Kwa wale wanaoamka wakiwa na mikwaruzo, ondoa shaka, usipaniki. Nami nishawahi kupata hii hali na huu ndio mrejesho wangu

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,040
Screenshot_20230626_130237.jpg

Mara kadhaa nimeona hili tatizo watu wakiliibua na hata humu ni juzi juzi kuna mtu kaanzisha uzi, nimeona ni vema nilete experience yangu.

Mimi hali ishawahi kunipata, dah we acha tu, nikafikiria mbali kwamba natembelewa na wachawi, nilipaniki sanaaaaa!! nilianza kulala saa tisa au kumi natumia simu ila nikiamka imoo!! nilianza kulala sizimi taa lakini wapi! nikiamka nakuta mikwaruzo nahisi kuchanganyikiwa kwakweli, nilienda kuombewa kanisani, mimi mkristo lakini nilienda kusomewa vifungu na sheikh (sikiaga kwa wengine usitake yakukute), niliogea chumvi, kutuma ndulele, kufukiza chumba moshi wa bangi, kuweka kisu kwenye ndoo ya maji, kufukiza mmavimavi ule wanaovaa watoto wachanga kwenye bangili, n.k. hii yote ni kwa hofu kwamba natembelewa na vigagula lakini wapiii!!! kwa sasa imepungua sana ila kwa mwezi lazima nikute kamkwaruzo shavuni, utosini, mkononi, begani au kifuani.

Jibu la hii hali nililipata nilipoweza kushuhudia live kwamba hii mikwaruzo hata mchana wa jua kali inaweza kutokea.

Inakuwa kwamba mwanzoni ngozi ni kama inaumuka hivi inakuwa laini sanaa, baada ya muda uvimbe huo ukikauka ndio vinatokea hivyo vimikwaruzo. ikitokea uvimbe huu upo ukiwa umelalia sehemu iliyotokea ama inasuguliwa na shuka ama blanketi basi hio sehem laini inatoa vidamu. kwa utafiti wangu wa ziada sehemu hii huwaga ukiilamba kunakuwa na ladha kama ya betri la simu kule kwenye umeme.

Kinachosababisha sijui nini ila mimi nahisi labda allege ama ulimwengu wa roho ila sio level ya uchawi maana hii ni mikwaruzo si chale, zile chale huwa ni kama umepigwa wembe uliozama ndani ya nyama kabisa na huwa hazifutiki, huwa wanaweka na dawa ukiamka utaona kuna vitu vimepakwa kwenye chale. sio hivi vimikwaruzo baada ya wiki tu vinapotea na ukiamka kama kidonda bado kibichi huoni chochote kilichopakwa.

Mambo haya nilifanya na kwa sasa ni adimu sana mimi kupata hii mikwaruzo ila sijui ni kipi sasa.

Usafi wa kitanda na kuoga, zamani kusema kweli suala la usafi nilikuwa nyuma, kwa sasa kitanda lazima kibadilishwe shuka kila wiki na lazima nioge kila siku ama nisipooga siku hio basi lazima ninawe kichwa, kwapa na mitaa ya kati.

Zamani nilikuwa na tabia ya kujichua usiku au ku-sex nikipata ugeni, nilikuwa na kitabia shahawa nafutia kitambaa nakificha tu sehemu kinakauka na shahawa, kitambaa hiki kinaweza kukaa hata wiki hakifuliwi, alafu pia ilikuwa kawaida naweza nisinawe baada ya kupizi, Niliacha tabia hii nilianza kuhakikisha natumia tishu kufutia shahawa, nikijifuta natupa chooni naflashi naenda bafuni kunawa mitaa ya kati hata kama nilishaoga kabla, ni mwiko kusex au kujichua masaa mawili kabla ya kuomba kuingia kulala (exception ni kwa mke au mume tu)

Nikiri pia zamani nilikuwa nalala kama ngombe sisali, niliacha hii tabia.

Kunywa dawa za minyoo, wengi mara ya mwisho kunywa hizi dawa ni shuleni, mimi niliamua nipige dozi ya hii dawa zile za kutafuna na hapo nilikuwa nina miaka mitano sijatumia dawa ya minyoo, labda huenda hili tatizo minyoo inahusika, may be.
 
Ushwahi kuoigwa chale..? Usku unaamka asubuh unaona kabsa huu wembe tena kwenye paji la uso mzee
Chale ni tofauti kabisa hizo huwa zinazama ndani zaidi na huwa wakipiga wanapaka na dawa, ni ngumu kuziondoa hizi zinabaki kama alama.

Hii mikwaruzo ikikauka ukikwangua inapotea ndani ya siku kadhaa
 
Ushwahi kuoigwa chale..? Usku unaamka asubuh unaona kabsa huu wembe tena kwenye paji la uso mzee
Mi nilinyolewa usiku aisee..tena na wembe kabisa nywele za utosini. Yaani mtu unaamka tu nywele zimenyolewa. Zilikaa karibu miezi 6 bila kuota mpaka kikaja kiajuza kimoja kutoka Musoma huko ndani ndani kikanipaka tumafuta fulani tweupe tunanuka mara vuu nywele hizo. Ila kenge aliyeninyoa aliRIP sasa sijui kile kiajuza kilimfanya nini mi sijui wala sikuhusika. Nilikuwa darasa la saba (LY)....

Dunia hii ina mambo!

Ila hii ya mikwaruzo kama ulivyosema yawezekana ni allergy fulani tu...na kwa watu wanaotumia blood thinners huwa inawapata sana. Hata wanaokula garlic kwa wingi....ila kunyolewa nywele usiku mtu unaamka tu umelimwa upara aisee nilinyosha mikono!
 
Mm kuna sku naamka nina alama za viwembe kila sehemu kuanzianoaji la uso kweny shngo nyuma mgongoni suruali ilichafuka maana sku hyo nililala na suruali kpnd nko form2 nakumbuka dah mi nachukia wachawi bora hata ya mwizi kuliko mchawi
 
Pole sana aisee. Hata mimi aliyeninyoa usiku alinichanja na chale tatu - moja ikiwa kitovuni. Na dawa kabisa nyeusi akaweka. Kiajuza kile kilinipaka mafuta yale yale chale zikafutika pia.

Akina Mshana Jr hawa noma sana yaani 😁😁😁
 
Mara kadhaa nimeona hili tatizo watu wakiliibua na hata humu ni juzi juzi kuna mtu kaanzisha uzi, nimeona ni vema nilete experience yangu.

Mimi hali ishawahi kunipata, dah we acha tu, nikafikiria mbali kwamba natembelewa na wachawi, nilipaniki sanaaaaa!! nilianza kulala saa tisa au kumi natumia simu ila nikiamka imoo!! nilianza kulala sizimi taa lakini wapi! nikiamka nakuta mikwaruzo nahisi kuchanganyikiwa kwakweli, nilienda kuombewa kanisani, mimi mkristo lakini nilienda kusomewa vifungu na sheikh (sikiaga kwa wengine usitake yakukute), niliogea chumvi, kutuma ndulele, kufukiza chumba moshi wa bangi, kuweka kisu kwenye ndoo ya maji, kufukiza mmavimavi ule wanaovaa watoto wachanga kwenye bangili, n.k. hii yote ni kwa hofu kwamba natembelewa na vigagula lakini wapiii!!! kwa sasa imepungua sana ila kwa mwezi lazima nikute kamkwaruzo shavuni, utosini, mkononi, begani au kifuani.

Jibu la hii hali nililipata nilipoweza kushuhudia live kwamba hii mikwaruzo hata mchana wa jua kali inaweza kutokea.

Inakuwa kwamba mwanzoni ngozi ni kama inaumuka hivi inakuwa laini sanaa, baada ya muda uvimbe huo ukikauka ndio vinatokea hivyo vimikwaruzo. ikitokea uvimbe huu upo ukiwa umelalia sehemu iliyotokea ama inasuguliwa na shuka ama blanketi basi hio sehem laini inatoa vidamu. kwa utafiti wangu wa ziada sehemu hii huwaga ukiilamba kunakuwa na ladha kama ya betri la simu kule kwenye umeme.

Kinachosababisha sijui nini ila mimi nahisi labda allege ama ulimwengu wa roho ila sio level ya uchawi maana hii ni mikwaruzo si chale, zile chale huwa ni kama umepigwa wembe uliozama ndani ya nyama kabisa na huwa hazifutiki, huwa wanaweka na dawa ukiamka utaona kuna vitu vimepakwa kwenye chale. sio hivi vimikwaruzo baada ya wiki tu vinapotea na ukiamka kama kidonda bado kibichi huoni chochote kilichopakwa.

Mambo haya nilifanya na kwa sasa ni adimu sana mimi kupata hii mikwaruzo ila sijui ni kipi sasa.

Usafi wa kitanda na kuoga, zamani kusema kweli suala la usafi nilikuwa nyuma, kwa sasa kitanda lazima kibadilishwe shuka kila wiki na lazima nioge kila siku ama nisipooga siku hio basi lazima ninawe kichwa, kwapa na mitaa ya kati.

Zamani nilikuwa na tabia ya kujichua usiku au ku-sex nikipata ugeni, nilikuwa na kitabia shahawa nafutia kitambaa nakificha tu sehemu kinakauka na shahawa, kitambaa hiki kinaweza kukaa hata wiki hakifuliwi, alafu pia ilikuwa kawaida naweza nisinawe baada ya kupizi, Niliacha tabia hii nilianza kuhakikisha natumia tishu kufutia shahawa, nikijifuta natupa chooni naflashi naenda bafuni kunawa mitaa ya kati hata kama nilishaoga kabla, ni mwiko kusex au kujichua masaa mawili kabla ya kuomba kuingia kulala (exception ni kwa mke au mume tu)

Nikiri pia zamani nilikuwa nalala kama ngombe sisali, niliacha hii tabia.

Kunywa dawa za minyoo, wengi mara ya mwisho kunywa hizi dawa ni shuleni, mimi niliamua nipige dozi ya hii dawa zile za kutafuna na hapo nilikuwa nina miaka mitano sijatumia dawa ya minyoo, labda huenda hili tatizo minyoo inahusika, may be.
Unafuga kucha? Shuka au blanketi zinaweza kukwaruza kiasi hiki?!

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom