Dogo1
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 1,361
- 576
TAHADHARI KWA WANAONUNUA MAGARI: Kabla ya kununua gari ulilochagua, iwe show room au kwa mtu mwengine yeyote hakikisha kabla ya kufanya malipo chukua nambari ya chassis ya gari hilo na uwasiliane na ofisi ya Interpol iliyopo ghorofa ya saba Jengo la Makao Makuu ya Polisi mtaa wa Ghana mkabala na jengo la Posts ili waangalie kwenye system ya Interpol iwapo gari hilo halijawahi kusajiliwa kuwa ni la wizi miongoni mwa nchi zaidi wanachama wa Interpol duniani.
Bila kupata uhakika kutoka interpol kuna hatari ukanunua gari la wizi na ukajikuta unaliacha mikononi mwa polisi pindi ukikamatwa nalo wakati wa operesheni za interpol za kukamata magari ya wizi miongoni mwa nchi wanachama zinazofanyika kila Mwaka.