Mrejesho: Mchepuko kamuweka selo mke wa jamaa

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,495
99,294
Habari za masiku wakuu, natumai mko poa sana, nmewakumbuka sana.

Namshukuru Bungu nmetoka kwenye ban mzima wa afya, ni mambo mengi sana yametokea hapo katikati nilipokua sipo hewani. Moja wapo ni hili la kesi ya jamaa yangu, mchepuko wake aliyemuweka selo mkewe kwa kumshambulia akiwa mjamzito.

Ni hivi, baada ya ugomvi mkali kati ya mke na mchepuko wa jamaa uliopelekea mchepuko kung'atwa sikio na kuumizwa tumbo, kesi ilienda mahakamani. Wakati kesi ikiunguruma, mchepuko alionekana afya yake kiasi chake imetengamaa na aliruhusiwa kutoka hospitali kuja kusikiliza kesi iliyofunguliwa inayohusu mke wa jamaa kumshambulia na kumjeruhi.

Namshkuru Mungu siku ya kesi mahakamani nilihudhuria, na nilihusika vilivyo mwanzo mwisho. Tulipofika mahakamani mashemej tulishampanga mke wa jamaa kuwa kesi akishasomewa akane shitaka, lazima kesi hiyo itapigwa kalenda.

Halafu tutatumia mwanya huo kuyazungumzia pembeni na kumshawishi mchepuko afute kesi na tuna uhakika kesi itafutwa. Hapo wachonganishi ni ndugu wa mchepuko, inaonekana kana kwamba wanataka kumkomesha mke wa Jamaa.

Sijui ni uoga wa shemeji pale kizimbani au vipi, basi tuliyopanga yakaenda ndivyo sivyo, kesi ilipotajwa tu mahakamani mke wa jamaa tukashangaa akakiri kosa. Hakimu akasema mahakama imeahirishwa mpaka saa 8 mchana na tutarejea.

Tukajua hapa tushaingia mkenge, hakimu anaenda kuandika hukumu, na huenda mke wa jamaa anaenda jela. Basi tukawatumia wazoefu tunafanyaje kumnusuru shemeji yetu asiende jela. Mrejesho ukaja tusiwe na shaka, tusubiri hiyo saa nane kila kitu kiko sawa.

Saa 8 mahakama iliporejea Hakimu akasoma hukumu kuwa mke wa jamaa kahukumiwa kifungo cha nje miez 6 na atapaswa kuhudhuria mahakamani kila siku saa 2 asubuhi na kusaini kisha kupangiwa kazi mbalimbali pale mahakama pamoja na faini ya shilingi laki 3 na kugharamia matibabu ya mchepuko huko hospitali. Vilipwe ndani ya siku 7.

Mke wa jamaa alipopewa nafasi ya kusema chochote aliishia tu kulia machozi. Kisha hakimu akagonga kinyundo kumalizana na kesi. Mchepuko akainua mkono juu anaomba kusema, hakimu akampa nafasi. Akasema anaomba kujua kuhusu hatma ya matunzo ya hii mimba ya jamaa.

Hakimu akamjibu kuwa hilo ni shauri jingine, wakafaili upya hiyo kesi kisha wailete ataishugulikia. Leo alikuwa anashughulikia kesi aliyoletewa inayohusu kushambulia mwili tu. Basi kesi ikawa imeisha hivyo, tukatawanyika nje.

Ila sasa upande wa ndugu wa mchepuko wakawa kama hawajaridhika, wamejiweka makundi makundi wanajadili hukumu ile. Upande wa mke wa jamaa wakawa wanafurahia na vicheko vya chini chini kupongezana Hapa na pale.

Mimi sikupenda kuonyesha niko upande gani, nilikaa kimya kivyangu. Maana tangu mwanzo nilikua nacheza pande zote mbili. Kwa mchepuko nipo, kwa mke wa jamaa nipo, nang'ata huku, kisha napuliza kule, kusawazisha mambo.

Jioni yake ikabidi nimpigie mchepuko nimuilizie afya yake, ila lengo ni kujua ameipokeaje hukumu ile na anawaza nini ili kama kuna mpango wa kukata rufaa nijue mapema, wadau tujue tunajipangaje tena kumnusuru mke wa jamaa.

Nikagundua mamna mpango wa rufaa, ameridhika ila wanataka kufungua kesi ya kudai matunzo ya mtoto. Nikamtia moyo kuwa asifungue kesi, jamaa hana tatizo atamhudumia mtoto. Akasema kanielewa.

Niliporudi upande wa jamaa, nikawaita jamaa na mke wake, nikawashauri kuwa kipind hiki jamaa ajitahidi asioneshe chuki dhidi ya mchepuko yule na aendelee kumhudumia mimba yake kwa muda fulani mpaka mwezi mmoja wa rufaa uishe ili kumshawishi wasije kukata rufaa maana hukumu ile ilkuwa ya mchongo mchongo.

Mchepuko akikata rufaa hii ngoma bado ni mbichi maana hajapona vizuri lile tumbo lake. Anaweza jidhuru kusudi au kukata rufaa ilimradi tu amhangaishe tena mke wa jamaa. Wakiona huu upepo mchafu umepita, huyu mchepuko apotezewe moja kwa moja. Jamaa na mke wake wakasema wamenielewa.

Basi nikamuita jamaa pembeni, tukashauriana tunafanyaje, ikawa kila jion namsindikiza tunanaenda Kigamboni kupeleka matumizi na jamaa anapata kuongea mawili matatu na mchepuko wake ili kumuweka sawa kisaikolojia asiendeleze kesi. Baadaye jamaa walivokaa sawa na mchepuko wake, akawa anaenda tu mwenyewe kisha mimi nikaendelea na mambo yangu.

