Makonda: Wakuu wa Wilaya waondoeni Machinga ndani ya siku 14

Inabidi siasa ziwekwe pembeni mji uwe safi na biashara zitengewe maeneo maalum.
 
Kariakoo ni aibu kwa Taifa.Bidhaa zinapangwa mpaka barabarani.Watanzania,ni nani ameturoga?
 
Muheshimiwa hajawahi kuanzisha project akaimaliza, alikuja na ;
Kuondoa malaya
Kuondoa mashoga
Kupanda miti
Kuondoa ombaomba
Kuondoa machinga
Halafu hashtuki tuu kila siku yupo clouds fm anatoa maagizo :rolleyes::rolleyes:
 
Hivi idadi ya machinga wote ni kiasi gani ...tukijua hili itatusaidia na tunaweza kuwaomba watu wazuri kama GSM akawaweka kwenye shopping malls zake wakachangamsha biashara huko!

Wamachinga wengi ni vijana wa kiume ambao wengi ni wa kiume ambao hawana 'kazi'...hivi vijana wa kike wasio na kazi huishia wapi????? (NB:...swali langu ni la uchokozi).....
 
Nasikia mtaa wa Congo hakufai, sijaendaga kitambo pale ngoja weekend hii niende nikajionee kwa macho tena sikuhizi kuna Mwendokasi kuanzia Moroco nitaupanda huo.

Mwenyekiti CCM JF
Hakufaaaiii mimo nilienda 2month ago nikasema sirudi .ingawa nina shida kweli ya kwenda kkoo...hakuna pa kupita kuanzia mlangoni mwa geti la stand ya mwendo kasi...mpk msimbazi..unapita yanakopita magari ukigongwa juu yako...service road biashara tupu...kongo ndio balaaa
 
Makonda anamjaribu mzee.. si alishasema waachwe? nasikia majuzi kidogo waue tena pale Msimbazi
 
Hawa jamaa ni wasumbufu sana bora watolewe tu kwenye hayo maeneo ili kuwe na ustaarabu. Wakianza kupanga bidhaa zao chinii hata nafasi ya kupita inakuwa finyu na wezi wa mifukoni wanajazana sana hayo maeneo nadhani huwa wanaushirikiano na hawa wamachinga.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom