Maneno ya busara ya Zitto yalivyochukuliwa juu juu

yeyote anatarajia kuivuruga chadema kupitia zitto aandike maumivu- by zitto.

kama ni kweli ana nia njema mbona wale vijana wa 4 wa bavicha wanapita pita mitaani wanasema zzk amewatuma watukane viongozi wa chama kwamba wanampigania yeye. Sasa awekemee kwn hayo ya udini na ukabila na matusi ndo kauli mbiu yao na yeye anawajua vizuri sana.
 
mkuu umeuliza maswali haya,which means hujui,sasa kwanini usijipe muda ujibiwe kwanza hayo maswali ili uwe kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuponda ukiwa umeelimika kupitia jukwaa hili?

Naelewa sana, na wewe kwa kujibu hivyo, maana yake unaelewa.
Umri wa kugombea urais Tanzania ni miaka 40 au zaidi (kwa mujibu wa katiba).
Wewe, Zitto na wengine mnalijua hili, ila bado mnaandika kuhusu kugombea urais mtu ambaye mwaka 2015 hatakuwa amefikisha umri huo !!
Na katika kuandika hoja hiyo, unasema hayo ni maneno ya 'Busara' !!!
Kazi unayo !!
 
Naelewa sana, na wewe kwa kujibu hivyo, maana yake unaelewa.
Umri wa kugombea urais Tanzania ni miaka 40 au zaidi (kwa mujibu wa katiba).
Wewe, Zitto na wengine mnalijua hili, ila bado mnaandika kuhusu kugombea urais mtu ambaye mwaka 2015 hatakuwa amefikisha umri huo !!
Na katika kuandika hoja hiyo, unasema hayo ni maneno ya 'Busara' !!!
Kazi unayo !!
kwa hiyo uliuliza maswali ambao majibu yake unayo!
 
Ukiwa great thinker utakubaliana na mimi kuwa zitto hana nia ya kugombea urais 2015,kitu nisichoelewa ni kwamba ana nia gani..japo pia sikubali kabisa kuwa ana nia ya kuihujumu chadema.
 
jazba za kushindwa uchaguzi hazisaidii,huo ndio mchezo wa kisiasa,M4C is not gonna help either,kama ilivyokua oparesheni sangara tu,kuchukua nchi si kazi ndogo,nyie endeleeni kudanganyana tu na kuchangishwa pesa

Wewe ni makamba family. Tunakujua vzr
 
Mawazo yake tu anatoa. Mwanza umeya kwani wanachagua wananchi? Ili kuwa injulikana kuwa ccn itashinda umeya. Mwanza bado, wananchi wanaiamini cdm
 
kwa hiyo uliuliza maswali ambao majibu yake unayo!

Hii ndio maana ya kuwa greater thinker, unatazama uelewa wa watu kwanza !!
yaani wewe unaandika kuwa ni maneno ya busara kwa mtu kusema kuwa anagombea urais mwaka 2015 wakati yeye mwenyewe anajua kuwa hatakuwa na sifa hizo !!
Zitto amewapata sana, hatagombea urais wala ubunge.
Kishakusanya chake, sasa anatafuta njia ya kutoka kwenye siasa !!
Mwaka 2015 atayeyuka taratibu, kimya-kimya na huyoo kisharidhika na alichochuma.
Siku nyingine usiandike hizo 'Busara' zako bila kuangalia kwa kina maswala ya siasa yanavyokwenda.
 

Swala la Zitto kutoa kauli hizo is a smart move, akijaribu kuangalia uongozi utamjibuje ili atengeneze makundi, pili ni kujaribu ku'win support ya wananchi katika nia yake.

Kauli ya Mbowe ni sahihi na ya wakati, ili kujaribu kuwaonya wapiga kura ambao Zito anategemea, kujaribu kuwaonya wananchama wao wanaotaraji kujiunga na kundi la zitto kuwa hawana nafasi.........!

Wana CCM na wote mnaofaidika na hii hali mbaya ya maisha kwa wananchi walio wengi, mikataba mibovu inaonufaisha wachache...........muelewe kuwa, wananchi wamewachoka......wananchi hawadanganyiki......! Kuna maeneo hata CHADEMA wakisimamisha JIWE na mgombea yeyote wa CCM, jiwe litashinda.......!

Kibanga Msese
 
Siasa za ubabe ndani ya chadema ndo kaburi Lao.Mwanza wamelamba mchanga Slaa kaondoka usiku wa manane mwanza alifikiri Wanajf ndo madiwani kule.Pole kikongwe
 
Zito kweli amekomaa kisiasa hana siasa za kinafiki wala za uoga anafanya kile anachoamini haburuzwi na viongozi wake wababe na anasimamia mawazo na maamuzi yake. Cdm km kweli wanatakakuchukua hii nchi wanatakiwa kumuunga mkono zito na sio kumpinga, hongera sana zzk kura yako ntakupatia. Zidumu fikra za zito idumu cdm
 
Maneno yake mafupi kwenye FB wall yake:

