Moronight walker
JF-Expert Member
- Aug 3, 2021
- 3,105
- 4,635
Habari wana Jamii forum.
Ngoja leo nilete hii kesi niliyoishuudia kwa macho yangu.
Kulikuwa na Baba mmoja na familia yake wa watoto 4, wapili ni wakiume ambae alimzaa nje na wengine 3 Wandoa wakike alizaa na mkewe.
Niliambiwa hivi, Baada ya mkewake kujifungua mtoto wa kwanza ikapita kama mwaka hivi Baba akazaa nje mtoto wa kiume ila aliyamaliza na mkewe.
Mtoto alipofika umri wa miaka 6 mzee alimchukua na kukaa nae home.
Mke wake alikubaliana na hali na kumlea tu bila shida yoyote. Na likizo akawa anaenda kwa mama yake.
Sasa baada ya kufika utu uzima watoto wote.
Yule Baba alifariki na kuacha nyumba mbili tu. 1 aliyokuwa anaishi na mke wake nyingine walipangisha.
Sasa mtoto wa kiume wa baba ambae alimzaa nje akawa anag'ang'ania awe msimamizi wa mirathi kwa kigozo cha yeye ndiyo wa kiume ndiyo anaendeleza familia ya mzee.
Na pia analazimisha nyumba zote mbili ziuzwe wagawane ila yeye akawa anahitaji kupata asilimia kubwa.
Kesi ilikuwa kubwa mpaka kupelekana mahakamani , ila walipofika mahakamani mabinti wale watatu wakasema wao hawaitaji nyumba kuuza kwa sababu mama yao atakaa wapi.
Lakini mahakama wakamwambia jamaa wote ni watoto wa baba mmoja kwa hio wote mtapata sawa hakuna huyu wa kiume wala huyu wa kike wote mnapata kwa usawa.
Lakini mwishoni walikubaliana wauze nyumba mmoja halafu kaka yao wampe pesa zake na zingine ili wafidie ile nyumba nyingine ambayo Mama yao anakaa.
Nyumba iliuzwa 1 jamaa akachukua pesa ndefu tu ili kufidia ile nyumba nyingine ambayo mama wa mabinti alikuwa anaishi na mume wake.
Sidhani kama wanaundugu mpaka leo wa karibu.
Nafikiri jamaa alitaka ziuzwe zote bila kujali mama yule atakaa wapi.
Hiyo ni kwa sababu yule hakuwa mama yake, hata nyumba ikiuzwa yeye ataumia chochote.
Karibuni jamani mutoe uzoefu wenu kama umewahi kutana na migogoro kama hii.
Karibu.