Makonda: Wakuu wa Wilaya waondoeni Machinga ndani ya siku 14

Hili suala la machinga ni kaa la moto kweli kweli.

Natambua umuhimu wa kuwawezesha wafanye biashara ili waendeshe maisha yao kama raia wengine.

Lakini biashara au shughuli zao zisilete madhara kwa raia wengine kama wenye maduka ambao hushindwa kufanya biashara kwa kuwa machinga wamepanga bidhaa nje ya maduka yao.

Kuna machinga wanapanga bidhaa barabarani hasa Kariakoo. Au wanapanga bidhaa sehemu ya waenda kwa miguu ambao hulazimika kupita barabarani na kuzuia magari kupita.

Lazima tufike mahali kama nchi tupate ufumbuzi wa kudumu. Haiwezekani ukawa ufumbuzi wa kukwaza raia wengine.

Wakati ufumbuzi huo unatafutwa lazima waondolewe sehemu ambazo ni kwa kikwazo kwa wengine.
 
Leo Raisi kawadhalilisha wakuu wa Mikoa na Wilaya.... Sasa hata mie nimeaanza kuvidharau hivyo vyeo kumbe hawana uchungu na Wananchi.... Ila Wamachinga ndio pembezoni mwa barabara wapita njia tunafikia kutembea barabarani pamoja na magari ni hatarishi hii
 
Tengezeni mazingira mazuri wafanye Kazi zao vizuri na kwa faida.

Kwa mkoa wa DSM ni vyema kila Wilaya (Ubungo, kingamboni, Temeke na Ilala) zikatenga maeneo maalum kwa ajili ya kujenga soko la machinga ambapo watafanya biashara zao kwa uhakika bila usumbufu wowote!
 
Tengezeni mazingira mazuri wafanye Kazi zao vizuri na kwa faida.

Kwa mkoa wa DSM ni vyema kila Wilaya (Ubungo, kingamboni, Temeke na Ilala) zikatenga maeneo maalum kwa ajili ya kujenga soko la machinga ambapo watafanya biashara zao kwa uhakika bila usumbufu wowote!

unajua maama ya concept ya Machinga (matching guys) ..... in other words peddlers

siyo rahisi unavyodhani .....
 
Debe tupu limeibuka tena; kabla ya Novemba 15 hili suala litakuwa limeshasahaulika.
Kama wamachinga wanavunja sheria, itajwe hiyo sheria na kisha polisi wafanye kazi yao, wakuu wa wilaya inawahusu nini wakati masuala hayo ni majukumu ya mameya?
november ya tarehe 15 ya mwaka upi?
 
Back
Top Bottom