Majanga yaliyonikuta kwa kutokunywa maji mengi, usiombe yakukute

Pole sana...jitaid uwe unakunywa maji after meals tena vizur yakawa vuguvugu ili kulainisha chakula vizuri kwan ya baridi kama umevyakula vya mafuta vinagandisha na matunda kwa wingi...hosp wangekupa vidonge Ducolax/bisacodly au ungefanyiwa enema
 
Nyamazaaaa,daah,yamenikuta babaa,inatisha,zege lahitaji maji mengi,jasho lilinitoka,sasa hivi maji nayanywa yakutosha
 
NASHUKURU SANA WADAU WOOOTE MLIONISHAURI, NITAZINGATIA USHAURI WOTE; PIA NATANGULIZA SAMAHANI KWA WOTE WALIOKWAZIKA; LAKINI USIOMBE YA KUKUTE; SIPATI PICHA YAANI NIKIWAZA HALI KAMA HII IKUKUTE HALAFU KUWE NA TETEMEKO LA QRDHI KAMA KULE BUKOBA, WAWEZA OMBA ARDHI IPASUKE AISEE!
 
pole sana..
lakini je:Mkeo ana utaalamu wowote wa mambo ya Afya?..Jiridhishe na wataalamu...
 
Pole sana mkuu,inabidi umwambie waifu ukufanyie ukaguzi eneo la tukio huenda kuna jeraha lililojificha.
Halafu hapo ukute kabla hapajapoa vizuri haja inakuja tena!!.
bora haja ije amogoe na kidole kuliko kale kapele mbuzi kama kameota alafu kakataka kukunwa na nyama!
 
Haijawani tokea;
Nilikuwa nasikia Kwa watu tu hii kadhia.
Leo nimeingia chooni, kwakweli choo nilikuwa nayo, lakini ilikwama kutoka ilikuwa ngumu sana, nimekaa chooni karibia lisaa, choo kimechungulia ila hakitoki, kwakweli maumivu niliyoyapata yalikuwa ni makubwa sana, haijawahi tokea, nilijaribu kukibana kipungue ukubwa lakini wapi, choo kilikuwa kigumu sana, yaani ikabidi nianze kusali tu, maana nilihisi kuchanganyikiwa kabisaa na Yale maumivu makali,
Baada ya mda nikapata wazo la kumogoa kipande kidogo kidogo Kwa vidole, yaan nilikuwa namogoa halafu nasimama kuyabana then nachuchumaa, hivyo tena Kwa maumivu makali sana!
Namshukuru Mke Wangu Kwa kunitia moyo kwamba nijikaze, Mke Wangu alinisisitiza kwamba tatizo hilo huja kutokana na kutokunywa Maji mengi (Constipation) . Kanisisitiza sana niwe nakumbuka kunywa Maji meji, na ni kweli sina kasumba ya kunywa Maji kabisa nikiwa katika kazi zangu, na pengine huwa Niko busy sana kiasi kwamba saingine nikishakunywa chai asubuhi mchana huwa sipati lanchi, kiufupi Mimi ni miongoni mwa watu wavivu kunywa Maji mengi. Lakini kuanzia sasa nazani nitakuwa mfano Wa kuigwa, nimeumia sana, ilifika hatua niiaanza kuwaza na yasiyowazika, niliwaza hivi hali ile ingenikuta nikiwa ugenini au kwenye ndege ningefanyeje!
Nimejifunza mwenzenu, na nimeweka hii post ili kuwanuru nanyi msijisahau kunywa Maji balaa hili lisije wakuta ambalo sijui kama hata hospital ukizindiwa wanakusaidiaje
Hapa ********* unauma balaa! Nimemogoa taratibu hivo hadi choo kikatoka chote, ila nimeumia sana, nimewaza kumbe wanawake wanapojifungua huumia kiasi kile! Maana Mke Wangu kaniambia hayo maumivu niliosikia ni Mara tano kwa maumivu ayapatayo mwanamke
Kwakweli NIMEKOMA SITASAHAU KUNYWA MAJI MWENZENU TENA,
KUNYWENI MAJI NANYI YASIJE WAKUTA WADAU. Ni ushauri tu msinielewe vibaya.
 
jitahidi kunywa maji mengi, kula mapapa, maeme pia,
Jitahidi kunywa na maziwa mgando ikiwezekana,
Kwa kuanzia anza na dawa ya maji inaitwa Osmolaxis ikalainishe kopo hilo matakoni
 
Back
Top Bottom