"Narudia, mwaka 2015 sitagombea Ubunge. Nitafanya kampeni ya Urais, ama mimi kama mgombea wa chama changu CHADEMA au kama mpiga debe wa mgombea wa chama changu. Miaka 10 ya Ubunge inatosha na kwa ngazi hiyo ni vema niwaachie wengine wasukume mbele gurudumu la maendeleo ya Jimbo na mkoa wetu. Huu ndio uamuzi wangu wa mwisho na nimeshawaeleza wananchi wa Jimbo langu na mkoa wa Kigoma toka mwaka 2005"[/QUOTE

Natangaza rasmi nitagombea jimbo la Kigoma Kaskazini, nina support kubwa sana kuanzia manyovu mpaka mwandiga. Watu wa kalinzi, matyazo, kibila na bitale wamekuwa wakisisitiza mara kwa mara nigombee, mimi nikawambia namwamini Zitto anafanya kazi nzuri.

Lakini kwa kuwa ameamua kutoka mwenyewe, nitagombea.
 
"Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha. Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola," alisema Zitto.
Atagombea urais kupitia Chama chake au ataomba ridhaa kwanza na kama chama kitamkubali ndiyo agombee kupitia chama chake??
Haka kajamaa mbona ka-babe sana...yaani zama hizi bado kanaishi kichwani mwake? Mshaurini ajaribu kufunguka zaidi kwa kuushirikisha ubongo badala ya hisia peke yake.
Kuhusu yeye kuingia Chadema akiwa na miaka kumi na sita (16) haimfanyi yeye kuwa zaidi ya wengine au anataka apewe zawadi?, by that time kila mtu alikuwa mahali fulani akifanya jambo fulani ambalo kwa namna moja au nyingine ndiyo vimeifikisha Chadema au nchi hapa vilipo.....
 
Ccm wasitegemee mkono udondoke, cdm hatutogombona kwaajili ya urais- zitto

CCm wanatumia nguvu nyingi kupambana na cdm hata vyombo vya habari vinatumika kuwawekea watu maneno midomoni ili mradi kutimiza lengo la mafisadi kuivuruga cdm.

Kamwe urais hautotugombanisha.
 
...
Kuhusu yeye kuingia Chadema akiwa na miaka kumi na sita (16) haimfanyi yeye kuwa zaidi ya wengine au anataka apewe zawadi?, by that time kila mtu alikuwa mahali fulani akifanya jambo fulani ambalo kwa namna moja au nyingine ndiyo vimeifikisha Chadema au nchi hapa vilipo.....

halafu hata kaborou alijiunga chadema akiwa dogo na alishawahi kupata msukosuko shuleni kwa ajili ya upinzani wake kwa chama tawala lakini sasa yu wapi? kwa hiyo kuingia cdm akiwa na miaka 16 sio hoja ya kumfanya aaminike sana, labda atoe hoja nyingine.
 
KIM KARDASH,

..sasa Zittto asizungumzie tena Uraisi mpaka hapo chama chake kitakapotoa maelekezo kwa wanachama kutangaza nia ya kugombea Uraisi.
 
Last edited by a moderator:
Kitu kimoja nafurahishwa nacho ni vile viongozi wakuu katika CDM wameamua kupiga kimya katika kauli za Nyepesi Zuberi Kabwe. Huyu ni kibaraka anayetumiwa ili kukigawa chama cha CDM kwani ni dhahiri CCM inamgwaya Dr. Slaa na inahofu kuwa akisimama tena, na mgombea akawa EL mwenye kashfa, patachimbika na ukizingatia now days wananchi hasa wa huko vijijini ambako jua linachelewa kutoka na kuwahi kuzama, ndio wamezibuka na sio wa kudanganywa tena.

Mimi nafikiri sio Nyepesi tu, watokee watu wengi tu wengine wachukue form za kugombea urais ndani ya CDM, lakini baada ya hapo si kuna NEc ya CDM....ambayo itam'bashe asiyestahili. Halfu ikatuletea mtu wa ukweenh....hah hah!

Zito yupo katika mkakati mzito wa CCM na tiss, ili kupunguza upinzani katika kuhakikisha walioshika rasilimali za nchi au wanao nufaika na mikataba mibovu wanaendelea kubunya hadi mwisho......kwani Zito ni nani has ili akisema jambo tayari libebeshwe vichwa vya habari kama sio mpango mahususi wakumpaisha?

Humu katk JF, ndugu Ritz anajua kuwa endapo waziri mkuu (mjiuzuru kwa kashfa) akipita kama mgombea wa CCM, kikwazo ni Slaa.....sasa anakuja na ishu ya ukanda baada ya kuona ishu ya udini, inawatufuna walioianzisha.

Kibanga Msese

Bila shaka wewe ndio utakuwa mwenyekiti wa kile kiwanda alichokisema Mh, kikwete hongera sana maana unataka kutuaminisha mawazo yako yasiyo na ukweli'tukikuambia leta ushahidi wa kauli zako hapa kama kweli wewe sio mwenyekiti wa kiwanda cha fix
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom