Suala la nauli kupanda ni kuwanufaisha wamiliki wa magari na kuwaumiza wananchi

je parle

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
1,881
3,619
Inashangaza sana nauli KUPANDA mara dufu kiasi hiki bila sababu za kueleweka! Ukiulizwa unaambiwa gharama za uendeshaji ndio zimepelekea haya kutokea. Hii ni aibu na kituko cha mwaka.

Sasa mtu mtu kama biashara yake Ina gharama kubwa za uendeshaji si afunge hiyo biashara atafute biashara nyingine? Kwahiyo hao wafanyabiashara ndio wamewashawishi LATRA kuongeza bei kutokana na gharama na sio tena mafuta KUPANDA?

How come latra wanapandisha bila kufanya tathmini ya kutosha kuhusu matokeo ya kupandisha hizi bei?

Au WAMILIKI wamagari walijichanga wakatoa hongo kwa latra ili zoezi lao la bei lipewe kipaumbele? Inashangaza.

Hili ongezeko ni kubwa sana hii haikubaliki hata kidogo

Ila ninacho ogopa ni kuwa watanzania ni wepesi sana kuhsahau na waliyopo kwenye madaraka wanalijua Hilo! Watu tutapiga kelele wiki Moja tutanyamaza na gharama zitakuwa zile zile na watu hawana la kufanya.

Tutakachofanya kwa sasa ni kupunguza safari zisizo za lazima tu ili kukwepa hizo nauli.

Katika hili sakata la nauli KUPANDA hapa wanaufaika wakubwa sana ni WAMILIKI WA MAGARI na maderava na makondakta.

Sasa makondakta wanatamba Kuna mmoja nlikuwa naongea nae akasema sasa hivi ALHAMDULILAH IKIFIKA SAA SITA MCHANA NISHAPATA HELA YA BOSS NA POSHO YANGU SASA HAPA NATAFUTA HELA YA MAFUTA!

NYIE LATRA KAMA HAMJAWAI KUSAFIRI WALA KUPANDA DALADALA.? MNAONGEA KABISA CONFORTABLE ETI GHARAMA ZA UENDESHAJI ZIMEPANDA? NYIE ***** nlitaka nitukane hapo ila kipande nimekiruka.

Awamu hii madereva na makondakta msipojenga ni nyie tu na laana ZENU mana kama ni Hela mnakusanya.!
 
sasa watunga sera na wasimamizi wahizo sera wengi ni wamiliki wa hivi vyombo vya usafili hasa mabasi .
laima waweke mipango kufanya biashara zao zishamili
 
Back
Top Bottom