Maandamano ya Chadema yatishia Serikali ya CCM madarakani

Dk. Slaa: Moto ni ule ule
• Kikwete asafiri tena nje, CUF nao wamshambulia

na Waandishi wetu


amka2.gif
WAKATI Rais Jakaya Kikwete akihamishia matatizo yanayolikabili taifa katika mikono ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwamba wanachochea vurugu, viongozi wa chama hicho wamejibu mapigo kwa kumtaka aache kuogopa kivuli chake na kama ameshindwa kuliongoza taifa, ajiuzulu mara moja.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho taifa, Dk. Wilbrod Slaa, wakati wa mahojiano na gazeti hili jana.
Dk. Slaa na viongozi wenzake, akiwemo mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe, ambao wako mikoa ya Kanda ya Ziwa wakifanya mikutano ya hadhara maarufu kama Operesheni Sangara, alisema wameshangazwa na kauli ya Rais Kikwete kwamba CHADEMA inafanya vurugu ili kuvunja amani ya nchi.
"Tunataka kumwambia Rais Kikwete kuwa hakuna Mtanzania mwenye hofu na CHADEMA, isipokuwa ni hofu na ‘msoto' wa maisha magumu na ya mateso bila chuki! CHADEMA si tishio kwa usalama wa nchi bali ni kielelezo cha utashi wa jamii ya walalahoi na wavuja jasho maskini wenye shida, dhiki na taabu za maisha ya kiuchumi, kijamii na kisiasa," alisema Dk. Slaa.
Dk. Slaa ambaye amepata kuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita na kutoa upinzani mkubwa kwa CCM, aliendelea kusema Rais Kikwete ni kiongozi aliyeshindwa kuleta maisha bora, sasa amefikia hali ya woga na ana wasiwasi na hali tete ya wananchi kwani ameshachoka akili na hawezi tena kufikiria utatuzi wa matatizo ya wananchi wake.
"Ukweli ni kwamba Watanzania wana kero za maisha magumu na hawahofii usalama wa maisha yao mikononi mwa CHADEMA. Na yeyote anayesema juu ya CHADEMA kuvuruga amani ya nchi ni katika kujenga hoja nyepesi ili kwa hoja hiyo chakavu CHADEMA kama chama kionekane mbele ya macho ya jamii kwamba ni chama cha vurugu," alisema kiongozi huyo maarufu nchini.
Kwa mujibu wa Dk. Slaa, Rais Kikwete ana wajibu wa kurekebisha hali ya uongozi wake ili kuleta tija na ufanisi kiuchumi na kijamii kwani Watanzania wanataka hali bora na si maneno yasiyokuwa na mashiko.
"Kikwete anapaswa kujua kwamba ukiona wananchi wamechoka na kupigika kimaisha, usiwahubirie amani na utulivu kwa kuwa hakuna amani mahala penye shida, dhiki, taabu ya maisha na njaa," alisema.
Aliwaahidi Watanzania kuwa CHADEMA imejipanga kufanya mikutano nchi nzima kuelezea matatizo yanayolikabili taifa kwa sasa na kusisitiza CHADEMA haina uwezo wa kumng'oa Rais madarakani bali wananchi ndiyo wenye uwezo huo wakiamua.
Akizungumzia kauli hiyo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine, Profesa Mwesiga Baregu, amemshangaa Rais Kikwete na kumwita kuwa mwoga wa siasa za upinzani na kumtaka awe na ngozi ngumu.
Baregu alisema hakutegemea kama Rais angetumia muda mwingi kuilaumu CHADEMA badala ya kuzungumzia matatizo yanayoikumba taifa.
"Nimeshangaa kidogo nadhani Rais sio mkomavu wa upinzani, ni kama vile anataka kulishtua taifa bila kuwa na sababu; CHADEMA inazungumza mambo ya kawaida kabisa katika mikutano yake huko ni kutokomaa na siasa na woga usio na sababu," alisema Prof Baregu.
Alisema kama CHADEMA wamekuwa wakifanya mikutano yao na kuifananisha nchi kuweza kuwa kama Libya ni kutokana na kuwa na matatizo mengi ambayo hayajapatiwa ufumbuzi hivyo aliitahadharisha serikali ya CCM kuwa makini.
"Sisi tunafanya kazi za kuwaambia watu CCM ndio iliyotufikisha hapa tulipo hatuna makosa na wanatakiwa kufanya mambo ya msingi ambayo Watanzania wanayahitaji na kama hawajafanya kuna hatari ya kutokea ya Libya, tatizo liko wapi?" alihoji Profesa huyo.
CCM yapigwa ganzi
Wakati Rais Kikwete akiamua kuwalipua viongozi wa CHADEMA, ndani ya chama hicho viongozi wake ni kama wamepigwa ganzi kiasi cha kushindwa kuamua jinsi ya kujibu hoja zinazotolewa na viongozi wa CHADEMA kwenye mikutano yao ya hadhara ya Operesheni Sangara.
Baadhi ya vigogo wa CCM waliozungumza na gazeti hili, walisema kuwa chama hicho kimegawanyika kuhusu mbinu itakazozitumia kujibu hoja za CHADEMA kwani baadhi wanataka uitishwe mkutano wa vyombo vya habari, huku wengine wakipendekeza waende kwenye mikutano ya hadhara katika maeneo waliyopita CHADEMA.
"Tatazo tulilonalo sasa, nani atasimama kwenye mikutano ya hadhara kuhutubia kupinga hoja za CHADEMA na watu wakamsikiliza? Je, tukienda mikoani walimopita CHADEMA, nasi tutapata idadi kama ile ya CHADEMA? Lakini tukiamua kuitisha mkutano wa wana habari, utakuwa na maana kama ile mikutano ya hadhara ya Operesheni Sangara?" alihoji mmoja wa viongozi wa CCM.
Kigogo huyo ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) na Mkutano Mkuu wa chama hicho tawala, alikiri kuwa CHADEMA imekiweka chama hicho katika wakati mgumu na hiyo imetokana na udhaifu wa CCM katika kushughulikia kero za wananchi.
"Hoja zote za CHADEMA, tumewapa wenyewe kwa sababu ya udhaifu wetu kiuongozi hasa tabia ya kupenda kulindana. Angalia matatizo kama ya mgawo wa umeme na kupanda kwa gharama zake, sakata la ufisadi wa Dowans na Richmond, wizi wa EPA, Kagoda, ukosefu wa ajira, makundi yanayokinzana ndani ya CCM, maisha magumu ni miongoni mwa mambo tuliyoyaachia na ndiyo CHADEMA wanayatumia kutushambulia, hapa uchochezi uko wapi," alihoji kigogo huyo.
Hotuba yake yamponza
Wananchi mbalimbali waliotoa maoni yao wameishutumu hotuba ya Rais Kikwete wakisema kuwa ni ya uchochezi.
Mwenyekiti wa taasisi isiyo ya kiserikali ya FORD, Seneta Julius Miselya, alisema jana kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) si wachochezi kama anavyosema Rais Kikwete bali anayechochea hayo ni Rais mwenyewe kwa kushindwa kutimiza wajibu wake kwa wananchi.
"Hotuba yake ni ya uchochezi, napinga kwa nguvu zote kuwa CHADEMA ni wachochezi bali wanazungumza ukweli kwamba wakipata madaraka watawatendea vipi wananchi. Sisi hatuoni mantiki yoyote kuishutumu," alisema Miselya.
Aliongeza kuwa Rais Kikwete ameshindwa kuwatimizia wananchi maisha bora hali ambayo inasababisha maisha ya sasa kuwa magumu mara tano ya wakati wa utawala wa Rais Benjamin Mkapa.
Alimshauri kujiuzulu kwani hali inayoendelea kutokea nchini ni matokeo mabaya ya utawala wake.
Aliitaka CHADEMA kutotishika na kauli ya Rais bali kuendeleza wimbi lao la kukutana na wananchi ili kuwaelimisha kuhusu mambo mbalimbali.
Naye Jerry Tillya alimshangaa Rais kwa hatua yake ya kutumia muda mwingi kuiponda CHADEMA badala ya kueleza matatizo yanayoikabili nchi.
Alisema hivi sasa nchi inakabiliwa na wimbi la mgawo wa umeme, maisha magumu lakini badala ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo hayo ameigeuza hotuba yake kuwa uwanja wa kufanya kampeni.
Alisema badala ya kutoa shutuma angewaeleza wananchi katika kipindi cha siku 100 za uongozi wake ametekeleza jambo gani la maana.
Naye Amina Hassan, alisema Rais anapaswa kutumia busara hasa katika kuzungumzia vitu vinavyoigusa nchi.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Mtatiro Julius, alisema alichokifanya Rais katika hotuba yake ni kuwadanganya Watanzania kwani hali ya maisha kwa sasa inatisha.
Alitolea mfano tatizo la umeme nchini ambalo lilikuwepo tangu alipofariki Mwalimu Julius Nyerere ambalo halijapatiwa ufumbuzi hadi leo na hiyo inatokana na mikakati mibovu ya uongozi.
Kuhusu tatizo la njaa alisema hali hiyo inatokana na serikali kutokuwa na mipango madhubuti ya kuitokomeza kwa kuwawezesha wakulima bali inachokifanya ni kubadili maneno na misamiati ya kilimo kila kukicha.
Naye Juma Khalfan, alisema ameshangazwa na Kikwete kuzungumza masuala ya maandamano ya CHADEMA na jambo hilo linaonyesha dhahiri asivyojiamini.
"Tunazidi kupoteza imani na Rais wetu, wananchi tuna matatizo mengi yanayotukabili badala ya kutueleza namna ya kuyakabili tunashangaa kuona anatueleza masuala ya CHADEMA, hii inaonyesha kwamba hajiamini kabisa," alisema Khalfan.
"Tulitegemea atatuahidi kumaliza matatizo hata kwa asilimia kidogo lakini anasema hawezi kuyamaliza kwa kuwa Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa hawakufanya hivyo.
"Yeye alitakiwa awaonyeshe mfano marais waliopita na sisi wananchi wake tuliomchagua kwa imani kubwa," alisema Olotu.
Kikwete safarini tena
SIKU tano baada ya kurejea nchini akitokea nchini Mauritania na baadaye Ivory Coast, Rais Jakaya Kikwete ameondoka tena nchini jana kuelekea Paris, Ufaransa, kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa kimataifa wa Tansnia ya Uzinduaji (Global Extractive Industries Transparency Initiative -EITI).
Katika mkutano huo unaoanza leo, Rais Kikwete anatarajiwa kutoa mada juu ya umuhimu wa shughuli za uziduaji na uwazi katika mapato ya madini.
Baada ya kumaliza mkutano huo wa Paris, Ufaransa, Rais Kikwete atasafiri kuelekea Noukchott, Mauritania kwa ajili ya kikao cha marais wa Afrika wanaotafuta suluhisho la tatizo la kisiasa nchini Ivory Coast.
Akiwa nchini Mauritania, Rais Kikwete atajiunga na marais wa Mauritania, Afrika Kusini, Burkina Faso, Chad, Nigeria na Equatorial Guinea pamoja na wawakilishi wa Jumuia ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) Balozi Jean Ping na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN).
Ivory Coast imegawanyika katika sehemu mbili, moja ikimuunga mkono aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo, Alassane Quattara, na nyingine ikimuunga mkono Rais aliyekuwa anatetea kiti chake katika uchaguzi huo, Laurent Gbagbo.
 
Maandamano ya CHADEMA yaitia kiwewe CCM


na Ali Lityawi, Kahama


amka2.gif
JOTO la maandalizi ya maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) limeonekana kuwatia kiwewe wajumbe wa Kikao cha Halmashauri ya Chama cha Mapinduzi, (CCM) mkoani hapa, kiasi cha kuficha sare zao na kwenda kuzivalia ukumbini.
Wajumbe hao walikuwa wakihofia kuzomewa mitaani kama wangevalia sare hizo majumbani kwao kama ilivyo kawaida ya mikutano mingine.
Katika hali isiyo ya kawaida wajumbe hao walikosa kujiamini baada ya kukatiza mitaani ilhali wameficha sare zao na kuelekea kwenye mkutano huo uliofanyika juzi kwenye ukumbi wa CCM mkoani Shinyanga.
Wajumbe hao walionekana wakiingia ukumbini na mikoba huku wakiwa wamevalia nguo za kawaida na baada ya kuingia walivalia humo ndani sare hizo hali ambayo siyo kawaida ya makada hao wa chama tawala katika vikao kama hivyo.
Walipohojiwa na waandishi wa habari wa wajumbe wa mkutano huo walikiri kuwa kipindi hiki ambacho CHADEMA wana maandalizi ya maandamano mkoani hapa imewatia hofu hasa ukizingatia upepo wa kisiasa kwa chama chao katika mji wa Shinyanga tangu kufanyika uchaguzi hali si shwari.
"Hali halisi ya mji huu nanyi mnaitambua kwa upandee wa CCM kuwa si shwari hivyo kupita mitaani na sare za CCM ni kujiletea matatizo ndio maana tunazivaa kwa machale kwa kuhofia kuzomewa hata kupigwa na vijana wa mji wa shinyanga ambao hawataki kusikia chama cha mapinduzi hata harufu yake, '' alisema Paschal Ntale ambaye ni mjumbe kupitia UVCCM kutoka wilayani Kahama ambaye pia ni kada mkubwa wa chama hicho.
Aidha mjumbe mwingine, Charles Maduhu kutoka Bariadi alisema tatizo lililowachukiza vijana ni matokeo ya ubunge jimbo la shinyanga mjini ambayo matokeo yake yalileta utata hali ambayo jamii haitaki kuona wana CCM wakilanda landa mjini.
Alisema hali hiyo tu imetia hofu kwa baadhi ya makada kuonekana mitaani wakiwa wamevalia sale kama ilivyokuwa kawaida kwenye mikutano mingine.
Wajumbe walioonekana kuvaa sare hizo ni wale waliokuwa kwenye magari lakini watembea kwa miguu hawakuthubutu hata baada ya kumalizika kwa mkutano huo walizivua na kuziweka kwenye mikoba.
Wakati huo wafuasi wa CHADEMA walikuwa wakiranda mitaani kutangaza mkutano wao wa maandamano yaliyofanyika siku ya Jumatatu wiki hii mjini Shinyanga.
Hata hivyo katika mkutano huo wa Halmashauri ya CCM mkoa wa Shinyanga uliokuwa ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Hamis Mgeja wajumbe walivutana zaidi kuhusu wakuu wa wilaya kuwakumbatia mawakala wa pembejeo za vocha wanaodaiwa kuchakachua malipo ya fedha za ruzuku ambazo hutolewa na serikali.
Pia wajumbe hao walilalamikia zoezi zima la wakuu hao wa wilaya ambao baadhi yao wanajihusisha na uwakala huo wa usambazaji wa pembejeo kwa kutumia migongo ya ndugu zao ama jamaa zao wa karibu hali inayosababisha kushindwa kuwadhibiti mawakala wanaochakachua fedha hizo za ruzuku kwa kugawa mbolea hewa kwa wakulima.
Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mgeja alisema taarifa kamili ya kikao hicho itatolewa kwa maandishi huku akisisitiza chama hicho huenda kikatoa kauli nzito juu ya zoezi zima la usambazaji wa pembejeo za ruzuku kwa wakulima.
Mwenyekiti huyo wa CCM alisema kuwa taarifa hiyo itakwenda pamoja na kujibu makombola yaliyotolewa juzi na viongozi wa CHADEMA katika mkutano wao uliofanyika mjini shinyanga baada ya kumaliza maandamano yao yaliyokusanya umati mkubwa wa wakazi wa manispaa hiyo.
 
Jeshi la Polisi lagawanyika
• Askari wadogo watishia kufanya hujuma

na Bakari Kimwanga


amka2.gif
SASA ni dhahiri kuwa Jeshi la Polisi nchini limegawanyika kimaslahi baada ya kuelezwa kuwa askari wadogo ndio wamekuwa wakikatwa mishahara bila kurudishiwa huku wale wa makao makuu na walio karibu na vigogo wakipewa nafuu.
Wakati wabunge wakiwa wameshaweka kibindoni zaidi ya sh milioni 300 za mikopo na posho, askari polisi waliokuwa wamekatwa posho bila maelezo katika mishahara ya Desemba mwaka jana na Januari mwaka huu, hawajalipwa hadi sasa, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
Uchunguzi huo umebaini kuwa askari waliolipwa baada ya sakata hilo kuripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari mwanzoni mwa mwaka huu, ni askari wachache hasa wale wa makao makuu na vitengo vingine vya jeshi hilo ndio waliolipwa, huku askari wengi hasa wa mikoani wakiachwa.
Askari hao waliahidiwa kulipwa mwezi uliopita, lakini hadi sasa ni askari wachache waliorejeshewa wengi wao wakitajwa kuwa ni wa makao makuu na watoto wa vigogo.
Baadhi ya askari polisi walithibitisha kukatwa kwa mishahara yao, huku taasisi husika za serikali ambazo ni polisi makao makuu na hazina, wakirushiana mpira kuhusu suala hilo.
"Huu ni unyonyaji wa wazi yaani mwezi huu tumekatwa posho zetu zote hakika sijui kama haya wanafanyiwa maofisa wa jeshi letu wa ngazi za juu," alisema mmoja wa askari toka mkoani Ruvuma ambaye aliomba asiandikwe jina lake gazetini kwa kuhofia usalama wake.
Askari polisi mwingine aliliambia Tanzania Daima Jumatano kuwa hatua hiyo imemsononesha hata kufikia kuharibu bajeti yake ya mwezi Januari.
Aidha, alisema kitendo cha kukatwa posho huenda kikasababisha askari polisi katika vituo kuwabambikizia kesi raia ili waweze kujiongezea kipato cha fedha.
Askari huyo alidai kuwa katika mshahara wake wa mwezi Desemba mwaka jana, alikatwa sh 150, 000 jambo ambalo limemfanya akope kwa ajili ya kuwapeleka watoto shule.
Hata hivyo, kukatwa kwa fedha hiyo kumeibua utata hasa baada ya uongozi wa Jeshi la Polisi kutupiana mpira na Wizara ya Fedha walipotakiwa kutoa maelezo kuhusu suala hilo.
Wakati polisi ikisema yenyewe haihusiki na malipo ya askari wake, Wizara ya Fedha na Uchumi ilisema inaandaa malipo ya wafanyakazi kulingana na maelekezo ya mwajiri husika.
Msemaji wa polisi, Advera Senso, aliliambia gazeti hili jana kuwa hawezi kuzungumzia suala hilo kwani malipo ya polisi yanafanywa na Wizara ya Fedha (Hazina).
Tanzania Daima Jumatano iliwasiliana na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali wa Jeshi la Polisi, CP Clodwig Mtweve, na kusema kuwa hawezi kulizungumzia suala hilo kwa kuwa kwa sasa yuko likizo.
"Ndugu yangu mimi niko likizo kulizungumzia hilo nje ya ofisi si utaratibu mzuri lakini ni vema ukawasiliana na Chagonja ambaye yuko ofisini kwa sasa," alisema Mtweve.
Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ingiahedi Mduma, alisema kuwa wizara haihusiki na suala la kupanga mishahara ya watu.
"Sisi kama Hazina tunalipa kutokana na maagizo ya mwajiri na jukumu letu ni kufuata maelekezo hayo," alisema Mduma.
Hata hivyo, alisema masuala yanayohusu mishahara ya polisi ni vizuri jeshi likatoa ufafanuzi lenyewe kuliko ilivyo sasa kwani wao ndio wenye idadi ya watumishi wao kamili.
Mduma alisema Jeshi la Polisi haliko chini ya Wizara ya Fedha bali Ofisi ya Rais - Manejimenti ya Utumishi wa Umma, kwa hiyo mishahara inayopangwa kutoka Utumishi, ndiyo inayolipwa na Hazina.
"Sisi ni kama mawakala tu suala la kulipa mishahara linatokana na mipango iliyotolewa na utumishi na jeshi hilo, kwa hiyo hatuwezi kubadilisha chochote tunacholetewa," alisema.
Lakini Mduma alidokeza kuwa kuna uwezekano wa baadhi ya polisi ambao hawajalipwa fedha za pango kuwa tayari wamepewa nyumba za kuishi.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Tasisi ya Wanaharakati wa Maendeleeo barani Afrika (ForDIA) ambayo ilitolewa Januari 18, mwaka huu, Idara ya Polisi ni kinara wa rushwa ikizitangulia idara nyingine za serikali ambazo ni Afya na Mahakama.
Kwa mujibu wa Fordia, polisi inaongoza kwa kupokea rushwa, huku sekta za Afya, Mahakama, Elimu, TANESCO na Idara za Leseni na Ushuru zikitajwa pia kuwa na kiwango kikubwa cha rushwa.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Bubelwa Kaiza alisema, "Polisi ndio vinara wa rushwa kwa sasa."
Buberwa alisema, utafiti unaonyesha kuwa Jeshi la Polisi linaongoza kwa asilimia 81.9 kwa kupokea na kutoa rushwa.
"Polisi imeendelea kushika nafasi ya kwanza baada ya kuongoza idara nyingine kwa kuwa na asilimia 85.3 mwaka jana kutoka nafasi ya pili ya asilimia 75.8 waliyokuwa wakiishikilia mwaka 2009,'' alisema Bubelwa.
Utafiti huo uliofanywa na Fordia ulifanyika katika mikoa 11 ya Tanzania ambayo ni Dar es salaam, Tanga, Kagera, Manyara, Rukwa, Tabora, Kilimanjaro, Mwanza, Mara, Pwani na Mtwara.
Na kumejumuisha serikali za mitaa 47 katika wilaya tofauti nchini na kulishirikisha watu mbalimbali wapatao 1,122 ambao waliulizwa maswali, lengo likiwa kujua kinara wa rushwa nchini.
Kati ya watu hao 1,122 waliohojiwa wanaume walikuwa 646 na wanawake 476. Hata hivyo watu walioweza kutoa majibu walikuwa 367, ambapo wanaume walikuwa 248 na wanawake 119, huku Bubelwa akieleza kuwa watu waliohojiwa ni wanaoishi mijini na vijijini.
Buberwa alisema na kufafanua kuwa walipata majibu na maoni mbali mbali kutoka kwa wananchi kuhusu suala la polisi ambapo walielezwa kuwa watu hukamatwa kwa uonevu na hulazimika kutoa 'kitu kidogo' (rushwa), ili waachiwe hata kama hawakuwa na makosa, ambapo pia watu wenye makosa wanapofikishwa polisi huachiwa baada ya muda mfupi kutokana na kutoa kitu kidogo.
 
Hotuba ya Kikwete moto


*Yadaiwa haijaeleza suluhisho la matatizo
*CCM waifagilia, wasema ilikuwa ya faraja


Na Tumaini Makene

HOTUBA ya mwisho wa mwezi Februari ya Rais Jakaya Kikwete, imepokewa kwa
hisia tofauti, huku ikielezwa na wengi kuwa imeshindwa kuonesha mtazamo mpana juu ya chanzo na suluhisho la matatizo yanayoikabili nchi na jamii ya Watanzania kwa sasa.

Wakazi wasomi na baadhi ya wananchi wameikosoa wakisema kuwa tishio kubwa la usalama na mstakabali wa nchi kwa sasa si vyama vya siasa, bali ni kushindwa kwa mfumo wa uzalishaji mali na siasa, makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameipongeza wakisema ilikuwa ya faraja ambayo imeeleza matatizo makubwa ya nchi.

Hayo yamekuja siku moja baada ya Rais Kikwete kutoa hotuba yake ya kila mwezi kwa taifa, ambapo kati ya masuala aliyoyazungumzia ni pamoja na suala la hali ngumu ya maisha inayoongeza umaskini miongoni mwa wananchi, huku bei za bidhaa muhimu zikizidi kupaa.

Katika hotuba hiyo, Rais Kikwete alikiri kuwepo kwa ugumu wa maisha ya Mtanzania unaosababisha matatizo kadhaa, lakini akawaomba kuyakabili kwani yote hayawezi kuisha haraka kama ambavyo Watanzania wengi wanapenda iwe.

Rais Kikwete alisema kuwa serikali imeelekeza nguvu na raslimali zake katika nyanja mbalimbali hivyo kikwazo si upungufu wa sera wala dhamira, bali kikwazo kikubwa ni kiwango kidogo cha maendeleo ya kiuchumi nchini, huku pia akilinganisha hali ilivyo bora sasa kuliko katika awamu tatu za serikali zilizopita, kuanzia wakati wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.

Ubovu wa mfumo wa uchumi


Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa na Utawala, Chuo Kikuu Dar es Salaam (CKD), Bw. Bashiru Ally, alisema kuwa ni wakati mwafaka kwa nchi kukaa chini kufikiria kwa mapana chanzo hali cha matatizo yanayoikumba nchi kwa sasa, badala ya kushughulika na dalili zake, ikidhaniwa kuwa ndiyo vyanzo.

"Nafikiri kuna tatizo katika namna tunavyoyaona na kuyaeleza matatizo yetu na vyanzo vyake, ni kweli rais kazungumza vitu vya msingi kabisa, lakini tatizo ni namna anavyoonekana kuhitimisha, ni kama kwamba hatuna tatizo kabisa katika sera na mfumo wetu wa uzalishaji mali, bali inaonekana kwamba tatizo liko katika uwezo wetu, hilo ndilo tatizo tulilonalo.

"Kuna tatizo kubwa katika sera na mfumo wetu wa uzalishaji mali tuliokumbatia, na haya yanayoonekana ni dalili tu za ubovu wa mfumo wetu huo unaopelekea sekta muhimu kama ya kilimo kutoa mchango mdogo sana katika pato la taifa.

"Mfumo unaotufanya tunaua wakulima wadogo kwa kuwanyang'anya ardhi...tunapaswa kufikiria kwa mapana, chanzo cha mtatizo yanayosababisha mfumo wa siasa kufeli, mfumo wa demokrasia kufeli, kiasi ambacho watu hawataki kupiga kura, mfumo wa elimu umefeli kiasi ambacho nusu ya watahiniwa wamefeli mitihani," alisema Bw. Ally.

Alisema ni vyema Tanzania kama nchi ikatafakari kwa kina mfumo huo iwapo unaweza kusaidia kilimo kinachokufa, ukosefu wa ajira kwa waliosoma na wasiosoma, watu kukatishwa tamaa na michakato ya kidemokrasia kama vile kupiga kura.

"Sasa hivi ni baadhi ya vitu unapovichambua unaonekana wewe ni mtu wa ajabu, ndiyo maana hata rais analalamika juu ya CHADEMA. Ukiangalia kwa undani haya si matatizo ya CHADEMA...CHADEMA hawakuwepo kule Darajani (Zanzibar) ambako vijana wamachinga waliandama na kupambana na askari.

"Matatizo ya Darajani hayana tofauti na matatizo ya maeneo mengine, CHADEMA hawako katika uporaji mkubwa wa ardhi ya wakulima wadogo ambao sasa tunawaona wanajitokeza kupambana na wawekezaji wakubwa.

"Hawako katika uporaji mkubwa unaofanyika katika raslimali zetu kama vile madini, hawako katika kufeli kwa nusu ya wanafunzi wetu...bali ni mfumo unaotugawa vibaya kiasi ambacho pengo la walionacho na wasionacho ni kubwa sana," alisema Bw. Ally na kuongeza;

"Ni wakati mwafaka tukakaa chini na nafikiri moja ya nafasi ni katika mjadala wa katiba mpya, tutafakari mfumo wa uzalishaji mali, tutafakari mfumo wetu wa siasa, tujadiliane kwa kina...tujadili juu ya miiko ya uongozi, si maadili, miiko ya uongozi, tuweke wazi ukitaka kuwa tajiri uende kwenye sekta binafsi.

"Huwezi kuwa na serikali iliyojaa wajasiriamali, walanguzi, kisha ukatarajia watatoa huduma kwa wananchi, huwezi kuzungumzia hali ngumu ya maisha lakini serikali haiendani na hali hiyo...wananchi wana maisha magumu lakini juzi wanasikia wabunge wanakopeshwa milioni 90, hapo watu watakuwa na hasira tu, hawawezi kuvumilia viongozi walanguzi.

Hotuba ya faraja

Kwa upande wake, mmoja wa wanasiasa waandamizi nchini, Bw. John Chiligati alisema kuwa hotuba ya rais ilikuwa ni 'faraja' kwa sehemu kubwa, kuanzia kwa waathirika wa mabomu, waliokumbwa na uhaba wa chakula na wapenda amani ya nchi, kwani Rais Kikwete alikemea uchochezi unaofanywa na wanasiasa hata kuhatarisha amani ya nchi.

"Hotuba ya rais kwa kiasi kikubwa imetuliza wasiwasi uliokuwepo...ilikuwa ni ya faraja...wenzetu waliopatwa na athari ya mabomu huko Gongolamboto imewapatia faraja kubwa sana kwa kujengewa nyumba zao...suala la ukame ambalo limeleta tishio la chakula pia kalizungumzia akisema kuwa kuna tani zaidi ya elfu moja, hayo ni matumaini makubwa.

"Lakini pia kwa sisi wapenda amani ya nchi imetupatia faraja baada ya kukemea matamshi yanayoashiria vurugu nchini...hivi kweli mwanasiasa anakwenda kusema kuwa tutafanya kama Libya, anajua maana ya siasa kweli huyo, maana vurugu hazina macho, waangalie kwa mapana, kwa kweli imetupatia faraja sana hotuba hiyo," alisema Bw. Chiligati.

Kwa upande wingine Mkuu wa Kitengo cha Propaganda wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Tambwe Hiza alisema kuwa hotuba ya Rais Kikwete ilikuwa nzuri, ikiweka mambo mengi wazi kwa mtu yeyote kuweza kuelewa uhalisia wa mambo yanayoendelea nchini.

Alisema kuwa Rais Kikwete ama ilivyo kawaida yake, alitumia hali ya utulivu na ukweli kufikisha ujumbe mahsusi kwa wananchi wake.

"Kwa kifupi hotuba ilikuwa nzuri sana, kwa kweli kwa mtu yeyote ambaye hana jambo lolote, ila anataka kujua hali halisi, rais ameeleza kila jambo vizuri sana, kwangu mimi nimeshika mambo manne kwa haraka...kwanza suala la Dowans ambalo watu wanapenda kulisema lakini wanalipotosha kwa kutumia uongo.

"Ameliweka sawa kama alivyosema Dodoma kuwa maamuzi ya kamati kuu na yale ya kamati ya wabunge wa CCM ni kuwa suala la Dowans lisubiri mahakama, lakini watu wanapotosha ikilipwa itakuwa hivi, kwani wanasema hivyo mwenye mamlaka ameshakubali kulipa," alisema Bw. Hiza.

Naye Katibu wa CCM wilaya Kilindi mkoani Tanga Bw. Aluu Segamba amesifu hotuba ya Rais Kikwete na kusema imeibua matumaini mapya kwa Watanzania hususani kwa hatua ya serikali yake kuchukua jukumu la kuwajengea nyumba waathirika.

"Rais amefanya jambo jema sana kuamua kuwajengea nyumba wananchi hao, bila kufanya hivyo wangeingia waliomo na wasiokuwe kwa lengo la kutaka kujinufaisha," alisema Bw. Segamba.

Akizungumzia kauli ya Rais Kikwete kuhusu CHADEMA alisema ametumia lugha ya upendo na uugwana kushauri chama hicho kuepusha vurugu kwa kuzingatia umoja na mshikamano wa Watanzania.

Alisema maendeleo si jambo linalofikiwa kwa miaka 40 au 50 bali ni mchakato wa mrefu hata Marekani iliendelea baada ya miaka mingi huku ikiungana majimbo 51.

Kukabili majanga


Kwa upande wake Dkt. Peter Bujari alisema kuwa nchi inahitaji suluhisho la muda mrefu ili kukabiliana na madhira yanayowakabili wananchi na nchi kwa ujumla, badala ya kutegemea mipango ya muda mfupi.

Alisema kuwa viongozi watapoteza heshima mbele ya jamii iwapo hawatakuwa makini katika sera za kupunguza umaskini hasa kwa kujikita katika kunusuru upatikanaji wa nishati ya uhakika katika nyanja za umeme na mafuta ambazo ndizo zinagusa maisha ya kila siku ya kila Mtanzania.

"Nilimsikiliza rais kidogo, mchango wangu unaweza kuwa katika maeneo kadhaa...katika suala la mabomu ya Gongolamboto, ingawa serikali imeonesha kitu kizuri kwa kuamua kuwajengea nyumba walioathirika, yaani ime-sympathise nao (imewahurumia), lakini rais alipaswa kutuambia namna gani majanga kama hayo hayatajitokeza tena.

"Yaani badala ya kuzungumzia crisis management (utatuzi wa migogoro), tulipaswa kuzungumzia preventive management (uzuiaji wa majanga ya aina hiyo), angetupatia uhakika wa kutotokea kitu kama hicho, maana kilitokea mwaka 2009, kisha 2011, hilo la mikakati ya kuzuia milipuko isitokee tena hakuligusia.

"Katika suala la umeme rais alizungumza kina cha maji katika mabwawa yetu kilivyoshuka na mipango mingine ya serikali ya kupata umeme kama huko Mwanza na kadhalika...lakini suala kubwa kwangu ni mstakabali wetu kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa yaliyopo sasa na yanayotarajiwa miaka ishirini ijayo.

"Katika hali kama hiyo ni hatari sana kwa nchi kutegemea umeme wa maji. Tunavyo vyanzo kadhaa vinavyoweza kuchochea umeme mwingi tu, mathalani upepo wa Singida una unavuma kwa kasi na una uwezo wa kuzalisha umeme mara tatu zaidi ya ule upepo wa nchi za Scandinavian (Norway, Sweden, Denmark, Finiland).

"Lazima tupunguze utegemezi wa mvua, kuna vyanzo vya umeme pale Rufiji ambavyo zikifungwa mashine tatu tuna uwezo wa kuzalisha megawati 2,100 kila mashine ikizalisha megawati 700, na sisi mahitaji yetu ni megawati 900, kunatakiwa long term solutions (mipango ya muda mrefu ya ufumbuzi).

"Lazima tukubali kuingia gharama katika kuwekeza ili tutumie gharama kidogo wakati wa uendeshaji badala ya sasa ambapo tunategemea maji na mafuta ambayo ni ghali sana, pia kukitokea rabsha tu katika nchi kama Libya zinazozalisha mafuta, hata sisi pia tunaathirika,' alisema Dkt. Bujari, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Human Develompent Trust (HDT).

Katika suala la uzalishaji wa chakula cha kutosha alisema ni vyema mkakati wa kilimo kwanza ukajikita katika kilimo cha umwagiliaji badala ya kununua matrekta kwa kila kijiji au kata, kwani si maeneo yote yanahitaji zana hizo za kilimo, hivyo kusababisha upotevu wa fedha.

Akizungumzia kupanda kwa gharama za maisha, Dkt. Bujari alisema kuwa ni matokeo ya mzingo/mzunguko wa umaskini, unaosababishwa na ukosefu na kupanda kwa bei ya vitu muhimu kwa uchumi kama nishati ya umeme na mafuta, ambavyo athari yake ni kubwa katika sekta karibu zote za uzalishaji.

Suala jingine alisema ni kushuka kwa thamani/nguvu ya sh. ya Tanzania dhidi ya fedha nyingine katika soko la dunia, ambapo kwa miaka 15-20 iliyopita, fedha hiyo imepungua kwa kasi kutokana na nchi kushindwa kuuza bidhaa katika soko la dunia, kwani hakuna uzalishaji wenye tija na fanisi hasa katika eneo la viwanda.

"Iwapo mikakati ya kulenga watu wengi itazidi kuwa butu, watu watazidi kuwa maskini kuliko hivi sasa, umaskini utaongezeka sana na watu watakata tamaa na uongozi utakosa heshima," alisema Dkt. Bujari.

Sukari si tatizo pekee


Mwananchi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Malamilo John, mkazi wa Kigamboni alisema kuwa itakuwa vigumu maendeleo kupatika iwapo ufisadi hautapigwa vita kwa nia na dhamira thabiti, kwani unaathiri nyanja zote za uchumi nchini.

Alisema iwapo Serikali ya Rais Kikwete, ingeamua kuwa makini na kushughulikia matatizo na kero za wananchi, wapinzani wangekosa cha kusema hata kupunguza uungwaji mkono wanaoupata sasa.

"Unajua bwana, bei ya vitu haijapanda katika sukari tu, imepanda karibu kila mahali, lakini pia uongozi tulionao hata ukitoa maelekezo hayafuatwi, labda kwa sababu wao hawanunui katika maduka tunayonunua sisi, lakini hakuna mahali sukari inauzwa sh. 1,700, karibu kila sehemu ni sh. 2,000 mpaka 2,200, sh. 1,700 ni bei ya kufikirika tu.

"Lakini pia katika suala jingine, rais atambue kuwa CHADEMA hawakumwambia kuwa alete maendeleo ndani ya siku tisa, walichosema wao ni kuwa ndani ya siku hizo atoe kauli juu ya hoja zao, wananchi wanawaunga mkono CHADEMA kwa sababu wanazungumzia kero hizo, kama serikali wakiyafanyia kazi moja baada ya jingine, watakosa agenda.

"Lakini pia rais hataki kulisikia hili suala la ufisadi, ufisadi unaathiri nyanja zote za uchumi, ikiwemo hata hiyo kilimo kwanza...kwa mfano walioweka ten percent kwenye ndege ya rais hawawezi kushindwa kufanya hivyo kwenye ununuzi wa matrekta, barabara badala ya kujenga kwa shilingi moja, tunatumia shilingi tatu.

"Fedha ambazo zingetumika kusaidia mahali pengine, zinaliwa na watu wachache wasiochukuliwa hatua," alisema Bw. John.

 
Mbowe: Tutaandamana hadi kieleweke


Na Suleiman Abeid, Shinyanga

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe amemjibu Rais Jakaya Kikwete akisema chama chake kitaendelea
kuwahamasisha wananchi kufanya maandamano ya amani mpaka pale serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) itakaposikia kilio chao.

Alisema CHADEMA haitaogopa vitisho vilivyotolewa juzi na Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa Taifa wa CCM kwa vile serikali yake imeshindwa kuweka sera sahihi zitakazowaondolea Watanzania ugumu wa maisha.

Bw. Mbowe alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Shinyanga na vitongoji vyake mara baada ya maandamano makubwa yaliyoanzia eneo la daraja la Mhumbu hadi katika viwanja vya Joshoni kata ya Kambarage, manispaa ya Shinyanga.

Rais Kikwete hivi sasa amepata presha kubwa kutokana na maandamano haya ya amani pamoja na mikutano ya hadhara inayoendeshwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, anasema CHADEMA tunachochea vurugu na kuwahamasisha wananchi waikatae serikali na wamuondoe rais madarakani.

Sisi tunasema tutaendelea na maandamano haya mpaka pale kitakapoeleweka, ni maandamano ya amani, kama yeye Kikwete anaona yanamkera basi atukamate atuweke ndani, na tunasema watu wa usalama wa taifa mpo hapa, mpelekeeni salaamu hizi, hatuogopi kitu, tutaandamana, tutaandamana na kuandamana mpaka kieleweke.

Kikwete anapaswa aelewe kwamba sisi siyo wendawazimu, tunaandamana kwa kuwa hatutaki ailipe DOWANS kama vile kamati kuu yake ya CCM ilivyokuwa imeamua, serikali yake iwaondolee Watanzania ugumu wa maisha, sasa anapozuia maandamano na mikutano anatarajia Watanzania tutazungumzia wapi.

Ni budi ajifunze utaratibu mwingine wa nguvu ya umma wa kuzungumzia matatizo yao, maana njia zile za kidemokrasia zimeshindikana kutokana na maamuzi ya wananchi kupitia sanduku la kura kuchakachuliwa na watu wa CCM.

Hii ni njia mpya njia muafaka ya kuiamsha serikali ya CCM ijue ina wajibu kwa Watanzania, leo Kikwete anazungumzia matatizo ya sukari, anafikiri matatizo ya Watanzania ni sukari peke yake, maisha ya wananchi yamepanda kwa ujumla kwa sababu serikali yake haina sera mbadala.

Tunamweleza rais kuwa huu ni mwanzo tu, hana haja ya kupata presha, hatuwezi kuiheshimu serikali ambayo inashindwa kuondoa kero za wananchi na kuwaheshimu wananchi wake, haitaki kuwasikiliza,"

"Ameshindwa kuwawajibisha watendaji wake pale wanapofanya makosa ya makusudi.

Hakuna waziri anayethubutu kujiuzulu kutokana na uzembe unaofanyika katika wizara zao, tatizo la umeme mmeliona, mabomu ya Mbagala mwaka juzi na sasa Gongolamboto hakuna anayewajibika, sasa tufanye nini kama siyo kuandamana?� alihoji Bw. Mbowe.




1 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... mboe tatizo sio ww nimakengeza ndio yanayosababisha wewe umelaniwa na mungu ndiomaana ukawa na makengeza wewe ni shetani atakae kufuata ni shetani mwenzio
March 1, 2011 9:02 PM
 
Wanaotishia amani wakamatwe

ban_tahariri.jpg

amka2.gif
JUZI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilihutubia taifa kupitia utaratibu wake aliojiwekea wa kuzungumza na wananchi kila mwisho wa mwezi.
Hata hivyo tukiwa chombo huru cha habari na sehemu ya jamii pana ya Watanzania, tunaomba kutofautiana na mheshimiwa Rais katika baadhi ya kauli zake.
Kwanza tumeshangazwa na jinsi alivyozungumzia matatizo ya maendeleo ya nchi hii pale alipojilinganisha na viongozi waliopita.
Alisema na hapa tuna mnukuu: "Nyerere aliongoza kwa miaka 23 na hakuyamaliza matatizo ya maendeleo ya nchi hii. Na wale wa umri wangu au kunizidi wanakumbuka hali ilivyokuwa wakati anang'atuka. Hakuacha nchi ikiwa tajiri. Mzee Mwinyi kakaa miaka 10 hakuyamaliza, Mzee Mkapa naye kakaa miaka 10 hakuyamaliza. Mie nimekaa miaka mitano hayakwisha na nitamaliza mitano hayataisha yote. Lililo muhimu kuliko yote ni kuwa katika kila awamu nchi yetu imekuwa inapiga hatua ya kusonga mbele katika kujiletea maendeleo."
Sisi tunaamini kuwa sio sahihi kwa kiongozi wa nchi kuwatumia viongozi wastaafu kuficha udhaifu wa serikali iliyopo kwani kila awamu ilitekeleza majukumu yake kutokana na mazingira yaliyokuwepo.
Tunakumbuka wakati Rais wetu anaomba kura kuwa kiongozi mkuu wa nchi mwaka 2005 na 2010 hakutugusia kwamba tusitegemee kama atayamaliza matatizo yetu kwa sababu Nyerere, Mwinyi na Mkapa hawakuyamaliza. 2005 alisema atayamaliza matatizo yetu kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya na Tanzania yenye neema inawezekana.
Mwaka jana alisema anakwenda kufanya hata sehemu ya nchi yetu kuwa Dubai kwa nguvu zaidi, ari zaidi na kasi zaidi.
Haikubaliki kuanza kujitetea leo kwamba hatamaliza matatizo yetu kwa kuwa waliotangulia hawakuyamaliza.
Tumeshangazwa pia na kauli ya Rais dhidi ya CHADEMA pale aliposema, "Hivi karibuni wananchi wengi wameingiwa na hofu kubwa kuhusu usalama wa nchi yetu."
Kwa mujibu wa Rais ni mara ya kwanza Watanzani kuwa na hofu hiyo ambayo alidai imetokana na kauli na vitendo vya viongozi wa CHADEMA vyenye dhamira ya kutaka kuleta machafuko makubwa na uvunjifu wa amani nchini.
Alisema kufanya maandamano na mikutano ni haki ya msingi ya vyama vya siasa na raia, lakini kuigeuza fursa hiyo kuwa ni jukwaa la kuchochea ghasia na kwa nia ya kuiondoa serikali iliyoko madarakani kwa mabavu ni matumizi mabaya ya fursa hiyo.
Hilo limetushangaza zaidi. Ikiwa kikundi cha watu kama viongozi wa CHADEMA wanachochea ghasia na kutaka kuiondoa serikali iliyoko madarakani maana yake wanafanya uhaini.
Tulitegemea mpaka Rais anakuja kusema jambo hilo hadharani, tayari viongozi wa CHADEMA wangekuwa wamekwishakamatwa na kufunguliwa mashtaka ya uhaini.
Sisi tunatambua kuwa CHADEMA kuwaongoza wananchi kudai haki yao ya Kikatiba ambayo ni serikali iliyoko madarakani kuhakikisha lengo lake kuu ni ustawi wa wananchi, si uhaini na sio kuchochea ghasia wala si kutaka kuiondoa serikali iliyoko madarakani kwa mabavu.
Tunashauri wasaidizi wa Rais wahakikishe wanapomsaidia kuandaa hotuba waifanye kazi hiyo vizuri. Imekuwa ni kawaida sasa Rais kulihutubia taifa na kuacha nyuma wananchi wakihoji na kuikosoa sana hotuba yake.
Mfano wa karibu sana ni pale Rais alipowahutubia wazee wa Dar es Salaam na kutumia maneno ambayo hayakustahili kutumiwa na mkuu wa nchi ikiwa ni pamoja na kutumia sehemu kubwa ya hotuba yake kumshambulia mwananchi mmoja aliyeitwa Nicolaus Mgaya.
 
