RC Makalla: Benki ya Afrika kushirikiana na Serikali kujenga masoko ya kisasa ya machinga

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
RC MAKALLA: BANK YA AFRICA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA MASOKO YA KISASA YA MACHINGA.

- Ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Samia kuboresha mazingira ya Machinga.

- Awaelekeza Wakuu wa Wilaya/ Wakurugenzi kuweka Mkazo jambo Hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amefanya kikao baina ya Bank ya Maendeleo ya Africa ADB na Viongozi wa Mkoa wa Dar es salaam, Dodoma, Wizara ya Fedha, TAMISEMI na TANROAD kujadili ofa iliyotolewa na Bank hiyo ya Ujenzi wa Masoko ya kisasa kwaajili ya Machinga kwenye Wilaya zote tano za Mkoa huo.

Akizungumza wakati wa kikao hicho kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa, RC Makalla amesema Bank hiyo imeamua kushirikiana na Serikali ya awamu ya sita kuboresha mazingira ya Machinga walioamua kuitikia wito wa Serikali kufanya biashara kwenye maeneo waliyopangwa.

Ili kufanikisha Mpango huo unaokwenda kuchochea biashara, RC Makalla amewaelekeza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kumkabidhi taarifa kamili inayoainisha Wapi Masoko hayo yajengwe, Michoro na Gharama halisi kabla ya ijumaa ili awasilishe kwa Bank hiyo kwaajili ya utekelezaji.

Pamoja na hayo RC Makalla amewaelekeza TANROAD, TARURA, DAWASA, TANESCO, LATRA kuhakikisha kuanza maandalizi ya kuhakikisha Maeneo yanapojengwa Masoko hayo yanakuwa na huduma zote muhimu ili kuchochea biashara.

Kwa upande wake Meneja Wa Bank ya maendeleo Afrika tawi la Tanzania Patricia Laverley amesema kuwa Bank hiyo ipo tayari kutekeleza Ujenzi wa Masoko hayo kwakuwa wameguswa na jitiada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Wafanyabiashara wanaendesha biashara kwenye maeneo sahihi na Bora.
IMG-20220627-WA0016.jpg
IMG-20220627-WA0017.jpg
IMG-20220627-WA0014.jpg
IMG-20220627-WA0015.jpg
 
Back
Top Bottom