Manumba: Polisi lipizeni kisasi

raymg

JF-Expert Member
Jun 30, 2012
842
214
Katka kile ambacho hata mm ckutarajia kukisikia kutoka kiongozi mkubwa kama Manumba n kauli yake ya jana wakati wa kukumuaga marehem Barlow kua watalipiza kisasi kwa yeyote aliyehusika!....

kama police wataanza kujichukulia sheria mkonon tena kwa kutanganza hadhari kuua raia n dhahiri kua hatuna viongoz wala sheria hazifuatwi tena hapa TZ
MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba amewataka Polisi kuhakikisha wanalipa kisasi dhidi ya mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow (53).

Akitoa salamu za polisi, wakati wa ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Barlow, DCI Manumba alisema polisi wamefundishwa kuwa watulivu wakati wa hatari, lakini kwa kifo cha kamanda huyo "wanatakiwa kulipiza kisasi" kwa kuwakamata waliohusika.

"Wakati wa hatari, askari tunafundishwa kutulia, ninawashukuru askari mlitulia, lakini katika hili ninawataka kuhakikisha mnalipa kisasi kwa waliohusika, kwa kuwakamata wote walioshiriki mauaji haya," alisema Manumba.

Mwili kwa Kamanda Barlow aliyeuawa na watu wasiojulikana usiku wa Oktoba 13, mwaka huu, uliagwa na maelfu ya wakazi wa Mwanza wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi katika ibada iliyofanyika katika Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.

Ibada hiyo pia ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo na viongozi mbalimbali, wakiwamo makamanda wa polisi wa mikoa ya Tabora, Shinyanga, Geita, Mara, Kagera na Simiyu.DCI Manumba alisema ulipizaji huo wa kisasi lazima ulenge kuwakamata washiriki wa matukio mengine ya mauaji kama yale ya albino pamoja na wazee vikongwe kwa sababu za imani za kishirikina.

Kuhusu upelelezi wa tukio hilo, Manumba alisema ushirikiano walioupata kutoka kwa wananchi umefanikisha kazi hiyo kufikia hatua nzuri kwani tayari wamewabaini baadhi ya watuhumiwa."Taarifa mlizotupa zimetusaidia na muda si mrefu tutakuwa tumemaliza kazi na wale wote waliotusaidia watakuwa wadau wetu," alisema DCI Manumba na kuongeza:

"Tabia mbovu za kutekeleza mauaji kwa kujichukulia hatua mikononi, yakiwamo yale ya vikongwe na albino bila ya kujali uwepo wa Mahakama ni changamoto, Watanzania wanatakiwa kutafakari wapi wanalipeleka taifa hili."

Alisema Jeshi la Polisi limejipanga kukabiliana na uhalifu wa namna hiyo kwa sababu wahalifu hawana dini wala kabila na kuwataka wananchi kuimarisha ulinzi shirikishi kutokana na uchache wa askari katika jeshi hilo.

Ibada ya kuaga
Ibada ya kuaga mwili wa kamanda huyo iliongozwa na Padri Raymond Manyanga wa Parokia ya Nyakahoja.

Akizungumza katika ibada hiyo, Waziri Lukuvi aliwataka wananchi wa Mwanza kuwa na imani na Serikali yao akisema ipo kwa ajili ya kuwalinda pamoja na mali zao.

Lukuvi alisema kuuawa kwa Barlow hakuwezi kusababisha kuvurugika kwa amani katika mkoa huo kwa kuwa Serikali ipo makini kulinda usalama wa nchi.

Katika salamu zake za Mkoa wa Mwanza, Ndikilo alisema katika kipindi hiki, polisi hawataweka silaha chini na watasonga mbele mpaka hapo ushindi wa kuwakamata wauaji utakapopatikana. Alisema vyombo vya usalama vimepanga kuhakikisha vinawawajibisha wahusika wa mauaji hayo ambayo aliyaita ya kinyama.

Alisema mkoa umepata pigo kwa kuwa Kamanda Barlow alikuwa mtu mwenye ushirikiano akimsifia kwa ushirikiano wake wa kuhakikisha Mkoa wa Mwanza unakuwa salama.

"Tangu Kamanda Barlow alipoteuliwa kuja katika mkoa huu, amefanya kazi nzuri ya kuhakikisha usalama wa Wana - Mwanza pamoja na mali zao na kukomesha mauaji ya albino, vikongwe pamoja na ujambazi wa majini na barabarani," alisema Ndikilo.

Padri Manyanga alimwombea msamaha marehemu kwa wale wote ambao aliwakosea na kuwataka wamwombee ili apumzike kwa amani.

Alisema hategemei katika kazi aliyokuwa akifanya marehemu asiwe na maadui kwa sababu yeye ni binadamu kama walivyo wengine... "Marehemu alijitahidi kuwatumikia Watanzania kwa kuhakikisha kuwa haki inatendeka. Kama alikuwa na upungufu, basi alikuwa kama watu wengine ila kwa uwezo wake Mungu alimjalia kufanya kazi yake. Maisha ya mwanadamu ni zawadi kutoka kwa Mungu, hakuna mtu ambaye ana haki ya kutoa uhai wa mtu yeyote."

Salaam za Kikwete
Rais Jakaya Kikwete ameliagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha linachukua hatua za lazima kuwakamata na kuwafikisha mbele ya sheria watu wote wanaotuhumiwa kupanga na kutekeleza mauaji ya Kamanda Barlow.

Katika salamu za rambirambi alizompelekea Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Saidi Mwema, Rais Kikwete amesema ameshtushwa na kuhuzunishwa na mauaji hayo.

"Nimepokea kwa mshtuko mkubwa na huzuni nyingi taarifa za kifo cha ACP Barlow kilichotokea usiku wa Ijumaa katika jiji la Mwanza ambako watu wasiojulikana walimpiga risasi na kumuua ofisa huyo mwandamizi wa Jeshi letu la Polisi," alisema na kuongeza:

"Historia ya ACP Barlow ni ya mfano katika utumishi wa umma na hususan katika Jeshi la Polisi. Kwa hakika, Jeshi la Polisi limempoteza kamanda hodari na wananchi wa Tanzania, hususan wale wa Mkoa wa Mwanza, wamempoteza mlinzi shupavu wa usalama wao na mali zao."

Mwili wa Barlow uliwasili Dar es Salaam jana na leo utaagwa nyumbani kwake Ukonga kuanzia saa 6:00 mchana kabla ya kupelekwa katika Kanisa Katoliki Majumba Sita kwa ajili ya misa na watu mbalimbali kutoa heshima zao za mwisho.

Wasifu wa Barlow
Marehemu Barlow alizaliwa Desemba 26, 1959 mkoani Kilimanjaro na kusoma katika Shule ya Msingi Lombeta Moshi Vijijini na kuhitimu mwaka 1974.Mwaka 1979 alimaliza elimu ya sekondari katika Shule ya Seminari Maua na mwaka 1981 alijiunga na Shule ya Sekondari Mirambo, Tabora katika mchepuo wa Lugha.

Mwaka 1982 aliajiriwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Iringa na mwaka huohuo alijiunga na Chuo cha Polisi Moshi kusoma sheria ya uhamiaji. Baada ya kuhitimu, mwaka 1984 aliajiriwa katika Idara ya Uhamiaji na kupelekwa katika ofisi zake za Mkoa wa Mtwara.

1984 alitunukiwa shahada ya kwanza ya utawala mafunzo, Chuo cha Polisi Dar es Salaam na baadaye kupata mafunzo ya ukaguzi mnamo mwaka 1987.

Mwaka huohuo wa 1987 alihamishiwa Polisi na kuanza kazi katika makao makuu ya Idara ya Upelelezi.

Katika uhai wake, aliwahi kufanya kazi katika Wilaya ya Musoma, Mkoa wa Kigoma kabla ya kupandishwa cheo na kuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi na kufanya kazi ya kuongoza jeshi hilo katika mikoa ya Mara na Tabora kabla ya kuhamishiwa Mwanza.


Chanzo: Mwananchi
 
Ukweli hatuna viongozi wala watendaji bali tuna kundi la wendawazimu wanaojua kuropoka kila wanapoona hadhira.

Kauli kama hizo katika tukio hili zimetolewa pia na Lukuvi, Nchimbi, Rubani.

Nchi yetu sasa ni ya visasi na sio kufuata sheria tena!!
 
Katka kile ambacho hata mm ckutarajia kukisikia kutoka kiongozi mkubwa kama Manumba n kauli yake ya jana wakati wa kukumuaga marehem Barlow kua watalipiza kisasi kwa yeyote aliyehusika!....

kama police wataanza kujichukulia sheria mkonon tena kwa kutanganza hadhari kuua raia n dhahiri kua hatuna viongoz wala sheria hazifuatwi tena hapa TZ
```````````````wewe Kalaghabaho hukujua kuwa Nchi ilishakuwa pori kama somalia! Jilinde ndugu. Usije ukafikiri kuna walinzi wala serikali. Ukiweza kujitetea kipigo cha polisi jitetee kwa nguvu zote!!
 
Wametuua vya kutosha hawa polisi,yaliyotokea kwa barlow ni sauti ya wananchi kuchoshwa na ukatili wa jeshi la polisi,na kibaya zaidi wanatetea serikali ambayo hata wao wenyewe haiwajali,haiji akilini msiba mkubwa kama huu umetokea rais ndo kwanza anaondoka kwenda kupanda farasi oman,hili ni funzo kwa mapolisi kuwa wanayemtetea hana habari nao,endeleeni kujikomba mtapukutika mmoja mmoja mpaka mtakwisha,wananchi wameshaamua
 
Kwa kaul hii nawaomba wa TZ popote walipo hata kama sio Mwanza wajipange kwan kuna kila dariri za police kuua raia ili kulipiza
 
Duh, anatakiwa kukanusha haraka kauli hiyo, ila naona hata Mh. Raisi katoa tamkoooo, hivi Iringa na Arumeru alisema chochote? jamani mtu kuwa CDM, CUF bado ni watanzania!
 
binafsi nimeiskia hii kauli kwenye mapitio ya magazeti. Hapa ofsini imebidi tuijadili manake kiongozi kukiri kwamba watalipa kisasi inamaana wanatuthibitishia kwamba wako tayari hata kama ni kwakuvunja sheria. na hapa kama ndio wasimamizi wa amani na wanasema wanalipa kisasi basi hakuna amani tena hapa
 
Katka kile ambacho hata mm ckutarajia kukisikia kutoka kiongozi mkubwa kama Manumba n kauli yake ya jana wakati wa kukumuaga marehem Barlow kua watalipiza kisasi kwa yeyote aliyehusika!....

kama police wataanza kujichukulia sheria mkonon tena kwa kutanganza hadhari kuua raia n dhahiri kua hatuna viongoz wala sheria hazifuatwi tena hapa TZ

Kama ni kweli alisema...basi hisia zilitawa zaidi ya akili yake baada ya kumwona kamanda mwenzake akiwa amelala milele kwa kupigwa risasi za shingo.
 
```````````````wewe Kalaghabaho hukujua kuwa Nchi ilishakuwa pori kama somalia! Jilinde ndugu. Usije ukafikiri kuna walinzi wala serikali. Ukiweza kujitetea kipigo cha polisi jitetee kwa nguvu zote!!

hapa n kila raia kulitambua hilo
 
Me mwenyew jana nilipockia nilishangaa sana, sasa kama wao wanataka kulipiza kisasi sasa na huyu aliyekuwa anachukuliwa mke wake nae alipize kisasi kwa kwenda kula mzigo wa marehemu rpc? Hebu tuacha uvivu wa kufikir inachosha sana kuwa na nchi yenye ubovu kama huu'kwaiyo wao hili swala liliwauma sana mbona kwa mwangosi hawakulipiza kisasi??

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Watalipiza! Hii kauli sio nzuri! kazi ya polisi ni kulinda raia sio kuwaua! chondechonde Manumba msitumie vitu vizito kwa hao watuhumiwa wa mauaji.
Kuna uwezekano mkubwa sana wahusika halisi wasipatikane kabisa, ila raia wengine wasio na hatia watakamatwa na kuuwawa ili ku-sympathy situation.
Omba Mungu atakaye kamatwa usiwe wewe, ndugu yako, rafiki yako au jirani yako.
 
... ni kauli dhaifu (kulipa kisasi) kuwahi kutolewa hadharani na kiongozi wa ngazi ya juu kama Mzee Manumba na mwenye dhamana ya kuhakikisha usalama kwa raia wote mpaka mahakama kuweza kuwatia hatiani.

Ndio,
na hii vile vile ni ishara tosha ya ule usemi wa
'MWIZI ANAPOKAZANA KUMSAIDIA MWENYE MALI KUTAFUTA KILE ALICHOKIPORA MWENYEWE tena hata kujitia mwenye huzuni na uchungu mkali kuliko hata wafiwa wenyewe.
 
Watatuua lakini wao pia tutawaua,jeshi lenyewe dhaifu linazidiwa na sungusungu,kamanda wa polisi eti wa mkoa mwenye dhamana ya ulinzi na usalama mkoa mzima anauawa kizembe namna hii,hakuna cha kisasa wala nini wataua lakini watauawa
 
Kama ni kweli alisema...basi hisia zilitawa zaidi ya akili yake baada ya kumwona kamanda mwenzake akiwa amelala milele kwa kupigwa risasi za shingo.

hii n kaul yake mwenyew na amekaririwa hadi kwenye TV's na baadhi ya magazeti ya leo
 
Katka kile ambacho hata mm ckutarajia kukisikia kutoka kiongozi mkubwa kama Manumba n kauli yake ya jana wakati wa kukumuaga marehem Barlow kua watalipiza kisasi kwa yeyote aliyehusika!....

kama police wataanza kujichukulia sheria mkonon tena kwa kutanganza hadhari kuua raia n dhahiri kua hatuna viongoz wala sheria hazifuatwi tena hapa TZ


ni hatari sana. nilidhani muandishi wa Mwananchi amekurupuka, kumbe ni kweli DCI katamka yale maneno.

ametumia kauli ya 'kulipiza kisasi kwa kuwakamata', lakini Barlow hakukamatwa.

Barlow aliuliwa, na kama mtu mkubwa kama yeye anatumia kauli ya 'kulipiza kisasi', kisasi pekee kwa ajili ya Barlow ni mauwaji, so tujiandae kwa mauwaji, maana polisi hufanya kazi kwa amri, na bosi wao katoa amri.
 
Kama ni kweli alisema...basi hisia zilitawa zaidi ya akili yake baada ya kumwona kamanda mwenzake akiwa amelala milele kwa kupigwa risasi za shingo.
Na waliomuua kamanda leo hii wakijitokeza hadharani na kusema hawakukusudia kumuua bali ni hisia tu za hasira kuona kamanda ukichukua mzigo wao na wao pia tuwaachie?
 
Ni kweli jana aliropoka hivyo...watalipiza kisasi, so nasie tunamwambia tutalipiza kisasi, atakapolipiza kisasi nadhani aliongozwa na falsafa ya "dawa ya moto ni moto" its simple nasi tuta-i-apply.
 
labda walishajiandaa kuingiza nchi kwenye machafuko so kilichobaki ni utekelezaji wa hio mipango yao kama anavyotaka kutuaminisha manumba kwa kutoa siri zao za ndani
 
Back
Top Bottom