Magaidi na wauaji wa kukodiwa, je hawa viumbe wa silika za hisia za huruma na ubinadamu?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,638
697,929
Kwamba kuna mazingira wanaweza kughairi kutekeleza mauaji kwa silika za hisia za upendo, huruma ama ubinadamu!?

Case study 1
Kuna shambulishi la kigaidi lilitokea Kenya kwenye jengo moja maarufu mtaa wa Westland wakati wa utawala wa Kenyatta.. Magaidi waliua watu wengi sana lakini kuna kijana alinusurika kwa kudra tu kisa ni kumhudumia vizuri gaidi kila alipokuja kwenye mgahawa wao ndani ya hilo jengo wakati huo gaidi akichora racket
Ni katikati ya milio ya risasi na watu kukimbia huko huko macho yao yalikutana na gaidi yule akaelekeza bunduki yake na kuendelea kuua wengine akimuacha hai yule kijana mhudumu waliyefahamiana pale mgahawani.. Hizi ni silika za ubinadamu na hutokea kwa ghafla sana!

Case study 2
Kuna muuaji maarufu wa kukodiwa ambaye alitajwa kama mmojawapo wa watu wenye roho mbaya zaidi duniani.. Huyu akapewa tenda ya kumuua binti mmoja mrembo aliyekuwa anadate na muuza madawa mmoja
Jamaa akapewa racket nzima na kila alichohitaji ili kukamilisha kazi yake ya mauaji... Akaenda mpaka mji aliokuwepo mrembo husika, akafika mpaka kwenye nyumba aliyokuwa anaishi huyo mrembo.. Akaingia ndani kwa mbinu zake
Kufika sitting room akamkuta binti mpweke kaka pekeyake.. Kuna kitu kikamkumbusha udogoni lakini akakikataa haraka sana akainua bastola amalize kazi lakini ghafla yule binti akamwambia.... Natambua umekuja kunimaliza na sina uwezo wa kujitetea ila nisaidie kitu kimoja tuu...

Jamaa akashikwa na butwaa kwakuwa alitegemea binti angepiga kelele na kukimbia ili apate vibe ya kummliza vizuri, lakini kinyume chake binti alitulia na kumwambia naomba kumbatio lako na busu lako moja tu kishapo ndio uniuwe.. Maana nimemiss kukumbatiwa na nimemiss kubusiwa tangu wazazi wangu walipofariki
Kwa sekunde chache ni kama jamaa alitaka kupoteza fahamu kuna vitu kama video inayoenda kasi sana vilipita machoni pake
Alivuta hatua mbili mbele akanyanyua mikono yote mmoja wa kulia ukiww bado na bastola akafumba macho akahisi tu mikono laini ikiwa kiunoni pake huku kichwa kikiwa kifuani mwake.. Kuna hisia anasema hajawahi kuzipata tangu azaliwe.. Walikiss na busu lile lilibadilisha kila kitu
Alibadili mawazo palepale akaisogelea simu na kumpigia boss aliyempa kazi na kumwambia nimeghairi kumuua nimeamua kuwa naye mpaka kifo kitakapotutenga...!

Kwanini nimeamua kutanguliza mifano hiyo miwili japo ipo mingi.. Kuna kitu kinaitwa the soft part of every human being.. Hapo mahali pakiguswa watu hubadilika kabisa tena ndani ya sekunde.. Na hiyo sehemu ina connection kubwa sana na macho! Macho huongea mengi zaidi sana kuliko mdomo..

Kilichonifanya niwaze haya ni kuhusiana na mauaji ya Neema! Bila kujali nini kilisababisha mpaka mwisho wake ukawa ule.. Nina hakika macho yalifanya kazi yake.. Kivipi?
Mdungaji sindano ya alikutanisha macho na mhanga.. Na inawezekana kabisa akaona ile hofu kubwa kwenye macho yake na pengine ile innocence katika wakati ule mgumu alishindwa kushindilia sumu yote! Na ilipofika wakati wa kumchoma moto alishindwa kabisa kummwagia mafuta usoni akikumbuka yake macho! Na ndio maana marehemu aliweza kukimbia kwakuwa alikuwa anaona.. (Haya ni mawazo yangu mimi)

Wazungu wanajua vema madhara makubwa ya 'soft part' kwenye mwili wa binadamu.. Soft part inaweza kutafsirika kama sehemu dhaifu/laini lakini haiko maungoni iko nafsini kupitia mlango wa macho
Wazungu wana mifano na kumbukumbu nyingi zilizofelisha mipango mikubwa hatari na ya siri kwasababu tu ya soft part..!

Kwa ajili ya kulikabili hili walifanya project nyingi za kuangalia namna ya kuua silika za hisia za kibinadamu ndani ya mwili wa mtu na wakagundua kuwa kwa sehemu kubwa zinabebwa na background katika makuzi ya mtu , toka utotoni, ujanani shuleni mpaka mtu anapofikia kwenye mafunzo ya ujasusi na mafunzo mengine yanayohitaji ukakamavu roho mbaya, roho ngumu nk..