CCM yamtimua mwenyekiti Wazazi Hai


Na Heckton Chuwa, Moshi

HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kilimanjaro, imemfukuza uanachama wa CCM, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya
chama hicho Wilayani Hai, Bw. James Mushi.

Akielezea sababu ya uamuzi huo jana mjini Moshi, Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Stephen Kazidi, alisema uamuzi huo umetokana na Bw. Mushi kutokuwa muadilifu ndani ya chama na kupungukiwa sifa za kimaadili.

"Uamuzi huu umechukuliwa kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya mwaka 1977 Toleo la mwaka 2010, kwenye kifungu cha 93, kifungu kidogo cha 14," alisema.

Akinukuu kifungu hicho cha 14, Bw. Kazidi alisema Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa ina wajibu wa kumwachisha au kumfukuza uanachama mwanachama yeyote endapo itaridhika kwamba tabia yake na mwenendo wake vinamuondolea sifa za uanachama.

"Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa imeridhika kuwa Ndugu James Mushi, tabia yake na mwenendo wake vimemuondolea sifa ya kuwa mwanachama wa CCM," alisema.

Alisema kutokana na uwezo wake wa kikatiba, halmashauri hiyo imemfukuza uanachama Bw. Mushi kuanzia Februari 28, mwaka huu.

Uamuzi huo umekuja miezi kadhaa baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 kumalizika ambapo CCM ilipoteza majimbo kadhaa mkoani humo likiwemo jimbo la Hai ambapo kumekuwa na madai kuwa baadhi ya wanachama wa CCM wamekuwa mamluki jambo lililopelekea kushindwa kwa chama hicho tawala.

Akizungumza na Majira mjini hapa jana, Bw. Mushi alisema hakuwa amepata barua yoyote kutoka ya CCM ikimtaarifu maamuzi hayo, hivyo asingeweza kusema chochote kuhusiana na uamuzi huo.
 
Uzito wa wanasiasa utapimwa kwa hoja
ban.nasema.jpg

Christopher Nyenyembe

amka2.gif
WAKATI wa kutafuta maoni ya wananchi juu ya nchi kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa, watu wachache sana ndio waliokuwa wakiunga mkono mfumo huo ambao kwa mtazamo wa wengi walionekana kuwa wasaliti na hawakupaswa kuwepo.
Kuanzishwa kwa mfumo huo mwaka 1992 licha ya asilimia 20 ya Watanzania kuonyesha wazi dhamira ya kuwepo kwake, asilimia 80 walipinga, wakiogopa na pengine walizuiwa na vitisho vilivyokuwa vikitajwa wakati huo.
Kitendo cha Watanzania wachache kuunga mkono mfumo huo na kuridhiwa moja kwa moja na Rais mstaafu wa Serikali ya awamu ya pili,Ali Hassan Mwinyi ndiko kulikofungua rasmi milango ya demokrasia na uhuru wa wananchi kuchagua viongozi wanaowataka.
Licha ya kukubaliwa na idadi ndogo ya watanzania,kikubwa ninachokiona hapa leo hakukuwa na elimu ya kutosha iliyolenga kuwaamsha wananchi wote bali wachache waliokuwa jasiri ndio waliojitokeza kuwa viongozi wa upinzani.
Hoja za wananchi wachache na viongozi wao walioamua kujiingiza kwenye vyama vya upinzani hawakuwa na lengo la kuleta machafuko ama vurugu au vita kama walivyokuwa wakichochewa na baadhi ya wanasiasa waliobaki kwenye chama tawala.
Turufu ya wanasiasa wa kambi ya upinzani ilianza kuonekana kwa mara ya kwanza mwaka 1995 wakati wa uchaguzi mkuu wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi vya siasa,duru ya wakati huo ilimuegemea zaidi, Augustino Lyatonga Mrema aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani aliyeamua kujitoa CCM na kujiunga NCCR-Mageuzi.
Kwa wale wanaokumbuka vizuri na hawa wanaopaswa kupewa historia jinsi ilivyokuwa, kama Mwalimu Julius Kambarage Nyerere asingekuwepo leo hii tungekuwa tunazungumzia historia ya Mrema kuwa alikuwa miongoni mwa watanzania waliokaribia kuinusa Ikulu au kuingia kabisa.
Wananchi mwaka huo waliamka kwa kasi, walihitaji mabadiliko ya amani na hapo ndipo walipoanza kuonyesha fikra zao za kukichoka chama tawala kwa kuwa katika muda wote hawajaona unafuu mkubwa wa maisha ya dhiki na tabu ambayo mzigo wake ulipaswa kutuliwa na viongozi waasisi wa nchi hii.
Kilichompa umaarufu Mrema wakati huo kulitokana na hoja zake, ujasiri wa kutatua matatizo ya wananchi na kuwabana watendaji jeuri na wafanyabiashara ambao walikuwa wakiwanyanyasa wananchi,huyo alikuwa Mrema wa wakati huo sio wa sasa.
Naweza kusema kuwa moto uliowashwa na wananchi mwaka 1995 ulisababisha chama tawala kitikisike na hapo ndipo kilipoweza kujipanga zaidi bila utani kazi kubwa ilifanywa na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa ya kuwarudishia imani wananchi na kuujenga upya uchumi ulioyumba.
Kwa hakika hakuna mwananchi aliyeonja utamu wa uongozi wa Mkapa ambaye hawezi kuwa na fadhila na kuonyesha kukubali uwezo mkubwa wa kiuongozi aliokuwa nao kiongozi huyo ambaye hakupenda mzaha,alikuwa na hoja zilizokuwa zikitekeleza kile alichodhamiria kifanywe.
Kama binadamu, Mkapa aliweza kuisimamisha shilingi ya Tanzania kwa miaka 10 aliyokuwa madarakani,mfumuko wa bei ulisimama na kwa upande mwingine unafuu wa maisha uliweza kuonekana kwa thamani ya fedha iliyokuwa ikipatikana,alikuwa kiongozi wa hoja na msimamo.
Kila tunapopiga hatua fulani tunapaswa kukumbuka kule tuliko toka na hiyo inaweza kuwa njia pekee ya kukionyesha kizazi hiki cha leo kuwa adha ya maisha wanayoiona leo pengine imebadilika kutokana na viongozi waliopo ambao hoja zao haziwaamshi wananchi.
Kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya uongozi ndani ya chama tawala na kukua kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa ndiko kunakoendelea kuwaamsha wananchi waliokuwa wamelala wakati serikali ikitafuta maoni ya kuwepo kwa mfumo vyama vingi vya siasa.
Inawezekana kabisa kuwa lile jedwali la mahesabu ya maoni limegeuka na grafu inazidi kuonekana tofauti kwa kuonyesha dhahiri kuwa watanzania zaidi ya asilimia 80 sasa wanaunga mkono mfumo wa vyama vingi vya siasa kwa hamu na utashi mkubwa na sasa wanahitaji mabadiliko.
Mabadiliko hayo yanakuja kwa kasi kutokana na hoja za viongozi wa kambi za upinzani,wenye lengo na dhamira ya kweli ya kuwaambia wananchi, mchwa unaowatafuna na kuifanya nchi isiendelee na hapo ndipo ambapo dhana ya utawala bora na uwajibikaji inapoweza kuibuliwa upya.
Mlolongo wa matukio ya kisiasa na vikwazo vinavyofanywa na vyombo vya dola kutaka kufifisha au kuzima moto walionao wananchi wa kupigania haki zao na maslahi bora katika maisha yao hauwezi kuzimwa kwa risasi za moto au mabomu ya machozi na maji ya kuwasha,wakati ukifika hakuna kinachoweza kuzima nguvu ya umma.
Viongozi wasiokuwa na hoja zinazotokelezeka ndio wanaozidi kuwachefua wananchi na hii kasi ya viongozi wa kambi ya upinzani,wakiongozwa na Chama Kikuu cha Upinzani (CHADEMA) hakupaswi kubezwa kwa kuwa maendeleo ya nchi au ukombozi wake utaletwa na watu wachache wenye moyo na uchungu wa nchi yao.
Hoja za msingi zinazolenga kutatua kero za wananchi ndizo zinazopaswa kusikilizwa sasa hivi,wananchi hawategemei kuchezewa tena,kudanganywa, kunyonywa na kunyanyaswa na viongozi walioamua kujitajirisha wenyewe bila kuwaonea huruma watu wanyonge na masikini wa kutupwa.
Naamini kabisa kuwa takwimu za maoni ya wananchi zimebadilika tofauti na zile za miaka ya 90, wananchi wamechoka na hoja zisizowajenga,wamechoka kusikia siasa za udanganyifu na siasa zisizoleta ukombozi wa maisha yao, wanataka kuona nchi ina kwenda na uchumi wake unakua kwa kasi.
Naweza kusema kuwa mfumo wa vyama vingi vya siasa umewafumbua macho wananchi,umewafanya wawe na uwezo wa kujadili mambo yao ndani ya vyama vyao ili kuchochea msukumo wa kimageuzi na maendeleo ya nchi, watu sasa hawataki kulala wanadai haki zao za msingi wanazostahili kupata.
Wananchi wanapaswa kukiri wazi kuwa moto uliowashwa na viongozi waandamizi wa CHADEMA wa kupinga kuilipa Dowans, kupinga ongezeko la gharama za umeme na kutaka mafisadi wote washughulikiwe na serikali iliyopo madarakani, wamekuja na hoja nzito zinazopaswa kufanyiwa kazi na mamlaka husika.
Kuna mambo ambayo serikali iliyopo madarakani inaweza kupuuza na kuacha kuwadhihaki viongozi wa upinzani kuwa wanataka kujijengea umaarufu lakini katika suala la gharama za umeme, kuilipa Dowans na kuwashughulikia mafisadi huko hakuhitaji umaarufu isipokuwa serikali inapaswa kukubali kuwa imebanwa kwa hoja.
Wananchi ndio watakaoweza kupima ni upande upi unaohitaji umaarufu ni Serikali iliyopo madarakani au ni chama chenye nguvu cha upinzani kilichodhamiria kufichua maovu yote yanayofichwa na serikali iliyoshika dola,umma ndio wenye majibu na mizani ya kupima umaarufu huo.
Ni wazi kuwa wale wanaofanya kazi vizuri bila unafiki wowote watapata umaarufu bila hata kuuomba na wale wanaofanya kazi ya kuwalaghai wananchi na kuwapotezea dira ya maisha yao wataukosa umaarufu wanaouhitaji hata kama watatumia fedha za mafisadi kujikweza.
Kilicho mbele yetu hivi sasa ni kuambiana ukweli kuwa nchi ipo pabaya,uchumi wa nchi umeyumba,zaidi ya asilimi 90 ya watanzania hawajui uhakika wa maisha yao ya kila siku, wanataka kauli na hoja za msingi za kutatua matatizo yao hawawezi kuwajengea umaarufu viongozi waliowatenga.
Ili tuwe salama tunapaswa kujifunza kwa yale yanayotokea kwenye nchi za wenzetu,tusijione kuwa tumesimama kumbe hatupo salama kila mwananchi anapaswa kufaidi keki ya Taifa, ndio maana nawaomba sana, Acha Niseme kuwa sasa tunataka hoja za kutatua matatizo.
 
Mdee ataka vigogo wa CCM wapuuzwe


Na Suleimani Abeid, Shinyanga

MBUNGE wa Jimbo la Kawe, Bi. Halima Mdee aliwataka wananchi kukinga mkono Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kupuuza
kauli zinazotolewa na viongozi wa CCM na wale wa serikali yake kuhusu kufanyika kwa maandamano na mikutano ya chama hicho .

Akizungumza katika mkutano uliofanyika jana mjini Mwanhuzi wilayani Meatu mara baada ya maandamano makubwa yaliyofanyika katika mji huo, Bi. Mdee alisema maneno mengi yanayotolewa na vigogo wa CCM kama husani hotuba ya Rais Jakaya Kikwete yamelenga kutaka kuwatia hofu isiyo na sababu Watanzania ili vigogo hao waendelee kufaidi matunda ya nchi hii peke yao.

Alisema hivi sasa Watanzania wanakabiliwa na matatizo chungu nzima ikiwemo ukosefu wa nishati ya umeme lakini serikali ya CCM imeshindwa kuwatatulia matatizo hayo, lakini CHADEMA tunaieleza serikali ya Kikwete kuwa kizazi hiki cha leo siyo kile cha jana, ni kizazi cha ‘digital' na siyo cha ‘analogy' kilichopitwa na wakati.

"Tunawaeleza CCM na Kikwete kama hawataki kuona maandamano na mikutano hii ya hadhara, basi wawasikilize wananchi na watekeleze ahadi walizozitoa kwa wananchi wakati wa kipindi cha kampeni, vinginevyo watarajie mabadiliko makubwa wakati wowote, wakati wa vitisho haupo tena.

"Si kweli kwamba CHADEMA tunafanya vurugu au kuchochea wananchi bali hali hiyo inasababishwa na serikali ya CCM yenyewe kutokana na kuwasababishia wananchi hali ngumu ya maisha na wananchi hao sasa wameamua kuiunga mkono ili kuelekea kwenye mabadiliko," alisema.

Bi. Mdee alisema huko nyuma Watanzania walisoma bure kwa kutumia raslimali chache zilizokuwepo, lakini mara baada ya kuanza kuwa ufisadi elimu imekuwa ni mzigo kwa Watanzania na hata huduma za afya zimekuwa ni za matatizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Habari wa CHADEMA Taifa, Bw. Erasto Tumbo aliwaomba Watanzania kuiunga mkono CHADEMA ili kuleta mabadiliko ya kweli hapa nchini na kwamba serikali ya CCM imekuwa ikiwajaza hofu ili waogope na iendelee kutawala nchini huko wanaotawaliwa wakihangaika kwa maisha magumu.

Aidha kwa upande mwingine aliwaomba wanaume wote kuwazuia wake zao pale wanapotaka kwenda hospitali kujifungua wasijaribu kupata Bajaj zilizoahidiwa na Rais Kikwete ambazo alidai kuwa atazileta nchini zifanye kazi ya kuwapeleka hospitali akina mama wajawazito.

"Ndugu zangu Bajaj zilizoahidiwa na Kikwete, ni hatari kwa akina mama wajawazito, pamoja na kwamba Kikwete hajatekeleza ahadi yake ya kuzileta hapa nchini, lakini nakushaurini msiwaruhusu wake zenu kubebwa na Bajaj hizo kwani ni hatari kwa maisha ya mama mjamzito,"

"Kwa kawaida Bajaj inapokuwa barabarani huwa inaruka ruka sana , sasa nielezeni kweli hapa Kikwete alitumia busara kusema ataingiza nchini Bajaj 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito, si wote watakuwa wanafia njiani kabla ya kufikishwa hospitali kujifungua, nakuombeni hata kama atazileta, wakatazeni wake zenu wasizipande," alieleza Bw. Tumbo.

 
Mbowe amjibu Rais Kikwete Send to a friend Tuesday, 01 March 2011 21:32 0diggsdigg

f.mboye.jpg
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe

Waandishi Wetu
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kusema Chadema kinataka kuleta machafuko kwa kudai mambo yasiyoweza kutekelezeka, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amemtaka apishe Ikulu ili kitekeleze madai hayo.

Akilihutubia taifa juzi, pamoja na mambo mengine, Rais Kikwete alisema: "Ni kweli kuna hali ngumu ya maisha na kukabiliana nayo ndiyo kazi tunayoendelea kufanya kila siku. "Tumeelekeza nguvu zetu na rasilimali zetu huko na mafanikio yanaonekana katika nyanja mbalimbali na maeneo mbalimbali. Hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa."

Rais Kikwete alifafanua kuwa kikwazo siyo upungufu wa sera wala dhamira, bali ni kiwango cha maendeleo madogo ya uchumi wa nchi na hivyo uwezo siyo mkubwa wa kuyakabili na kuyamaliza matatizo yote haraka kama ambavyo ingepaswa iwe.

Kikwete akirejea zama mbali za viongozi mbalimbali tangu uhuru, alisema hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliongoza kwa miaka 23 na hakuyamaliza matatizo ya maendeleo ya nchi hii.

"Wale wa umri wangu au kunizidi wanakumbuka hali ilivyokuwa wakati anang'atuka. Hakuacha nchi ikiwa tajiri. Mzee Mwinyi kakaa miaka 10 hakuyamaliza, Mzee Mkapa naye kakaa miaka 10 hakuyamaliza. Mie nimekaa miaka mitano hayakwisha na nitamaliza mitano hayataisha yote," alisema.

Hata hivyo, akiwahutubia wakazi wa Miji ya Isaka, Kahama na Bukombe jana, Mbowe alisema "Kama siku tisa hazimtoshi kutekeleza hayo, aipishe Chadema ifanye kwani inaamini inawezekana."

Akiwa wilayani Kahama, msafara wake ulikuwa ukisimamishwa mara kwa mara na umati wa watu waliokuwa wamejipanga kando ya barabara wakimshinikizwa azungumze nao. Katika Mji wa Isaka, alisimamishwa na wafuasi wa chama ambao walisukuma gari lake huku wakimtaka azungumze nao.

"Rais Kikwete anasema kuwa njia ya kubadilisha uongozi ni uchaguzi na kuwasilisha matatizo ni bungeni, hatuendi huko. Tukisema bungeni wanatuzomea kwa vile wao wako 300, tukifanya uchaguzi wanachakachua kura zetu sasa na sisi tukiwa nje tuko milioni, tumepita mikoa mitatu sasa analalamika," alisema Mbowe.

Aliwataka wananchi kusimama na kudai haki kwa vile serikali ya CCM imezoea kutenda hivyo kutokana na wananchi kuwa wapole na kutoa mfano kuwa katika malalamiko yao ya siku tatu, tayari serikali imeanza kujadili namna ya kushusha bei ya sukari.

Naye mbunge wa Musoma Mjini (Chadema), Vincent Nyerere akizungumza mjini Kahama alisema kuwa wananchi wanapaswa kufikiria zaidi na kuunga mkono jitihada za chama chake kutokana na kuwa na sera za kuwasaidia.

Alisema ikiwa serikali ya sasa inashindwa kutumia rasilimali watu, chama chake kinampango wa kuangalia namna ambavyo kinaweza kuwatumia wafungwa wenye taaluma mbalimbali kusaidia matatizo mbalimbali kama nchi nyingine badala ya kuwafungia gerezani huku wakipasua kuni na mawe.

Katika hatua nyingine, wasomi na wanasiasa wameiponda hotuba ya Rais Kikwete wakisema haina jipya. Baadhi yao wamekitetea Chadema na kupinga kauli ya Rais kwamba chama hicho kina lengo la kuleta machafuko.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana wasomi hao walisema pamoja na uzuri wa hotuba yake, Rais Kikwete amekosea kitu kimoja, kuishambulia Chadema.

Mwasisi wa Chadema Edwin Mtei alisema madai ya Rais Kikwete dhidi ya Chadema hayana ukweli kwani lengo la maandamano yake siyo kuiondoa serikali iliyopo madarakani, bali kufikisha ujumbe wa kudai haki.

"Ah! Nimemsikia jana anasema kuwa sisi tunataka kuleta machafuko. Hakuna, hawana jipya sisi lengo letu ni kuwaeleza wananchi kuhusu ufisadi uliopo ndani ya serikali ya CCM na tutaendelea kuandamana hadi kieleweke," alisema Mtei

Alisema serikali ya CCM imeshindwa kuondoa hali ya umaskini kwa Watanzania, badala yake viongozi wa chama hicho wamekuwa wakijilimbikizia mali kwa ukwasi na alisisitiza kuwa Chadema kitaendelea kupigana kufa na kupona na kupaza sauti zao kwa kueleza shida za Watanzania.

Kwa upande wake, Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), limepongeza mikakati ya serikali kukabiliana na ugumu wa maisha lakini likaonya kuwa kama gharama za uzalishaji hazitapungua, hali inaweza kuwa mbaya zaidi.

Mtendaji Mkuu wa CTI, Christina Kilindu akizungumza ofisini kwake Dar es Salaam jana alisema jambo la kwanza ni kukabiliana na tatizo la nishati ya umeme.

''Kwa kweli, mfumuko wa bei ni tatizo kubwa linaloumiza kichwa. Chanzo ni ongezeko la gharama za uzalishaji na gharama za uzalishaji hazitashuka kuondoa mfumuko wa bei itakuwa ngumu,'' alisisitiza Kilindu.

Alifafanua kwamba gharama za kufanya biashara nchini zimekuwa zikipanda huku akitoa mfano wa mwajiri kupaswa kulipa asilimia sita tofauti na nchi kama Kenya na Uganda ambako ni kati ya asilimia moja hadi mbili.

"Asilimia sita ni nyingi, asilimia mbili kulipwa kwa ajili ya Elimu ya Ufundi kwa VETA sawa lakini hizi asilimia nne zinazoingia Hazina zingepaswa kuondolewa," aliaema na kuongeza:

"Zamani kiasi hicho cha asilimia nne kilikuwa kikiingia kama 'housing levy' lakini sasa hivi hakuna benki ya nyumba hizo asilimia nne zinakwenda wapi?"

Akizungumzia umeme, alisema kama mali zilizopo hazitatumika kwa sasa hali itakuwa mbaya zaidi kwani uzalishaji utakuwa mgumu kwa kutumia majenereta, ambayo hutumia mafuta.

''Sasa hivi pipa tunasikia limefikia dola 120 lakini kama ghasia katika nchi za Kiarabu zitaendelea, kuna hatari likafikia hatua ya juu kabisa ya dola 200. Libya sasa hivi mambo siyo mazuri."

Licha ya kuonyesha matumaini juu ta mipango ya Serikali, alisema kupanda kwa mafuta pia kutaongeza gharama za usafirishaji mazao kutoka mashambani na huduma za usafiri.

Alisema ni vyema serikali ikatumia rasilimali za ndani kumaliza tatizo la umeme nchini ikiwa ni pamoja na kufanya uamuzi mgumu wa kuzalisha umeme katika mradi mkubwa wa Stiglers, ambao utaifanya nchi kuuza ziada nje.

Akirejea ahadi ya Rais Kikwete alipohutubia Bunge na kuahidi kuendeleza mradi huo aliwapa matumaini wawekezaji wakiwemo wao wenye viwanda,
Kilindu alisema msimamo huo wa kutaka uzalishaji katika eneo hilo pia umewasilishwa na CTI mbele ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.

''Mgawo wa umeme tangu mwaka 1992 hauishi, huwezi kuzungumzia uchumi kama huzungumzii umeme. Sasa hivi tumesema kila kinachoweza kuzalisha umeme nchini kizalishe na tuweke kando siasa,'' alisema.

Chama cha APPT-Maendeleo kimeitetea Chadema kikieleza kuwa yote yanayozungumzwa na chama hicho ni mambo ambayo yapo na yanayomgusa Mtanzania.

Mwenyekiti wa chama hicho, Peter Mziray alisema jana kuwa anachotakiwa kufanya Rais Kikwete kwa sasa ni kutekeleza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni na zile za kiporo kabla ya mwaka jana kwa kuwa wananchi wanataka kuona maendeleo.

Alisema licha ya mkuu huyo wa nchi kumaliza siku 100 katika ngwe yake ya pili, hakuna cha maana kinachoendelea bali kumekuwa na shida kila mahali.

"Mimi sioni kama Chadema wana kosa, mfano wamezungumzia suala la mgawo wa umeme ambao umedumu kwa zaidi ya miaka saba sasa hapa wana kosa gani wakati suala hili linamgusa kila Mtanzania? Sasa kama anawaambia watu wasikifuate Chadema wafuate nini, wafuate CCM ambayo inakufa? Alisema Mziray.

Mziray alimshauri Rais Kikwete kuwa makini na kwamba asiendelee kufanya kazi za kila siku pekee, bali aangalie jinsi gani watu wanaweza wakamsaidia kutatua matatizo mbalimbali yanayolikabili taifa.

Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila alisema hotuba ya Rais Kikwete imeshindwa kutoa majibu kwa maswali mengi ambayo wananchi wamekuwa wakijiuliza... "Cha kushangaza Rais Kikwete anazungumzia kutenga asilimia 10 ya bajeti ambayo ilizungumzwa miaka ya nyuma, tunakwenda wapi?"

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally aliipongeza hotoba ya Rais akisema imebashiri kuwa Tanzania ina tatizo la msingi lakini akaikosoa kuwa haikujielekeza kwenye tatizo la msingi ambalo ndiyo chanzo cha kutoweka kwa amani.

Alisema tatizo walilonalo Watanzania kwa sasa ambalo linafanya hali kuwa tete nchini ni mfumo mbovu wa uchumi na siasa.

"Maandamano ya Chadema hayawezi kuwa chanzo cha kutoweka kwa amani hapa nchini, nilitarajia Rais angezungumzia mfumo mzima wa uchumi na siasa ambayo ni mbovu na imeshindwa kuwasaidia wananchi wake," alisema Bashiru.

Alisema mfumo wa uchumi na siasa ni mbovu na kwamba hali hiyo ndiyo inayoonyesha viashiria vya kutoweka kwa hali ya amani hapa nchini.

"Yapo matatizo mengi ambayo ni viasharia vya kutoweka kwa amani, kitendo cha polisi kupigana na wafanyabishara katika eneo la Darajani Visiwani Zanzibar, migogoro ya ardhi baina ya wanachi na wawekezaji, vijana kukosa ajira na wengine kukosa elimu, hivyo ndivyo viasharia vya kutoweka kwa amani," alisema.

Bashiru alisema Rais Kikwete hakustahili kuzungumzia maandamano badala yake angejikita katika mambo ya msingi likiwamo suala la kuporomoka kwa elimu, ukosefu wa ajira na tatizo la ugumu wa maisha linalowakabili wananchi kwa sasa.

"Kuna wananchi wengi wamekata tamaa, watu hawa hawana muda wa kusikiliza hutoba ya Rais wala kwenda kwenye maandamano ya Chadema wao wanazungumzia ugumu wa maisha, hali hii inatutaka kuchukua hatua ya kutafakari na kuufanyia kazi mfumo wetu wa uchumi," alisema.

Alisema ili kutatua tatizo hilo, juhudi za makusudi zinafaa kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kutafakari kwa kina ili kuhakikisha mfumo wa uchumi na ule wa kisiasa unaboreshwa na kwenda sambamba na mahitaji ya wananchi.

Bashiru alisema huu si wakati wa malumbano ya kisiasa na baina ya vyama kwa kuwa hayatalisaidia taifa, bali kinachopaswa kufanywa ni kwa wadau kushughulikia tatizo la msingi ambalo ni mfumo uliopo sasa.

Mkazi wa Tabata, Mndame Mchande alisema anakubaliana na kinachofanywa na Chadema na kwamba hatua inayofanywa na chama hicho ndiyo inayotakiwa kwa kuwa hata wabunge wake wakipeleka hoja bungeni hupingwa.

"Wanachofanya ni sawa…. hao wanaolalamika juu ya Chadema hawawezi kufanya kitu kama hicho, wao wanachokijua ni kung'ang'ania madaraka tu," alisema Mchande.

Alisema wanaopiga makelele dhidi ya Chadema ni kama wanataka kuidanganya jamii akisema chama hicho kinatekeleza yale kilichoahidi ikiwa ni pamoja na kuwatetea wananchi maskini.

Mfanyabiashara kutoka Mafinga, Victory Kipanguala alisema kwamba alitegemea Rais Kikwete angejadili tatizo la umeme na namna ya kumaliza mgawo na lakini akasema kitendo chake cha kusema kwamba bidhaa zitapungua bei wakati viwanda vinatumia umeme wa bei kubwa zaidi ni kuidanganya jamii.

Alisema kitendo cha kuijadili Chadema na kuacha mambo ya msingi ndiyo sababu ya yeye kuiona hotuba ya Rais haina lolote.

Mfanyabiashara mwingine kutoka Iringa, Godson Sanga alisema alitegemea Rais Kikwete angefafanua sakata la Kampuni ya kufua umeme ya Dowans.

"Kuna mchakato wa kuilipa kampuni hii ya Dowans, mimi nilifikiri Rais angezungumzia msimamo wa serikali kuhusu ulipaji wa kampuni hii, lakini amezungumzia mambo mengine kabisa ambayo hayana tija kwa Watanzania," alisema Sanga.

Habari hii imeandaliwa na Moses Mashalla, Arusha; Frederick Katulanda, Mwanza; Ramadhan Semtawa, Nora Damian Fidelis Butahe, Geofrey Nyang'oro na Raymond Kaminyonge, Dar es Salaam.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Last Updated on Wednesday, 02 March 2011 08:23 Comments




0 #13 mwl marwa ryoba 2011-03-02 08:34 mi binafsi nichukue fursa hii kumpongeza mshikaji kwa kutambua kwamba maisha ni magumu kwa sasa na hata swahiba wake wa karibu(Richmond uli) amelitambua hilo baada ya kuwaita waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa ataishauri serikali kuongeza mishahara ya watumishi wa umma maana mfumuko wa bei uko juu sana.lakini haya wameyatambua baada ya Chadema kuandamana kwa amani bila kufanya fujo kama wenzao wa ccm .naomba nimkosoe jk kwamba tz hatutapiga hatua za kimaendeleo n kuondoa umasikini wa watz kama mambo yafuatayo hayapo
*UMEME THABITI
*VIWANDA ANGALAU VIWILI VIDOGO(SIDO WAWEZESHWE KUFANFA HII KAZI MAANA UWEZO WANAO,MABILION YA KIKWETE YATUMIKE NA ZILE ZA DOWANS &EPA)
*WAKULIMA WAZAWA WAWEZESHWE KUANZISHA KILIMO CHA KISASA(KILIMO CHA JEMBE LA MKONO NA KUTEGEMEA MVUA KIKOMESHWE HARAKA)
*WAFUGAJI WAPEWE MAENEO YAO MAALUMU KWA KAZI HIYO BILA HIVYO MIFUGO ITAISHA
*KILA JIMBO LIWE NA CHANZO KIKUBWA CHA KUVUNA MAJI YA MVUA(BWAWA)
Haya ni baadhi tu ya mambo yatakayo tusaidia vingenevyo kikwete asiilaumu chadema bali ajilaumu yeye na ccm yake kwa kuchukua cho mapema kwa kutokuwa waaminifu kama muasisi wa chama hicho alivyo kuwa.

Quote









0 #12 koku 2011-03-02 08:33 NI KWELI WACHANGIA MADA HUU NI UDINI NA UKABILA KWENDA MBELE, WATANZANIA WENZANGU TUSIDANGANYIKE KWA KUSHABIKIA VYAMA KWA AJILI YA UKABILA NA UDINI, MIMI NI MKRISTO LAKINI NACHUKIA KUONA UDINI TUMEUWEKA MBELE SISI WANANCHI WENYEWE NDIYO TUTAKUWA WAATHIRA WAKUIKIMBIA NCHI YETU WENYEWE.

ENYI WAANDISHI WA MWANANCHI MLIO NA ELIMU NDOGO YA UANDISHI ACHENI KUSHABIKIA CHAMA NA UDINI MTATUARIBIA NCHI YETU KAMA MLIVYOFANYA KWENU KENYA.

Quote









-1 #11 Mwanaweja 2011-03-02 08:29 mbowe pamoja na wasomi wezetu mmenena wala haikuhitaji kuelezea CDM bali ni kutenda katika mapungufu yaliyopo. maana naamini kama safu ya rais ingekuwa inawajibika vizuri hata CDM ninaimani wasingeweza kufanya maandamano lakini kwa kuwa jk na wabunge wa ccm hawana kinachofanyika cha maana bali ni usanii,kubeza, kuzomea na kutokufikiria kama hizi ni point tuzifanyie kazi. hata kama za upinzani lakini kwa kuwa zinamanufaa kwa taifa basi wa zitumie. Nje ya hapo jk aelewe tz mpaka kijijini hawandanganyiki maana ugumu wa maisha wanapatwa kwa kila level ya maisha na kila nyanja .
Quote









0 #10 Asante Mungu 2011-03-02 07:51 Kweli Nimeamini kuwa kuna baadhi ya watu kufikiria kwao ni shida. Suala la maandamano ya Chadema sio kampeni bali ni dhamira ya dhati ya kuitaka serikali ichangamke katika kuwahudhumia wananchi wake. Chadema ni chama cha demokrasia na maendeleo kama unajua hilo ni dhahiri kuwa utaona wanachokifanya kinaenda sawa na jina lao. Viongozi wanaojali na kujikita katika kutenda haki ni viongozi wanaostahili kuiongoza nchi hii na sio wengine ila ni chadema pekee.Kauli ya JK imekosa utashi na inastahili kupuuzwa na viongozi wetu wanaoijali nchi yao.
Quote









0 #9 Jeremiah 2011-03-02 07:45 Rais Kikwete anasema kuwa njia ya kubadilisha uongozi ni uchaguzi na kuwasilisha matatizo ni bungeni, hatuendi huko. Tukisema bungeni wanatuzomea kwa vile wao wako 300, tukifanya uchaguzi wanachakachua kura zetu sasa na sisi tukiwa nje tuko milioni, tumepita mikoa mitatu sasa analalamika,"
Huu ni Ukweli dhabiti. Jukwaa la nje ya Bunge ni fursa muhimu na adhimu.
Quote . GOOD POINT.

Quote









-1 #8 Gudu Maganga 2011-03-02 07:19 Ukisoma maoni unaweza kubashiri dini ya mtu, hasa wenzetu ambao kwao JK ni safi.
Quote









+2 #7 CHACHA 2011-03-02 07:10 Ina maana katika mambo yote kikwete hakuona kwamba kufeli watoto wa form four ni janga la kitaifa?

Au ndo lengo la shule za kata kufelisha watu,...maana kakaa kimya tu badala yake anaongelea chadema!

Hivi unadhani hao 89% walofeli wanaenda wapi na wanafanya nini saivi kama sio kwenda kwenye mikutano ya chadema kutafuta tumaini la maisha ya uhakika?

Quote









0 #6 CHACHA 2011-03-02 07:06 Quoting PEPE S:
HAPA MWANDISHI UMEEGEMEA UPANDE MMOJA.

MAKALA HII HAIKO BALANCED. SI KWELI KWAMBA HATUA ZA CHADEMA HAZIPINGWI NA WENGI.

ULICHoFANYA NI KUANDIKA MAONI YA WANAO IUNGA MKONO HATUA YA CHADEMA NA KUYAWEKA KAPUNI YA WANAOIPINGA HATUA YA CHADEMA


Hahahaha,utalia tu!
Huo ndo ukweli wenyewe kama kahoji kila mtu anapingana na raisi wako unategemea aandike nini?
Pole sana,hata hivo kama unataka wanao mpongeza kikwete kawasome kwenye gazeti la uhuru wapo kibao sio kwenye magazeti huru kama haya

Quote









-1 #5 EC 2011-03-02 07:05 "Rais Kikwete anasema kuwa njia ya kubadilisha uongozi ni uchaguzi na kuwasilisha matatizo ni bungeni, hatuendi huko. Tukisema bungeni wanatuzomea kwa vile wao wako 300, tukifanya uchaguzi wanachakachua kura zetu sasa na sisi tukiwa nje tuko milioni, tumepita mikoa mitatu sasa analalamika,"
Huu ni Ukweli dhabiti. Jukwaa la nje ya Bunge ni fursa muhimu na adhimu.

Quote









0 #4 Salma 2011-03-02 07:01 Wewe Pepe sijui Januari Makamba na dada yako dadia au Mary Chatanda acheni hizo. CHADEMA ni chama kinachokubalika nchi nzima mpende msipende. Tumekuja kuwashika. Na mimi kwa taarifa yako sio mwanachama wa chama chochote nchini.
Quote









-1 #3 Kruger 2011-03-02 06:32 Kiukweli unazi hausadii bali kazi ifanyike kwa ajili ya kutekeleza Ilani za Uchaguzi.Kama mwenye dhamana ukiona hali yaenda mrama, si kuanza kulumbana bali ni kufanya kazi inayoonekana wananchi waione
Quote









-5 #2 dadia d 2011-03-02 05:33 CHADEMA kampeni za urais, ubunge, na udiwani za mwaka 2010 zimeisha. Za mwaka 2015 hazijaanza

Mbona wenzenu wanajua kua kampeni za 2015 hazijaanza?

kwanini nyie muanze kampeni za 2015 sasa kwa kisingizio kua mnachofanya ni kufikisha ujumbe kwa wananchi?

Quote









-5 #1 PEPE S 2011-03-02 05:27 HAPA MWANDISHI UMEEGEMEA UPANDE MMOJA.

MAKALA HII HAIKO BALANCED. SI KWELI KWAMBA HATUA ZA CHADEMA HAZIPINGWI NA WENGI.

ULICHoFANYA NI KUANDIKA MAONI YA WANAO IUNGA MKONO HATUA YA CHADEMA NA KUYAWEKA KAPUNI YA WANAOIPINGA HATUA YA CHADEMA

Quote

 
Mbowe amjibu Rais Kikwete Tuesday, 01 March 2011 21:32

f.mboye.jpg
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe

Waandishi Wetu
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kusema Chadema kinataka kuleta machafuko kwa kudai mambo yasiyoweza kutekelezeka, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amemtaka apishe Ikulu ili kitekeleze madai hayo.

Akilihutubia taifa juzi, pamoja na mambo mengine, Rais Kikwete alisema: "Ni kweli kuna hali ngumu ya maisha na kukabiliana nayo ndiyo kazi tunayoendelea kufanya kila siku. "Tumeelekeza nguvu zetu na rasilimali zetu huko na mafanikio yanaonekana katika nyanja mbalimbali na maeneo mbalimbali. Hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa."

Rais Kikwete alifafanua kuwa kikwazo siyo upungufu wa sera wala dhamira, bali ni kiwango cha maendeleo madogo ya uchumi wa nchi na hivyo uwezo siyo mkubwa wa kuyakabili na kuyamaliza matatizo yote haraka kama ambavyo ingepaswa iwe.

Kikwete akirejea zama mbali za viongozi mbalimbali tangu uhuru, alisema hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliongoza kwa miaka 23 na hakuyamaliza matatizo ya maendeleo ya nchi hii.

"Wale wa umri wangu au kunizidi wanakumbuka hali ilivyokuwa wakati anang’atuka. Hakuacha nchi ikiwa tajiri. Mzee Mwinyi kakaa miaka 10 hakuyamaliza, Mzee Mkapa naye kakaa miaka 10 hakuyamaliza. Mie nimekaa miaka mitano hayakwisha na nitamaliza mitano hayataisha yote," alisema.

Hata hivyo, akiwahutubia wakazi wa Miji ya Isaka, Kahama na Bukombe jana, Mbowe alisema "Kama siku tisa hazimtoshi kutekeleza hayo, aipishe Chadema ifanye kwani inaamini inawezekana."

Akiwa wilayani Kahama, msafara wake ulikuwa ukisimamishwa mara kwa mara na umati wa watu waliokuwa wamejipanga kando ya barabara wakimshinikizwa azungumze nao. Katika Mji wa Isaka, alisimamishwa na wafuasi wa chama ambao walisukuma gari lake huku wakimtaka azungumze nao.

“Rais Kikwete anasema kuwa njia ya kubadilisha uongozi ni uchaguzi na kuwasilisha matatizo ni bungeni, hatuendi huko. Tukisema bungeni wanatuzomea kwa vile wao wako 300, tukifanya uchaguzi wanachakachua kura zetu sasa na sisi tukiwa nje tuko milioni, tumepita mikoa mitatu sasa analalamika,” alisema Mbowe.

Aliwataka wananchi kusimama na kudai haki kwa vile serikali ya CCM imezoea kutenda hivyo kutokana na wananchi kuwa wapole na kutoa mfano kuwa katika malalamiko yao ya siku tatu, tayari serikali imeanza kujadili namna ya kushusha bei ya sukari.

Naye mbunge wa Musoma Mjini (Chadema), Vincent Nyerere akizungumza mjini Kahama alisema kuwa wananchi wanapaswa kufikiria zaidi na kuunga mkono jitihada za chama chake kutokana na kuwa na sera za kuwasaidia.

Alisema ikiwa serikali ya sasa inashindwa kutumia rasilimali watu, chama chake kinampango wa kuangalia namna ambavyo kinaweza kuwatumia wafungwa wenye taaluma mbalimbali kusaidia matatizo mbalimbali kama nchi nyingine badala ya kuwafungia gerezani huku wakipasua kuni na mawe.

Katika hatua nyingine, wasomi na wanasiasa wameiponda hotuba ya Rais Kikwete wakisema haina jipya. Baadhi yao wamekitetea Chadema na kupinga kauli ya Rais kwamba chama hicho kina lengo la kuleta machafuko.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana wasomi hao walisema pamoja na uzuri wa hotuba yake, Rais Kikwete amekosea kitu kimoja, kuishambulia Chadema.

Mwasisi wa Chadema Edwin Mtei alisema madai ya Rais Kikwete dhidi ya Chadema hayana ukweli kwani lengo la maandamano yake siyo kuiondoa serikali iliyopo madarakani, bali kufikisha ujumbe wa kudai haki.

“Ah! Nimemsikia jana anasema kuwa sisi tunataka kuleta machafuko. Hakuna, hawana jipya sisi lengo letu ni kuwaeleza wananchi kuhusu ufisadi uliopo ndani ya serikali ya CCM na tutaendelea kuandamana hadi kieleweke,” alisema Mtei

Alisema serikali ya CCM imeshindwa kuondoa hali ya umaskini kwa Watanzania, badala yake viongozi wa chama hicho wamekuwa wakijilimbikizia mali kwa ukwasi na alisisitiza kuwa Chadema kitaendelea kupigana kufa na kupona na kupaza sauti zao kwa kueleza shida za Watanzania.

Kwa upande wake, Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), limepongeza mikakati ya serikali kukabiliana na ugumu wa maisha lakini likaonya kuwa kama gharama za uzalishaji hazitapungua, hali inaweza kuwa mbaya zaidi.

Mtendaji Mkuu wa CTI, Christina Kilindu akizungumza ofisini kwake Dar es Salaam jana alisema jambo la kwanza ni kukabiliana na tatizo la nishati ya umeme.

''Kwa kweli, mfumuko wa bei ni tatizo kubwa linaloumiza kichwa. Chanzo ni ongezeko la gharama za uzalishaji na gharama za uzalishaji hazitashuka kuondoa mfumuko wa bei itakuwa ngumu,'' alisisitiza Kilindu.

Alifafanua kwamba gharama za kufanya biashara nchini zimekuwa zikipanda huku akitoa mfano wa mwajiri kupaswa kulipa asilimia sita tofauti na nchi kama Kenya na Uganda ambako ni kati ya asilimia moja hadi mbili.

"Asilimia sita ni nyingi, asilimia mbili kulipwa kwa ajili ya Elimu ya Ufundi kwa VETA sawa lakini hizi asilimia nne zinazoingia Hazina zingepaswa kuondolewa," aliaema na kuongeza:

"Zamani kiasi hicho cha asilimia nne kilikuwa kikiingia kama 'housing levy' lakini sasa hivi hakuna benki ya nyumba hizo asilimia nne zinakwenda wapi?"

Akizungumzia umeme, alisema kama mali zilizopo hazitatumika kwa sasa hali itakuwa mbaya zaidi kwani uzalishaji utakuwa mgumu kwa kutumia majenereta, ambayo hutumia mafuta.

''Sasa hivi pipa tunasikia limefikia dola 120 lakini kama ghasia katika nchi za Kiarabu zitaendelea, kuna hatari likafikia hatua ya juu kabisa ya dola 200. Libya sasa hivi mambo siyo mazuri."

Licha ya kuonyesha matumaini juu ta mipango ya Serikali, alisema kupanda kwa mafuta pia kutaongeza gharama za usafirishaji mazao kutoka mashambani na huduma za usafiri.

Alisema ni vyema serikali ikatumia rasilimali za ndani kumaliza tatizo la umeme nchini ikiwa ni pamoja na kufanya uamuzi mgumu wa kuzalisha umeme katika mradi mkubwa wa Stiglers, ambao utaifanya nchi kuuza ziada nje.

Akirejea ahadi ya Rais Kikwete alipohutubia Bunge na kuahidi kuendeleza mradi huo aliwapa matumaini wawekezaji wakiwemo wao wenye viwanda,
Kilindu alisema msimamo huo wa kutaka uzalishaji katika eneo hilo pia umewasilishwa na CTI mbele ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.

''Mgawo wa umeme tangu mwaka 1992 hauishi, huwezi kuzungumzia uchumi kama huzungumzii umeme. Sasa hivi tumesema kila kinachoweza kuzalisha umeme nchini kizalishe na tuweke kando siasa,'' alisema.

Chama cha APPT-Maendeleo kimeitetea Chadema kikieleza kuwa yote yanayozungumzwa na chama hicho ni mambo ambayo yapo na yanayomgusa Mtanzania.

Mwenyekiti wa chama hicho, Peter Mziray alisema jana kuwa anachotakiwa kufanya Rais Kikwete kwa sasa ni kutekeleza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni na zile za kiporo kabla ya mwaka jana kwa kuwa wananchi wanataka kuona maendeleo.

Alisema licha ya mkuu huyo wa nchi kumaliza siku 100 katika ngwe yake ya pili, hakuna cha maana kinachoendelea bali kumekuwa na shida kila mahali.

“Mimi sioni kama Chadema wana kosa, mfano wamezungumzia suala la mgawo wa umeme ambao umedumu kwa zaidi ya miaka saba sasa hapa wana kosa gani wakati suala hili linamgusa kila Mtanzania? Sasa kama anawaambia watu wasikifuate Chadema wafuate nini, wafuate CCM ambayo inakufa? Alisema Mziray.

Mziray alimshauri Rais Kikwete kuwa makini na kwamba asiendelee kufanya kazi za kila siku pekee, bali aangalie jinsi gani watu wanaweza wakamsaidia kutatua matatizo mbalimbali yanayolikabili taifa.

Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila alisema hotuba ya Rais Kikwete imeshindwa kutoa majibu kwa maswali mengi ambayo wananchi wamekuwa wakijiuliza... “Cha kushangaza Rais Kikwete anazungumzia kutenga asilimia 10 ya bajeti ambayo ilizungumzwa miaka ya nyuma, tunakwenda wapi?”

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bashiru Ally aliipongeza hotoba ya Rais akisema imebashiri kuwa Tanzania ina tatizo la msingi lakini akaikosoa kuwa haikujielekeza kwenye tatizo la msingi ambalo ndiyo chanzo cha kutoweka kwa amani.

Alisema tatizo walilonalo Watanzania kwa sasa ambalo linafanya hali kuwa tete nchini ni mfumo mbovu wa uchumi na siasa.

“Maandamano ya Chadema hayawezi kuwa chanzo cha kutoweka kwa amani hapa nchini, nilitarajia Rais angezungumzia mfumo mzima wa uchumi na siasa ambayo ni mbovu na imeshindwa kuwasaidia wananchi wake,” alisema Bashiru.

Alisema mfumo wa uchumi na siasa ni mbovu na kwamba hali hiyo ndiyo inayoonyesha viashiria vya kutoweka kwa hali ya amani hapa nchini.

“Yapo matatizo mengi ambayo ni viasharia vya kutoweka kwa amani, kitendo cha polisi kupigana na wafanyabishara katika eneo la Darajani Visiwani Zanzibar, migogoro ya ardhi baina ya wanachi na wawekezaji, vijana kukosa ajira na wengine kukosa elimu, hivyo ndivyo viasharia vya kutoweka kwa amani,” alisema.

Bashiru alisema Rais Kikwete hakustahili kuzungumzia maandamano badala yake angejikita katika mambo ya msingi likiwamo suala la kuporomoka kwa elimu, ukosefu wa ajira na tatizo la ugumu wa maisha linalowakabili wananchi kwa sasa.

“Kuna wananchi wengi wamekata tamaa, watu hawa hawana muda wa kusikiliza hutoba ya Rais wala kwenda kwenye maandamano ya Chadema wao wanazungumzia ugumu wa maisha, hali hii inatutaka kuchukua hatua ya kutafakari na kuufanyia kazi mfumo wetu wa uchumi,” alisema.

Alisema ili kutatua tatizo hilo, juhudi za makusudi zinafaa kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kutafakari kwa kina ili kuhakikisha mfumo wa uchumi na ule wa kisiasa unaboreshwa na kwenda sambamba na mahitaji ya wananchi.

Bashiru alisema huu si wakati wa malumbano ya kisiasa na baina ya vyama kwa kuwa hayatalisaidia taifa, bali kinachopaswa kufanywa ni kwa wadau kushughulikia tatizo la msingi ambalo ni mfumo uliopo sasa.

Mkazi wa Tabata, Mndame Mchande alisema anakubaliana na kinachofanywa na Chadema na kwamba hatua inayofanywa na chama hicho ndiyo inayotakiwa kwa kuwa hata wabunge wake wakipeleka hoja bungeni hupingwa.

“Wanachofanya ni sawa…. hao wanaolalamika juu ya Chadema hawawezi kufanya kitu kama hicho, wao wanachokijua ni kung’ang’ania madaraka tu,” alisema Mchande.

Alisema wanaopiga makelele dhidi ya Chadema ni kama wanataka kuidanganya jamii akisema chama hicho kinatekeleza yale kilichoahidi ikiwa ni pamoja na kuwatetea wananchi maskini.

Mfanyabiashara kutoka Mafinga, Victory Kipanguala alisema kwamba alitegemea Rais Kikwete angejadili tatizo la umeme na namna ya kumaliza mgawo na lakini akasema kitendo chake cha kusema kwamba bidhaa zitapungua bei wakati viwanda vinatumia umeme wa bei kubwa zaidi ni kuidanganya jamii.

Alisema kitendo cha kuijadili Chadema na kuacha mambo ya msingi ndiyo sababu ya yeye kuiona hotuba ya Rais haina lolote.

Mfanyabiashara mwingine kutoka Iringa, Godson Sanga alisema alitegemea Rais Kikwete angefafanua sakata la Kampuni ya kufua umeme ya Dowans.

“Kuna mchakato wa kuilipa kampuni hii ya Dowans, mimi nilifikiri Rais angezungumzia msimamo wa serikali kuhusu ulipaji wa kampuni hii, lakini amezungumzia mambo mengine kabisa ambayo hayana tija kwa Watanzania,” alisema Sanga.

Habari hii imeandaliwa na Moses Mashalla, Arusha; Frederick Katulanda, Mwanza; Ramadhan Semtawa, Nora Damian Fidelis Butahe, Geofrey Nyang’oro na Raymond Kaminyonge, Dar es Salaam.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Last Updated on Wednesday, 02 March 2011 08:23 Comments




0 #13 mwl marwa ryoba 2011-03-02 08:34 mi binafsi nichukue fursa hii kumpongeza mshikaji kwa kutambua kwamba maisha ni magumu kwa sasa na hata swahiba wake wa karibu(Richmond uli) amelitambua hilo baada ya kuwaita waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa ataishauri serikali kuongeza mishahara ya watumishi wa umma maana mfumuko wa bei uko juu sana.lakini haya wameyatambua baada ya Chadema kuandamana kwa amani bila kufanya fujo kama wenzao wa ccm .naomba nimkosoe jk kwamba tz hatutapiga hatua za kimaendeleo n kuondoa umasikini wa watz kama mambo yafuatayo hayapo
*UMEME THABITI
*VIWANDA ANGALAU VIWILI VIDOGO(SIDO WAWEZESHWE KUFANFA HII KAZI MAANA UWEZO WANAO,MABILION YA KIKWETE YATUMIKE NA ZILE ZA DOWANS &EPA)
*WAKULIMA WAZAWA WAWEZESHWE KUANZISHA KILIMO CHA KISASA(KILIMO CHA JEMBE LA MKONO NA KUTEGEMEA MVUA KIKOMESHWE HARAKA)
*WAFUGAJI WAPEWE MAENEO YAO MAALUMU KWA KAZI HIYO BILA HIVYO MIFUGO ITAISHA
*KILA JIMBO LIWE NA CHANZO KIKUBWA CHA KUVUNA MAJI YA MVUA(BWAWA)
Haya ni baadhi tu ya mambo yatakayo tusaidia vingenevyo kikwete asiilaumu chadema bali ajilaumu yeye na ccm yake kwa kuchukua cho mapema kwa kutokuwa waaminifu kama muasisi wa chama hicho alivyo kuwa.

Quote









0 #12 koku 2011-03-02 08:33 NI KWELI WACHANGIA MADA HUU NI UDINI NA UKABILA KWENDA MBELE, WATANZANIA WENZANGU TUSIDANGANYIKE KWA KUSHABIKIA VYAMA KWA AJILI YA UKABILA NA UDINI, MIMI NI MKRISTO LAKINI NACHUKIA KUONA UDINI TUMEUWEKA MBELE SISI WANANCHI WENYEWE NDIYO TUTAKUWA WAATHIRA WAKUIKIMBIA NCHI YETU WENYEWE.

ENYI WAANDISHI WA MWANANCHI MLIO NA ELIMU NDOGO YA UANDISHI ACHENI KUSHABIKIA CHAMA NA UDINI MTATUARIBIA NCHI YETU KAMA MLIVYOFANYA KWENU KENYA.

Quote









-1 #11 Mwanaweja 2011-03-02 08:29 mbowe pamoja na wasomi wezetu mmenena wala haikuhitaji kuelezea CDM bali ni kutenda katika mapungufu yaliyopo. maana naamini kama safu ya rais ingekuwa inawajibika vizuri hata CDM ninaimani wasingeweza kufanya maandamano lakini kwa kuwa jk na wabunge wa ccm hawana kinachofanyika cha maana bali ni usanii,kubeza, kuzomea na kutokufikiria kama hizi ni point tuzifanyie kazi. hata kama za upinzani lakini kwa kuwa zinamanufaa kwa taifa basi wa zitumie. Nje ya hapo jk aelewe tz mpaka kijijini hawandanganyiki maana ugumu wa maisha wanapatwa kwa kila level ya maisha na kila nyanja .
Quote









0 #10 Asante Mungu 2011-03-02 07:51 Kweli Nimeamini kuwa kuna baadhi ya watu kufikiria kwao ni shida. Suala la maandamano ya Chadema sio kampeni bali ni dhamira ya dhati ya kuitaka serikali ichangamke katika kuwahudhumia wananchi wake. Chadema ni chama cha demokrasia na maendeleo kama unajua hilo ni dhahiri kuwa utaona wanachokifanya kinaenda sawa na jina lao. Viongozi wanaojali na kujikita katika kutenda haki ni viongozi wanaostahili kuiongoza nchi hii na sio wengine ila ni chadema pekee.Kauli ya JK imekosa utashi na inastahili kupuuzwa na viongozi wetu wanaoijali nchi yao.
Quote









0 #9 Jeremiah 2011-03-02 07:45 Rais Kikwete anasema kuwa njia ya kubadilisha uongozi ni uchaguzi na kuwasilisha matatizo ni bungeni, hatuendi huko. Tukisema bungeni wanatuzomea kwa vile wao wako 300, tukifanya uchaguzi wanachakachua kura zetu sasa na sisi tukiwa nje tuko milioni, tumepita mikoa mitatu sasa analalamika,”
Huu ni Ukweli dhabiti. Jukwaa la nje ya Bunge ni fursa muhimu na adhimu.
Quote . GOOD POINT.

Quote









-1 #8 Gudu Maganga 2011-03-02 07:19 Ukisoma maoni unaweza kubashiri dini ya mtu, hasa wenzetu ambao kwao JK ni safi.
Quote









+2 #7 CHACHA 2011-03-02 07:10 Ina maana katika mambo yote kikwete hakuona kwamba kufeli watoto wa form four ni janga la kitaifa?

Au ndo lengo la shule za kata kufelisha watu,...maana kakaa kimya tu badala yake anaongelea chadema!

Hivi unadhani hao 89% walofeli wanaenda wapi na wanafanya nini saivi kama sio kwenda kwenye mikutano ya chadema kutafuta tumaini la maisha ya uhakika?

Quote









0 #6 CHACHA 2011-03-02 07:06 Quoting PEPE S:
HAPA MWANDISHI UMEEGEMEA UPANDE MMOJA.

MAKALA HII HAIKO BALANCED. SI KWELI KWAMBA HATUA ZA CHADEMA HAZIPINGWI NA WENGI.

ULICHoFANYA NI KUANDIKA MAONI YA WANAO IUNGA MKONO HATUA YA CHADEMA NA KUYAWEKA KAPUNI YA WANAOIPINGA HATUA YA CHADEMA


Hahahaha,utalia tu!
Huo ndo ukweli wenyewe kama kahoji kila mtu anapingana na raisi wako unategemea aandike nini?
Pole sana,hata hivo kama unataka wanao mpongeza kikwete kawasome kwenye gazeti la uhuru wapo kibao sio kwenye magazeti huru kama haya

Quote









-1 #5 EC 2011-03-02 07:05 “Rais Kikwete anasema kuwa njia ya kubadilisha uongozi ni uchaguzi na kuwasilisha matatizo ni bungeni, hatuendi huko. Tukisema bungeni wanatuzomea kwa vile wao wako 300, tukifanya uchaguzi wanachakachua kura zetu sasa na sisi tukiwa nje tuko milioni, tumepita mikoa mitatu sasa analalamika,”
Huu ni Ukweli dhabiti. Jukwaa la nje ya Bunge ni fursa muhimu na adhimu.

Quote









0 #4 Salma 2011-03-02 07:01 Wewe Pepe sijui Januari Makamba na dada yako dadia au Mary Chatanda acheni hizo. CHADEMA ni chama kinachokubalika nchi nzima mpende msipende. Tumekuja kuwashika. Na mimi kwa taarifa yako sio mwanachama wa chama chochote nchini.
Quote









-1 #3 Kruger 2011-03-02 06:32 Kiukweli unazi hausadii bali kazi ifanyike kwa ajili ya kutekeleza Ilani za Uchaguzi.Kama mwenye dhamana ukiona hali yaenda mrama, si kuanza kulumbana bali ni kufanya kazi inayoonekana wananchi waione
Quote









-5 #2 dadia d 2011-03-02 05:33 CHADEMA kampeni za urais, ubunge, na udiwani za mwaka 2010 zimeisha. Za mwaka 2015 hazijaanza

Mbona wenzenu wanajua kua kampeni za 2015 hazijaanza?

kwanini nyie muanze kampeni za 2015 sasa kwa kisingizio kua mnachofanya ni kufikisha ujumbe kwa wananchi?

Quote









-5 #1 PEPE S 2011-03-02 05:27 HAPA MWANDISHI UMEEGEMEA UPANDE MMOJA.

MAKALA HII HAIKO BALANCED. SI KWELI KWAMBA HATUA ZA CHADEMA HAZIPINGWI NA WENGI.

ULICHoFANYA NI KUANDIKA MAONI YA WANAO IUNGA MKONO HATUA YA CHADEMA NA KUYAWEKA KAPUNI YA WANAOIPINGA HATUA YA CHADEMA

Quote
 
Misri wana neema hawamtaki Mubarak, Tanzania mmelogwa?
ban.blank.jpg

Mwandishi wetu

amka2.gif
BAADA ya kushuhudia maandamano ya kuangusha wezi wenye madaraka huko Maghreb, nimeanza kufanya utafiti juu ya hulka na tabia za watu duniani.
Nilifikia hitimisho hili baada ya kushuhudia Hossein Kibaraak akidondoshwa na nguvu ya umma pale Masri huku Mwamali Kashafi akizidi kugeuka kuku alaye mayai na vifaranga vyake.
Yule shujaa tuliyemzoea katoweka zamani gani! Nafasi yake imefichua shetani anayeweza kutumia madege ya kijeshi kumaliza watu wanaodai haki na heshima yao! Kweli madaraka yanaficha mengi nimegundua.
Katika utafiti wangu nimegundua kuwa kumbe nyuma ya sura nzuri kunaweza kuwa na ukatili na ubaya vya kutisha! Hii ndiyo siri ya watu wenye tabia ya kuchekacheka kuwa na tabia tofauti nyuma ya pazia. Ni wakatili hakuna mfano.
Kwa kimombo watu wa sura kama Kashafi huitwa flamboyant au warembo, tuseme. Ila ukiwachunguza, si warembo kitu bali maharamia waliofunikwa na bashasha.
kitaka kujua nimaanishacho hebu angalia sura na hulka za wezi wa Dowanis. Most of them are beautiful if not flamboyant. But in actual fact they are but vampires.
Lo! Samahani kwa kumwaga ung'eng'e. Hii imesababishwa na mwenembago na si kujidai ili mjue nimesoma. Najua: mnajua nimebukua. Sijafoji kama wale wasoheshima vihiyo waliotuhumiwa kughushi wakanywea na kuthibitisha kuwa kweli walighushi kuanzia kura hadi shahada.
Wako madaktari wengi vihiyo walioghushi tena bungeni na kabitenini. Hata pale Site mkuu wake mpya ni kihiyo aliyeghushi. Muulize Bachelor yake aliipata wapi.
Sasa tuachane na gendaeka wachache. Tuangalie umma ambao nimejipa kazi ya kuutafiti na kutoa matokeo ili yatumika kusaidia kuleta ukombozi.
Kwa utafiti huu wa kisayansi nimegundua kuwa nami ni sehemu ya mapinduzi matakatifu yatakayofuata baada ya watu kujua udhaifu wao. Isitoshe ni juzi juzi nilikwa Benghazi, Tobruk, Sabha, Kuffra, Ghadames, Berdi na kwingine kwingi.
Maana nilikwenda kule kuwashauri njagu wasijiingize kwenye kulinda maiti inayonuka na kujiletea aibu na dharau bure toka kwa umma. Nashukuru Subhanna wengi walinisikiliza na kutia akilini hadi wakamuasi jamaa. Hata wale marubani waliogoma kushambulia waandamanaji nilikuwa nimeongea nao siku moja kabla ya kitendo hiki cha kishujaa na kizalendo.
Najiuliza. Wangekuwa mandata wetu hata magesi yetu hovyo wangeweza kufanya hivi wasiogope kuwakasirisha mabwana zao wanaowafuga kama mbwa? Ila ukiondoa wakubwa wao, ukiwachunguza wa chini ni makapuku kuliko hata walevi wenyewe lakini bado wanatumika na wasijijue. Jamani amkeni kwani nanyi mnaliwa. Muulize Nyangenyange na Shimboshimbo. Wataanza kukutisha utadhani si kweli!
Nimegundua: wamanga wakipatwa na ukosefu wa kazi hawajiingizi kwenye umachinga au udokozi wa mali ya umma kuganga njaa. Wanaingia mitaani kinaeleweka. Waswahili, kwa upande wao, ni tofauti. Wanafanya nini? Kila mmoja anajua.
Nimegundu wamanga, japo wanalalamika umaskini, ikilinganishwa na wenzao walevi wao wana nafuu tena sana. Nilishuhudia Cairo umeme ukiwaka masaa 48.
Pamoja na kutokuwa na vyanzo vya maji kama vyetu, hawajui neno mgao au ulanguzi wa umeme wala maji. Nilipowaambia kuwa kayani kwangu umeme ni ishu walinishangaa na kuuliza kama wanakaya wa kaya yangu ni watu au mbuzi.
Nimegundua pamoja na watawala wa kimanga kuwa wezi, kwa kiasi fulani wana nafuu. Wana angalau maadili ya utawala siyo haya Madili ya watawala ninayoona uswahilini.
Kitu kimoja wamanga walivumilia na sasa wameamua kuachana nacho-kutawaliwa kwa muda mrefu huku wezi wao wakila kwa muda mrefu mikono na miguu bila kusali wala kunawa.
Gonjwa jingine lililowachelewesha wamanga ni kujuana. Kila rais alikuwa anataka kumrithisha mwanae urais asikue urais ni wa umma. Wao wanatawalana kwa makundi ya kikabila tofauti nay a kifisadi kama ulevini.
Kitu kimoja wezi wa kimanga walijua. Hawakuacha wanakaya wao wawe makapuku kwa kuwupuuzia, kuwanyonya na kuwadhalilisha kwa kiwango cha wamakonde. Walihakikisha bei ya mkate, umeme, petrol na mahitaji ya muhimu na lazima inakuwa ya chini huku wakijitahidi kuwajengea watu maskini majumba ya kuishi.
Juzi nilicheka nusu kunyotoka roho. Nilicheka pale imla wa Saudia aliporejea kutoka kwenye matibabu na kumwaga zaidi ya dola 35,000,000,000 kwa wanachi wake ili wasimbarake au kumgadafi. Je hili ni jibu?
Maskini hajui kuwa kwa kumwaga kitita hiki amethibitishia umma kuwa kumbe anazo na hivyo watazidi kumdai zaidi. Hata utoe pesa kiasi gani, huwezi kununua uhuru na haki za watu. Huwezi kununua haki za binadamu wala demokrasia.
Je huku si kutapatapa? Heri mfalme anazo za kuwahonga wananchi wake. Je wale niwajuao watahonga nini iwapo wana uroho na akili kama panya? Watahonga nini iwapo wachukuaji walishachukua kila kitu?
Nimegundua wamanga ni wajanja. Hawaogopi kupigwa risasi wala kumwagiwa upupu na kudondoshewa mibomu ya michozi. Mswahili anaishi kwenye zizi na bado anaendelea kuaminishwa kuwa hayo ndiyo maisha bora.
Kwa wale wenye nyumba za maana walio wengi wanatembea na suto la wizi nyoyoni mwao. Kwani wamezipata kifisadi hadi wengine hata kutotaka zijulikane kuwa ni zao kama mimi ilivyonitokea kule G'Mboto hivi karibuni.
Hata hivyo nisiwalaumu sana walevi. Ulevi umewamaliza akili kiasi cha kutenzwa kama wanyama hasa kondoo ambaye waweza kuchinja wakati wowote na asifurukute.
Kuna swali linanisumbua sana. Tunisia wako milioni kumi lakini wana akili kuliko wabonglalalanders milioni zaidi ya 40. Anayebishia hili aniambia wabongolalalanders pamoja na wingi wao wamefanya nini la maana zaidi ya kuzidi kuishi kizani kama kupe, mende na panya? Jaribu hili kwa watunisia au wamasri uone.
Masri kuna barabara nzuri, umeme ni twenty four hours, maisha ni nafuu ikilinganishwa na wabongolalaland lakini bado wamemtimua kibaraak.
Najiuliza wangekatiwa umeme au kuibiwa njuluku kama hizi wanazolipana kidowans dowans si wangemnyotoa mtu roho? Wangekuwa wanagawiwa giza badala ya umeme hali ingekuwaje? Bila shaka kungechimbika bila jembe. Bila shaka kusingetosha hata kwa wiki moja.
Ngoja niwahi taarifa ya habari nisijeikosa fursa ya kumuona Mwamali Kashaffi akiburuzwa mitaani na kuchapwa bakora baada ya kuangushwa. Nanyi wangu make mkao wa kuliwa. Du kumbe ni kweli! Khalas kweis Intahabib yuuni.
 
