Mabalozi 12 wa CCM Arumeru Mashariki wahamia CDM?

Chama kilichojitafutia msingi mpya wa siasa za kuongopea wananchi kwa kila kitu kamwe hakiwezi kusimama pindi wananchi hao wanapofanikiwa kujua ukweli wote juu ya mienendo yake.

CCM kitalipa gharama kubwa ajabu kwa WaTanzania kwa kuishi kwa ulaghai na ufisadi miaka yote. Maadam vijijini kote Tanzania watu wameshafunguka na kuona mwanga mpya sasa kinachofuata ni CCM kubakia chama cha watu wa Masaki kule Dar es Salaam basi.

Habari hizi zimetoka kwa ka-nzi (kakitokea Arumeru) huko kuwa tayari hilo limeshafanyika..

Hawa ni mabalozi wa kata ya Maroroni huko Arumeru mashariki. Ati wameamua kuhamia CDM kwa sababu "hawana watu wa kuwaongoza kwani watu wao wote wameingia CDM"!
 
labda hiyo ni nyingine..maana ni jana tu kwenye mkutano uliofanywa na sugu na halima mdee hao mabalozi walirudisha kadi za ccm na mmoja liichana chana kwa hasira kisha wakachukua za chadema na wakamshukuru Mungu kwa kutua mzigo mzito ...mmoja alisema kila siku wanafatwa usiku na vuongozi wa ccm ili wanunue kadi za kupigia kura toka kwa wananchi......
Tunawashukuru kwa kujitambua na kuamua kufanya maamuzi yenye heri kwa mustakabali wa taifa letu ikifikia siku viongozi wengi wa ngazi ya shina wakafanya hivyo nchi nzima basi ukoloni mambo Leo wa CCM utanq'oka kabisa
 
kama sio hawa watu wanaoitwa mabalozi wa nyumba 10...usingekuta ccm bado ipo madarakani....hao ndio wanaongoza kwa kugawa kanaga kofia na hela za ccm


ni kweli ndugu. Mabalozi nyumba kumi ndiyo ngome yenyewe ya ccm. Mbinu iliyotumika kuwapata hawa 12 iendelezwe
 
Mkuu leo naona umeamua kumtukuza Mungu, Ameni atabaki kuitwa Mungu milele na sio Allah


Mungu ni mmoja tu na hatishiwi mawe wala barafu, ila vijimiungu viko vingi na vina majina kibao mengine hujawahi kuyasikia tangu uzaliwe na mengine hutayasikia hadi unakufa!!

Uliza waliotembelea india, china, japan, singapore, burma, tibet, na maeneo mengi ya mashariki ya mbali, au gugo 'gods'

NB. hata hapa kwetu wapo!!! Tembelea mitaa ya kisutu, utapatwa na kichefuchefu, ila sheria yetu ya uhuru wa kuabudu/kutokuabudu pamoja na itifaki zake zote zimezingatiwa.
 
Habari hizi zimetoka kwa ka-nzi (kakitokea Arumeru) huko kuwa tayari hilo limeshafanyika.. Hawa ni mabalozi wa kata ya Maroroni huko Arumeru mashariki. Ati wameamua kuhamia CDM kwa sababu "hawana watu wa kuwaongoza kwani watu wao wote wameingia CDM"!

Hawa wamefanya uamuzi sahihi! inabidi uwe na roho ya paka kuendelea kuitumikia CCM iliyofilisi nchi!
 
Maumivu ya kichwa huanza pooolepole, Mabalozi wa shina wamekosa watu wa kuwaongoza, mara Matawi yanakosa machina, mara majani yanakosa matawi na mwisho magamba yanakosa wa kuyavaa!!
 
Habari hizi zimetoka kwa ka-nzi (kakitokea Arumeru) huko kuwa tayari hilo limeshafanyika.. Hawa ni mabalozi wa kata ya Maroroni huko Arumeru mashariki. Ati wameamua kuhamia CDM kwa sababu "hawana watu wa kuwaongoza kwani watu wao wote wameingia CDM"!
.........mkuu mbona hili liko wazi tu, na bado, magamba yataisha yote
 
Mbona hii imetokea tangu wiki iliyopita mkuu na kutangazwa na REDIO WAPO FM Pekee hapa Tanzania.
Wale wale kina Wassira eti hii si habari kwa vile yeye alishasema jana, kama ilitoka wiki iliyopita mbona ulikuwa hujaiweka humu JF umesubiri MKJJ aiweke ndipo useme, hata hivyo hawa ni mabalozi wengine si hao unaowasema wewe kwa sababu kila siku wanahama.
 
Hii ni baada ya kuona upepo sio mzuri kwa upande wa CCM..Na bora wamefanya haraka maana walikuwa wanaelekea pabaya...
 
Kwa ninavyojua kila Balozi anasimamia kitongoji chake...ina maana hapa ni vitongoji 12....ni hatua nzuri sana kwa Cdm 2015,
Mabalozi si viongoziawa vitongoji wao wanaongoza nyumba kumi tu na hawa mara nyingi si viongozi wa serikali zaidi ya kutumika na chama cha mapinduzi kupitishia rushwa ya kanga, vitenge na kofia.
 
Habari hizi zimetoka kwa ka-nzi (kakitokea Arumeru) huko kuwa tayari hilo limeshafanyika.. Hawa ni mabalozi wa kata ya Maroroni huko Arumeru mashariki. Ati wameamua kuhamia CDM kwa sababu "hawana watu wa kuwaongoza kwani watu wao wote wameingia CDM"!

Kwa hiyo hao watu wakiamua kurudi tena CCM na hao mabalozi watarudi pia CCM au watandelea kubakia CDM?
 
Cha ajabu ni kipi unachojiuliza mabalozi 12 kuhamia cdm? Mwulize 6 na wakubwa wenzie wanasubiri yakutokea ktk ccm wapate sababu ya kujirasmisha cdm, na tayari kadi wanazo. Eboh chezea peoplz power wewe!!
 
Back
Top Bottom