ACT Wazalendo wanaamini wanaweza kushirikiana na CCM kumwondoa Mbowe Madarakani? Mbowe anaathiri vipi kustawi kwa vyama hivi shikizi?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Viongozi wa ACT walikuwa wana Chadema hapo awali. Wakaandaa njama za kuivuruga Chadema mwisho wa siku wakakamatwa na kufukuzwa uanachama. Zito na Kitila wakafika kwa msajili chini ya wana CCM na kusajili chama chao.

Wakatafuta wafuasi wakakosa na hivyo Kitila akaamua rasmi kurejea CCM kisha akasaidiwa kubebwa akapewa Ubunge. Zitto katika uchaguzi wa 2020 akiamini JPM atamwonea huruma, ikalazimu naye achinjiwe baharini na hivyo kupelekea kufa kwa ndoto yake ya chama kikubwa cha upinzani.

Zitto akashiriki kuiua CUF akishirikiana na Lipumba. Maalimu Seif akavutwa ACT na bado chama kikosa nguvu Zanzibar kama ilivyokuwa awali. Akajaribu kukieneza chama akashindwa na sasa amekaa pembeni kinadharia ila kwenye kiti kivitendo kama ambavyo wenyeviti wa CCM mara zote wamekuwa wakikaa pembeni lakini wakiwa na kura ya veto katika maamuzi ya chama.

Pamoja na ACT kupewa uhuru mkubwa bado wao wanaamini Mbowe ndiye anayewazuia wao kuua upinzani Tanzania. Kila wanachofanya chadema act wazalendo wanapinga na kukosoa kwa line ile ile inayotumiwa na CcM. Tunajiuliza Mbowe aliowakosea nini? Wanaamini wakiungana na CcM wanaweza kuiua chadema? Wananufaikaje? Kwanini zito asiombe nafasi ya uwaziri ale pensheni atulie kama anatamani kukaa meza ya watawala?
 
Kumtoa Freeman siyo kirahisi hivyo
Mzee Mbowe ansaidiwa na aina ya siasa anazoziendesha na ndio maana misukle ya ufipa inaona ni viguma sana, sababu ni kama ifuatavyo;

1. Amefanikiwa sana kupachika ukabila kwenye hiki chama

2. Amekosa mtu wa kumrithisha kufuatiala alietaka kumrithisha kuonekana ni kituko mbele ya jamii kwa siasa zake za kuropoka (Lema)

3. Mwanae James ndio anasubiriwa kuchukua usukani baada ya miaka kumi ijayo
 
Viongozi wa ACT walikuwa wana Chadema hapo awali. Wakaandaa njama za kuivuruga Chadema mwisho wa siku wakakamatwa na kufukuzwa uanachama. Zito na Kitila wakafika kwa msajili chini ya wana CCM na kusajili chama chao.

Wakatafuta wafuasi wakakosa na hivyo Kitila akaamua rasmi kurejea CCM kisha akasaidiwa kubebwa akapewa Ubunge. Zitto katika uchaguzi wa 2020 akiamini JPM atamwonea huruma, ikalazimu naye achinjiwe baharini na hivyo kupelekea kufa kwa ndoto yake ya chama kikubwa cha upinzani.

Zitto akashiriki kuiua CUF akishirikiana na Lipumba. Maalimu Seif akavutwa ACT na bado chama kikosa nguvu Zanzibar kama ilivyokuwa awali. Akajaribu kukieneza chama akashindwa na sasa amekaa pembeni kinadharia ila kwenye kiti kivitendo kama ambavyo wenyeviti wa CCM mara zote wamekuwa wakikaa pembeni lakini wakiwa na kura ya veto katika maamuzi ya chama.

Pamoja na ACT kupewa uhuru mkubwa bado wao wanaamini Mbowe ndiye anayewazuia wao kuua upinzani Tanzania. Kila wanachofanya chadema act wazalendo wanapinga na kukosoa kwa line ile ile inayotumiwa na CcM. Tunajiuliza Mbowe aliowakosea nini? Wanaamini wakiungana na CcM wanaweza kuiua chadema? Wananufaikaje? Kwanini zito asiombe nafasi ya uwaziri ale pensheni atulie kama anatamani kukaa meza ya watawala?
Wazito Makabwela bwana,full matitizo😅😅😅
 
Lakini na nyie chadema ina maana kiongozi ni mbowe tu? Ebu kuweni serious kidogo basi miaka yote hakuna mwenye uwezo kumzidi yeye? Sasa hiyo democracy au ufalme?
Wanashangaza saana ,hivi wamesahau kuwa mzee mbowe alipataga kura laki name alivyogombea uraisi wa nchii hii? Na aliweza kupata kura elfu tano tu toka kwa mikoa mingine dhidi ya Kilimanjaro na Arusha?
 
