Hapana mkuu wangu hapana na wale watoe wanaotaka kuaminisha watu wengine kwamba CCM sio sababu ya Umaskini wetu bali uzembe wa wananchi wenyewe ndio wale wasiokuwa na haya hata kukubali kwamba umaskini wetu unatokjana na SIASA MBAYA na UONGOZI MBOVU.Mkuu: Ni kweli kuwa siasa ni moja ya nyanja kuu za maisha, pamoja na tamaduni(kwangu kama msingi mkuu), na uchumi. Vitu hivi havitengani kamwe! Kila mtu ni mwanasiasa, mwanauchumi, na mwanatamaduni katika taifa lake...yaani hizo ni sifa kuu zinazo m-shape binadamu! Tujiulize hapa, ni nani haishi siasa, tamaduni, ama uchumi? Mambo hayo yote hupaswa kusimikiwa mifumo ya kuyaendesha kufikia maendeleo ya watu. Mifumo hiyo ni lazima isadifu (a) MAZINGIRA yaani sura ya nchi na watu wake (b) NYAKATI, yaani mahusiano yaliyopo katika mazingira, yaani baina ya watu na watu, na watu na sura yao ya nchi. ,, Hapo ndipo tunapohoji ufanisi na uzito wa mifumo iliyopo katika kuendesha nyanja hizi za maisha kuleta maendeleo. Je, mifumo hiyo inakidhi haja?
Kisiasa tupo chini ya "demokrasia", kiuchumi tupo chini ya "uchumi huria-free economy" Kitamaduni nako tunasema "uhuru-freedom". Yote hayo yapo chini ya katiba inayoitwa "HAKI ZA BINADAMU-HUMAN RIGHTS"
Tukiruhusu fikra zetu, kufanya upembuzi yakinifu juu ya mifumo iliyopo "HUWEZI KUKATAA KWAMBA, KUAMINI MAENDELEO YATALETWA NA SIASA ILIYOPO NI KUJIDANGANYA"
Ubunifu haujawai kufika mwisho. Tunayo nafasi ya kuutumia!
Mungu wetu anaita!
SIASA ni ramani blueprint ya ujenzi wa kile ulokusudia hata iwe nyumba huwezi jenga tu ukitumia nguvu au kila mjenzi afikirie yeye ataweza vipi kuweka tofali na kipimo cha mafanikio kiwe nguvu zake. Hakuna kitu maendeleo ati ni ya kila mtu kwa nguvu na juhudi zake ati kwa sababu kuna DEMOKRASIA maana Demokrasia ni kipimo tu cha wazo lipi linakubaliwa kama vile unavyochagua ramani ipi ya nyumba itakufaa, lakini hutaki kuamini kwamba kuna umuhimu wa kuwepo ramani ya nyumba ktk makadirio ya fedha, vifaa na matumizi mengine.
Hakuna mtu anayejenga nyumba bila kuelewa ana kiasi gani mfukoni, nyumba hiyo ni kwa ajili gani na malengo haya ndio pale siasa zinapoingia kwa maana kwamba wewe unaamini njia ipi ni bora zaidi ya wazo la mtu mwingine. Na hata sisi binafsi ktk bongo zetu hukabiriwa na mtihani wa kifira ktk kuchagua njia bora ya kukabiriana na matatizo hivyo sio nguvu ama uwezo wa mtu bali siasa ni maamuzi yanayokubalika kufuatwa na wengi.
Free economy ni jina tu ambalo linatupa fursa watu kumiliki biashara badala ya serikali lakini pia serikali inalazimika kuhakikisha fursa hizo zinapatikana sii kwa njia haramu na pia kuhakikisha kila pato linalipiwa kodi na kwa kiasi gani. Bila siasa ni sawa na kusema kodi za wananchi hazijengi nchi, sasa sijui hizo barabara, maji, umeme na kadhalika vitajengwa vipi?. Siasa ni tofauti za kimawazo ktk Vipaumbele ktk maendeleo ya nchi na umuhimu wake utabakia pale pale..
HAKI za BINADAMU ama human Rights hazina uzito wowote isipokuwa makubaliano ya kimataifa ktk UTU wetu lakini Haifungwi na mkataba ambao unaweza piga marufuku tamaduni ambazo sii za kijamii iliyopo. Kwa mfano ndo ya wake zaidi ya mmoja haikubaliwi Marekani wakati Tanzania inakubalika. Ushoga unapigwa vita wakati nchi nyingine unakubalika hivyo hata hiyo haki za binadamu inatambua haki ya pande zote mbili husika na sio matakwa ya mtu mmoja mmoja.