Madhara ya kuzaa nje: Familia inajuta mpaka leo kwa uamuzi walioufanya kwenye urithi wa kaka yao. So sad

Hivi umesoma vizuri alivyoeleza ujaona kifo hapo cha mama huyo.

Fikilia watoto wa kaka yako kabisa wa baba mmoja na mama mmoja, wanawasusa na kuwasahamu kwa kitendo kilichotokea kwa mama yao.
Utajisikiaje?

Kwa hio unaona ni sawa tuu.
Hayo ndo madhara yenyewe ujayaona mkuu
Ndo maana kuna mental illness
 
Kwanini huwa mnagombania mirathi?
Ni umasikini au
Kwanini zisiwe za wote tu kama mnaamua hivyo na je zimefuatwa taraibu za dini gani au mila zipi
 
Mama alikufa kwa roho yake mbaya akitaka mjane mwenzake ateseke na watoto wadogo bila pa kuanzia. Mumewe akifanya kuncheat sasa kwanini watoto ambao katika kucheat hawakushirikishwa wakazaliwa wateseke kisa baba aliyecheat kafa.
Tujifunze kusamehe na kusonga mbele. Alikufa kwa sababu ya kutosamehe
Ndo hivyo yashatokea.
Nafikili watakuwepo tuu wanaambaa macho.

Kumbuka aliyechukua mali hakuwa mke wa marehemu
 
Bro wangu yupo USA,
Alikutana na mtoto wao mmoja anaishi Washington DC.
Ameoa mzungu na ana watoto wa kiume 2.

Anafanya kazi kwenye bank moja moja ameajiri kabisa.
Daa bro alimwambia mzee pale wanalipa mshahara mzuri kweli kama $25,000/= kwa mwezi kwa jumla. Ila yeye anaelimu kubwa.
ntundaga
Black Sniper
Nzagambaaa
Peaceforever
To yeye
 
Inaumiza,mmepambanaa weweee mmeejinyimaa wee,mshua anadodoka danga tu anakujaa takaa mgaoo na wanaee bila jashoo. Si aletee na zakee tugawaneeee!
Kwa ubande mwingine utasema yesu.
Ile sheria ya kusema watoto hawana makosa. Ipo sahihi.
Ila inachukuliwa fursa na madanga.
Kupata mgao.
Na mara nyingi wanawake wanaozaa na wanaume za watu , lengo lake kubwa ni kuvizia mali za yule baba, alizoshilikiana na mke wake kuzijenga.
 
Mama alikufa kwa roho yake mbaya akitaka mjane mwenzake ateseke na watoto wadogo bila pa kuanzia. Mumewe akifanya kuncheat sasa kwanini watoto ambao katika kucheat hawakushirikishwa wakazaliwa wateseke kisa baba aliyecheat kafa.
Tujifunze kusamehe na kusonga mbele. Alikufa kwa sababu ya kutosamehe
Sasa na hao watoto wa baba kuondoka na kubadili mpk jina la mwisho.
Bro wangu alikutana na mmoja usa. Wapo fresh tuu na familia yako ila ndo hivyo wapo tuu huko. Hkn mpango hata wa kurudi
 
Mahusiano yoyote yana pande zote mbili, hasi na chanya!

Kwenye baadhi ya familia yaweza kutokeza vita
Vipo vita baina ya watoto wa nje ya ndoa vesus watoto ndoa
Vipo vita baina ya watoto wa nje ya ndoa vesus baba yao aliyewazaa
Vipo vita baina ya watoto wa nje ya ndoa vesus mama wa kambo ambayo ndiye mke rasmi wa baba yao


Kumbe Basi,
Kwenye baadhi ya familia yaweza kutokeza heri
Watoto wa nje ya ndoa kuwa heri kwa baba aliyemzaa
Watoto wa nje ya ndoa kuwa heri kwa mama wa kambo mke wa baba yake aliyemzaa
Watoto wa nje ya ndoa kuwa heri kwa ndugu zake za ndani ya ndoa

Kwahio,
Maadam mtoto wa nje ya ndoa aweza kuwa na upande wa faida au hasara, haiwezekani kusema ni madhara kuzaa nje ya ndoa

Hasara ya kuzaa mtoto inapatikana kwenye ndoa pia nje ya ndoa

Faida ya kuzaa mtoto inapatikana kwenye ndoa pia nje ya ndoa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Habari za weekend,

Jana kuna dogo wangu mmoja alikuwa wanaongea na mzee na mimi nilikuwepo home alikuwa anawaambia madhara ya kuzaa nje ya ndoa yanayoweza kujitokeza baadae.

Alitoa kisa kimoja hivi cha kweli kabisa.

Ilikuwa hivi.

Kulikuwa na Baba mmoja alizaa na mkewe watoto 3, wakike 2 na wakiume 1, watoto asilimia kubwa walifanana na mama yao.

Mzee alisema kuwa walikuwa wanapenda na kwenye ile familia tena sana.

Mtoto wake wa kwanza kwenye ile familia aliolewa na mzungu wa USA. Na wa pili ambaye ni binti pia alikuwa anasoma USA. Ila wa mwisho ni wakiume alikuwa hapa bongo.

Yule Baba alikuja kuugua kisukari ambapo ilimpeleka mpaka kufariki. Siku ya msiba alikuja mdada mmoja ana watoto 2 wakiume wamefanana sana na Baba. Mmoja kama miaka mitano hivi na mdogo wake.

Watu ndiyo wakajua kumbe Baba alikuwa na nyumba mbili. Japo watoto wa nje walipishana umri mkuwa tuu na watoto wa ndani ya ndoa.

Mama wa ndoa alishituka sana lile tukio na watoto wake. Kumbe Mume wake alishawatambulisha watoto kwa baadhi ya ndugu.

Baada ya msimba. Kwenye mgawanyo wa mali walisema hizi mali ni za kaka yetu na hawa watapata , waliogombana mapaka mahakamani ila ilishindikana walimwambia tuu mama kwa sababu watoto walitambulishwa. Walikuwa na nyumba kadhaa na mali zingine.

Waligawa sawa na tuu na wengine. Kitendo kile kilimpelekea mama kupata msongo wa mawazo mpaka kufariki. Ile ishu iliwaumiza sana watoto wake wakaamua kumzika tuu mama yao.

Mwishowe wale watoto waliuza mali zote za Baba yao wakamchukua mdogo wao wa kiume na kwenda nae USA.

Mpaka leo wapo USA na hawana mawasiliano na familia yao upande wa baba tangu waondoke.

Na yule binti baada ya kuchukua mali alikata mawasiliano na ndugu wa Yule Baba aliyezaa nae.

Alichukua nyumba moja, mwishowe aliolewa na mume wake alimwambia kuwa anataka watoto wadogo wawe wake kwa hio wabadili jina la mwisho la watoto wawili.

Aliishi kwenye nyumba ya yule Baba aliyopewa na mume mpya.

Ni ishu ya kweli yani ndugu wale mzee alisema walijilaumu sana baadae.

JAMANI WANAUME TUACHE KUZAA NJE YA NDOA , KAMA IMETOKEA BASI KUWA MAKINI MADHARA BAADAE YASIJITOKEZE.
MI NI HAYO TUU FRIENDS.
Kwa kifupi hatuachi kuzaa nje pia story yako haieleweki..😊😊
 
Back
Top Bottom