2014 nilirogwa kwa kununua dawa ya mvuto mtaani, sikuwa najitambua, ponea yangu ni ndugu yangu kunijua nina tatizo na kunipeleka kwa mtaalam

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
Nawaasa sana watu mnaonunua hizi dawa za mvuto wa mapenzi, kusafisha nyota, n.k. muwe makini sana, hizo dawa nyingine mnazonunua huwa mnajitoa sadaka kwa wanaoziuza, wanawaibia vitu vyenu ama kuwaharibia maksudi baraka mlizopewa pengine ili wanufaike na matatizo yenu, Ridhika na ulichopewa, Tia juhudi kukikuza na uwe na juhudi ya kuthamini imani yako.

..........

2014 nikiwa na miaka 19 nilianza maisha ya kujitegemea mtaani, nilikuwa tayari nimeanza kujishughulisha lakini kipato changu kidogo kilinifanya niishi mazingira ya kawaida sana tofauti na tamaa ya vizuri nilivyovitaka nikiwa bado kijana mdogo niliepata ladha ya kuishi maisha yenye uhuru mtaani tofauti na nyumbani.

Katika moja ya vitu nilivyokuwa vikinitesa ni mapenzi, nilikuwa nachukia sana kuona mabinti wananichukulia poa, kwa akili zangu za enzi hizo niliamini kwamba labda sina mvuto ila nililpokuwa mkubwa hapo baadae nikajua sababu ilikuwa ni hali yangu kiuchumi haikuwa vizuri. Hata mabinti niliopata mara nyingi waliniacha hatukuweza kudumu hata wiki.

sasa katika stori za hapa na pale nikasikia kuna dawa za mvuto wa mapenzi kwamba ukiweka chini ya ulimi au ukiogea siku kadhaa mabinti unawapata kirahisi sana kama vile kukamata kuku wa kisasa.

nilikuwa mdau mzuri sana wa kutumia facebook kwenye kisimu changu enzi hizo, nikajiunga magroup ya tiba asili, nikauliza wapi naweza kupata dawa ya kuongeza mvuto kwa mkoa wangu, kuna wadau wakanipa connection niende kwa mtu flani anauza dawa hizo pamoja na dawa zingine za kusafisha nyota, mvuto wa mapenzi, kurudisha mpenzi, kukamata mwizi, kinga, n.k.

Nilipofika kwake aliniuzia dawa ni ya unga unga nililipia elfu 20, dawa ile aliinadi inaongeza mvuto, akaniambia ni mwiko kutongoza wake za watu nikaona hii huenda ndio yenyewe basi nikalipia, niliioga kwa siku 3 mchana na usiku.

mwezi umepita sikuona cha ajabu hali ilikuwa ile ile tu.

mziki ukaanza baada ya mwezi hivi watu wanasema nimepunguza uchangamfu, nimepunguza ucheshi wananiuliza kama nimefiwa, nimepunguza ari yangu ya kufanya kazi, n.k. kwa upande wangu nami huku malengo ya kufungua ofisi yangu nikaanza kupuuzia, natumia pesa ovyo sizitunzi hata chakula cha usiku naenda kula mgahawani, n.k. mimi nilikuwa naona sawa tu hakuna shida.

Hali hiyo ilidumu kwa mwaka na nusu hivi, watu wa karibu wakaanza kudhani natumia bangi, kuna ndugu yangu ambae ni rafiki pia wa karibu ndio akawa ananichunguza kwa ukaribu akaniambia sijitambui, kiukweli akaanza jitihada ya kunipeleka kanisani huko tumezunguka makanisa kama matatu lakini wapi maana huko kunahitaji Imani na mimi nilikuwa hata sina imani thabiti mda huo.

Niliwahi pelekwa pia kwa sheikh, yule sheikh alikuwa sio mbaguzi wa dini hivyo alinipiga visomo vya maana tu lakini bado tatizo lilikuwa kwamba mimi sina Imani.

Ndipo ikabidi sasa nisafiri na ndugu huko Dodoma, Kondoa . Uncle aliniambia kuna mtoto wa rafiki wake aliaguliwa huko so na sisi tujaribu.

Tulifika usiku huko, na sehemu ya kwanza tulifikia ni kwa mtaalam, mattalam huyu alikuwa pia ni shehe ila nilishindwa kujua ni vipi inakuwa hivi ila nikapotezea nikajikita na kilichonipeleka, mtaalam alikuwa yupo kwenye miaka 46 hivi na mke wake ni kama 25 nadhani, huenda alikuwa mke wa pili.

nilikuwa nimekaa kwenye kochi mtaalam alikuwa amekaa kwenye mkeka, akaniambia nami nikae kwenye mkeka, nilipata shida kidogo maana sikuzoea ila kibishi nikakaa.

Hakupoteza muda alipanisha majini hapo anaongea vitu habieleweki mixer kucheka kucheka, duh niliogopa aisee, kanitolea macho hapo, wakati natahamaki kinachoendelea anaongea vitu sielewi, il muda wotw huu mke wake anamwangalia na ni kama anamuongelesha mtaalam bila sauti. Baada ya dakika hivi mtaalam kajirudi yani jasho tele anahema na kutokwa jasho,

Nikaambiwa nifungue mdomo, yule mke wake nae ni kama akapandisha ila yete alikuwa anafunga macho tu, zimepita dakika 1 hivi nimechoka kufungua mdomo yule mtaalam akaniambia nifunge, mke wake bado hajajirudi hapo, akatokea binti wa miaka 15 hivi akawa anampiga began yule mke wa mtaalam nadhani ili ajirudi, baada ya sekunde kama 10 akajirudi, mke wake akaanza kumweleza vitu yule mtaalam kwa lugha zao sijui kiarabu au kirangi.

Basi tukaambiwa kwamba tukae hapo Kondoa kwa siku 3, usiku ule ule tukaenda kutafuta gesti.

Siku ya kwanza ya matibabu tulifika pale kwake ila hatukumkuta, yule binti alikuwepo aliachiwa maelezo atupeleke huko shambani ni umbali wa dakika 5 hivi, tulipofika binti akarudi sisi tukaenda sehemu aliyotuonyesha, yule mtaalam alipotuona akatuonesha ishara twende.

Ni kajumba kaudongo kadogo hivi kuna vyumba vya ghala, stoo ya kutunza majembe, ila kuna chumba tuliingia ndio cha shughuli, tulifika pale akarudia nikaambiwa niombe kwa Imani yangu, nilipomaliza akapiga dua yake pale, ndugu yangu wakawa wanaongea nae shida zangu anazitolea ufafanuzi zaidi, mke wake alikuwa pembeni akatuambia kwamba kuna mtu kanipokonya vitu vyangu aidha anavitumia yeye ama kuna mwengine kampa.

Mtaalam alitoka nje kidogo tukasikia sauti kama ya njiwa hivi anapiga mabawa kwa nguvu, mtaalam alirudi na manyoya kavaa softi / rambo kwenye mkono ili manyoya yasiguse ngozi yake, nikapewa hayo manyoya niyaweke kwenye kiganja changu cha mkono wa kulia, nilipoyaweka mtaalam akatoa unga flani hivi kwenye chupa za pale akamimina kwenye manyoya niliyoshika akaanza kuchanganya, manyoya yalopochanganyika akaanza kama kuyasugulla kwa nguvu kwenye kiganja changu, ni kama vile kiganja kilikuwa na uchafu sugu sasa anakisafisha kwa manyoya yale, mda wote huo bdo kavaa ile softi, alipomaliza akaniambia niyaweke manyoya kwenye mfuko flani hivi.

kabla sijaondoka,akaniongezea na sharti niwe naomba kila siku kabla sijalala na nikiamka, ndugu yangu akanicheki anakinisisitiza nifanya hivyo na ndicho nilikuwa nafanya.

Mchana ikafika nikaambiwa niende kusomewa dua ya maji, najiombea kisha nae anapiga dua yake huku nakunywa maji.

Usiku ulipofika akatuambia twende kule shambani, kule tumefika akaniambia nichote mwenyewe yale manyoya kiasi kinachogawanyika mara 3 kwajili ya siku 3, nayaweka kwenye kikopo nampa hicho kikopo, tunatoka nje naenda sehemu flani nakaa kwenye kigoda, nafunikwa shuka, kisha kuna kashimo kanachimbwa anatia mkaa wa moto kisha anafusha hayo manyoya moshi wote unakuja kwangu, dah, ule moshi wake msipime, moshi mzito unakohoa mpaka kujihisi kufa.

Siku ya pili asubuhi ni dua ya asubuhi nyumbani kwake na mimi najiombea, mchana dua tena ya maji na mimi najiombea, usiku anafusha manyoya

Siku ya tatu na ya mwisho nayo hivyo hivyo ila mchana aliweza kunipa dawa ya kuogea kwa siku 3 nikifika kwangu kwa masharti niogee ndoo nyeupe, niogee bafu safi nilifanyie usafi kabla ya kuoga na si chooni, nilitii na kutekeleza.

Matokeo nilianza kuyaona baada ya wiki 1 tu, nikawa ni mtu ambae kabla ua kulala natafakari sana maisha yangu ni vipi nakuwa sina malengo, ni vipi nakuwa naridhika kidogo kidogo, ni vipi nimekuwa mzito, n.k. huku nako kazini nikaanza kuona uvivu umeondoka nachapa kazi haswa, nimekuwa mchangamfu, mcheshi, n.k.

Ndugu alikuwa anani observe na akaona kweli nimebadilika aisee, Tulimshukuru sana yule mtaalam, tulienda kabisa huko kwake mimi nilimpelekea mzigo wangu kabisa kutoka jasho langu, ilibidi tumlazimishe sana achukue lakini alichochukua hata nusu hakikufika.

Nilianza kupata maendeleo kwa kupiga kazi zaidi na kuwa na umakini wa malengo yangu, niliweza kununua pikipiki, uchumi uliimarika, mabinti hawakuniumiza kichwa, niliweza kuhama uswazi kwenda sehem standard si haba, n.k.

Hadi sasa naendelea na mishe zangu, nilikuwa saidia fundi nilieridhika lakini nikafungua ofisi yangu, nilichoka kukaa mageto kwa sasa nimepanga nyumba huku nikiwa naendelea na ujenzi wa kajumba kangu, pikipiki niliona kifo njenje nikaiuza kwa sasa nina gari yangu ya kuzugia, nina familia, n.k.

Mtaalam alisharest in peace, nilisikia alifariki mwaka 2018 na familia yake ilihamia kwengine.
 
Nikiwa na miaka 19 nilipoanza maisha ya kujitegemea mtaani nilikuwa tayari nimeanza kujishughulisha lakini kipato changu kidogo kilinifanya niishi mazingira ya kawaida sana tofauti na tamaa ya vizuri nilivyovitaka nikiwa bado kijana mdogo.

