Ishmael alizaa Maseyidi (watoto) 12 ambao ndio Waarabu wa leo. Eneo lao la umiliki ni kuanzia Saudi Arabia kuelekea Ashuru na mashariki ya Misri

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
ISHMAEL ALIZAA MASEYIDI(WATOTO) 12 AMBAO NDIO WAARABU WA LEO. ENEO LAO LA UMILIKI NI KUANZIA SAUDI ARABIA KUELEKEA Ashuru NA MASHARIKI YA MISRI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Kuna Watu wengi wanachanganya Madesa, kuchanganya waarabu na jamii zisizo na uhusiano na waarabu. Jamii za waarabu ni jamii zenye uhusiano wa kinasaba na uzao wa Ibrahimu ambazo zinatoka kwa mtoto wa kwanza wa Ibrahim aitwaye Ishmael kwa Mwanamke aitwaye Hajiri. Ikiwa jamii yoyote imetoka kwa Ishmael basi jamii hiyo inauhalali kuitwa Waarabu.

Hii ni kusema Muarabu ni mchanganyiko wa kidamu baina ya Muebrania" Hebrew"(Ibrahim) na Mmisri (Hajiri). Hapo ndipo anatoka Ishmael baba wa Waarabu aliyezaa Majumba, MASEYIDI, watoto kumi na mbili ambao ni jamii na jamaa zinajulikana leo kama Waarabu.

Ibrahim pia alizaa na Mwanamke mmoja aitwaye Ketura na kutoa mataifa mengine lakini hao sio waarabu. Hii ni nje ya mada.

Pia Ibrahimu alizaa na mkewe Sarah mtoto aitwaye Isaka ambaye huyu alitoa Mataifa Mawili, Waisrael kupitia Yakobo, na Waedomu kupitia Esau. Hii pia Ipo nje ya mada. Hao Waedomu na Waisraeli pia sio Waarabu kwani hawatokani na Ishmael ila wote ni ndugu kwa Baba yao Ibrahim.

Huwezi wataja Waarabu bila kumtaja Ibrahim na Sarah Mkewe kwa sababu bila Sarah kuchelewa kuzaa basi kusingekuwa na Waishmael. Huko pia ni nje ya mada.

Wanazuoni wakubwa wengi hupatana kuwa Waarabu Baba yao ni Ishmael na Babu yao ni Ibrahim.

Tofauti ya Waisraeli na Waarabu ni kuwa Waarabu wanaasili ya Afrika kupitia Wamisri(Hajiri).

Hajiri aliahidiwa na Malaika akiwa na mimba kuwa atamzaa Mtoto wa kiume na akaamrishwa amuite Ishmael, yaani Bwana amesikia mateso yake" utabiri ukaambatana na Baraka kuwa Mtoto huyo atatoa taifa kubwa lakini litakalopitia magomvi na misukosuko (sijajua kikomo chake)
Mwanzo 16:11-12
[11]Malaika wa BWANA akamwambia, Tazama! Wewe una mimba, utazaa mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Ishmaeli, maana BWANA amesikia kilio cha mateso yako.

[12]Naye atakuwa kama punda-mwitu kati ya watu, mkono wake utakuwa juu ya watu wote na mkono wa watu wote utakuwa juu yake, naye atakaa mbele yao ndugu zake wote.

Baada ya Hajiri na Ishmael kufukuzwa wakaelekea. Wakaelekea kuishi katika jangwa la Paran ambapo kwa leo ni kusini kwa nchi ya Saudi Arabia. Ukisema Saudi Arabia hutokuwa unakosea. Huko Kijana akakua. Maana yake akarudi kwao Misri kumchukulia kijana wake Mke. Kijana akaoa mke wa kimisri kama alivyo mama yake.

Mwanzo 21:20-21
[20]Mungu akawa pamoja na huyo kijana, naye akakua, akakaa katika jangwa, akawa mpiga upinde.
[21]Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.

