Maendeleo hayaletwi na vyama vya siasa

Ndugu wananchi maendeleo hayaletwi na vyama vya siasa, maendeleo yanaletwa na watu walioamua kuendelea.

Nchi ikiwa na wananchi walioamua kuendelea itaendelea tu.

Vijana changamkeni tumieni nguvu zenu. Nchi yetu ipo wanasiasa hawataweza hata siku moja kutuletea maendeleo.
wala hayaletwi na katiba
 
serikali inatumia rasilimali fedha kwa maana ya kodi kutekeleza ilan ya chama kilichopo madarakani kama ilani imejikita kukimbiza mienge na maadhimisho yasiyo na tija unategemea nn? ile post ya ile research inayoonyesha IQ level yetu inahold hapa.
 
Mbona hujataja Ccm Kwani sio chama cha siasa? acha chuki kama huipendi CDM kaa kimya umeleta mada vizuri halafu unaiharibu kwa kuanza ushabiki. Hivi jamani Chadema imewafanya nini?

Hakika Mkuu unajua wanatapatapa wamekosa hoja zenye mashiko za kuwaambia wananchi ndio maana wamekurupuka na hiyo hoja finyu kuwa maendeleo hayaletwi na vyama vya siasa wakati huo huo wanazunguka kuhubiri kuwa chama chao kimewaletea wananchi maendeleo makubwa kutokana na sera zao je ccm sio chama cha siasa? hakika wameshikwa pabaya tusishangae wakisema maendeleo hayaletwi na watu
 
We rudi darasani ukajuzwe uhusiano uliopo kati ya siasa na vyama vya siasa pia siasa na maendeleo.acha kutumiwa kama kalai orofani utakuwa huru
 
Hapana nakataa,,,sera thabiti na mipango anuai ndio geti la maendeleo. Hata wote tukifanya kazi masaa 24 bila sera (micro and macro-economic models) hatutaenda.
 
Ndugu wananchi maendeleo hayaletwi na vyama vya siasa, maendeleo yanaletwa na watu walioamua kuendelea.

Nchi ikiwa na wananchi walioamua kuendelea itaendelea tu.

Vijana changamkeni tumieni nguvu zenu. Nchi yetu ipo wanasiasa hawataweza hata siku moja kutuletea maendeleo.

Naunga mkono hoja 100%.
 
Siasa ni nini?
Siasa ni mfumo na mtindo au utaratabu wa maisha ya jamii ya binadamu uliokubaliwa na watu katika jamii au jumuiya hiyo ikiwa ni pamoja na uendeshaji wa utawala, mipangilio ya utawala, umiliki wa nguvu za umma, na muingiliano na mahusiano ya maslahi ya makundi mbalimbali katika jamii [Tafsiri yangu]. Siasa ni elimu, maarifa na ujuzi ambao hutoa msimamo na msingi wa jamii.

Kila jamii huwajibika kufuata misingi iliyowekwa katika maisha ya kila siku, hivyo matokeo na maamuzi ya kuchagua, kulinda, kuhifadhi mfumo mbovu au mzuri wa utawala ni matokeo ya jamii husika. Vilevile kuna siasa ya serikali ambayo ni mipango na kanuni za utekelezaji wa shughuli za kiserikali kwa chama kinachotawala kwa kufuata katiba ya nchi ambayo ndio mtoa sheria mkuu.

Ni ufinyu wa kifikra kutenganisha maendeleo, siasa na vyama vya siasa. Siasa ni sawa na maji ya kunywa au kupikia n.k. haiepukiki. Ni ushabiki tu wa kisiasa usiozingatia umantiki wa HOJA na UFANISI wa kiutendaji ndio umetuletea aina ya viongozi ambao sasa ni mzigo kwa Taifa letu na kukosa jinsi ya kufanya isipokuwa kupokea matokeo ya ushabiki wetu kwa hoja za kutenganisha maendeleo, siasa na vyama vya siasa.

Hapa mkuu uko sawa kuna watu wanaotaka kwa makusdi kupotosha wenzao. hawa ni sawa na wale wanaokuambia katiba siyo muarobaini wa matatizo ya mwananchi halafu akimaliza analalamika:
- watoto kukaa chini
- nauziwa dawa feki za ruzuku
- hospitali haina dawa
-nakatazwa kuuza mahindi pale penye bei nzuri .nk.

hajui hayo ni matokeo katiba dhaifu na yote ni siasa
naungana na aliyesema SIASA=UCHUMI =MAISHA

acheni kuwapotosha watanzania iliwawaachie muendelee kuwakandamiza
 
sasa mbona hujatoa mfano hata mmoja wa jinsi vyama vyote vinavyofanana kulinda maslahi ya viongozi wao ili tuweze nasi kulinganisha.maana nionavyo mimi tofauti ipo tena kubwa nashangaa mtanzania mwenzangu kutoina hiyo tofauti.naukiitaka mimi nipo tayari kukueleza hizo tofauti.
Fuatilia visa vyote vihusuvyo green, red or blue maybe utanielewa, halafu angalia mtazamo wa viongozi wa vyama vyote kuhusu kumuinua mtanzania wa chini (masikini) na matendo yao, matumizi ya mali zao za halali na zisizo za halali labda utanielewa.

Naamini hakuna Chama chochote kitakachotuletea maendeleo endapo sisi wenyewe hatutaamka na kuwawajibisha viongozi wabovu, mafisadi na wala rushwa hata kama chama hicho kitatoka wapi. KWA SASA tumekuwa kama watoto yatima tunaosubiri wapita njia watupe makombo tuokote.
 
Ndiyo maana binafsi siamini kabisa kuwa mabadiliko nchini yataletwa na wasomi hasa wale wenye kufurahia utawala wa CCM! Ni sawasawa na hapa Marekani ambapo historia inatuonesha tofauti ya “watumwa wa nyumbani”na “watumwa wa kondeni”.

Watumwa wa nyumbani walikuwa karibu sana na bosi na walipewa mahali pa kula na kulala na walitendewa vizuri zaidi kuliko watumwa wa kondeni. Matokeo yake ni wale watumwa wa kondeni ndio hatimaye waliweza kuwa chachu ya mabadiliko kuliko watumwa wa nyumbani. Maana hawa wa nyumbani kuambiwa kuwa kuna uhuru wanajikuta hawaamini kwamba watoke katika ‘maisha mazuri’ na kwenda kwenye ‘uhuru’haiingii akilini.

Lakini wenginewalipoweza kufunguliwa kiakili waligeuka wapelelezi wazuri sana; lakini wengine walikufa wakiwa wanafurahia kuitwa “mtumwa mzuri kwa bwana wake!”....

Haya ni maneno ya Makala ya M.M wanakijiji 2012
 
Ndiyo maana waliyoichoka ccm wanafanya mambo yao kimyakimya, mradi una nyumba yako, unakula vizuri wewe na familia yako una usafiri, watoto wanasoma shule nzuri basi unatulia
 
Kwenye siasa siku hizi kuna kitu kinaitwa kubadili gia angani
 
Ndiyo maana binafsi siamini
kabisa kuwa mabadiliko nchini
yataletwa na wasomi hasa wale
wenye kufurahia utawala wa
CCM! Ni sawasawa na hapa
Marekani ambapo historia
inatuonesha tofauti
ya “watumwa wa nyumbani”
na “watumwa wa kondeni”.
Watumwa wa nyumbani
walikuwa karibu sana na bosi
na walipewa mahali pa kula na
kulala na walitendewa vizuri
zaidi kuliko watumwa wa
kondeni. Matokeo yake ni wale
watumwa wa kondeni ndio
hatimaye waliweza kuwa
chachu ya mabadiliko kuliko
watumwa wa nyumbani. Maana
hawa wanyumbani kuambiwa
kuwa kuna uhuru wanajikuta
hawaamini; kwamba watoke
katika ‘maisha mazuri’ na
kwenda kwenye ‘uhuru’
haiingii akilini. Lakini wengine
walipoweza kufunguliwa kiakili
waligeuka wapelelezi wazuri
sana; lakini wengine walikufa
wakiwa wanafurahia
kuitwa “mtumwa mzuri kwa
bwana wake!”....Haya ni maneno ya Makala ya M.M wanakijiji 2012

MBUNGE WA UBUNGO SAED KUBENEA ALIVYOELEZA UNAFIKI NA UFISADI WA LOWASSA KATIKA KAMPUNI HEWA YA RICHMOND.

Lowassa anajua uzalendo au ni machozi ya mamba?

Saed Kubenea's picture
Na Saed Kubenea - Imechapwa 18 January 2012

Printer-friendly version
Gumzo la Wiki
EDWARD Lowassa, yule aliyejiuzulu nafasi ya waziri mkuu kutokana na kashifa ya kuingiza nchi kwenye mkataba wa kinyonyaji wa makampuni ya Richmond/Dowans, sasa anasaka utakaso.

Katika kasi yake, anakemea hata asiostahili kukemea na anasema yale ambayo wengi wanajenga shaka kama anaweza kuyasimamia.

Akiwa mkoani Kigoma, kwenye harambee ya ujenzi wa Sekondari ya Kanisa la FPCT Bigabiro, Lowassa amenukuliwa akisema, “Nguvu ya umma inayotumiwa na baadhi ya vyama vya siasa kushinikiza serikali kutekeleza mambo mbalimbali, haiwezi kuleta maendeleo wala tija kwa taifa.”

Mbunge huyo wa Monduli, alifika mbali zaidi. Alidai kuwa hivi sasa wananchi wengi hawataki kujitolea kwa sababu “wamepoteza uzalendo.” Alisema kila wanachokifanya, ikiwamo kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao, wanataka kulipwa fedha.”

Jumla ya Sh. 125 milioni zikiwamo ahadi, zilichangwa kwenye harambee hiyo, huku taarifa zikisema Lowassa na wale aliowaita “marafiki zake,” walitoa Sh. 60.5 milioni.

Lowassa hakutaja jina la chama cha siasa ambacho ametaka kiachane na matumizi ya nguvu ya umma yanayolenga kushinikiza serikali kutekeleza matakwa ya wananchi. Wala hakutaja chama ambacho amekitaka kitumie nguvu ya umma kushinikiza wananchi kufanya kazi za kujitolea.

Bali kila mmoja anajua kuwa Lowassa amelenga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Hiki ndicho kinajitambulisha kwa kauli mbiu ya nguvu ya umma – “People’s Power.”

Je, Lowassa anaamini anachokisema? Anastahili kueneza anachokihubiri? Kama haamini anachokisema na anahubiri asichostahili kuhubiri, nini kimemsukuma kueleza haya sasa?

Kwanza, Lowassa haamini kwenye kujitolea “nguvu kazi.” Ndiyo maana kila anakopita, hakuna ambako aliweka nguvu kazi yake. Hakuna alikotoa jasho lake. Bali kote alikopita, kuanzia mkoani Singida, Mwanza, Arusha, Dar es Salaam, Pwani, Kilimanjaro na Kigoma, Lowassa amemwaga fedha, badala ya kujitolea nguvu kazi.

Pili,Lowassa anajua sababu za wananchi kupoteza uzalendo na kutaka kulipwa ujira kwa kazi wanayoifanya. Ni kwa sababu, wamechoshwa na vitendo vya viongozi wao waliowapa dhamana.

Kwa mfano, baraza la mawaziri liliagiza mkataba kati ya serikali na makampuni ya Richmond/Dowans uwe wa mwaka mmoja. Lakini baadhi ya viongozi, Lowassa akiwa miongoni mwao, walibadilisha maelekezo ya baraza la mawaziri na kuliamuru Shirika la Umeme la Taifa (TANESCO), kujifunga kwenye mkataba wa miaka miwili.