Hii ndiyo nguvu ya umma iliyokata tamaa
ban.rais.jpg

Paschally Mayega

amka2.gif
RAIS wangu, nilikuandikia kuwa usipowafuta kazi wale uliowakabidhi dhamana ya kuhakikisha kuwa nchi na wananchi wake pamoja na mali zao hawaathiriwi na mabomu na makombora waliyoyanunua kwa kodi yao, msalaba wao utaubeba wewe.
Yameanza kutimia kule Mwanza!. Mwana mwema Shija wa Mbagala/Chalambe aliyekuwa huko aliniandikia ujumbe ufuatao, "Tulipofika uwanja wa Furahisha, baada ya Dk. Slaa kushuka jukwaani alipanda Freeman Mbowe. Alipouliza nani wanataka Hussein Mwinyi na Ngeleja wajiuzulu uwanja mzima ulinyosha mikono.
Mbowe alipoishia hapo watu wakaanza kupaaza sauti zao, kutaka na Kikwete ajiuzulu. Ikabidi Mbowe aanze kuwatuliza na jazba zao. Wakaanza kusema tuko tayari kufia barabarani kuliko kuishi maisha magumu namna hii!
Wengi na hasa akina mama na vijana walianza kulia na kutokwa na machozi!". Baba kumbuka ahadi iliyokuingiza Ikulu 2005, ‘maisha bora kwa kila Mtanzania,' yako wapi maisha bora kwa watu wako hawa baba? Haya sasa wanataka ujiuzulu.
Hilo tutaliangalia huko mbele ya safari.
Waliomsoma Kiona Mbali, katika makala yake ya ‘Tumeamua kufuta dhamana ya uwajibikaji?', kama ilivyoandikwa na mwana mwema Juvenalis Ngowi Jumatano iliyopita watakuwa wameuona usaha ndani ya jibu ambalo linakaribia kupasuka.
Juveni hakai Gongo la mboto lakini ameathiriwa vikubwa na mlipuko wa makombora ya Gongo la mboto. Mtu wake wa karibu, dada yetu mpenzi katibu muhtasi wao amepoteza mkono wake wote.
Ameachwa na kilema cha maisha. Bado anauguza kilema chake.
Waziri mwenye dhamana bado anakalia ofisi ya wananchi wale wale walioathirika. Hii ni sawa na kuwatupia wananchi kebehi za matusi.
Wanajiuliza, nafasi ile alipewa au aliinunua? Yule aliyempa au aliyemuuzia akae akijua kuwa hukumu ya wananchi itakapokuwa inapitishwa haitawatofautisha.
Anayempa jeuri ya kuendelea kutumbua huku maisha ya Watanzania yakiendelea kupukutika kwa uzembe atahukumiwa zaidi. Wahenga walisema mchelea mwana kulia hulia yeye!
Namshauri bwana Hussein Mwinyi ayasome makala yale gazeti Tanzania Daima Jumatano 23-2-2011 ili yamsaidie kuondoka mwenyewe kwa amani.
Vyombo vya habari vimeonyesha majeneza matatu yaliyobeba miili ya wafu watatu wa familia moja mama na watoto wake wawili waliofikwa na mauti kutokana na milipuko ya makombora yale. Bwana Hussein Mwinyi aliyaona! Wanadamu wengine wameubwa na uso usio na haya na mioyo migumu kama chuma. Unasimamaje hadharani wakati nguo zote zimekuvuka?
Kwao kuwajibika si heri, heri ni kutimuliwa kwa aibu na wananchi. Heshima ya kiongozi haitoki kwa wananchi bali kwa kiongozi mwenyewe.
Kwa wananchi inaenda kudunda tu na kisha kumrudia kiongozi mwenyewe. Kiongozi ukishapoteza heshima yako mbele ya wananchi unangoja nini?
Ndani ya CCM wako watu wengi tu wenye busara na akili kubwa lakini wanakuwa kama wamedungwa sindano ya ganzi. Hakuna hata mmoja anayethubutu kumwambia Mwinyi, bwana wewe pisha unaharibu picha nzuri ya chama chetu kwa wananchi.
Kwa nini CCM inawaachia CUF au CHADEMA ndiyo wafanye kazi ya kumuondoa Hussein Mwinyi? CHADEMA walimpa siku tisa awe ameondoka. Ni aibu kubwa kwake na zaidi kwa anayeendelea kumlea na kwa chama chake, CCM.
Mafanikio makubwa ya CHADEMA yametokana na uozo kama huu ndani ya CCM.
Nchi yetu inaongozwa kistaarabu, hatuwezi kufuta dhamana ya uwajibikaji. Ni matumaini ya Watanzania walio wengi kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge yenye nguvu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ndugu Edward Lowassa atamsaidia Rais wa Jamhuri kutia shinikizo ili bwana Hussein Mwinyi ajiuzulu kwa kuwajibika akifuata mfano aliouonyesha yeye mwenyewe pale alipojiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu kwa kuwajibika.
Wananchi wanajua ufuatiliaji na utendaji kazi wake, hivyo ni matarajio yao kuwa kwa shinikizo lake bwana Mwinyi ataondoka na hivyo kukitolea ukungu mweusi chama chake na kumfanya Rais Kikwete aonekane ni mtendaji.
Rais wangu maandamano makubwa yaliyofanyika jijini Mwanza ni ushahidi usio shaka dhidi ya ujinga uliofanywa na jeshi la Polisi
kuzuia maandamano ya Arusha. Aliyefanya hivyo bado anakalia ofisi.

Sasa CHADEMA wanawachezea Polisi kama nyoka wasio na meno.
Akitaka kuthibitisha ujinga huo, mwana mwema Godbless Lema, nadhani kwa makusudi kabisa aliamua kutembea kwa miguu kutoka mahakamani kule alikoshtakiwa kwenda ofisini kwake. Alijua wafuasi wake watamfuata. Alijua pia kuwa havunji sheria. Akataka tu kupima akili ya polisi.
Bila fikra zozote polisi wakaingia katika mtego wakawafyatulia mabomu ya machozi raia wema kabisa waliokuwa wanatembea kwa amani.
Mwana Mwema Godbless Lema amepita katika misukosuko mingi ya Polisi. Kuna wakati amepigwa na polisi mpaka akazimia. Kwa hakika Polisi wamesaidia sana kuinua jina la mtu huyu.
Kwa sababu ya ujinga huo leo jina la Godbless Lema linaonekana ni jina la ukombozi, siyo wa Arusha tu bali ukombozi wa nchi yetu yote.
Bila upuuzi huu wa polisi wako wengi ambao wangekuwa hawamjui mtu huyu hadi leo.
Mwana mwema Samson Mwigamba kafungwa jela kwa tuhuma ya kuandamana bila kibali huku akiwa na barua mkononi iliyomruhusu kuandamana kutoka kwa polisi hao hao.
Naye, Polisi wamefaulu kuingiza jina lake katika kitabu cha wapigania uhuru wa awamu ya pili wa nchi yetu.
Ni kweli hawa wanaojiita vijana wa CCM hawaoni kuwa hapa kuna kasoro ndani ya chama chao? Kama hawalioni hili basi CCM imefika mwisho wa reli.
Rais wangu maandamano ya Mwanza yaliyoasisiwa na CHADEMA yalikuwa makubwa sana. Maandamano ya Msoma yalifunika zaidi. Mpaka askari polisi walishiriki kuandamana. Nao walionyesha ishara ya vidole viwili inayotumika na CHADEMA.
Wameanza kutambua kuwa wanachodai CHADEMA ni unafuu wa maisha yao pia. Watu wamechoshwa na uongozi unaoonekana kutojali hali ngumu ya maisha yao. CHADEMA au CUF wanaonekana wakombozi hata kama siyo.
Ndugu Rais, moyo wangu ulilipuka pale Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Freeman Mbowe alipouliza ule umati mkubwa kuwa, "Mnataka na Kikwete ajiuzulu pia?" Wananchi walimjibu kwa sauti kubwa, "Ndiyooo!".
Nikaikumbuka Tunisia. Nikaikumbuka Misri. Maskini Ben Ali, maskini Hosni Mubarak, maskini Muamali Gaddafi! Nikainamisha kichwa nikiwaza, kama umati mkubwa kiasi kile wanataka baba ujiuzulu kumbe ulichaguliwa na nani?
Wageni na watu wa mataifa wanaposhuhudia maandamano makubwa kama yale ya Mwanza, Musoma na Arusha hawakosi kujiuliza sasa huyu mtu
alichaguliwa vipi? Hawaoni tofauti ya maandamano ya Tunisia, Misri na haya. Hawawaoni wanaokuunga mkono zaidi ya sisi tulioko nyuma yako lakini hatuandamani.

Ije mvua, lije jua baba hatutakuacha, lakini na wewe ututegee sikio lako usikie kilio cha watu wako!
Mbowe aliendelea kusema, "Sawa nimewaelewa kumbe mnataka Rais Kikwete naye ajiuzulu pamoja na Ngeleja na waziri Mwinyi (Hussein) pia ajiuzulu! Aha! Ngojeni kwanza Kikwete tunataka kwanza tumalize kupita mahali pote na kuzunguka, yeye inakuja yake babu kubwa kama ya Misri na Tunisia".
Kama hadhira niliiona Mwanza, Musoma, Arusha wakati wa maandamano na wakati wa maziko inataka mageuzi, basi mageuzi katika nchi yetu yanaweza yasiwe yakutisha kama yale ya Tunisia, Misri au Libya. Hafi mtu!
Baba yanaweza yakafanana na kitendo cha mtu kumsukuma mlevi katika mteremko! Watanzania watamuua Tembo kwa ubuwa!
Ndugu Rais kulitangazia Taifa kuwa CHADEMA wanaleta fujo bila kueleza chanzo ambacho ni umeya wa Arusha hakuwezi kumaliza mtafaruku wala kulinda hadhi ya matamshi yako.
Hukuzungumzia lolote kuhusu mauaji ya Arusha kama vile waliouawa ni wanyama au si watu wako!. Kwa wakubwa‘Mabalozi' uliwaambia kuwa ni bahati mbaya, kwa watu wako mwenyewe kimya.
Rais wangu mauaji ya Arusha yamembabua Waziri Mkuu Bungeni. Umeya wa Arusha siyo kitu cha kufanyia mzaha hata kidogo. Mkiendelea kuung'ang'ania, sitabiri, lakini umeya wa Arusha una uwezo wakuusitisha utawala wako kabla. Utakuja yakumbuka haya maneno!
Mkiurudia, kukata mzizi wa fitina kuna ubaya gani?
Unazungumzia ya Mwanza, Musoma na kanda ya ziwa kwasababu ni kweli ni tishio linaloonekana moja kwa moja na kila mtu mashaka ya wewe kuendelea kuwepo madarakani.
Upepo unaovuma mikoani hivi sasa, siku utakapoingia katika jiji la Dar es salaam, mbichi na mbivu zitajulikana na kazi itakamilika. Kwanini baba usianze hata kwa kumtimua bwana Hussein Mwinyi tu kuwapoza Wananchi? Baba anapolalamika sisi tufanyeje?
Nguvu ya umma maana yake ni nini? Nani anamiliki nguvu ya umma? Ukiona upinzani una nguvu ya umma jua wewe huna. Nina hakika katika maandamano ya Arusha, katika maziko ya Arusha na katika maandamano ya Mwanza, Musoma, ukerewe na kote yanakoasisiwa na CHADEMA baadhi ya washiriki ni wanachama wa CCM na wa vyama vingine.
Hii ndiyo nguvu ya umma. Wananchi walioungana kwa lengo moja. Majeshi yenye nguvu na yenye silaha kali kama ya Tunisia, Misri na sasa Libya yako wapi?
Katika ukurasa wa 22 kitabu cha Mwalimu Mkuu wa watu imeandikwa, "Tumeshikwa, lazima tushikamane. Hakuna nguvu yoyote duniani inayoweza
kushinda nguvu ya wananchi waliokata tamaa na kuamua kuwa sasa basi!

Liwalo na liwe! Nguvu ya wananchi wenye haki hushinda vita yoyote duniani!".
Rais wangu wananchi wameanza kusema ujiuzulu huku CHADEMA wanazunguka na kupita mahali pote wakimwaga upupu, unadhani ni nini kitatokea?
Swali hili aliuliza Waziri Mkuu wetu pale alipotuhumiwa kulidanganya Bunge.
Ndugu Rais, pamoja na Waziri mkuu wetu kutuhumiwa kulidanganya Bunge na Taifa wakati akitoa maelezo ya kile kilichotokea Arusha wakati wa mauaji ya raia wasio na hatia ya tarehe 5-1-2011 yaliyofanywa na polisi, huyu mtu siyo mwizi kabisa. Kudanganya ni kusema uongo, Bungeni hairuhusiwi kabisa.
Kitakacho mfanya aathirike zaidi na taarifa isiyokuwa ya kweli aliyoitoa ni kihelehele cha Spika wa Bunge la Jamhuri. Spika Anna Makinda aliulizwa swali, "Mama unaitwa nani?"
Spika Anna Makinda akajibu kwa hamaki, "Mimi natoka Njombe!"
Alichoomba mbunge Godbless Lema ni mwongozo. Alichotoa Spika, kitu tofauti. Spika akafanya kana kwamba mbunge ametamka tayari kuwa waziri mkuu kasema uongo. Ni kweli ndiko alikokuwa anakwenda mbunge lakini alikuwa hajatamka hivyo.
Akasema adabu iwepo bila kufafanua nani awe na adabu, anayesema uongo au anayemwonyesha anayesema uongo. Akamchimbia waziri mkuu shimoni kwa kumtaka Mbunge athibitishe hadharani ukweli ulio wazi.
Wapelelezi wanaopeleleza tukio lile wamekiri Mahakamani kuwa upelelezi bado haujakamilika, maelezo aliyokuwa anayatoa Bungeni Waziri Mkuu aliyapata wapi? Sasa Spika huyo huyo anahaha. Anataka iwe siri.
Wabunge wote wafahamu kuwa kinachotendeka Bungeni sasa hivi hakuna ambacho wananchi hawakijui. Walioupande wa wananchi wanajulikana kwa wananchi na wabunge vibaraka pia wanajulikana.
Utafika wakati wabunge wanaozomea wenzao bungeni wataanza kuzomewa na wananchi katika majimbo yao na kote watakakopita. Hii iliishawahi kutokea na sasa inakuja! Unajiita mheshimiwa halafu unazomeazomea hovyo Bungeni kama wafanyavyo walevi wa pombe za kienyeji, jitambue kuwa wewe hukustahili kuwa hapo.
Wewe ni ndago.
Ni ukweli usiofichika kuwa mwenye busara na akiri hutumia kichwa chake kufikiri ili apate hoja ya msingi ya kumpinga mpinzani wake, naye zezeta hutumia domo lake kuzomea.
Ndiyo, hana akili ya kufikiri, punguani, afanyeje? Ndago, ‘Magugu' yaliyoota pamoja na ngano! Hatuwezi kuyang'oa sasa tutasubiri mpaka wakati wa mavuno tuyafunge vitita vitita tukayachome moto! Rais wangu kwaheri ya kuonana!.


h.sep3.gif

Tel: 0713334239
 
CCM imepoteza uongozi wa kisiasa
ban.blank.jpg

Mwandishi wetu

amka2.gif
KATIKA uhai wake Mwalimu Nyerere amewahi kuwafundisha wananchi wa Tanzania kwamba ili tuendelee tunahitaji mambo manne (4) ya msingi katika mchakato wa kisiasa katika kuleta maendeleo ya watu. Mwalimu Nyerere alisisitiza zaidi uongozi bora wa kisiasa miongoni mwa mambo ya msingi kama vile ardhi, watu na siasa safi kama nyenzo za kusukuma maendeleo ya watu kwa uwiano unaozingatia uendelevu wenye ufanisi na tija ya matumizi bora ya rasilimali na mali ya asili.
Kwa jinsi hiyo, hata msisitizo wa kiitikadi wa chama (TANU na hata baadaye Chama cha Mapinduzi - CCM) ulilenga katika kuwaondoa wananchi wa Tanzania kutoka kwenye maisha ya uchumi dhaifu na kuwapeleka kwenye uchumi wa kujitegemea kwa utumizi wa uongozi bora wa kisiasa. Na ndiyo maana, CCM iliamini juu ya "Ujamaa na Kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu waliyo sawa na huru." Kwa msingi huu, uhuru wa wananchi wa Tanzania uliainishwa kwenye msingi wa "kujitegemea."
Tangu CCM ilipotimiza miaka kumi (10) na Azimio la Arusha kuazimisha miaka ishirini (20) ya kuzaliwa kwake, uongozi wa nchi ulikuwa chini ya CCM kama chama dola (na ndicho chama kilichoshika hatamu za uongozi wa kisiasa). Ilikuwa mwezi wa Oktoba, tarehe 22 hadi 31, mwaka 1987, CCM ilifanya upitizi wa malengo yake mahsusi ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa utumizi wa sera na programu zenye kuzingatia utashi wa siasa safi na uongozi bora.
Oktoba 1987, CCM ilionyesha jinsi ilivyodhamiria kuwa chama kiongozi kwa minajili ya kuwatumikia wananchi wa Tanzania kwa kuzingatia misingi ya utu (ubinadamu), uhuru, haki, usawa na uadilifu wa hali ya juu. CCM ilidhamiria kutumia rasilimali na fursa zote zinazopatikana Tanzania katika kufikia malengo ya ukombozi halisi wa kiuchumi kwa misingi ya uongozi mujarabu na makini wa kisiasa unaozingatia utashi wa watu wote (wakulima na wafanyakazi) wavuja jasho wa Tanzania.
Inawezekana viongozi wa CCM wa enzi zile ambapo Mwalimu Nyerere alikuwa akionyesha njia ya "Ujamaa na Kujitegemea" walikuwa na shauku na utashi wa hali ya juu katika kutimiza irada (azma au kusudio) ya kuondoa aina zote za unyonyaji, dhuluma, vitisho na kuutokomeza unyonge wa kiuchumi uliyotokana na ukoloni mkongwe na mabaki ya ukoloni mamboleo. CCM ilisimamia utashi wa watu wake na hakika kilikuwa chama kilichojitambulisha kuwa ni cha kutetea wanyonge wa Tanzania – wakulima na wafanyakazi wavuja jasho.
CCM iligeuka kwa kasi ya ajabu! Ni afadhali mabadiliko ya uoni, misheni, madhumuni, sera na programu yangechukua muda mrefu; ilikuwa si zaidi ya miaka sita tangu pale CCM ilipopitisha Programu ya CCM 1987 hadi 2002! CCM iliachana na Azimio la Arusha na kuanza kuelekea kwenye siasa-huria (kwa mujibu wa soko la siasa). Viongozi wa kisiasa ndani na nje ya CCM walianza kutamani nafasi za kisiasa kwa maslahi ya kibinafsi zaidi badala ya kuwatumikia wananchi.
CCM ilipoteza muelekeo! Na ndiyo maana aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimb alidiriki kusema, "CCM imekosa dira na imepoteza muelekeo." Japokuwa maneno ya Horace Kolimba yalimfanya mwanasiasa huyo kuitwa Dodoma kwa mahojiano na Kamati Kuu ya CCM na hatimaye kukumbwa na kifo-tata; ukweli utabaki kwamba, "CCM imekosa dira na haina muelekeo." Kuzimika kwa nyota ya Horace Kolimba kisiasa kulificha mambo mengi ya kisiasa hata hivyo utafiti na hali halisi ya uongozi wa kisiasa wa CCM unaonyesha ukweli huo.
Uongozi wa kisiasa, unahitaji sifa maalum ambazo ndizo chemchemi ya fikra na uoni wa kuongoza watu na maendeleo. Kwa msingi huu, uongozi wa kisiasa lazima uonyeshe muelekeo na ujitambue kabla haujajitambulisha kwa wanachama. Uongozi wa kisiasa unahitaji watu wenye uoni sahihi na fikra angavu na zilizopevuka juu ya matumizi ya haki, usawa na uadilifu katika kusimamia maendeleo ya watu muafaka kwa utumizi sahihi na endelevu wa rasilimali za nchi. Uongozi wa kisiasa lazima uoneshe njia ya manufaa kwa watu katika sekta zote za maisha ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.
CCM imepoteza watu wenye satwa ya uongozi wa kisiasa. Na hata wale wachache waliyomo kwenye mduara wa ndani wa maamuzi ya kisiasa kama vile Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wamezibwa midomo na au wamefanywa "msukule wa kisiasa." CCM imekuwa kama kampuni la wenye hisa kushindanisha hisa; mwenye hisa nyingi ndiye anayesikilizwa na au kuwa na kauli (na au sauti) yenye nguvu juu ya maamuzi yake!
CCM imepoteza sera yake ya kusimamia ujenzi wa ujamaa. Na kibaya zaidi, kwa kuwa ndicho chama kinachoongoza Serikali, kimewafanya wananchi kukosa imani ya mustakabali murua wa maisha ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Ushahidi wa wazi juu ya CCM kupeteza uongozi wa kisiasa ulianza Awamu ya Pili ya Mzee Ali Hassan Mwinyi. Hali ya kuchafuka kwa kada ya uongozi wa kisiasa ndani ya CCM ilishika kasi kubwa kwenye Awamu ya Tatu na sasa (Awamu ya Nne) tunashudia uongozi wa kisiasa shelabela (shaghalabaghala).
Kwa kuwa wapo watu wanaohitaji ushahidi juu ya nukta moja moja inatosha kuandikwa hapa kwamba pamoja na ushahidi wa kauli ya Horace Kolimba (aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM) kuna kila sababu ya wasomaji kuangalia hali ya mwenendo wa uchumi, jamii na siasa kwa sasa. Hali ya uchumi ni mbaya na inakatisha tamaa; hali ya jamii inakwenda segemnege; na mwendo wa siasa unachukua sura ya chuki na uhasama unaoashiria uvunjifu wa amani na kutishia usalama wa watu na mali sawiya.
Viongozi wengi wa CCM kwa sasa wameshikwa na ugonjwa wa ubinafsi kayaya; na kwa jinsi hiyo wamesahau dhima ya uongozi wa kisiasa ya kuwatumikia wananchi. Badala yake wanatumia vyeo vyao vya kisiasa kwa manufaa ya kibinafsi zaidi. Uongozi wa kisiasa umepoteza dhamana na viongozi wengi wa CCM wanadhani uongozi ni "mali binafsi" (rejea kauli ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa anachukua na au anarejesha fomu ya kugombea kuteuliwa kugombea Urais, 2010 aliyoitoa Dodoma).
CCM ilishaona jinsi itakavyopoteza muelekeo na uongozi wa kisiasa tangu Oktoba, 1987. Na ufuatao utakuwa upembuzi yakinifu juu ya hoja kwa nini CCM imepoteza uongozi wa kisiasa. Hoja hizi zitachambuliwa na au kupembuliwa kutoka kwenye Programu ya CCM 1987 hadi 2002. Upembuzi huu utazingatia nukta nne (4) zilizoainishwa kwenye kabrasha la programu hiyo ukurasa wa 76 na 77 kwenye fungu la 209 na la 210.
Kwanza, viongozi wengi wa CCM hawana uelewa wa dhana ya kazi za chama. Hili linatoa taswira kwamba viongozi wa CCM badala ya kufanyakazi za chama kwa minajili ya maendeleo ya watu (wafanyakazi na wakulima) wa Tanzania wameng'ang'ania kazi za binafsi katika kufanikisha maslahi binafsi na au ya kifisadi. Viongozi wa CCM wa zama hizi siyo wale waliyokuwa wakiongoza kwa kuzingatia miiko na maadili kama yalivyoainishwa kwenye Azimio la Arusha, 1967 bali ni wale wanaoongozwa kwa mitazamo ya kifisadi – fedha kwanza na faida kibao!
Uongozi wa kisiasa ndani ya CCM unauzwa na au kununuliwa kama bidhaa. Mwenye fedha na au nguvu ya kutumia fedha ndiye mwenye satwa (nguvu) ya kuchagua na au kuchaguliwa kiongozi wa kisiasa ndani ya CCM. Uongozi wa kisiasa umegeuzwa mradi wa kibiashara kwa falsafa ya mwenye mtaji ndiye anayepata faida ya biashara ya siasa. Hata wale wenye uwezo wa akili na au karama ya uongozi wa kisiasa wamepigwa kumbo na au kutupwa nje ya uongozi kwa kukosa fedha na au kuchukiwa na wenye fedha! Hii ndiyo CCM mamboleo!
Pili, viongozi wa CCM wanadhani kazi ya CCM ni operesheni na au kulipua na ndiyo maana wanaongoza kwa ahadi za uongo (na za kinafiki) na au zisizotekelezeka. Wengi wa viongozi wa CCM kwa sasa wamekuwa wakitosheka na kufanya mikutano isiyokuwa na tija wala ufanisi ilhali dhima ya kuwaletea wananchi maendeleo imekuwa kitendawili kisichoteguka. Angalia hali mbaya ya uchumi; upungufu na katizo la umeme; ukosefu wa ajira kwa nguvukazi kubwa; na hali mbaya ya uchumi binafsi.
Viongozi wa CCM hawana mikakati madhubuti ya kuongoza uchumi na jamii badala yake wanautumia uchumi kidogo (rasilimali) wa nchi kwa manufaa ya kibinafsi ya kisiasa. Huu ni mtazamo hasi kwenye kujenga jamii ya watu waliyo sawa na huru. Na hakika huu ni mwenendo mbaya wa jamii ya watu wanaotaraji kuondoa aina zote za dhuluma na vitisho vya kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Tatu, umangimeza umewatawala viongozi wengi wa CCM na makada wake. Wengi wa viongozi wa CCM wanapenda ukubwa na hata kutamani kusifiwa kwa "ukubwa" wao hali inayowafanya wengi wao kuwa na hisia za kujifanidi na ukubwa ilhali utendaji wao kwenye chama hauna tija wala ufanisi unaozingatia utumishi kwa wananchi. Ukubwa umewafanya viongozi wengi wa CCM kujiingiza kwenye mashindano ya kuwania nafasi za kisiasa si kwa minajili ya kuwatumikia wananchi bali ni kwa faida ya ukubwa!
Ukubwa ndiyo unaowafanya viongozi wengi wa CCM kuonekana wakijipitisha huku na kule katika kutafuta nafasi na au fursa za matumizi ya vyombo vya habari ili kuuza sura kwa mambo hata yasiyokuwa na tija kwa maendeleo ya watu na jamii. Marazote, viongozi waandamizi wa CCM wamekuwa wakitumia muda mwingi katika kujijenga kwenye majukwaa ya kisiasa si kwa vile wana sababu za msingi juu yake bali ni katika kutafuta nafasi za kimkakati katika kufanikisha umangimeza!
Nne, ni kushindwa kwa itikadi ya "Ujamaa na Kujitegemea." Ujamaa na Kujitegemea, kama itikadi, mwanzo ilidhaniwa kuwa ndiyo njia pekee ya kujenga jami ya watu waliyo huru na wenye usawa wa kiuchumi na kijamii. Hata hivyo, viongozi wengi wa CCM wameitelekeza itikadi hii na kujiingiza kwenye kutumia muda wa kutekeleza kazi za chama kwa kazi za binafsi. Jambo la kusikitisha sana, viongozi wengi wa CCM siku hizi wanaendeleza starehe zao badala ya kuwatumikia wananchi.
Viongozi waandamizi wa CCM ndiyo wanaoongoza kwa starehe na kuponda raha bila ya wasiwasi wa kufikiriwa kinyume na wananchi wanaowaongoza. Tunapozungumzia starehe na au kuponda raha kwa viongozi waandamizi wa CCM lazima tutumie mifano hai yenye dhamira ya kuonyesha juu ya kwa nini madai hayo! Na haiwezekani kwa kiongozi mbinafsi, mpenda starehe na kupenda kuponda raha akawa na uchungu na wananchi wenye shida na taabu za kiuchumi na au kijamii.
Viongozi wapenda raha huchukua sehemu kubwa ya muda wa uongozi wao kufanya mambo ya anasa kama safari zisizokuwa na tija wala ufanisi kwa maendeleo ya wananchi. Uongozi wa CCM unaounda Serikali umekuwa kwa nyakati tofauti ukifanya safari nyingi nje ya nchi ambazo kwa sehemu kubwa hazina tija wala ufanisi wa moja kwa moja. Nyingi ya safari hizo zimekuwa za kitalii zaidi kuliko kujenga mujtamaa na mustakabali wa maisha ya wananchi wa kawaida.
Ukiachilia mbali safari nyingi za nje ya nchi, kuna matumizi makubwa na ya gharama yasiyozingatia hali halisi ya watu na maisha yao. Kwa kuwa maisha ya wananchi wengi wa mijini na vijijini ni ya msoto na ya "choka mbaya" tulitegemea uongozi wa kisiasa wa CCM ufanyekazi usiku na mchana katika kutafuta njia ya kuondokana na ugumu wa maisha ya kiuchumi na kijamii, badala yake viongozi waandamizi wa CCM wanaponda raha bila karaha na hawataki kujitesa katika bangua-bongo ili kutafuta utatuzi wa matatizo ya kiuchumi na kijamii yanayowakabili wananchi wa Tanzania.
Tuchukuwe masuala mawili nyeti kwa sasa. Moja, ni tatizo la mfumuko wa bei na kuporomoka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania. Kutokana na hali hii, maisha ya mwananchi wa kawaida na wa kipato cha chini amekuwa akihangaika kumudu maisha yake na hali mbaya inayoukabili mziunguko wa fedha na upatikanaji wa bidhaa muhimu. Bei za bidhaa muhimu ni ya juu mara mbili zaidi ya ilivyokuwa mwaka 2005.
Mbili, ni upungufu mkubwa wa nishati ya umeme uliyosababishwa na uongozi wa kisiasa wa CCM kukosa sera na programu mahsusi katika kutatua tatizo la upungufu wa nishati ya umeme nchini. Kwa kuwa umeme ni kichecheo cha viwanda, ukosefu wa umeme wa kutosha na wa uhakika umeifanya sekta ya uzalishaji na uwekezaji kukosa mvuto wa kiuchumi na hata kusababisha gharama za uzalishaji kupanda na hivyo kusababisha kupanda kwa bei za bidhaa.
Viongozi wa CCM wamechoka kifikra na hawana njia ya kujinasua kutoka hapo. Ni vema basi kwa wanachama wa chama hicho kinachounda Serikali kuchukua nafasi yao kukinasua chama hicho ili kisiiangamize Tanzania. Kushindwa kwa uongozi wa kisiasa kwa CCM kumeifanya Tanzania kukosa uongozi wenye uoni na dira angavu kwa maendeleo endelevu.



h.sep3.gif

Mwandishi wa makala ni Mhadhiri Msaidizi Kitivo cha Biashara, Chuo Kikuu Mzumbe, anapatikana kwa simu namba +255 713 593347 au barua pepe: maligwa1968@yahoo.com, bakari.mohamed@mzumbe.ac.tz
 
Maandamano ya Chadema yaashiria mengi Send to a friend Tuesday, 01 March 2011 21:03

chademamass.jpg
Editha Majura
MWITIKO wa wananchi jijini Mwanza kwa maandamano ambayo yamefanywa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema), yanaashiria mambo mengi likiwamo la kukata tamaa ya maisha.
Maandamano yalibeba mada kuu tatu, kupinga mfumuko wa bei, kupinga malipo ya DOWANS na kudai kuharakishwa kwa mabadiliko ya katiba.

Chama Cha Mapinduzi, (CCM), kinachoongoza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinatakiwa kufanya kazi kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi, kikizingatia yote ya msingi yanayoibuliwa na vyama vya upinzani kwa kuwa mengi yanagusa maslahi ya umma.

Ikumbukwe kuwa maandamano yamefanywa siku na saa za kazi, lakini umati mkubwa uliyaitika na kuyashiriki kikamilifu ni ishara kuwa jamii ya Watanzania imebadilika, inahitaji mabadiliko ya kiuongozi.

Pia ikumbukwe maandamano hayo yamefanywa takribani miezi miwili tangu maandamano yaliyoandaliwa na Chadema jijini Arusha, Polisi wakatumia risasi za moto na kuuwa waandamanaji na watu wengine ambao hata hyawakuwamo katika maandamano, akiwemo raia mmoja wa Kenya.

Kitendo cha Chadema kuandaa maandamano mengine muda mfupi baada ya tukio hilo na yakapokewa kama ilivyoshuhudiwa ni ishara kwamba CCM inatakiwa kuacha mzaha na kuchukua hatua za kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwa raia wake.

Maandamano hayo yalianzia Uwanja wa Shule ya Msingi Buzuruga, yakapita kwenye Barabara za Nyerere, Pamba, Kenyatta, Uwanja wa Ndege na kuhitimishwa Uwanja wa Furahisha, kwa mkutano wa hadhara.

Kupitia mkutano huo, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, anaeleza kuwa hatua hiyo ni uzinduzi wa mkakati wa kuomba kibali kwa wananchi ili wakiunge mkono chama hicho kuiondoa CCM.

"Tumekuja kwenu kuomba kibali cha kuhakikisha mnatuunga mkono ili kuiondoa CCM, tumeanzia Mwanza kuzindua mkakati huu wa kupita tukifanya kazi hiyo…,"Mbowe anakaririwa akisema.

Wahenga walisema, "haba na haba, hujaza kibaba" na hata Roma haikujengwa kwa siku moja. CCM na jamii kwa ujumla itambue kuwa Watanzania sasa wanaanza kuwa na hulka mpya ambazo awali hawakuwa nazo. Yote haya ni kutokana na taifa kukumbwa mgawanyiko wa kitabaka.

Dhana kwamba yanayoendelea kutokea katika baadhi ya nchi barani Afrika hayawezi kutokea nchini kwa kigezo kwamba watanzania ni woga, watiifu, hawana ujasiri wa kufanya hivi au vile hayana mashiko kwa kuwa baadhi ya matukio yanathibitisha kuwa hali inaelekea kusiko.

Hakuna aliyetarajia kuwa askari wa kikosi cha kuzuia na kutuliza ghasia wanaweza kufika mahala penye vurugu, watu wakabaki na hata kuthubutu kuwarushia mawe lakini sasa, mambo hayo yanatokea, yanashuhudiwa.

Rejea tukio la kuvunjwa kwa maandamano ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM).

Kupitia mkutano wa jijini Mwanza, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibroad Slaa anatoa siku tisa kwa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kutoa kauli kuhusu kushamiri kwa vitendo vya ufisadi, malipo ya Dowans na suluhisho la kupanda kwa gharama za maisha kwa Watanzania.

Itakuwa heri endapo CCM litafanyia kazi yanayojiri kwenye maandamano na mikutano ya Chadema ili kurejesha imani ya jamii kwa viongozi wake ambayo imekwisha.

Kupuuza ushauri wenye mantiki kwa sababu tu umetolewa na kambi ya upinzani, tabia hiyo iachwe kwa sababu moja ya kazi ya vyama vya upinzani ni kuikosoa serikali hivyo endapo CCM inafahamu hilo basi ikubali kukosolewa.

Mengi ya mambo yanayozungumzwa na viongozi mbalimbali wa Chadema kupitia mkutano huo jijini Mwanza yapo dhahiri. Mengi ni vikwazo kwa wananchi wote bila kujali itikadi za kisiasa.

Mathalani ugumu wa maisha unaotokana na mfumuko wa bei. Katika baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, hata chakula kinachotumiwa na kundi kubwa la watu husani wanaofanya kazi kama mlo wa mchana, chips (viazi mviringo vinavyokaushwa kwenye mafuta) pia vimepanda bei.

Mohammed Abdallah, mfanyakazi ya kuandaa chakula hicho, Tabata Aroma wilayani Ilala, anasema sahani ya chips kavu (bila mayai, mishikaki wala vipande vya nyama ya kuku) imepanda kutoka Sh800 mpaka kufikia Sh1500

Baadhi ya maeneo ya katikati ya jiji kiasi hicho cha chakula kimepanda mpaka kufikia Sh1800 hali inayoelezwa kutokana na kupanda kwa bei ya gunia la viazi kutoka kati ya Sh55,000 na Sh70,000 mwishoni mwa mwaka jana mpaka kufikia Sh80,000 mwanzoni mwa mwaka huu.

Mafuta ya kula yanayotumiwa kupikia chakula nayo yamepanda kwa kati ya Sh4,000 mpaka Sh7000 kutegemea aina na kiasi cha mafuta. Gunia la mkaa pia limepanda kutoka S 38,000 mpaka Sh45,000

Dk Slaa anasema iwapo Serikali itakaa kimya Chadema kitaitisha maandamano nchi nzima kushinikiza mabadiliko kama ilivyotokea kwenye nchi za Misri na Tunisia.

"Rais Kikwete kuendelea kukaa kimya kutasababisha tuchukue hatua ya pili ambayo ni kuitisha maandamano Nchi nzima," anasema Dk Slaa

Jambo la pili deni la zaidi ya Sh94 bilioni, ambazo Kampuni ya Dowans inasema inalidai Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco).

Suala hilo ni kero kwa wananchi bila kujali itikadi zao na endapo deni hilo limetokana na umeme unaodaiwa kutumiwa nchini, haliwahusu raia wa Tanzania kwa kuwa wote wanalipa umeme wanaotumia.

Dk Slaa anasema; "Kamwe kodi ya wananchi haitotumika kuilipa kampuni hiyo kama wanataka ilipwe basi zitumike fedha za Rais Kikwete, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz."

Anataka kukoma kwa tabia ya wabunge wa CCM kuwazomea na kuwatisha wabunge wa Chadema ili wasiongee Bungeni kwani tofauti na hivyo wananchi watahamasishwa kuwazomea wabunge wa CCM majimboni kwao kama ilivyokuwa wakati wa kashfa ya ufisadi ndani ya Mfuko wa Madeni ya Nje ndani ya Benki Kuu, (BOT), EPA.



Kwa upande wake Mbowe, anawaomba wananchi waliokuwapo kwenye mkutano huo kuieleza Serikali ikiwa wapo tayari kudai haki zao kwa maelezo kwamba viongozi wa Chadema wakiongea, CCM wanasema wanaongopa, hawajawatuma.




Mbowe anahoji, "mnataka na Kikwete ajiuzulu pia?" wananchi wanamjibu kwa sauti "Ndiyo!" Mbowe anaeleza, "Sawa nimewaelewa kumbe mnataka Rais Kikwete naye ajiuzulu pamoja na Ngeleja na Waziri Mwinyi (Hussein) pia ajiuzulu…, hivyo wajiandae kwani inakuja babu kubwa kama ya Misri na Tunisia.
 
Chadema waanza kutoa cheche Send to a friend Tuesday, 01 March 2011 20:56

Elias Msuya
HIVI karibuni kumekuwa na mfululizo wa maandamano yanayofanywa na wananchi kwa lengo la kuwang'oa watawala katika baadhi ya nchi barani Afrika.

Mnamo Januari 13, Rais wa muda mrefu wa Tunisia Zine el-Abidine Ben Ali, alilazimika kukimbia nchi yake kufuatia shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi wake waliofanya ghasia kwa wiki kadhaa kumtaka kuacha madaraka.
Ben Ali aliyetawala nchi hiyo kwa miaka 23 aliondoka kwa ndege maalum na kukimbilia uhamishoni Saudi Arabia.

Moto wa mapinduzi ukazagaa hadi nchini Misri ambapo baada ya mwezi mmoja tu rais wa nchi hiyo Hosni Mubarak naye alitumiliwa. Kutimuliwa kwake kulikuja baada ya wananchi wa Misri kuandamana kwa siku 18 mfululizo wakimtaka Mubarak aondoke.

Mubarak ameitawala nchi hiyo kwa miaka 30 mfululizo akijilimbikizia mali huku wananchi wake wakimlalamikia kwa hali ngumu za maisha na kuongezeka kwa rushwa.

Moto huo haikuishia hapo, sasa umehamia nchini Libya ambapo wananchi nao wameanza kuandamana wakimtaka kiongozi wao Kanali Muammar Gadafi kujiuzulu.

Hata hivyo kwa wananchi wa Libya, mambo siyo rahisi kiasi hicho. Gadafi aliyedumu madarakani kwa miaka 42 ameshawatahadharisha wananchi wanaoandamana kuwa hataondoka madarakani, bali yuko tayari kufia hapo kama shahidi.

Kidogo kidogo hali hiyo inaanza kuambukiza Tanzania ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekuwa katika harakati za maandamano ambapo hivi karibuni kiliandaa maandamano makubwa jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa na wabunge kadhaa waliowaongoza maelefu ya waandamanaji katika kile walichosema kuwa ni kupinga kupanda kwa gharama za maisha, malipo kwa Kampuni ya Dowans na kupanda kwa gharama za umeme.



Katika mkutano wa hadhara uliohitimishwa katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, Dk Slaa ametoa siku tisa kwa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kutoa kauli kuhusu kushamiri kwa vitendo vya ufisadi, malipo ya Dowans na suluhisho la kupanda kwa gharama za maisha kwa Watanzania.



Dk Slaa anasema iwapo Serikali itakaa kimya basi Chadema kitaitisha maandamano ya nchi nzima ili kushinikiza mabadiko kama ilivyo katika nchi za Misri na Tunisia.


"Kitendo cha Rais Kikwete kuendelea kukaa kimya kitasababisha Chadema kuchukua hatua ya pili ambayo wataitisha maandamano nchi nzima," anasema Dk Slaa.


Dowans

Akizungumzia suala la Dowans, Dk Slaa amesema ujio wa mmiliki wa Dowans, Suleyiman Al Adawi ni mbinu za kutaka kuwahadaa Watanzania.



"Dowans haiwezi kulipwa kwa kodi za wananchi kutokana na kampuni hiyo kuwa mtoto haramu, mama na baba yake ni Richmond na hayo yote yanayofanyika Rais Kikwete anayajua sababu yanafanyikia katika Serikali ya Tanzania," anasema Dk Slaa.



Anasema Rais Kikwete ana maswali mengi ya kujibu kutokana na Dowans kwa sababu Serikali ilitoa fedha nyingi za wananchi za kuleta mitambo hiyo ya umeme na kununua vifaa ili Dowans izalishe umeme, lakini leo nchi ipo gizani.

Kupanda kwa gharama za maisha
Katika kipindi kifupi baada ya rais Kikwete kurudi madarakani, gharama za maisha zimepanda ghafla hasa kutokana na kupandishwa kwa gharama za umeme huku umeme huo ukipatikana kwa mgawo.

Dk Slaa ameliona suala hilo na kuonya kuwa kama umeme hautashushwa bei hali itakuwa mbaya zaidikwani hakutakuwa na uzalishaji kama ilivyokuwa awali.

Naye Mbunge wa Ubungo, John Mnyika anagusia kupanda kwa bei ya sukari mpaka kufikia Sh 2000 kwa kilo moja kutoka katika bei ya kawaida iliyokuwapo ya Sh 1600.

"Watanzania agizo hilo la Serikali limetokana na maandamano ya leo waliposikia tuna andamana kupinga mfumuko wa bei pamoja na Dowans kutokulipwa kwa kodi za wananchi na wao wakajifanya kutoa agizo hilo," anasema Mnyika.

Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje anasema kuwa ni aibu kwa wana-Mwanza kuchachuka na maisha wakati mkoa huu uonaongoza kwa kuwa na rasilimali nyingi ambazo kama zitasimamiwa ipasavyo zitawakomboa wananchi wake.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe anasema kama Serikali haitaweza kuinua maisha ya Watanzania kwa kuwaondolea ugumu wa maisha, wananchi wanaweza kutumia nguvu kukabiliana na mafisadi.

"Tumenyanyaswa, tumetishwa sasa tunasema kuwa tumechoshwa na tunasonga mbele kudai haki pamoja na uhuru na kama hawatoweza kutupatia nguvu zetu zitakuwa zaidi ya Libya," anasema Mbowe.


Anabainisha mpango wa Serikali wa kukodisha umeme kwa muda wa miezi minne na katika kipindi hicho wanazalisha umeme kwa kutumia kodi za Watanzania Sh 400 bilioni kulipa kampuni inayokodisha mitambo hiyo ya umeme kuwa ni ufisadi.


"Tumevumilia vya kutosha, safari hii ni ama zao ama zetu. Hatuwezi kukubali nchi imekaa miaka minne hakuna ufumbuzi wa umeme, taifa linalipa fedha za ajabu, hakuna anayejiuzulu na safari hii hatukubali,"anasema Mbowe 

Katiba 

Mbowe amewataka wananchi kuvumilia kwani japo Mbunge wa Ubungo John Mnyika alishapeleka hoja binafsi ya mabadiliko ya Katiba, haikujadiliwa. Hata hivyo anasema kuwa mjadala wa Katiba utaanza mwezi Aprili.

Maandamano ya Mwanza yamefanyika takribani miezi miwili tangu kutokee mauaji ya raia waliopigwa risasi na polisi mkoani Arusha, wakati walipokuwa wakizuia maandamano ya Chadema mkoani humo.


Katika tukio hilo la Januari 6, mwaka huu polisi wa Arusha walimwaga damu za watu kadhaa na wengine zaidi ya 30 walijeruhiwa miongoni mwao wakiwamo walioshiriki na wasioshiriki maandamano yaliyoandaliwa na Chadema.

Risasi za moto na mabomu ya machozi vilitumika katika jitihada za polisi kuzima maandamano hayo, wakitekeleza amri ya Mkuu wa Jeshi hilo, Ispekta Jenerali Said Mwema ambaye awali aliyapiga marufuku baada ya awali kuwa yameruhisiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye.

Je, Maandamano haya yatafikia ya Misri na Tunisia? 

Japo Maandamano haya yameanza kuonyesha cheche kwa utawala wa Rais Kikwete wapo wanaoona kuwa hayahusiani vuguvugu la mapinduzi yanayoendelea Afrika Magharibi.

Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Mbunda anasema kuwa maandamano ya Chadema hayahusiani nay ale ya nchi za Tunisia, Misri na Libya akitoa sababu kadhaa.

"Haya maandamano ya nchi za Afrika Kaskazini yamekuwa na hisia tofauti ikiwa ni pamoja na kuhusishwa na njama za nchi za Magharibi kutaka kuangusha tawala zenye nguvu za Afrika. Lakini kwa kweli nchi hizo zina matatizo ya msingi, viongozi wenyewe wamekaa muda mrefu madarakani. Watu baada ya kuona yamewezekana Tunisia wakaamua nao kuanzisha kwao," anasema Mbunda.

Hata hivyo anayatofautisha maandamano hayo na yale yanayoendelea nchini chini ya Chadema,

"Ukiangalia maandamano ya Tunisia, yalianzishwa na mtu wa kawaida tu. Lakini hapa kwetu wanasiasa ndiyo wameshika bango la maandamano. Leo utaona CUF kesho Chadema, siyo wananchi wenyewe wanaoanzisha".

Anavikosoa vyama vya upinzani akisema kuwa bado havijajenga imani kwa wananchi kiasi cha kuamsha hamasa kwao. Anavishauri vyama hivyo viungane kwanza ili kuaminika kwa wananchi.

"Maandamano hayo yanaweza yasipate nguvu kubwa kama tunayoona kwa wenzetu kwasababu kila chama kinafanya kivyake. Chadema wakiandamana, CCM na CUF hawaungi mkono, CUF wakiandamana, Chadema hawaungu mkono.
Bado ni mapema mno kwa Watanzania kuwa na moyo wa kuandamana hadi vyama hivyo vityakapomaliza kasoro zake za ndani na kuwaunganisha wananchi kwa pamoja ili kupigania mambo yao kama inavyofanyika nchi nyingine" anasema Mbunda.
 
Kasulumbayi: Wanasiasa wana wajibu wa kuwatumikia wanyonge Send to a friend Tuesday, 01 March 2011 20:40

Na George Maziku

"Wakati wote nashughulikia matatizo ya wananchi, natetea watu wenye matatizo, natumia akili, nguvu na mali zangu kusaidia watu wangu na hata wananchi kutoka maeneo mengine ndani na nje ya wilaya ya Maswa.

Hiyo ni kauli ya mbunge wa Maswa Mashariki, Sylvester Mhoja Kasulumbayi wakati alipofanya mahojiano na mwandishi wa makala haya wakati akihudhuria semina ya wabunge iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.

Kasulumbayi, mmoja wa wabunge wapya katika Bunge la sasa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa ameingia katika chombo hicho muhimu cha kutunga sheria, kupitia Chadema, anasema siku zote amekuwa karibu sana na watu wanyonge akitatua shida zao mbalimbali hususan manyanyaso na uonevu kutoka kwa watendaji wa serikali wasio waaminifu hususan polisi na maafisa watendaji wa kata na vijiji.

"Vijijini kuna matatizo mengi yanayowakabili wananchi wanyonge, polisi na maafisa watendaji wa kata na vijiji huwabambikiza kesi wananchi na kuwalazimisha kutoa rushwa, wanaporwa mali zao hususan mifugo kwa kutungiwa kesi mbalimbali ikiwemo kesi za mauaji, kwahiyo natumia muda wangu mwingi kushughulikia matatizo haya", anasema Kasulumbayi.

Kasulumbayi ambaye ni mwalimu kitaaluma, aliyelazimishwa na serikali kustaafu kazi baada ya kutakiwa kuchagua kati ya kazi na siasa, anasema aliingia katika siasa ili atoe mchango wake katika kuleta mabadiliko yenye manufaa kwa watanzania walio wengi kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Baada ya kuwatumikia Watanzania akiwa diwani wa kata ya Ipililo, Kasulumbayi aliamua kugombea ubunge mwaka 2010 kwa tiketi ya Chadema na kujipatia ushindi mkubwa.

"Niliamua kugombea ubunge ili kuchangia juhudi za maendeleo kwa wananchi wengi zaidi, nataka kutumikia watu wengi zaidi, natambua wapo wananchi wengi wanaohitaji utumishi wangu, ni wajibu wangu kujitokeza na kuwatumikia kwa moyo wangu wote, akili na nguvu zangu zote", anabainisha Kasulumbayi.

Kasulumbayi anasema kuwa kutokana na tabia yake ya kuwa karibu na watu na kuwasaidia kwa hali na mali, hakupata taabu sana wakati wa kampeni zake za kuomba ubunge na kwamba sehemu kubwa ya kampeni zake zilifanywa na wananchi wenyewe huku wengine wakijitolea kugharamia chakula, malazi, usafiri (magari) na mafuta kwa ajili ya msafara wake wa kampeni.

Kasulumbayi amepanga kuboresha kilimo na ufugaji katika jimbo lake kwa kuwaelimisha wakulima na wafugaji mbinu za kilimo cha kisasa na ufugaji wa kisasa kwa kuwatumia kikamilifu wataalam wa kilimo na mifugo.

"Ninakerwa mno na umaskini unaowazunguka wananchi walio wengi, ndoto zangu ni kuona watu wengi wakiboresha hali zao za kiuchumi, nataka kuwawezesha wananchi wengi hususan wakulima na wafugaji kukuza vipato vyao.

"Kwa hiyo, mipango yangu ya miaka mitano ni kuwawezesha wakulima na wafugaji kulima na kufuga kisasa ili kupata mazao mengi zaidi," anabainisha Kasulumbayi.

Kasulumbayi ni mmoja wa waasisi wa harakati za mageuzi nchini. Alijiunga na vyama vya upinzani tangu mfumo huo uliporejeshwa mwaka 1992 akiwa mwanachama wa Chama Cha Wananchi (CUF).

Amekuwa diwani kwa tiketi ya CUF kwa miaka 14 (1994-2008), mwenyekiti wa CUF wilaya ya Maswa na hatimaye mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho, wadhifa alioushikilia mpaka wakati anajiuzulu uanachama mwaka 2008.

Mwaka 2008 Kasulumbayi alijiunga na Chama cha Ustawi wa Jamii (CHAUSTA), cha James mapalala ambako alifanikiwa kuchaguliwa kwa mara nyingine tena kuendelea kuwa diwani wa kata ya Ipililo.

Hata hivyo, Kasulumbayi hajadumu katika CHAUSTA kwani mwaka 2010 alihama tena na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho alikitumia mwaka 2010 kugombea na kushinda ubunge wa jimbo la Maswa mashariki na udiwani wa kata ya Ipililo.

Akizungumzia kuhusu sababu zilizomfanya avihame vyama vyake vya awali, Kasulumbayi anasema ilitokana na vyama hivyo kushindwa kukidhi malengo na matarajio yake.
 
Kasulumbayi: Wanasiasa wana wajibu wa kuwatumikia wanyonge Send to a friend Tuesday, 01 March 2011 20:40

Na George Maziku

“Wakati wote nashughulikia matatizo ya wananchi, natetea watu wenye matatizo, natumia akili, nguvu na mali zangu kusaidia watu wangu na hata wananchi kutoka maeneo mengine ndani na nje ya wilaya ya Maswa.

Hiyo ni kauli ya mbunge wa Maswa Mashariki, Sylvester Mhoja Kasulumbayi wakati alipofanya mahojiano na mwandishi wa makala haya wakati akihudhuria semina ya wabunge iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.

Kasulumbayi, mmoja wa wabunge wapya katika Bunge la sasa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa ameingia katika chombo hicho muhimu cha kutunga sheria, kupitia Chadema, anasema siku zote amekuwa karibu sana na watu wanyonge akitatua shida zao mbalimbali hususan manyanyaso na uonevu kutoka kwa watendaji wa serikali wasio waaminifu hususan polisi na maafisa watendaji wa kata na vijiji.

“Vijijini kuna matatizo mengi yanayowakabili wananchi wanyonge, polisi na maafisa watendaji wa kata na vijiji huwabambikiza kesi wananchi na kuwalazimisha kutoa rushwa, wanaporwa mali zao hususan mifugo kwa kutungiwa kesi mbalimbali ikiwemo kesi za mauaji, kwahiyo natumia muda wangu mwingi kushughulikia matatizo haya”, anasema Kasulumbayi.

Kasulumbayi ambaye ni mwalimu kitaaluma, aliyelazimishwa na serikali kustaafu kazi baada ya kutakiwa kuchagua kati ya kazi na siasa, anasema aliingia katika siasa ili atoe mchango wake katika kuleta mabadiliko yenye manufaa kwa watanzania walio wengi kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Baada ya kuwatumikia Watanzania akiwa diwani wa kata ya Ipililo, Kasulumbayi aliamua kugombea ubunge mwaka 2010 kwa tiketi ya Chadema na kujipatia ushindi mkubwa.

“Niliamua kugombea ubunge ili kuchangia juhudi za maendeleo kwa wananchi wengi zaidi, nataka kutumikia watu wengi zaidi, natambua wapo wananchi wengi wanaohitaji utumishi wangu, ni wajibu wangu kujitokeza na kuwatumikia kwa moyo wangu wote, akili na nguvu zangu zote”, anabainisha Kasulumbayi.

Kasulumbayi anasema kuwa kutokana na tabia yake ya kuwa karibu na watu na kuwasaidia kwa hali na mali, hakupata taabu sana wakati wa kampeni zake za kuomba ubunge na kwamba sehemu kubwa ya kampeni zake zilifanywa na wananchi wenyewe huku wengine wakijitolea kugharamia chakula, malazi, usafiri (magari) na mafuta kwa ajili ya msafara wake wa kampeni.

Kasulumbayi amepanga kuboresha kilimo na ufugaji katika jimbo lake kwa kuwaelimisha wakulima na wafugaji mbinu za kilimo cha kisasa na ufugaji wa kisasa kwa kuwatumia kikamilifu wataalam wa kilimo na mifugo.

“Ninakerwa mno na umaskini unaowazunguka wananchi walio wengi, ndoto zangu ni kuona watu wengi wakiboresha hali zao za kiuchumi, nataka kuwawezesha wananchi wengi hususan wakulima na wafugaji kukuza vipato vyao.

“Kwa hiyo, mipango yangu ya miaka mitano ni kuwawezesha wakulima na wafugaji kulima na kufuga kisasa ili kupata mazao mengi zaidi,” anabainisha Kasulumbayi.

Kasulumbayi ni mmoja wa waasisi wa harakati za mageuzi nchini. Alijiunga na vyama vya upinzani tangu mfumo huo uliporejeshwa mwaka 1992 akiwa mwanachama wa Chama Cha Wananchi (CUF).

Amekuwa diwani kwa tiketi ya CUF kwa miaka 14 (1994-2008), mwenyekiti wa CUF wilaya ya Maswa na hatimaye mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho, wadhifa alioushikilia mpaka wakati anajiuzulu uanachama mwaka 2008.

Mwaka 2008 Kasulumbayi alijiunga na Chama cha Ustawi wa Jamii (CHAUSTA), cha James mapalala ambako alifanikiwa kuchaguliwa kwa mara nyingine tena kuendelea kuwa diwani wa kata ya Ipililo.

Hata hivyo, Kasulumbayi hajadumu katika CHAUSTA kwani mwaka 2010 alihama tena na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho alikitumia mwaka 2010 kugombea na kushinda ubunge wa jimbo la Maswa mashariki na udiwani wa kata ya Ipililo.

Akizungumzia kuhusu sababu zilizomfanya avihame vyama vyake vya awali, Kasulumbayi anasema ilitokana na vyama hivyo kushindwa kukidhi malengo na matarajio yake.
 
Dk Slaa akamatwa Send to a friend Wednesday, 02 March 2011 20:54

AACHIWA BAADA YA KUHOJIWA KWA SAA MOJA
Frederick Katulanda Bukombe na Shija Felician, Kahama
SIKU tatu baada ya Rais Jakaya Kikwete kuonya kile alichokiita ajenda ovu za Chadema kutaka kuvuruga nchi, jana Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa na wabunge wawili wa chama hicho wameitiwa mbaroni na polisi na kuhojiwa kwa saa kadhaa kwa madai ya kufanya mkutano wa wa uchochezi katika Jimbo la Maswa Mashariki.

Akituhutubia taifa katika utaratibu wake wa kila mwisho wa mwezi, Rais alionya akisema Chadema kimekuwa kikitumia fursa ya kufanya maandamano ya kidemokrasia huku wakiwa na lao jambo ambalo ni kuvuruga amani ya nchi.

Wakati mjadala wa hotuba hiyo ukiwa haujatulia, jana habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Diwani Athumani zilisema Dk Slaa alikamatwa mnamo saa 8: 05 asubuhi kwa madai ya kufanya mkutano katika Kijiji cha Malampaka wilayani Maswa kilichopo Jimbo la Maswa Mashariki, linaloongozwa na John Shibuda. Hata hivyo, Shibuda hajashiriki maandamano yoyote ya chama chake yanayoendelea.

Wabunge waliokamatwa pamoja na Dk Slaa ni Rachel Mashishanga na Chiku Obwao ambao ni wa viti maalum. Walikamatwa na polisi mjini Kahama baada ya polisi kuzingira Hoteli ya Pine Ridge walikokuwa wamefikia wakitokea Maswa.
Kamanda Athumani alisema viongozi hao wa Chadema ambao wako kwenye mpango wao wa maandamano ya amani Kanda ya Ziwa walikamatwa wakati wakijianda kwenda Wilaya ya Bukombe kuungana na wenzao kabla ya kuelekea mkoani Kagera kuendelea na mikutano yao.

Kamanda huyo alisema juzi, Dk Slaa na wabunge hao wakiwa wilayani Maswa walifanya maandamano na baadaye kufanya mkutano wa uchochezi katika Mji wa Malampaka bila kutoa taarifa Polisi na baadaye kukimbilia wilayani Kahama ambako waliungana na wenzao.

"Kawaida ukiwa na mkutano ni lazima ufike polisi na kutueleza kuwa unataka mkutano ama maandamano na sisi tutakubaliana na wewe baada ya kuridhishwa na sababu za mkutano wako," alieleza Kamanda huyo wa Polisi.
Alisema mkutano huo ulikuwa nje ya ratiba na barua yao kwa vile wakati wakitoa taarifa hawakueleza iwapo watafanya mkutano katika mji huo wa Malampaka.

"Walifanya mkutano huo nje ya ratiba ya kibali chao cha kufanya maandamano mkoani Shinyanga ambacho jeshi la polisi linacho hivyo ilikuwa kinyume cha taratibu na sheria, tulimfuata alipolala na kutaka kupata maelezo yake," alisema Kamanda Athumani.

Wakiongozwa na Ofisa Upelelezi wa Mkoa wa Shinyanga (RCO), Kashindye Hussen polisi waliwakamata viongozi hao wa Chadema na kuwapeleka Kituo Kikuu cha Polisi ch Wilaya hatua ambayo ilisababisha wafuasi wengi wa chama hicho kumiminika hapo kujua hatma ya viongozi hao.

Kamanda Athumani katika maelezo yake alisema Dk Slaa na wenzake waliieleza polisi kwamba wao wakiwa viongozi wa juu walifanya mkutano wao kwa nia njema na kwamba walisimama hapo wakijua kuwa viongozi wao wa wilaya walikuwa na mawasiliano na polisi.

Viongozi hao wote waliachiwa kwa dhamana na Kamanda huyo alisema jeshi lake linaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na hali hiyo ikiwa ni pamoja na kuwasaka viongozi wa wilaya ili kujua aliyehusika kuandaa mkutano huo.
Mbowe aliwaambia waandishi wa habari jana wilayani Bukombe kwamba Dk Slaa alifuatwa na ofisa wa polisi akitakiwa kufika kituoni wilayani Kahama ambako alikaa muda wa saa moja akitoa maelezo yake.

"Polisi walikuwa wakimshutumu kwa kufanya mkutano katika eneo ambalo halikupangwa, lakini Dk Slaa aliwaeleza kuwa kazi ya kuandaa mikutano siyo yake ni ya viongozi wa Wilaya ya Maswa hatua mbayo iliwafanya kumuachia na sasa tunaendelea na safari yetu ya Mkoa wa Kagera," alisema.

Baada ya kuruhusiwa kuondoka mjini Kahama Dk Slaa aliungana na viongozi wenzake wa Chadema na jama mchana walifika katika Mji wa Kemondo mkoani Kagera ambako walipokewa na viongozi wa chama hicho wa mkoa huo na kisha kuelekea mjini Bukoba.

 
Bukoba wafurika maandamano ya CHADEMA


Na Suleiman Abeid, Bukoba

PAMOJA na Rais Jakaya Kikwete juzi kuwaomba wananchi kususia maandamano yanayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), maelfu ya
wakazi wa mji wa Bukoba na vitongoji vyake jana wamepuuza ushauri huo na wamejitokeza kwa wingi kushiriki maandamano hayo.

Hata hivyo msafara wa viongozi wa CHADEMA ukiongozwa na Katibu Mkuu wake, Dkt. Willibroad Slaa ulichelewea kuwasili mjini Bukoba kutokana na kiongozi huyo kukamatwa na kuhojiwa na polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa saa kadhaa.

Polisi jana saa 1:15 asubuhi walimkamata Dkt. Slaa pamoja na wabunge wawili wa viti maalumu, Bi. Chiku Abwao na Bi. Rachel Mashishanga wakituhumiwa kwa kosa la kufanya mkutano katika eneo la Malampaka wilayani Maswa ambao haukuwa na kibali cha polisi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Bw. Diwani Athumani alisema jeshi lake liliamua kumkamata Dkt. Slaa na wabunge wawili wa viti maalumu ambao walihojiwa kutokana na kitendo hicho cha kufanya mkutano katika eneo hilo bila kibali kwa kuwa wangeweza kusababisha kutokea kwa uvunjifu wa amani.

Kamanda Athumani alisema baada ya mahojiano ya takriban saa moja na robo viongozi hao waliachiwa na kuendelea na msafara wao kuelekea mkoani Kagera ambako waliendelea na ratiba yao kama kawaida.

Viongozi wa CHADEMA kwa upande wao walikanusha madai ya kuendesha mkutano pasipo kibali kwa vile kila mkoa wanakopita kufanya maandamano ya amani na mikutano ya hadhara hutolewa kibali kwa wilaya zote za mkoa husika.

Dkt. Slaa alisema anazo habari zilizodai kwamba kukamatwa kwao haikuwa sababu ya tatizo la kibali bali ni katika juhudi za kutaka kuvuruga ratiba za shughuli ya maandamano ya amani na mkutano mkubwa wa hadhara uliokuwa umeandaliwa kufanyika mjini Bukoba jana mchana.

Alisema mipango hiyo inatokana na shinikizo la Balozi Khamis Kagasheki, ambaye ni mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi kutaka kukwamisha maandamano hayo yasifanyike katika jimbo lake, baada ya njama za awali za kuwazuia vijana waendesha pikipiki na baiskeli kushiriki katika maandamano
kukwama.

Mbali ya tukio hilo la kukamatwa kwa viongozi hao wa CHADEMA, maelfu ya wakazi wa mji wa Bukoba walijipanga kuanzia eneo la Kemondo Bay ambako ndiko walikowapokea viongozi hao na kuandamana kwa msafara wa magari, pikipiki na baiskeli hadi eneo la Rwamishenye ambako maandamano ya kutembea kwa miguu yalipoanzia.

Maandamano hayo yalipita katika mitaa mbalimbali ya mji wa Bukoba na kuishia katika uwanja wa Uhuru katikati ya mji huo ambako shughuli zote za kibiashara zilisimama kwa muda kabla ya Bw. Mbowe na Dkt. Slaa kuwahutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi.

Akihutubia katika mkutano huo, Dkt. Slaa aliwashukuru wakazi wa mji wa Bukoba na vitongoji vyake kwa kupuuza wito wa Rais Kikwete na kujitokeza kwa wingi na pia kwa jinsi walivyoshiriki katika maandamano ya amani.

Alisema wakazi wa Bukoba wameonesha jinsi gani ambavyo wanakiunga mkono CHADEMA kwa vile ndicho chama ambacho hivi sasa kinaonesha wazi nia halisi ya kuwakomboa Watanzania katika kupigania haki zao.

Hata hivyo alisema amepata taarifa ya kufanyika kwa ziara ya Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda ambapo aliwaomba wajitokeze kwa wingi katika mkutano utakaohutubiwa na Bw. Pinda, na wamuulize kuhusu fedha za Watanzania zilizopotea katika mazingira ya kifisadi ikiwa ni pamoja na zile zilizochotwa na kampuni ya Meremeta zaidi ya sh. bilioni 155.

Ndugu zangu mimi nakupongezeni sana kwa jinsi mlivyotuunga mkono katika uchaguzi mkuu uliopita, pamoja na mlivyoshiriki katika maandamano ya amani na mkutano wa hadhara leo hii (jana) bila kujali vitisho vya Rais Kikwete.

Rais wetu ni mtu wa ajabu ni sawa na kinyonga, anasahau sana, awali alikuwa akivilaumu vyama vya upinzani kwamba haviendi vijijini ambako ndiko waliko wananchi, lakini leo tumekwenda anapata hofu na kutaka kutuzuia kwa kisingizio kuwa tunawachochea Watanzania kufanya vurugu,� alieleza Dkt. Slaa.

Alisema CHADEMA haiwatii hofu Watanzania bali CCM na serikali yake ndiyo inayowatia hofu kutokana na kuwakumbatia matajiri wanaomiliki biashara zote kubwa na kupandisha bei za bidhaa ovyo na hivyo kupanda kwa bei za vitu kila siku na Watanzania kukabiliwa na ugumu wa maisha.

Alisema Rais Kikwete na waziri mkuu wake Bw. Pinda wanapaswa sasa kutoa majibu yote yanayoulizwa na Watanzania kuhusiana na ugumu wa maisha, Meremeta, Kagoda na Mwananchi Gold Mine ambazo zote kwa pamoja zimechota zaidi ya moja ya tano ya bajeti ya nchi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Taifa, Bw. Mbowe alisema pamoja na kupinga suala la malipo ya Dowans, lakini huenda chama chake kikawahamasisha wananchi kuingia tena mitaani kupinga mkataba mwingine unaofanana na ule wa Richmond ambao serikali inatarajia kuingia tena kwa kipindi cha miezi minne.

Bw. Mbowe alisema serikali hivi sasa inakamilisha mchakato wa kuingia mkataba mwingine mfano ya ule wa Richmond, ambapo itakodi mitambo ya kuzalisha umeme kwa kipindi cha miezi minne kuanzia Julai mwaka huu ambapo kila mwezi itakuwa ikilipa sh. bilioni 400.

Ndugu zangu serikali yetu inatushangaza, hivi sasa inajipanga kuingia mkataba mwingine wa kifisadi wa kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme kwa gharama ya sh. bilioni 400 kila mwezi ambapo pia itakuwa ikilipa sh. bilioni 23 kwa ajili ya kununulia mafuta, sasa hii tunaikataa pia,� alieleza Bw. Mbowe.

Leo viongozi wa CHADEMA wanahitimisha ziara yao katika mikoa ya kanda ya Ziwa ambapo pia kitatoa tamko rasmi kuhusiana na hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa mwishoni mwa mwezi uliopita akiituhumu CHADEMA kutaka kuchochea vurugu nchini.

 
Back
Top Bottom