Sijui wana matatzo gani. Kwamba hakuna mtu mwingine anayefaa wanaamini ni yeye tu? Mfano sasa hivi anaratibu maandamano. Haya maandamano chama kinanufaikaje?
 
Mzee Mbowe ansaidiwa na aina ya siasa anazoziendesha na ndio maana misukle ya ufipa inaona ni viguma sana ,sababu ni kama ifuatavyo;
1.Amefanikiwa sana kupachika ukabila kwenye hiki chama ,
2: Amekosa mtu wa kumrithisha kufuatiala alietaka kumrithisha kuonekana ni kituko mbele ya jamii kwa siasa zake za kuropoka (Lema)
3: Mwanae James ndio anasubiriwa kuchukua usukani baada ya miaka kumi ijayo .
Inaelekea wewe hujui Siasa za Tanzania

CCM haitakubali Mbowe aondoke Chadema na Tundu Antipas Lisu na John Heche wakabidhiwe Uongozi
 
Kwenye hotuba yake ya kuaga Zitto ametumia muda mrefu kurejea alivyofukuzwa Chadema na kuwaita waliomfukuza kuwa ni watu waliomuogopa.
Kwa yakini kama Zitto na Kitila wangefanikiwa Leo Chadema ingekuwa hoi kama TLP na UDP
 
Ni kwa vipi chadema itakufa endapo Mbowe atang'atuka uenyekiti? Kwann chadema isisimame imara kwa kutegemea mifumo imara iliyojiwekea?

Na kama kweli chadema imesimama kwasbb ya Mbowe, basi tutarajie kuona inatoweka mara tu Mbowe anapotwaliwa .
 
Sijui wana matatzo gani. Kwamba hakuna mtu mwingine anayefaa wanaamini ni yeye tu? Mfano sasa hivi anaratibu maandamano. Haya maandamano chama kinanufaikaje?
Wanakusanya hela mkuu ,umesahahu kuwa huwa msukule wa maandamano huwa wanaambiwaga wachangie harakati🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
Inaelekea wewe hujui Siasa za Tanzania

CCM haitakubali Mbowe aondoke Chadema na Tundu Antipas Lisu na John Heche wakabidhiwe Uongozi
mzee mbowe alishasema hao wawili hawana hela ya kuendesha chama🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Ndio maana yak
Ni kwa vipi chadema itakufa endapo Mbowe atang'atuka uenyekiti? Kwann chadema isisimame imara kwa kutegemea mifumo imara iliyojiwekea?

Na kama kweli chadema imesimama kwasbb ya Mbowe, basi tutarajie kuona inatoweka mara tu Mbowe anapotwaliwa .
Ndio madhara ya kujenga mtu badala ya kukenga taasisi,wajifunze kwa udp,tlp na hata cuf,mzee mbowe hata kama atangania madaraka ni swala la muda tu uzee utoanza kuchukua nafasi yake na kuanza kuonekana kituko kama ilivyokuwa kwa akilan cheyo,lyantonga na Lipumba
 
Sijui wana matatzo gani. Kwamba hakuna mtu mwingine anayefaa wanaamini ni yeye tu? Mfano sasa hivi anaratibu maandamano. Haya maandamano chama kinanufaikaje?
Nani aliyekwambia maandamano wanayoratibu Chadema ni kwa ajili ya manufaa yao? mbona unawafundisha Chadema ubinafsi?

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Mti wenye matunda ndiyo hutupiwa mawe ,MBowe anawanyima usingizi SISIEMU na SISIEMU B's wenzao.

Nashauri tu Chadema endeleeni na Mbowe maana amepitia mapito makubwa sana na amekivukisha chama kipindi cha mpito...MWAMBA TUVUSHE.

Mbona Lipumba hazungumziwi?
 
Back
Top Bottom