Aidha, kwa kisingizio cha nchi kutaka kuingia gizani, Lowassa aliamuru kubadilishwa kwa vigezo vya utoaji wa zabuni kutoka 24 vilivyowekwa awali hadi vinne ili kuweza kuibeba Richmond.

Pale alipoona Richmond imeshindwa kukidhi hata kigezo kimoja kutoka miongoni mwa vigezo vinne vipya vilivyowekwa, kikiwamo kile kinachoweka sharti la kampuni kuwa na uzoefu wa angalau mwaka mmoja katika miradi ya umme, aliamuru kazi ya kutafuta mzabuni ifanywe na kamati ya serikali, badala ya Bodi ya Tenda ya TANESCO.

Mbali na hayo, Lowassa anafahamu thamani halisi ya mitambo ya Richmond/Dowans; si zaidi ya dola za Marekani 40 milioni. Lakini kwa makusudi alikubali serikali kujifunga kwenye mkataba unaowalazimisha kuilipa kampuni hiyo, kwa kila siku, kama malipo ya kuweka mitambo – Capacity Charge – dola za Marekani 100,000; karibu Sh. 152 milioni.

Kiasi hiki ni nje ya fedha zinazotumika kununulia umeme; zitakazolipia matengenezo ya mashine na zitakazotumiwa kugharamia usafirishaji mafundi kutoka nje ya nchi.

Katika kipindi cha miezi 21 ya uhai wa mkataba, tayari Richmond/Dowans walishavuna kutoka serikalini, zaidi ya dola za Marekani 66.4 milioni (karibu Sh. 90 bilioni). Kiasi hiki cha fedha, ni mara mbili ya bei halisi ya mitambo.

Baadaye wanaojiita wamiliki wa Dowans wakaenda mahakamani kudai serikali kwa kisingizio cha kuvunjwa kwa mkataba wake wa miezi 24. Mahakama bila kuhoji uhalali wa fedha inayodaiwa; bila kuhoji sababu za Richmond/Dowans kutaka kulipwa mkataba wote, wakati uhai wa mkataba ulibaki miezi mitatu, ikaamuru TANESCO kulipa kiasi cha Sh. 90 bilioni.

Mahakama ikaweka hata sharti jingine la serikali kulipa riba ya karibu asilimia 30 kwenye viwango vya dola. Sasa deni linaendelea kukua siku hadi siku hadi kufikia Sh. 120 bilioni.

Ukichua kiasi ambacho mahakama imeamuru kilipwe kwa Dowans, ukakichanganya na fedha ambayo tayari serikali imelipa katika kipindi cha miezi 21 ya uhai wa mkataba, utapata jibu moja: Mashine zenye thamani ya dola za Marekani 40 bilioni, tayari zimevuna ama zinatarajiwa kuvuna dola za Marekani 258 milioni (Sh. 397 bilioni) ndani ya muda mfupi wa miaka mitano.

Kama hiyo haitoshi, serikali ikakubali kujifunga kwenye mkataba mwingine wa milele na milele na kampuni ileile iliyojibadili jina tu na kujiita Symbon Power LLC, lakini ikiwa inatumia mitambo ileile ambayo italipwa Sh. 365 bilioni.

Hadi hapa, nani anaweza kuitikia wito wa Lowassa wa “kujitolea?” Nani anaweza kumsikiliza? Kama kujitolea, mbona ni yeye aliyekuwa anatakiwa kufanya hivyo kwenye kipindi cha kusaini mkataba na kutafuta mzabuni?

Lowassa ameshindwa nini, wakati alikuwa analipwa na serikali; analishwa na serikali na anavishwa na serikali? Hata sabuni ya kufulia mto wa kitandani kwake, shuka la kujifunika, sabuni na makochi anayotumia, vyote vinalipiwa kwa fedha za wananchi?

