Ijue Hadhi ya Ubalozi, its Rights & Privileges. Wajua Kufutwa Ubalozi Dr. Slaa Hakutokani na Ukosoaji wa Bandari na Anaweza Kurejeshewa Ubalozi Wake?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,608
Wanabodi
Juzi September Mosi Imetolewa taarifa ya Ikulu kumhusu aliyekuwa Balozi Dr. Wilbroad Slaa kufutiwa hadhi ya Ubalozi, taarifa hiyo ya Ikulu haikutoa sababu za kumfutia hadhi hiyo ya Ubalozi.

Hatua hii imezua mijadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii wengi waki speculates sababu za kufutiwa hadhi ya Ubalozi ni kwasababu ya ukosoaji wake wa mkataba wa DPW na Bandari zetu.

Kwanza naomba ifahamike wazi, hakuna kosa lolote kwa mtu yoyote, mwenye hadhi yoyote, kufanya ukosoaji wowote, wa jambo lolote, as long as ukosoaji huo haukiuki sheria yoyote.

Hivyo Dr. Wilbroad Slaa ana haki ya kukosoa jambo lolote kama ilivyotolewa na ibara ya 18 ya Katiba yetu kwenye freedom of speech and expression.

Ubalozi ni hadhi ya kimataifa inayoendana na rights na privileges fulani fulani zikiandamana na immunities, hivyo ubalozi una masharti ya kufuatwa mtu unapokuwa Balozi na kuna vitu hutakiwi kuvifanya.

Hili ni bandiko elimishi kuhusu
Ijue Hadhi ya Ubalozi, its Rights & Privileges. Wajua Kufutwa Ubalozi Dr.Slaa Hakutokani na Ukosoaji wa Bandari na Anaweza Kurejeshewa Ubalozi Wake?

Miongoni mwa privileges na immunities za diplomatic status ni pamoja na kinga ya kibalozi, ya kutokushitakiwa popote kwa kosa la jinai.

Mtu yoyote mwenye hadhi ya Ubalozi akitenda jinai yoyote, kabla hajapandishwa mahakamani kushitakiwa, hatua ya kwanza ni kuvuliwa kwanza hadhi ya Ubalozi, ndipo aweze kushitakika kwasababu hadhi ya Ubalozi ina kinga ya kibalozi kutokushitakiwa.

Kuna msemo wa Kiswahili usemao, ukiona zinduna, ujue ambari iko nyuma!, au dalili ya mvua ni mawingu na panapo fuka moshi chini kuna moto!.

Kuvuliwa huku Ubalozi kwa Dr. Slaa ni Zinduna, ni mawingu, ni kufuka tuu kwa moshi, ajiandae kuipokea Ambari, kujikinga na mvua na kuuzima moto unaokuja.

Hii sio mara ya kwanza kwa mtu mwenye hadhi ya Ubalozi kuvuliwa hadhi hiyo, wa kwanza ni balozi wetu wa kwanza jijini London nchini Uingereza Balozi Christopher Kasanga Tumbo, alivuliwa Ubalozi na kushitakiwa kwa jinai enzi za Nyerere. Mwingine ni Balozi Antony Pastor Ngaiza alivuliwa Ubalozi na kushitakiwa kwenye ile kesi ya uhaini ya mwaka 1982. Pia Balozi Prof. Costa Rick Mahalu akivuliwa hadhi ya Ubalozi na kushitakiwa kwa uhujumu ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania jijini Rome nchini Italy, alliposhinda kesi na kukutwa hana hatia, alirejeshewa Ubalozi wake.
.
Hivyo hata kwa Dr. Slaa, tusubirie yatokanayo na kufutiwa hadhi hii ya Ubalozi, yakishindwa kuthibitishwa, anarejeshewa Ubalozi wake.

