Mick one john
New Member
- Oct 16, 2012
- 3
- 0
Manumba anatakiwa kutulia katika uchunguzi wake hasitake kulopoka bila uchunguzi
Katika hali halisi, Manumba amethibitisha kuwa Jeshi la Polisi ni la kulipiza visasi. Hata kifo cha Mwangosi kilitokana na yeye kumuuliza kamanda Kamuhanda, amfafanulie tofauti ya Internal meeting na Inside meeting, kutokana na kukerwa na swali hilo, ndiyo sababu iliyomfanya yeye Kamuhanda kusimamia ile 'OPERESHENI UA MWANGOSI' na kwa hali halisi, ile operesheni ilkuwa na baraka ya uongozi wote wa juu wa Polisi na Ikulu yenyewe,ushahidi wa wazi opo, ni kutokana na kuwa, pamoja na ripoti ya Jaji Manento kutamka waziwazi kuwa watuhumiwa 2 wakubwa wa mauaji ya Mwangosi ni Kamuhanda na Tendwa, kutokana na maagizo yao yaliyokiuka sheria za nchi, lakini hatujasikia yeyote kati yao kujiuzuru wadhifa wake, wala hatujasikia mkuu wa nchi aliyewateua, kuwawajibisha, badala yake tumemsikia mkuu wa nchi naye akisisitiza wauaji wa RPC wasakwe kwa nguvu zote, wakati wa mauaji ya Mwangosi, hakuwahi kutoa kauli yoyote. Kama Polisi wameamua kulipiza kisasi kwa kuwaua watuhumiwa wote wa Barlow, tutawashangaa sana, kwani wakubwa wengi wa Polisi wamesoma sheria, na wanaijua principle muhimu ya natural justice, inayosema kuwa 'man can not be a judge on his own case' kwa hiyo ni dhahiri wanachotakiwa kufanya ni kuwapeleka mahakamani na kuwasomea mashtaka, ili mahakama ndiyo iamue kama wana hatia au laa. Wakianzisha mfumo alioutangaza kamanda Manumba kuwa watalipiza kisasi kwa kuwarushia vitu vizito watuhumiwa wa mauaji ya kamanda Barlow, wanakaribisha jungle law nchini mwetu, ambayo tafsiri yake, nchi haitatawalika, kwa maana kila mtu atakuwa anachukuwa sheria mkononi mwake!!Me mwenyew jana nilipockia nilishangaa sana, sasa kama wao wanataka kulipiza kisasi sasa na huyu aliyekuwa anachukuliwa mke wake nae alipize kisasi kwa kwenda kula mzigo wa marehemu rpc? Hebu tuacha uvivu wa kufikir inachosha sana kuwa na nchi yenye ubovu kama huu'kwaiyo wao hili swala liliwauma sana mbona kwa mwangosi hawakulipiza kisasi??
Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
Na Gwaride la mazishi km hawatapiga mizinga basi risasi kibao, RPC wetu alikuwa mtu mzuri sana na alikuwa akimsindikiza Dada yake bahati mbaya ikamkuta.Halafu ukitaka kujua binadamu wanamkashifu Mungu, kwenye ibada ya mazishi ya huyu marehemu mtasikia eti Sisi tulimpenda sana lakini Mungu alimpenda zaidi! Yaani utembee na mali za watu uuwawe halafu eti Mungu alimpenda sana???:frusty:
Manumba katoa kauli hiyo kwa sababu anatambua RPC kauwawa katika tukio la kulipiza kisasi na sio uambazi. Polisi wana silaha kemkem na mabomu kama walivyomlipua Mwangosi, lakini ukimkuta polisi yuko peke yake ni mwoga kama mbwa koko na ndipo hapo fursa inapatikana ya kisasi. Hata yeye Manumba akipita kwenye anga za majita hatoki.......
Katka kile ambacho hata mm ckutarajia kukisikia kutoka kiongozi mkubwa kama Manumba n kauli yake ya jana wakati wa kukumuaga marehem Barlow kua watalipiza kisasi kwa yeyote aliyehusika!....
kama police wataanza kujichukulia sheria mkonon tena kwa kutanganza hadhari kuua raia n dhahiri kua hatuna viongoz wala sheria hazifuatwi tena hapa TZ
Watatuua lakini wao pia tutawaua,jeshi lenyewe dhaifu linazidiwa na sungusungu,kamanda wa polisi eti wa mkoa mwenye dhamana ya ulinzi na usalama mkoa mzima anauawa kizembe namna hii,hakuna cha kisasa wala nini wataua lakini watauawa
kwani ni lini manumba aliwahi kuwa na akili?