Ukaaji wa jangwani na uwindaji na maisha ya kuhamahama (Nomad life) na kufanya uchuuzi na biashara ( Merchant) ndiko asili ya jina Arab. Hivyo kusema Arab kiasili utarejelea neno Jangwa au maisha ya kuhamahama.

Ishmael akajaliwa kupata watoto, majumbe kumi na wawili. Ambao waliitwa Waishmael " Ishmaelites" ambao nao walizaa jamii na jamaa zao.

Waishmael waliishi maeneo mengi ya mashariki ya kati, Kaskazini mwa pembe ya Afrika, kuanzia maeneo ya Somalia kaskazini, Arabia Peninsula mpaka maeneo ya Nchi za Hindi.

Mwanzo 25:16-18
[16]Hao ndio wana wa Ishmaeli, na hayo ni majina yao, katika miji yao, na katika vituo vyao, maseyidi kumi na wawili kwa kufuata jamaa zao.
These are the sons of Ishmael, and these are their names, by their towns, and by their castles; twelve princes according to their nations.
[17]Na hii ndiyo miaka ya maisha ya Ishmaeli, miaka mia na thelathini na saba. Akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake.
And these are the years of the life of Ishmael, an hundred and thirty and seven years: and he gave up the ghost and died; and was gathered unto his people.
[18]Wakakaa toka Havila mpaka Shuri, unaoelekea Misri, kwa njia ya kwenda Ashuru. Akakaa katikati ya ndugu zake wote.
And they dwelt from Havilah unto Shur, that is before Egypt, as thou goest toward Assyria: and he died in the presence of all his brethren.

Ishmael alizikwa alipozikwa Baba yake Ishmael. Pia Ishmael alimzika Baba yake Ibrahim.

Waarabu na Waisrael na Waedomu na jamii zote zinazotokana na Ibrahim zinafanana kiutamaduni kwa kiwango kikubwa. Ingawaje kuna utofauti kama wao wenyewe walivyo na utofauti wa kimaumbile kutokana na Mama zao kuwa na asili tofauti.

Gen 25:18 “These descendants of Ishmael were scattered across the country from Havilah to Shur (which is a little way to the northeast of the Egyptian border in the direction of Assyria)…compare
to 1Samuel 15:7 where Saul 'butchered the Amalekites from Havilah all the way to Shur, east of Egypt’ ..compare
Exodus 17:8 when “the Amalekites came and attacked the Israelites at Rephidim"
Based on these scriptures the ancient 'land of Havilah’ would be located in what is now Saudi Arabia.

Waishmael kutokana na shughuli zao za uchuuzi na biashara ( Merchantalism) ndio waliomnunua Yusufu kutoka kwa wanawayakobo na kwenda kumuuza Misri. Zingatia Waishmael na Waisraeli wakati huo walikuwa wanajuana kabisa kuwahi Babu yao ni mmoja ambaye ni Ibrahim.

Kuhusu ugomvi unaoendelea hapo Palestina, Ibrahim ambaye ndio chanzo kikuu cha mzozo huo yeye alimrithisha Isaka pekeake eneo hilo.
Huku akisahau au kupuuza iwe kwa bahati mbaya au makusudi kuwapa urithi watoto wake wengine akiwepo Ishmael na watoto wa Ketura.

Hii inatupa funzo sisi wababa yakuwa tunapotaka kutoa urithi tusitoe kwa upendeleo kwani inaweza kuleta matatizo.

Ingawaje siku hizi wapo wanaosema Uarabu ni utamaduni na haihusiani na Masuala ya damu, yaani mtu anaweza kufanyiwa assimilation akawa muarabu kwa kuwa na tamaduni za kiarabu. Hiyo inaweza kuwa sawa. Ni kama vile Wayahudi nao wanasheria hiyo ya kumsilimisha mtu asiyemyahudi kuwa MYAHUDI kwa utaratibu maalum. Hata Wafaransa nao walifanya hivyo.
Lakini tukizungumzia Masuala ya vinasaba basi Huwezi kuwa muarabu kama huna vinasaba au damu ya Ishmael. Mama au mama yako akiwa muarabu basi wewe utaitwa muarabu. Halikadhalika na kwa wayahudi na wafaransa na mataifa mengine.
Lakini hiyo ya kusilimishwa, assimilation ni mambo ya kisiasa tuu.

FaizaFoxy, Wairan, Wamedi(Iraq) Waashuru ( Syria) hao sio waarabu. Na sikatai kuwa zipo jamii na jamaa au makabila ya waarabu yanayoishi katika mataifa hayo. Ni kama hapa Tanzania kuna waarabu lakini huwezi sema Watanzania ni waarabu. Pia wapo machotara waliozaliwa.

Taikon acha nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Ila ukweli ni kwamba hao wapalestina sio waarabu kwa sababu hawana mafungamano yoyote na Ismael wala Ibrahim na kihistoria inasemekana hawa watu walitokea huko nchini Ugiriki kwenye kisiwa cha Crete milenia nyingi zilizopita hali inayoonyesha kwamba hii jamii wala sio Semitic People kama wengi wanavyodhani.
 
Edomu(Edomite), siyo uzao wa Ketura, bali ni uzao wa Esau. Soma mwanzo sura ya 36View attachment 2783484View attachment 2783485
 
Ibrahim hakuwa muarabu mtu wa katikati ya iraq huko na, hajiri alikua ni cheusi wa misri ..hao waarabu wa ishmael wanatokea wapi?
The point is pengine Ibrahim hakuwahi kuwepo is just a myth.

Biblia anafanya hadithi za Ibrahim zionekane kama matukio ya Jana, but the reliatity is miaka kati ya Yesu na Ibrahim ni miaka 3000 kati ya Mtume na Ibrahim ni miaka 4000, hata sisi tunaweza tukamuunganisha Mbowe na kizazi cha Ibrahim.

Hadithi zote za Musa, Ibrahim, Noah ni Mapokeo ya watu wa Mashariki ya kati
 
Ishmael hakuwa baba wa waarabu maana hakuwa mwarabu why?

Yakobo alizaa na mwanamke wa kimisri ambaye kwa mujibu wa vitabu misri ni mwana wa ham (ukoo wa jamii ya watu weusi) hivyo basi hata mtoto aliyezaliwa kutoka kwa ibrahimu ambaye nae race yake ina utata(si mwarabu si mzungu) hivyo ishmael lazima angekuwa Afro-Asiatic, mujue kuwa misri ya kale sio hii ya leo inayokaliwa na majizi mapandikizi kutoka uarabun, misri ya kale ilikuwa ardhi isiyo na watu weupe.

Hivyo basi mwana wa Yakobo si mwarabu na si baba wa waarabu na hakuitwa ishmael kwakua hana Asili wala , uhusika na watu wa Asia.

Qur'an imeharibu sana historia ya babu zetu kwa kuiba na kuweka ktk vitabu vyao vyenye stori za kubuni.

Someni vizuri na muelewe hizo dini tumepigwa, tumefundishwa vitu vingi vya uongo.

Mwarabu asili yake haihusiki na huyo ishmael wa mchongo, Yakobo hausiki na uzao wa waarabu wala jamii ya hao waisrael wa uongo hapo middle east.

Siku si nyingi mtakuja kugundua ushenzi wa hizi dini zilizoharibu mfumo wa maisha kwa kuwapandikiza uongo+chuki.
 
Where did the Palestinians come from in the Bible?
The Philistines are first mentioned in the Bible in Genesis 10:14 in the Table of Nations as being the descendants of two people groups called the “Pathrusim and Casluhim.” These folks were sea people and invaded Egypt in waves, from 2400 BC and again in a significant way in 1200 BC

Who was the father of the Philistines in the Bible?

The Hebrew Bible mentions in two places that they originate from a geographical region known as Caphtor (possibly Crete/Minoa), although the Hebrew chronicles also state that the Philistines were descended from Casluhim, one of the 7 sons of Ham's second son, Miṣrayim.
 
Wafilisti ndio wapalestina? Wafilisti ni wachaga bwana
 
Back
Top Bottom