Lijue Bunge la Afrika Mashariki na Jee Uchaguzi wa Wabunge wa CCM EALA Ulikuwa ni Uchaguzi Kweli Au Kiini Macho cha Uchaguzi?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,605
Wanabodi,
Hii ni makala ya Jumapili ya Leo
Screen Shot 2022-10-02 at 7.40.58 PM.png
Screen Shot 2022-10-02 at 7.41.19 PM.png

Kwa Maslahi ya Taifa, inaendelea na makala elimishi za kuijua Jumuiya ya Afrika Mashariki, leo ni makala elimishi kuhusu kulijua Bunge la Afrika Mashariki, EALA na kiini macho cha uchaguzi wa Wabunge wa EALA wa Tanzania uliofanywa na Bunge letu!. Kilichofanyika kwenye uchaguzi wa EALA ndani ya Bunge letu, kunaacha maswali ya kujiuliza, hivi sisi Watanzania, "Do we real know what we need and what we want?!", "if we do, we wouldn't have let this joke of an election just passby!". Bunge letu lilipaswa kuletewa majina angalau mawili mawili kwa kila nafasi, halafu Bunge ndio lichague!. Kilichofanyika ni Bunge lilipelekewa majina ya kuchagua, uchaguzi uliofanyika ni wa mbunge mmoja tuu wa kutoka upinzani na kuthibisha majina 8 ya CCM!. Ili uchaguzi ufanyike, there must be choices to choose from, if there was no choices to choose from, huo haukuwa ni uchaguzi, ulikuwa ni kiini macho cha uchaguzi!.

Declaration of Interest
Kwa vile mimi nilishiriki mchakato wa uchaguzi huu ndani ya chama, nikashindwa kwa vigezo na kukubali kushindwa EALA: Waliopitishwa CCM, ni Kwa Haki!, Tulioachwa ni kwa Haki, Tumezidiwa Vigezo!. Thanks4 for Support, Nimekubali Matokeo Kiroho Safi! Kazi Iendelee! hivyo makala hii sio ya kutema nyongo ya kushindwa EALA bali hii ni makala elimishi kuelimisha umma kuhusu Bunge la Afrika Mashariki na kuwatendea haki Watanzania kwa kuwaonyesha matundu kwenye paa letu, hivyo kujua sisi Watanzania tunakwama wapi!.

leo tunamalizia mfululizo huu kwa SURA YA TISA: LIJUE BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI, JEE UCHAGUZI WA WABUNGE WA EALA ULIOFANYWA NA BUNGE LETU NI ULIKUWA UCHAGUZI KWELI AU NI KIINI MACHO CHA UCHAGUZI?.

Sura hii inajumuisha Ibara ya 48 mpaka Ibara ya 65. Bunge la Afrika Mashariki ni chombo kilichaonzishwa ili kutekeleza majukumu ya kutunga sheria za Jumuiya.

Ibara ya 48 inahusu Muundo wa Bunge.
Bunge lina wajumbe 9 wa kuchaguliwa kutoka kila nchi na wajumbe 9 ambao wataingia kwa nyadhifu zao. Hawa ni mawaziri 7 wa wizara za Nje na Katibu Mkuu wa jumuiya na Mwanasheria Mkuu wa EAC.

Spika atakuwa na madaraka ya kumwalika mtu yeyote ambaye mchango wake utahitajika katika kujadili hoja yoyote iliyoletwa mbele ya Bunge.

Ibara ya 53 inahusu Spika wa Bunge.
Spika atachaguliwa kutokana na wajumbe wa Bunge. Cheo hiki kitashikwa kwa mzunguko kati ya Nchi Wanachama.

Ibara ya 49 inahusu Kazi za Bunge.
Mbali na wajibu wa kutunga sheria, Bunge la jumuiya litakuwa pia chombo cha kuendeleza mahusiano na mbunge ya kitaifa ya Nchi Wanachama kwa mambo yanayohusu jumuiya.

Bunge litakuwa na kazi ya kupitisha bajeti ya jumuiya. Kabla ya kupitisha bajeti, Bunge litaangalia na kutathmini ripoti za shughuli za Jumuiya. Kazi nyingine ya Bunge itakuwa ni kujadili mambo yote yanayohusu jumuiya na kupeleka mapendekezo kwenye Baraza la Mawaziri. Bunge litakuwa pia na kazi ya kupendekeza majina ya watu kwa ajili ya uteuzi wa nafasi za Katibu Mkuu na maofisa wengine wateule wa jumuiya.

Utaratibu wa Kutunga Sheria
Utungwaji wa sheria utaanza kwa kupelekwa muswada Bungeni. Ikiwa muswada utapitishwa na Bunge, Spika ataupeleka kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi ili wautolee kibali.

Wakuu wa Nchi wakiukubali, unakuwa sheria. Wakiukataa utahesabika kuwa umepitwa na wakati.

Kupitishwa kwa muswada wa sheria na Wakuu wa Nchi unataka makubaliano ya Wakuu wote wa Nchi. Iwapo Mkuu mmoja wa Nchi atakataa, bado muswada huo hauwezi kupita.

Kanuni za Bunge
Bunge lina uwezo wa kutengeneza kanuni zake. Sheria na kanuni hizi zaweza kuhusiana na uwezo, haki, kinga ya wabunge na utaratibu wa uendeshaji wa shughuli zake.

Miswada ya kupelekwa Bungeni inaweza kupendekezwa na mjumbe yeyote. Lakini miswada hii iwe inahusiana na shughuli za Jumuiya na sheria zilizoainishwa katika Mkataba wa Jumuiya, kufuati Tanzania kupeleka majanga EALA, Tangu kuundwa kwa EALA, hakuna mbunge yoyote wa Tanzania, amewahi kupeleka muswada wowote!, Wabunge wa Kenya na Uganda pekee ndio wanaotamba mule!, Tanzania ipo ipo tuu kama hatupo!, au ni tupo tuu kama watazamaji zaidi kuliko washiriki!.

Uchaguzi wa Wabunge
Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki watachaguliwa na Bunge la Taifa la kila Nchi Mwanachama. Kwa hiyo, kila anayetaka kugombea itabidi akapigiwe kura na Bunge la nchi yake. Kwa Tanzania sio kila anayetaka, bali kila aliyepitishwa na chama cha siasa!.

Kila nchi itachagua wabunge tisa, ambao watakuwa siyo wabunge katika bunge la nchi husika. Uteuzi wa wabunge hao utaangalia uwiano wa uwakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa vilivyoweza kuingia katika bunge la nchi husika. Uteuzi utaangalia pia jinsia na uwakilishi mwingine muhimu katika kila Bunge la nchi, husika.

Sifa za kuchaguliwa kuwa Mbunge katika Bunge la Jumuiya:
Awe ni raia wa Nchi Mwanachama
Awe na sifa ya kuchaguliwa kuwa mbunge katika nchi yake kulingana na sheria na taratibu za nchi hiyo. Wabunge wa EALA sio wabunge wa vyama, wala Bunge la EALA sio Bunge la kupiga siasa. Nchi majirani zetu, hutangaza nafasi hizi, raia wake huziomba sio kupitia vyama, ili kupata watu wenye uwezo.

Kwa sisi Tanzania, nafasi hizi hugombewa kupitia vyama, mimi kama mwandishi wa habari, nimekuwa nikihudhuria vikao vya Bunge hili, ukiangalia jinsi wabunge wa nchi za wenzetu wanavyochangia mada na mijadala, ukilinganisha ni michango ya wabunge wa Tanzania, kusema ukweli, ukiondoa wabunge wawili watatu waliokuwa active mule, kiukweli kabisa katika EALA iliyopita, Tanzania tulipeleka majanga!.

Kufuatia Tanzania kupeleka majanga EALA iliyopita, fursa ya EALA ilipojitokeza tena, kwanza mimi nami kama Mtanzania mwingine yeyote, pia nilitupa karata yangu, lakini pia nikatoa ushauri wa jinsi ya kupata watu mahiri. Nilishauri
  1. Kwa waliokuwa wawakilishi wetu kwenye Bunge hilo ambao wanataka kuwania tena nafasi hizo ili kuendelea kwa awamu yao ya pili, waulizwe katika uwakilishi wao, ndani ya Bunge hilo kwa miaka 5 iliyopita, wamechangia nini na wamelisaidia nini taifa?. Hili ndio Swali la Mhe. Msukuma kwa mmoja wa wagombea.
  2. Wagombea wa set agenda za Tanzania kama nchi anazotaka kwenda kuzipigania kwenye EALA na kupewa dakika 5 za kujieleza kwa lugha ya Kiingereza safi kilicho nyooka!. Moja ya sababu za baadhi ya wawakilishi wetu kuwa mabubu kwenye mijadala ya kuchangia hoja za Bunge la EALA, ni mtiririko wa Lugha, yaani kuongea Kiingereza safi fluently.
Kufuatia Watanzania 'kuwakataa wapinzani' kwenye sanduku la kura, kupitia uchaguzi mkuu 'huru' na wa 'haki' kufuatia Tanzania kuendesha chaguzi zetu kwa mutatis mutandis, ni Mbunge mmoja tuu huku Bara toka upinzani ndio amechaguliwa, tena kuchaguliwa kwake ni kwa bahati tuu ya Mtende, kufuatia wananchi wa jimbo lake kumuadhibu mbunge wao, kwa kitendo chake cha kushabikia uvunjifu wa katiba katika ukomo wa uongozi, ile ya "Atake Asitake", hivyo wananchi wakaamua kumpiga chini. Hivyo Bunge hili ni Bunge la chama kimoja predominantly, hivyo katika nafasi 9 za EALA, CCM ikapata nafasi 8 na upinzani nafasi 1.

Kiini Macho cha Uchaguzi Wa Wabunge wa EALA Bunge la Tanzania.
Sifa kuu ya kuchaguliwa EALA ni uraia wa nchi husika na (e) has proven experience or interest in consolidating and furthering the aims and the objectives of the Community.
Uchaguzi wa Wabunge
Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki watachaguliwa na Bunge la Taifa la kila Nchi Mwanachama. Kwa hiyo, kila anayetaka kugombea itabidi akapigiwe kura na Bunge la nchi yake.

Haki ya kila Mtanzania Kupiga Kura Ipo, ila Haki ya Kupigiwa Kura, Imeporwa!.
Kwa mujibu wa Ibara ya 5 ya Katiba ya JMT, kila Mtanzania aliyetimiza umri wa miaka 18, anaruhusiwa kupiga kura na kuchagua viongozi wake. Haki hii ya kila Mtanzania kuruhusiwa kupiga kura kuchagua viongozi wake, ilipaswa kwenda sambamba na kila Mtanzania kuwa na haki ya kupigiwa kura.
Hili nimelizungumza kwa kirefu hapa Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
Wanabodi,

Shurti la Mgombea Uongozi wa Umma, Kudhaminiwa na Chama cha Siasa ni Sheria Mbovu, ni...
Kinyume cha Katiba,
Kinyume cha Universal Declaration of Human Rights
Kinyume cha The United Nations Human Rights Committee,
Kinyume cha African Chatter of People and Political Rights
Inaminya Haki na Kulitia Hasara Taifa, Ibadilishwe!.

Kwa Nini Sheria Yetu ya Uchaguzi ni Sheria Mbovu, Bad Law.
Kifungu 21 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinatoa haki ya kila Mtanzania mwenye sifa, kuwa huru kushiriki katika siasa na uongozi kuanzia serikali za mtaa hadi serikali kuu, bila ubaguzi wowote.

Sheria hiyo inasema hivi na hapa ninanukuu

Uhuru wa kushiriki shughuli za umma
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

Lakini kukatokea kikundi fulani cha watu, kwa maslahi yao, na kwa vile serikali ni yao, wakaipindua katiba kwa kuinyofoa haki hiyo ya kila mtu kushiriki siasa, iliyotolewa na katiba, na kupachika shurti la kudhaminiwa na chama, hivyo kujenga ubaguzi katika kushiriki shughuli za uongozi umma kwa watu kulazimishwa kwanza kujiunga na vyama vya siasa, ndipo upate haki ya kugombee nafasi yoyote ya uongozi wa umma, huku sio kuwatendea haki Watanzania wengine wote, wasiotaka kujiunga na vyama vyovyote vya siasa, kutokana na kuviona karibu vyama vyote ni vyama vya hovyo hovyo, lakini wana uwezo wa uongozi. Hii ni haki muhimu iliyotolewa na katiba, kitendo cha kuingiza shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa ni kinyume cha katiba. Hivyo sheria hii ibadilishwe ili kukidhi kile ambacho katiba ilidhamiria ilipoitoa haki hii, hivyo baada ya mabadiliko hayo ya mlango wa nyuma, kipengele hicho sasa kinasomeka hivi

Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ya ib.4
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

Ule uhuru uliotolewa na Katiba wa kila mtu kuwa huru kushiriki shughuli za uongozi, kupitia ibara ya 21, umekuja kunyofolewa na ibara ya 39 na 67 (b)(c) kwa kuweka sherti, ili mtu kuweza kugombea nafasi yoyote ya uongozi wa umma, ni lazima awe ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa hivyo lazima adhaminiwe na chama cha siasa!, Haki zinatolewa na ibara moja halafu zinaporwa na ibara nyingine ya katiba hiyo hiyo!.

Mchungaji Mtikila (Mungu amuweke mahala pema peponi), mwaka 1993, alifungua kesi No. 5 ya 1993, alifanya kuhudi kubwa kukipinga kifungu hiki na Mahakama Kuu kupitia kwa Jaji Lugakingira, (Mungu amuweke mahala pema peponi), ikatamka wazi na bayana kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT ya mwaka 1977, hivyo kifutwe, na kutoa haki kwa kila Mtanzania ana haki ya kushiriki kugombea Uongozi

Baada tuu ya Mtikila kushinda kesi serikali ikafanya mambo mawili makubwa ya ajabu!, kwanza ilikata rufaa!. Hivi kwa uamuzi kama huu, serikali ilikata rufaa kwa maslahi ya nani?. Pili serikali ilipeleka bungeni kwa hati ya dharura, sheria No. 34 ya mwaka 1994, kufanya marekebisho ya 8 ya Katiba ya JMT na kukichomeka kipengele hicho ndani ya katiba, hivyo kuibatilisha ile hukumu ya Jaji Lugakingira!. Hapa ndipo ujinga unapoanzia katika siasa zetu kwa serikali kufanya kazi kwa maslahi ya kisiasa ya watu fulani, hivyo kupoteza haki ya wengi kwa ajili ya kuwanufaisha wachache.

Kuhusu haki ya kila Mtanzania kugombea nafasi yoyote, ibara ya 21 ya Katiba ya Tanzania ilisema hivi na hapa nina nukuu
“Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au wa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria”.

Lakini baada ya kufanywa marekebisho, ibara hiyo ilisomeka hivi, na hapa ninanukuu
“ Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 39, ya 47 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchaguwa na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi”

Hiki kilichofanyika, mimi nakiita ni kitendo cha kihuni!, Watanzania tulifanyiwa uhuni na serikali yetu, kwa kuinajisi katiba yetu!, kitu kimeelezwa ni kinyume cha katiba, kinatoa haki zilizotolewa na katiba, halafu serikali hiyo inakuja kuihalalisha haramu hiyo kwa kuiingiza rasmi kwenye katiba!, huku ni kuinajisi katiba yetu!.

Mchungaji Mtikila, licha ya kuwa ni mwanasiasa, Mwenyekiti wa chama cha siasa cha DP, (Democratic Party), lakini alikuwa ni mtu wa Mungu kiukweli kabisa, kwa sababu hakukubali kabila yetu inajisiwe!, hivyo akafungua kesi nyingine No. 10 ya mwaka 2009 kupinga marekebisho hayo ya 8 ya katiba na kuyaita ni ubatili!.

