Baada ya vyama vya upinzani kushika dola Zimbabwe, Kenya, Malawi na Zambia, tunajifunza nini?

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
18,653
20,987
Ni kipi physical ambacho nchi husika zimefaidika nacho, binafsi sioni chochote ambacho labda tunaweza kuiga na kukifuata toka katika nchi hizo ambazo zilialika vyama vya upinzani viwaongoze, zaidi ya gasia tu.

Zimbabwe na Zambia vyama vya upinzani vimeshindwa hata kudhibiti kipindupindu mpaka kufikia kuomba msaada wa kupigiwa dawa kwenye vyoo vyao.

Mwenye ushahidi wa chama cha upinzani kilichoingia madarakani na ambacho kikawaletea wananchi wake maendeleo awake hapa ili tujifunze kwa kina ufanisi wa vyama vya upinzani hasa katika Afrika yetu hii.
Opposition Wame fail by100% kila walipo twaa ushindi na kusababisha wananchi kujutia!

#Waafrika_ni_waafrika_tu.
#TUMEFANANA.
IMG_20240208_043630_571.jpg
IMG_20240208_044531_792.jpg
IMG_20240208_050115_464.jpg
 
Wamefeli vibaya mno,kote Hadi huko Senegal, Ghana, Malawi na Kenya hakuna kitu cha maana.

Walivyokuwa wanahubiri ni kinyume na wanayotenda.
Watu ni wale wale walianzia kwa mfano KANU ,wakalelewa nayo wakakuwa nayo.Tofauti ya vyama vipya (upinzani)
Ni nani awe kiongozi au viongozi wa serikali.
Lakini ni mapema mno kuzibeza serikali changa zitokonazo na vyama vya upinzani.wape chaguzi 4 mara miaka 5 yaani miaka 20.
 
Hao hao ambao Wameshindwa huko Senegal wanataka kufurushwa na Wananchi wanang'ang'ania madaraka 😆😆😆😆

Mjinga ndio anaweza weka matumaini yake Kwa mwanasiasa.
 
Amani na maendeleo mazuri kushinda hao
Amani ni katika mafanikio ya ccm hapa Tanzania? Kwa lipi wanalofanya hadi kufanya hii nchi kuwa na amani?

Ni maendeo yapi hayo mazuri ambayo yapo Tanzania kwa kuletwa na ccm tokea uhuru hadi leo?

Ni yapi tunajivunia hayo maendeleo kwa kuongozwa na chama kimoja kuanziani katika elimu? Afya? Au kuondoa umasikini ni wapi kwenye maendeo mazuri kushinda wenzetu?
 
Ni kipi physical ambacho nchi husika zimefaidika nacho, binafsi sioni chochote ambacho labda tunaweza kuiga na kukifuata toka katika nchi hizo ambazo zilialika vyama vya upinzani viwaongoze, zaidi ya gasia tu.

Zimbabwe na Zambia vyama vya upinzani vimeshindwa hata kudhibiti kipindupindu mpaka kufikia kuomba msaada wa kupigiwa dawa kwenye vyoo vyao.

Mwenye ushahidi wa chama cha upinzani kilichoingia madarakani na ambacho kikawaletea wananchi wake maendeleo awake hapa ili tujifunze kwa kina ufanisi wa vyama vya upinzani hasa katika Afrika yetu hii.

#Waafrika_ni_waafrika_tu.
#TUMEFANANA.
Ni lini Zimbabwe chama cha upinzani kilishika dola?
 
Back
Top Bottom