Yule aliyeshitaki serikali; aliyelipwa mabilioni ya shilingi na serikali kwa mashine zenye thamani ya Sh. 60 bilioni; na ambaye sasa anashinikiza kulipwa mabilioni mengine, ni mmoja wa maswahiba wakuu wa Lowassa na mshirika wake mkubwa kisiasa, Rais Jakaya Kikwete.

Rostam Aziz, mwanachama mashuhuri na muhimu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndiye aliyeshitaki, aliyeajiri mawakili, ndiye alidai na ndiye anayepokea na atakayepokea malipo yoyote ya fedha kwa niaba ya makampuni ya Dowans Holding SA, Dowans Tanzania Limited (DTL) na Richmond Development Company (LLC).

Lakini kuna hili pia. Lowassa anafahamu jinsi katibu wa TANESCO, Subira Wandiba, alivyojitolea kwa taifa lake. Alieleza kwa ufasaha ubatili wa hatua ya Richmond ya kuhamisha mkataba.

Wandiba alikuwa akiandikia mwenyekiti wa bodi ya TANESCO, Balozi Fulgence Kazaura, tarehe 28 Novemba 2006, kwamba “…kufuatana na mkataba wa 23 Juni 2006, Richmond hairuhusiwi kuhamisha mkataba wao kwenda kampuni nyingine yeyote.” Hii ilikuwa kabla ya mkataba kumilikishwa kwa Dowans.

Lakini nani alimsikiliza Wandiba? Nani alisikiliza ushauri wake, kwamba Richmond – kampuni iliyopewa mkataba kwa upendeleo, ikiwa haina fedha, haina utaalam wala historia ya kufua umeme – haikupaswa kuhamisha mkataba wake kama ilivyofanya tarehe 23 Desemba 2006. Ilikuwa kinyume cha sheria za nchi.

Akiwa nchini Canada, Nazir Karamagi aliyekuwa waziri wa nishati na madini, aliamuru Richmond kuruhusiwa kuhamisha mkataba wao. Leo hii, Wandiba ameondolewa kwenye nafasi yake hiyo. Je, uzalendo ambao Lowassa anasema uko wapi, ikiwa wale ambao wameonyesha uzalendo ndio wanasakamwa na hata kuondolewa kazini?

Nani anaweza kuwa mzalendo, wakati wale ambao wamesababisha haya, wanaendelea kupeta? Wanalipwa na serikali. Wanahudumiwa na serikali. Wanatumia magari ya serikali; wanakaa nyumba za serikali na wanatibiwa nje ya nchi kwa gharama za walipa kodi wa hapa?

Nani ataweza kuwa na moyo wa kujitolea, wakati Lowassa mwenyewe anaendelea kulipwa mafao ya waziri mkuu mstaafu, wakati ukweli ni kuwa hakustaafu?

Nani anaweza kujitolea nguvu kazi yake wakati anaona rasilimali za taifa zinatumika kugharamia watu walioshindwa kazi; waliongiza nchi kwenye mikataba yenye utata na wanaoendelea kulipwa, wao na wasaidizi wao, kwa fedha za walalahoi?

Nani ataweza kutumia nguvu kazi yake kufanya kazi ya maendeleo, wakati nguvu walizotumia kufanya kazi zao binafsi na kulipa kodi kubwa isiyo na kipimo, inatumiwa na wale waliosaidia kufikisha taifa hapa lilipo?

Nani atakubali kumwaga jasho lake kufanya kazi za kujitolea, wakati wanaona kiongozi wao – Waziri Mkuu Mizengo Pinda – anayelipiwa kila kitu na serikali akisaini posho ya Sh.250,000 kwenye semina ya Bunge?

Ilitegemewa badala ya Lowassa kuwaalani na kuwadhihaki wanaoshinikiza wananchi kupinga udhalimu huu; wanaotaka serikali kuwajibika kwa wananchi wake; wanaotaka kupunguzwa kwa ugumu wa maisha; angesimama pamoja nao – hata kama yeye si miongoni mwa wanaojua bei ya sukari, mafuta, chuvi, umeme na kibiriti – kuhimiza serikali kutekeleza wajibu wake.

Angalau angefanya hivyo, angeweza kusamehewa kwa dhambi hii aliyosababishia taifa hili. Lakini kwa hatua yake ya kusema wananchi – wenye njaa, wanaopunjwa bei ya mazao yao, wanaolazimishwa kutoa rushwa kwa kila huduma wanayostahili – wamepoteza uzalendo; basi amefanya dhihaka ambayo inahitaji toba.

Wananchi waandamanaji ambao Lowassa anawalaani wanataka kuona taifa lao linatokomeza ufisadi; linakuwa taifa huru kwa watu huru. Wanaoandamana wanataka kuona heshima, utu wao na mali za taifa vikirejeshwa.

Wanaoandamana wanataka kuona misingi ya haki inatolewa kwa raia wote, bila kujali kipato cha mtu, umaarufu wa mtu au nasaba yake. Wananchi wanaoandamana wanataka kuona utawala wa matabaka nchini unatokomezwa. Hakuna tena mabwana na watwana.

Wanataka kuona tofauti kubwa ya kipato kati ya masikini na matajiri inaondoka. Huduna zinapatikana katika hospitali za umma. Karo kwenye shule za msingi, sekondari na vyuo, zinalipwa na serikali, tena bila ubaguzi.

Wananchi wanataka kuona wote walioiba au walioshiriki wizi, ukwapuzi na ufisadi wa aina yoyote ile lakini bado wamejificha nyuma ya siasa au wanalindwa na watawala, wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.

Wanataka kuona walioshiriki kuuza nchi kwa njia ya kunadi raslimali za taifa kwa bei ya karanga, wakichukuliwa hatua na jeuri yao inakoma mbele ya nguvu ya umma.

Wanaotetea nguvu ya umma wanataka kuona walioingiza taifa hili katika mikataba ya kinyonyaji wanaswekwa mahakamani na wanazuiwa hata kugombea uongozi wa ngazi yoyote.

Kuchukuliwa kwa hatua hizi ndiko pekee kunakoweza kurejesha uzalendo; chini ya watawala wapya ambao mikono yao haihusiki hata kidogo na ukamuaji jasho na damu ya wananchi.

Moyo wa utaifa – uzalendo – utarejea chini ya watawala wapya ambao wanathamini nguvu kazi ya umma; wale ambao hawahusiki hata kidogo na wala hawajawahi
kushiriki ufisadi na ukamuaji jasho na damu ya wananchi.

Copy and paste from Mwanahalisi online.
 
WENYELE
Kwa hiyo upuuzi wao (kama ni wapuuzi) ndio justification ya MMK naye kugeuka jiwe? Siamini kama watu wenye akili wanaishangilia CCM leo hii kwa sababu tu wapo watu waliomshangilia Lowassa! Inawezekana kabisa CDM walikosea sana kumkubali Lowassa lakini hiyo sio sababu ya kuifanya CCM sasa kuwa malaika maana, kwa ukweli, hakuna kilichobadilika. Labda watu wamebadilika - wale wameondoka hawa wamekuja. Na uzoefu huu tunao - aliondoka Nyerere akaja Mwinyi - akaondoka akaja Mkapa - akaondoka akaja Kikwete - naye ameondoka amekuja Magufuli. Kitu kimoja kimebaki pale pale - CCM.
 
Ccm ubaya wake una julikana haina hata haja ya kusema, CDM sarakasi ya kumchukua Eddo mwaka jana nayo haiwafanyi kuwa bora kabisa

Kwa sasa wapigania taifa ki ukwli ni wachache mno
 
lowasa kateuliwa mkuu wa wilaya gani ?
 
Nyie mnafikiri dr Dau akisimamishwa na waziri wa ujenzi wa wakati huo nae si atawajibishwa.
 
Mzee Mwanakijiji amekuwa mpiga zomari wa Magufuli. Naye anatamani awe mteule kama mwenzie Slow slow.
 
Back
Top Bottom