Maandamano ya Chadema yatishia Serikali ya CCM madarakani

Dk. Slaa: Nchi haitatawalika
• Anasa waraka wa siri CCM, afichua wizi wa mabilioni Hazina

na Edward Kinabo

amka2.gif
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.Willbrod Slaa, sasa ametamka rasmi kwamba nchi haitatawalika, kwani chama chake hakiko tayari kuona Watanzania wakiendelea kuwa katika hali ngumu ya maisha, huku Chama cha Mapinduzi (CCM) kikitekeleza mkakati wa siri wa kuwajaza matumaini hewa badala ya kutatua matatizo yao.
Dk. Slaa ameeleza kuunasa waraka wa siri wa CCM ambao ndani yake chama hicho kimekiri waziwazi kupoteza ladha kwa umma, huku mkakati pekee wa kujinusuru ukielezwa kuwa ni kubadili sura za viongozi wa chama hicho ili kuwajengea matumaini mapya Watanzania.
Kwa mujibu wa Dk.Slaa, waraka huo wenye mhuri mkubwa wa neno “siri” uliandaliwa na baadhi ya wataalam wa CCM waliofanya tathmini ya hali ya chama chao kisiasa na kuuwasilisha kwa viongozi wa juu wa chama hicho ambao tayari wameanza kuufanyia utekelezaji wa “kujivua gamba” kwa lengo la kuwapa matumaini hewa wananchi.
Dk. Slaa alifichua siri za waraka huo wakati akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja wa shule ya sekondari Msakila mjini Sumbawanga ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya chama hicho mkoani Rukwa, baada ya kuutikisa mkoa wa Mbeya kwa maandamano na mikutano ya hadhara kwa siku tatu mfululizo.
Alisema katika waraka huo CCM imekiri kuwa haikubaliki kwa Watanzania na kwamba iliporomoka sana katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, lakini badala ya kurejesha tunu za taifa kama uadilifu, upendo, amani, umoja na uwajibikaji wa kuleta maendeleo yatakayoirejeshea imani toka kwa wananchi, chama hicho kimeamua kubadili tu sura za viongozi wake wa kitaifa.
“CHADEMA tunafanya mambo kwa utafiti. CCM wana waraka wa siri uliowafanya wajivue gamba lakini wanaume tayari tumeshaunasa, tena una mhuri mkubwa wa neno siri lakini tayari tunao. Katika waraka wao CCM wamekiri wenyewe kwamba hawakubaliki tena kwa Watanzania walio wengi, wamekiri wenyewe kwamba wamepoteza ladha kwa wananchi. Wamekiri wenyewe katika waraka huo, kwamba hawakubaliki kwa sababu wameacha siasa ya ujamaa na kujitegemea.
“Na ni kweli wameacha siasa ya ujamaa na kujitegemea. Mabilioni ya Kikwete sio ujamaa na kujitegemea. Mabilioni ya mtoto wake, anayeitwa Ridhawani nayo ni ushahidi tosha kuwa wameacha ujamaa na kujitegemea kama walivyokiri wenyewe kwenye waraka wao.
“Tatizo lao ni kwamba badala ya kuacha ufisadi na kurejesha tunu za taifa kama uadilifu, upendo, amani, umoja na uwajibikaji…badala ya kupunguza kodi kwenye mafuta, sukari, saruji, na bidhaa nyingine, ili wajijengee uhalali kwa umma, wao katika waraka wao wameamua wabadili sura za viongozi kwa kujivua gamba. Hawataji popote kwenye waraka wao jinsi watakavyoboresha maisha yenu,” alisema Dk.Slaa na kuongeza.
“CHADEMA hatuko tayari kuona Watanzania wakiteseka huku CCM yenye serikali badala ya kuchukua hatua za dharura kuwanusuru, inapanga kuendelea kuwadanganya kwa kubadili viongozi kwa kujivua gamba. Arusha nilitoa hotuba moja wakasema Dk. Slaa mchochezi…sasa leo nawatuma usalama wa taifa nendeni mkawaambie CCM kwamba nchi haitatawalika. Wasipochukua hatua CHADEMA itachukua hatua…kama Watanzania hawajui wanakula nini, wanavaa nini, watoto wao wanasoma vipi, wanatibiwa vipi, basi nchi hii haitatawalika.”
Alisisitiza kuwa nchi haitatawalika kwani kila kukicha ufisadi unakithiri badala ya kupungua huku akibainisha kuwa hata ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali ya hivi karibuni imeonyesha katika wizara moja pekee, wizara ya fedha na uchumi, jumla ya sh bilioni 365 ziliibiwa wakati zingeweza kutumika kunusuru maisha ya Watanzania.
Mwenyekiti wa chama hicho akihutubia wakazi hao wa Sumbawanga, alisema kupitia maandamano na mikutano ya hadhara inayofanywa na chama hicho nchi nzima, CHADEMA imedhamiria kuamsha nguvu ya umma katika kuishinikiza serikali kupunguza kodi kwenye bidhaa na huduma muhimu ili bei zishuke na maisha ya wananchi yawe nafuu.
Alisema kupanda kwa gharama za maisha kumesababishwa na ufisadi na sera mbovu za serikali ya CCM, ambayo inawatoza kodi kubwa wananchi maskini kupitia bidhaa na huduma mbalimbali huku serikali hiyo hiyo ikiwasemehe kodi wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa.
Katika hotuba yake hiyo iliyoonekana dhahiri kuwateka wakazi wa Sumbawanga, Mbowe alisema CHADEMA haipingi watu kulipa kodi, lakini haiko tayari kuona Watanzania maskini wakilipishwa kodi kubwa, huku serikali ikishindwa kuwapa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Akifafanua zaidi historia ya kodi na athari zake kwa wananchi, kiongozi huyo wa kambi ya upinzani bungeni alisema baada ya serikali ya Rais Benjamin Mkapa kuondoa kodi ya maendeleo, ilileta kodi nyingine ya Ongezeko la Thamani (VAT), ambayo wananchi wote sasa wanatozwa kila wanaponunua bidhaa dukani na kulipia huduma mbalimbali kama usafiri.
“Nyerere alikuwa akikusanya kodi bilioni saba kwa mwezi, mzee Mwinyi aliondoka akiwa anakusanya kodi ya bilioni 27, akaja Mkapa yeye hadi anaondoka alikuwa anakusanya bilioni 300 na ushei. Baada ya hapo akaja Kikwete, yeye anakusanya bilioni 420 kwa mwezi. Anakusanya fedha nyingi kwa sababu kuna kodi ya VAT iliyoongezwa katika bei za bidhaa na huduma mnazolipia. Mnalipa kodi bila kujua, mnalipa kodi kwenye mafuta, kwenye soda, usafiri, sukari, sanda, pipi...kila kitu kodi kodi kodi,” alisema Mbowe na kuongeza.
“Kwa sababu ya kodi ya VAT, leo katika nchi hii kila mwananchi analipa kodi, mtoto, mjane, kijana, mwanafunzi wote wanalipa kodi …hadi maiti nazo zinalipiwa kodi mnaponunua sanda kwa ajili ya kuzikia. ...lakini kodi hizo zinaishia kustawisha maisha ya vigogo wa serikali, wananchi wa Sumbawanga na Watanzania wengine wanazidi kuwa maskini, mmefikia mahali hamuwezi hata kununua kilo moja ya sukari kwa ajili ya chai au kilo ya mafuta mnaanza kupimiwa kwenye vifuko vya shilingi mia moja...hali ya hatari hii, taifa lina msiba wa umaskini, wananchi wanalia kila mahali sasa, kila kona ya nchi,” alisema.
Akitoa mfano wa jinsi kodi inavyofanya bei za vitu kuwa juu, Mbowe alisema katika kila Sh elfu moja anayotumia Mtanzania kununua bidhaa sokoni au dukani au kulipia huduma, serikali humkata kodi ya wastani wa sh 500 hadi 600, kodi ambayo kama ikiondolewa gharama za maisha zitakuwa nafuu.
“Soda moja inapotoka kiwandani inapaswa kuuzwa kwa Sh 150 lakini kwa sababu ya kodi iliyowekwa na CCM kuanzia viwandani soda moja mnauziwa kwa sh 500 hadi 600. Kila mnaponunua mfuko mmoja wa cement mnakatwa kodi ya Sh 7,500 ambayo kama ikiondolewa au kupunguzwa bei ya saruji itakuwa nafuu na wengi mtaweza kujenga.
“Kila chupa moja ya bia unayonunua unakatwa kodi ya sh 800. Ndiyo maana Kikwete kwa mwezi anakusanya bilioni 420 kutoka kwenu, lakini maendeleo hakuna. CHADEMA tutakomaa na suala la gharama za maisha ndani na nje ya bunge mpaka Watanzania maisha yao yawe nafuu,” alisema Mbowe na kushangiliwa.
Katika mkutano huo pia Mbowe aliwahamasisha wakazi wa Sumbawanga kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kupata Katiba mpya na kushinikiza katiba hiyo itokane na wananchi na sio itokane kwa utashi na maamuzi ya Rais Kikwete kama ilivyopendekezwa katika Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba.
Naye Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe akiwahutubia wananchi hao alisema kwa nafasi yake kama Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, ameagizwa na chama chake kuwasilisha bajeti mbadala katika bunge lijalo la bajeti ambayo pamoja na mambo mengine itashinikiza serikali kupunguza kodi kwenye mafuta ya petroli na dizeli kwa asilimia 50 ili yauzwe kwa angalau Shs 1665 kwa lita kutoka kwenye bei ya zaidi ya sh 2000 ya sasa.
“Gharama za maisha ziko juu kwa sababu ya mfumuko wa bei za mafuta ambao unasababisha na kodi. Bei ya mafuta ikishuka hadi 1,665 gharama za usafiri na bei za sukari na vyakula nazo zitakuwa angalau. Tutawataka waondoe kodi kwenye mafuta halafu wapunguze misahamaha ya kodi wanayoitoa kwa wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa … serikali inasemehe bilioni 635 za kodi zinazopaswa kulipwa na matajiri, sasa hizo zikafidie kwenye mafuta baada ya kupunguza kodi. Wakikataa watakiona cha moto, tutafanya maandamano ndani na nje ya bunge mpaka kieleweke,” alisema Zitto.
 
Chadema,Chadema,Chadema, kila kukicha ni nyimbo hiyo hiyo humu JF. Hawa CDM Mbona wameandama sana tu bila mafanikio yeyote? Mikutano kibao, kelele nyingi. Mwisho watanzania watawaona ni wapuuzi tu. Wanataka washike nchi na wao wajitajirishe.
 
Tatizo la watu kama wewe nadhani hamsomi alama za nyakati zamani mliwafanya wajinga na kila kitu mlichowaambia walikubali na baada ya muda mfupi watu wamesoma na wengi wao wanajua kuchambua mambo kwa kina wameona mwelekeo uko chadema na wameshachoka kuibiwa kama watoto wadogo ndiyo maana wamefanya maamuzi na kukiunga mkono chama chenye mwelekeo.
 
Chadema,Chadema,Chadema, kila kukicha ni nyimbo hiyo hiyo humu JF. Hawa CDM Mbona wameandama sana tu bila mafanikio yeyote? Mikutano kibao, kelele nyingi. Mwisho watanzania watawaona ni wapuuzi tu. Wanataka washike nchi na wao wajitajirishe.

Akjili ya kuku bwana, anafikiri dua yake itampata mwewe.:israel:
 
Yaani hizo nyomi katika mikutano ya CDM, watu kwenda katika mikutano bila kubebwa, hawahongwi na wanavyoguswa na ujumbe, jamaa zangu CCM wamepoteza network.:A S 103:
 
Chadema,Chadema,Chadema, kila kukicha ni nyimbo hiyo hiyo humu JF. Hawa CDM Mbona wameandama sana tu bila mafanikio yeyote? Mikutano kibao, kelele nyingi. Mwisho watanzania watawaona ni wapuuzi tu. Wanataka washike nchi na wao wajitajirishe.

Hilo ni tatizo la uvivu wa kufikiri bwana mdogo. Usiiishi kwa mazoea. Try to think deeper.
 
Yaani hizo nyomi katika mikutano ya CDM, watu kwenda katika mikutano bila kubebwa, hawahongwi na wanavyoguswa na ujumbe, jamaa zangu CCM wamepoteza network.:A S 103:

Asante mkuu kwa ujumbe huo mahususi kwa CCM iliyo kosa mwelekeo
 
Chadema,Chadema,Chadema, kila kukicha ni nyimbo hiyo hiyo humu JF. Hawa CDM Mbona wameandama sana tu bila mafanikio yeyote? Mikutano kibao, kelele nyingi. Mwisho watanzania watawaona ni wapuuzi tu. Wanataka washike nchi na wao wajitajirishe.

CCM na viongozi na wafuasi wote kwele mnavuta nyuma kwa uelewa ukilinganisha na wananchi. U [ccm] all are lagging (trailing) behind to catch the pace of knowledge sweeping in z community. Have insight to dicern the reality, purge out that self-willed & cracked brains of yours
 
Tatizo hawa ccm hujifanya bado wanapendwa kwa kuangalia shangwe za wanaojikomba (Wazee wa Dar) ambao muda wao wa kufanya uchawi unaelekea kwisha halafu wapandwe ardhini. Kwa kuona hivo pamoja na Salute wanahitimisha wao ndo daima lakini hawajui kuwa saluti baadaye inaweza kugeuka kofi. Bye bye Gbagbo!
 
"Nyerere alikuwa akikusanya kodi bilioni saba kwa mwezi, mzee Mwinyi aliondoka akiwa anakusanya kodi ya bilioni 27, akaja Mkapa yeye hadi anaondoka alikuwa anakusanya bilioni 300 na ushei. Baada ya hapo akaja Kikwete, yeye anakusanya bilioni 420 kwa mwezi. .

Wakuu zangu haya mahesabu kidogo yananipa taabu hasa napozingatia value ya fedha zilizokuwa zikikusanywa..Ebu nitazame haya mahesabu kwa uhalisia wake..Na kama nimefanya makosa naomba kusahihishwa..

1. Nyerere alikusanya kodi Billioni 7 / 17 Usd dollar (exchange rate when he left) = 411,764,706 Usd
2. Mwinyi alikuwa akikusanya kodi Billioni 27/ 500 Us dollar (exchange rate when he left) = 54,000,000 Usd
3. Mkapa alikuwa akikusanya Billioni 300/1100 Us dollar (exchange rate when he left) = 272,727,273 Usd
4. JK naye anakusanya kodi billioni 420/1500 Us dollar (currect exchange rate) = 280,000,000 Usd..

Kama hivyo ndivyo sijui hata niseme nini...
 
  • Thanks
Reactions: Ame
“Nyerere alikuwa akikusanya kodi bilioni saba kwa mwezi, mzee Mwinyi aliondoka akiwa anakusanya kodi ya bilioni 27, akaja Mkapa yeye hadi anaondoka alikuwa anakusanya bilioni 300 na ushei. Baada ya hapo akaja Kikwete, yeye anakusanya bilioni 420 kwa mwezi. .

Wakuu zangu haya mahesabu kidogo yananipa taabu hasa napozingatia value ya fedha zilizokuwa zikikusanywa..Ebu nitazame haya mahesabu kwa uhalisia wake..Na kama nimefanya makosa naomba kusahihishwa..

1. Nyerere alikusanya kodi Billioni 7 / 17 Usd dollar (exchange rate when he left) = 411,764,706 Usd
2. Mwinyi alikuwa akikusanya kodi Billioni 27/ 500 Us dollar (exchange rate when he left) = 54,000,000 Usd
3. Mkapa alikuwa akikusanya Billioni 300/1100 Us dollar (exchange rate when he left) = 272,727,273 Usd
4. JK naye anakusanya kodi billioni 420/1500 Us dollar (currect exchange rate) = 280,000,000 Usd..

Kama hivyo ndivyo sijui hata niseme nini...

Alafu bado utaona watu wanalalamika eti Nyerere kaharibu uchumi duh watu wako below kwa almost 50% kwenye makusanyo then utegemee development kweli? Hata huduma za jamii ukilinganisha leo na Nyerere's time ni kama vile baada ya Nyerere kuondoka tuliingia vitani na mapka sasa tupo bado ndiyo maana tunaendelea kurudi nyuma mpaka tumefika kwenye hatua ya kuwa tumia kina Yahya kutabiri future na kuua Albino (ujima), terrific!

Kwa luga ya uchumi ni kuwa tax base ambayo kwa Tanzania kama nchi nyingi zilivyo ni labour tax ime shrink kwahiyo kumekuwa na tax errosion maana viwanda vilivyo binafsishwa zimeua ajira nyingi na hapo hapo VAT imepandisha prices ya goods consumed so the real labor wage ime pungua in responce to low wages watu wame opt leisure (Vijana wengi mtaani/vijiweni) badala ya kuajiriwa hasa kwenye kilimo maana hizo industries zilikuwa zina link na kilimo. Capital iliyo patikana kwenye ubinafsishaji imepelekwa kwenye account za mafisadi nje ya nchi hakuna re investment so tumebakia na wale vijana ambao wana akili wame migrate mjini kufanya umachinga ambapo wakifika huko kwakua supply ya umachinga kama industry ni ndogo kuliko demand; wakaamua kuwa wavuta bangi; vibaka; machangudoa etc. Kweli Dr. Slaa alisema kweli kuchagua CCM ni maafa!
 
Sasa mkuu wangu inakuwaje hadi wasomi wetu wanamsifia Mkapa kwa kurekebisha ukusanyaji wa kodi, hii ina maana kutoka kwa Mwinyi au? maanake kila mchumi anamlaani Nyerere wakati ukweli unajieleza zaidi ktk takwimu..Maanake tukifata namba tu Hata Zimbabwe wanakusanya kodi kubwa leo hii kuliko wakati wa Ian Smith lakini haina maana pato la taifa kweli limeongezeka bali fedha ukweli unajificha ktk thamani ya fedha zinazokusanywa...
 
Kwasababu benchmark yao ni Mzee Mwinyi na siyo Nyerere ukiona hapo from Mwinyi to Mkapa changes zilikuwa very significant if I am to make your data the reference. Na ujue kuwa wachumi wa tz wako very subjective na wapo kuiridhisha IMF na worldbank ki takwimu kuliko uhalisia wa ukuaji wa uchumi kuna mambo mengi sana ya ki uchumi ukifanya objective analysis na kuu evaluate unavyotakiwa utagundua Nyerere was by far better than the three presidents kwenye uchumi na siasa yake ya ujamaa na kujitegemea ilikuwa bora mara elfu kuliko huu ufisadi.

Lakini pia shida ya takwimu kuwa ndiyo tegemeo kubwa haliko tu Tanzania kwenye uchumi of recent wachumi wa dunia wamekubali kuwa hizo model ni decisive from what happened kwenye kuanguka kwa uchumi wa dunia. siyo kwamba hazifai kabisa ila kuna factor zinatakiwa kuangaliwa zaidi kuliko absolute figures!
 
Back
Top Bottom