Manumba: Polisi lipizeni kisasi

Ckutegemea kuisikia kauli hiyo hapo jana..kwa kauli iyo wameshindwa tu kuisingizia chadema.MANUMBA NA Luku_vi Wanafikiri kwa kutumia UKOPE.
 
Watalipiza! Hii kauli sio nzuri! kazi ya polisi ni kulinda raia sio kuwaua! chondechonde Manumba msitumie vitu vizito kwa hao watuhumiwa wa mauaji.
Chukueni hatua acheni kutoa mapovu coz kaishasema tayari. Akilipiza tu na sisi tunalipiza tena..!
 
ni hatari sana. nilidhani muandishi wa Mwananchi amekurupuka, kumbe ni kweli DCI katamka yale maneno.

ametumia kauli ya 'kulipiza kisasi kwa kuwakamata', lakini Barlow hakukamatwa.

Barlow aliuliwa, na kama mtu mkubwa kama yeye anatumia kauli ya 'kulipiza kisasi', kisasi pekee kwa ajili ya Barlow ni mauwaji, so tujiandae kwa mauwaji, maana polisi hufanya kazi kwa amri, na bosi wao katoa amri.

Mkuu mbaya Zaidi huyo kamanda kafa kwa mazingira machafu ya Uzinzi, viongozi wa dini nao wanafiki sana mnaendesha ibadaa kwa mzinzi live? its sad
 
Na waliomuua kamanda leo hii wakijitokeza hadharani na kusema hawakukusudia kumuua bali ni hisia tu za hasira kuona kamanda ukichukua mzigo wao na wao pia tuwaachie?

Mkuu Concrete, Uchungu na hasira huondoa busara...Wakikamatwa watapelekwa mbele ya pilato nafikiri ndo yalitakiwa kutamkwa na huyo jamaa.
 
Kwa maana hiyo, watuhumiwa wakikamatwa hawatapewa muda wa kujitetea, tutaambiwa walikua wakirushiana risasi, na wote 20 wameuawa, hakuna askari aliyejeruhiwa.
 
tumeisikia wengi kumbe iyo kauli,hata kama mtu anashtakiwa kwa mauaji si sheria ndio inafata mkondo?au kwa hili la rpc halina kufata sheria kwamba wakishikwa tu ni "kulipiza kisasi",nazidi kuamini polisi wa tanzania ni wauaji na wakiukaji haki/sheria namabari one....

awa ndio polisi,tunasubiria ilo la ICC
 
Manumba hivi hajui kwamba anaowataka walipize kisasi tunaishi nao huku uswazi maana hata nyumba hawajawajengea waanze tuone
 
Manumba: Polisi lipizeni kisasi


Monday, 15 October 2012 20:47
ASEMA WALIOMUUA KAMANDA BARLOW LAZIMA WAKAMATWE, KUAGWA DAR LEO


Sheilla Sezzy, Mwanza
MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba amewataka Polisi kuhakikisha wanalipa kisasi dhidi ya mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow (53).
Akitoa salamu za polisi, wakati wa ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Barlow, DCI Manumba alisema polisi wamefundishwa kuwa watulivu wakati wa hatari, lakini kwa kifo cha kamanda huyo “wanatakiwa kulipiza kisasi” kwa kuwakamata waliohusika.

“Wakati wa hatari, askari tunafundishwa kutulia, ninawashukuru askari mlitulia, lakini katika hili ninawataka kuhakikisha mnalipa kisasi kwa waliohusika, kwa kuwakamata wote walioshiriki mauaji haya,” alisema Manumba.
Mwili kwa Kamanda Barlow aliyeuawa na watu wasiojulikana usiku wa Oktoba 13, mwaka huu, uliagwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi katika ibada iliyofanyika katika Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.

Ibada hiyo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo na viongozi mbalimbali, wakiwamo makamanda wa polisi wa mikoa ya Tabora, Shinyanga, Geita, Mara, Kagera na Simiyu.DCI Manumba alisema ulipizaji huo wa kisasi lazima ulenge kuwakamata washiriki wa matukio mengine ya mauaji kama yale ya albino pamoja na wazee vikongwe kwa sababu za imani za kishirikina.

Kuhusu upelelezi wa tukio hilo, Manumba alisema ushirikiano walioupata kutoka kwa wananchi umefanikisha kazi hiyo kufikia hatua nzuri kwani tayari wamewabaini baadhi ya watuhumiwa.“Taarifa mlizotupa zimetusaidia na muda si mrefu tutakuwa tumemaliza kazi na wale wote waliotusaidia watakuwa wadau wetu,” alisema DCI Manumba na kuongeza:

“Tabia mbovu za kutekeleza mauaji kwa kujichukulia hatua mikononi, yakiwamo yale ya vikongwe na albino bila ya kujali uwepo wa Mahakama ni changamoto, Watanzania wanatakiwa kutafakari wapi wanalipeleka taifa hili.”
Alisema Jeshi la Polisi limejipanga kukabiliana na uhalifu wa namna hiyo kwa sababu wahalifu hawana dini wala kabila na kuwataka wananchi kuimarisha ulinzi shirikishi kutokana na uchache wa askari katika jeshi hilo.

Ibada ya kuaga
Ibada ya kuaga mwili wa kamanda huyo iliongozwa na Padri Raymond Manyanga wa Parokia ya Nyakahoja.
Akizungumza katika ibada hiyo, Waziri Lukuvi aliwataka wananchi wa Mwanza kuwa na imani na Serikali yao akisema ipo kwa ajili ya kuwalinda pamoja na mali zao.

Lukuvi alisema kuuawa kwa Barlow hakuwezi kusababisha kuvurugika kwa amani katika mkoa huo kwa kuwa Serikali ipo makini kulinda usalama wa nchi.

Katika salamu zake za Mkoa wa Mwanza, Ndikilo alisema katika kipindi hiki, polisi hawataweka silaha chini na watasonga mbele mpaka hapo ushindi wa kuwakamata wauaji utakapopatikana.Alisema vyombo vya usalama vimepanga kuhakikisha vinawawajibisha wahusika wa mauaji hayo ambayo aliyaita ya kinyama.

Alisema mkoa umepata pigo kwa kuwa Kamanda Barlow alikuwa mtu mwenye ushirikiano akimsifia kwa ushirikiano wake wa kuhakikisha Mkoa wa Mwanza unakuwa salama.

“Tangu Kamanda Barlow alipoteuliwa kuja katika mkoa huu, amefanya kazi nzuri ya kuhakikisha usalama wa Wana - Mwanza pamoja na mali zao na kukomesha mauaji ya albino, vikongwe pamoja na ujambazi wa majini na barabarani,” alisema Ndikilo.

Padri Manyanga alimwombea msamaha marehemu kwa wale wote ambao aliwakosea na kuwataka wamwombee ili apumzike kwa amani.

Alisema hategemei katika kazi aliyokuwa akifanya marehemu asiwe na maadui kwa sababu yeye ni binadamu kama walivyo wengine... “Marehemu alijitahidi kuwatumikia Watanzania kwa kuhakikisha kuwa haki inatendeka. Kama alikuwa na upungufu, basi alikuwa kama watu wengine ila kwa uwezo wake Mungu alimjalia kufanya kazi yake. Maisha ya mwanadamu ni zawadi kutoka kwa Mungu, hakuna mtu ambaye ana haki ya kutoa uhai wa mtu yeyote.”

Salaam za Kikwete
Rais Jakaya Kikwete ameliagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha linachukua hatua za lazima kuwakamata na kuwafikisha mbele ya sheria watu wote wanaotuhumiwa kupanga na kutekeleza mauaji ya Kamanda Barlow.Katika salamu za rambirambi alizompelekea Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Saidi Mwema, Rais Kikwete amesema ameshtushwa na kuhuzunishwa na mauaji hayo.

“Nimepokea kwa mshtuko mkubwa na huzuni nyingi taarifa za kifo cha ACP Barlow kilichotokea usiku wa Ijumaa katika jiji la Mwanza ambako watu wasiojulikana walimpiga risasi na kumuua ofisa huyo mwandamizi wa Jeshi letu la Polisi,” alisema na kuongeza:

“Historia ya ACP Barlow ni ya mfano katika utumishi wa umma na hususan katika Jeshi la Polisi. Kwa hakika, Jeshi la Polisi limempoteza kamanda hodari na wananchi wa Tanzania, hususan wale wa Mkoa wa Mwanza, wamempoteza mlinzi shupavu wa usalama wao na mali zao.”

Mwili wa Barlow uliwasili Dar es Salaam jana na leo utaagwa nyumbani kwake Ukonga kuanzia saa 6:00 mchana kabla ya kupelekwa katika Kanisa Katoliki Majumba Sita kwa ajili ya misa na watu mbalimbali kutoa heshima zao za mwisho.

Wasifu wa Barlow
Marehemu Barlow alizaliwa Desemba 26, 1959 mkoani Kilimanjaro na kusoma katika Shule ya Msingi Lombeta Moshi Vijijini na kuhitimu mwaka 1974.Mwaka 1979 alimaliza elimu ya sekondari katika Shule ya Seminari Maua na mwaka 1981 alijiunga na Shule ya Sekondari Mirambo, Tabora katika mchepuo wa Lugha.

Mwaka 1982 aliajiriwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Iringa na mwaka huohuo alijiunga na Chuo cha Polisi Moshi kusoma sheria ya uhamiaji. Baada ya kuhitimu, mwaka 1984 aliajiriwa katika Idara ya Uhamiaji na kupelekwa katika ofisi zake za Mkoa wa Mtwara.

1984 alitunukiwa shahada ya kwanza ya utawala mafunzo, Chuo cha Polisi Dar es Salaam na baadaye kupata mafunzo ya ukaguzi mnamo mwaka 1987.

Mwaka huohuo wa 1987 alihamishiwa Polisi na kuanza kazi katika makao makuu ya Idara ya Upelelezi.
Katika uhai wake, aliwahi kufanya kazi katika Wilaya ya Musoma, Mkoa wa Kigoma kabla ya kupandishwa cheo na kuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi na kufanya kazi ya kuongoza jeshi hilo katika mikoa ya Mara na Tabora kabla ya kuhamishiwa Mwanza.

Gazeti la Mwananchi:ONLINE
 
Nawachukia mapolisi wote! Nawauwawe tu, hawana maana kwetu. Sasa hapo at least watafeel mke wa mwangosi alichofeel, hivi kwa nini haikuwa kamuhanda??
 
Nilisikiliza hiyo taarifa.
Nitakusahihisha kidogo mtoa mada. Manumba alisema watalipiza kisasi kwa kuhakikisha wale wote waliohusika kumuua kamanda wanakamatwa na kuchukuliwa hatua stahili.
 
mkuki kwa ngurue kwa binadamu mchungu wakati mwangosi anauawa hapakuwa na ulipaji kisasi kwa nini hapa idaiwe kisasi kitalipwa? noooooo sio utawala bora huo
 
Kama ni kweli alisema...basi hisia zilitawa zaidi ya akili yake baada ya kumwona kamanda mwenzake akiwa amelala milele kwa kupigwa risasi za shingo.

Ni Kweli alitamka hayo maneno kwamba watalipiza kisasi lkn baadae aliona amechemka akasema iwe raia,askari mdogo au ofisa etc Manumba Futa kauli yako utalipiza kisasi kivipi? Angalia usije ukaingia na wewe mtegoni mwa unaotaka kuwalipizia visasi maana mnajuana nyinyi na mnajua ukweli kuhusu kifo cha barlow(Rejea alivyotamka siku moja kabla ya kifo chake alipokua anaelezea mtego alioingia ofisa uhamiaji)
 
Nilisikiliza hiyo taarifa.
Nitakusahihisha kidogo mtoa mada. Manumba alisema watalipiza kisasi kwa kuhakikisha wale wote waliohusika kumuua kamanda wanakamatwa na kuchukuliwa hatua stahili.

Haaaaaa Call a spade a spade and not a big spoon................Kuwakamata watuhumiwa ndio kulipiza kisasi? lol
 
nimekasilishwa na kauli hii ya kiongozi mkubwa wa jeshi la police kama manumba ni hatari sana katika ustahimili wa taifa letu. kauli hii ni mbovu na ni ukosefu wa maadili.
 
Nadhani amekua hajiandai vyema kwa anachokusudia kuzungumza na MEDIA na hafikirii Impact ya maneno anayotamka na nafasi yake ktk jamii
 
nimekasilishwa na kauli hii ya kiongozi mkubwa wa jeshi la police kama manumba ni hatari sana katika ustahimili wa taifa letu. kauli hii ni mbovu na ni ukosefu wa maadili.

kumbuka hata amri jeshi mkuu katoa kauli kama hiyo pia
 
Kauli sahihi ilikuwa "tutawasaka wahalifu waliohusika na mauaji ya kama Barlow hadi wote wakamatwe na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria". Ili la kulipa kisasa, inabidi sasa wananchi wema tuingie ndani saa 12 jioni maana inaelekea polisi wataanza zoezi la kulenga shabaha raia wema kwa kisingizio la kuhisi ni jambazi.
 
Hakujua ukali wa maneno aliyoyaongea kwenye nchi inayopaswa kuongozwa kwa kufuata sheria. Msameheni bure huyo jamaa ingawa inawezekana alimaanisha aliyosema.
 
Back
Top Bottom