KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,136
NAKUOMBA UFUATILIE KWA MAKINI KAULI ZA ZITO HAPA CHINI UTAELEWA VIZURI. TUWE MAKINI NA VYOMBO VYA HABARI AMBAVYO VINACHUKUA MANENO NUSU NUSU KWA INTEREST ZAO. NIMEPENDA GAZETI LA MWANANCHI, LIMEANDIKA MANENO YA ZITO KWA UPANA WAKE: FUATILIA... NUKUU HAPA CHINI
"CCM imewahi kudai CUF ni chama cha Waislamu, na sasa wanasema Chadema ni chama cha Wakristo, sasa wao CCM ni chama cha wapagani au cha watu gani?" Alihoji Zitto.
"Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola," alisema Zitto.
"Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndio msimamo wangu.
"Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi."
"Ndugu zangu naomba mnielewe, Chadema si chama cha ukabila, ukanda wala udini bali ni chama cha kitaifa. Hizo ni propaganda za wapinzani wetu," alisema Zitto baada ya kuulizwa na mmoja wa washiriki kuhusu tuhuma za chama hicho kuwa cha Kikanda.
aliongeza kusema KUNA WATU WANAJIFANYA WAO NI CHADEMA ZAIDI YAKE WAKATI YEYE ANA MIAKA 16 CDM