Wanaume acheni kuzaa na wanawake ambao hamtawaoa

Zemanda

JF-Expert Member
Jan 10, 2021
6,886
14,402
Inakwaza na kufedhesha sana kwasasa kuona kuna ongezeko kubwa la watoto ambao hawajulikani baba zao ni akina nani na hata kama baba wanajulikana basi hawapo katika maisha ya mtoto.

Big up kwa akina baba ambao wanapambania kuwatunza na kuwalea watoto wao wa damu na kuwajibika kama baba na kutowatenga hawa watoto.

Kimsingi baba ni mtu muhimu sana katika maisha ya mtoto na baba anapokosekana katika maisha ya mtoto ni rahisi sana kwa mtoto kupoteza direction ya Maisha utu uzimani.

Mtoto wa kiume unakutana na mdada haujui history yake haumfahamu anaishi kwa mwenendo gani kisa tu kakuruhusu kumpelekea moto unaachia mbegu zako kwenye mji wake wa uzazi ukijua wazi matokeo yake ni yapi.

Hivi huwazii mtoto wako anapozaliwa huyo ndie atakuwa mama yake na wewe ndie baba yake na ndio mwanzo wa familia? Why sasa unaanzisha kitu kikubwa namna hiyo katika hali ya kizembe sana.

Hauoni kuwa unakuja kumpa maisha ya mateso na maumivu huyo mtoto ambaye alitakiwa kukuzwa kwenye maisha ya upendo wa baba na mama na yeye aje kuwa raia mwema?

Je, umemuwazia huyo mwanamke namna atateseka na mtoto huyo usiku pekee yake mchana pekee yake, hapo inakupa fahari gani kama mwanaume kuona damu yako ipo huko na wewe upo huku usijali inaishi maisha ya namna gani?

Kama kwako ni muhimu kuchuja nafaka, si upige hata nyeto au uzingatie ngono salama ambayo haitaleta mtoto ambaye hautakuwa hiyari kumlea kwa upendo?

Hivi unatakiwa uwe na akili ya namna gani hadi kukimbia mtoto wako mwenyewe ambaye hata ukimtazama unajiona kabisa wewe yule pale katika mwili na damu?

Hebu ifike muda tuanze kuambiana ukweli, hawa watoto tunaweza wapata katika mazingira salama na tukawalea. Kama mwanamke ni mkorofi hushindwi kuchukua mtoto wako ukapeleka kwa bibi yake yaani mama yako au ukatafuta mwanamke akusaidie kulea hata beki tatu wapo kibao ambao utamuacha pale room kwako akae na mtoto na wewe umpatie mshahara na akusaidie kuishi na mtoto wako vizuri tu hadi atakapofika umri wa kuanza kujisimamia.

Trust me, mtoto yupo salama zaidi akikua mazingira ya shida pembeni ya baba yake kulikoni akiishi maisha ya shida pembeni ya mama yake ambapo ni rahisi kuharibika tabia na kuwa tatizo ukubwani.

Siku zote linapokuja swala la kulea mtoto huwa wanaume kuna ile tabia ya kujitisha kuwa mtoto atateseka akilelewa na watu baki, huu ni upotoshaji mkubwa sana. Ipo mifano hai ya wanaume waliolea watoto wao wenyewe bila mama wa mtoto kwa msaada wa mfanyakazi na familia yake hadi mtoto kawa mtu mzima, si watoto wa kiume tu hata wa kike.

Inawezekana na nirahisi sana zaidi ya unavyofikiria. Mimi nimeshalea wajomba wawili kwa msaada wa bibi yao na dada wa kazi baada ya kuona upumbavu wa mama zao unavyowagharimu watoto. Ndio maana nauchukia sana usingle mother sababu naelewa madhara na mateso yake kwa watoto wasio na hatia.

Inaanza na wewe kuwajibika na sio kuwategemea hawa mabinti wa sasa ambao hawawajibiki na maamuzi yao. Kama wewe hautatoa mbegu zako kwa mtu ambaye hautaanza nae familia masingle mother watatokea wapi na watoto watapatikana vipi?

Hebu wanaume tuchague kuwajibika na sio kuwa vilaza ambao kwa makusudi tunachagua kushirikiana na wanawake irresponsible kuleta watoto duniani na kuwatesa bila hatia. Hebu tuanze kuwa na maono ya wapi tunapeleka uzao wetu ili tusipoteze mbegu zetu zikaotea mibani.

Utafurahi siku unakutana na binti yako amekuwa mdangaji, kahaba, ana ma'tattoo amekuwa mtu wa hovyo kama akina Giggy money, au Amber Rutty?

Au unakutana na mtoto wako wa kiume amekuwa kituko, kasuka marasta au kaweka dreads, matattoo mwili mzima, kavaa mlegezo, anakimbiza bodaboda halafu wewe ni mtu na heshima zako unapita, unaweza kumrekebisha tena samaki aliyekauka? Ni kazi rahisi sana kujenga kizazi bora kupitia malezi bora ya watoto kuliko kurekebisha taifa na jamii iliyoharibika kwa gharama na program za kuwarekebisha watu wazima ambao wamekomaa kiakili na wameshapinda.

Acheni kuzaa watoto ambao hamna mpango wa kuwalea na kuwatunza kwa upendo kifamilia mnatutesea watoto wasio na hatia na kuleta laana ambazo hazikuwa na nafasi kwenye jamii yetu. Watoto waliopo kwa sasa iwe ni funzo tubadilike.
 
1715139306630.jpg


Wanawake ndio wana jukumu la Ku control afya zao ambapo ni pamoja na upatikanaji wa Mimba..!!!

#YNWA
 
Mithali 14:1
Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake;
Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe
 
1. Kwanini lawama abebe mwanaume peke yake, mwanamke hajui madhara ya ngono zembe?

2. Mwanamke kuzaa na mwanaume asiye na malengo naye ndiyo sababu pekee ya usingle mother?

Yaani unawadekeza wanawake, unawaonea huruma, unawachukulia kama wajinga wakati na wao wanajitambua vizuri tu.
 
Back
Top Bottom