PatPending
JF-Expert Member
- Aug 17, 2007
- 491
- 102
Sidhani kama bandiko hilo linawakaanga maskofu hata kidogo, hata kama hawakutumia lugha kali kama ambavyo tungependa iwe hivyo...hivi kweli mngetegemea hao maaskofu watamke kuwa hawamtambui Komandoo Salmin Amour ndio turidhike kuwa wametoa tamko kali???
Ukilinganisha na kichwa cha thread hii, bandiko haliendani na kichwa hicho. Kuna tofauti kati ya neno "Kulaani" na "Kusikitika" au "Kuonyesha masikitiko". Kwa hali ya kawaida mtu yoyote yule husikitika pale tukio baya kama ghasia na vifo vinapotokea na kusikitika huku kutokana na kuguswa na madhara ya tukio kama hilo. Kulaani ni kupinga kwa nguvu zote na katika tukio kama hilo mtu wa kawaida hulaani yule aliyesababisha masahibu hayo iadha kwa kutoa amri ya kudhuru au kudhuru.
Either way, it will be interesting to revisit what was said on Feb the 8th, 2001. Unajua tatizo la imani linaamsha hisia sana kwa baadhi yetu na ni lazima tukubali kwamba kuna baadhi bado wanafeel aggrieved kutokana na kuona kwamba wenzao hawakuwasupport vya kutosha pindi walipowahitaji.
Mkuu umeibua a very interesting point, je siku ikitokea viongozi fulani wa dini fulani wakasema hawamtambui rais na wenzao wa dini nyingine wakawapinga itakuwaje especially in light ya haya matatizo ya Arusha?
Tisa kumi, umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, hata katika kudai haki au kupinga perceived injustice. Hivi hawa viongozi wa dini za Abrahamu walishindwa kuwasiliana, kuketi na kutoa tamko la pamoja kuhusiana na kule Arusha au Zanzibar kabla ya hapo? Siku hizi kuna njia nyingi tu za mawasiliano na isitoshe Arusha mjini ni eneo dogo. Wangeweza kuepusha malumbano yote haya ya sasa hivi kwa kufanya hivi.
Ndiyo maana narejea ujumbe wangu wa awali, viongozi wa dini za Abrahamu warudi kwenye nyumba zao za ibada waziombee amani nafsi zao,zetu na taifa kwa ujumla. Na pia wasisahau kuomba tuepushwe na dhambi ya ubaguzi ambayo inawezekana pasi kukusudia wamezileta.