Kwa vile hili ni bandiko elimishi, nitakuelimisha kidongo na kwa kifupi
  1. Hadhi ya Ubalozi ni nini?
  2. Sifa za mtu kuwa na hadhi ya Ubalozi ni zipi?
  3. Kuna cheo cha Ubalozi (career diplomats) na Ubalozi wa kuteuliwa.
  4. Privileges za diplomatic status ni zipi?.
  5. Ijue diplomatic immunity
  6. Je kila Balozi lazima awakilishe nchi ubalozini?
  7. Jee maofisa wote ubalozini ni mabalozi au wana hadhi za Ubalozi?
  8. Wajue Local Staff ubalozini wasio na hadhi za Ubalozi
  9. Ukifanya makosa gani unapoteza hadhi ya Ubalozi?
  10. Jee kila diplomat anayefanya jinai ni lazima avuliwe Ubalozi?.
  11. Ijue diplomatic Bag?
  12. The Doctrine of Diplomatic Reciprocity
  13. Jee mwenye diplomatic status ni Balozi?.
  14. Jee kila mwenye diplomatic passport ni diplomats?
  15. Maisha baada ya kuvuliwa Ubalozi, psychological depression etc.
  16. Wajue Wafanya Biashara Matajiri wenye diplomatic status na sio mabalozi!
    1. Balozi ni Nani na Hadhi ya Ubalozi ni nini?- Neno Balozi maana yake ni Mwakilishi, au mjumbe. Hata Balozi wa nyumba 10 ni mwakilishi wa zile nyumba 10 mtaani, ambapo enzi za chama kimoja, mabalozi wa nyumba 10 walikuwa very strong. Balozi wa nchi ni mwakilishi wa nchi moja kwenye nchi nyingine. Hadhi ya ubalozi ni hadhi anayokuwa nayo huyo mwakilishi, hadhi inayoitwa diplomatic status. Mtu mwenye diplomatic status anakuwa na hadhi fulani inayoambatana na some rights na privileges za hadhi hiyo. Privileges kubwa ya kwanza ni kupatiwa a diplomatic passport, hivyo anakuwa ni VIP, akisafiri anapitia VIP, na kupatiwa huduma zinazoitwa diplomatic services. Rights and privileges za diplomatic status zinaongozwa na mkataba wa kimataifa wa Viena Convention on diplomatic relations ambapo kila nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa, UN, lazima auridhie, hivyo Tanzania tumeridhia. Hii Vienna Convention was adopted on 14 April 1961, hivyo Tanzania tumeingizwa na wakoloni tulipokuwa bado Tanganyika ila kuna optional protocol ambazo Bunge la Tanganyika tuliratify na tarehe 24/06/1964, Balozi wetu UN, Chief Erasto Mang'enya akazi file kule UN kwenye central depository ya UN kwa No.7311 na hii niliiona wakati niki reach mkataba wetu wa muungano kule UN, huyu Balozi ali file tuu NV no. 14 May, 1964 na kwenye NV hiyo akasema The Articles of Union ziko attached, but in reality, there was no attachment!. Kila NV inayokuwa filed, kuna back copies MFA na Ubalozi wetu UN, nilipoulizia ubalozini nikaomba kuonana na Balozi, yule shemeji yetu akaniwekea kauzibe ya kuandika barua ku fix appointment!. Niliporejea Bongo nikaamua ku seach Nyaraka za Taifa, mkataba ule haukuwepo hivyo nikauliza Je, wajua kuwa kuna uwezekano Tanzania sio nchi halali Kisheria (De Jure) Bali ni De Factor?!
    2. Sifa za mtu kuwa na hadhi ya Ubalozi ni zipi? . Mtu yoyote mwenye elimu yoyote na sifa zozote anaweza kuteuliwa kuwa Balozi, hakuna kigezo cha elimu wala uzoefu, ila maofisa ubalozi ndio wanapaswa kuwa na sifa fulani fulani. Ila kabla ofisa ubalozi yoyote hajapostiwa kituo cha kazi, CV yake na public as well as private life status inatumwa nchi husika, hiyo nchi inawatumia maofisa wake (wale jamaa zetu) ku verify data zako ndipo ikuruhusu kuja. Na ukiisha wasili wale jamaa hukufanyia security clearance, ndipo nchi husika imruhusu Balozi kuleta credentials zake kwa Mkuu wa nchi husika. Sisi kuna mabalozi tumewahi kuwakatalia wakiwemo mabalozi toka nchi za ulaya wale zile tabia za ajabu ajabu ambazo nchi mwetu hazikubaliki!. Na kuna Balozi wetu fulani, baada ya kukubaliwa alipofika nchi husika, utambulisho ukagomewa kupokelewa for a long time, ila baadae akakubaliwa, ila juzi kati hapa alipokula uteuzi fulani mnene, ndio nikajua kwanini ile inchi ilitaka kumgomea!. Wengi wa maofisa ubalozi wanchi mbalimbali ni 'wale jamaa' hivyo wakiwa kule vituoni hufanya kazi mbili mbili!, hivyo kwenye balozi zetu tunapeleka wale wana diplomasia diplomasia na wana diplomasia 'diplomasia!..
