Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
UPDATE:
WIZARA YA AFYA YAUNDA KAMATI KUCHUNGUZA MADAI YA MADAKTARI WATARAJALI
Madaktari Tarajali wanatoa malalamiko yao dhidi ya Baraza la Madaktari Tanganyika (MCT)
Akizungumza katika mkutano huo wa Wanahabari, Dkt. Warsha Wilson ambaye ni mmoja wa waathirika wa matokeo mabaya ya mitihani ya madaktari Nchini, amesema:
Baada ya matokeo kutoka na kuonekana idadi kubwa ya Madaktari wamefeli katika mitihani tulifuata njia za kawaida kuwasilisha malalamiko yetu lakini tulipuuzwa.
Tuliwasilisha changamoto tunazopitia kwa Baraza la Madaktari (MCT) na waliahidi kulishughulikia suala letu lakini haikufanyika hivyo, kilichofuata tukawasilisha suala letu kwa Naibu Waziri, Dkt Moleli ambaye alilipokea na kulikabidhi kwa Mkurugenzi wa Tiba wa Wizarara ya Afya.
Mkurugenzi akasema ameunda Tume kulishughulikia suala hilo, lakini haikuwa hivyo, kwani baada ya zaidi ya miezi miwili tulipoenda kufuatilia mrejesho kwake na kwa MCT, tukagundua kuwa MCT haijui hata kama kuna Tume imeundwa.
Baada ya hapo tukaandika barua ya wazi kwenza kwa Rais, tulifanya hivyo na nakala ikaenda Wizarani, lakini zaidi ili Rais apate maombi yetu tukaamua tuandae taarifa hii kwa Wanahabari, ili Mheshimiwa Rais apate maombi.
Hoja ni mazingira ya tata ya mitihani
Tunaamini taratibu za mtihani baada ya mafunzo ya vitendo (Post internship) ni chanzo cha kupoteza umahiri kuliko kuweka uratibu mzuri.
Kwanza ni muda wa mitihani, kawaida baada ya mafunzo ya vyuoni kukamilika utaratibu unaofuata ni kuwa tunafanya mtihani kabla ya kwenda kwenye mafunzo ya vitendo (internship) kisha tunaenda kujifunza chini ya Madaktari Bingwa katika vituo vya Afya.
Baada ya mafunzo ya vitendo Daktari anakaa nyumbani kwa zaidi ya miezi 8, 9 hadi zaidi kisha anakutana na mtihani mwingine wa pili wa nadharia, hiyo inataegeneza mazingira ya kumpotezea ubora wake, hata akifanya mtihani akafaulu anakuwa ni daktari wa nadharia na sio vitendo.
Kwa nini fani yetu ina kelele nyingi?
Mitihani yetu imekuwa na kelele nyingi kwa kuwa fani yetu inahusisha vitendo zaidi kuliko nadharia, hivyo tunapotaka kumhukumu au kutegemea kumpata Daktari kwa njia ya nadharia unadhani atafanya vizuri?
Changamoto nyingine, mitihani haina uwazi, Wanafunzi au wafanya mitihani hawajui matokeo yao kwa maana ya alama, hakuna uwazi ili utambulike umefaulu unatakiwa upate alama ngapi, hakuna kitu kama hicho, wanasema tu wewe umefaulu au umefeli.
Hata kuambiwa ulifanya mtihani fulani haukupata matokeo mazuri katika somo fulani na kufaulu somo fulani, hilo halipo na huwezi kujua.
Wadau Msajili wa Madaktari amewadharau
Kupitia Gazeti la Mwananchi, Msajili wa Madaktari, Dkt. Mnzava alisema Madaktari wanafeli kwa kuwa wana uwezo mdogo wa darasani, hatukufurahishwa na hiyo kauli kwa sababu kwa muundo wa utaratibu wa Udaktari, ni sawa ametudharau sisi Madaktari wenzake, pia ni sawa na kuwadharau wakufunzi wetu.
Kwani kabla ya kufika hatua tuliyopo sisi tunakuwa tumepitishwa na TCU, tumepitishwa na Wakufunzi wa ngazi ya chuo na katika taasisi za afya ambazo wanatufundisha, hivyo kauli yake ni kama amedharau mamlaka zote hizo na ametudharau sisi ambao ni Madaktari wenzake.
Mbali na hapo amesema Madaktari wanafeli masomo ya upasuaji, sisi inajulikana wazi kuwa fani yetu ni vitendo zaidi kuliko nadharia, lakini mazingira yaliyopo wanatupima kwa njia za nadharia.
Pia soma: Madaktari wataraji wamekuwa ombaomba Mtaani kisa leseni, wamuangukia Waziri Ummy Mwalimu na Rais Samia