Makubwa yaliyompata jamaa yangu

Tall

JF-Expert Member
Feb 27, 2010
1,425
165
Jamaa yangu ndio kwanza ameoa, yeye na mkewe wote wanafanya kazi benki, sio ofisi moja.

Katika pitapita zake kwenye internet, kakutana na blog ya facebook, kasachiiiiiiiii, hadi kikaeleweka kampata binti mmoja aliyemvutia kimeseji na kusikia ni wale watokao moja ya makabila ya Arusha, akazidi kuchanganyikiwa, maana kabila hilo wasichana wake huwa wanamuacha hoi daima, hata mkewe anatoka kabila hilohilo.

Sijui ni shetani, sijui ni kutoridhika na mkewe, sijui ni tamaa, au labda sijui ni ukware tu... ila kilichofuata ni kuwa akawa na mapenzi mazito na huyo dada. Yeye jamaa yangu hakutaja jina lake halisi.

Jana jioni waliamua wakutane saa 12 jioni kwenye bar fulani maeneo ya kinondoni. Kwa vile kila mtu ana simu ya mwenzake hivyo walikubaliana, wakifika sehemu hiyo watapigiana. Huyu jamaa ananiambia kuwa walielezana pia kuwa kila mtu atavaaje, huyo dada alisema angevaa gauni la blue na jamaa akasema atavaa shati jeupe mikono mirefu... nilishasema huyu jamaa ni benka hivyo hapo ni kuvua tai tu na kuingia bar.

Jamaa saa 12 kasorobo akatia timu bila kuchelewa, kabla hajafika eneo la tukio akapiga simu na akaelekezwa na bibie eneo alipokaa kwani yeye bibie keshafika saa nyingi anamngoja. Jamaa akaingia bar kwa mikogo yote huku akipepesa macho na udenda ukimtoka, kwa vyovyote ville mkono wa kulia ukiwa mfukoni mwa suruali.

Kulia alimwona mrembo mmoja amekaa kavalia gauni la bluu, looooh alipoangalia vizuri kumbe ni MKEWE WA NDOA NDIE WANATAZAMANA NAE USO KWA USO.

Anasikitika sana kwa yaliyomkuta, anasema sasa ndoa yake inalegalega, ANAMPENDA SANA MKEWE. ANAJUTIA FACEBOOK.

UNASEMAJE MWANA JF? AFANYEJE KUWEKA MAMBO SAWA?
 
Inamaana mkewe alikuwa anajua kuwa ni mumewe anayewasiliana naye ama??
 
story sio ya kweli ni vigumu kwa watu kuwa na uhusiano na mke/mme wako bila kujuana, labda uniambie mwanamke alikua anajua akaweka mtego, lakini nje ya hapo sio rahisi kwa watu kujigeuza kwa asilimia mia na kuwa mtu mwingine kabisa kiasi hata mme/mke msifahamiane/msitambbuane
 
This looks like a fabricated story. I doubt whether this can happen:
-yaani jamaa unataka kusema hakujua namba ya mkewe?
-kwenye hiyo facebook unayosema aliipitia, hakuona sura ya huyo mwanamke?
-kama aliongea naye kwa simu, ina maana hata sauti ya mkewe hakuitambua? acha utani bwana

Nashauri hii thread ihamishiwe kwenye jukwaa la "jokes". Let us avoid fabricating stories and ask people to comment. We need real life issues here. Heshima mbeleeee
 
hii si kweli itawezekanaje namba ya mkeo au sauti yake wakati anakuelekeza usishtuke au huyo mke kwa nn hakujua namba ya simu ya mumewe au sauti yake

TOPIC CLOSED KWA UDANGANYIFU
 
Charity, sawa hampendi mkewe. Na mke vipi? anampenda mumewe? wote ni wezi.
 
hii si kweli itawezekanaje namba ya mkeo au sauti yake wakati anakuelekeza usishtuke au huyo mke kwa nn hakujua namba ya simu ya mumewe au sauti yake

TOPIC CLOSED KWA UDANGANYIFU

ndio na mie nilikuwa nataka kuuliza hapo, achia mbali sauti, no tu mtu angeshash2ka!
 
Huyu Tall ni mpuuzi tu! angalia nn unaweza kukiweka hapa watu wachangie nadhani hii thread ingefutwa maana haipo hata kwenye jokes,
kwenye facebook jamaa kama alikumbana na picha kama unavyosema na akamzimikia mrembo! inamaana yeye hajui sura ya mkewe?
number hana ya mkewe? sauti je? acha zako tall .....boaring:redfaces:

Kaburunye nakubaliana na wewe kwamba hii ni fabricated story
 
Acha ubabaishaji, peleka kwa Shigongo au Komedy Original because its a script enough for a short comedy au ongeza mineno itamfaa Kanumba and family at Darywood :hail:
 
story sio ya kweli ni vigumu kwa watu kuwa na uhusiano na mke/mme wako bila kujuana, labda uniambie mwanamke alikua anajua akaweka mtego, lakini nje ya hapo sio rahisi kwa watu kujigeuza kwa asilimia mia na kuwa mtu mwingine kabisa kiasi hata mme/mke msifahamiane/msitambbuane

na kaam huo mtego aliuweka bac mtoa thread aje atuambie na no ya cmu ilibadilishwa, vinginevyo hii kitu ni ngumu.
 
Huyu Tall ni mpuuzi tu! angalia nn unaweza kukiweka hapa watu wachangie nadhani hii thread ingefutwa maana haipo hata kwenye jokes,
kwenye facebook jamaa kama alikumbana na picha kama unavyosema na akamzimikia mrembo! inamaana yeye hajui sura ya mkewe?
number hana ya mkewe? sauti je? acha zako tall .....boaring:redfaces:

Kaburunye nakubaliana na wewe kwamba hii ni fabricated story
ha ha ha ha, ubarikiwe mkuu, pale kwenye facebook wote hawakuweka picha zao aliesema waliweka picha face book nani? haikuwa rahisi kujuana.
 
hii si kweli itawezekanaje namba ya mkeo au sauti yake wakati anakuelekeza usishtuke au huyo mke kwa nn hakujua namba ya simu ya mumewe au sauti yake

TOPIC CLOSED KWA UDANGANYIFU
mke alitumia namba ya simu ya shoga yake hasa baada ya jamaa kudokeza kuwa yupo kwenye taasisi za pesa
 
Humu jamvini kumejaa watu wa ajabux2,hawana uvumbuzi kila kukicha kuleta ushi-gongo tuuu.Upuuuuuuuziiiiiiiiiiiiiiiii
 
Back
Top Bottom