    3. Kuna cheo cha Ubalozi (career diplomats) na Ubalozi wa kuteuliwa. Kuna mabalozi ambao ni carriers diplomats wanasomea kabisa mfano Wizara ya Nje, MFA, mtu anapanda cheo hadi kufikia level ya juu kabisa ya Balozi, na kuna mabalozi wa kuteuliwa tuu, wale mabalozi wa kuteuliwa tuu, wakiboronga ndio hadhi yao ya ubalozi inafutwa, lakini wale carrier diplomats ubalozi wao ni cheo, huwezi kufutwa ila tuu anaondolewa hadhi na bado anaendelea kuwa Balozi. Mabalozi wana diplomasia diplomasia wakivuliwa hadhi ya Ubalozi, baadaye utajua sababu, lakini wale wana diplomasia 'diplomasia' wakivuliwa hadhi ya Ubalozi itatangazwa tuu ila sababu hutazijua!.
    4. Privileges za diplomatic status ni zipi?. Rights and privileges za ubalozi ziko nyingi baadhi ya haki hizo ni mke/wake na familia ya diplomat wote wanapatiwa diplomatic passport, wenzi wao wanalipwa allowance ya spouse, watoto wao up to 4, wanalipiwa international school, eneo la ubalozi na nyumba za ma diplomats linahesabika ni nchi husika hivyo lina diplomatic immunity, police haruhusiwi kuingia, au kukamata mtu, hivyo mhalifu yoyote au hata kibaka akifanya uhalifu na kukimbilia ubalozi wowote, hawezi kukamatwa mpaka ubalozi wenyewe wamripoti na kuruhusu akamatwe, kama ilivyotokea kwa Jullian Asange au Tundu Lissu. Ukitafutwa na polisi ukambilia ubalozi wowote, polisi hawawezi kukukamata, ila watakungojea hapo nje, ukitoka tuu unadakwa!. Ila hapo ulipokimbilia wakijiridhisha na sababu za wewe kukimbilia ubalozini, ili usikamatwe, ubalozi huo unakupatia kitu kinachoitwa asylum status, unapatiwa Diplomats status ya nchi iliyo kuhifadhi, unasafirishwa kwa diplomatic car, huwezi kukamatwa hivyo unapelekwa airport na kuruhusiwa kuondoka nchini under diplomatic status hivyo hukamatwi. Privileges nyingine ni a diplomatic car with diplomatic number plate kwa Tanzania ni CD, gari la Balozi lina number ya CDM1, Balozi akiwemo lina peperusha bendera ya nchi husika, ikitokea kuna foleni yoyote, CDM1 imawasha tuu taa na inapishwa njia kama fire, ambulance na vingora!. Diplomats pia hawalipi kodi, wana vitambulisho maalum na nchi nyingine maduka maalum ambayo ni duty free. Privileges nyingine ni wanalipwa allowances za kuwawezesha kuishi very comfortably hivyo mishahara yao yate kuwa kama ni akiba tuu, kuanzia nyumba bure, usafiri bure, ada unalupiwa, spouse wanalipwa, kuna family allowance ya up to 4 dependants, unatibiwa bure, unasafiri Business Class balozi 1st class, etc etc, mwenza anapewa preferential treatment ya kuajiriwa ubalozini as a local staff. etc etc.
    5. LIjue mtu kuwa a diplomats na diplomatic immunity ni kinga mbalimbali za kibalozi anazopewa mtu mwenye hadhi ya ubalozi, kinga hizi zina hadhi mbalimbali, kuna ma diplomats wenyewe ni wale maofisa ubalozi wenye hadhi za ubalozi na nyingine ni maofisa ubalozi wenye hadhi zisizo na diplomatic immunity, wakiwemo family members au maofisa wa kawaida wa ubalozi wenye diplomatic passport ila hawana diplomatic immunity.
    6. Je kila Balozi lazima awakilishe nchi ubalozini?, hapana, kama nilivyosema kuna mabalozi wa kuteuliwa na mabalozi wa kuajiriwa. Kwenye mabalozi wa kuajiriwa unaweza ukapanda cheo hadi kufikia level ya Balozi, lakini ukaishia kuwa a desk officer pale MFA. Kuna nafasi fulani fulani ili uteuliwe zinashikwa na mtu mwenye hadhi ya Balozi, ukiwemo cheo cha Katibu Mkuu Kiongozi, Mkuu wa Chuo cha Diplomasia, au mtu mwingine yeyote anaweza kuteuliwa cheo cha Balozi na asipostiwe nchi yoyote!.
    7. Jee maofisa wote ubalozini ni mabalozi au wana hadhi za Ubalozi? Hapana, kwenye Balozi zote kuna maofisa ubalozi wenye hadhi za Balozi na kuna maofisa ubalozi wasio na hadhi ya ubalozi, wanakuwa ubalozini ila sio wote ni diplomats. Pia kuna taasisi za kimataifa maofisa wake wana hadhi za ubalozi wakiwemo Jumuiya ya Africa Mashariki, na taasisi zake, AU, EU, SADIC, Central Corridor, na mashirika yote ya UN, kwa US, hadi VSO, US Aid etc.
    8. Wajue Local Staff ubalozini wasio na hadhi za Ubalozi hawa ni maofisa ubalozi wengine wote ambao hawafanyi kazi za kibalozi, lakini wana diplomatic status bila diplomatic immunity na wengine wameajiriwa kama local staff. Mfano yule shemeji yetu wana JF, wa ubalozi wetu pale New York, ni local staff (naomba msiniulize nani). Hawa local staff wanaajiriwa Balozi zote kama wenyeji ambapo wenza wa diplomats wanapewa preferential treatment ya kuajiriwa as locals.
    9. Ukifanya makosa gani unapoteza hadhi ya Ubalozi? hadhi ya ubalozi ni hadhi ya heshima sana, mtu anapoteuliwa kuiwakilisha nchi yetu kama Balozi lazima uwe ni mtu muadilifu and well behaving person with integrity na usiwe mlevi, mhuni, mropolaji, you have to be smart both upstairs and look ndio maana wana good dressing allowances. Maofisa ubalozi wote wanatakiwa wasifanye makosa ya jinai na kuzingatia miiko ya diplomatic immunity, na kama nilivyosema kule nyuma, maofisa wengi wa ubalozi ni 'wale jamaa zetu' wa kazi mbilimbili, ili kuwadhibiti maofisa hawa wasinuse nuse kila kitu mpaka jikoni and sometimes chumbani, ile Vienna Convention imeweka utaratibu ofisa ubalozi yoyote akitaka kufanya jambo lolote nje ya shughuli za kawaida za kibalozi, lazima aandike barua ya kibalozi iitwayo Note Verbale MFA kuomba kibali na kujibiwa ndipo ajichanganye. Sasa ili kupunguza huu mlolongo wa kuomba ruhusa kila leo, baadhi ya Balozi zimewaajiri the locals na huwatumia hao locals
    10. Jee kila diplomat anayefanya jinai ni lazima avuliwe Ubalozi?. No sio lazima!. Kuna jinai za aina mbili, jinai ya kwanza ni jinai in the line of duty, na jinai ya pili ni jinai ya personal. Diplomats akifanya jinai in the line of duty, nchi husika ama inamfukuza na kulazimisha nchi yake kumpa recalls kumrejesha nyumbani. Lakini akifanya jinai personal kama ulevi, uzinzi, kusababisha ajali, au jinai nyingine yoyote ikiwemo kuua, anapaswa avuliwe hadhi ya ubalozi na sheria za nchi husika kuchukua mkondo wake. Lakini kwa maofisa ubalozi wa nchi za kibeberu zikiongozwa na kubwa la mabeberu, Marekani, ofisa wake ubalozi popote akifanya jinai, nchi yake ina m shield kwa kumuondoa fasta, kumrejesha nyumbani fasta, nakifika kule anavuliwa ubalozi fasta na kumstaafisha, nchi husika ikimhitaji kuja kujibu tuhuma, jamaa wanasema he is retired no whereabouts zake ili kumkingia criminal liabilities, kama yule ofisa aliye tutafunia dada zetu, baada ya kumtafuna akamshusha, akageuza akam hit and run, akadakwa akatiwa nguvuni kesho yake Balozi wa Marekani akamtoa na kumsepesha Marekani!.
    11. Ijue diplomatic Bag? Hii ni mizigo ya ubalozi ambayo huingizwa na kutolewa bila kukaguliwa, mizigo hii ina kinga za kidiplomasia hairuhusiwi kukaguliwa. Rais wa nchi anaposafiri, pia mizigo yote ya msafara wa rais inapewa hadhi ya diplomatic bag, hakuna cha kodi wala ukaguzi. Serikali za wasio waaminifu huutumia mwanya huu kubeba mambo yao!. Rais Hu Jin Tao wa China alipokuja nchini, alikuja ni midege hiyo...!. Siku anaondoka midege ilikuwa inapakia mzigo usiku kucha, kila mzigo una stika ya diplomatic bag!, baada ya mgeni kuondoka, waliopakia mzigo wakatoa siri wamepakia nini, story ya kilichobebwa usiku kucha ikaibukia Al Jazeera, MFA wetu akakanusha, tukauliza humu Membe amejuaje Contents za 'Diplomatic Bag'? Uwezo kukanusha kaupata wapi? - Tusidanganyane! na kwa wale wa zamani, naamini mnakijua kisa cha Umaru Dikko kutaka kuwa smuggled out of UK, kurejeshwa Nigeria kama mzigo kwenye diplomatic bag, Scotland Yard wakalazimisha kufungua, ndipo kukuta smuggled person!, uhusiano wa kibalozi ilibidi uvunjike.
    12. The Doctrine of Diplomatic Reciprocity hii ni kanuni ya kufanya malipizi, pale ofisa ubalozi wako anapofanya makosa fulani nchi ya kigeni na kufukuzwa, ili yako kuonyesha inapinga huko kufukuzwa na inchi yako inaamua kuwafukuza idadi ya maofisa wako bila kosa lolote!. Hii inaitwa Tit for tat!.
    13. Jee kila mwenye diplomatic status ni Balozi?. Sio kila mwenye diplomatic status ni Balozi, waheshimiwa wabunge wetu wana diplomatic passport lakini wote sio mabalozi. Wakuu wa taasisi mbalimbali za Kitaifa na kimataifa wana diplomatic status na sio mabalozi
    14. Jee kila mwenye diplomatic passport ni diplomats? sio kila mwenye diplomatic passport ni Balozi, kuna watu kibao wana diplomatic passport na sio ma diplomats. Kuna Wafanyabiashara matajiri wengi wenye diplomatic status na sio mabalozi!, having a diplomatic passport ni kitu kizuri kwa mfanya biashara yoyote mkubwa, just for easy passage, hivyo kuna wafanyabiasha kibao, wakubwa nawafahamu wana diplomatic passport na sio mabalozi, it's about connections. Waheshimiwa wabunge wana diplomatic passport, wakuu wa taasisi zote nyeti wana diplomatic passport, hata wajanja wa mujini wanazo na wanaishi kama ma diplomats.
    15. Maisha baada ya kuvuliwa Ubalozi, psychological depression etc. Mtu mwenye diplomatic status, kama maisha yake aliyaendesha kwa kutegemea diplomatic status, kitendo cha kuvuliwa hadhi ya ubalozi, hatua ya kwanza ni kuchukua diplomatic passport yao, hivyo sasa ukisafiri unapanga foleni huku kajamb. nani!, hakuna watumishi wa kukubebea mizigo yako, kinachofuatia ni psychological depression na hapo hapo psychosomatic disease zinakubishia hodi usipo gangamala, ni soon...! . Kwa hili sina shaka na Dr. Wilbroad Slaa kwasababu, kwasababu tukubali tulatae kuna makabila wagumu na kuna makabila laini laini, wateke!. Mtu wa makabila wagumu akipata matatizo ana gangamala!, Dr. Slaa ni kutoka kwa wagumu!, anaweza kushindia mihogo, na akadunda, hivyo kumvua ubalozi hakuta mtisha kitu wala hakuta mbabaisha!. Pia kuna kitu kizuri kuhusu kuvuliwa hadhi ya ubalozi for criminal liabilities, anayevuliwa hiyo hadhi ni yeye mhusika tuu pekee, wategemezi wanaendelea kupeta na diplomatic passports.
Paskali
Mwandishi ni mwana habari aliyefanya kazi ubalozi fulani kwa miaka 4, as a local staff na kufutia fani yake ya uandishi wa habari, ametembelea Balozi za Tanzania katika nchi nyingi za Africa, Ulaya. Asia na America, atawaletea visa na mikasa mbalimbali ya balozi zetu mbalimbali.
 
Wanabodi
Juzi September Mosi Imetolewa taarifa ya Ikulu kumhusu aliyekuwa Balozi Dr. Wilbroad Slaa kufutiwa hadhi ya Ubalozi, taarifa hiyo ya Ikulu haikutoa sababu za kumfutia hadhi hiyo ya Ubalozi.

Hatua hii imezua mijadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii wengi waki speculates sababu za kufutiwa hadhi ya
Damage control!
 
Noted but hayo uliyasema kibongobongo hayatekelezeki ,Kwa mfano Sheria za vyombo vya habali zipo wazi uhuru ,mipaka yao nakadharika lakin mbona Huwa waziri au kiongozi yeyote anaweza piga mkwala taarifa frani itoke au istoke

Slaa ni kweli ana hadhi ya ubalozi kibongobongo hata Kama ikidhibitika Hana hatia hawez rudishwa ubalozini.
 
Brother Mayalla sikukatalii bali nakazia tu kuwa ndani ya ccm lolote linawezekana tu.
Hadhi ya Ubalozi has nothing to do with CCM, tena usikute hata Rais has nothing to do with Dr. Wilbroad Slaa, lakini kwa vile Rais ndio mamlaka, amelazimika kutimiza wajibu wake ili mambo mengine yaendelee, ikukutikana sio kweli na hahusiki, anarejeshewa Ubalozi wake!.
P
 
Kwa hiyo unataka tuamini kwamba kufutiwa hadhi yake ya Ubalozi haihusiani na ukosoaji wa serikali ya mama SSH? Bro, haya mambo mengine hayahitaji shahada ya sheria au PhD. Yapo wazi. Why him and not someone else?
reality is: hivi vyeo vya kupeana kirafiki au kwa vile mtu amekufurahisha, hata kunyanganywa…..ni hivo hivo.

