Madee amekufuru!

Madee mwanamuziki wa midundo ya bongo flavor amekufuru kwenye wimbo wake anaosema amepata mateso makali kuliko ya Yesu.

Wakristo wanaamini kuwa hamna mtu amewahi kuteswa kama yesu. Madee akiwa ni muislamu, hakupaswa kulinganisha taabu zake na mateso ya yesu.

Madee amekufuru.
kaimba bange...:(
 
ajaribu kujifananishe na Mtume Mohamed ndipo atajua mambo ya dini hayataniwi,ingekuwa kajifananisha na mtume nahisi saa hizi bakora zingetembezwa na fatwa kusoma,mnakumbuka marehemu Mwanyiro alivyochimbwa mkwara mzito kwa kuvaa kanzu akiwa stejini akingurumisha besi lake au Imani Madega alipochapisha tiketi zikiwa na dua na waislamu wakaja juu kwa kuona hizo tiketi zikiwa zimetupwa hovyo na zingine zimekanywaga,tukambiwa dua limesiginwa lol sisi wana wa kristu ama kwa hakika ni wavumilivu
 
Mungu amsamehe maana hajui atendalo. Tumwombee ili apate kuelewa na ujuzi wa kupambanua mambo.
 
Mara nyingi ukiangalia wasanii wa bongo wanakashifu sana dini ya kikristo na ukristo kwa ujumla kuna mfano kama huu wa Madee lakini pia kuna jinsi waigizaji wa Comedy wanavyo tumia vionjo vya Kikristo kufurahisha watu. Dini na mabo yake yote sio kwa ajili ya kufurahisha watu. Laiti Madee angelikuwa Mkristo akasema chochote cha namna hiyo kuhusu Waislam kesho uneona maandamanao nchi nzima...lakini tumfikishie ujumbe then tumkanye na kumsamehe maana hajui alitendalo.
 
Madee mwanamuziki wa midundo ya bongo flavor amekufuru kwenye wimbo wake anaosema amepata mateso makali kuliko ya Yesu.

Wakristo wanaamini kuwa hamna mtu amewahi kuteswa kama yesu. Madee akiwa ni muislamu, hakupaswa kulinganisha taabu zake na mateso ya yesu.

Madee amekufuru.


Historia imetufundisha kuwa wanamuziki huimba wimbo halafu baadaye yanakuja kutokea waliyoimba. Huenda Madee anajitabiria jambo..............halafu tatizo la huyu Bwana mkubwa anayeitwa Yesu huwa anajibu fasta...si unakumbuka 2pac baba ake madee kisanaa????? Badala ya misumari msalabani ilikuwa bulleeeeetssss ........
 
Historia imetufundisha kuwa wanamuziki huimba wimbo halafu baadaye yanakuja kutokea waliyoimba. Huenda Madee anajitabiria jambo..............halafu tatizo la huyu Bwana mkubwa anayeitwa Yesu huwa anajibu fasta...si unakumbuka 2pac baba ake madee kisanaa????? Badala ya misumari msalabani ilikuwa bulleeeeetssss ........

Inawezekana na huyu dogo madee yakamkuta ya mabomuuuu.
 
Kwa kweli amkekufuru..Kijilinganisha na YESU?angekuwa hai kama mateso yake yangekuwa makali kama ya YESU?YESU alikuwa baada ya mateso makali.
 
Yesu mwenyew ni a mythical figure.

The only blasphemy is the thought that anything - apart from the idea of something being blasphemous- can be blasphemous, the very medieval nature of that thought should be blasphemous - the only blasphemous thing- to a reasoning man.

Everything else, including Jesus, the Pope and Elizabeth the second, is game.

I doubt half of y'all can follow.
 
Ni kwamba hana adabu ukichanganya na ukosefu wa elimu ndio maana wanang'ang'ana na vina pasipo kuangalia usanifu wa lugha na maudhui. Huyu jamaa ndio anajiita Rais wa Manzese, kwa kweli anawakosea adabu wakazi wa eneo hilo kwa kujitangazia ukuu mtu mwenye upeo mdogo wa kufikiri kama yeye. Ndio maana sishangai kila siku yeye anatangaza mabifu tu na Afande Sele ambao wamemzidi kwa mbali katika fani hiyo ya muziki. Ipo haja hizi studio kuwa na editors wa lugha maana hata wazalishaji wengine wa muziki hawajui umuhimu wa lugha na athari zake kwenye muziki na masoko kwa ujumla.
 
Tuombe huo wimbo ufungiwe kwa kuwa unashusha hadhi ya mateso ya Yesu. Watoto wetu tunawafundisha kuhusu mateso makali aliyoyapata mkombozi wa ulimwengu sasa wakisikia huyo chizi kapata zaidi ya hayo, basi hawatamwamini huyu mwana wa Mungu.
 
Tuombe huo wimbo ufungiwe kwa kuwa unashusha hadhi ya mateso ya Yesu. Watoto wetu tunawafundisha kuhusu mateso makali aliyoyapata mkombozi wa ulimwengu sasa wakisikia huyo chizi kapata zaidi ya hayo, basi hawatamwamini huyu mwana wa Mungu.

Orangutang-like Ottoman Ombudsman on the onslaught of Orwellian obfuscation

We don't want the manifestation of the ugly head of censorship. Onc it starts, it will never stop.

Wakianza kufungia nyimbo kwa minajili kama hii who knows, kesho watatumia vigezo hivyo hivyo kufungia JF.

Hivi watu hawaoni paralells kati ya JF na Bongoflava? Mbona tunakuwa myopic hivi?

Society yoyote ilioyendelea inafahamu freedom of speech, na hii inajumuisha uhuru wa watu kubwabwaja. After all Yesu mwenyewe anasemwa kwamba alisema tukiwa na imani tunaweza kutembea juu ya maji kama yeye, sasa nyie mnaokimbilia kumkashifu huyu kijanain maana hamna imani kwamba anaweza kuw kama Yesu?

Kama hupendi mziki wake usinunue. Hizi habari za censorship zitawatokea puani mshindwe hata kuja kubweda hapa JF.
 
Utashangaa hawa wasema ovyo eti ndio wanaitwa wasanii wa kizazi kipya!! Kizazi kipya? Aibu kwao! Usanii wa ajabu ajabu tu, kuvaa milegezo na kuigiza maisha wasiyoyaweza.
 
Huyu kijana nina mashaka sana na elimu yake, exposure yake, watu wanaomzuka, mazingira aliyokulia na historia yake.
Lazima tukiyazingatia hayo tutagundua kuwa huyu ni nyani ng'ombe ndani ya mwili wa mwanadamu.
Hana nidhamu, kama hawezi kuheshimu wengine basi hawezi kujiheshimu hata yeye mwenyewe.
Huyu ni mwehu punguani.

hajatusi mtu wala kutukana sasa kati ya yeye na wewe nani anaonekana punguani na mwehu
 
Taarifa nilizozipata hivi punde Msanii huyu amefiwa na Girlfriend wake wa siku nyingi aitwae Pendo katika ajali ya Basi la Shabiby iliyotokea jana...
 
Oooh my god Pole zake kwa kufiwa na mpendwa wake..............
hakutakiwa kusema amepata mateso zaidi ya yesu ..
ameshawahi kutokwa jjashi lilichanganyika na damu????
 
Pole sana Madee....
Kipigo kama kilichompata Ayoubu kimekuanza hivyo.
heshima ni kitu cha bure rafiki.
 
Kwa vile yeye ni muislamu, na kwa vile waislamu wengi hawaamini kuwa YESU aliteswa, mimi simlaumu ila furahi amekubali kuwa YESU aliteswa- hilo ni jambo kubwa sana kuliko la kujilinganisha maana hiyo kila mtu anajua hajapata mateso hayo. Mimi namfagilia kwa hilo, yeye ni bora zaidi kuliko wachungaji, wakristo na maaskofu na wakristo wanaosema hakuna uponyaji katika zama hizi na mtu hawezi kuokoka duniani- si bora huyo mwanamziki ambaye hakani nguvu za YESU
 
Nashukuru wakristo mnasubira ingekuwa ni sisi waislam kamtaja mtume hivyo angejuta..
Fanya jokes na vitu vingine sio imani za watu na dini.. Ni bangi ndio zinazoimba sio yeye...

Namchukia mtu anaye leta mzaha na imani au dini ya mwingine... Vile vile mimi kama muislam sijafurahi na upuuzi wa madee maana yesu kwa imani yangu ni Mtume wa mungu..


Regards
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom