chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 12,505
- 21,563
Katika taaluma ambayo ina " wasanii" wengi ni taaluma ya habari, kulikuwa na tukio moja la kubomoa nyumba katika eneo letu, jamaa mmoja mjanja mjanja akasema ana namba ya mwandishi wa habari, akampigia akaja fasta.
Baada ya kufika akadai tumpe za kwake kwanza, na pili, ili habari iwe ya kwanza au ya pili, lazima tufanye mpango mhariri wa makao makuu, aonwe, tukampa.
Baada ya hapo alitoa ushauri ulioacha kizaa zaa na fadhaa, akasema kila mtu akusanye hisia aanze kulia kwa sauti kuu kama mjita au mkerewe au mnyakyusa amefiwa.
Kwa wanaume ikawa changamoto, watu walikuwa wanakamua macho chozi litoke, wapi, sauti za kulia zinagoma, zinatoka kama za spika iliyopasuka, wengi wakaishia kudondosha kope tu kwa kukaza macho.
Kwa wanawake ilichukua sekunde, zilifyatuka sauti kama mtu kaumwa na nyoka. Habari ikaenda.
Nchi hii usanii mwingi sana, baada ya hapo mwandishi akawapongeza walioloa kwa sauti kubwa, akasema lazima kesho watapata majibu.