Vyama vya siasa ni sawa na dini, hakuna kilicho sahihi

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Jan 2, 2023
228
554
Wanaoamini katika Biblia kwamba ni kitabu kitakatifu hakuna sehemu inasisitiza kuwa dini ya mtu kwa maana ya haya madhehebu itamfikisha mbingu bali wale wote wenye moyo safi na wacha Mungu

Na kizuri zaidi Biblia iko wazi katika kutaja dini safi ni ipi? Kuwajali wasio jiweza, kusaidia yatima, wajane nk nk...yaani kuwa na upendo na kumcha Mungu

Leo hii ukisema ufanye sensa ya makanisa/madhehebu hasa ya Kikristo yaliyopo kwenye miji kadhaa mikubwa hapa Tanzania, utahitimisha kwa kusema kama kweli inavyosemekana kwamba Yesu hata rudi hadi injili imfikie kila Mwanadamu, basi kama hayupo Chalinze yuko Mbezi kabisa maana karibu kila mahali injili inahubiriwa kuanzia kwenye social media hadi barabarani na visipika tunawaona wahubiri

Kwa sehemu kubwa waumini wa kanisa fulani wanafungwa ndani ya kile anachokitaka kiongozi wa kanisa au mlengo wa dini hiyo

Hali kadhalika katika vyama vya siasa. Ni vigumu sana kwenda kinyume na mitazamo wa viongozi au waanzilishi wa vyama hivyo

Leo hii tunashuhudia wanaokuwa na mitazamo tofauti ndani ya CCM wanavyoitwa wasaliti na kuzushiwa kila aina skendo. Hata wabunge wenye mamlaka kamili ya wananchi wanaogopa zaidi chama kuliko wananchi wenyewe

Kule CHADEMA nani wa kwenda kinyuma na maono ya Mbowe? Pale ACT nani ataenda kinyume na matamanio ya Zitto abaki salama?

Kwa haraka haraka ukiangalia walioanzisha siasa za vyama ndio walioharibu system nzima ya uongozi wa serikali. Kwa mtazamo wangu naamini walifanya makusudi

Siasa za vyama zimeanzia nchi za dunia ya kwanza huko kisha zikaambukizwa kwetu dunia ya tatu. Cha kushangaza wao kwenye maslahi ya nchi wanasimama pamoja lakini sisi huku tunagawanyika

Ili tusonge mbele kama Taifa ni muhimu tuondoe imani kwenye vyama na tuwekeze kwa watu tunaowachagua. Tusilenge zaidi kinaongoza chama gani bali anayeongoza ana uwezo gani?

Dini au dhehebu halimpeleki mtu mbinguni bali matendo yake safi yanayompendeza Mwengezi Mungu. Vivyo hivyo, chama cha siasa hakitailetea nchi maendeleo bali watu wenye moyo safi, waadilifu, wenye uwezo na utayari wa kutumika kwa ajili ya nchi

Eid Mubarak
 
Back
Top Bottom