Katika kesi hiyo, Mchungaji Mtikila aliomba mambo mawili makuu

(a) Mahakama itamke ibara 39 na 67 za katiba zilizorekebishwa na marekebisho ya 8 kwa sharia No. 34 ya mwaka 1994, ni batili na kinyume cha katiba.

(b) Kutamka wazi kuwa Kila Mtanzania ana haki ya kugombea kwa mujibu wa ibara ya 21 ya Katiba, bila kulazimishwa kudhaminiwa na chama cha siasa, hivyo mtu anaweza kugombea kama mgombea binafsi.

Mahakama Kuu chini ya majaji watatu, (majaji watatu kisheria inaitwa Half Bench), Manento, Masati na Mihayo, wakayakubali mambo yote ya Mchungaji Mtikila na kumpa ushindi tena kwa kutamka marekebisho hayo ya katiba ni batili!. Lakini serikali yetu ilivyo ya ajabu, ikakata tena rufaa, na safari hii Mahakama Kuu ikakaa Full Bench ya majaji 7, chini ya Jaji Mkuu Mwenyewe, Agustino Ramadhani, akisaidiwa na Jaji Munuo, Jaji Msoffe, Jaji Kimaro, Jaji Mbarouk, Jaji Luanda, na Jaji Mjasir, ambapo tarehe 17 mwezi June, mwaka 2010 ikatoa hukumu ya ajabu kabisa kuwa kutokea Tanzania!. Tena Mahakama haikuwa peke yake, bali iliwaita mabinga wabobezi wa sheria na katiba kuisaidia, hawa ni wanaitwa marafiki wa mahakama, kwa kiingereza ni friends of the Court, kisheria wanaitwa Amicus Curiae, hivyo ma Amicus Curiae hawa, Mr. Othman Masoud, Prof. Palamagamba Kabudi, na Prof.Jwan Mwaikusa(Mungu Aiweke Roho yake Mahala Pema Peponi)

Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Rufaa uliamua kitu cha ajabu sana na hapa naomba ninanukuu
“So as to let the will of the people prevail as to whether or not such [independent] candidates are suitable. We are definite that the Courts are not the custodian of the will of the people. That is the property of elected Members of Parliament”.

Hii kiukweli ni kauli ya ajabu sana kutolewa na mahakama yetu kwenye jambo zito na muhimu kama hili!. Kitendo cha Mahakama kujivua jukumu la kuwa the custodian of the will of the people!, ni kitendo cha ajabu sana na kushangaza sana!. Hakuna will of the people kubwa kuliko katiba!, kama katiba imetoa haki Fulani, halafu Bunge likatunga sheria ya ajabu kabisa kuifuta haki hiyo, halafu mahakama ikatamka haiwezi kuliingilia Bunge!, where is the doctrine of separation of powers, checks and balance?.

Kwa ajili ya kulinda heshima ya Mahakama Kuu, naomba niweke ilichokisema bila kukitafsiri.

“In our case, we say that the issue of independent candidates has to be settled by Parliament which has the jurisdiction to amend the Constitution and not the Courts which, as we have found, do not have that jurisdiction. The decision on whether or not to introduce independent candidates depends on the social needs of each State based on its historical reality. Thus the issue of independent candidates is political and not legal However, we give a word of advice to both the Attorney General and our Parliament: The United Nations Human Rights Committee, in paragraph 21 of its General Comment No. 25, of July 12, 1996, said as follows on Article 25 of the International Covenant on Civil and Political Rights, very similarly worded as Art 23 of the American Convention and our Art 21: The right of persons to stand for election should not be limited unreasonably by requiring candidates to be members of
parties or of specific parties. Tanzania is known for our good record on human rights and particularly our militancy for the right to self determination and hence our involvement in the liberation struggle. We should seriously ponder that comment from a Committee of the United Nations, that is, the whole world.
DATED at DAR ES SALAAM this 17th day of June, 2010”

Mahakama Kuu ya Rufaa ikaamua kuwa Mahakama haina mamlaka ya kuliingilia Bunge, katika vipengele vya katiba, kumaanisha kwa vile marekebisho hayo ya 8 yamefanywa na Bunge, hivyo ni Bunge ndio lirekebishe kipengele hicho!, kiukweli kabisa, kwa maoni yangu, uamuzi huu sio utii wa mhimili wa Mahakama kwa mhimili Bunge, bali huu ni ukondoo wa hali ya juu kwa Mhimili wa Mahakama kwa serikali kwa manufaa ya watu wachache!.

Uchaguzi wa Mwaka 2015 ukalithibitisha hili, kumbe baadhi ya majaji wetu ni makada!, Jaji Mkuu Mstaafu aliyeongoza jopo hilo, alichukua fomu kugombea urais!, for what my God?!. Baadhi ya wale ma amicus curiae naamini tunawajua na tunawaona na ukada wao!. Unategemea nini kama sheria za nchi hii zitafinyangwa finyangwa kwa manufaa ya wachache?!. This must stop!.
Paskali
pascomayalla@gmail.com
Rejea.
Rev. Mtikila ashida kesi ya kuruhusu mgombea binafsi mahakama ya ...
Mtikila: Shujaa wa Demokrasia, Mwanamapinduzi halisi na Shujaa ...
Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini? | Page 9 | JamiiForums ...

Hukumu ya mgombea binafsi hii hapa (AG vs Mtikila)

Kipengele hiki cha wagombea uongozi kudhaminiwa na chama cha siasa ndio kimeligharimu taifa hili kukosa viongozi wazuri kwa mizengwe tuu!. Kati ya wagombea 186 wa EALA, kulikuwa na watu fulani 4 ambao mimi nawafahamu, wana good track records, they would have made the best of the best EALA MPs!, lakini kwasababu ya ubatili huu wa kudhaminiwa na chama cha siasa, kati ya wanne hao, the good ones, ni mmoja tuu ndio alipitishwa na CCM na akaenda kuchinjiwa kwenye vikao vya CCM!.

Kiukweli kabisa, dhulma hii inalikosesha taifa letu viongozi wazuri!, hili nimeishaliandikia sana tuu Je, jicho la Rais Samia litauangazia Ubatili huu ndani ya Katiba yetu unaopora Haki ya Msingi, uliochomekewa kibatili ili kuuhalalisha?

Bunge letu limeweka uwiano wa wabunge 8 kutoka CCM na Mbunge 1 wa upinzani, CCM kikateua majina 8 kwenda kupigiwa kura bungeni!, yaani nafasi ni 8, CCM ikateua majina 8 kupigiwa kura na wabunge!, hebu tuambiane ukweli, Bunge lilikuwa linachagua au ni kiini macho tuu cha kuthibitisha chagua lo CCM?. Kwa maoni yangu, kiukweli kabisa, CCM imelikosea sana Bunge letu, na kuwakosea Watanzania kwa kulipatia Bunge letu wabunge 8 wa CCM, kwa ajili ya Bunge kuwathibitisha tuu!, something which is not right at all!.

Mkataba wa Afrika Mashariki umesema Mabunge yatachagua, toka uchaguzi wa kwanza wa EALA, vyama vilipeleka majina angalau mawili mawili kwa kila nafasi, halafu Bunge ndio likachagua, this time around, CCM ndio imechagua majina 8 na kulipa Bunge sio kuchagua, bali kuthibitisha tuu, chaguo la CCM!. Kwa tafsiri yangu, maana ya kuchagua, there must be some choices to choose from!, kama nafasi n inane, halafu unawapelekea majina 8!, huko ni kuchagua au kuthibitisha tuu?. Hivi tukikiita kilichofanyika Bungeni kwa wabunge wa EALA, ni Bunge letu tukufu kufanywa rubber stamp ya chaguo la Chama, jee sasa tunarejea kwenye Party Supremacy au….?!

Kwa maoni yangu, uchaguzi wa wabunge wa EALA uliofanywa na Bunge letu, Bunge limefanya uchaguzi wa kumchagua mbunge mmoja tuu wa upinzania ambapo ndio pekee kwenye choices, na kuwathibitisha wabunge 8 wa chaguo la CCM!.

Kufanya kosa sii kosa!, kosa ni kurudia kosa!, kama mwanzo tulipeleka majanga EALA, halafu tukarudia makosa yale yale!, unategemea nini?. Tena hapa naomba kutoa pongezi kwa Mbunge wa Geita, Dr. Joseph Kasheku Musukuma, swali lake, ndilo limeliokoa Bunge letu, angalau kuliondoa kokoro moja tuliopeleka EALA!.

Japo mimi ni mwana CCM, lakini pia ni mzalendo kwa taifa langu, kunapotokea mgongano wa kimaslahi kati ya maslahi ya CCM na Maslahi ya Taifa, mimi nitatanguliza mbele maslahi ya Taifa kwanza ndipo nije kwenye maslahi ya chama.

Tanzania ni nchi yetu sote, ni mali ya Watanzani wote wa vyama vyote, kunapokuja kwenye issues serious za kitaifa kama kuchangua wawakilishi wa nchi, tulipaswa tuweke pembeni siasa za vyama na kutanguliza mbele maslahi mapana ya Taifa.

Mungu Ibariki Tanzania.

Wasalaam
Paskali
 
Hata hili Bunge lina uhalali?

2020 tulikuwa na uchaguzi au uchafuzi?

Kama Bunge lenyewe si halali, hao wawakilishi wanaowachagua kwenda Bunge la Africa Mashariki wana uhalali gani?

CCM hii unayoiunga mkono, ndio CCM hiyo hiyo isiyotaka Tume Huru ya Uchaguzi Kama ambavyo haitaki tuwe na wagombea binafsi. Hivyo, ukipenda boga, penda na ua lake.
 
Pascal hivi ule uchaguzi wa ndani kupitia kura za maoni 2020 ulioshiriki jimbo la kawe wagombea mlikuwa 183 kama nakumbuka vzr..hivi chama kikongwe kama ccm kinakosa mfumo mzuri wa kuchuja wagombea kabla ya kupigiwa kura na bado ukaamini kinazo sifa za kuwa fair??? Wapi..na wakati gani??badala ya kulaumu kilichofanyika kwenye uchaguzi EALA..jilaumu wewe kwanza kuweka imani kwa watu wasiostahili ccm kwamba watakuwa fair this time wakati jana hawakuwa fair!
 
Wanabodi,
Ijue Jumuiya ya Afrika Mashariki:
Lijue Bunge la Afrika Mashariki na Jee Uchaguzi wa Wabunge wa CCM EALA Ulikuwa ni Uchaguzi Kweli Au Kiini Macho cha Uchaguzi?
View attachment 2375100View attachment 2375101
Kwa Maslahi ya Taifa, inaendelea na makala elimishi za kuijua Jumuiya ya Afrika Mashariki, leo ni makala elimishi kuhusu kulijua Bunge la Afrika Mashariki, EALA na kiini macho cha uchaguzi wa Wabunge wa EALA Kwa Tanzania!, Do We Real Knows What We Want?, if we do, we wouldn't let it go!. Bunge letu lilipaswa kuletewa majina Bunge ndio lichague!. Kilichofanyika ni Bunge lilipelekewa majina ya kuichagua mbunge mmoja wa kutoka upinzani na kuthibisha majina 8 ya CCM kwasababu, there was no choices to choose from.

Declaration of Interest
Mimi hushiriki mchakato wa uchaguzi ndani ya chama na nikashindwa kwa vigezo na nikubali kushindwa hivyo makala hii sio ya kutema nyongo ya kushindwa bali kuelimisha umma na kuwatendea haki Watanzania.

leo tunamalizia mfululizo huu kwa SURA YA TISA: LIJUE BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI, JEE UCHAGUZI WA WABUNGE WA EALA ULIOFANYWA NA BUNGE LETU NI ULIKUWA UCHAGUZI KWELI AU NI KIINI MACHO?.

Sura hii inajumuisha Ibara ya 48 mpaka Ibara ya 65. Bunge la Afrika Mashariki ni chombo kilichaonzishwa ili kutekeleza majukumu ya kutunga sheria za Jumuiya.

Ibara ya 48 inahusu Muundo wa Bunge. Bunge lina wajumbe 9 wa kuchaguliwa kutoka kila nchi na wajumbe 9 ambao wataingia kwa nyadhifu zao. Hawa ni mawaziri 7 wa wizara za Nje na Katibu Mkuu wa jumuiya.

Spika atakuwa na madaraka ya kumwalika mtu yeyote ambaye mchango wake utahitajika katika kujadili hoja yoyote iliyoletwa mbele ya Bunge.

Ibara ya 53 inahusu Spika wa Bunge.

Spika atachaguliwa kutokana na wajumbe wa Bunge. Cheo hiki kitashikwa kwa mzunguko kati ya Nchi Wanachama.

Ibara ya 49 inahusu Kazi za Bunge.

Mbali na wajibu wa kutunga sheria, Bunge la jumuiya litakuwa pia chombo cha kuendeleza mahusiano na mbunge ya kitaifa ya Nchi Wanachama kwa mambo yanayohusu jumuiya.

Bunge litakuwa na kazi ya kupitisha bajeti ya jumuiya. Kabla ya kupitisha bajeti, Bunge litaangalia na kutathmini ripoti za shughuli za Jumuiya. Kazi nyingine ya Bunge itakuwa ni kujadili mambo yote yanayohusu jumuiya na kupeleka mapendekezo kwenye Baraza la Mawaziri. Bunge litakuwa pia na kazi ya kupendekeza majina ya watu kwa ajili ya uteuzi wa nafasi za Katibu Mkuu na maofisa wengine wateule wa jumuiya.

Utaratibu wa Kutunga Sheria

Utungwaji wa sheria utaanza kwa kupelekwa muswada Bungeni. Ikiwa muswada utapitishwa na Bunge, Spika ataupeleka kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi ili wautolee kibali.

Wakuu wa Nchi wakiukubali, unakuwa sheria. Wakiukataa utahesabika kuwa umepitwa na wakati.

Kupitishwa kwa muswada wa sheria na Wakuu wa Nchi unataka makubaliano ya Wakuu wote wa Nchi. Iwapo Mkuu mmoja wa Nchi atakataa, bado muswada huo hauwezi kupita.

Kanuni za Bunge

Bunge lina uwezo wa kutengeneza kanuni zake. Sheria na kanuni hizi zaweza kuhusiana na uwezo, haki, kinga ya wabunge na utaratibu wa uendeshaji wa shughuli zake.

Miswada ya kupelekwa Bungeni inaweza kupendekezwa na mjumbe yeyote. Lakini miswada hii iwe inahusiana na shughuli za Jumuiya na sheria zilizoainishwa katika Mkataba wa Jumuiya, kufuati Tanzania kupeleka majanga EALA, Tangu kuundwa kwa EALA, hakuna mbunge yoyote wa Tanzania, amewahi kupeleka muswada wowote!, Wabunge wa Kenya na Uganda pekee ndio wanaotamba mule!, Tanzania kama hatupo, au ni watazamaji tuu!.

Uchaguzi wa Wabunge

Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki watachaguliwa na Bunge la Taifa la kila Nchi Mwanachama. Kwa hiyo, kila anayetaka kugombea itabidi akapigiwe kura na Bunge la nchi yake. Kwa Tanzania sio kila anayetaka, bali kila aliyepitishwa na chama cha siasa!.

Kila nchi itachagua wabunge tisa, ambao watakuwa siyo wabunge katika bunge la nchi husika. Uteuzi wa wabunge hao utaangalia uwiano wa uwakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa vilivyoweza kuingia katika bunge la nchi husika. Uteuzi utaangalia pia jinsia na uwakilishi mwingine muhimu katika kila Bunge la nchi, husika.

Sifa za kuchaguliwa kuwa Mbunge katika Bunge la Jumuiya:

Awe ni raia wa Nchi Mwanachama
Awe na sifa ya kuchaguliwa kuwa mbunge katika nchi yake kulingana na sheria na taratibu za nchi hiyo. Wabunge wa EALA sio wabunge wa vyama, wala Bunge la EALA sio Bunge la kupiga siasa. Nchi majirani zetu, hutangaza nafasi hizi, raia wake huziomba sio kupitia vyama, ili kupata watu wenye uwezo.

Kwa sisi Tanzania, nafasi hizi hugombewa kupitia vyama, mimi kama mwandishi wa habari, nimekuwa nikihudhuria vikao vya Bunge hili, ukiangalia jinsi wabunge wa nchi za wenzetu wanavyochangia mada na mijadala, ukilinganisha ni michango ya wabunge wa Tanzania, kusema ukweli, ukiondoa wabunge wawili watatu waliokuwa active mule, kiukweli kabisa katika EALA iliyopita, Tanzania tulipeleka majanga!.

Kufuatia Tanzania kupeleka majanga EALA iliyopita, fursa ya EALA ilipojitokeza tena, kwanza mimi nami kama Mtanzania mwingine yeyote, pia nilitupa karata yangu, lakini pia nikatoa nikatoa ushauri wa jinsi ya kupata watu mahiri. Nilishauri
  1. Kwa waliokuwa wawakilishi wetu kwenye Bunge hilo ambao wanataka kuwania tena nafasi hizo ili kuendelea kwa awamu yao ya pili, waulizwe katika uwakilishi wao, ndani ya Bunge hilo kwa miaka 5 iliyopita, wamechangia nini na wamelisaidia nini taifa?. Hili ndio Swali la Mhe. Msukuma kwa mmoja wa wagombea.
  2. Wagombea wa set ajenda za Tanzania kama nchi anazotaka kwenda kuzipigania kwenye EALA na kupewa dakika 5 za kujieleza kwa lugha ya Kiingereza safi kilicho nyooka!. Moja ya sababu za baadhi ya wawakilishi wetu kuwa mabubu kwenye mijadala ya kuchangia hoja za Bunge la EALA, ni mtiriko wa Lugha, yaani kuongea Kiingereza safi fluently.
Kufuatia Watanzania kuwakataa wapinzani kwenye sanduku la kura, kupitia uchaguzi huru na wa haki, ni Mmbunge mmoja tuu huku Bara toka upinzani ndio amechaguliwa, tena kuchaguliwa kwake ni kwa bahati ya Mtende, kufuatia wananchi wa jimbo lake kumuadhibu mbunge wao, kwa kitendo chake cha kushabikia uvunjifu wa katiba katika ukomo wa uongozi, hivyo wananchi wakaamua kumpiga chini. Hivyo Bunge hili ni Bunge la chama kimoja predominantly, hivyo katika nafasi 9 za EALA, CCM ikapata nafasi 8 na upinzani nafasi 1.

Kiini Macho cha Uchaguzi Wa Wabunge wa EALA Bunge la Tanzania.

Ibara ya Mkataba wa Afrika Mashariki, unasema

Uchaguzi wa Wabunge

Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki watachaguliwa na Bunge la Taifa la kila Nchi Mwanachama. Kwa hiyo, kila anayetaka kugombea itabidi akapigiwe kura na Bunge la nchi yake.

Kwa mujibu wa Ibara ya 5 ya Katiba ya JMT, kila Mtanzania aliyetimiza umri wa miaka 18, anaruhusiwa kupiga kura na kuchagua viongozi wake. Haki hii ya kila Mtanzania kuruhusiwa kupiga kura kuchagua viongozi wake, ilipaswa kwenda sambamba na kila Mtanzania kuwa na haki ya kupigiwa kura.

Ibara ya 21 ya Katiba ya JMT, ikatoa uhuru wa kila Mtanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 21, anayohaki kushiriki kwenye uongozi kuanzia serikali za mitaa, hadi serikali kuu, bila kuweka masharti yoyote.

Serikali yetu ikatunga sheria ya uchaguzi, kwenye sheria ya uchaguzi, kukawekwa kipengele cha shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa ndipo ugombee. Kipengele hicho kinakwenda kinyume cha Ibara ya 21 ya katiba ya JMT, kinachotoa uhuru kwa kila Mtanzania kushiriki kugombea uchaguzi.

Mchungaji Mtikila (RIP), Mungu amuweke roho yake mahali pema peponi, akafungua kesi mahakama Kuu kupiga kipengele hicho, akashinda!. Jaji Mwalusanya (RIP), Mungu amuweke roho yake mahala pema peponi, alisema…

Serikali baada ya kushindwa, ikafanya mambo mawili kwa pamoja, kwanza ilikata rufaa dhidi ya hukumu ya Jaji Mwalusanya, pili ilifanya jambo moja kubwa la ajabu ambalo ni dhulma kubwa kwa Watanzania, ikapeleka Bungeni, muswada wa marekebisho ya katiba, na kuuchomekea ule ubatili ndani ya katiba yetu!. Kwa maoni yangu, usafi wa katiba ni usafi wa tenga la samaki, samaki mmoja akioza, wote wameoza!. Katiba safi iliyochomekewa ubatili tena ubatili huo umechomekwa kibatili, unaibadilisha katiba yote kuwa batili!. Kuchomekea kwa ubatili kipengele batili ni kuinajisi Katiba yetu!.

Sasa ile sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, sasa ikawa imechomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!. Hii ni dhulma kubwa sana kwa Watanzania, na karma itaendelea kula vichwa vya viongozi wetu, lakini akina sisi tunaijua karma and how it operates, tuna wajibu wa kuwasaidia viongozi waliopo kuepuka muendelezo wa karma hii kwa kutuondolea hii dhulma kubwa kwa Watanzania. Hivyo tumeisha mshauri Rais Samia, hili aliangazie!.

Mchungaji Mtikila, hakukubali Katiba inajisiwe, hivyo akatinga tena mahakamani kuyapiga hayo marekebisho batili ya katiba yetu, yaliyochomekea vifungu batili ndani ya katiba yetu, na mahakama kuu ikaka kama bench (majaji watatu) ikampa ushindi, Mtikila, ikayatamka mabadiliko hayo ya katiba ni mabadiliko batili, sheria ya shurti la kudhaminiwa na chama cha siasa ni shurti batili, na kuitaka serikali kuuondoa ubatili huo na kuruhusu wagombea binafsi!.

Serikali ikakata rufaa, mahakama kuu ikakaa as half bench, (majaji 5) Mtikila akashinda tena, serikali ikapigwa chini serikali, ikashindwa, ikabwagwa!. Ndipo serikali ikakata rufaa juu ya rufaa, na mahakama kuu sasa ikakaa kama full bench (majaji 7) wakiongozwa na CJ Mwenyewe. Tena ikawaita mabingwa wabobezi washeria watatu, kuisaidia mahakama kwa kuwa ni marafiki wa mahakama, wanaitwa kwa lugha ya Kilatini “Amicus Kuriae” ambao ni Prof. Palamagamba Kaubudi, na Prof. Jwan Mwaikusa (RIP) na Hamid (Sasa VP-1 wa Zanzibar). Mahakama ya Rufani, ikatoa uamuzi wa ajabu na kushangaza haijawahi kutokea!. Haikuzungumzia tena ule ubatili unaokwenda kinyume cha katiba ya JMT, wala haikuzungumzia ubatili uliotumika kukichomekea kifungu hicho batili ndani ya Katiba yetu, Mahakama ikasema haina uwezo wa kuliingilia Bunge katika utungaji wa vipengele vya katiba. Hivyo kulitaka Bunge ndio liviondoe vipengele hivyo batili!.

Katiba ya nchi ndio kila kitu!, Ndio baba, na ndio sheria mama!, sheria yoyote inayokwenda kinyume cha katiba, ni sheria batili. Mamlaka pekee yenye jukumu la kutafasiri sheria ni Mahakama Kuu, Serikali, Bunge na Mahakama vyote viko chini ya katiba, Bunge limetunga sheria batili!, Mahakama ikatamka sheria hiyo ni batili!, serikali ikakata rufaa, ikashindwa!, serikali ikauchukua ubatili huo na kuuchomekea ndani ya katiba yetu, na kuchomekea kwenyewe ni kwa ubatili!, Mahakama ikatamka tena sheria hiyo ni batili, na imechomekewa ndani ya katiba kwa ubatili!.

Kitendo cha kuchomekea kitu kwa ubatili ni kubaka!, Serikali imetunga sheria batili, na kulipa bunge liipitishe kwa kuibaka katiba yetu!. Mahakama Kuu imesema huo ni ubakaji, halafu mahakama ya Rufani haizungumzii kabisa ubatili huu wala ubakaji uliofanywa kwenye katiba yetu, bali inazungumzia uwezo wa mahakama kutengua kipengele cha katiba, kilichoingizwa na Bunge, ni kuliingilia Bunge, hivyo ikalitaka Bunge ndilo liondoe kipengele hicho!,

Binti yako ( haki ya kugombea) amebakwa, kaka mtu (Mahakama Kuu) akathibitisha huo ubakaji na kuamuru binti arejeshwe nyumbani haraka, Baba Mtu mwenye uamuzi wa mwisho (Mahakama Kuu ya Rufani) uamuzi wake ni wa mwisho final and conclusive, akaamua, eti hawezi kuingilia mapenzi ya wawili hao, na hazungumzii kabisa ubakaji!, baba mtu anasema amempa uhuru mbakaji ndie aache kumbaka binti yake!, mambo ya kubakana ni mapenzi, baba hawezi kuingilia mapenzi ya watoto!, what sort of parent is this?!.

Kipengele hiki cha wagombea uongozi kudhaminiwa na chama cha siasa ndio kimeligharimu taifa hili kukosa viongozi wazuri kwa mizengwe tuu!. Kati ya wagombea 186 wa EALA, kulikuwa na watu fulani 4 ambao ni best of the best!, kwenye wane hao, ni mmoja tuu ndio alipitishwa na CCM na akaenda kuchinjiwa kwenye vikao vya CCM!.

Bunge letu limeweka uwiano wa wabunge 8 kutoka CCM na Mbunge 1 wa upinzani, CCM kikateua majina 8 kwenda kupigiwa kura bungeni!, yaani nafasi ni 8, CCM ikateua majina 8 kupigiwa kura na wabunge!, hebu tuambiane ukweli, Bunge lilikuwa linachagua au ni kiini macho tuu cha kuthibitisha chagua lo CCM?. Kwa maoni yangu, kiukweli kabisa, CCM imelikosea sana Bunge letu, na kuwakosea Watanzania kwa kulipatia Bunge letu wabunge 8 wa CCM, kwa ajili ya Bunge kuwathibitisha tuu!, something which is not right at all!.

Mkataba wa Afrika Mashariki umesema Mabunge yatachagua, toka uchaguzi wa kwanza wa EALA, vyama vilipeleka majina angalau mawili mawili kwa kila nafasi, halafu Bunge ndio likachagua, this time around, CCM ndio imechagua majina 8 na kulipa Bunge sio kuchagua, bali kuthibitisha tuu, chaguo la CCM!. Kwa tafsiri yangu, maana ya kuchagua, there must be some choices to choose from!, kama nafasi n inane, halafu unawapelekea majina 8!, huko ni kuchagua au kuthibitisha tuu?. Hivi tukikiita kilichofanyika Bungeni kwa wabunge wa EALA, ni Bunge letu tukufu kufanywa rubber stamp ya chaguo la Chama, jee sasa tunarejea kwenye Party Supremacy au….?!

Kwa maoni yangu, uchaguzi wa wabunge wa EALA uliofanywa na Bunge letu, Bunge limefanya uchaguzi wa kumchagua mbunge mmoja tuu wa upinzania ambapo ndio pekee kwenye choices, na kuwathibitisha wabunge 8 wa chaguo la CCM!.

Kufanya kosa sii kosa!, kosa ni kurudia kosa!, kama mwanzo tulipeleka majanga EALA, halafu tukarudia makosa yale yale!, unategemea nini?. Tena hapa naomba kutoa pongezi kwa Mbunge wa Geita, Dr. Joseph Kasheku Musukuma, swali lake, ndilo limeliokoa Bunge letu, angalau kuliondoa kokoro moja tuliopeleka EALA!.

Japo mimi ni mwana CCM, lakini pia ni mzalendo kwa taifa langu, kunapotokea mgongano wa kimaslahi kati ya maslahi ya CCM na Maslahi ya Taifa, mimi nitatanguliza mbele maslahi ya

Tanzania ni nchi yetu sote, ni mali ya Watanzani wote wa vyama vyote, kunapokuja kwenye issues serious za kitaifa kama kuchangua wawakilishi wa nchi, tulipaswa tuweke pembeni siasa za vyama na kutanguliza mbele maslahi mapana ya Taifa.

Mungu Ibariki Tanzania.

Wasalaam
Paskali
Kwani Hilo umelijua Leo? Wapinzani walipokuwa wanalalamiki hukuona Hilo. Au kwa kuwa limekugusa wewe. Eti mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu ni mchungu!
 
Kile siyo chama ni genge la matapeli watanashati walio vaa suti.
"Kama Mwasisi wake Mwalimu Nyerere aliikataa CCM na kusema CCM si Mama yake,nyinyi wanyonge ni nani mpaka mlazimishe kuwamo hu mo ndani ya icho chama?? Mwachieni Mama na wanawe wakina Nape, January, Mwigulu na Ridhiwan et al ambao wanaona kile chama na hii nchi ni urithi kutoka kwa Baba na Babu zao"
 
Mayalla wewe mwenyewe Kuna uzi hapa ulipongea kabisa kuwa wabunge waliopatikana kutoka ccm wote walipatikana kihalali.
Mkuu Mmawia , kwenye upatikanaji wa wabunge wa EALA, wabunge hao wanachaguliwa na mabunge ya nchi husika. The bottom line ni uchaguzi unafanywa na Bunge. Kwa Tanzania mchakato wake unapitia two stages
1. Uchaguzi wa wagombea kwenye ngazi ya vyama. Mchakato huu kwa CCM ndio umekwenda vizuri, waliochaguliwa wamechaguliwa kwa haki, na tulioshindwa, tumeshindwa kwa haki kwa kuzidiwa sifa na waliochaguliwa EALA: Waliopitishwa CCM, ni Kwa Haki!, Tulioachwa ni kwa Haki, Tumezidiwa Vigezo!. Thanks4 for Support, Nimekubali Matokeo Kiroho Safi! Kazi Iendelee!

Baada ya mchakato huu, CCM ilipaswa ichague angalau majina mawili kwa kila nafasi ili kulipa Bunge fursa ya kuchagua.
Kilichofanyika hapa ni majina ya walioteuliwa na CCM yakapelekwa kwenye party caucas ya CCM, wakaibuka na majina 8 kwa zile nafasi 8 za CCM ndio yakapelekwa Bungeni.
2. Bunge kupokea majina kutoka kwenye vyama vya siasa, kisha wabunge ndio wafanye uchaguzi kuwachagua wabunge wa EALA. Ni vyama vya upinzani pekee ndio vimepeleka bungeni majina na bunge kuchagua, lakini kwa zile nafasi 8 za EALA za CCM, hakukuwa na uchaguzi because there was no choice to choose from, bali kuthibitisha wale 8 wa CCM.
Hili ni Bunge la 4 la EALA, mabunge yote matatu yaliyotangulia, Bunge la JMT, lilichagua wabunge wa EALA by choices from vyama vya siasa ikiwemo CCM ambayo ilichagua majina mawili mawili. This time CCM ndio imechagua wawakilishi 8 na kulipa Bunge kuwathibitisha tuu na sio kuwachagua!.
P
 
kitu kidogo sana unashindwa kukieleza ni kwamba chama chako bado kinashindwa kutembea kidemokras hili ndio tatizo lenu kuu. tarajio lilikuwa kura ipigwe ndani ya bunge lkn uhuni waliouzoea Chama chako cha lumumba kuzoea kucheza rafu .... kinacheza rafu mpaka ndani yake hili ndio tatizo SUGU. MMETEULIWA MAJINA NA CHAMA KIMEPITISHA NA BUNGE LENU LIKAITIKIA TU NDIOOOO.
 
Wanabodi,
Hii ni makala ya Jumapili ya Leo
View attachment 2375100View attachment 2375101
Kwa Maslahi ya Taifa, inaendelea na makala elimishi za kuijua Jumuiya ya Afrika Mashariki, leo ni makala elimishi kuhusu kulijua Bunge la Afrika Mashariki, EALA na kiini macho cha uchaguzi wa Wabunge wa EALA Kwa Tanzania!, Do We Real Knows What We Want?, if we do, we wouldn't let it go!. Bunge letu lilipaswa kuletewa majina Bunge ndio lichague!. Kilichofanyika ni Bunge lilipelekewa majina ya kuichagua mbunge mmoja wa kutoka upinzani na kuthibisha majina 8 ya CCM kwasababu, there was no choices to choose from.

Declaration of Interest
Mimi hushiriki mchakato wa uchaguzi ndani ya chama na nikashindwa kwa vigezo na nikubali kushindwa EALA: Waliopitishwa CCM, ni Kwa Haki!, Tulioachwa ni kwa Haki, Tumezidiwa Vigezo!. Thanks4 for Support, Nimekubali Matokeo Kiroho Safi! Kazi Iendelee!
hivyo makala hii sio ya kutema nyongo ya kushindwa EALA bali kuelimisha umma na kuwatendea haki Watanzania.

leo tunamalizia mfululizo huu kwa SURA YA TISA: LIJUE BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI, JEE UCHAGUZI WA WABUNGE WA EALA ULIOFANYWA NA BUNGE LETU NI ULIKUWA UCHAGUZI KWELI AU NI KIINI MACHO?.

Sura hii inajumuisha Ibara ya 48 mpaka Ibara ya 65. Bunge la Afrika Mashariki ni chombo kilichaonzishwa ili kutekeleza majukumu ya kutunga sheria za Jumuiya.

Ibara ya 48 inahusu Muundo wa Bunge.
Bunge lina wajumbe 9 wa kuchaguliwa kutoka kila nchi na wajumbe 9 ambao wataingia kwa nyadhifu zao. Hawa ni mawaziri 7 wa wizara za Nje na Katibu Mkuu wa jumuiya na Mwanasheria Mkuu wa EAC.

Spika atakuwa na madaraka ya kumwalika mtu yeyote ambaye mchango wake utahitajika katika kujadili hoja yoyote iliyoletwa mbele ya Bunge.

Ibara ya 53 inahusu Spika wa Bunge.
Spika atachaguliwa kutokana na wajumbe wa Bunge. Cheo hiki kitashikwa kwa mzunguko kati ya Nchi Wanachama.

Ibara ya 49 inahusu Kazi za Bunge.
Mbali na wajibu wa kutunga sheria, Bunge la jumuiya litakuwa pia chombo cha kuendeleza mahusiano na mbunge ya kitaifa ya Nchi Wanachama kwa mambo yanayohusu jumuiya.

Bunge litakuwa na kazi ya kupitisha bajeti ya jumuiya. Kabla ya kupitisha bajeti, Bunge litaangalia na kutathmini ripoti za shughuli za Jumuiya. Kazi nyingine ya Bunge itakuwa ni kujadili mambo yote yanayohusu jumuiya na kupeleka mapendekezo kwenye Baraza la Mawaziri. Bunge litakuwa pia na kazi ya kupendekeza majina ya watu kwa ajili ya uteuzi wa nafasi za Katibu Mkuu na maofisa wengine wateule wa jumuiya.

Utaratibu wa Kutunga Sheria
Utungwaji wa sheria utaanza kwa kupelekwa muswada Bungeni. Ikiwa muswada utapitishwa na Bunge, Spika ataupeleka kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi ili wautolee kibali.

Wakuu wa Nchi wakiukubali, unakuwa sheria. Wakiukataa utahesabika kuwa umepitwa na wakati.

Kupitishwa kwa muswada wa sheria na Wakuu wa Nchi unataka makubaliano ya Wakuu wote wa Nchi. Iwapo Mkuu mmoja wa Nchi atakataa, bado muswada huo hauwezi kupita.

Kanuni za Bunge
Bunge lina uwezo wa kutengeneza kanuni zake. Sheria na kanuni hizi zaweza kuhusiana na uwezo, haki, kinga ya wabunge na utaratibu wa uendeshaji wa shughuli zake.

Miswada ya kupelekwa Bungeni inaweza kupendekezwa na mjumbe yeyote. Lakini miswada hii iwe inahusiana na shughuli za Jumuiya na sheria zilizoainishwa katika Mkataba wa Jumuiya, kufuati Tanzania kupeleka majanga EALA, Tangu kuundwa kwa EALA, hakuna mbunge yoyote wa Tanzania, amewahi kupeleka muswada wowote!, Wabunge wa Kenya na Uganda pekee ndio wanaotamba mule!, Tanzania kama hatupo, au ni watazamaji tuu!.

Uchaguzi wa Wabunge
Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki watachaguliwa na Bunge la Taifa la kila Nchi Mwanachama. Kwa hiyo, kila anayetaka kugombea itabidi akapigiwe kura na Bunge la nchi yake. Kwa Tanzania sio kila anayetaka, bali kila aliyepitishwa na chama cha siasa!.

Kila nchi itachagua wabunge tisa, ambao watakuwa siyo wabunge katika bunge la nchi husika. Uteuzi wa wabunge hao utaangalia uwiano wa uwakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa vilivyoweza kuingia katika bunge la nchi husika. Uteuzi utaangalia pia jinsia na uwakilishi mwingine muhimu katika kila Bunge la nchi, husika.

Sifa za kuchaguliwa kuwa Mbunge katika Bunge la Jumuiya:
Awe ni raia wa Nchi Mwanachama
Awe na sifa ya kuchaguliwa kuwa mbunge katika nchi yake kulingana na sheria na taratibu za nchi hiyo. Wabunge wa EALA sio wabunge wa vyama, wala Bunge la EALA sio Bunge la kupiga siasa. Nchi majirani zetu, hutangaza nafasi hizi, raia wake huziomba sio kupitia vyama, ili kupata watu wenye uwezo.

Kwa sisi Tanzania, nafasi hizi hugombewa kupitia vyama, mimi kama mwandishi wa habari, nimekuwa nikihudhuria vikao vya Bunge hili, ukiangalia jinsi wabunge wa nchi za wenzetu wanavyochangia mada na mijadala, ukilinganisha ni michango ya wabunge wa Tanzania, kusema ukweli, ukiondoa wabunge wawili watatu waliokuwa active mule, kiukweli kabisa katika EALA iliyopita, Tanzania tulipeleka majanga!.

Kufuatia Tanzania kupeleka majanga EALA iliyopita, fursa ya EALA ilipojitokeza tena, kwanza mimi nami kama Mtanzania mwingine yeyote, pia nilitupa karata yangu, lakini pia nikatoa nikatoa ushauri wa jinsi ya kupata watu mahiri. Nilishauri
  1. Kwa waliokuwa wawakilishi wetu kwenye Bunge hilo ambao wanataka kuwania tena nafasi hizo ili kuendelea kwa awamu yao ya pili, waulizwe katika uwakilishi wao, ndani ya Bunge hilo kwa miaka 5 iliyopita, wamechangia nini na wamelisaidia nini taifa?. Hili ndio Swali la Mhe. Msukuma kwa mmoja wa wagombea.
  2. Wagombea wa set agenda za Tanzania kama nchi anazotaka kwenda kuzipigania kwenye EALA na kupewa dakika 5 za kujieleza kwa lugha ya Kiingereza safi kilicho nyooka!. Moja ya sababu za baadhi ya wawakilishi wetu kuwa mabubu kwenye mijadala ya kuchangia hoja za Bunge la EALA, ni mtiririko wa Lugha, yaani kuongea Kiingereza safi fluently.
Kufuatia Watanzania kuwakataa wapinzani kwenye sanduku la kura, kupitia uchaguzi huru na wa haki, ni Mbunge mmoja tuu huku Bara toka upinzani ndio amechaguliwa, tena kuchaguliwa kwake ni kwa bahati tuu ya Mtende, kufuatia wananchi wa jimbo lake kumuadhibu mbunge wao, kwa kitendo chake cha kushabikia uvunjifu wa katiba katika ukomo wa uongozi, ile ya "Atake Asitake", hivyo wananchi wakaamua kumpiga chini. Hivyo Bunge hili ni Bunge la chama kimoja predominantly, hivyo katika nafasi 9 za EALA, CCM ikapata nafasi 8 na upinzani nafasi 1.

Kiini Macho cha Uchaguzi Wa Wabunge wa EALA Bunge la Tanzania.
Sifa kuu ya kuchaguliwa EALA ni uraia wa nchi husika na (e) has proven experience or interest in consolidating and furthering the aims and the objectives of the Community.
Uchaguzi wa Wabunge
Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki watachaguliwa na Bunge la Taifa la kila Nchi Mwanachama. Kwa hiyo, kila anayetaka kugombea itabidi akapigiwe kura na Bunge la nchi yake.

Haki ya kila Mtanzania Kupiga Kura Ipo, ila Haki ya Kupigiwa Kura, Imeporwa!.
Kwa mujibu wa Ibara ya 5 ya Katiba ya JMT, kila Mtanzania aliyetimiza umri wa miaka 18, anaruhusiwa kupiga kura na kuchagua viongozi wake. Haki hii ya kila Mtanzania kuruhusiwa kupiga kura kuchagua viongozi wake, ilipaswa kwenda sambamba na kila Mtanzania kuwa na haki ya kupigiwa kura.
Hili nimelizungumza kwa kirefu hapa Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.

Kipengele hiki cha wagombea uongozi kudhaminiwa na chama cha siasa ndio kimeligharimu taifa hili kukosa viongozi wazuri kwa mizengwe tuu!. Kati ya wagombea 186 wa EALA, kulikuwa na watu fulani 4 ambao mimi nawafahamu, wana good track record, they would have made best of the best EALA MPs!, lakini kwasababu ya ubatili huu wa kudhaminiwa na chama cha siasa, kati ya wanne hao, the good ones, ni mmoja tuu ndio alipitishwa na CCM na akaenda kuchinjiwa kwenye vikao vya CCM!.

Kiukweli kabisa, dhulma hii inalikosesha taifa letu viongozi wazuri!, hili nimeishaliandikia sana tuu Je, jicho la Rais Samia litauangazia Ubatili huu ndani ya Katiba yetu unaopora Haki ya Msingi, uliochomekewa kibatili ili kuuhalalisha?

Bunge letu limeweka uwiano wa wabunge 8 kutoka CCM na Mbunge 1 wa upinzani, CCM kikateua majina 8 kwenda kupigiwa kura bungeni!, yaani nafasi ni 8, CCM ikateua majina 8 kupigiwa kura na wabunge!, hebu tuambiane ukweli, Bunge lilikuwa linachagua au ni kiini macho tuu cha kuthibitisha chagua lo CCM?. Kwa maoni yangu, kiukweli kabisa, CCM imelikosea sana Bunge letu, na kuwakosea Watanzania kwa kulipatia Bunge letu wabunge 8 wa CCM, kwa ajili ya Bunge kuwathibitisha tuu!, something which is not right at all!.

Mkataba wa Afrika Mashariki umesema Mabunge yatachagua, toka uchaguzi wa kwanza wa EALA, vyama vilipeleka majina angalau mawili mawili kwa kila nafasi, halafu Bunge ndio likachagua, this time around, CCM ndio imechagua majina 8 na kulipa Bunge sio kuchagua, bali kuthibitisha tuu, chaguo la CCM!. Kwa tafsiri yangu, maana ya kuchagua, there must be some choices to choose from!, kama nafasi n inane, halafu unawapelekea majina 8!, huko ni kuchagua au kuthibitisha tuu?. Hivi tukikiita kilichofanyika Bungeni kwa wabunge wa EALA, ni Bunge letu tukufu kufanywa rubber stamp ya chaguo la Chama, jee sasa tunarejea kwenye Party Supremacy au….?!

Kwa maoni yangu, uchaguzi wa wabunge wa EALA uliofanywa na Bunge letu, Bunge limefanya uchaguzi wa kumchagua mbunge mmoja tuu wa upinzania ambapo ndio pekee kwenye choices, na kuwathibitisha wabunge 8 wa chaguo la CCM!.

Kufanya kosa sii kosa!, kosa ni kurudia kosa!, kama mwanzo tulipeleka majanga EALA, halafu tukarudia makosa yale yale!, unategemea nini?. Tena hapa naomba kutoa pongezi kwa Mbunge wa Geita, Dr. Joseph Kasheku Musukuma, swali lake, ndilo limeliokoa Bunge letu, angalau kuliondoa kokoro moja tuliopeleka EALA!.

Japo mimi ni mwana CCM, lakini pia ni mzalendo kwa taifa langu, kunapotokea mgongano wa kimaslahi kati ya maslahi ya CCM na Maslahi ya Taifa, mimi nitatanguliza mbele maslahi ya

Tanzania ni nchi yetu sote, ni mali ya Watanzani wote wa vyama vyote, kunapokuja kwenye issues serious za kitaifa kama kuchangua wawakilishi wa nchi, tulipaswa tuweke pembeni siasa za vyama na kutanguliza mbele maslahi mapana ya Taifa.

Mungu Ibariki Tanzania.

Wasalaam
Paskali
PASKALI, nje ya mada!!embu siku moja tuletee wasifu wa wakili Murtaza Lakha(na picha yake ili tumjue)wengine mwaka ule wa 1976 hatukuepo!
 
kitu kidogo sana unashindwa kukieleza ni kwamba chama chako bado kinashindwa kutembea kidemokras hili ndio tatizo lenu kuu. tarajio lilikuwa kura ipigwe ndani ya bunge lkn uhuni waliouzoea Chama chako cha lumumba kuzoea kucheza rafu .... kinacheza rafu mpaka ndani yake hili ndio tatizo SUGU. MMETEULIWA MAJINA NA CHAMA KIMEPITISHA NA BUNGE LENU LIKAITIKIA TU NDIOOOO.
Mkuu Mwala, haya usemayo ni kweli, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kuzungumzia dhambi ya ubaguzi, baada ya kuwabagua wapinzani, sasa tumeanza kubaguana sisi kwa sisi, wenyewe kwa wenyewe!, na hata kukulana, sasa tunakulana wenyewe kwa wenyewe!.

Kwenye EALA, CCM imepitisha watu wazuri kisha CCM hiyo hiyo ikawachinjia baharini baadhi yao!, na kutumia kokoro kuyabeba baadhi yale mazagazaga na makorokocho yao!, simply because ...
Ila pia ndio maana watu kama sisi tuko CCM kumsaidia chama kirudi kwenye line.
P
 
Back
Top Bottom