Madee amekufuru!

hajatusi mtu wala kutukana sasa kati ya yeye na wewe nani anaonekana punguani na mwehu

Wewe Kisiki sijui Kigogo uliyekatazwa kuvaa suti kwa hiyo unaona Madee kafanya sawa? Mtu unapoongea au msanii anapoimba kuna maneno au statement fulani akizitoa unajua kabisa uwezo wake wa kufikiri ni mdogo..

Kasema nilipata mateso kuliko "YESU" nia yake ni kuonyesha kateseka kwa kiasi kikubwa, but hakufikiria statement hii itakuwa na impact gani kwa jamii ya kikristo na kiislam pia...

Angekuwa ni msanii mwenye upeo mkubwa wa kufikiri angejaribu kutumia lugha nyingine kuelezea mateso aliyoyapata rather than kuweka jina na ISA a.s

Regards
 
tatizo bangi ya malawi bora hata angevuta ya tarime
natamani nionane naye nimpe mawaiza mawili matatu hivi.
 
Yesu amsamehe Maana hajui alisemalo!
Waefeso 6:12 imeandikwa hivi: "Kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho".
Wangekuwa wenzetu hapa kesho ungeona majambia na mabango mtaani
 
Kasema nilipata mateso kuliko "YESU"
.................rather than kuweka jina na ISA a.s

Regards
Mimi sijausikia huo wimbo lakini ningesema, 1. Kama alisema alipata mateso kuliko ISA basi nikiwa kama mkristo najua ISA Bin Mariam anayezungumzwa na wenzetu sio yule Yesu Kristo wa Nazareth aliyesulubiwa zamani za pontio Pilato, 2. Kama amesema YESU akimaanisha YESU Kristo wa Mnazareth mwana wa Mungu sitaona bado ni kufuru kwani mateso ni comparison term, na hakuna katika biblia ambapo panasema mtu hawezi kujifananisha na YESU, Biblia inasema yesu alizaliwa duniani kama Mtu na aliishi kama mtu kwanini tuanze kutumia maneno ya "Kufuru" huu sio msamiati wa kikristo, sisi tuna maneno ya Heri yao au Ole wao basi mumeaanza kuchanganya mambo wakuu wangu! Mnaogopa kuwa kama wao wakati huo huo mnaanza ku-reason kama wao
 
ndio hivyo tena akil ya kivivu,fikra chakavu,zimekosa upevu na wala si endelevu.
 
Kuna mmoja ilikuwa asomewe albadiri, sijui hii iliishiaje:

picture.php
Dah... hii kali
 
sawa inawezekana hivi wanajamii hakuna watu wanaoteseka mateso zaidi ya huyo yesu acheni utani bwana musilete udini kama vipi tembeleeni maohospitals

We "upele".. tulia kimya usiongee kitu kama hukielewi!!
 
wasanii wengi wanaimba ilimradi vina tu, hilo la elimu pia sina shaka nalo pia kwani asilimia kubwa ya wanabongo fleva hawana shule, std.7, form 2, 3 amejitahidi form 4! wako wachache wanaoimba na heshima yao iko kama mwana fa, prof. j, ay, joh makini na wachache wengine, hao ukisikiliza nyimbo zao huwezi kusikia pumba kama hizo. kulinganisha kufulia kwako na mateso ya Yesu??? bhange mbaya sana....
 
Madee mwanamuziki wa midundo ya bongo flavor amekufuru kwenye wimbo wake anaosema amepata mateso makali kuliko ya Yesu.

Wakristo wanaamini kuwa hamna mtu amewahi kuteswa kama yesu. Madee akiwa ni muislamu, hakupaswa kulinganisha taabu zake na mateso ya yesu.

Madee amekufuru.
waambie hao wakristo wafuatilie mateso waliyopewa wayahudi na hitler na afuatilie mateso waliyapewa watumwa wa kiafrica na wakoloni.ndipo ataona nani aliteseka zaidi
 
MADEE AONDOKEWA NA KIPENZI CHAKE.

Wakati jamii ya muziki wa Kizazi Kipya na mashabiki wao wakiwa bado katika maombolezo ya msiba wa Julieth D. Mrina ‘Pendo’ (24), kubwa zito limeibuka kuhusu anayetajwa kuwa ni mchumba wake, Hamad Ally ‘Madee’, Amani limekusanya vielelezo

Baadhi ya waombolezaji kwenye msiba huo uliokuwa umepigwa kambi Kimara, jijini Dar ni wanamuziki wa Kizazi Kipya, akiwemo Joseph Haule ‘Profeja J’, ‘Tundaman’, Khadija Shaban ‘Keisha’, Kasim Maganga ‘Kasim’ na ma-andagraundi wengine kibao.

