ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,060
- 49,744
View: https://www.instagram.com/p/C4IKzMCq3zK/?igsh=MWJuYmhjOGptYWk4Mw==
Uongozi ni kuachiana Kijiti. Hivyo ndivyo amefanya bwana Zitto Kabwe baada ya kung'atuka nafasi ya Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Ili damu changa na Mpya zishike hatamu.
Zitto anaachia ngazi ikiwa amekijenga chama hicho kujikita kwenye hoja na mambo ya msingi(issues) badala ya kile Chama Kingine Cha Matukio na kisicho na ajaenda yaani Chadema.
Chadema imekuwa chama Cha Matukio na upepo Kwa sababu ya kuwa na Kiongozi Sultani bwana Mbowe ambae kimsingi hana jipya, kiasi kwamba kadiri anavyozeeka ndivyo na chadema kinazeeka 😁😁
Alichosema Zitto akiwa katika kipindi cha Power Breakfast, Clouds FM
"Na sasa hivi Zitto Kabwe anatoka kwenye uongozi na chama kinapaswa kuendelea kuwepo. Sisi tunajitahidi kutengeneza taasisi ambayo ni zaidi ya mtu mmoja. Sasa inawezekana kwamba vyama vingine wao hawaoni kama ni jambo ambalo lina manufaa kwao. Kwahiyo ni vigumu sana Mimi Kiongozi wa Chama kingine kutoa maoni kuhusiana na taratibu za vyama vingine na ukitaka hayo maoni inabidi uwaite na uwaulize wao" Zitto Kabwe, aliyekuwa Kiongozi ACT WAZALENDO
My Take
Hongera bwana Zitto kwa Kufuata misingi ya Baba wa Taifa.
ACT imeonesha Uongozi kwenye mambo mengi hasa kwenye uchambuzi wa kiuchumi na jambo la Bima ya Afya, kule mna hoja za msingi sana Serikali ifuate ushauri wao.
View: https://twitter.com/MwanzoTvPlus/status/1764739794402189370?t=lnKeyQud0ZKG-xFneHxuSQ&s=19