Manumba: Polisi lipizeni kisasi

Mbona aliuawa Prof. Mwaikusa na hadi leo hakuna mtu aliekamatwa na hatujasikia kesi yeyote....kwani Barlow ni kiongozi wa kwanza kupigwa risasi? Je Prof. nae sio kiongozi? Au angekuwa muuza mitumba je polisi wangehaha ki hivyo? Kila anaekufa alizaliwa na wazazi wake na uchungu ni huohuo bila kujali cheo cha mtu. Hivyo wangekuwa wanatoa kauli hizo tangu mwanzo. Je filamu ya Kova juu ya Dr. Ulimboka nayo imeishia wapi?
 
Kwa kauli hii ya Manumba sasa nimeshaamini kumbe Polisi wote nchini ni STD 7!
 
Halafu ukitaka kujua binadamu wanamkashifu Mungu, kwenye ibada ya mazishi ya huyu marehemu mtasikia eti Sisi tulimpenda sana lakini Mungu alimpenda zaidi! Yaani utembee na mali za watu uuwawe halafu eti Mungu alimpenda sana???:frusty:
 
Kwa kauli hii ya Manumba sasa nimeshaamini kumbe Polisi wote nchini ni STD 7!
Kama IGP mtarajiwa hii ndio ilikuwa CV yake hapo unategemea nini? Jeshi la Polisi ndio kichaka cha unskilled people.

Wasifu wa Barlow

Marehemu Barlow alizaliwa Desemba 26, 1959 mkoani Kilimanjaro na kusoma katika Shule ya Msingi Lombeta Moshi Vijijini na kuhitimu mwaka 1974.Mwaka 1979 alimaliza elimu ya sekondari katika Shule ya Seminari Maua na mwaka 1981 alijiunga na Shule ya Sekondari Mirambo, Tabora katika mchepuo wa Lugha.

Mwaka 1982 aliajiriwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Iringa na mwaka huohuo alijiunga na Chuo cha Polisi Moshi kusoma sheria ya uhamiaji. Baada ya kuhitimu, mwaka 1984 aliajiriwa katika Idara ya Uhamiaji na kupelekwa katika ofisi zake za Mkoa wa Mtwara.

1984 alitunukiwa shahada ya kwanza ya utawala mafunzo, Chuo cha Polisi Dar es Salaam na baadaye kupata mafunzo ya ukaguzi mnamo mwaka 1987.
 
Mimi nimesikitishwa na kushangaa kwa kauli hiyo lakini nilipokumbuka kauli ya mtoto wa mkulima kwamba liwalo na liwe halafu yaliyomkuta Dr Uli mshangao ukatoweka ghafla,nikajisemea moyoni ni Style ya Uongozi Dhaifu katika serikali dhaifu!
 
Katka kile ambacho hata mm ckutarajia kukisikia kutoka kiongozi mkubwa kama Manumba n kauli yake ya jana wakati wa kukumuaga marehem Barlow kua watalipiza kisasi kwa yeyote aliyehusika!....

kama police wataanza kujichukulia sheria mkonon tena kwa kutanganza hadhari kuua raia n dhahiri kua hatuna viongoz wala sheria hazifuatwi tena hapa TZ
mpaka sasa hakuna hata mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa kwa mauaji hayo!kwa hilo tu usalama wa Taifa hawana cha kufanya ila kulinda watu na kufanya umbeya tu chondechonde oneni aibu jamani!
 
mpaka sasa hakuna hata mtuhumiwa mmoja aliyekamatwa kwa mauaji hayo!kwa hilo tu usalama wa Taifa hawana cha kufanya ila kulinda watu na kufanya umbeya tu chondechonde oneni aibu jamani!
Wacha kuropoka wewe, Usalama wa Taifa si kazi yao kukamata watuhumiwa na wala hawahusiki kwa lolote kwenye kupeleleza kifo hiki. siku nyingine kama hujui majukumu ya Usalama wa Taifa ni bora uulize ili uambiwe.
 
kumbuka hata amri jeshi mkuu katoa kauli kama hiyo pia

Sijapata taarifa ya amri jeshi mkuu kusema hayo kutokana na eneo nilipo kwa sasa kama kweli kasema maneno ambayo ni chuki za pandikizi zidi ya jamii na mapolice wa kibongo tuandike tumekwisha lasha basi umma tuamue kuendelea watawala,viongozi na watendaji wa aina hii au dep peace revolution kwa manufaa yetu kiuchumi, na ustawi wa maendeleo.maamuzi ni ya umma
 
Siku zote ukiwa unaangalia mbele huwezi kuona wa nyuma yako wao ndo wanasituka kuona RPC anauwawa wakati sisi tulishapiga kelele polisi kuuwawananchi na dunia inajuwa .
 
mimi mwenyewe sikutegemea kauli kama aliyoto manumba na hii inathibitisha ya kuwa watu wanapewa uongozi bila kuzingatia uwezo wa wahusika na hii inasababishwa na dhana ya kufahamu nani na walasiyo unafahamu nini
 
Ukweli hatuna viongozi wala watendaji bali tuna kundi la wendawazimu wanaojua kuropoka kila wanapoona hadhira.

Kauli kama hizo katika tukio hili zimetolewa pia na Lukuvi, Nchimbi, Rubani.

Nchi yetu sasa ni ya visasi na sio kufuata sheria tena!!

Kwa akili yeke ndogo (MANUMBA) anafikiri kuwa wananchi nao hawawezi kumlipizia naye kisasi. Basi atangaze vita RASMI kati ya POLICCM na RAIA tuone nani atashindwa
 
MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba amewataka Polisi kuhakikisha wanalipa kisasi dhidi ya mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow (53).

Akitoa salamu za polisi, wakati wa ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Barlow, DCI Manumba alisema polisi wamefundishwa kuwa watulivu wakati wa hatari, lakini kwa kifo cha kamanda huyo
“wanatakiwa kulipiza kisasi” kwa kuwakamata waliohusika.

MSISOME KICHWA CHA HABARI TU NA KUANZA KUTOA MANENO SOMA HABARI YOOTE NA KUIELEWA,
 
Ukweli hatuna viongozi wala watendaji bali tuna kundi la wendawazimu wanaojua kuropoka kila wanapoona hadhira.

Kauli kama hizo katika tukio hili zimetolewa pia na Lukuvi, Nchimbi, Rubani.

Nchi yetu sasa ni ya visasi na sio kufuata sheria tena!!

Kwa akili yake ndogo (MANUMBA) anafikiri kuwa wananchi nao hawawezi kumlipizia naye kisasi. Basi atangaze vita RASMI kati ya POLICCM na RAIA tuone nani atashindwa
 
Watalipiza! Hii kauli sio nzuri! kazi ya polisi ni kulinda raia sio kuwaua! chondechonde Manumba msitumie vitu vizito kwa hao watuhumiwa wa mauaji.

kwa kauli hii siana shaka kabisa kwamba Manumba has taken leave of his faculties, lol!

Lakini kama Waziri mkuu aliwahi kutamka "auwaye auwawe" kuhusu wauaji wa alibino kisha akatamka "liwalo na liwe" wakati wa mgomo wa madaktari unategemea nini! si ni wazi sasa kwamba nchi ya Kambarage imekwenda alijojo!!

It is total impunity, total disregard of the rule of law ambayo wanapenda sana kuishadidia lakini hawajui namna ya kuishamirisha na kuistawisha, God save our country.
 
MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba amewataka Polisi kuhakikisha wanalipa kisasi dhidi ya mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow (53).

Akitoa salamu za polisi, wakati wa ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Barlow, DCI Manumba alisema polisi wamefundishwa kuwa watulivu wakati wa hatari, lakini kwa kifo cha kamanda huyo
"wanatakiwa kulipiza kisasi" kwa kuwakamata waliohusika.

MSISOME KICHWA CHA HABARI TU NA KUANZA KUTOA MANENO SOMA HABARI YOOTE NA KUIELEWA,

Hata wewe umesoma mstari mmoja tu huo lol; usijinasibu kwamba ni wewe tu uliyeielewa kauli hiyo kuliko mtu mwingine yoyote!!
When the title of a topic is repugnant no amount of explanation is enough to put it right! the two will remain at variance.
Linganisha kauli za Lukuvi na Ndulile na hiyo ya Manumba uone tofauti! Ujumbe ni ule ule lakini kauli za Ndulile na Lukuvi zimezingatia maudhui ya utawala wa sheria na nguzo muhimu ya kazi za jeshi la polisi; KULINDA MAISHA NA MALI ZA RAIA. Sasa kamanda wa polisi akianza kutoa blanket statements kama kulipiza kisasi raia wa kawaida watakuwa confused na kuogopa, afterall sio kila mtu alikuwapo nyamagana kumsikia live na kuchambua alichomaanisha kumbuka watu wana uwezo tofauti sana katika kuchambua mambo, sio vizuri kiongozi kutii jazba zake, Kiongozi lazima awe makini sana na kauli zake sio kupiga kabla hajalenga. Do not shoot first and take aim later Nops, its vice versa.
 
hili jeshi lina laana aiseee..yaani wanapanuapanua tu midomo bila kujielewa
 
Watatuua lakini wao pia tutawaua,jeshi lenyewe dhaifu linazidiwa na sungusungu,kamanda wa polisi eti wa mkoa mwenye dhamana ya ulinzi na usalama mkoa mzima anauawa kizembe namna hii,hakuna cha kisasa wala nini wataua lakini watauawa
kamanda anshindwa hata kunusa hatari,cheo chote hicho hakuhisi dalili yeyote maamuma wanapeana vyeo kimaamumamaamuma.
 
Hata wewe umesoma mstari mmoja tu huo lol; usijinasibu kwamba ni wewe tu uliyeielewa kauli hiyo kuliko mtu mwingine yoyote!!
When the title of a topic is repugnant no amount of explanation is enough to put it right! the two will remain at variance.
Linganisha kauli za Lukuvi na Ndulile na hiyo ya Manumba uone tofauti! Ujumbe ni ule ule lakini kauli za Ndulile na Lukuvi zimezingatia maudhui ya utawala wa sheria na nguzo muhimu ya kazi za jeshi la polisi; KULINDA MAISHA NA MALI ZA RAIA. Sasa kamanda wa polisi akianza kutoa blanket statements kama kulipiza kisasi raia wa kawaida watakuwa confused na kuogopa, afterall sio kila mtu alikuwapo nyamagana kumsikia live na kuchambua alichomaanisha kumbuka watu wana uwezo tofauti sana katika kuchambua mambo, sio vizuri kiongozi kutii jazba zake, Kiongozi lazima awe makini sana na kauli zake sio kupiga kabla hajalenga. Do not shoot first and take aim later Nops, its vice versa.
neno kulipiza kisasi ni zito sana kaka,ila akili fupi haziwezi kung'amua
 
kulipa kisasi sio kwamba na wao waue, jaribu kuelewa maana yake, alitaka kuhakikisha kwamba wanafanya jitihada kulipa kwa kufanikisha kuwakama waliohusika na mauaji hayo, sioni kibaya zaidi ya kukuza tu kwa hiyo heading na kuielewa hivo, lakini sio mbaya wakilipa kisasi hasa kwa hao walioua.
 
Back
Top Bottom