Magaidi na wauaji wa kukodiwa, je hawa viumbe wa silika za hisia za huruma na ubinadamu?

FB_IMG_1679108142176.jpg
 
Kwamba kuna mazingira wanaweza kughairi kutekeleza mauaji kwa silika za hisia za upendo, huruma ama ubinadamu!?

Case study 1
Kuna shambulishi la kigaidi lilitokea Kenya kwenye jengo moja maarufu mtaa wa Westland wakati wa utawala wa Kenyatta.. Magaidi waliua watu wengi sana lakini kuna kijana alinusurika kwa kudra tu kisa ni kumhudumia vizuri gaidi kila alipokuja kwenye mgahawa wao ndani ya hilo jengo wakati huo gaidi akichora racket
Ni katikati ya milio ya risasi na watu kukimbia huko huko macho yao yalikutana na gaidi yule akaelekeza bunduki yake na kuendelea kuua wengine akimuacha hai yule kijana mhudumu waliyefahamiana pale mgahawani.. Hizi ni silika za ubinadamu na hutokea kwa ghafla sana!

Case study 2
Kuna muuaji maarufu wa kukodiwa ambaye alitajwa kama mmojawapo wa watu wenye roho mbaya zaidi duniani.. Huyu akapewa tenda ya kumuua binti mmoja mrembo aliyekuwa anadate na muuza madawa mmoja
Jamaa akapewa racket nzima na kila alichohitaji ili kukamilisha kazi yake ya mauaji... Akaenda mpaka mji aliokuwepo mrembo husika, akafika mpaka kwenye nyumba aliyokuwa anaishi huyo mrembo.. Akaingia ndani kwa mbinu zake
Kufika sitting room akamkuta binti mpweke kaka pekeyake.. Kuna kitu kikamkumbusha udogoni lakini akakikataa haraka sana akainua bastola amalize kazi lakini ghafla yule binti akamwambia.... Natambua umekuja kunimaliza na sina uwezo wa kujitetea ila nisaidie kitu kimoja tuu...

Jamaa akashikwa na butwaa kwakuwa alitegemea binti angepiga kelele na kukimbia ili apate vibe ya kummliza vizuri, lakini kinyume chake binti alitulia na kumwambia naomba kumbatio lako na busu lako moja tu kishapo ndio uniuwe.. Maana nimemiss kukumbatiwa na nimemiss kubusiwa tangu wazazi wangu walipofariki
Kwa sekunde chache ni kama jamaa alitaka kupoteza fahamu kuna vitu kama video inayoenda kasi sana vilipita machoni pake
Alivuta hatua mbili mbele akanyanyua mikono yote mmoja wa kulia ukiww bado na bastola akafumba macho akahisi tu mikono laini ikiwa kiunoni pake huku kichwa kikiwa kifuani mwake.. Kuna hisia anasema hajawahi kuzipata tangu azaliwe.. Walikiss na busu lile lilibadilisha kila kitu
Alibadili mawazo palepale akaisogelea simu na kumpigia boss aliyempa kazi na kumwambia nimeghairi kumuua nimeamua kuwa naye mpaka kifo kitakapotutenga...!

Kwanini nimeamua kutanguliza mifano hiyo miwili japo ipo mingi.. Kuna kitu kinaitwa the soft part of every human being.. Hapo mahali pakiguswa watu hubadilika kabisa tena ndani ya sekunde.. Na hiyo sehemu ina connection kubwa sana na macho! Macho huongea mengi zaidi sana kuliko mdomo..

Kilichonifanya niwaze haya ni kuhusiana na mauaji ya Neema! Bila kujali nini kilisababisha mpaka mwisho wake ukawa ule.. Nina hakika macho yalifanya kazi yake.. Kivipi?
Mdungaji sindano ya alikutanisha macho na mhanga.. Na inawezekana kabisa akaona ile hofu kubwa kwenye macho yake na pengine ile innocence katika wakati ule mgumu alishindwa kushindilia sumu yote! Na ilipofika wakati wa kumchoma moto alishindwa kabisa kummwagia mafuta usoni akikumbuka yake macho! Na ndio maana marehemu aliweza kukimbia kwakuwa alikuwa anaona.. (Haya ni mawazo yangu mimi)

Wazungu wanajua vema madhara makubwa ya 'soft part' kwenye mwili wa binadamu.. Soft part inaweza kutafsirika kama sehemu dhaifu/laini lakini haiko maungoni iko nafsini kupitia mlango wa macho
Wazungu wana mifano na kumbukumbu nyingi zilizofelisha mipango mikubwa hatari na ya siri kwasababu tu ya soft part..!

Kwa ajili ya kulikabili hili walifanya project nyingi za kuangalia namna ya kuua silika za hisia za kibinadamu ndani ya mwili wa mtu na wakagundua kuwa kwa sehemu kubwa zinabebwa na background katika makuzi ya mtu , toka utotoni, ujanani shuleni mpaka mtu anapofikia kwenye mafunzo ya ujasusi na mafunzo mengine yanayohitaji ukakamavu roho mbaya, roho ngumu nk..

Waligundua soft part inahusika sana na muingiliano kwenye makuzi na wazazi, ndugu, jamaa, marafiki, wapenzi na hata maadui..silika za hisia hujengwa toka makundi hayo

Naendelea..

