MREJESHO; Ushauri, niwahusishe watoto wangu wa nje ya ndoa kwenye urithi?

Johnson12345

JF-Expert Member
May 29, 2023
206
422
Habari wanajf.
Nilileta uzi hapa kuhusu rafiki yangu mmoja ambaye alizaa nje watoto 2. Na mkewe alizaa nae watoto wawili.

Thread 'Ushauri, niwahusishe watoto wangu wa nje ya ndoa kwenye urithi?' Ushauri, niwahusishe watoto wangu wa nje ya ndoa kwenye urithi?

Alipata kigugumizi kuhusu mali alizochuka na mkewe ambazo zipo kwa majina yake yeye kama mume.
Nyumba tatu na biashara.

Sasa yeye kaniambia kuwa mke wake ni mtu mzuri sana hajawahi kumkosea kitu chochote, ni mtu mwema sana kwake.

Ameniambia kuwa hataki mke wake apate maumivu yoyote ni mtu mzuri sana.

Sasa alichoamua jamaa yangu ni kwamba kaamua nyumba 3 alizojenga na mke wake ,
Nyumba 1 amempa mtoto mmoja na ya pili kamapa mtoto wake mwingine, wote ni wa ndani ya ndoa. Na nyumba moja kampa mkewe.

Alifanya hivyo wote na mke wake kwenye kubadili jina bila mkewe kujua kwa nini kafanya hivyo.

Yeye hataki mzazi mwezie yule aje kuchukua mali za huku.

Ila alikuwa na kiwanja kimoja maeneo ya Goba alijenga msingi na boma na fensi , alichukua pesa na kumalizia , sasa ameshaezeka na wiring,
Pasta tayari.
Kasema mwishoni mwa mwezi huu inaweza ikakalibia kuisha.

Hiyo ndo atawapa watoto wa nje.

Ila mimi nimemwambia atafute namana ya kuwaandikisha hao watoto , maana kikitokea mke wa ndoa atataka percentage kwenye hio nyumba kama itakuwa na jina lako.

Ni mgojwa na shida yake haina Tiba mda wowote ataondoka.

Kaamua hivyo.
 
Usibague watoto wako, wakishazaliwa haijalishi walikuwa ndani au nje ya ndoa. Kama una mali wape wote, dam ni nzito sana!!
Alafu ubaguzi ulivyo na dhambi mbaya, unaweza kuta wale unaosema ni wanao wa ndani siyo wanao wa damu,na wale unaowaona kua wa nje ndiyo unaweza kuta ndiyo damu yako asilimia mia!! 'Maisha ni fumbo'
 
Kama hakuwa anapenda ugomvi na mkewe, kwanini aliamua kuzaa nje ya ndoa yake?

Mwambie hajawatendea haki watoto wake hao wa nje, alipaswa angewapa sawa na hao wengine wa mkewe.
 
Kama hakuwa anapenda ugomvi na mkewe, kwanini aliamua kuzaa nje ya ndoa yake?

Mwambie hajawatendea haki watoto wake hao wa nje, alipaswa angewapa sawa na hao wengine wa mkewe.
Mkuu huo ni mtazamo wako ila kisheria haiko hivyo.
Kwa mujibu wa sheria mtoto wa nje hana haki yeyote kwenye mali ulizo zitambulishwa kuwa ni za familia.

Ww kama umezaa watoto nje ya ndoa unatakiwa kuhakikisha unawatafutia mali zao nje ya zile za familia.
Kwa hiyo mzee yuko sawa.
 
Hajawabagua watoto kila mmoja kampa sawa kabisa.
Watoto pamoja na kupewa sawa,hawahitaji kujuana ni ndugu?

Kuna jamaa mmoja, wa mkoa wa Mara huko. Kahamia Dar mda mrefu kwa ndugu,kasoma,kamaliza chuo hadi kuoa. Sijui ni bahati mbaya au vipi,kumbe mwanamke aliyempa mimba ni ndugu wa karibu. Badae mambo yakagoma,kamfukuza kama mbwa. Mjamzito,mimba yake, af ndugu wa karibu. Kapata kidada kikampeleka kwa baba kapewa chumba na kulelewa. Sijui mvutano wa damu,sijui akili kujirudi, jamaa kaamua ampeleke kwa mama yake kutambulisha mzazi mtarajiwa.
Acha wafike home!!! Eti mama mtu alikimbia ka mwehu baada ya kuambiwa hii mimba yangu.
Ni kasori karefu kidogo. Ila lengo tu ni moja. Ndugu ni ndugu tu. Makosa ya wazazi. Unapofichaficha watoto mwishowe itakuwaje? Ukute mmoja anapata shida,ndugu yake yupo karibu,na huenda ana uwezo wa kusaidia,na hatekelezi. Kwa sababu hajuii
 
Wanaume wa hovyo mnasupport uzinzi tu, yani utafute na mkeo then mwishoni umletee watoto wa nje et ni wanao so wagawane mlichonacho!! Ili iyo case iwe sawa INABIDI UMWACHIE MWANAMKE MIAKA KAMA MI NNE NAYE AKAPELEKEWE MOTO NJE YA NDOA AMWAGIWE SPARM APATE MIMBA WATOTO WAWILI then arudi mkae mezani namna yakugawanya mali zenu kwa watoto wenu kwa haki na upendo bila ubaguzi.
 
Back
Top Bottom