Kilichoendelea sasa, baada ya ule mwezi mmoja wa rufaa mahakamani kupita kimya, ikabd nimuulize jamaa vipi kuhusu makubaliano yetu kuhusu kumpotezea mazima yule mchepuko?

Jamaa akanijibu kuwa wameshasameheana na mchepuko wake, penzi lao limerejea upya ila anaomba nimtunzie siri hii kwa mkewe. Maana mkewe anaamini keshampotezea na hana tena mawasiliano naye, nikamkubalia "Sawa, haina shida brother".

Wakuu, ieleweke siyo kwamba nafurahia jamaa kurudiana na mchepuko yule au kufurahia maumivu ya mke wa jamaa kwa mlolongo ule wa mambo ya hovyo na kusikitisha sana aliyofanyiwa. Bali Kama mnavojua, mambo ya mapenzi ya wawili waliyokwishapendana kiukweli ni magumu sana kuyaingilia.

Hatujui jamaa anapewa nini huko kwa huyo mchepuko wake mpaka anamng'ang'ania vile pamoja na changamoto zote hizo jamaa anazopitia. Jamaa ni mtu mzima, mimi jukumu langu ni kushauri na kuweka mizani sawa panapobidi kwa mustakabali wa familia yake, maana jamaa ni zaidi ya rafiki yangu.

Sina uwezo wa kumshurutisha jamaa amuache mchepuko wake kama yeye mwenyewe hajaridhia kutoka moyoni. Kujifanya nashupaza mishipa ya shingo ili jamaa amuache, kuwasagia kunguni waachane, sijui unawawekea visirani au kutafuta kuonekana mwema kwa shemeji kwa kumchoma jamaa kwa mkewe kisa wamerudiana na mchepuko inakua ni sawa nakumpigia mbuzi gitaa, zaidi zaidi ntaonekana msaliti.

Binafsi niliishia kumshauri jamaa yafuatayo, kama atayazingatia sawa;

1. Asiwekeze zaidi mali yoyote ile na mchepuko yule, vinginevyo amejiridhisha na mabadiliko ya tabia zake mbovu, amemzalia na amemuoa kama mke mdogo rasmi.

2. Adumishe zaidi heshima na upendo kwa mkewe, maana yakijirudia tena kama haya sidhan kama atamuelewa na kumuamini.

Kama nimekosea kwa ushauri niliyotoa kwa jamaa au kuna la zaidi kushauri, maoni, au mapendekezo zaidi natanguliza shukrani.

Pia soma: Tushauriane: Mchepuko kamuweka selo Mke wa jamaa
 
Kwanza ndugu mwenyekiti pole na kifungo cha ban. Natamani kujua ulikosea wapi.
Pil, kuhusu huyu jamaa yako, kwakweli anakoenda n pabaya zaidi ya alipotoka. Mwanzon mahusiano yalivokua ya siri, hakukua na shida, lakn sasa hv n kama amelegalize mahusiano na mchepuko.
What will happen n kwamba mke wake atajua tu, na kitachofata ni mojawapo kati ya vitu 2, moja, wife atatafta jamaa na yeye awe anakamuliwa tege au mbili, huyo mama atajipanga kulipa kisasi kibaya either kwa jamaa au kwa mchepuko. Na nna uhakika ndugu mwenyekiti unawajua hawa wanawake zetu walivo wakiamua kulipiza kisasi.
All in all mwanaume kichwa cha chini kikikuongoza af cha juu kijawa kinafata mkumbo, lazma uuze bunduki na kununua rungu.
 
Mwanaume unaamua kwa reason ukishaona mwanaume anaamua kwa hisia u're in wrong direction
Jmaako tangu nianze kusoma hiki kisa anaamua kwa hisia so yeye ndo mleta matatizo the only solution hapo n kmuacha uyo malaya full stop.
I can guarantee u only two months utaleta kisa hapa.
 
Kama jamaa ana hela na anatoa huduma fresh mke hawezi sumbua, Mwanamke kwenye pesa huvumilia kila aina ya tukio hata akikufumania ukataka muachane anajirudi😁
 
Mwanaume unaamua kwa reason ukishaona mwanaume anaamua kwa hisia u're in wrong direction
Jmaako tangu nianze kusoma hiki kisa anaamua kwa hisia so yeye ndo mleta matatizo the only solution hapo n kmuacha uyo malaya full stop.
I can guarantee u only two months utaleta kisa hapa.
Sasa ntamshurutishaje amuache uyo Mchepuko Kama yeye mwnyw hajaridhia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza ndugu mwenyekiti pole na kifungo cha ban. Natamani kujua ulikosea wapi.
Pil, kuhusu huyu jamaa yako, kwakweli anakoenda n pabaya zaidi ya alipotoka. Mwanzon mahusiano yalivokua ya siri, hakukua na shida, lakn sasa hv n kama amelegalize mahusiano na mchepuko.
What will happen n kwamba mke wake atajua tu, na kitachofata ni mojawapo kati ya vitu 2, moja, wife atatafta jamaa na yeye awe anakamuliwa tege au mbili, huyo mama atajipanga kulipa kisasi kibaya either kwa jamaa au kwa mchepuko. Na nna uhakika ndugu mwenyekiti unawajua hawa wanawake zetu walivo wakiamua kulipiza kisasi.
All in all mwanaume kichwa cha chini kikikuongoza af cha juu kijawa kinafata mkumbo, lazma uuze bunduki na kununua rungu.
Shukran Sana chief,
Umeongea UKWELI japo khs MKE wa jamaa sidhan Kama anaweza fanya hayo Maana Ni mama wa kanisani.

Ana hofu ya mungu Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom