana walio wabunifu, sijui tunawasaidia na maneno ya kuvutia rukuki, ila kiuhalisia hao hao watu wa serikali ndio wanawakwamisha hawa vijana na kuua ndoto zao.
Juzi kati kipindi cha radio Power Breakfast cha Clouds FM walienda Dodoma ambapo walimfanyia mahojiano kijana wa kitanzania ambaye kitaaluma yeye ni Engineer wa mazingira (Environmental Engineer).
Kijana huyu aliweza kubuni mtambo mdogo wa uzalishaji Petrol, Dizeli, Home Cooking Gas, Kerosene nakadharika kwa kutumia takataka za plastiki. Yani plastiki zinachomwa na kisha kugeuzwa kuwa Petroli hii ya kuendeshea magari, ambayo leo hii tunaangalia nayo kuwa imepanda bei.
Cha kushangaza ni namna ambavyo kijana huyu aliamua kwenda kwenye ofisi za Serikali hapo Dodoma kuomba hile milioni 50 kama mkopo wa vijana ili aendeleze project yake hiyo na azalishe petroli, dizeli, gas, na Kerosene ya kutosha kwa ajili ya matumizi ya taifa lake. Lakini alivyofika kwenye hizo ofisi akakatishwa tamaa na afisa wa serikali kuwa ni bora aachane na hiyo project, ajikite kwenye Kilimo. Yani aachane na uzalishaji wa Petrol na product zingine zinazoambatana na petrol aamie kwenye Kilimo ambacho kila mtu anafanya. Sasa kwa hiyo taifa zima tuwe walimaji?. Lakini kuna afisa mwingine aliyekuwa pembeni akisikiliza akatoka na kumwambia kuwa kijana hiyo project ni nzuri na usiiiche hata kama umekosa pesa jitahidi ukomae nayo, usikatishwe tamaa. Kijana akatoka hapo akarudi nyumbani.
Leo hii nchi kama China inapiga hatua ya maendeleo kwa kuwekeza nguvu kwa vijana wabunifu. Ndio maana bidhaa nyingi hasa za kiteknolojia nyingi zinatoka China. Ukisikiliza mahojiano ya huyo kijana anasema moja kwa moja kuwa China inatengeneza Petrol kwa kutumia mfumo huu ambao yeye pia ameugundua. China ni mnunuzi mkubwa wa Takataka za plastiki Duniani kote kwa ajili ya kubuni na kutengeneza vitu mbalimbali ikiwemo petrol hizi tunazolia nazo leo zimepanda Bei.
Alafu wanakuja watumishi wa serikali wanakwambia achana nayo, nenda ukalime. Sasa serikali yetu inataka kila mtu afanye kazi ya Siasa na Kilimo. Yani wote tuwe wafuasi wa vyama vya siasa na wakulima. Mwisho wa siku hawa vijana ndio wanarundikana kwenye Siasa na mashambani, huku Taifa likishindwa kuzalisha kina Elon Musk wapya.
Masoud Kipanya anaonekana kuonyesha nia ya kutaka kumsaidia kijana huyu, kwa sababu Masoud Kipanya naye ni mbunifu wa magari ya umeme, naye amewahi kukwamishwa sana na watu kwenye project yake ya magari ya umeme. Kwa sababu anayajua machungu, ameamua kuonyesha nia ya kumsaidia kijana huyu ili ndoto isonge.
Tizama maelezo kwenye video hii hapo chini, unaweza kusogeza mbele kuepusha matangazo ya kipindi.
View: https://www.youtube.com/live/6Iyn83XI7lw?si=WcHfkyUD1GvFS21K