Kwa Tanzania yetu survival ya mtu kwenye mfumo ni matakwa ya watawala. Ndo maana kila mtu ni muoga kusema au kufanya lolote lenye mlengo tofauti na watawala.

Hata mtu akiangalia uchambuzi wako, your perspective is telling.

Wasalaam,
 
Mimi sio mshauri wa yoyote, ni mtu tuu mwenye ufahahamu wa issues za kidplomasia hivyo kujitolea kuelimisha watu humu kuhusu mtu kufutiwa hadhi ya Ubalozi Hakutokani na Ukosoaji, bali kufutiwa kule ni Zinduna tuu, Ambari iko nyuma...
P
Tanzania sheria zinatekelezwa kutokana na utashi wa kiongozi aliye madarakani na genge lake. Hata uorodheshe vipi matakwa ya kisheria ya ubalozi, bado utekelezaji utafuata mtazamo wa kiongozi na genge lake. Hivyo utakacholeta ni story za furahisha genge.
 
Wanabodi
Juzi September Mosi Imetolewa taarifa ya Ikulu kumhusu aliyekuwa Balozi Dr. Wilbroad Slaa kufutiwa hadhi ya Ubalozi, taarifa hiyo ya Ikulu haikutoa sababu za kumfutia hadhi hiyo ya Ubalozi.

Hatua hii imezua mijadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii wengi waki speculates sababu za kufutiwa hadhi ya Ubalozi ni kwasababu ya ukosoaji wake wa mkataba wa DPW na Bandari zetu.

Kwanza naomba ifahamike wazi, hakuna kosa lolote kwa mtu yoyote, mwenye hadhi yoyote, kufanya ukosoaji wowote, wa jambo lolote, as long as ukosoaji huo haukiuki sheria yoyote.

Hivyo Dr. Wilbroad Slaa ana haki ya kukosoa jambo lolote kama ilivyotolewa na ibara ya 18 ya Katiba yetu kwenye freedom of speech and expression.

Ubalozi ni hadhi ya kimataifa inayoendana na rights na privileges fulani fulani zikiandamana na immunities, hivyo ubalozi una masharti ya kufuatwa mtu unapokuwa Balozi na kuna vitu hutakiwi kuvifanya.

Hili ni bandiko elimishi kuhusu
Ijue Hadhi ya Ubalozi, its Rights & Privileges. Wajua Kufutwa Ubalozi Dr.Slaa Hakutokani na Ukosoaji wa Bandari na Anaweza Kurejeshewa Ubalozi Wake?

Miongoni mwa privileges na immunities za diplomatic status ni pamoja na kinga ya kibalozi, ya kutokushitakiwa popote kwa kosa la jinai.

Mtu yoyote mwenye hadhi ya Ubalozi akitenda jinai yoyote, kabla hajapandishwa mahakamani kushitakiwa, hatua ya kwanza ni kuvuliwa kwanza hadhi ya Ubalozi, ndipo aweze kushitakika kwasababu hadhi ya Ubalozi ina kinga ya kibalozi kutokushitakiwa.

Kuna msemo wa Kiswahili usemao, ukiona zinduna, ujue ambari iko nyuma!, au dalili ya mvua ni mawingu na panapo fuka moshi chini kuna moto!.

Kuvuliwa huku Ubalozi kwa Dr. Slaa ni Zinduna, ni mawingu, ni kufuka tuu kwa moshi, ajiandae kuipokea Ambari, kujikinga na mvua na kuuzima moto unaokuja.

