Maaskofu Katoliki walivyolaani mauaji Pemba 2001

Ok nimeshakipata ulichojisadikisha kwenye akili yako, sawa ni ngumu kumwelewesha mtu ambaye tayari ameshakiona anachokielewa ni sahihi, Kumbe waislam si watanzania? Aisee udini huu utatubagua mpaka basi!

Kwa tunaomjua Bw. Miruko hatushangai kwani ni kati ya waandishi wanaoipeleka nchi kubaya kwa kuandika habari za kishabiki.

Kwa sababu ya ushabiki, anajaribu kulazimisha tamko la Maaskofu liwe laana wakati ambapo kwa sababu ya nia njema na ya dhati au kwa kumuogopa Ben, wakalazimika kutoa tamko ambalo naamini kuwa lilihaririwa mara nyingi kabla ya kutolewa.
 
Hapa mkuu umezidi kuwakandamiza Maaskofu Wakatoliki.

Hakuna walipokemea serikali na ukisoma unaona wametoa lawama kwa vyama vya siasa na ukosefu wa elimu ya uraia

Hujaisoma vizuri! Mbona iko CRYSTAL CLEAR. "...Maaskofu wametaka vyombo vya dola vielimishwe njia za kisasa za kukabiliana na vurugu na kuwa na utu katika kutekeleza majukumu yao"...Je, ulitaka wasema nini?
 
Mimi sijazungumzia uislam. Ninachozungumzia ni kuwa kwa wakati huo wa mwaka 2001, Tamko liliegemea moja kwa moja upande wa serikali na kuwa jukumu la kuleta amani waliwaachia vyama vya siasa.

Tamko la mwaka huu limeegemea kwenye upande wa vyama/chama cha siasa na kuipinga serikali.

Gaijin, naamini hauko sahihi. Tamko lilikuwa linakemea na kujumuisha "wote waliohusika" na hizo ghasia hii ina maana serikali, vyama vya siasa n.k. Kama unakumbuka kulikuwa na hali ya "visasi" Pemba kuliko wakati wowote ule kabla. Hata hivyo, ninapolisoma tamko hilo nikilinganisha na uzito wa yaliyotokea wakati ule na haya yaliyotokea hivi juzi, tamko hilo halikuwa kali vya kutosha dhidi ya serikali. Lilijaribu kutengeneza moral equivalency kati ya waliouawa na serikali. Sasa hivi, serikali imenyoshewa mkono wazi.

Hata hivyo, inajibu kwa upande hoja kuwa maaskofu walikaa kimya, sasa watu wamekumbushwa kuwa hawakukaa kimya. Sasa kulinganisha tamko hili na tamko la Mashehe hivi karibuni ni wazi mjadala unahamia zaidi kwa mashehe vile vile kuwa wakali.

La pili hata hivyo ni kuwa, wakati ule ulikuwa ni msimamo wa Baraza la Maaskofu lakini hatukumbuki kama kulikuwa na maaskofu mmoja mmoja (wa Kikatoliki na Kiprotestanti) ambao walitoa kauli kali kama zilizotolewa majuzi na kina Laizer na hata Pengo. Ninaamini aidha kuwa wamejifunza na sasa hata likitokea jambo Pemba maaskofu hawatokuwa wapole (docile) kama ilivyo katika tamko hili.

Tamko lilitolewa na kubebesha lawamba pande zote; hata hivyo halikuwa tamko kali vya kutosha dhidi ya serikali kama matamko ya hivi karibuni yalivyokuwa.
 
You are my true great thinker M.M.Mwanakijiji, sina wa kukufananisha nae labda Masoud Kipanya kwa mbali coz the guy has sensi ovu hyuma.
 
Gaijin, naamini hauko sahihi. Tamko lilikuwa linakemea na kujumuisha "wote waliohusika" na hizo ghasia hii ina maana serikali, vyama vya siasa n.k. Kama unakumbuka kulikuwa na hali ya "visasi" Pemba kuliko wakati wowote ule kabla. Hata hivyo, ninapolisoma tamko hilo nikilinganisha na uzito wa yaliyotokea wakati ule na haya yaliyotokea hivi juzi, tamko hilo halikuwa kali vya kutosha dhidi ya serikali. Lilijaribu kutengeneza moral equivalency kati ya waliouawa na serikali. Sasa hivi, serikali imenyoshewa mkono wazi.

Hata hivyo, inajibu kwa upande hoja kuwa maaskofu walikaa kimya, sasa watu wamekumbushwa kuwa hawakukaa kimya. Sasa kulinganisha tamko hili na tamko la Mashehe hivi karibuni ni wazi mjadala unahamia zaidi kwa mashehe vile vile kuwa wakali.

La pili hata hivyo ni kuwa, wakati ule ulikuwa ni msimamo wa Baraza la Maaskofu lakini hatukumbuki kama kulikuwa na maaskofu mmoja mmoja (wa Kikatoliki na Kiprotestanti) ambao walitoa kauli kali kama zilizotolewa majuzi na kina Laizer na hata Pengo. Ninaamini aidha kuwa wamejifunza na sasa hata likitokea jambo Pemba maaskofu hawatokuwa wapole (docile) kama ilivyo katika tamko hili.

Tamko lilitolewa na kubebesha lawamba pande zote; hata hivyo halikuwa tamko kali vya kutosha dhidi ya serikali kama matamko ya hivi karibuni yalivyokuwa.

Ni vizuri umekumbushwa ukweli wa maaskofu kulaani lile tendo ovu, labda hukupenda kuutafuta.
Ni muhimu sana kuangalia historia ya wakati huo kama unavyofanya na iwe kwa uhalisia bila upendeleo. Kudai maelezo ya mmoja mmoja, uipime kwa misingi hiyo pia na wala isiwe kisingizio tu.
Wewe ni mchambuzi makini, tena mwenye heshima sana (high esteem) lakini kwa suala hili la imani mbona unatukwaza? Hoja ya mashekh ukitazama kwa undani haiangalii tatatizo tajwa bali kwa ujumla wa matatizo ambayo ni kama ya kutungwa na kuaminisha watu, mimi naona kama wanaona mauaji ya Arusha ni sawa vile! Je hata kwa muislamu aliye uawa Arusha hawaoni kuwa hilo siyo suala la imani. Ukitazama kwa undani siya mashekh bali ni ya wana sisiem tena wale mafisadi ambao wewe unapigana nao kufa na kupona. Hii ni kwa tamko ambalo Topical ameleta kama thread ambapo wewe umemshuku hivyo unakubali uhalisia wake.
Zaidi naona mijadala ya namna hii na hasa agenda hizi siya kujenga bali ni ya kubomoa mahusiano jamii tuiliyo nayo ambayo.
 
ukweli unabaki kuwa maaskofu wana nguvu na wana maono ya mbali kuliko hata serikali yenye kila kitu! angalia taasisi makini kama mahosptal, vyuo, shule nk ziko chini ya makanisa! Pia masheikh makini wanafanya kazi nzuri katika taasisi zao kwa ustawi wa Taifa ila wapo masheikh na maaskofu wanaokubali kutumiwa na wanasiasa uchwara! Matamko ya mauaji ya pemba na arusha lazima yawe tofauti sana, siku za nyuma watu walipenda kukaa upande wa serikali, lakini kwa sasa maovu ya serikali yamefanya watu kuondoa shilingi upande wa serikali, kwahiyo lazima matamko yatofautiane! Kitu kimoja ambacho najiuliza, kwanini masheikh huwa wa mwisho kila wakati kutoa tamko au miongozo nk? Inaonekana huwa hawana cha kusema, hivyo usubiria wanachosema maaskofu ndiyo wakipinge! Kwa ufupi nafikiri masheikh wanakaa mbali na jamii na mambo mengi huwatokea kwa kushtukizwa au matatizo ya kijamii hayawagusi moja kwa moja! Sio wabunifu mara nyingi tatizo lao ni roho ya kwanini na siyo hoja zenye mashiko! Ni mtazamo wangu kwa sasa.......!
 
hitimisho;

a) Maaskofu walitoa tamko mwaka 2001.

b) Tamko hilo lilikemea kilichotokea.

Hoja ilikuwa maaskofu hakukemea. Safari hii wamekemea. Sasa hoja ya nyongeza ni kwa nini hawakukemea vikali. Sidhani kama hoja ya nyongeza ina mshiko kwa sasa. Cha msingi walikemea na wakshauri. Serikali haikusikiliza ushauri wao kwa hiyo safari hii wameikemea zaidi. Hata kama walikuwa upande wa serikali then basi kwa kitendo hicho kurudiwa wana kila sababu ya kutoitetea serikali zaidi. Tusubiri kama CUF watapigwa tena tuone kama maaskofu wataitea serikali. Lakini CUF na wao wapigwe kwa kuonewa sio wafanye ukaidi ili wapigwe wategemee kutetewa na maaskofu na watu wengine! Waandamane kuhusu Dowans tujiunge nao. Wakipigwa na maaskofu wakikaa kimya ukweli utajulikana!

NAKUBALIANA NA HITIMISHO-Huo ndo ukweli, umebainika. Kuendeleza ubishi ni ulalamishi usio na tija. Tuliaminishwa kuwa maaskofu walikaa kimya, kumbe ukwelu umejulikana kamwe hawakukaa kimya kuona serikali inasababisha maafa kwa roho za watanzania mwaka 2001, bila kujali dini zao (period).
 
Kumbe TAMKO lilitolewa Hata mwaka 2001 ni swala la kumbukumbu tuu mtoa hoja wa mwanzo hakuonyesha hata sehemu ndogo kuwa kuna tamko jepesi lilitolewa ila kaeleza moja kwa moja hakuna tamko lililotolewa, maadamu lilitolewa basi hakuna hoja tena pili huwezi kulazimisha utoaji wa Tamko la 2001 ulingane sawa sawa na mwaka 2011 haiwezekanikabisa. Hata Serikali yenyewe inatofautiana sana wanavyolieleza Tatizo la Arusha sasa na Ilivyokuwa mwaka 2001.
 
hitimisho;

a) Maaskofu walitoa tamko mwaka 2001.

b) Tamko hilo lilikemea kilichotokea.

Hoja ilikuwa maaskofu hakukemea. Safari hii wamekemea. Sasa hoja ya nyongeza ni kwa nini hawakukemea vikali. Sidhani kama hoja ya nyongeza ina mshiko kwa sasa. Cha msingi walikemea na wakshauri. Serikali haikusikiliza ushauri wao kwa hiyo safari hii wameikemea zaidi. Hata kama walikuwa upande wa serikali then basi kwa kitendo hicho kurudiwa wana kila sababu ya kutoitetea serikali zaidi. Tusubiri kama CUF watapigwa tena tuone kama maaskofu wataitea serikali. Lakini CUF na wao wapigwe kwa kuonewa sio wafanye ukaidi ili wapigwe wategemee kutetewa na maaskofu na watu wengine! Waandamane kuhusu Dowans tujiunge nao. Wakipigwa na maaskofu wakikaa kimya ukweli utajulikana!

Wakifanya hii kitu, mama angu mzazi naenda kuchukua fom ya uanachama
 
Ukilinganisha na kichwa cha thread hii, bandiko haliendani na kichwa hicho. Kuna tofauti kati ya neno "Kulaani" na "Kusikitika" au "Kuonyesha masikitiko". Kwa hali ya kawaida mtu yoyote yule husikitika pale tukio baya kama ghasia na vifo vinapotokea na kusikitika huku kutokana na kuguswa na madhara ya tukio kama hilo. Kulaani ni kupinga kwa nguvu zote na katika tukio kama hilo mtu wa kawaida hulaani yule aliyesababisha masahibu hayo iadha kwa kutoa amri ya kudhuru au kudhuru.

Either way, it will be interesting to revisit what was said on Feb the 8th, 2001. Unajua tatizo la imani linaamsha hisia sana kwa baadhi yetu na ni lazima tukubali kwamba kuna baadhi bado wanafeel aggrieved kutokana na kuona kwamba wenzao hawakuwasupport vya kutosha pindi walipowahitaji.

Mkuu umeibua a very interesting point, je siku ikitokea viongozi fulani wa dini fulani wakasema hawamtambui rais na wenzao wa dini nyingine wakawapinga itakuwaje especially in light ya haya matatizo ya Arusha?

Tisa kumi, umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, hata katika kudai haki au kupinga perceived injustice. Hivi hawa viongozi wa dini za Abrahamu walishindwa kuwasiliana, kuketi na kutoa tamko la pamoja kuhusiana na kule Arusha au Zanzibar kabla ya hapo? Siku hizi kuna njia nyingi tu za mawasiliano na isitoshe Arusha mjini ni eneo dogo. Wangeweza kuepusha malumbano yote haya ya sasa hivi kwa kufanya hivi.

Ndiyo maana narejea ujumbe wangu wa awali, viongozi wa dini za Abrahamu warudi kwenye nyumba zao za ibada waziombee amani nafsi zao,zetu na taifa kwa ujumla. Na pia wasisahau kuomba tuepushwe na dhambi ya ubaguzi ambayo inawezekana pasi kukusudia wamezileta.

Kwa maandishi haya, naomba nikuamkie SHIKAMOO
 
Acheni udini huo. mbona muuza sura wenu anateua waislamu tu kila kona na watu hawapigi kelele. Au ndo mnapiga kelele kutuzuga ili tusione kinachofanyika! Kila anayechaguliwa ni walewale tu. Kati ya makatibu tawala 6 walioteuliwa hivi karibuni wa5 ni waislamu, mlishasikia mkristu hata mmoja kapiga kelele? Nafasi za wabunge wa kuteuliwa na rais hadi sasa wameshateuliwa wangapi na ni wa dini gani? Mbona watu wamekaa kimya tu ila nyie ndo mnaweweseka.
 
Katika kipande cha hilo gazeti hakuna sehemu ambapo maaskofu walipoikemea au kukosoa serikali juu ya hayo mauaji.

Lakini jamani mnakumbuka viongozi wa zanzibar walivyokuwa mbogo hata rais mkapa akajivua urais wa eneo lile? hivi maaskfu ndio wangeweza kumkemea rais wa ZNZ na serikali yake? mauwaji ya znz hayakuwa ya kidini wala hakuna mkristo ambaye angepnda kuingilia mauwaji yale zaidi ya kutoa ushauri!!! wakati ule demokrasia ya kuwaruhusu Maaskofu watoe tamka kali ilikuwa haipo!
 
Wakuu,
hapa lumbaneni. itaneni majina, semeni udini.
Ukweli utabaki kuwa 2001, wengi wetu tuliwaona Wazanj, wapemba kuwa ni wakorofi waliostahiki kushughulikiwa.

Tafuteni kauli, matamko, yaliyotolewa na masheikhe, misikiti au mapadri,wachungaji, makanisa.
Kwa ujumla wetu kama watz bara tuliona ni mambo yasiyotuhusu na yasiyotugusa kabisa.
La msingi sasa ni kuwa tunajua, "mwenzako akinyolewa. wewe tia maji".

kwa hiyo haki za raia mwenzetu yeyote ,akiwa mwanachama wa chama cha siasa, au hana chama, wa kikundi fulani au dini fulani au dhehebu fulani inapokanyagwa basi ni lazima tuhakikishe, tunasimama pamoja kulaani uovu huo na kutaka uwajibikaji kwa waliotenda ovu hilo au kuwajibishwa.

kuendeleza malumbano haya, yanatugawa tu badala ya kuungana..au bado hatujasoma, hatujang'amua kuwa tulitenda kosa kuona ya wazenj hayatuhusu? kuwa ni watu wakorofi waliostahiki rungu la dola?
Tusitake kumuosha mtu, kumsafisha mtu...yale ya 2001 yalipita na ni vizuri tuache kubeza maridhiano huko Zanzibar...na sasa tushughulikie haya ya leo yanayotukabili.

tusitoneshe vidonda vya 2001, hivyo vimeanza kupatiwa dawa, tutizame haya tulionayo leo, tuyakabili haya ,bila ya kunyoosheana vidole
 
Sasa jamani mbona masheikh wanasema maaskofu walikaa kimya mauwaji ya pemba mwaka huo? Ninyi hili gazet lenye tamko la maaskofu juu ya mauwaji hayo mmelipata wap?
 
kumekuwa na taarifa mbalimbali kuhusu tamko la maaskofu kuhusu mauaji ya arusha, huku wengine wakisema hakukuwa na taarifa kama hiyo kwa mauaji ya pemba mwaka 2001. Kwenye attachment ipo story ya gazeti la majira februari 25, 2001 (iko kama picha jpg) , likionesha jinsi maaskofu katoliki walivyolaani pamoja na mapendekezo yao, tusome kwa ajili ya kumbukumbu.

nyongeza

nomepata story ya tamko la viongozi wa dini (kwa ujumla) la februari 8, 2001 kuhusu mauaji ya pemba. Source: Majira

maaskofu_zanzibar_mauaji.jpg

asante umetusaidia kuondoa mziziz wa fitna..waosha vinywa sasa mnalakusema?
 
Thanks a lot Mirumo kwa kuleta kumbu kumbu hiyo muhimu, maana kuna watu wanadhani Maaskofu wanakemea Uislamu au ni kwamba hawaitaki serikali iliyoko madarakani.Ukweli ni kwamba maaskofu au ukipenda viongozi wa dini, wamekuwa wakikosoa serikali na kukemea uovu mbali mbali katika jamii yetu tangu enzi na enzi.Na isitoshe uzoefu unaonyesha kwamba Maaskofu huwa wanatoa mapendekezo namna ya kutatua tatizo husika (Si kushambulia kama wafanyavyo baadhi ya watu).Kwa hivyo watu wanaodhani eti ukosoaji ukemeaji au ukosoaji wa maaskofu ni kuingilia siasa au umelenga kiongozi wa dini fulani ni ufinyu wa mawazo na hawana uelewa wowote kuhusiana na suala la GOVERNANCE.Governance inhitaji ushirika wa wadau wote katika kuamua namna bora ya kuendesha nchi kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa.Hao wanaotoa vijitamko dhaifu vya kuwashambulia maaskofu, badala ya kujadili issues za msingi, kama vile kuuawa kwa raia Arusha, na wizi unaotaka kufanywa na wamiliki wa Dowans, inaonyesha aidha wanatumiwa na wanasiasa ili ionekana nchi inavurugwa na matamko ya viongozi wa dini, au ni mbumbumbu ambao hawajui nini wanachokisema na implications zake kwenye jamii yetu.Intelligent people are the ones who discuss issues, and not people.
 
Wakuu,
hapa lumbaneni. itaneni majina, semeni udini.
Ukweli utabaki kuwa 2001, wengi wetu tuliwaona Wazanj, wapemba kuwa ni wakorofi waliostahiki kushughulikiwa.

Tafuteni kauli, matamko, yaliyotolewa na masheikhe, misikiti au mapadri,wachungaji, makanisa.
Kwa ujumla wetu kama watz bara tuliona ni mambo yasiyotuhusu na yasiyotugusa kabisa.
La msingi sasa ni kuwa tunajua, "mwenzako akinyolewa. wewe tia maji".

kwa hiyo haki za raia mwenzetu yeyote ,akiwa mwanachama wa chama cha siasa, au hana chama, wa kikundi fulani au dini fulani au dhehebu fulani inapokanyagwa basi ni lazima tuhakikishe, tunasimama pamoja kulaani uovu huo na kutaka uwajibikaji kwa waliotenda ovu hilo au kuwajibishwa.

kuendeleza malumbano haya, yanatugawa tu badala ya kuungana..au bado hatujasoma, hatujang'amua kuwa tulitenda kosa kuona ya wazenj hayatuhusu? kuwa ni watu wakorofi waliostahiki rungu la dola?
Tusitake kumuosha mtu, kumsafisha mtu...yale ya 2001 yalipita na ni vizuri tuache kubeza maridhiano huko Zanzibar...na sasa tushughulikie haya ya leo yanayotukabili.

tusitoneshe vidonda vya 2001, hivyo vimeanza kupatiwa dawa, tutizame haya tulionayo leo, tuyakabili haya ,bila ya kunyoosheana vidole
Heshima kwenda mbele.
 
Udini...udini....udini! Hii nchi sijui inakwenda wapi.
Btw, napata taabu kidogo (kimantiki) kama kuna uwezekano wa askofu,mchungaji, padre au sheikh asiwe mdini:A S 39:!
 
Back
Top Bottom