Waligundua soft part inahusika sana na muingiliano kwenye makuzi na wazazi, ndugu, jamaa, marafiki, wapenzi na hata maadui..silika za hisia hujengwa toka makundi hayo

Naendelea..

Ukurasa wa pili
Ili kuweza kuua silika za hisia project mbili au tatu hivi zikaonekana zina matokeo chanya zaidi
Project ya kwanza ilikuwa ni kupata binadamu mpya ambaye tangu udogoni hajui wazazi,hajui marafiki hajui ndugu hajui furaha hajui huzuni nknk .. Zaidi ya anaokutana nao ambao nao nyuso zao hazioneshi hisia zozote zaidi ya kupewa kama ni chakula nguo au mafunzo
Hapa ndio wakaja na project ya watoto wa chupa.. Wanatungwa mimba kwenye chupa, mimba inalalewa maabara kwenye chupa na wanazaliwa maabara.

Wakitoka huko wanapelekwa mahali mbali kusiko na harakati za kidunia na kufunzwa kila watakacho mpaka wanapokuwa wakubwa wakiwa wameiva kwa mafunzo

Hawa hawana silika za hisia zozote kabisa! Hawajui kupenda, hawajui kupendwa, hawajui machozi hawajui huzuni hufanya kile wanachotumwa basi.. Hawashawishiki kwa pesa kwa ngono wala kwa chochote na kama nusu robot
Shida ilikuja kuonekana kwa baadhi kuanza kuwa na silika za hisia za kibinadamu baada ya kuanza kuchanganywa na binadamu wa kawaida waliozaliwa kupitia ngono na kubebwa mimba na mwanamke

Project ya pili
Hii ilikuwa ni kuwahuisha na unyama na ukatili binadamu waliokwisha zaliwa kawaida na wenye back kwa kuua silika zao za hisia kupitia mafunzo magumu mno yenye kuumiza nafsi zaidi kuliko mwili
Kuna viini vikuu vya hisia
Furaha
Huzuni
Maumivu
Matamanio
Chuki
Visasi
Roho ngumu
Roho mbaya
Yote haya kwa asilimia 90 silika zake za hisia huonekana kupitia mlango wa fahamu wa macho
Kwa hiyo mafunzo ya kwanza ni kuwa na uso mtupu.. Uso usioonyesha hisia zozote..kivipi
Kushuhudia, kulazimishwa kila siku kuangalia mtu akiteswa mpaka kifo
Kushuhudia, kuangalia kila siku mtu akichinjwa mbele yako
Kulazimishwa kuangalia kila siku watu wakifanya ngono mbele yako na mafunzo mengi yanayofanana na hayo. . ni mengi mno

Haya mafunzo hurudiwa maranyingi mpaka kufikia kuona ni kitu cha kawaida kabisa na baada ya hapo huingia kwenye vitendo nawe ukitakiwa kufanya.. Mwanzoni utapata tabu kidogo na adhabu kubwa sana za kikatili so next time utakaza roho ili usiumizwe.. Ndani ya mwezi nawe ni muuaji usiye na huruma

Naendelea
Ukurasa wa tatu
Watu hawa magaidi na wauaji wa kukodiwa hawa wa mafunzo huchaguliwa kutokana na background zao hasa za utotoni na ujana wa awali
Kamwe na ni aghalabu kuchukua kijana aliyelelewa maisha mazuri na ya upendo, maisha ya dini na kumshika sana Mungu huku upendo vikitamalaki kila upande kuanzia nyumbani hadi shuleni mtaani hadi kwa ndugu na marafiki

Wanaochaguliwa ni wale ambao tayari mioyo yao imepata damage mbalimbali zenye kugusa moja kwa moja silika za hisia kibinadamu,
Ambao walinyanyasika udogoni,
Ambao waliteswa
Ambao walibaguliwa nknk
Hawa ndio target bora sana shida iliyopo ni kwamba bila kujali binadamu ni katili kiasi gani hakosi sehemu dhaifu ndani ya mwili wake nafsini kutoka kwenye makuzi yake!

Sasa katika ukatili wake anapokutana na situation inayompelekea kwenye soft part yake.. Hubadilika hapo hapo na kuwa mtu mpya mwingine kabisa! Na hili limewafanya wazungu waingie kwenye project za cloning

Je, tupo pamoja? Your soft part...!
 
Ndugu mshana, kiasili kila mtu huwa ana hiyo hulka ya huruma ila mara nyingi sana katika mauaji ya aina hii huwa mhusika marehem saa zingine wanakuwaga wabishi, kumekuwa na ile hali ya watu kuchukuliana poa labda kwa kujuana au kutojua na saa zingine unaweza kumjibu vibaya mtu usiyejua dhamira yake ni ipi kwako.
Unaweza kuta mtu amekuja kwako akiwa na hasira za kupitiliza juu yako na aliedhamiria kukutendea unyama lakini wewe kwa kutojua dhamira yake ukajikuta manajibizana na unampandisha hasira mara20 zaidi ya alizokuwa nazo awali,

Mara nyingi mauaji ya hivi huwa hayana huruma wala majuto kwa mtendaji anaweza kukuua lakini bado kwa hasira zake anaona kama bado hiyo haikutoshi na akatamani ufufuke akuuwe tena, ndio maana unakuta mtu ameua alafu amechoma mto na ikiwezekana kutenganisha viungo kimoja baada ya kingine.

Na siku zote mtu akidhamiria kukutendea ubaya pasipo wewe kujua mara nyingi huja na gia ya kukutaka umkere ili apate vibe la kukudhuru bila huruma,

Chamsingi na chakujifunza hapa ni kwamba tuishi na watu vizuri, na unapoona mtu usiyemjua anatafta sababu kwako hebu tujifunze kuwa unyenyekevu na wapole, huwezi kujua unaepusha yapi
 
Ndugu mshana, kiasili kila mtu huwa ana hiyo hulka ya huruma ila mara nyingi sana katika mauaji ya aina hii huwa mhusika marehem saa zingine wanakuwaga wabishi, kumekuwa na ile hali ya watu kuchukuliana poa labda kwa kujuana au kutojua na saa zingine unaweza kumjibu vibaya mtu usiyejua dhamira yake ni ipi kwako.
Unaweza kuta mtu amekuja kwako akiwa na hasira za kupitiliza juu yako na aliedhamiria kukutendea unyama lakini wewe kwa kutojua dhamira yake ukajikuta manajibizana na unampandisha hasira mara20 zaidi ya alizokuwa nazo awali,

Mara nyingi mauaji ya hivi huwa hayana huruma wala majuto kwa mtendaji anaweza kukuua lakini bado kwa hasira zake anaona kama bado hiyo haikutoshi na akatamani ufufuke akuuwe tena, ndio maana unakuta mtu ameua alafu amechoma mto na ikiwezekana kutenganisha viungo kimoja baada ya kingine.

Na siku zote mtu akidhamiria kukutendea ubaya pasipo wewe kujua mara nyingi huja na gia ya kukutaka umkere ili apate vibe la kukudhuru bila huruma,

Chamsingi na chakujifunza hapa ni kwamba tuishi na watu vizuri, na unapoona mtu usiyemjua anatafta sababu kwako hebu tujifunze kuwa unyenyekevu na wapole, huwezi kujua unaepusha yapi
Ni sahihi kabisa na hili lipo hata kwa wanyama.. Kuna opposite reaction isipoonekana upande wa pili kuna NGUVU fulani hupungua upande mwingine

Sasa ishu inakuja kwa hawa professional killers.. Ambao ni trained killers .. Wenye utaalam wa kuua kwa aina nyingi tuu.. Na ile pleasure wanayoipata pale wanapoangalia mhanga wao anavyokata roho!

Sasa watu kama hawa huwa na kichokoo kilichowafanya mpaka kufikia kufanya hiyo kazi LAKINI kuna mahali huguswa hisia zao za ndani (silika) kwa namna ya ajabu kabisa na kujikuta nukta moja tuu ikawabadili mtazamo mazima
Na hii hali hutokana na matukio adimu ya utotoni.. Matukio ambayo yalikuwa ya kipekee kiasi cha kujihifadhi kwenye ile soft part ya nafsi!
Hayo matukio yenye kubeba hisia maalum yakija kujitokeza tena mahali ukubwani huwa na impact kubwa sana
 
Mbona ipo wazi ishu ni maslahi kwa namna yeyote..

Mbele ya pesa watu weny ubinadany ju wachache.

Jaalia watu wanagombana kisa wamekopeshana hata kuwa maadui .je mtu akilipwa pesa nyingi akumalize atashindwa kweli?

Huruma inakuwepo na ndo tabia za binadamu ila Inakuwa imepotea pale inapozidiwa na Tamaa za maslahi .


Jamii zenye kuendekeza pesa hazina utu kabisa na ni wakatili kabisa..watu wanatoa kafara watoto wao wa kuwazaa kisa maslahi
 
Umenikumbusha kisa cha mnyongaji wa watu katika dola moja hivi aliwahi kusimulia kua kila alipomaliza kazi alikua hawezi kua na amani na alilia akiwa kajifungia chumbani peke yake na pombe na vilevi vingine alivyotumia viliisha haraka sana , alikuja kuachana na ile kazi kwa hiari, na chanzo ni kua yeye alilelewa na bibi yake ambaye alikua anamwonesha upendo sana na alipata kumweleza wauwaji walivowaua wazazi wake, na bibi akawa anasisitiza asijekua muuaji awe mpenda watu kwahiyo hilo lilimtesa sana ,
 
Back
Top Bottom