Maisha yamenishinda!!

Uliamua kuoa mwenyewe au ulifuata maneno ya watu ya mbona mpk Leo hujaona!! Ukaamua kuoa golikipa kufurahisha watu!! Jamani jiandaeni kabla ya kuingia kifungoni coz at the end of the day ni msalaba wako sio wa hao waliokushauri . anyway yashatokea we mtafutie bby kazi msaidiane
 
Huku kijijini na mimi maisha yananishinda.
Nataka niuze mahindi nije mjini, mjini kuna nyumba nzuri na magari. Nasikia magari madogo ila yanakimbia hayo. Yakikua makubwa ndio yanazidi kukimbia. Nikiyaona nitahamasika kutafuta vyangu.
Huku kijijini tunacheza na ngedere tu.

Usije mjini nakwambia usije mjini nasema tena usije ni bora ukacheza na ngedere kuliko kucheza na wenye nyumba mjini.
 
Duh! Mshahara wa 542,000/= mtu unashindwa kuishi mjini....!!!wakati watu tunalipwa laki na nusu 150,000 kwa muhindi na maisha yanasonga...wewe lazima utakuwa una matumizi mabovu kupindukia....

Mimi nikipata mshahara kama wako baada ya mwaka mmoja tu namiliki kibanda pembezoni mwa jiji la dar es salaam....
 
Huyu jamaa amenishangaza sana, yani mshahara was 524,000Tsh/ bado analalama plus 300,000 ya wife kwa mwez uhakika was 824,000/Tsh. Hapa hesabu inahitajika kwanza matumizi ya home per day yapunguze kutoka 8000 mpaka 5000-6000
Pili nauli pamoja na msosi wa mchana mkiwa kazin wewe na mke wako punguza kutoka 10000 mpaka 6000 kwa mahesabu ya haraka kwa mwez uta save 210,000 kwa mwaka 2.5M pia jaribu kupunguza matumiz mengne na kugundua maeneo/masoko ya kununulia vitu bei nafuu hasa vyakula. Mwisho usiwe mvivu wa kufikiri
duuh, halafu kumbe huu uzi ni wa 2011 mtu alikua anachukua zaidi ya nusu milioni alikua analalamika??? nilifikiri hata ni mwaka huu
 
I believe that if life give you lemons you should make lemonade....... And trie to find somebody whose life has given them vodka and have a party!!
 
Du kwel akil na mipango atufanan lak tano na upuuz ndogo aya kalime alaf uwne balaa lake
 
Wakuu Maisha ya Mjini yamenishinda, yaani nikiangalia kipato changu na majukumu niliyonayo naona siwezi kabisa.

Maisha kama haya naona afadhali yale maisha niliishi kwa wazazi wangu enzi za mwalimu pamoja na kuwa babangu alikuwa mkulima lakini tulienda shule na tuliishi maisha mazuri.

Mimi sijui wenzangu mnaishije? mnapata haya machungu nayoyaona mimi? nasimama asubuhi kituoni kwenda kazini naona magari yanapita tu huku mmefunga vioo hivi kweli mna matatizo kama yangu kweli? Hivi nyie pesa mnazipata wapi? mbona najiona mpweke katika nchi yangu hii?

Wakuu siyo siri natafakari kama mambo yakizidi kuwa magumu basi nitafute nauli nirudi kwetu angalau huko nitakuwa na uhakika wa kusogeza siku.

Kipato changu wakuu ni Tshs 542,000/- Nina Mke na mtoto mmoja (5), nimepanga nyumba viwili na sebure - Mambo yamegoma kabisa.

Nipeni ushauri nateketea mtanzania mwenzenu.
We rudi tu kijijini...sisi hata tushindie mihogo...hata yaje mafuriko haturudi kijijini ng'o
 
Back
Top Bottom