Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,610
Wanabodi,
Declaration of Interest
Mimi ni Mkatoliki, tena sio Mkatoliki mlei tuu, ni miongoni mwa Wakatoliki wacheche waliokwenda kuhiji Israel, na waliofika St. Peter's Basilica, Rome, Italy, nikiwa mdogo nimehudunu utumishi kanisani chini ya Muadhama Laurian, Cardinal Rugambwa, na nimemhudumia Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

Nimelisoma tamko hili, News Alert: - Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu in disbelief, hili kweli ni tamko la TEC, au tamko la Fr. Kitima?. Naulizia, huku sio kuchanganya dini na siasa?.

Kama Mama Samia ndiye Mkuu wa nchi, ameikubali DPW, ameileta, Bunge ambalo ndio wawakilishi halali wa wananchi wameikubali, na kuridhia ile IGA ya DPW, CCM ndio chama tawala na chama pekee cha Watanzania, wameikubali DPW, mhimili wa Mahakama umeikubali DPW, kwa kuipiga chini kesi ya kupinga DPW, who the hell is TEC ikatae DPW?!.

Katika uendeshaji wa nchi yetu, kumewahi kuwepo tuhuma za kitu kinachoitwa "Mfumo Kristo", hata uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, uliwahi kutuhumiwa kujaza Wakatoliki!. Mwalimu Nyerere akamtuma msaidizi wake Bi. Wickens amuhesabie idadi ya mawaziri Wakatoliki kwenye cabinet yake, akawakuta wawili, mmoja wao ni Sir George Kahama, wakati huo Sir George ameisha endelea, ana wake 2!.

Japo Tanzania ni secular state, nchi yetu haina dini na serikali haina dini, ila watu wake wana dini, na dini Kuu mbili ni Wakristo na Waislamu. Ukiangalia development index ya maendeleo na personal development ya watu hawa wawili ni tofauti, kuna mmoja ni more influential kuliko mwingine, hivyo akisema kitu kinasikilizwa na kisipo sikilizwa...

Tukubali tukatae, Kanisa Katoliki lina upper hand kwenye siasa za nchi hii!, si wengi wanajua kuwa kila rais wa JMT anapokuwa ni Mkristo ni lazima awe Mkatoliki!, Nyerere alikuwa Mkatoliki, Mkapa Mkatoliki na Magufuli Mkatoliki, na atakaye mfuatia Mama Samia baada muda wake, ni lazima awe Mkatoliki!, je kuna uwezekano Wakatoliki wamedekezwa na sasa wameota pembe na kuthubutu kumgomea Mama kwasababu sio Mkatoliki?.

Zanzibar ilipojiunga na OIC na kwa vile Zanzibar sio nchi, hivyo Tanzania ndio ikahesabika kujiunga na OIC, ni TEC ndio wa kwanza kupiga kelele, Tanzania tukajitoa!, lakini tupo Wakristo Wakatoliki, tuliisupport Zanzibar na kuitaka JMT ijiunge na OIC OIC - Zanzibar kujiunga kivyake vyake

Waislamu walipotaka Mahakama ya Kadhi, na CCM chini ya rais Muislamu, ikawakubalia na kuuingiza hoja ya Mahakama ya Kadhi kwenye Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, ni TEC walipiga kelele, Mahakama ya Kadhi ikakataliwa na ilani ya CCM iliyofuata ya 2015 ambapo ni zamu ya rais Mkristo, hoja ya Mahakama ya Kadhi ikaondolewa kwenye ilani ya CCM!. Tupo baadhi yetu tena ni Wakristo Wakatoliki, tuliwaunga mkono ndugu zetu Waislamu kudai Mahakama ya Kadhi Kuahidiwa Mahakama ya Kadhi, kujiunga na OIC kumeleta mshikamano na serikali? na mpaka tukapendekeza Mwarobaini wa Kweli wa Mahakama ya Kadhi ni Huu, Wakristo, Waislamu, Kuukubali Bila Matatizo!.

Tuambiane ukweli, jiulize, rais angekuwa ni MkatolikinMagufuli ndio ameileta hii DPW, TEC wangetoa waraka huu?.

Kuna mabaya mangapi yamefanywa na marais Wakatoliki lakini TEC wamenyamaza?. Kuna kosa kubwa zaidi ya rais wa JMT kukiuka katiba?. Mbona rais Mkatoliki alikiuka katiba na TEC walikuwepo, mbona sikuona waraka?.

Bwana wetu Yesu Kristo alituasa tumpe Kaisari yaliyo ya Kaisari na tumpe Mungu yaliyo ya Ki Mungu, jee waraka mzito kama huu, haujachanganya ya Ki Mungu na ya Kaizari?.

Pia Bwana wetu Yesu Kristo alituusia tuwe makini sana na manabii wa uongo, niliwahi kuandika hivi humu Angalizo: Kuna Wengi Wanamwabudu Shetani Wakidhani ni Mungu!. Jee Wewe Unajijua?, Jitambue!.

Sipingi uhuru wa Maaskofu Katoliki kutoa kutoa maoni yao binafsi kuhusu jambo lolote, lakini maoni ya kupinga jambo lolote la kisiasa yanayotolewa na TEC, ni sawa na amri kwa Wakatoliki wote kuikataa DPW!, kitu ambacho kitawakwaza Wakotoliki wa CCM, Serikali, Bunge na Mahakama, wanao unga mkono DPW, hivyo baada ya tamko hili, wakiendelea kuunga mkono DPW ni kama kwenda kinyume cha msimamo wa Kanisa Katoliki!.

Sina tatizo kiongozi yoyote wa dini akihubiri amani, mimi mwenyewe ile 2010, JK alipokuwa na hali mbaya, nimezunguka nchi nzima na Askofu Moses Kulola kuokoa jahazi Askofu Kulola: Kuna mtandao wa kisiasa makanisani

Niliwahi kuuliza maswali haya kuhusu viongozi hawa wa dini
Hitimisho
Kufuatia waraka huu kunasibishwa na Sauti ya Mungu mwenyewe, kama ni kweli Vox Populi is Vox Dei yaani
Sauti ya Wengi ni Sauti ya Mungu, na Kanisa Katoliki ni kanisa la Mungu, hii maana yake Maaskofu Katoliki ni watu wa Mungu, hivyo waraka huu ni sauti ya Mungu wa kweli, na kama hawa Maaskofu Katoliki sio manabii wa uongo, ushauri wangu wa bure kwa Mama, Rais Samia, kama hiki hawa Maaskofu Katoliki wamewasilisha ni sauti ya Mungu wa kweli, uzoefu umeonyesha sio vizuri kuwakatalia Maaskofu, na mfano mzuri ni ushauri huu niliompa rafiki yangu Benard Membe, Bernard Membe usibishane na Maaskofu, samehe tu. Yule ni kichaa anastahili msamaha, hakujua atendalo tangu Membe alipoupuuza ushauri huu,... (naomba nisimalizie), ila hakuchukua round!.

Hivyo mimi nikiwa ni mmoja wa wana jf wenye kauli umba "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je, Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba? Shuhudia
Nakushauri tuu Mama, pamoja na mema yote DPW waliokutendea wewe na serikali yetu during Expo Dubai, and after, nakushauri tuu kubaliana na ushauri wa hawa Maaskofu Katoliki Tanzania wa TEC, huu ni ushauri tuu, hili jambo la DPW achana nalo kwa sasa, kisha anzisha upya mchakato wa kumpata a strategic investor wa Bandari yetu kwa kufuata a due process, hakuna strategic investor wa Bandari duniani anaweza kushindana na DPW!, hivyo DPW atakuwa ameingia kwa heshima, and very honourably.

Paskali.
Rejea za Mwandishi kuhusu DPW na Bandari zetu
  1. Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?
  2. Wabunge Wetu, Macho ya Watanzania Wote Leo ni Kwenu!. Maslahi ya Taifa Mbele!. Tuwaogope Kama Ukoma Muflis Hawa!, Kama Huwezi, ni Lazima Usaidiwe Tuu!
  3. Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!
  4. Hakuna Ubaya Wowote kwa Mtu Yoyote, Taasisi Yoyote, Nchi Yoyote Kusaidiwa Pale Inaposhindwa, Muhimu ni Kuwa Makini Tusipigwe. Je DPW Tunapigwa?
  5. Bunge letu ni Bunge la ovyo? Bunge linafanya Uhuni? Wabunge Wetu ni Wahuni? Tumshauri Spika naye aanze kuita Watu kwenye Kamati, au waachwe tu?
  6. DP World: Hizi Kelele, Kulalamika, Shutuma, na Lawama ni za Kweli au ni Ujinga Tu? Rais Samia Anastahili Kulaumiwa au Kupongezwa?
  7. Je, ni Kweli Bunge letu ni Dhaifu na Kibogoyo?
  8. Watanzania ni Watu wa ajabu. Wanapigiaje kelele jambo dogo la Bandari, lakini Mambo Muhimu ya Msingi kama Katiba na Uhuru wao wapo Kimya?
  9. Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?
  10. Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!
  11. Bunge, Serikali na Mahakama, Sio Mungu, Sio Malaika, Zinaweza Kukosea!. Zinapokosea, Zina Wajibu Kurekebisha na Kutenda Haki, Vinginevyo Karma Will Do
  12. Wito: Hoja za Kisheria za TLS, Prof. Shivji na wengine wote kupinga IGA, zisijibiwe Kisiasa kwa maneno matupu!, zijibiwe Kisheria kwa Vifungu!.
  13. Wajua kuna ndoa halali, batili na batilifu? Ndoa ya TPA na DPW, ni Ubakaji? Wajua ubakaji unaweza kuwa alali? IGA batili yaweza kuzaa HGA halali?
  14. IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria vilaza wa Ajabu. Je, Bunge letu na Serikali navyo ni vya Ajabu?
  15. Katiba mbovu, sheria mbovu, mikataba mibovu. Leo tumetozwa zaidi ya Tsh. Bilioni 260. Kufanywa kichwa cha Mwendawazimu hadi lini?
  16. IGA ya DPW imetusaidia mambo mengi. Kwanza kuonyeshea tuna wanasheria wa aina gani, pili kuidogosha fani ya sheria na sasa kila mtu ni Mwanasheria?
  17. Mwenye dada hakosi shemeji, IGA ni posa tu. Je, tuendelee kupiga kelele kuzozania posa, au tutulie tupange Mahari ya maana kwenye HGA?
  18. Je, umefika wakati kutimiza Uzalendo wa kweli wa kwenda kwenye Serikali moja?
  19. Na kufuatia baadhi ya watu wenye akili fupi humu kudhani mimi ni chawa, nawahakikishia mimi sio chawa Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!
  20. Chawa hawezi kupandisha bandiko kama hili Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
 
Wanabodi,
Declaration of Interest
Mimi ni Mkatoliki, nimelisoma tamko hili, News Alert: - Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu naulizia, huku sio kuchanganya dini na siasa?.

Mama Samia ameikubali DPW, ameileta, Bunge ambalo ndio wawakilishi halali wa wananchi wameikubali, who the hell is TEC ikatae DPW?

Paskali
Hizi mada unarudia rudia sana.

Mods waunganishe na mada yako ya kuchanganya dini na siasa.

Unazo nyingi tu.

Moderator
 
Wanabodi,
Declaration of Interest
Mimi ni Mkatoliki, nimelisoma tamko hili, News Alert: - Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu naulizia, huku sio kuchanganya dini na siasa?.

Mama Samia ameikubali DPW, ameileta, Bunge ambalo ndio wawakilishi halali wa wananchi wameikubali, who the hell is TEC ikatae DPW?

Paskali
Umesoma vizuri Tamko brother? Kwani Maaskofu hawana haki ya kulinda Rasilimali za Taifa hili.

Tunasubiri na Bakwata nao waunge mkono.

Bikira Maria ndiyo mlinzi wa Taifa letu.

Kanisa Moja Takatifu la mitume
 
Wanabodi,
Declaration of Interest
Mimi ni Mkatoliki, nimelisoma tamko hili, News Alert: - Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu naulizia, huku sio kuchanganya dini na siasa?.

Mama Samia ameikubali DPW, ameileta, Bunge ambalo ndio wawakilishi halali wa wananchi wameikubali, who the hell is TEC ikatae DPW?

Paskali
Hakuna kingine wanaogopa influence ya mwarabu, wanajua uislam ulifika Tanganyika kupitia mwarabu, bila ujio wa mwarabu pasingekua na uislam, wanajua mwarabu ana pesa, pesa zitaleta miradi Kama shule na hospital ambazo wao wametumia kuvuna waamini
 
Kuchanganya dini na siasa maana yake nini?

Unataka kuacha rasilimali za watanganyika zichezewe, kwasababu wale wenye nafasi ya kuzilinda ambao ndio huyo Kaisari wako aliyepewa rushwa asikemewe?

Kwanini hamtaki TEC watoe maoni yao kama ambavyo wengine wote wamekuwa wakiyatoa bila kujali nafasi zao?

Wewe mtu kweli unazidi kuwa mjinga, unapotumia hoja ya kusema angekuwa ni Magufuli ameileta DPW ingekuwaje?

Mbona hukusema neno wakati TEC walipomshutumu Magufuli na serikali yake kwa kuminya haki za binadamu, na uhuru wa vyombo vya habari? au unataka mpaka Magufuli nae atoe bure bandari zetu?

Hakutoa ndio maana wakakaa kimya, lakini alipokosea, walimpinga.

Hiki ulicholeta hapa hakitakiwi kutiliwa maanani na wote wanaojilewa, umeandika unafiki na kujipendekeza kwa hali ya juu sana, tena bahati mbaya ukiwa wa kiume!, kwa sababu siku hizi unajulikana umekuwa mtu wa aina gani.
 
Back
Top Bottom