Katika moja ya vitu nilikuwa napenda ni warembo ambao nilikuwa naishia kupigwa nyundo za mbavu kutoswa ama nikibahatika naachwa, chanzo kikuu kilikuwa hali yangu ya uchumi maana hata nauli tu kutuma ilikuwa inanipiga chenga, Kwa akili zangu za enzi hizo nikaona nahitaji kuboost mvuto wanipende zaidi kuzidi navyowapenda, niliamini nahitaji kujiongeza hivyo inabidi nitumie dawa nazozisikiaga zinaongeza mvuto niwe kama baadhi ya wale watundu wanaojua kuwafanya mabinti wawagombanie ( nyuma ya pazia wengi huwa wanahonga ila kwa umri wangu ule sikuwa nimeona mengi niliamini wengi ni dawa za mvuto)

nilikuwa mdau mzuri sana wa kutumia facebook kwenye kisimu changu enzi hizo 2014, nikajiunga magroup ya tiba asili, nikauliza naweza vp kuongeza mvuto kwa mkoa wangu, kuna wadau wakanishauri niende kwa mtu flani anauza dawa hizo pamoja na dawa zingine za kusafisha nyota, mvuto wa mapenzi, kurudisha mpenzi, kukamata mwizi, kinga, n.k.

Nilipofika kwake aliniuzia dawa ni ya unga unga nililipia elfu 20, dawa ile aliinadi inaongeza mvuto nikaioge kwa siku 3 mchana na usiku ntayaona matokeo.

nilifanya hivyo ila sikuona cha ajabu, nikaamua kupotezea tu niendelee na life, mziki ukaanza baada ya mwezi hivi watu wanasema nimepunguza uchangamfu, nimepunguza ucheshi wananiuliza kama nimefiwa, nimepunguza ari yangu ya kufanya kazi, n.k. kwa upande wangu nami huku malengo ya kufungua ofisi yangu nikaanza kupuuzia, natumia pesa ovyo sizitunzi hata chakula cha usiku naenda kula mgahawani, n.k. mimi nilikuwa naona sawa tu hakuna shida.

Hali hiyo ilidumu kwa mwaka na nusu hivi, watu wa karibu wakaanza kudhani natumia bangi, kuna ndugu yangu ambae ni rafiki pia wa karibu ndio akawa ananichunguza kwa ukaribu akaniambia sijitambui, kiukweli akaanza jitihada ya kunipeleka kanisani huko tumezunguka makanisa kama matatu lakini wapi maana huko kunahitaji Imani na mimi nilikuwa hata sina imani thabiti mda huo.

Niliwahi pelekwa pia kwa sheikh, yule sheikh alikuwa sio mbaguzi wa dini hivyo alinipiga visomo vya maana tu lakini bado tatizo lilikuwa kwamba mimi sina Imani.

Ndipo ikabidi sasa nisafiri na ndugu huko Dodoma, Kondoa . Uncle aliniambia kuna mtoto wa rafiki wake aliaguliwa huko so na sisi tujaribu.

Tulifika usiku huko, na sehemu ya kwanza tulifikia ni kwa mtaalam, mattalam huyu alikuwa pia ni shehe ila nilishindwa kujua ni vipi inakuwa hivi ila nikapotezea nikajikita na kilichonipeleka, mtaalam alikuwa yupo kwenye miaka 46 hivi na mke wake ni kama 25 nadhani, huenda alikuwa mke wa pili.

nilikuwa nimekaa kwenye kochi mtaalam alikuwa amekaa kwenye mkeka, akaniambia nami nikae kwenye mkeka, nilipata shida kidogo maana sikuzoea ila kibishi nikakaa.

Hakupoteza muda alipanisha majini hapo anaongea vitu habieleweki mixer kucheka kucheka, duh niliogopa aisee, kanitolea macho hapo, wakati natahamaki kinachoendelea anaongea vitu sielewi, il muda wotw huu mke wake anamwangalia na ni kama anamuongelesha mtaalam bila sauti. Baada ya dakika hivi mtaalam kajirudi yani jasho tele anahema na kutokwa jasho,

Nikaambiwa nifungue mdomo, yule mke wake nae ni kama akapandisha ila yete alikuwa anafunga macho tu, zimepita dakika 1 hivi nimechoka kufungua mdomo yule mtaalam akaniambia nifunge, mke wake bado hajajirudi hapo, akatokea binti wa miaka 15 hivi akawa anampiga began yule mke wa mtaalam nadhani ili ajirudi, baada ya sekunde kama 10 akajirudi, mke wake akaanza kumweleza vitu yule mtaalam kwa lugha zao sijui kiarabu au kirangi.

