Mpui Lyazumbi
JF-Expert Member
- Sep 1, 2010
- 1,856
- 371
Kwa kipato cha shs 542,000 hutakiwi kulalamika. Kuna watanzania kama 85% ambao wanapata 1/4 ya unachopata (135,000) na wanaishi na familia zao watoto wa3 and above na bado utakuta ana kibanda chake Charambe, Kongowe, Kitunda au Kipate.
Wewe una mke na mtoto mmoja na unatumia daladala unalalamika nini. Nakushauri kuwa na vipaumbele, acha makundi ya starehe kama ulevi. uzinzi then hicho kipato kinaweza kukutoa. Hebu tufanye mchanganuo hapa chini.
Tshs 542,000/=
1. Kodi ya nyumba shs 100,000
2. Chakula nyumbani shs 150,000
3. Chakula kazini shs 60,000
4. Nauli ya dala dala 30,000
5. Mengineyo shs 100,000
Jumla ya matumizi ni shs 440,000 hivyo unabaki na akiba ya 102,000. Ukitunza hii akiba kwa miezi sita unaweza ukampatie mke wake mtaji wa shs 612,000 baada ya miezi sita na mkaanza mkakati wa kununu ka plot Gongolamboto.
Chukua huo ushauri na usirudi kijijini utajuta.
Asisubiri miezi 6 ya kujibana. Ana ajira na ni dhamana tosha. Akubali hiyo laki 1 iwe inakatwa kutokana na mikopo iliyoko benki na inapatikana within a week. Tazama hesabu hii, laki 1 kwa mwaka ni 1.2ml. Na kama utakopa kwa miaka mi4 ni 4.8ml. Utapewa karibu 4ml. Huo ni mtaji maridadi wa kabiashara kwa mjasiriamali. Mpe mkeo na fungua biashara makini ya bidhaa isiyochacha. Dar kuzuri utatoka broda!