Ukurasa wa pili
Ili kuweza kuua silika za hisia project mbili au tatu hivi zikaonekana zina matokeo chanya zaidi
Project ya kwanza ilikuwa ni kupata binadamu mpya ambaye tangu udogoni hajui wazazi,hajui marafiki hajui ndugu hajui furaha hajui huzuni nknk .. Zaidi ya anaokutana nao ambao nao nyuso zao hazioneshi hisia zozote zaidi ya kupewa kama ni chakula nguo au mafunzo
Hapa ndio wakaja na project ya watoto wa chupa.. Wanatungwa mimba kwenye chupa, mimba inalalewa maabara kwenye chupa na wanazaliwa maabara.

Wakitoka huko wanapelekwa mahali mbali kusiko na harakati za kidunia na kufunzwa kila watakacho mpaka wanapokuwa wakubwa wakiwa wameiva kwa mafunzo

Hawa hawana silika za hisia zozote kabisa! Hawajui kupenda, hawajui kupendwa, hawajui machozi hawajui huzuni hufanya kile wanachotumwa basi.. Hawashawishiki kwa pesa kwa ngono wala kwa chochote na kama nusu robot
Shida ilikuja kuonekana kwa baadhi kuanza kuwa na silika za hisia za kibinadamu baada ya kuanza kuchanganywa na binadamu wa kawaida waliozaliwa kupitia ngono na kubebwa mimba na mwanamke

Project ya pili
Hii ilikuwa ni kuwahuisha na unyama na ukatili binadamu waliokwisha zaliwa kawaida na wenye back kwa kuua silika zao za hisia kupitia mafunzo magumu mno yenye kuumiza nafsi zaidi kuliko mwili
Kuna viini vikuu vya hisia
Furaha
Huzuni
Maumivu
Matamanio
Chuki
Visasi
Roho ngumu
Roho mbaya
Yote haya kwa asilimia 90 silika zake za hisia huonekana kupitia mlango wa fahamu wa macho
Kwa hiyo mafunzo ya kwanza ni kuwa na uso mtupu.. Uso usioonyesha hisia zozote..kivipi
Kushuhudia, kulazimishwa kila siku kuangalia mtu akiteswa mpaka kifo
Kushuhudia, kuangalia kila siku mtu akichinjwa mbele yako
Kulazimishwa kuangalia kila siku watu wakifanya ngono mbele yako na mafunzo mengi yanayofanana na hayo. . ni mengi mno

Haya mafunzo hurudiwa maranyingi mpaka kufikia kuona ni kitu cha kawaida kabisa na baada ya hapo huingia kwenye vitendo nawe ukitakiwa kufanya.. Mwanzoni utapata tabu kidogo na adhabu kubwa sana za kikatili so next time utakaza roho ili usiumizwe.. Ndani ya mwezi nawe ni muuaji usiye na huruma

Naendelea
Ukurasa wa tatu
Watu hawa magaidi na wauaji wa kukodiwa hawa wa mafunzo huchaguliwa kutokana na background zao hasa za utotoni na ujana wa awali
Kamwe na ni aghalabu kuchukua kijana aliyelelewa maisha mazuri na ya upendo, maisha ya dini na kumshika sana Mungu huku upendo vikitamalaki kila upande kuanzia nyumbani hadi shuleni mtaani hadi kwa ndugu na marafiki

Wanaochaguliwa ni wale ambao tayari mioyo yao imepata damage mbalimbali zenye kugusa moja kwa moja silika za hisia kibinadamu,
Ambao walinyanyasika udogoni,
Ambao waliteswa
Ambao walibaguliwa nknk
Hawa ndio target bora sana shida iliyopo ni kwamba bila kujali binadamu ni katili kiasi gani hakosi sehemu dhaifu ndani ya mwili wake nafsini kutoka kwenye makuzi yake!

Sasa katika ukatili wake anapokutana na situation inayompelekea kwenye soft part yake.. Hubadilika hapo hapo na kuwa mtu mpya mwingine kabisa! Na hili limewafanya wazungu waingie kwenye project za cloning

Je, tupo pamoja? Your soft part...!
Somo maridhawa
 
SIKU YA HUKUMU: Video hii ya kusisimua inaonyesha wakandarasi wa zamani wa ujenzi wakiongozwa hadi mahali pa kunyongwa na askari wa Kijeshi wa Uturuki baada ya kupatikana na hatia na kuhukumiwa kifo. Walikuwa na hatia ya kuidhinisha kazi mbovu ya ujenzi kwenye majengo mengi yaliyobomoka wakati wa tetemeko la ardhi. Kulingana na watu wa ndani, wakandarasi hao hawakufuata mipango iliyohitaji Dampers za Seismic chini ya misingi yote - kunyonya harakati za tetemeko la ardhi. Badala yake, walizika matairi ya gari chini ya majengo mengi wakidhani kwamba matairi yangestahimili matetemeko mabaya ya ardhi. Kama matokeo, majengo mengi ya juu yalianguka wakati wa tetemeko la ardhi la 7.8 ambalo liliua zaidi ya watu elfu 55 nchini Uturuki hivi karibuni.
 
Back
Top Bottom