Hii sio mara ya kwanza kwa mtu mwenye hadhi ya Ubalozi kuvuliwa hadhi hiyo, wa kwanza ni balozi wetu wa kwanza jijini London nchini Uingereza Balozi Christopher Kasanga Tumbo, alivuliwa Ubalozi na kushitakiwa kwa jinai enzi za Nyerere. Mwingine ni Balozi Antony Pastor Ngaiza alivuliwa Ubalozi na kushitakiwa kwenye ile kesi ya uhaini ya mwaka 1982. Pia Balozi Prof. Costa Rick Mahalu akivuliwa hadhi ya Ubalozi na kushitakiwa kwa uhujumu ununuzi wa jengo la Ubalozi wa Tanzania jijini Rome nchini Italy, alliposhinda kesi na kukutwa hana hatia, alirejeshewa Ubalozi wake.
.
Hivyo hata kwa Dr. Slaa, tusubirie yatokanayo na kufutiwa hadhi hii ya Ubalozi, yakishindwa kuthibitishwa, anarejeshewa Ubalozi wake.

Kwa vile hili ni bandiko elimishi, nitakuelimisha kidongo na kwa kifupi
  1. Hadhi ya Ubalozi ni nini?
  2. Sifa za mtu kuwa na hadhi ya Ubalozi ni zipi?
  3. Kuna cheo cha Ubalozi (career diplomats) na Ubalozi wa kuteuliwa.
  4. Privileges za diplomatic status ni zipi?.
  5. Ijue diplomatic immunity
  6. Je kila Balozi lazima awakilishe nchi ubalozini?
  7. Jee maofisa wote ubalozini ni mabalozi au wana hadhi za Ubalozi?
  8. Wajue Local Staff ubalozini wasio na hadhi za Ubalozi
  9. Ukifanya makosa gani unapoteza hadhi ya Ubalozi?
  10. Jee kila diplomat anayefanya jinai ni lazima avuliwe Ubalozi?.
  11. Ijue diplomatic Bag?
  12. Jee mwenye diplomatic status ni Balozi?.
  13. Jee kila mwenye diplomatic passport ni diplomats?
  14. Maisha baada ya kuvuliwa Ubalozi, psychological depression etc.
  15. Wajue Wafanya Biashara Matajiri wenye diplomatic status na sio mabalozi!
Kufuatia hii topic ni topic ndefu hivyo nakwenda nayo mdogo mdogo, saa hizi nawahi misa ya kwanza, baada ya misa nitaikamilisha
Itaendelea...

Paskali
Mwandishi ni mwana habari aliyefanya kazi ubalozi fulani kwa miaka 4, ila kufutia fani yake ya uandishi wa habari, ametembelea Balozi za Tanzania katika nchi nyingi za Africa, Ulaya. Asia na America.
Asante sana Kwa Elimu nzuri.Huyo Babu aandae mawakili tuu na uzuri umeshaeleza kwamba sio wa kwanza kuvuliwa Ubalozi na umewataja wengine kibao.
 
Ule mkataba wa kihuni wa bandari alioingia Samia kwa kukiuka sheria za nchi, ndio umemfanya Dr. Slaa avuliwe hadhi yake ya ubalozi, hapa usipindishe maneno.

Samia kwa kumvua Dr. Slaa hadhi yake ya ubalozi amethibitisha yafutayo..

- Amevunja Katiba ya JMT 1977 inayotoa ruhusa kwa watanganyika kutoa maoni yao ilimradi wasivunje sheria za nchi, na amefanya hivyo kama alivyovunja sheria nyingine za nchi kwa kuruhusu ule mkataba wa hovyo wa bandari.

- Amejipambanua yeye ni kiongozi mwanamke dikteta asiyetaka kukosolewa.

- Ametuonesha ana kikundi chake cha wajinga wachache anaowapa vyeo kila wakitetea ujinga wake, akidhani anatukomoa, kumbe ndio anazidi kujivua nguo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom