Maandamano ya Chadema yatishia Serikali ya CCM madarakani

CHADEMA sasa haikamatiki
• Slaa atiwa mbaroni, aachiwa, apokewa kama rais Bukoba

na Sitta Tuma na Janet Josiah, Bukoba

amka2.gif
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea kuitikisa nchi kwa maandamano na mikutano yake ya hadhara kuzidi kuungwa mkono na umati mkubwa wa watu katika kila mkoa kinakopita.
Baada ya kuiteka mikoa ya Mwanza, Mara na Shinyanga, jana chama hicho kiliuteka kwa kishindo mji mzima wa Bukoba kwa mapokezi, maandamano na mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na wingi wa watu ambao kwa mujibu wa wenyeji wa hapa, haujapata kutokea huku Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk.Willbrod Slaa, akitoa tamko la msisitizo akisema "moto wa maandamano ya kudai mabadiliko sasa hautakoma, utaendelea nchi nzima."
Dk. Slaa aliwataka wakazi wa mji huo kumbana waziri mkuu, Mizengo Pinda, kuhusu kashfa mbalimbali za ufisadi na uzembe zinazoikabili serikali yake. Pinda anatarajiwa kuanza ziara yake mjini hapa leo.
Alisema CHADEMA itaendelea kufanya siasa kwa kuwafuata wananchi walipo na haitabakia kutegemea Bunge kama anavyotaka rais Kikwete wafanye kwani tayari chombo hicho cha wananchi kanuni zake zimechakachuliwa ili kudhibiti wabunge wa chama hicho.
Awali maelfu kwa maelfu ya wakazi wa mji wa Bukoba walitanda na kufunga barabara na mitaa ya mji huo kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nane mchana walipoanza maandamano makubwa ya kuelekea viwanja vya mashujaa mjini hapa kulikofanyika mkutano mkubwa wa hadhara. Maandamano hayo yalifanyika katika staili ya makundi huku kila kundi likichomoza katika mitaa tofauti na lingine na kujaza watu katika uwanja huo.
Baadhi ya waandamanaji hao walionekana wakiwa na mabango mbalimbali yaliyosheheni ujumbe wa kuilaani na kuipinga vikali serikali ya rais Jakaya Kikwete na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Wakati mji wa Bukoba ukiwa ni moja ya maeneo yaliyoathiriwa sana na janga la ugonjwa wa Ukimwi nchini, wananchi hao walionyeshwa kukerwa kwao na serikali ya CCM na katika moja ya mabango yao walisema hivi: "Keri ya ukimwi kuliko CCM".
Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa, alipokewa kwa nyimbo zilizokuwa zikimtaja kuwa yeye ndiye rais halali wa nchi hii.
"Rais, rais, rais, rais….", ulisikika umati wa watu ukiimba katika maandamano hayo.
Dk.Slaa aliingia kwa kishindo Bukoba baada ya kuachiwa huru na polisi mjini Kahama walikokuwa wanamshikilia akidaiwa kuwa alifanya mkutano bila kupata kibali wilayani Maswa.
Akizungumzia kukamatwa kwake katika mkutano huo wa hadhara jana, Dk. Slaa alisema "walionikamata walitumwa wanikamate kwa sababu Kikwete ananiogopa, lakini sasa hawatuwezi, CHADEMA haikamatiki"
Kabla ya tukio la kukamatwa kwa Dk Slaa juzi usiku askari polisi waliizingira hoteli ya Panich aliyokuwa amefikia kiongozi huyo.
Baada ya kufikishwa katika kituo cha polisi Mnadhimu huyo wa polisi alimhoji Dk Slaa: kwanini jana usiku ulikataa kuja polisi kama ulivyotakiwa? Dk Slaa alijibu "Nilihofia usalama wangu kwa sababu watu waionifuata hotelini sikuwatambua kwa sababu walikuwa wamevaa nguo za kiraia".
Mnadhimu Kamugisha alimuuliza tena kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani kwamba kwanini juzi alifanya mkutano Imalampaka bila kibali cha polisi? Dk Slaa alijibu, "nadhani mnafahamu kwamba chadema tunafanya maandamano na mikutano mikubwa ya hadhara na kila eneo tunalokwenda majimboni kuna ratiba, halafu ninyi mnauliza mambo kama haya hapa lakini juzi kiongozi wetu alipigwa jiwe na polisi hamjawakamata wahusika"
Mbali na Dk Slaa kukamatwa na kuhojiwa na polisi wa wilaya hiyo ya Kahama kwa zaidi ya saa 1:30 wabunge wengine wawili wa CHADEMA, Chiku Abwao na Rachel Mashishanga pia walishikiliwa kwa mahojiano na jeshi hilo.
Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Diwani Athumani (RPC) alipoulizwa sababu za jeshi lake kumkamata Dk Slaa wilayani Kahama badala ya kumkamatia wilayani Maswa alikofanyia mkutano huo, alisema waliogopa kumtia nguvuni wilayani Maswa kwa kuhofia uvunjifu wa amani.
 
Kafulila aifagilia CHADEMA

na Mwandishi wetu

amka2.gif
MBUNGE wa Kigoma Kusini David Kafulila (NCCR-Mageuzi) amemshangaa Rais Jakaya Kikwete kuogopa kazi nzuri inayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ya kuzungumza na wananchi.
Licha ya kumshangaa rais Kikwete kwa hofu aliyonayo amekipongeza CHADEMA na kusema chama chake kinajipanga kwenda kwa wananchi kwa kuwa ni utekelezaji wa kazi za siasa.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya NCCR-Mageuzi Dar es Salaam jana, Kafulila aliyewahi kuwa kada wa CHADEMA, alisema hofu ya kupinduliwa aliyonayo rais inatokana na watawala kushindwa kutimiza wajibu wao na kusababisha wananchi wengi kukata tamaa.
Mbunge huyo aliweka wazi msimamo wake kwamba licha ya kutofautiana kwenye baadhi ya mambo na chama alichokuwepo mwanzo alisema kazi nzuri inayofanywa na CHADEMA mikoani inastahili kuigwa na vyama vingine.
Alisema sababu ya kutoweka kwa hali ya amani nchini sio wanasiasa bali ni watawala kushindwa kutimiza wajibu wao hivyo ni rahisi kwa waliokata tamaa kufanya lolote watakaloona inafaa.
"Rais Kiwkete ni rais wetu namheshimu lakini katika hili natofautiana nae…CHADEMA wapo mikoani wanazungumza na wananchi, hiyo ni kazi ya chama chochote cha siasa binafsi nawapongeza, mimi na chama changu tunawaunga mkono. Wapo sahihi kabisa.
"…Hata sisi tutakwenda kwa wananchi tutafanya mikutano, unajua kuvunjika kwa amani ni matokeo ya watawala kushindwa kutimiza wajibu wao sasa wananchi wanakata tamaa wanaamua kufanya yao," alisema Kafulila.
 
CCM watimuana Kilimanjaro

na Beatrice Maina, Moshi

amka2.gif
HALMASHAURI kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoani Kilimanjaro imemfukuza uanachama wa chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Wilaya ya Hai mkoani hapa, James Mushi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo utovu wa nidhamu.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro,Steven Kazidi alisema Mwenyekiti huyo amefukuzwa uanachama na kikao cha halmashauri kilichofanyika Februari 28 mwaka huu.
Alisema sababu zilizosababisha mwenyekiti huyo kufukuzwa uanachama ni pamoja na kutokuwa muadilifu ndani ya chama na kupungukiwa na sifa ya kimaadili.
Alisema kwa mujibu wa Katiba ya CCM ya mwaka 1997, toleo la mwaka 2010 kifungu cha 93 kifungu kidogo cha 14 kinaeleza kumwachisha au kumfukuza uanachama mwanachama yeyote endapo itaridhia kwamba tabia na mwenendo wake vinamwondolea sifa za Uanachama.
Alisema kuwa kifungu hicho pia kinasema mwanachama anayeachishwa au kufukuzwa uanachama anaweza kukata rufaa kwa kamati kuu ya halmashauri ya CCM Taifa.
Kazidi alisema kutokana na uwezo huo wa kikatiba Halmashauri hiyo ya mkoa Imetumia mamlaka hiyo kumtimua Mushi, kutokana na kuonekana kuwa tabia yake na mwenendo wake vimemwondolea sifa ya kuwa mwanachama wa chama hicho.

h.sep3.gif

Wastaafu jeshini wamuunga mkono Kikwete

Na Juddy Ngonyani

CHAMA cha Askari Wastaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (MUWATA) wamemuunga mkono Amiri Jeshi Mkuu, Rais Jakaya Kikwete kwa kuvionya
vyama vya siasa kuachana na tabia ya kuhamamisha maandamano na migomo kwa lengo la kuepuka uvunjifu wa amani ya nchi.

Aidha pia wananchi wametakiwa kuwa waangalifu na maandamano pamoja na migomo hiyo inayodaiwa kupangwa na baadhi ya wanasiasa kwa kuwa madhara ya migomo hiyo na maandamano ni kwa wananchi wa kawaida na si kwa viongozi hao.

Wastaafu hao wametoa kauli hiyo katika uzinduzi wa chama chao ulioambatana na kukabidhiwa vyeti kwa wanachama wa chama hicho mkoa wa Rukwa, ikiwa ni siku mbili baada ya Rais Kikwete kutoa onyo hilo wakati akilihutubia taifa katika Hotuba yake ya mwishi wa mwezi februari, huku wakidai kuwa chama hicho hakina itikadi zozote za vyama kisiasa.

Akifungua kikao hicho mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Bw. Asem Mahuji alisema kuwa ni lazima serikali iwe makini na nyendo za baadhi ya vyama vya siasa kwa lengo la kutowagawa wananchi.

Awali, akizindua chama hicho Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Kanali John Mzurikwao kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Bw. Daniel Ole Njoolay, aliunga mkono vigezo vya mtu akitaka kuajiriwa serikalini ni lazima apitie katika mafunzo ya jeshi lolote hapa nchini kwa lengo la kutela ufanisi katika kazi.

Akisoma taarifa ya wastafu hao, Bw. Chrisant Mzindakaya alisema kuwa moja ya madhumuni ya MUWATA ni kuisaidia serikali katika majukumu yake ya kila siku ikiwemo ile ya ulinzi na usalama, huku akishauri askari hao wastafu watumike katika ulinzi katika taasisi mbalimbali za serikali pamoja na bandari zilizopo hapa nchini ikiwemo ile ya Kasanga mkoani Rukwa.

PHP:

      [IMG]http://img2.blogblog.com/img/icon18_edit_allbkg.gif[/IMG]

Huu mkakati wa kuwatumia wastaafu kushinikiza kuzima vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi kamwe halitazaa matunda yoyote ile itakuwa ni kijinga cha moto kwenye petroli cha kuhamasisha kuharakisha mabadilko tajwa................................
 
Mgaya wa TUCTA amvaa Lowassa Send to a friend Wednesday, 02 March 2011 19:55

mgayatucta.jpg
Naibu Katibu Mkuu wa Tucta,Nicholaus Mgaya

Gedius Rwiza

SIKU mbili baada ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa kuitaka serikali kuongeza mishahara ya wafanyakazi, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) limemjibu Lowassa likisema mbunge huyo ana ajenda yake ya siri na kwamba wafanyakazi hawahitaji msaada wake.

Mapema wiki hii akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha, Lowassa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, alisema uchumi wa dunia sasa umeyumba na hivyo kusababisha vitu vingi kupanda bei.

Kwa mujibu wa Lowaasa, kuendelea kuwalipa wafanyakazi mishahara kwa viwango vya sasa ni kuwapunguzia ari ya kutekeleza wajibu wao kwa umma.
Lowassa alisema kama Serikali ikiunda tume ya kupitia upya mishahara ya wafanyakazi, inapaswa kushirikisha viongozi wa vyama vya wafanyakazi, wataalamu wa uchumi na wadau wengine.

Lakini Naibu Katibu Mkuu wa Tucta,Nicholaus Mgaya akizungumza na gazeti hili jana alisema kitendo cha Lowassa kuutangazia umma kwamba kuna kila sababu ya wafanyakazi kupandishiwa mishahara ni njia ya kutafuta ajenda yake.

"Kama kweli katoa kauli hiyo kutoka moyoni mbona wakati yupo katika serikali za mitaa aliambiwa suala hilo akasema serikali haina uwezo wa kufanya hivyo sasa huruma imetoka wapi ghafla?,"alihoji Mgaya.

Alisema kuwa Shirikisho lao halihitaji msaada wa Lowassa na wala asitegemee kuombwa msaada na kutoka kwa wafanyakazi na kwamba suala hilo kwa sasa limebaki ndani ya serikali na Tucta,linajadiliwa hata kama ikitokea mishahara ikapanda sio kwamba Lowassa ndiye alifanya hivyo.

"Suala hilo liko serikalini linajadiliwa kwa hiyo kitendo cha Lowassa kutaka kuwadanganya wananchi na wafanyakazi ni dhahiri kuna kitu anataka ila anaona njia rahisi ni kutoa kauli ambazo ziko nje ya uwezo wake hatudanganyiki kwa njia hiyo,"alisema Mgaya.

Alisema kuwa anamshangaa kwani maslahi ya sekta binafsi hakuyazungumzia ila ameona azungumzie watumishi wa umma akidhani watampa ushirikiano hali ambayo alisema asitegemee kuungwa mkono na wafanyakazi kupitia porojo za kisiasa.
Alisema kuwa kitendo cha Lowassa kutaka serikali iunde tume nyingine ni kutaka kuharibu fedha za umma kwani kuna tume iliyoundwa na Rais ya kuchunguza ongezeko la mishahara ya watumishi wa umma ikisimamiwa na Deogratias Ntukamazina.

"Tume ya kwanza haijaleta majibu sasa iundwe nyingine ili iweje naona anajipendekeza kutafuta kura zetu 2015 lakini hatumtaki hatuwezi kushawishika kwa njia hiyo,"alisema Mgaya.

PHP:
Lakini Naibu Katibu Mkuu wa Tucta,Nicholaus Mgaya akizungumza na gazeti hili jana alisema kitendo cha Lowassa kuutangazia umma kwamba kuna kila sababu ya wafanyakazi kupandishiwa mishahara ni njia ya kutafuta ajenda yake. 

 "Kama kweli katoa kauli hiyo kutoka moyoni mbona wakati yupo katika serikali za mitaa aliambiwa suala hilo akasema serikali haina uwezo wa kufanya hivyo sasa huruma imetoka wapi ghafla?,"alihoji Mgaya.

Kubwa ya yote ni kuwa lowassa aache ushambenga.........................tatizo siyo mishahahra kuwa ni midogo bali tatizo ni kuwa hakuna uzalishaji unaokidhi mahitaji ya jamii..................................Mugabe azliongeza mishahara maradufu bila ya kuongeza tija matokeo yake ni kuwa mfumuko wa bei ulifuta amana za watu wote ikiwemo serikali hiyo ya kijasusi..............................

Changa moto kwetu ni namna gani tutaongeza tija na pa kuanzia ni kuwa na katiba mpya iliyoandikwa na wawakilishi wetu tuliowachagua wenyewe na kuiandika katiba tajwa kupitia mkutano mkuu wa katiba na lengo likiwa ni kufuta uwakilishi haramu ambao ndiyo umezaa viongozi wabovu ambao hawana mchango wowote ule zaidi ya kujenga hoja za kulipora taifa hili changa mno duniani.........................
 
FFU, wamachinga wapambana Dar
• Risasi zafyatuliwa wakati wakipinga kubomolewa vibanda vyao

na Lucy Ngowi na Asha Bani

amka2.gif
HALI ya usalama katika Jiji la Dar es Salaam jana ilikuwa ya taharuki baada ya Jeshi la Polisi kutumia tena risasi kuwasambaratisha wafanyabiashara wa soko la mitumba la Urafiki, maarufu ‘Big Brother', walioanza kufanya maandamano ya kupinga kubomolewa kwa mabanda ya biashara katika soko hilo.
Jana majira ya saa nne asubuhi, wafanyabiashara hao walianza kujipanga kwa maandamano huku baadhi yao wakiweka vizuizi barabarani na kuvunja vioo vya magari yaliyokuwa yakipita katika eneo hilo.
Wakati wafanyabiashara hao wakionyesha hasira zao kwa vitendo hivyo, ghafla polisi walifika katika eneo la tukio na kuanza kurusha risasi hewani ili kuwatawanya, hali ambayo ilifanya amani kutoweka.
Wafanyabiashara hao maarufu kama ‘machinga' wanaokadiriwa kuzidi 3,000 walibomolewa vibanda vyao vya kufanyia biashara juzi usiku na kueleza wamepata hasara ya zaidi ya sh milioni 200.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika eneo la tukio, maarufu kama ‘Big Brother', Mwenyekiti wa Soko la Urafiki Mitumba, Idd Toatoa, alisema kuwa bomoa bomoa hiyo ilifanyika juzi majira ya saa sita usiku, ambapo katapila mbili ndizo zilizokuwa zikibomoa ili kupisha mradi wa mabasi yaendayo kasi (Dart).
Mwenyekiti huyo alisema, bomoa bomoa hiyo imefanyika siku moja baada ya kupeleka barua yao katika ofisi za Halmashauri ya Kinondoni kwa ajili ya kuomba maeneo waliyokuwa wameyapendekeza kwa ajili ya kufanyia biashara zao, lakini kabla ya kujibiwa usiku wake ndipo tingatinga lilifika na kubomoa.
Aliyataja maeneo ya wazi waliyokuwa wameyapendekeza kuwa yapo Shekilango, japo serikali iliwataka waende katika maeneo ya ‘Engle' karibu na soko la ndizi, Soko la Makumbusho na Mburahati.
"Maeneo yaliyopendekezwa na serikali hatukuwa tayari kwenda kwa kuwa katika soko la ‘Engle' kule wanauza ndizi na nyanya, sasa mitumba na nyanya wapi na wapi?" alihoji na kuongeza kuwa, maeneo ya Soko la Makumbusho na Mburahati serikali ilitumia nguvu kubwa kuwapeleka wafanyabiashara kule, kwa kuwa hakuna biashara.
Kwa maelezo ya mwenyekiti huyo, tukio hilo ni kubwa na ni janga la kitaifa, hivyo anamuomba Rais Kikwete aingilie kati, vinginevyo hawataiunga serikali yake mkono.
"Ninamuomba Rais Kikwete aingilie kati suala hili, vinginevyo mimi kama kada wa CCM, kwa jinsi hii sitaweza kumuunga mkono," alisema.
Aliongeza kuwa, kutokana na suala hilo imeonyesha ni jinsi gani serikali inavyowadharau, hivyo wafanyabiashara hao hawatakuwa tayari kuirudisha tena serikali hiyo madarakani.
Pia alisisitiza kuwa kwa hatua hiyo ilipofikia anaona rais Kikwete ndiye atakuwa mtawala wa mwisho katika chama chake cha CCM, kwa kuwa hakuna mtu atakayempigia kura mgombea mwingine.
Mbali na hilo mwenyekiti huyo alisema kuwa bomoa bomoa hiyo imesababisha wizi wa mali za wafanyabiashara hao, ambao wengi wao wamekopa katika Chama cha Kuweka na Kukopa (Saccos), cha soko hilo.
"Kutokana na umoja wetu huu wa kuuza mitumba, CRDB walitupa milioni 250, Self milioni 150 na Pride milioni 50, na pesa hizo wamekopeshwa wafanyabiashara hawa, sasa unafikiri watazilipaje?" alihoji mwenyekiti huyo.
Katika hatua nyingine, mwenyekiti huyo alieleza kuwa bomoa bomoa hiyo ilipoanza alipigiwa simu na baadhi wa wafanyabiashara waliokuwa karibu na tukio, na alipokwenda kuwahoji wahusika alipigwa na kuumizwa maeneo mbalimbali mwilini mwake.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, alisema kuwa atatoa taarifa rasmi ya tukio hilo leo.
Wakati huo huo, Chama cha Uzalishaji na Maendeleo Tanzania (TAMADA) kimesema kutokana na serikali kuwadharau wafanyabiashara wadogo wadogo wako tayari kufanya maandamano nchi nzima kuishinikiza serikali kuwajali wananchi wake.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Abel Mwakabenga, alisema kuwa ni jambo la ajabu kwa serikali kutowajali wafanyabiashara wadogo licha ya kuwasilisha kilio chao kila kukicha.
Akizungumzia jengo la Machinga Complex, alisema kuwa wafanyabiashara wamekuwa na maisha magumu kutokana na kuwaweka katika mabanda mfano wa vibanda vya mbwa wa polisi huku wakiwa hawana mitaji ya kutosha na kodi kubwa wanayotozwa ili kuweza kufanya biashara katika mabanda hayo.
"Kwa sasa tumebahatika kuwaingiza wafanyabiashara mia sita na hamsini na nne lakini kutokana na kuwa na kodi kubwa ya kulipia choo, nauli, chakula na kodi ya pango ambapo wanalipa shilingi 180,000 fedha ambazo biashara aliyoiweka haizalishi kwa kiasi hicho bila kuwa na mkono wa serikali hawatafanikiwa tena," alisema Mwakabenga.
Naye Mratibu wa Habari, Utetezi na Mawasiliano, Godfrey Dhahabu, alisema kuwa wanaiomba serikali iangalie namna ya kutoa ruzuku kwa wafanyabiashara wa Machinga Complex ili kuweza kupunguza makali ya maisha sambamba na kuwasaidia wafanyabiashara hao ili jengo hilo lisiweze kuangukia mikononi mwa walichonacho.

h.sep3.gif

juu
 
PHP:
HALI ya usalama katika Jiji la Dar es Salaam jana ilikuwa ya taharuki baada ya Jeshi la Polisi kutumia tena risasi kuwasambaratisha wafanyabiashara wa soko la mitumba la Urafiki, maarufu ‘Big Brother', walioanza kufanya maandamano ya kupinga kubomolewa kwa mabanda ya biashara katika soko hilo.
 Jana majira ya saa nne asubuhi, wafanyabiashara hao walianza kujipanga kwa maandamano huku baadhi yao wakiweka vizuizi barabarani na kuvunja vioo vya magari yaliyokuwa yakipita katika eneo hilo.
 Wakati wafanyabiashara hao wakionyesha hasira zao kwa vitendo hivyo, ghafla polisi walifika katika eneo la tukio na kuanza kurusha risasi hewani ili kuwatawanya, hali ambayo ilifanya amani kutoweka.
 Wafanyabiashara hao maarufu kama ‘machinga' wanaokadiriwa kuzidi 3,000 walibomolewa vibanda vyao vya kufanyia biashara juzi usiku na kueleza wamepata hasara ya zaidi ya sh milioni 200.

Penye dhuluma haki itaendelea kudaiwa tu.............................................na hakuna risasi ambayo itazima madai halali ya mnyonge................
 
Taifa la waoga ni ndoto kuwa imara kiuchumi Send to a friend Wednesday, 02 March 2011 20:18

gaddafi.jpg
Na Dismas Lyassa
KWA namna inavyoonekana ni kwamba ni vigumu na huenda ni jambo lisilowezekana kwa taifa ambalo watu wake ni wapole sana kuwa na maendeleo ya haraka kiuchumi.

Kwanini kwa sababu viongozi wezi wanaweza kujifanyia kadri wanavyotaka, kwa maana ya kuiba kadri wanavyotaka, huku wakiamini kuwa wanaowatawala ni sawa na mbwa koko, hawajui kubweka wala kukaripia.

Taifa likiwa na watu ambao kazi yao ni kusema ‘hewala Mungu atanilipia' ni dalili mbaya. Ni dalili kuwa litakuwa maskini hadi mwisho wa dunia. Kwa namna inavyoonekana ni kuwa imefikia wakati, wananchi wanapaswa kubadilika na kusema hapana kwa kila aina ya ukandamizi ambao wanafanyiwa.

Maendeleo ya taifa lolote duniani au ya mtu yeyote, huwa yanakuja kwa kutafutwa. Ni makosa kuamini maendeleo huja yenyewe kama upepo. Lakini pia wananchi wanapaswa kufahamu kuwa wao ndio wenye nguvu kuliko serikali au viongozi wote walioko madarakani.

Ilivyo ni kwamba nchi inayoheshimu demokrasia, wananchi ndio wanaokuwa na nguvu na kwa ujumla huwa wanaogopwa. Ukiona taifa ambalo wananchi wanaiogopa serikali, ni dalili kuwa hiyo ni serikali ya kidikteta.
Serikali ni nini? Kwa lugha rahisi tunaweza kusema ni chombo ambalo kimewekwa na wananchi ili kiwaongoze katika kutimiza matakwa yao wananchi (sio matakwa ya viongozi).

Ni kwamba tuko wananchi wengi, kwa hiyo haiwezikani kwa kila mtu kuwa kiongozi, ndio maana tunakuwa na utaratibu wa kuchagua watu ambao watakuwa wakituongoza katika kuharakisha maendeleo ya taifa, usawa wa kijamii na mambo mengine kama haya.

Hata hivyo inavyoonekana ni kwamba karibu wengi wa wale ambao wanaingia madarakani, wanapokuwa madarakani huwa hawajali tena maslahi ya wananchi wao, bali wanachoangalia zaidi ni namna gani wanaweza kubaki madarakani na kufanya mambo wanayoyataka, sio yale ambayo wananchi wanayataka.
Tumeshuhudia hasira za wananchi katika mataifa mbalimbali zinazoonyesha ni kwa kiasi gani wamechoshwa na viongozi wasiojali maslahi yao.