Basi tukaambiwa kwamba tukae hapo Kondoa kwa siku 3, usiku ule ule tukaenda kutafuta gesti.

Siku ya kwanza ya matibabu tulifika pale kwake ila hatukumkuta, yule binti alikuwepo aliachiwa maelezo atupeleke huko shambani ni umbali wa dakika 5 hivi, tulipofika binti akarudi sisi tukaenda sehemu aliyotuonyesha, yule mtaalam alipotuona akatuonesha ishara twende.

Ni kajumba kaudongo kadogo hivi kuna vyumba vya ghala, stoo ya kutunza majembe, ila kuna chumba tuliingia ndio cha shughuli, tulifika pale akarudia nikaambiwa niombe kwa Imani yangu, nilipomaliza akapiga dua yake pale, ndugu yangu wakawa wanaongea nae shida zangu anazitolea ufafanuzi zaidi, mke wake alikuwa pembeni akatuambia kwamba kuna mtu kanipokonya vitu vyangu aidha anavitumia yeye ama kuna mwengine kampa.

Mtaalam alitoka nje kidogo tukasikia sauti kama ya njiwa hivi anapiga mabawa kwa nguvu, mtaalam alirudi na manyoya kavaa softi / rambo kwenye mkono ili manyoya yasiguse ngozi yake, nikapewa hayo manyoya niyaweke kwenye kiganja changu cha mkono wa kulia, nilipoyaweka mtaalam akatoa unga flani hivi kwenye chupa za pale akamimina kwenye manyoya niliyoshika akaanza kuchanganya, manyoya yalopochanganyika akaanza kama kuyasugulla kwa nguvu kwenye kiganja changu, ni kama vile kiganja kilikuwa na uchafu sugu sasa anakisafisha kwa manyoya yale, mda wote huo bdo kavaa ile softi, alipomaliza akaniambia niyaweke manyoya kwenye mfuko flani hivi.

kabla sijaondoka,akaniongezea na sharti niwe naomba kila siku kabla sijalala na nikiamka, ndugu yangu akanicheki anakinisisitiza nifanya hivyo na ndicho nilikuwa nafanya.

Mchana ikafika nikaambiwa niende kusomewa dua ya maji, najiombea kisha nae anapiga dua yake huku nakunywa maji.

Usiku ulipofika akatuambia twende kule shambani, kule tumefika akaniambia nichote mwenyewe yale manyoya kiasi kinachogawanyika mara 3 kwajili ya siku 3, nayaweka kwenye kikopo nampa hicho kikopo, tunatoka nje naenda sehemu flani nakaa kwenye kigoda, nafunikwa shuka, kisha kuna kashimo kanachimbwa anatia mkaa wa moto kisha anafusha hayo manyoya moshi wote unakuja kwangu, dah, ule moshi wake msipime, moshi mzito unakohoa mpaka kujihisi kufa.

Siku ya pili asubuhi ni dua ya asubuhi nyumbani kwake na mimi najiombea, mchana dua tena ya maji na mimi najiombea, usiku anafusha manyoya

Siku ya tatu na ya mwisho nayo hivyo hivyo ila mchana aliweza kunipa dawa ya kuogea kwa siku 3 nikifika kwangu kwa masharti niogee ndoo nyeupe, niogee bafu safi nilifanyie usafi kabla ya kuoga na si chooni, nilitii na kutekeleza.

Matokeo nilianza kuyaona baada ya wiki 1 tu, nikawa ni mtu ambae kabla ua kulala natafakari sana maisha yangu ni vipi nakuwa sina malengo, ni vipi nakuwa naridhika kidogo kidogo, ni vipi nimekuwa mzito, n.k. huku nako kazini nikaanza kuona uvivu umeondoka nachapa kazi haswa, nimekuwa mchangamfu, mcheshi, n.k.

Ndugu alikuwa anani observe na akaona kweli nimebadilika aisee, Tulimshukuru sana yule mtaalam na katika zawadi tuliyompa nakumbuka niliongezea elfu 80 zangu mwenyewe sijui anko alimpa nini lakini kilifika.

Mtaalam alisharest in peace, nilisikia alifariki mwaka 2018 na familia yake ilihamia kwengine.
Mkuu hongera huyo Mtaalam alikurudisha nyota yako iliyo chukuliwa na maaduwi zako na pamoja na kukusafisha nyota yako mambo yako yatakwenda vizuri sasa Hongera zake huyo mtaalam ameshafariki RIP. Wapo wataalam wachache saa katika nchini yetu wanaoweza kukufanyia mambo yako yakawa. Kwani wengi wa Wataalam wa siku hizi ni matapeli. Mimi pia mmoja wapo nimesha wahi kuwafanyia watu wengi wamefanikiwa lakini hawaleti mrejesho kama wewe ulivyo leta hapa mrejesho wako.
 
Mkuu mimi huwa naulizaga kama kuna dawa ya kuvuta wateja?
 
sasa wale kuku siku za mwanzoni huwa ni kweli wanahusiana na kufanikisha utajiri au ni wao wanakula tu? Mimi tu KWA akili yangu ndogo huwa nafikiriaga damu ya kuku au mbuzi ingekua inahusiana na kupata utajiri africa hapa tungekuwa na matajiri wengi😂😂😂 . Halafu boss nieleweshe connection ya damu ya mtu na kuwa tajiri? Kuna mtu aliwahi kuniambia ukichukua kile kipande cha mti wa muhogo mchawi yoyote yule ukimpga nacho anaumia kitu kama hicho, nikamuuliza kwahyo kipande cha muhogo ndio mkuu wa wachawi? Akaniambia hapana, sasa kwanini wachawi wote ukiwapiga nacho wanaumia huoni kwamba kina nguvu kushinda wachawi wote ndo mana wanaumia kwakweli majibu yake mimi sikuyaelewa mpaka leo. Naonaga kaka Mshana Jr huwa anajuaga sana haya mambo mnieleweshe jamani😂😂😂🙏
Zipo lakini nyingi zinahitaji malipo ya kiroho ambayo huwa waganga wanaficha ficha.

kafara utaambiwa ni kuku tu siku za mwanzo, kuja kustuka wanahitaji utimamu wa mtu wako wa karibu na hakuna kuvunja mkataba.
 
sasa wale kuku siku za mwanzoni huwa ni kweli wanahusiana na kufanikisha utajiri au ni wao wanakula tu? Mimi tu KWA akili yangu ndogo huwa nafikiriaga damu ya kuku au mbuzi ingekua inahusiana na kupata utajiri africa hapa tungekuwa na matajiri wengi😂😂😂 . Halafu boss nieleweshe connection ya damu ya mtu na kuwa tajiri? Kuna mtu aliwahi kuniambia ukichukua kile kipande cha mti wa muhogo mchawi yoyote yule ukimpga nacho anaumia kitu kama hicho, nikamuuliza kwahyo kipande cha muhogo ndio mkuu wa wachawi? Akaniambia hapana, sasa kwanini wachawi wote ukiwapiga nacho wanaumia huoni kwamba kina nguvu kushinda wachawi wote ndo mana wanaumia kwakweli majibu yake mimi sikuyaelewa mpaka leo. Naonaga kaka Mshana Jr huwa anajuaga sana haya mambo mnieleweshe jamani😂😂😂🙏
Hangaika kuutafuta ufalme wa Mungu.
Haya mswali yako yatakufanya utamani kufanya ulozi.
 
Back
Top Bottom