Ulipofika muda wa kusomwa kwa wasifu wa marehemu Pendo, kwamba ni nani, alizaliwa wapi, mwaka gani na amefanya nini hadi kifo kinamkuta ndipo lilipoibuka jambo zito ambalo liliwaacha midomo wazi baadhi ya ‘kampani’ ya Madee.

Wasifu huo ulimalizika bila kutajwa kuwa, marehemu alikuwa amechumbiwa na Hamad Ally ‘Madee’ jambo ambalo lilizua maswali lakini hakukuwa na mwenye jibu.

Amani liliongea na baadhi ya wasanii waliohoji kulikoni kwenye vyombo vya habari kuandikwa wawili hao ni wachumba lakini asitajwe kwenye wasifu wa marehemu?

“Mimi nilijua nakuja kwenye msiba wa mchumba wa Madee, sasa mbona kwenye wasifu hawajasema kama marehemu mpaka kifo chake alikuwa ameshachumbiwa?” Alihoji msanii mmoja wa Bongo Fleva, jina tunalo.

Mwingine alisema kuwa, anavyojua yeye, wasifu wa marehemu unaacha kumtaja mtu kama alikuwa mpenzi tu, “lakini kuanzia mchumba mpaka mume au mke hutajwa,” alisema.

Aidha, habari nyingine zinadai kuwa, licha ya Madee kutotajwa kwenye msiba huo kama mchumba wa marehemu, mama yake mzazi ‘mama Hamadi’ naye alikuwepo msibani hapo kama binadamu kwa sababu shughuli ya msiba ni ya kibinadamu zaidi na haihitaji mwaliko kama ilivyo kwenye sherehe za ndoa ‘harusi’.

Habari zaidi chini ya zulia zinadai kuwa, baadhi ya ndugu wa marehemu wanamtambua Madee kama mchumba mtarajiwa, lakini hakuwahi kujitambulisha rasmi kwa barua na posa katika familia hiyo ndiyo maana hakupata ‘festiprioriti’ katika wasifu wa marehemu.

Hata hivyo, bado ‘tano’ inatolewa kwa msanii huyo kutoka ‘skwadi’ ya TiP Top Connection, Manzese jijini Dar ikisemekana kuwa, ndiye aliyefanikisha kuusafirisha mwili wa marehemu Pendo kutoka Hospitali ya Mkoa wa Pwani, Tumbi, Kibaha kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Jijini Dar es Salaam.

Marehemu Pendo alifariki dunia Machi, 13, 2010 katika ajali iliyoshirikisha basi la Shabiby na lori iliyotokea Kibaha, mkoani Pwani. Katika ajali hiyo, ni Pendo tu aliyepoteza maisha.

Taarifa nilizozipata hivi punde Msanii huyu amefiwa na Girlfriend wake wa siku nyingi aitwae Pendo katika ajali ya Basi la Shabiby iliyotokea jana...
Nasikitika sana kwa sababu kuna gazeti moja lina picha za msiba na habari fulani ambayo naona inawaongezea uchungu wafiwa. Wanadramatize kwa nini huyu msanii hakutajwa kwenye msiba katika utambulisho na mambo mengine mengi ya kijinga.
 
Jamaa nadhani alikuwa mpenzi na sio mchumba kwa vile hakutoa posa hivyo sio muhimu kutajwa.Ikiwa wakati wa mzishi basi wapenzi wa marehemu watajwe pia itakua balaa maana kuna watu wanao kwa mamia....
 
Madee mwanamuziki wa midundo ya bongo flavor amekufuru kwenye wimbo wake anaosema amepata mateso makali kuliko ya Yesu.

Wakristo wanaamini kuwa hamna mtu amewahi kuteswa kama yesu. Madee akiwa ni muislamu, hakupaswa kulinganisha taabu zake na mateso ya yesu.

Madee amekufuru.

Hold your Horse man,not too fast!Binafsi ni evident mateso yanayomkabili mtanzania wa kawaida(at physical and psychological level jamani si madogo).Tusiwashutumu sana generation dot com .
 
Jamaa nadhani alikuwa mpenzi na sio mchumba kwa vile hakutoa posa hivyo sio muhimu kutajwa.Ikiwa wakati wa mzishi basi wapenzi wa marehemu watajwe pia itakua balaa maana kuna watu wanao kwa mamia....
Siku hizi neno "mchumba" limepoteza maana yake halisi kwani hata "wapenzi" siku hizi wanaitana wachumba kiasi kwamba tofauti kati ya "mchumba" na "mpenzi" imekuwa kama haipo. Mtu akikutambulisha kwa mtu wake kama ni mchumba lazima uwe makini kuelewa kile anachomaanisha: kwani anaweza akawa na maana ya mchumba kweli au mpenzi tu. Mimi naamini uchumba una uzito zaidi katika mahusiano ya wawili na una process yake k.v. kuvishana pete, kujitambulisha kwa wazazi, kutoa posa, nk. Vikikoseakana hivi huwezi kumuita mpenzi wako ni mchumba kwani hajatimiza hivyo vigezo.

Kumbe si ajabu Madee alikuwa ni mpenzi tu wa marehemu kama walikuwa hawajapelekana kwa wazazi, nk. Nampa pole kijana.
 
Hold your Horse man,not too fast!Binafsi ni evident mateso yanayomkabili mtanzania wa kawaida(at physical and psychological level jamani si madogo).Tusiwashutumu sana generation dot com .
Suala hapa si mateso ya Yesu kama phyisical suffering tu lakini ni hasa ile implication ya mateso ya Yesu. Mateso yake yalikuwa redemptive, yaani kwa ajili ya wokovu wa wanadamu; ni mateso yenye hadhi ya pekee ambayo yeyote awaye hawezi kujilinganisha nayo. Mateso ya Madee na wanadamu wengine hayana hiyo sifa ya wokovu wa dunia. Ni mere physical sufferings. Kumbe kulinganisha mateso ya kibinadamu ya kila siku na mateso ya Yesu ni kukosea njia, ni kufuru kwa sababu mateso ya Yesu ni salvific na si sawa na mateso yoyote yale.
 
Babu yao umesema kweli, jamii inabidi itofautishe mchumba, mpenzi na rafiki. Naona kama tunaiga mno utamaduni wa wenzetu wa nje kiasi cha kutia aibu. Fikiria ungekuwa mzazi ama ndugu wa karibu wa binti aliyefariki ungejisikiaje kuwaona vijana wenye sura za BANGE wanalia tena kwa maonyesho kwenye msiba. Yaani wanafanya usanii kwenye msiba wa binti yenu?
 
Madee mwanamuziki wa midundo ya bongo flavor amekufuru kwenye wimbo wake anaosema amepata mateso makali kuliko ya Yesu.

Wakristo wanaamini kuwa hamna mtu amewahi kuteswa kama yesu. Madee akiwa ni muislamu, hakupaswa kulinganisha taabu zake na mateso ya yesu.

Madee amekufuru.

Nadhani ni muhimu kwa na udhibiti wa kauli zetu... sianDiki kwa nia mbaya ila nahisi hata msiba alio nao hivi sasa(japo ni mapenzi ya mungu) ni kama kuoneshwa kwa kuna mamlaka makubwa kuliko yeye... ajifunze kutokana na makosa..!Akumbuke ya Meli ya Titanic(waluonda walisema hata mungu hawezi kuzamisha), Ya Nabii Musa(alikaidi maagizo ya mungu akaishia kuion tu nchi ya ahadi pasipo kuiknyaga ardhi yake)...TUWE MAKINI NA KAULI ZETU..!
I STAND TO BE CORRECTED!!!
 
Babu yao umesema kweli, jamii inabidi itofautishe mchumba, mpenzi na rafiki. Naona kama tunaiga mno utamaduni wa wenzetu wa nje kiasi cha kutia aibu. Fikiria ungekuwa mzazi ama ndugu wa karibu wa binti aliyefariki ungejisikiaje kuwaona vijana wenye sura za BANGE wanalia tena kwa maonyesho kwenye msiba. Yaani wanafanya usanii kwenye msiba wa binti yenu?
Nilivo shubiri ningewatoa resi!!
 
Siku hizi neno "mchumba" limepoteza maana yake halisi kwani hata "wapenzi" siku hizi wanaitana wachumba kiasi kwamba tofauti kati ya "mchumba" na "mpenzi" imekuwa kama haipo. Mtu akikutambulisha kwa mtu wake kama ni mchumba lazima uwe makini kuelewa kile anachomaanisha: kwani anaweza akawa na maana ya mchumba kweli au mpenzi tu. Mimi naamini uchumba una uzito zaidi katika mahusiano ya wawili na una process yake k.v. kuvishana pete, kujitambulisha kwa wazazi, kutoa posa, nk. Vikikoseakana hivi huwezi kumuita mpenzi wako ni mchumba kwani hajatimiza hivyo vigezo.

Kumbe si ajabu Madee alikuwa ni mpenzi tu wa marehemu kama walikuwa hawajapelekana kwa wazazi, nk. Nampa pole kijana.
tatizo letu ni kwamba tunaamini kuwa kiswahili ni lugha ngumu sana kuliko lugha zote ulimwenguni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom