Maaskofu Katoliki walivyolaani mauaji Pemba 2001

Sasa jamani mbona masheikh wanasema maaskofu walikaa kimya mauwaji ya pemba mwaka huo? Ninyi hili gazet lenye tamko la maaskofu juu ya mauwaji hayo mmelipata wap?

Hawakufanya utafiti ikiwa kama taasis. Walipaswa waseme tamko la wakati huo halikuwa kali kama la sasa. Kama walikuwa hawana uhakika walikuwa na uwezo wao kama Taasis ya dini kutafuta hiyo habari hata kwa kwenda kuwauliza maaskofu wenyewe kabla ya kutoa hilo tamko
 
Watakuja tena walete longolongo lingine?? Wepesi wa kusahau!!!
kama unashindwa kuelewa hata maandishi ya kawaida kama haya!!!! nina wasiwasi na uwezo wako kiakili..
au ubongo wako unaelewa kwa kukidhi matakwa yako na sio kwa kuuangalia ukweli??????
Maaskofu hawajakemea zaidi ya kuonyesha kwamba hawana upande wowote katika mgogoro huo hapo juuu.
UDINI!!!! MTAJARIBU KUTUMALIZA LAKNI HAMTAWEZA
 
MSAAAAAADA JAMANI....Is there any 1 out there who can help here...tangu walipotoa viongozi wa dini wale tamuko lao huko Arusha, nimekuwa nikijiuliza swali moja, kwa nini HAWAKUWASHIRIKISHA VIONGOZI WA DINI (SIJUI MADHEHEBU) yote katika kutoa tamuko hilo??? Bila shaka tusingekuwa hapa sasa...lakini kama tunakubaliana kuwa viongozi wa dini ni 'walinzi' maadili, kwani hakuna maadili yanayoikukwa katika siasa, ambapo wanapaswa kuelekeza njia sahihi?? Kwani ukishakuwa kiongozi wa dini, automatically unakuwa umeondolewa haki/uhuru wa kutoa maoni katika siasa?? No freedom of expression, let alone opion??

Je walichozungumzia baadae viongozi wengine wa dini, wakiwakemea wale wa Arusha ile ilikuwa ni siasa, uchumi, utamaduni??? Hivi kama mtu hakutoa tamuko wakati wa mwembechai au pemba, kitu ambacho sidhani kama ni kweli saaana, hana haki ya kutoa maoni yake ikitokea 'ajali' ya namna hiyo siku nyingine, sehemu nyingine, kama Arusha?? Mwisho katika tamuko la udini, udini uko sehemu gani vile????????????? Ntashukuru
 
Hapa mkuu umezidi kuwakandamiza Maaskofu Wakatoliki.

Hakuna walipokemea serikali na ukisoma unaona wametoa lawama kwa vyama vya siasa na ukosefu wa elimu ya uraia
hawaangalii kilichoandikwa wala kukisoma kwa tafakuri! mradi waeona kichwa cha habari basi tayari wamemaliza kusoma yote yalio ndani!!! great thinkers!!! MAPENDEKEZO NDIO KULAANI!!!
 
Wajinga ndio waliwao. Nyinyi bishaneni nani katoa tamko na nana ajatoa tamko huku nyumba Rostam na wane wanahamisha visafleti vya pesa
 
I wish tamko kama hili lingetolewa kwa tatizo la Arusha. Tatizo la Arusha limetengenezwa kwa makusudi maalum na hata tamko la Maaskofu lilifuata umaalum huo huo. Lau kama kusingekuwa na umaalum huo, kusingekuwa na haja kwa Maaskofu kukariri hoja ya CDM ya kutomtambua Meya na kutaka uchaguzi urudiwe kana kwamba na wao ni wapiga kura. Haya mambo ndo yanayotoa nafasi ya hisia za udini.

Maaskofu katika matukio yote mawili waliona suluhu ya kweli ilikuwa kwa kukijua chanzo. Pemba inaonekana, kwa fikra za maaskofu, ilikuwa ni jazba na ukosefu wa elimu ya Urai, Arusha chanzo kilikuwa ni uchaguzi wa Meya. Huwezi kumaliza tatizo bila kuondoa chanzo cha matatizo.
 
Hata hivyo kilichowekwa hapa siyo tamko la Maaskofu ni habari iliyokuwa reported na mwandishi wa gazeti la Majira..mdau ingekuwa busara kama ungeliweka tamko lao ili watu walijadili, ila hii habari kutoka gazetini inatosha kwa kuanzia..
 
Ingekuwa vizuri ukawataja hao watu ili tuwasute hapahapa na u copy link ya jukwaa waliokuwa wakisema maneno hayo. ila kikubwa zaidi mara nyingi kuna maneno ukiyazungumza utajuta mfano Cardinal Pengo aliposema hakutegemea kama Tanzania bara kungeweza kutokea mauwaji. Hii ina maana wenzetu wa upande wa visiwani wataichukulia kuwa wengi na especial Kanisa ninategemea mauwaji ya kisiasa yanaweza kutokea visiwani tu.

My Take.

Pengo kama kiongozi wa dini na wa wanajamii ya watanzania asitake tuamini kuwa yeye hakuwahi kujua katiba ina matatizo, na kama alijua je alishawahi kuinyooshea Serikali kidole? Kwa mauwaji yaliyotokea kiongozi gani wa dini iwe ya KKKT, Anglican, Bakwata, Baraza kuu, TAG na Full Gospel Bible Followship ambae hawajibiki na mauaji yaliyotokea Arusha?

Kwa mtazamo wangu hakuna anaweza kujitoa kwenye ile kadhia, kuanzia viongozi wa kisiasa na wakidini.

Mkuu Mohammed Shossi,

Ni ukweli usiopingika kuwa Maaskofu wetu mara nyingi huwa ni wapole zaidi wanapozungumzia matatizo ya Tanzania-Zanzibar kwa kuwa hawana waumini wengi kule/influence yao ni ndogo....

Hivyo basi huwa wanajaribu kubalance matamko yao ili wasilete machafuko zaidi (either kuikasirisha serikali ya kule au kuwakasirisha wananchi wengi wa kule ambao 98.5% ni Waislam) badala ya kuleta maelewano.

Nadhani inajulikana kwanini Maoni/maonyo yao juu ya machafuko yanayotokea Tanzania-Bara huwa ni makali zaidi.....

Lakini kwa ujumla Maaskofu huwa hawafurahishwi na mambo ya vurugu iwe ni Tanzania-Zanzibar au Tanzania-Bara.
 
Bandiko hili limekuja baada ya maaskofu hawa wa Arusha kushutumiwa kwamba hawakutoa tamko lolote juu ya mauaji ya 2001, hawakushutumiwa kwa kutoa tamko laini... Hebu turudi mwaka 2001 tuone ni nani na nani waliotoa matamko ya kulaani mauaji yale kabla ya kuwahukumu viongozi hawa!

Tatizo ni kwamba wanaowashutumu maaskofu wanataka kutuaminisha kwamba wamelaani mauaji ya Arusha kwa maslahi ya kidini kitu ambacho si kweli hata kidogo.

Ohh yeah! Na kichwa cha habari kinasema "Maaskofu Katoliki walivyolaani mauaji Pemba 2001" huku hatuoni wapi hao maaskofu wamelaani hayo mauaji. Kutoa tamko la kusikitishwa siyo sawa na kutoa tamko la kulaani. Acheni kuzungushazungusha maneno mkijua kuwa hayo yaliyoandikwa kwenye tamko hilo hayafanani hata kwa asilimia 10 na tamko la mauaji ya Arusha. Halafu hizo sababu za "nyakati tofauti" utafikiri wale waliouawa 2001 waliuawa na mapanga halafu hawa wa mwaka huu wameuawa na silaha za baiolojia.

By the way, mnaweza pia kutuletea "tamko la kulaani" ama tamko la "kusikitikia" mauaji ya Mwembechai? Ama hata tamko la kulaani kupigwa marufuku kwa kitabu cha mauaji ya Mwembechai? Anybody?
 
Mkuu Mohammed Shossi,

Ni ukweli usiopingika kuwa Maaskofu wetu mara nyingi huwa ni wapole zaidi wanapozungumzia matatizo ya Tanzania-Zanzibar kwa kuwa hawana waumini wengi kule/influence yao ni ndogo....

Hivyo basi huwa wanajaribu kubalance matamko yao ili wasilete machafuko zaidi (either kuikasirisha serikali ya kule au kuwakasirisha wananchi wengi wa kule ambao 98.5% ni Waislam) badala ya kuleta maelewano.

Nadhani inajulikana kwanini Maoni/maonyo yao juu ya machafuko yanayotokea Tanzania-Bara huwa ni makali zaidi.....

Lakini kwa ujumla Maaskofu huwa hawafurahishwi na mambo ya vurugu iwe ni Tanzania-Zanzibar au Tanzania-Bara.

Mauaji ya Mwembechai yalitokea Tanzania bara... Hapo je?
 
Maaskofu katika matukio yote mawili waliona suluhu ya kweli ilikuwa kwa kukijua chanzo. Pemba inaonekana, kwa fikra za maaskofu, ilikuwa ni jazba na ukosefu wa elimu ya Urai, Arusha chanzo kilikuwa ni uchaguzi wa Meya. Huwezi kumaliza tatizo bila kuondoa chanzo cha matatizo.

Tafsiri yake ni kuwa yale mauaji ya Pemba walioandamana walikuwa wapumbavu. Hawa wa Arusha waliandamana kudai haki ya kukataa matokeo ya uchaguzi wa Arusha na wao pia wakatoka hadharani kupinga hayo matokeo na kutoa tamko la kutokumkubali huyo meya. Halafu watu wanataka kusema hayo matamko ya kusikitika na matamko ya kulaani ni sawa.

Hatudanganyiki lakini kudanganganya kama kawa... Mabingwa wa kulia kuchakachuliwa nidyo waalimu wa kuchakachua?
 
....Tamko lilitolewa na kubebesha lawamba pande zote; hata hivyo halikuwa tamko kali vya kutosha dhidi ya serikali kama matamko ya hivi karibuni yalivyokuwa.

Na tofauti yake ni kuwa hilo tamko la mauaji ya Pemba lilikuwa tamko la kusikitika na hili la Arusha ni tamko la kulaani.
 
Hapa mkuu umezidi kuwakandamiza Maaskofu Wakatoliki.

Hakuna walipokemea serikali na ukisoma unaona wametoa lawama kwa vyama vya siasa na ukosefu wa elimu ya uraia

Hii ilikuwa ni "wavaa vibarahashia na dola" hivyo lugha ilikuwa kuwasomesha namna ya kutii dola na dola upande wake utumie elimu kuwafahamisha "vibarahashia" kuitiidola. Nilitegemea kuona pahala fulani ikisemwa neno " kulaani" kama tunavyozooelea sasa
 
always ni watu wa kulalamika tu wanaonewa sijui hata kwanini bora miruko ulitunza na reference sasa wairuke na hiyo

Hivyo akili yako na macho yako yanakufanya usijue kuwa hili tamko halikulenga kuwatetea maaskofu bali kuwaonyesha undumila kuwiliwao?
 
Maaskofu katika matukio yote mawili waliona suluhu ya kweli ilikuwa kwa kukijua chanzo. Pemba inaonekana, kwa fikra za maaskofu, ilikuwa ni jazba na ukosefu wa elimu ya Urai, Arusha chanzo kilikuwa ni uchaguzi wa Meya. Huwezi kumaliza tatizo bila kuondoa chanzo cha matatizo.

He! Tafsiri nyengine bwana! Hivyo Pemba mauwaji yalitokea baada ya jambo gani lililo tofauti na lile la Arusha? Pemba wakidai kunyimwa ushindi na Arusha kulidaiwa kunyimwa ushindi. Hata hivyo roho za watu zina grade ya kuuliwa bila makosa? Roho za Arusha zina daraja kubwa hivyo lazima kukemewa na kususia Serikali ama za Pemba kuwaambia dola wawaelimishe watu kulitosha?
 
MSAAAAAADA JAMANI....Is there any 1 out there who can help here...tangu walipotoa viongozi wa dini wale tamuko lao huko Arusha, nimekuwa nikijiuliza swali moja, kwa nini HAWAKUWASHIRIKISHA VIONGOZI WA DINI (SIJUI MADHEHEBU) yote katika kutoa tamuko hilo??? Bila shaka tusingekuwa hapa sasa...lakini kama tunakubaliana kuwa viongozi wa dini ni 'walinzi' maadili, kwani hakuna maadili yanayoikukwa katika siasa, ambapo wanapaswa kuelekeza njia sahihi?? Kwani ukishakuwa kiongozi wa dini, automatically unakuwa umeondolewa haki/uhuru wa kutoa maoni katika siasa?? No freedom of expression, let alone opion??

Je walichozungumzia baadae viongozi wengine wa dini, wakiwakemea wale wa Arusha ile ilikuwa ni siasa, uchumi, utamaduni??? Hivi kama mtu hakutoa tamuko wakati wa mwembechai au pemba, kitu ambacho sidhani kama ni kweli saaana, hana haki ya kutoa maoni yake ikitokea 'ajali' ya namna hiyo siku nyingine, sehemu nyingine, kama Arusha?? Mwisho katika tamuko la udini, udini uko sehemu gani vile????????????? Ntashukuru

Pengine hufahamu nafasi ya kiongozi wa dini, tutakusamehe kwa hilo lakini hata wewe au mimi hatuna haki ya kukosowa jambo lilofanya au kutamkwa na mtu mwengine? Na kwa haki hiyo hiyo ndio tunajadili makosa yanayofanywa na viongozi wa dini kwa kuwa na kauli tofauti kwa mambo yanayofanana. Aidha unataka kutueleza pia kuwa wale viongozi wa Kanisa kule Arusha kutotambua uchaguzi wa Meya wao walikuwa wajumbe kwenye uchaguzi huo? Ninachojuwa mimim kila Taasisi ina wahusika wake na hawa ndio wanaweza kukataa au kukubali maamuzi yanayohusu Taasisi hiyo.
 
Back
Top Bottom