Kwa mfano sasa utawala wa Kanali Muammar Gaddafi wa Libya, kwa namna unavyoonekana ni vigumu kwake kuepuka kuondoka madarakani. Kama sio kuondoka kwa hiari, huenda hatima ya maisha yake isiwe nzuri kwa jinsi ambavyo imeanza kuonekana wazi kwamba hata wale wanaompinga, baadhi yake wameelezwa kuanza kutumia silaha kujilinda.
Gaddafi anakuwa kiongozi mwingine, baada ya Rais wa Tunisia, Zine Abedine Ben Ali pamoja na Rais wa Misri, Hosni Mubarak kutimuliwa Ikulu kwa nguvu na wananchi.

Kama ilivyokuwa kwa Ben Ali na Mubarak, Serikali ya Kanali Gaddafi aliyeitawala Libya kwa miaka 41 sasa nafasi yake kuendelea kuiongoza Libya ni finyu mno, kwani tayari hata baadhi ya wanajeshi wake wameachana naye.
Gaddafi, kiongozi ambaye amedumu madarakani kwa muda mrefu huenda kuliko viongozi wote barani Afrika huku akijipambanua kama 'Mfalme wa wafalme' wa Afrika na kutumia umaarufu wake kutaka kuleta Muungano wa Dola za Afrika, wazo ambalo hata hivyo, halikutekelezeka ameitawala Libya tangu alipofanya mapinduzi ya kijeshi mwaka 1969.

Gaddafi ameweka historia kwa majigambo na kutumia askari walinzi wa kike, kutotumia hoteli za kisasa kila anapokwenda safari nje ya nchi yake na kutumia mahema binafsi ya kifahari kama makazi awapo ugenini, huku akijitapa kuwa anasaidia sana wananchi wake kiuchumi.

Hata hivyo, hali halisi inaashiria kuwa sasa huenda ni zamu ya kiongozi huyo machachari kukumbwa na nguvu ya umma na kuachia madaraka. Wananchi wanaandamana hasa wakipinga kuwepo kwake madarakani kwa miaka mingi, huku pia baadhi wakilalamikia hali ngumu ya maisha.

Uchumi duni umekuwa ni tatizo kuu duniani na huenda likasababisha wananchi kuacha ile hali ya woga ambao wamekuwa nao dhidi ya viongozi wakiwemo wale wanaowanyanyasa na kuwaburuza kama mbwa.
Kwa bahati nzuri, Jumuiya ya kimataifa nayo inawaunga mkono waandamanaji baada ya kutokea mauaji yanayofananishwa na 'mauaji ya halaiki', ambapo Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki-moon amemkemea akimtaka kuacha mara moja mauaji.

Tayari Gaddafi ameanza kupata pigo ikiwemo kuondokewa na baadhi ya washirika wake, akiwemo balozi wake mdogo katika Umoja wa Mataifa, Ibrahim Babbashi aliyetangaza kujizulu kutokana na mauaji ya zaidi ya watu 300 wanaoelezwa kupoteza maisha kwa kushambuliwa na askari watiifu kwa kiongozi huyo.

Maofisa wengine wawakilishi wa Libya katika balozi nchini Australia, China, India na Malaysia, walitangaza kujitenga na Serikali ya Gaddafi wakieleza kwamba amepoteza uhalali wake mbele ya umma wa Libya.

Hata baada ya uvumi kwamba kiongozi huyo alikimbia katika mji wa Tripoli juzi usiku na kuelekea nchini Venezuela, Gaddafi alizungumza kupitia televisheni akieleza kwamba taarifa hiyo ni ya uongo na yeye ndiye kiongozi mkuu wa taifa hilo. Kanali Gaddafi alitokeza kwa muda mfupi na kutumia sekunde chache katika televisheni ya taifa, ambayo ilisema alikuwa akizungumza nje ya nyumba yake mjini Tripoli.

Iko haja kwa serikali katika mataifa mbalimbali kuheshimu matakwa ya wananchi wao ili kuepusha kama haya ambayo yametokea Libya na kwingineko.
Dismas Lyassa ni mwandishi wa makala gazeti la Mwananchi.
 
PHP:
Uchumi duni umekuwa ni tatizo kuu duniani na huenda likasababisha wananchi kuacha ile hali ya woga ambao wamekuwa nao dhidi ya viongozi wakiwemo wale wanaowanyanyasa na kuwaburuza kama mbwa.
Kwa bahati nzuri, Jumuiya ya kimataifa nayo inawaunga mkono waandamanaji baada ya kutokea mauaji yanayofananishwa na 'mauaji ya halaiki', ambapo Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki-moon amemkemea akimtaka kuacha mara moja mauaji.

It is true............................manmade poverty is the ticking bomb waiting to explode..............................
 
Jana usiku mida ya saa nne usiku nilikuwa nabadilisha badilisha channel bahati mbaya au nzuri nikaangukia TBC1, Nilikutana na kipindi maalum kilichokuwa kinajadili hotuba ya Rais ya mwisho wa mwezi wa pili.

Kilichonishangaza ni kwamba serilkali kupitia waziri ofisi ya rais mahusiano na uratibu, Ndg. Steven alijigamba kwamba CDM haina haki na haina uwezo wa kuindoa CCM madarakani kupitia maandamano yanayoendelea hivi sasa kanda ya ziwa.

Gabriel Zakaria ambaye ndio mwandishi aliyekuwa anamuhoji waziri aliendelea kumchokonoa Ndg. Wassira, kwamba ni nini hofu ya serikali kuhusu hayo maandamano kama wao wenyewe serikali wanayaruhusu na ni haki ya kikatiba kuandamana na kukusanyika, jamaa aliendelea kujiumauma huku akisoma ibara kadha wa kadha za katiba, mara sheria za usalama wa taifa na sheria za vyama vya siasa ambazo CDM wanafunja lkn hakusema watachukua hatua gani kuwadhibiti zaidi ya kusema wanachochea wananchi.

Je hakuna sheria ambayo inaweza kutumika kumbana mchochezi?

Au ndio kuweweseka kwa serikali ya bwana JK?

Naomba wataalamu wa sheria watuelimishe.
 
Chadema's defence Send to a friend Tuesday, 01 March 2011 22:16

dogombowepress.jpg
Chadema National Chairman Mr Freeman Mbowe

By Frederick Katulanda, The Citizen Reporter Kahama. The Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) came out fighting yesterday describing President Jakaya Kikwete's criticism of the party's demonstrations and rallies as signs of desperation on the part of the government.
Addressing a number of rallies in Shinyanga and Kahama districts yesterday, the Chadema national chairman, Mr Freeman Mbowe, said the era of threats was long gone and that President Kikwete should concentrate on solving the numerous problems "created by his leadership".

Insisting that the President had failed to solve major problems facing Tanzanians, Mr Mbowe said he was ready to show him how the country could be run successfully if given the chance.

"Let him give me the chance to show him how to manage the country... Chadema is able to run this country successfully because Tanzania has abundant resources which, if properly used, can improve the economy beyond its current status," he noted, adding: "We have given the President nine days to solve the problems; if he cannot do it then let him give us the mandate and we will show him how the problems can be solved within the given timeframe."

Addressing a rally in Isaka, Mr Mbowe said Chadema was not going to be cowed by President Kikwete's harsh words as what the party was doing was within the law.

There was a huge turnout at Kahama town to receive Mr Mbowe and his team when they arrived. The demonstrators walked for about five kilometres to the sports stadium where the Chadema leader addressed a rally before he left for Bukombe. However, he was stopped at Masumbwa where he addressed another rally.

"President Kikwete has suggested that the proper way of changing the government is through elections and as such we should do our work in Parliament. I am telling him that we will not go to Parliament because whenever we raise pertinent issues in the law-making organ they heckle us because they have a numerical advantage. Because they steal elections, our only hope is to use people's power... We have been in only three regions and he has started to lament?" he wondered.

Mr Mbowe urged wananchi to stand firm and demand their rights, noting that it was because of their extreme leniency that the CCM government had failed to deliver services to them. Giving an example of the rise in sugar prices, he said the government started to look into the issue after Chadema condemned the increase.

Elsewhere, there were mixed reactions to the President's speech, which was delivered on Monday evening, with some noting that Mr Kikwete was justified to rebuke Chadema.

Others, however, hit at the President noting that Chadema as a political party had the right to organise demonstrations, especially after the government failed to improve the lives of a majority of Tanzanians as it had promised in the past.

They censured President Kikwete for trying to use his power to threaten wananchi for demanding their basic rights, something which they said was undemocratic.

In his televised address, the President urged the public to ignore the opposition party and focus on safeguarding the country's peace. He stated that Chadema's move to organise rallies around the country was bent on disrupting peace.

Dr Azaveli Lwaitama of the University of Dar es Salaam said he was not surprised by President Kikwete's statement as he was using old tricks of discouraging demonstrations by trying to win the support of citizens' through the issue of peace. Dr Lwaitama argued that it would have not been a problem if Mr Kikwete had addressed the nation as the ruling party chairman, as his speech would have been regarded as a political stetement.

"But since he made the address as the Head of State, his speech might be acted upon by the Police Force as an order from their Commander-in-Chief to block Chadema from conducting more rallies," he said. He added: "That is where the chaos might begin... Because protesters do not carry weapons, I don't think that Chadema's demonstrations are aimed at disrupting peace."

The NCCR-Mageuzi national chairman, Mr James Mbatia, supported President Kikwete's sentiments, noting that Chadema's demonstrations could lead the nation into chaos.

"Issues of national interest could be resolved through round table discussions and not demonstrations. Harsh statements in the ongoing demonstrations may plunge our country into chaos," he warned.

But in a quick reaction, the Legal and Human Rights Centre (LHRC) executive director Francis Kiwanga, said the government should not stop Chadema from demonstrating since that was their right.

"The only thing that the government could do is to ensure a peaceful environment for demonstrations," he said.
But Prof Ibrahim Lipumba, the national chairman of the opposition Civic United Front (CUF) joined ranks with Mr Mbatia, noting that Chadema had ulterior motives behind the demos.

Mr Lipumba said some of the statements made in the demonstrations could trigger unrest in the country.

Additional reporting by Bernard Lugongo (Dar), Hawa Mathias (Mbeya) and Zulfa Mfinanga (Shinyanga)

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Last Updated on Thursday, 03 March 2011 08:11 Comments

12

+1 #18 VOICE OF THE PEOPLE 2011-03-02 20:51 There is a political tactic of deverting from real issues when the rulling class is in a crisis. JK is diverting from really issues that are pertinent and Tanzanians are facing. CHADEMA is not an issue here Mr. President, address issues that face our people. After all you have no option that is what you promised a forthnight ago during your campaigs. The issues raised by CHADEMA are true, you dont have to be a political analyst to see them if you live in Tanzania. Why cant JK adress them. I must be frank I dont see the conection between the the truth spoken by opposition and the breakage of Peace in the countr. Actually what will break the peace of this country are the greavances of wananchi that have been caused by hardships they are facing and they have harboured them in their hearts. MR. President we wananchi we are suffering. Those who are puting their business in place are discouraged by bomoabomoa to pave the way for this and that. Where shall we go?
Quote

+1 #17 uhuru 2011-03-02 19:04 what peace r they referring to? the peace of a certain elite sleeping in their air conditioned rooms, driving in a poor country expensive $70-90, 000 gas guzlers, (while ppl die on the streets of starvation) failing to protect the lives of innocent ppl by "negligence" bomb blasts!!!! & failing to bring to justice the criminals that are milking my beloved Tanzania dry!!!!! ALL this has been going on for the past two decades!!! What is sad is that not one, not one, of the alleged accused gvt. servant has been brought to justice!!! There has been NO accountability! !!! None!!!!
Quote

+3 #16 Venansio 2011-03-02 17:21 It's shocking that Prof Lipumba and Mr Mbatia can scoff at people exercising their democratic rights (freedom of assembly and association). It's clear now that only Chadema would guarantee such rights if it took over government. Demonstrators do not need threats and condemnation; they need protection instead! Clearly, they've not hurt a fly since they started and could end peacefully if not attempt is made to disperse them. Please let them be!
Quote

+2 #15 dunia19 2011-03-02 17:18 A simple but true reality: where there is NO JUSTICE, there can be NO PEACE.
Quote

+1 #14 Rahim 2011-03-02 16:33 What is the purpose of the so called PEACE if my family and I sleep empty stomach? I can't take my kids to school? I can't afford bus fare? I can't afford descent medical care? What is the "PEACE" for? Those are old tricks..as young people we are not ready to see our selves suffering including our children...CCM boasts those "wazee wa vijiweni" who do nothing but play cards whole day and admiring young girls...when you pass they are like "Kijana naomba msaada"..No! I will not be fooled...so CHADEMA we are ready to take to the streets for the sake of this beautiful country.
Quote

+1 #13 Mzalendo 2011-03-02 15:17 Quoting Beano:
Quoting Ruta:
Come on Mr Mombasa do your maths. Have you performed your statistics to justfy your claims? How did you calculate this "mass support?" I tell you if CCM today call its supporters into the streets, you will know what is mass support. Like it or not CCM still enjoys mass following in Tanzania.

Majority will not alter the fact. Let them be more than the numerals in number but you know well that we are suffering from CCM bureaucracy. BETTER TEAM UP WITH A DOZEN OF WISE THAN OVERWHELMING MAJORITY OF FOOLS. Most of the CCM supporters you are insinuating are kinamama and they are after khanga and vitenge but not the future

Now this is what is meant by political immaturity. The ability to hurl expletives and insults rather than to make valid points. Way to go Beano.

Quote

+2 #12 Let CHADEMA be! 2011-03-02 14:53 Ruta makes a good point when he says CHADEMA should be pressuring the government to act on its promises, that is the more sensible route. But it is wrong to suggest they have no right to call for peaceful protests. They can choose to wait till 2015, or they can decide they want to act now. As long as it is legal/constitutional, why are people getting their boxes in a twist?
Quote

0 #11 Beano 2011-03-02 14:42 Quoting Mahamed:
Mzalendo and Ruta make a lot of sense. I suggest you spread this words to all Tanzanians-beginning with your own families. I have recently visited some parts of the country, only to be shocked by the level of ignorance Tanzanians have been led into, by the pathetic Chadema's propoganda. I am neither a CCM member, nor a supporter, but I want to be realistic.

Being pathetic is a little better than being PATHETIC FOOL. If we real think that what CHADEMA is up to is 2015 state house propaganda, do we take into account what had been done by CHADEMA so far? If u really believe that we have a little of good will in what CCM is doing with power, should we return the EPA money to those thieves because it was CHADEMA motive to unmask them? Should we rejoice because someone have done 40% of his responsibilitie s or demand for the remaining 60? Fellow Tanzanians lets not prepare a way to be fooled. Lets be the conquerors of this stolen well-being of ours.

Quote

+2 #10 Beano 2011-03-02 14:24 Quoting Ruta:

-4 #9 Mahamed 2011-03-02 13:37 Mzalendo and Ruta make a lot of sense. I suggest you spread this words to all Tanzanians-beginning with your own families. I have recently visited some parts of the country, only to be shocked by the level of ignorance Tanzanians have been led into, by the pathetic Chadema's propoganda. I am neither a CCM member, nor a supporter, but I want to be realistic.
Quote

12
 
Chadema’s defence Send to a friend Tuesday, 01 March 2011 22:16

dogombowepress.jpg
Chadema National Chairman Mr Freeman Mbowe

By Frederick Katulanda, The Citizen Reporter Kahama. The Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) came out fighting yesterday describing President Jakaya Kikwete’s criticism of the party’s demonstrations and rallies as signs of desperation on the part of the government.
Addressing a number of rallies in Shinyanga and Kahama districts yesterday, the Chadema national chairman, Mr Freeman Mbowe, said the era of threats was long gone and that President Kikwete should concentrate on solving the numerous problems “created by his leadership”.

Insisting that the President had failed to solve major problems facing Tanzanians, Mr Mbowe said he was ready to show him how the country could be run successfully if given the chance.

“Let him give me the chance to show him how to manage the country... Chadema is able to run this country successfully because Tanzania has abundant resources which, if properly used, can improve the economy beyond its current status,” he noted, adding: “We have given the President nine days to solve the problems; if he cannot do it then let him give us the mandate and we will show him how the problems can be solved within the given timeframe.”

Addressing a rally in Isaka, Mr Mbowe said Chadema was not going to be cowed by President Kikwete’s harsh words as what the party was doing was within the law.

There was a huge turnout at Kahama town to receive Mr Mbowe and his team when they arrived. The demonstrators walked for about five kilometres to the sports stadium where the Chadema leader addressed a rally before he left for Bukombe. However, he was stopped at Masumbwa where he addressed another rally.

“President Kikwete has suggested that the proper way of changing the government is through elections and as such we should do our work in Parliament. I am telling him that we will not go to Parliament because whenever we raise pertinent issues in the law-making organ they heckle us because they have a numerical advantage. Because they steal elections, our only hope is to use people’s power... We have been in only three regions and he has started to lament?” he wondered.

Mr Mbowe urged wananchi to stand firm and demand their rights, noting that it was because of their extreme leniency that the CCM government had failed to deliver services to them. Giving an example of the rise in sugar prices, he said the government started to look into the issue after Chadema condemned the increase.

Elsewhere, there were mixed reactions to the President’s speech, which was delivered on Monday evening, with some noting that Mr Kikwete was justified to rebuke Chadema.

Others, however, hit at the President noting that Chadema as a political party had the right to organise demonstrations, especially after the government failed to improve the lives of a majority of Tanzanians as it had promised in the past.

They censured President Kikwete for trying to use his power to threaten wananchi for demanding their basic rights, something which they said was undemocratic.

In his televised address, the President urged the public to ignore the opposition party and focus on safeguarding the country’s peace. He stated that Chadema’s move to organise rallies around the country was bent on disrupting peace.

Dr Azaveli Lwaitama of the University of Dar es Salaam said he was not surprised by President Kikwete’s statement as he was using old tricks of discouraging demonstrations by trying to win the support of citizens’ through the issue of peace. Dr Lwaitama argued that it would have not been a problem if Mr Kikwete had addressed the nation as the ruling party chairman, as his speech would have been regarded as a political stetement.

“But since he made the address as the Head of State, his speech might be acted upon by the Police Force as an order from their Commander-in-Chief to block Chadema from conducting more rallies,” he said. He added: “That is where the chaos might begin... Because protesters do not carry weapons, I don’t think that Chadema’s demonstrations are aimed at disrupting peace.”

The NCCR-Mageuzi national chairman, Mr James Mbatia, supported President Kikwete’s sentiments, noting that Chadema’s demonstrations could lead the nation into chaos.

“Issues of national interest could be resolved through round table discussions and not demonstrations. Harsh statements in the ongoing demonstrations may plunge our country into chaos,” he warned.

But in a quick reaction, the Legal and Human Rights Centre (LHRC) executive director Francis Kiwanga, said the government should not stop Chadema from demonstrating since that was their right.

“The only thing that the government could do is to ensure a peaceful environment for demonstrations,” he said.
But Prof Ibrahim Lipumba, the national chairman of the opposition Civic United Front (CUF) joined ranks with Mr Mbatia, noting that Chadema had ulterior motives behind the demos.

Mr Lipumba said some of the statements made in the demonstrations could trigger unrest in the country.

Additional reporting by Bernard Lugongo (Dar), Hawa Mathias (Mbeya) and Zulfa Mfinanga (Shinyanga)

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Last Updated on Thursday, 03 March 2011 08:11 Comments

12

+1 #18 VOICE OF THE PEOPLE 2011-03-02 20:51 There is a political tactic of deverting from real issues when the rulling class is in a crisis. JK is diverting from really issues that are pertinent and Tanzanians are facing. CHADEMA is not an issue here Mr. President, address issues that face our people. After all you have no option that is what you promised a forthnight ago during your campaigs. The issues raised by CHADEMA are true, you dont have to be a political analyst to see them if you live in Tanzania. Why cant JK adress them. I must be frank I dont see the conection between the the truth spoken by opposition and the breakage of Peace in the countr. Actually what will break the peace of this country are the greavances of wananchi that have been caused by hardships they are facing and they have harboured them in their hearts. MR. President we wananchi we are suffering. Those who are puting their business in place are discouraged by bomoabomoa to pave the way for this and that. Where shall we go?
Quote

+1 #17 uhuru 2011-03-02 19:04 what peace r they referring to? the peace of a certain elite sleeping in their air conditioned rooms, driving in a poor country expensive $70-90, 000 gas guzlers, (while ppl die on the streets of starvation) failing to protect the lives of innocent ppl by "negligence" bomb blasts!!!! & failing to bring to justice the criminals that are milking my beloved Tanzania dry!!!!! ALL this has been going on for the past two decades!!! What is sad is that not one, not one, of the alleged accused gvt. servant has been brought to justice!!! There has been NO accountability! !!! None!!!!
Quote

+3 #16 Venansio 2011-03-02 17:21 It's shocking that Prof Lipumba and Mr Mbatia can scoff at people exercising their democratic rights (freedom of assembly and association). It's clear now that only Chadema would guarantee such rights if it took over government. Demonstrators do not need threats and condemnation; they need protection instead! Clearly, they've not hurt a fly since they started and could end peacefully if not attempt is made to disperse them. Please let them be!
Quote

+2 #15 dunia19 2011-03-02 17:18 A simple but true reality: where there is NO JUSTICE, there can be NO PEACE.
Quote

+1 #14 Rahim 2011-03-02 16:33 What is the purpose of the so called PEACE if my family and I sleep empty stomach? I can't take my kids to school? I can't afford bus fare? I can't afford descent medical care? What is the "PEACE" for? Those are old tricks..as young people we are not ready to see our selves suffering including our children...CCM boasts those "wazee wa vijiweni" who do nothing but play cards whole day and admiring young girls...when you pass they are like "Kijana naomba msaada"..No! I will not be fooled...so CHADEMA we are ready to take to the streets for the sake of this beautiful country.
Quote

+1 #13 Mzalendo 2011-03-02 15:17 Quoting Beano:
Quoting Ruta:
Come on Mr Mombasa do your maths. Have you performed your statistics to justfy your claims? How did you calculate this "mass support?" I tell you if CCM today call its supporters into the streets, you will know what is mass support. Like it or not CCM still enjoys mass following in Tanzania.

Majority will not alter the fact. Let them be more than the numerals in number but you know well that we are suffering from CCM bureaucracy. BETTER TEAM UP WITH A DOZEN OF WISE THAN OVERWHELMING MAJORITY OF FOOLS. Most of the CCM supporters you are insinuating are kinamama and they are after khanga and vitenge but not the future

Now this is what is meant by political immaturity. The ability to hurl expletives and insults rather than to make valid points. Way to go Beano.

Quote

+2 #12 Let CHADEMA be! 2011-03-02 14:53 Ruta makes a good point when he says CHADEMA should be pressuring the government to act on its promises, that is the more sensible route. But it is wrong to suggest they have no right to call for peaceful protests. They can choose to wait till 2015, or they can decide they want to act now. As long as it is legal/constitutional, why are people getting their boxes in a twist?
Quote

0 #11 Beano 2011-03-02 14:42 Quoting Mahamed:
Mzalendo and Ruta make a lot of sense. I suggest you spread this words to all Tanzanians-beginning with your own families. I have recently visited some parts of the country, only to be shocked by the level of ignorance Tanzanians have been led into, by the pathetic Chadema's propoganda. I am neither a CCM member, nor a supporter, but I want to be realistic.

Being pathetic is a little better than being PATHETIC FOOL. If we real think that what CHADEMA is up to is 2015 state house propaganda, do we take into account what had been done by CHADEMA so far? If u really believe that we have a little of good will in what CCM is doing with power, should we return the EPA money to those thieves because it was CHADEMA motive to unmask them? Should we rejoice because someone have done 40% of his responsibilitie s or demand for the remaining 60? Fellow Tanzanians lets not prepare a way to be fooled. Lets be the conquerors of this stolen well-being of ours.

Quote

+2 #10 Beano 2011-03-02 14:24 Quoting Ruta:
Come on Mr Mombasa do your maths. Have you performed your statistics to justfy your claims? How did you calculate this "mass support?" I tell you if CCM today call its supporters into the streets, you will know what is mass support. Like it or not CCM still enjoys mass following in Tanzania.

Majority will not alter the fact. Let them be more than the numerals in number but you know well that we are suffering from CCM bureaucracy. BETTER TEAM UP WITH A DOZEN OF WISE THAN OVERWHELMING MAJORITY OF FOOLS. Most of the CCM supporters you are insinuating are kinamama and they are after khanga and vitenge but not the future

Quote

-4 #9 Mahamed 2011-03-02 13:37 Mzalendo and Ruta make a lot of sense. I suggest you spread this words to all Tanzanians-beginning with your own families. I have recently visited some parts of the country, only to be shocked by the level of ignorance Tanzanians have been led into, by the pathetic Chadema's propoganda. I am neither a CCM member, nor a supporter, but I want to be realistic.
Quote

12
 
Kuna lijitu chonganishi kwenye hii sredi, mimi naondoka hadi litoke
 
Back
Top Bottom