Maandamano ya Chadema yatishia Serikali ya CCM madarakani

Slaa alipua mabomu Send to a friend Saturday, 26 February 2011 21:54

Frederick Katulanda na Anthony Mayunga, Musoma
slaa%20sitta.jpg
Dr. Slaa

MAANDAMANO ya Chadema yameingia mkoani Mara na kuuteka mji wa Musaoma huku Katibu mkuu wa chama hicho, Dk Wilibroad Slaa, akitoboa siri ya kulipuka kwa mabomu ya Gongo la Mboto na Mbagala.

Naye Mwenyekiti Chadema taifa, Freeman Mbowe aliitahadharisha Serikali kuwa taifa litaingia kubaya iwapo mchakato wa mabadiliko ya katiba utachakachuliwa kwa maslai ya mafisadi.

Akizingumza jana katika Uwanjwa wa Mukendo mjini Musoma baada ya maandamano ya kilomita 15 kutoka Bweri hadi mjini, Dk Slaa alisema kulipuka kwa mabomu hayo kumetokana na Serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete kupuuza ombi la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuwapa fedha kwa ajili ya kuteketeza mabomu yaliyokwisha muda wake.

Alisema kazi ya jeshi ni kulinda uhai wa watu wake nchini, lakini kupitia jeshi taifa limeweza kupoteza watu zaidi ya 40 kutokana na serikali kugoma kutoa fedha hizo ambazo ziliombwa na JWTZ.

"Tunataka Kikwete atueleze kwa kina kama ni kweli, maana tunaambiwa kabla ya mabomu kulipuka mwaka 2009 JWTZ (Mbagala) waliomba fedha kwa ajili ya kuteketeza mabomu, lakini kutokana na serikali kutothamini maisha ya watu wake ilikataa kuwa hakuna fedha.

"Tunaambiwa tena kuwa kabla ya mabomu haya ya mwisho kulipuka wanajeshi waliomba fedha serikalini kwa ajili ya kuteketeza mabomu hayo, lakini pia serikali hiyohiyo haikutoa kwa madai kuwa hakuna fedha," alieleza Dk. Slaa.

Kwa sababu hiyo akamtaka
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi alijiuzulu.

Dk Slaa alisema kuwa Watanzania wanataka Waziri Mwinyi afuate nyayo za baba yake kama ambavyo alijiuzulu kwa mauaji ya polisi mkoani Shinyanga na kwamba asipofanya hivyo baada ya siku tisa kuisha Chadema watatangaza hatua ya pili kwa ajili ya kumshinikiza ajiuzulu.

Onyo kuhusu Katiba

Akizungumza katika mkutano huo uliokuwa umefurika watu, Mweyekiti wa chama hicho, Mbowe alitahadharisha kuwa serikali ya CCM itaingilia na kuvuruga mchakato wa katiba kwa maslai yake binafisi, basi "Tanzania patachimbika kama Tunisia na Misri."

Hata hivyo, Mbowe alisema kwa muda sasa amekuwa akishangazwa na kauli za Rais Kikwete ambazo zimekuwa zikidai kuwa nchini kuna udini akisema hizo ni propaganda zake.

Alisema kama kweli Kikwete anauhakika juu ua jambo hilo basi anapaswa kuwachukulia hatua wahusika.

Kabla ya mkutano huo viongozi hao waliwaongoza wananchi wa Musoma kuandamana umbali wa kilomita 15 wakitembea kupinga ugumu wa maisha na kulipwa kwa Dowans.

"Tutaendelea kuandamana mpaka maskini wa Tanzania asikilizwe. Tutaandamana mpaka vijana wa kitanzania wapate ajira na hatutalala mpaka kieleweke," alisema Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia.

Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje alisema vijana wengi wanafanya kazi za umachinga kwa sababu ya mfumo mbovu uliowekwa na serikali unaowafanya wakose ajira.

"Musoma kulikuwa na kiwanda kizuri sana cha Mutex kilichokuwa kinatoa ajira kwa vijana, lakini kwa uzembe na ujanja wakawapa watu kwa madai ya kubinafsisha. Sasa kimefungwa hakuna ajira kwa vijana na matokeo yake ndiyo wamachinga ambao wanapigwa mabomu kila wakati," alisema Wenje na kuongeza.

"Kuna kila sababu ya kutafuta haki kwa njia mbalimbali. Andamaneni mpaka haki yenu ipatikane."

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi alisema Wamarekani wana msemo kuwa anayehifadhi magaidi naye ni gaidi, hivyo wasanii wanazunguka na CCM na kuimba kuwa nchi hii ina amani nao ni wasaliti.

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee alisema pamoja na kuwa jimbo lake linakaliwa na vigogo wote wa nchi hii, lakini mwaka jana walifikia hatua ya kuikataa CCM.

"Kama Kawe wamesema CCM baibai inakuwaje ninyi watu wa Mara. Nawaambieni kuwa mwaka 2015 majimbo yote saba yanatakiwa yachukuliwe na Chadema na kuingia Ikulu, maana sisi tumewaahidi kupambana na ufisadi mpaka mwisho," alisema.

Utetezi wa Mbunge Lema

Dk Slaa alizungumzia pia kitendo cha Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kutakiwa kuwasilisha ushahidi kwa madai yakuwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alidanganya bungeni hivi karibuni.

Dk Salaa alisema kuwa tayari amewasilisha ushahidi na kwamba unaonyesha wazi kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alidanganya mara 23 bungeni kuhusiana na suala la mauaji ya Arusha.

"Spika aliomba ushahidi Lema kapeleka, lakini kwa sababu alitaka kumlinda Pinda akasema kuwa ushahidi huo upelekwe kwake.

"Lema ameitwa muongo hadharani na ushahidi aliowasilisha umebainisha Pinda ndiye alidanganya mara 23, sasa tunataka apewe nafasi hadharani bungeni auseme ushahidi wake katika kikao cha bunge lijalo Aprili," alidai Slaa.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments

12

0 #17 Aloyce 2011-02-27 06:20 Slaa anazeeka vibaya. Hii yote ni laana ya kuacha upadre. Anaongea bila kutumia busara. Chadema kimekuwa chama cha genge la wambea. Wamepoteza mwelekeo na kuanza kusema ovyo ili mradi kutafuta umaarufu kwa gharama yoyote ile. Wanajichimbia kaburi come 2015. Kuna fisadi yeyote katika TZ kama Mbowe na Ndesamburo? Jamani nyie acheni tu. Sisi wengine tumenyamaza tu. Mkitaka kujua true colors of chadema fanyeni analysis ya wabunge wao wa viti maalumu: wangapi? wanatoka wapi? na wanahusiana na nani? Hawa tunawajuwa waache kabisa lugha ya kusema eti wana uchungu na nchi. It is a gang of liars looking for cheap popularity. It is really a shame.
Quote

-1 #16 mohsein 2011-02-27 06:04 Du kweli hili mwananchi ni gazeti la wapinzani wa chama tawala!jamani kwenye kuleta maendeleo ya nchi, tuweke pembeni itikadi zetu.acheni [NENO BAYA]!
mbona hata akina SLaa au mbowe wenyewe hawatukani! inasikitisha sana.ni mtizamo tu.

Quote

+2 #15 gadi 2011-02-27 05:32 Mhariri angalia lugha inayotumiwa na watoa maoni, wakati mwingine inakiuka maadili.
Quote

+2 #14 smartboy 2011-02-27 05:27 Slaa alete ushahidi wa kile anachosema, isije ikawa ni kauli ya kujitafutia umaarufu.
Ila km ni kweli JWTz waliomba pesa kuteketeza mabofu wakanyimwa ni kashfa nzito ambapo wahusika wote wanapaswa kuchukuliwa hatua.
Sitaki sana kuamini kauli ya wanasiasa. Tunataka ushahidi/uthibitisho.

Quote

+2 #13 Katiba TANGANYIKA 2011-02-27 03:01 Jamani kwanini kutumia uhuru wa kutoa maoni vibaya?!!

Hata kama ni hasira tujaribu kutumia busara tafadhali, [NENO BAYA] ya aina hiyo sio vzr!

Quote

+1 #12 Mkweli 2011-02-27 01:44 Quoting jakaya kikwete:
Quoting Mgmg:
chadema acheni kelele tumewachoka hatukuwachagua muende mkaandamane

k u m a mama yako m senge wewe

Hivi hili gazeti mnafanya editing kweli. kwa nini mnaruhusu [NENO BAYA] yasiyo ya kimaadili kuandikwa katika eneo hili? tadahali gazeti lenu linasomwa na watu wengi hasa sisi tulioko hapa UK. Tunahitaji kujua nini kinaendelea huko Tanzania kwa vile na sisi ni wazawa. tafadhali hatutaki [NENO BAYA]. Tunataka mtu atuletee story za kweli na si [NENO BAYA]. Mhariri usituangushe.
LUKE

Quote

-1 #11 Frank 2011-02-27 01:36 Quoting jakaya kikwete:
Quoting Mgmg:
chadema acheni kelele tumewachoka hatukuwachagua muende mkaandamane

k u m a mama yako m senge wewe

Haya umeruhusu umeona ni manene mazuri?

Quote

+1 #10 Frank 2011-02-27 01:34 Mhariri uko wapi? Unaruhusu vipi maoni kama #9. Hebu tuwe wastaarabu na tutoe maoni sio [NENO BAYA], si utamaduni wa mtanzania!!!
Quote

-1 #9 jakaya kikwete 2011-02-27 00:53 Quoting Mgmg:
chadema acheni kelele tumewachoka hatukuwachagua muende mkaandamane

k u m a mama yako m senge wewe

Quote

+1 #8 Mohamed 2011-02-27 00:33 Let us see if this is true
Quote

+2 #7 GILLIARD 2011-02-26 23:49 Kuna haja ya viongozi wa CHADEMA kutunga vijitabu vya maovu yanayotendeka ndani ya Serekali kila mtu ayaone. Ukweli CCM wanakera sana. Kama kila fedha inayoombwa kwa faida za Watanzania wanadai hakuna sasa madarakani wanakaa kufanya kazi gani?.
Quote

0 #6 George Lema 2011-02-26 23:29 Haya viongozi Chadema endeleeni kulisu[NENO BAYA] guruduma la maendeleo sisi tumeshachoshwa na ubinafisi Wa c c m na serikali Yao ,TU[NENO BAYA]MAA KICHWA MPAKA KIELEWEKE
Quote

0 #5 observer 2011-02-26 23:21 Hayo madai ya sababu za kulipuka kwa mabomu home kwetu yamenisikitisha sana. Lakini kwa vile ni madai na bado hayajathibitish wa WATANZANIA tutulie kwanza na tusihukumu..ila tuendelee kusubiri serikali ilijibu hilo kwa kutoa ufafanuzi maana ni issue iliyo sensitive sana..tunazungumzia maisha ya watu hapa jamani!! CHADEMA, mko juu na kuna kila sababu ya kuingia ikulu uchaguzi ujao!watu mkate mkubali, kuna kila sababu ya kukipa chama hiki (CHADEMA) nafasi na kuwaacha wazee wetu wapumzike maana nahis wameizoea nchi mpaka wameanza kuichukulia poa!
Quote

-3 #4 Mgmg 2011-02-26 22:54 chadema acheni kelele tumewachoka hatukuwachagua muende mkaandamane
Quote

-1 #3 Mchungu wa Bongo 2011-02-26 22:43 Asanteni Chadema, washa moto washa moto, mpaka kitaeleweka tu Tanzania, mraa mpaka kieleweke, songa mbele Chadema na Watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi hii tutaendelea kuwa-support...asomaye na afahamu
Quote

12
Refresh comments list
 
Slaa alipua mabomu Send to a friend Saturday, 26 February 2011 21:54

Frederick Katulanda na Anthony Mayunga, Musoma
slaa%20sitta.jpg
Dr. Slaa

MAANDAMANO ya Chadema yameingia mkoani Mara na kuuteka mji wa Musaoma huku Katibu mkuu wa chama hicho, Dk Wilibroad Slaa, akitoboa siri ya kulipuka kwa mabomu ya Gongo la Mboto na Mbagala.

Naye Mwenyekiti Chadema taifa, Freeman Mbowe aliitahadharisha Serikali kuwa taifa litaingia kubaya iwapo mchakato wa mabadiliko ya katiba utachakachuliwa kwa maslai ya mafisadi.

Akizingumza jana katika Uwanjwa wa Mukendo mjini Musoma baada ya maandamano ya kilomita 15 kutoka Bweri hadi mjini, Dk Slaa alisema kulipuka kwa mabomu hayo kumetokana na Serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete kupuuza ombi la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuwapa fedha kwa ajili ya kuteketeza mabomu yaliyokwisha muda wake.

Alisema kazi ya jeshi ni kulinda uhai wa watu wake nchini, lakini kupitia jeshi taifa limeweza kupoteza watu zaidi ya 40 kutokana na serikali kugoma kutoa fedha hizo ambazo ziliombwa na JWTZ.

“Tunataka Kikwete atueleze kwa kina kama ni kweli, maana tunaambiwa kabla ya mabomu kulipuka mwaka 2009 JWTZ (Mbagala) waliomba fedha kwa ajili ya kuteketeza mabomu, lakini kutokana na serikali kutothamini maisha ya watu wake ilikataa kuwa hakuna fedha.

"Tunaambiwa tena kuwa kabla ya mabomu haya ya mwisho kulipuka wanajeshi waliomba fedha serikalini kwa ajili ya kuteketeza mabomu hayo, lakini pia serikali hiyohiyo haikutoa kwa madai kuwa hakuna fedha,” alieleza Dk. Slaa.

Kwa sababu hiyo akamtaka
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi alijiuzulu.

Dk Slaa alisema kuwa Watanzania wanataka Waziri Mwinyi afuate nyayo za baba yake kama ambavyo alijiuzulu kwa mauaji ya polisi mkoani Shinyanga na kwamba asipofanya hivyo baada ya siku tisa kuisha Chadema watatangaza hatua ya pili kwa ajili ya kumshinikiza ajiuzulu.

Onyo kuhusu Katiba

Akizungumza katika mkutano huo uliokuwa umefurika watu, Mweyekiti wa chama hicho, Mbowe alitahadharisha kuwa serikali ya CCM itaingilia na kuvuruga mchakato wa katiba kwa maslai yake binafisi, basi "Tanzania patachimbika kama Tunisia na Misri."

Hata hivyo, Mbowe alisema kwa muda sasa amekuwa akishangazwa na kauli za Rais Kikwete ambazo zimekuwa zikidai kuwa nchini kuna udini akisema hizo ni propaganda zake.

Alisema kama kweli Kikwete anauhakika juu ua jambo hilo basi anapaswa kuwachukulia hatua wahusika.

Kabla ya mkutano huo viongozi hao waliwaongoza wananchi wa Musoma kuandamana umbali wa kilomita 15 wakitembea kupinga ugumu wa maisha na kulipwa kwa Dowans.

“Tutaendelea kuandamana mpaka maskini wa Tanzania asikilizwe. Tutaandamana mpaka vijana wa kitanzania wapate ajira na hatutalala mpaka kieleweke,” alisema Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia.

Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje alisema vijana wengi wanafanya kazi za umachinga kwa sababu ya mfumo mbovu uliowekwa na serikali unaowafanya wakose ajira.

“Musoma kulikuwa na kiwanda kizuri sana cha Mutex kilichokuwa kinatoa ajira kwa vijana, lakini kwa uzembe na ujanja wakawapa watu kwa madai ya kubinafsisha. Sasa kimefungwa hakuna ajira kwa vijana na matokeo yake ndiyo wamachinga ambao wanapigwa mabomu kila wakati,” alisema Wenje na kuongeza.

“Kuna kila sababu ya kutafuta haki kwa njia mbalimbali. Andamaneni mpaka haki yenu ipatikane."

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi alisema Wamarekani wana msemo kuwa anayehifadhi magaidi naye ni gaidi, hivyo wasanii wanazunguka na CCM na kuimba kuwa nchi hii ina amani nao ni wasaliti.

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee alisema pamoja na kuwa jimbo lake linakaliwa na vigogo wote wa nchi hii, lakini mwaka jana walifikia hatua ya kuikataa CCM.

“Kama Kawe wamesema CCM baibai inakuwaje ninyi watu wa Mara. Nawaambieni kuwa mwaka 2015 majimbo yote saba yanatakiwa yachukuliwe na Chadema na kuingia Ikulu, maana sisi tumewaahidi kupambana na ufisadi mpaka mwisho," alisema.

Utetezi wa Mbunge Lema

Dk Slaa alizungumzia pia kitendo cha Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kutakiwa kuwasilisha ushahidi kwa madai yakuwa kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alidanganya bungeni hivi karibuni.

Dk Salaa alisema kuwa tayari amewasilisha ushahidi na kwamba unaonyesha wazi kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alidanganya mara 23 bungeni kuhusiana na suala la mauaji ya Arusha.

“Spika aliomba ushahidi Lema kapeleka, lakini kwa sababu alitaka kumlinda Pinda akasema kuwa ushahidi huo upelekwe kwake.

"Lema ameitwa muongo hadharani na ushahidi aliowasilisha umebainisha Pinda ndiye alidanganya mara 23, sasa tunataka apewe nafasi hadharani bungeni auseme ushahidi wake katika kikao cha bunge lijalo Aprili,” alidai Slaa.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments

12

0 #17 Aloyce 2011-02-27 06:20 Slaa anazeeka vibaya. Hii yote ni laana ya kuacha upadre. Anaongea bila kutumia busara. Chadema kimekuwa chama cha genge la wambea. Wamepoteza mwelekeo na kuanza kusema ovyo ili mradi kutafuta umaarufu kwa gharama yoyote ile. Wanajichimbia kaburi come 2015. Kuna fisadi yeyote katika TZ kama Mbowe na Ndesamburo? Jamani nyie acheni tu. Sisi wengine tumenyamaza tu. Mkitaka kujua true colors of chadema fanyeni analysis ya wabunge wao wa viti maalumu: wangapi? wanatoka wapi? na wanahusiana na nani? Hawa tunawajuwa waache kabisa lugha ya kusema eti wana uchungu na nchi. It is a gang of liars looking for cheap popularity. It is really a shame.
Quote

-1 #16 mohsein 2011-02-27 06:04 Du kweli hili mwananchi ni gazeti la wapinzani wa chama tawala!jamani kwenye kuleta maendeleo ya nchi, tuweke pembeni itikadi zetu.acheni [NENO BAYA]!
mbona hata akina SLaa au mbowe wenyewe hawatukani! inasikitisha sana.ni mtizamo tu.

Quote

+2 #15 gadi 2011-02-27 05:32 Mhariri angalia lugha inayotumiwa na watoa maoni, wakati mwingine inakiuka maadili.
Quote

+2 #14 smartboy 2011-02-27 05:27 Slaa alete ushahidi wa kile anachosema, isije ikawa ni kauli ya kujitafutia umaarufu.
Ila km ni kweli JWTz waliomba pesa kuteketeza mabofu wakanyimwa ni kashfa nzito ambapo wahusika wote wanapaswa kuchukuliwa hatua.
Sitaki sana kuamini kauli ya wanasiasa. Tunataka ushahidi/uthibitisho.

Quote

+2 #13 Katiba TANGANYIKA 2011-02-27 03:01 Jamani kwanini kutumia uhuru wa kutoa maoni vibaya?!!

Hata kama ni hasira tujaribu kutumia busara tafadhali, [NENO BAYA] ya aina hiyo sio vzr!

Quote

+1 #12 Mkweli 2011-02-27 01:44 Quoting jakaya kikwete:
Quoting Mgmg:
chadema acheni kelele tumewachoka hatukuwachagua muende mkaandamane

k u m a mama yako m senge wewe

Hivi hili gazeti mnafanya editing kweli. kwa nini mnaruhusu [NENO BAYA] yasiyo ya kimaadili kuandikwa katika eneo hili? tadahali gazeti lenu linasomwa na watu wengi hasa sisi tulioko hapa UK. Tunahitaji kujua nini kinaendelea huko Tanzania kwa vile na sisi ni wazawa. tafadhali hatutaki [NENO BAYA]. Tunataka mtu atuletee story za kweli na si [NENO BAYA]. Mhariri usituangushe.
LUKE

Quote

-1 #11 Frank 2011-02-27 01:36 Quoting jakaya kikwete:
Quoting Mgmg:
chadema acheni kelele tumewachoka hatukuwachagua muende mkaandamane

k u m a mama yako m senge wewe

Haya umeruhusu umeona ni manene mazuri?

Quote

+1 #10 Frank 2011-02-27 01:34 Mhariri uko wapi? Unaruhusu vipi maoni kama #9. Hebu tuwe wastaarabu na tutoe maoni sio [NENO BAYA], si utamaduni wa mtanzania!!!
Quote

-1 #9 jakaya kikwete 2011-02-27 00:53 Quoting Mgmg:
chadema acheni kelele tumewachoka hatukuwachagua muende mkaandamane

k u m a mama yako m senge wewe

Quote

+1 #8 Mohamed 2011-02-27 00:33 Let us see if this is true
Quote

+2 #7 GILLIARD 2011-02-26 23:49 Kuna haja ya viongozi wa CHADEMA kutunga vijitabu vya maovu yanayotendeka ndani ya Serekali kila mtu ayaone. Ukweli CCM wanakera sana. Kama kila fedha inayoombwa kwa faida za Watanzania wanadai hakuna sasa madarakani wanakaa kufanya kazi gani?.
Quote

0 #6 George Lema 2011-02-26 23:29 Haya viongozi Chadema endeleeni kulisu[NENO BAYA] guruduma la maendeleo sisi tumeshachoshwa na ubinafisi Wa c c m na serikali Yao ,TU[NENO BAYA]MAA KICHWA MPAKA KIELEWEKE
Quote

0 #5 observer 2011-02-26 23:21 Hayo madai ya sababu za kulipuka kwa mabomu home kwetu yamenisikitisha sana. Lakini kwa vile ni madai na bado hayajathibitish wa WATANZANIA tutulie kwanza na tusihukumu..ila tuendelee kusubiri serikali ilijibu hilo kwa kutoa ufafanuzi maana ni issue iliyo sensitive sana..tunazungumzia maisha ya watu hapa jamani!! CHADEMA, mko juu na kuna kila sababu ya kuingia ikulu uchaguzi ujao!watu mkate mkubali, kuna kila sababu ya kukipa chama hiki (CHADEMA) nafasi na kuwaacha wazee wetu wapumzike maana nahis wameizoea nchi mpaka wameanza kuichukulia poa!
Quote

-3 #4 Mgmg 2011-02-26 22:54 chadema acheni kelele tumewachoka hatukuwachagua muende mkaandamane
Quote

-1 #3 Mchungu wa Bongo 2011-02-26 22:43 Asanteni Chadema, washa moto washa moto, mpaka kitaeleweka tu Tanzania, mraa mpaka kieleweke, songa mbele Chadema na Watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi hii tutaendelea kuwa-support...asomaye na afahamu
Quote

12
Refresh comments list
 
Chadema hapatoshi Mwanza Send to a friend Friday, 25 February 2011 21:29

f.mboye.jpg
Waandishi Wetu, Mwanza

VIONGOZI wa juu na wabunge wa Chadema jana walitawanyika katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Mwanza na kufanya mikutano ya hadhara kuendelea kupinga kupanda kwa gharama za maisha, malipo kwa Kampuni ya Dowans na kupanda kwa gharama za umeme.

Viongozi na wabunge hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe na Katibu wake mkuu Dk Willbrod Slaa aliyekuwa mgombea urais katika uchaguzi mkuu uliopita Oktoba 31 mwaka 2010 walichagiza katika mikutano hiyo ya mtawanyiko.

Mikutano hiyo ya hadhara ilikusanya maelfu ya wakazi wa mkoa wa Mwanza, huku mwenyekiti Mbowe akifanya mkutano wa hadhara wilayani Geita akiwa ameongozana na wabunge wanne wa chama hicho na Katibu wake Dk Slaa akiwa Kisiwani Ukerewe ambako naye aliambatana na mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemli na wabunge wa viti maalum, Rebecca Mngodo na Grace Kiwelu.

Freeman Mbowe
Mbowe alifuatana na Joseph Mbilinyi ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini, Halima Mdee (Kawe), Paulina Gekul na Anna Mallaki (viti maalum) pamoja na Profesa Kulikoyela Kahigi wa Bukombe.

Akihutubia katika mkutano huo Mbowe alisema wilaya ya Geita, ni masikini kupindukia kutokana na wananchi wake kuhujumiwa na viongozi wachache walioko serikali licha ya kuwa na mgodi mkubwa wa dhahabu.

Mbowe aliyasema hayo katika uwanja wa magereza nje kidogo na mji wa Geita, katika mkutano ambao ulitanguliwa na maandamano yaliyoaongozwa naye, huku wafuasi wa chama hicho wakibeba mabango mbalimbali, moja likilosomeka,''Dowans ikilipwa, mimi nitajiua. Mtanzania halali'.'

Huku akikatishwa na kelele za wananchi Mbowe alisema kuwa mgodi huo ilikuwa umejitolea kutoa umeme katika mji wa Geita kwa kuunganisha kwenye gridi ya taifa, lakini viongozi wa CCM waligoma kwa vile wao hawana uchungu na mgao wa umeme na kwa vile wana majenereta nyumbani kwao.

Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alirejea kauli yake kuwa kamwe Chadema hakitakubali ushirika na vyama vingine bungeni akidai kuwa vyama hivyo ni mawakala wa CCM, lakini akasema chama chake hakina ugomvi na wananchama wa vyama hivyo na kuwaomba radhi kuwa ugomvi uliopo ni kati ya chama hicho na viongozi wa vyama vingine vya upinzani hasa kile cha CUF.

Dk Wilbroad Slaa
Dk Slaa alifanya mkutano wake wilayani Ukerewe ambapo amemtaka Rais Jakaya Kikwete ajiuzulu kwa kile alichokiita uzembe wa serikali yake, kuendelea kusababisha maafa kwa wananchi pamoja na kauli yake ya kutowafaamu wamiliki wa kampuni ya kufua umeme ya Dowans.

Alisema haiingi akilini kuwa Rais Kikwete ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri lililoidhinisha mkataba wa kampuni tata ya Richmond ambao umerisishwa kwa Dowans kudai kuwa hafahamu wamiliki wake ambapo aliongeza kuwa ikiwa ni kweli Kikwete hawafahamu wamiliki wa kampuni hiyo, basi huo ni uzembe na anatakiwa kujiuzulu pamoja na serikali yake.

Dk Slaa alisema pia kwamba Chadema haitakubali Tanesco kuingia mkataba na Dowans kama Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba anavyoshauri, vinginevyo watatumia nguvu ya umma kupinga hilo .

Akifafanua alisema kimsingi mitambo hiyo inastahili kutaifishwa na kuonya kuwa kitendo cha kutaka kuingia mkataba na kampuni ya kifisadi ni ya kushangaza, kwani Serikali ilitambua tatizo la umeme wa kutegemea mabwawa ya maji tangu mwaka 2001 na baadaye tatizo hilo likajitokeza mwaka 2003.

"Serikali makini, ingenunua mitambo yake yenye uwezo wa kuzalisha nishati hiyo na siyo kuingia mikataba ya kifisadi kama ya Richmond na baadaye Dowans," alisema Dk Slaa.

Katibu Mkuu huyo wa Chadema alisema kwamba ameshangazwa na mtu aliyejitokeza kuwa ndiye mmiliki wa Dowans (Suleiman Al- Adawi) kujitokeza sasa akitoa madai tofauti ikiwemo na kutaka kusamehe deni hilo, baada ya kubaini mpango wa Chadema wa kutaka kutumia umma kupinga utapeli huo.

Mkutano wa Misungwi
Katika Wilaya ya Misungwi mkoani humo mkutano wa hadhara wa Chadema uliongozwa na mbunge wake wa Ilemela, Highness Kiwia huku ikielezwa kuwa mkutano huo ulisababisha kuvunjika kwa mkutano wa hadhara wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM, George Mkuchika uliokuwa ufanyike wilayani humo.

Katika mkutano huo Kiwia alifuatana na wabunge wa viti maalum wa Chadema Raya Ibrahim (Pemba) na Chiku Abwao (Iringa) ambapo alisema aliyekuwa mpinzani wake katika kuwania kiti cha ubunge Anthon Diallo amemfungulia kesi mahakamani akimtuhumu kwa kuiba kura katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2010.

Kiwia alisema pamoja na kumshitaki akidai aliiba kura kura zilizompa ushindi ametuhumiwa pia kufanya kampeni za vitisho na kusababisha wananchi kuogopa kujitokeza kwenda kupiga kura, lakini akasema ana uhakika kuwa waliomuweka madarakani ni wananchi kwa ridhaa yao na kudai kuwa atawapigania katika kuleta maendeleo.

Kuhusu Katiba Kiwia alisema Chadema haitapumzika hadi Serikali ifanye mabadiliko ya katiba ambayo itamuwezesha mtanzania kufanya uchaguzi wa haki na kweli bila ya kupigwa mabomu.
Katika mkutano huo wananchi waliohudhuria walipaza sauti wakisema kuwa Rais Kikwete hana budi kujiuzulu wakidai ameshindwa kuindesha nchi hii.

Mkutano wa Kwimba
Ezekia Wenje alifanya mkutano wake wa hadhara katika wilaya ya Kwimba huku akitoboa siri ya yaliyomsibu wakati wa kampeni za kuwania ubunge wa jimbo hilo.

Katika mkutano wake Wenje alifuatana na wabunge wenzake wa chama hicho ambao ni Rachel Mashishanga, Philip Maturano, Joyce Mukya pamoja na mkurugenzi wa fedha wa chama hicho Antony Komu.

Wenje alidai kuwa katika uchaguzi uliopita alihongwa Sh300 milioni ili ampishe aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na mgombea ubunge wa CCM katika jimbo hilo Lawrence Masha ambapo pia alidai moja ya chama siyo Chadema kilitenga Sh2.5 bilioni kwa ajili ya kuwagawia wapiga kura ili wachague chama hicho, lakini wananchi wa jimbo hilo waligoma na kulinda kura zao.

Viongozi hao wa Chadema na wabunge wao watafanya maandamo ya amani na baadaye mkutano wa hadhara leo katika mkoa wa Mara.

Kwa mujibu wa taarifa hizo maandamano hayo yataanza saa 5 asubuhi yakianzia eneo la Makutano na kuelekea katikati ya mji wa Musoma kwenye uwanja wa michezo wa Mkindo.

Habari zinaeleza kuwa ujumbe wa maandamano na mkutano wao wa hadhara ni sawa na ule walioutoa mkoani Mwanza, kupinga kupanda kwa gharama za maisha, malipo kwa Kampuni ya Dowans na kupanda kwa gharama za umeme.
Habari hii imeandaliwa na Sheila Sezzy, Misungwi, Frederick Katulanda, Kwimba na Jovita Kaijage, Ukerewe.
 
Slaa, Mbowe wamkaanga JK
• Wamshangaa kwenda nje wakati wa matatizo

na Mwandishi wetu

amka2.gif
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, wamemrushia kombora Rais Jakaya Kikwete kuwa analea nyufa za udini, ukabila pamoja na kukataa kutoa fedha za kuharibu mabomu yaliyozua balaa kwa wakazi wa Gongo la Mboto.
Viongozi hao walisema Rais Kikwete anashindwa kudhibiti nyufa za udini na ukabila kwa sababu ni mkakati wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kuidhoofisha CHADEMA ambayo hivi sasa imejizolea sifa na wanachama wengi, kwa sababu ya uimara wake wa kukiwajibisha chama tawala na serikali yake.
Wakizungumza kwa wakati tofauti katika viwanja wa Shule ya Mkendo mjini Musoma jana, viongozi hao walisema kwa hali ilivyo, Rais Kikwete, amekosa sifa za kuwa kiongozi imara.
Mbowe alisema Rais Kikwete ameshindwa kudhibiti nyufa za udini na ukabila ambao umeonekana dhahiri kuanza kuota mizizi hapa nchini, hivyo zinahitajika juhudi za haraka na makusudi kuuwajibisha utawala wake ili kuinusuru nchi.
"Taifa limeingia kwenye udini na ukabila ambao rais wa nchi ameshindwa kuudhibiti...sisi tunafahamu ajenda ya udini na ukabila ni mkakati wa CCM wa kutaka kuimaliza CHADEMA, jambo ambalo kamwe hatulikubali," alisema.
Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Waziri Mkuu Kivuli, aliwataka Watanzania kuunganisha nguvu zao kwa pamoja katika kulikomboa taifa hasa katika kipindi hiki ambacho umasikini unazidi kushamiri siku hadi siku.
"Tukiwaachia hawa CCM waendelee kututawala kama wanavyotaka kamwe umaskini hauwezi kutoweka miongoni mwetu, uwezo wa kubadilisha uongozi na hali zetu za kimaisha tunao, kwanini tunashindwa kuutumia?" alihoji.
Kuhusu uundwaji wa Katiba, Mbowe aliionya serikali kuwa ni vema isifanye hila mara baada ya wananchi kutoa maoni yao, kwani mchezo wowote utakaofanywa kwa lengo la kupinga maamuzi ya umma hukumu yake itakuwa kubwa kama ile inayoonekana hivi sasa nchini Libya au ile iliyotokea Misri.
Naye Dk. Slaa, alisema kuwa amesikitishwa na milipuko ya mabomu iliyotokea Gongo la Mboto ambayo kwa kiasi kikubwa imesababishwa na uzembe wa serikali ambayo iligoma kutoa fedha kwa ajili ya kuyaharibu mabomu hayo.
Alibainisha kuwa anazo taarifa kuwa Rais Kikwete alilinyima jeshi hilo fedha za kuharibu mabomu hayo ambayo yalionekana kwisha muda wake miaka miwili iyopita.
"Ninayo taarifa kwamba serikali ya Rais Kikwete iliombwa fedha mara mbili za kuharibu mabomu lakini ilishindwa kufanya hivyo...hali hiyo ndiyo iliyosababisha vifo vya Watanzania Mbagala na sasa Gongo la Mboto," alisema Dk. Slaa.
Aliongeza kuwa, kutokana na uzembe huo, anamtaka Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, pamoja na Mkuu wa Majeshi nchini, Jenerali Davis Mwamnyange, kujiuzulu mara moja nyadhifa zao na iwapo watashindwa, basi Rais Kikwete awafukuze.
Alisema Watanzania hawawezi kuendelea kuvumilia viongozi kama hao wazembe wa kazi na kwamba ni vema Waziri Mwinyi akaiga mfano wa baba yake, Ali Hassan Mwinyi, aliyeachia ngazi kutokana na mauaji yaliyotokea wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani.
"Tunamtaka Waziri Mwinyi ajiuzulu, na akishindwa basi Rais Kikwete amfukuze kazi huyu mtu pamoja na Mkuu wa Majeshi...wananchi wameshachoka kuona usanii wa uongozi," alisema.
Mbowe na Slaa waliongeza kuwa wamemshangaa Rais Jakaya Kikwete kwa kuacha msiba wa Watanzania waliokufa kwa mabomu ya Gongo la Mboto, kisha kwenda nchini Mauritania kusuluhisha mgogoro wa kisiasa wa Ivory Coast.
Walisema ni aibu kwa kiongozi wa wananchi kuacha msiba mkubwa nchini kwake na kukimbilia nje ya nchi kwenda kusuluhisha mambo ya nchi nyingine.
"Kwenda Mauritania kwa Rais kikwete ni kuwadhalilisha Watanzania ...ni sawasawa na baba mwenye familia kuacha watoto wake wanakufa njaa, yeye anakwenda kutoa chakula nyumba ya jirani," alisema Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.
Katika hotuba yake, Dk. Slaa alisema kamwe Watanzania hawawezi kuvumilia kuona usaliti wa namna hiyo unafanywa na mtu mkubwa kama Rais Kikwete, ambaye ndiye Amiri Jeshi Muu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Katika hatua nyingine, alimtaka Rais Kikwete na serikali yake kuitaifisha mitambo ya Dowans, kwani mitambo hiyo imeingizwa nchini kwa njia za kitapeli na ujanja ujanja, kinyume cha sheria za nchi.

h.sep3.gif

Vijana wataleta mabadiliko, tusiwabeze CHADEMA
ban.tusemezane.jpg

Padri Privatus Karugendo

amka2.gif
HOJA ninayoijenga hapa ni kwamba tunahitaji watu kuleta mabadiliko, lakini mara nyingi vijana ndiyo kundi muhimu sana katika jamii yoyote linalotegemewa kama chachu na nyenzo ya mabadiliko.
Duniani kote mabadiliko yameletwa na vijana. Mwalimu Nyerere, alianza mchakato wa kuleta mbadiliko akiwa na umri wa miaka 39. Mwanamapinduzi wa Cuba Fidel Castro, alianza mapambano akiwa kijana mdogo, rafiki yake Che, alikufa akiwa na umri wa miaka 39, hata Yesu wa Nazareti alikufa akiwa na umri wa miaka 33 akiwa katika harakati ya kuleta mabadiliko makubwa katika jamii yake ya Israeli.
Hivyo vijana ni muhimu sana katika kuleta mabadiliko; Mataifa yaliyo makini hayawatelekezi vijana, yanawaandaa na kuwaonyesha njia ya kupita ili walete mabadiliko yaliyo chanya; maana mabadiliko katika jamii yoyote ile ni lazima.
Mataifa yanayoshindwa kuandaa mfumo mzuri wa kuwaandaa vijana ili washike madaraka, wazalishe mali na kuendeleza uchumi wa nchi yao; yameshuhudia vijana wakijichukulia madaraka kwa nguvu.
Nchi nyingi za Afrika zilizoonja adha ya vita ya wenyewe kwa wenyewe au mapinduzi ya kijeshi ni zile zilizowapuuza vijana wake. Na mara nyingi vurugu, machafuko na vita katika nchi za Afrika vimewahusisha na kuwaathiri zaidi vijana.
Hata pale ambapo makundi ya uasi na vita hayakuongozwa na vijana, kuna ushahidi wa kutosha kwamba vijana ndio wanatumika kupigana na kuongoza mauaji. Rwanda, jeshi la Intelahamwe, liliendeshwa na vijana.
Viongozi wenye uchu wa madaraka waliwaandaa vijana kuwatumia kwa manufaa yao. Kenya, waliochoma majumba na kukata watu mapanga ni vijana. Iko mifano mingi ya kuonyesha jinsi vijana wanavyotumiwa vibaya kwa manufaa ya watu wachache wenye uchu wa madaraka.
Vijana wakiongozwa vizuri, wakipatiwa elimu bora na kuelekezwa katika njia sahihi ya kukuza uchumi na kutetea uhuru wa nchi, wanakuwa chachu ya mabadiliko. Wakiandaliwa vibaya na kupuuzwa wanakuwa kizingiti cha mabadiliko.
Tanzania tuna vijana wengi na wamegawanyika kwenye matabaka yasiyoshirikiana. Tuna kundi kubwa la vijana wasio na ujuzi na maarifa ya kujimudu kimaisha wanaohangaika kutafuta riziki mijini na vijijini. Kundi hili linaendelea kuwa kubwa siku hadi siku. Vijana hawa kwao kuishi na kufa ni mapacha, hivyo ni bomu ambalo linaweza kulipuka saa yoyote ile.
Hili ni kundi ambalo kama likiongozwa vizuri linaweza kuleta mabadiliko chanya, lakini likipuuzwa linaweza kutupeleka tusikopenda; na ni kwa vile tunaamini kuhubiri na kukemea tu inatosha!
Hata wale vijana wanaovuja jasho kubwa kutafuta riziki kwa kufanya kazi katika sekta za kilimo, biashara, uvuvi na madini hawanufaiki ipasavyo na jasho lao kutokana na vikwazo mbalimbali vikiwemo ukosefu wa mitaji, nyenzo, uongozi na maarifa.
Kundi hili la vijana maskini na waliokata tamaa haliwezi kuwa chachu ya mabadiliko tuyatakayo. Ni vigumu sana kundi hili la vijana kutunza amani na kuwa na mwelekeo wa kujenga taifa lenye maendeleo endelevu. Kundi la kati ni la wasomi wale waliopata shahada mbalimbali.
Ingawa si vijana wote katika kundi hili wanafanikiwa kupata kazi zenye ujira nzuri, wapo wachache wanaobahatika ajira nzuri serikalini na katika sekta binafsi na hata katika uongozi wa kisiasa.
Kwa bahati mbaya kundi hili dogo halijaandaliwa vema ili kuweza kutumia madaraka na fursa walizonazo kuleta mabadiliko kwa jamii zao.
Badala ya kufanya kazi na kuwa wabunifu na waaminifu, wanatengeneza mikakati ya kukwapua, kuingia kwenye mikataba mibovu yenye kuzalisha asilimia kumi za kuweka mfukoni na kujitumbukiza katika maisha ya anasa na ufujaji wa rasilimali za nchi.
Mbali na kwamba vijana wetu wametengwa kwenye matabaka ya wasomi na wasiokuwa na kisomo, wanaosoma shule za kimataifa na wale wanaosoma shule za kata, wanatofautiana sana kimtizamo kutokana na ushawishi mkubwa unaoelekezwa kwao na vikundi vyenye maslahi ya kiuchumi, kidini na kisiasa.
Kwa ujumla vijana wetu wamegawanywa kutokana na ukosefu wa mpango madhubuti wa kujenga uchumi wa kitaifa na mfumo mzuri wa elimu. Katika mazingira haya, vijana hawawezi kuwa na sauti moja.
Pamoja na ukweli kwamba tofauti katika jamii haziepukiki, bado hawana kitu cha kuwaunganisha kama vijana wa Tanzania. Na kama hawana umoja, ni vigumu kushiriki kikamilifu na kwa uaminifu katika mchakato mzima wa kuleta mabadiliko.
Enzi za Siasa ya Ujamaa na kujitegemea, tulikuwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT). Hiki kilikuwa ni chuo cha kumwandaa kijana Mtanzania kuwa tayari kulitumikia taifa lake kwa moyo wa kizalendo.
JKT, iliwakutanisha vijana kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania; pamoja na kwamba katika elimu ya sekondari, vijana wa Tanzania walikutanishwa kutoka mikoa mbalimbali na kuvunja ile dhana ya ukabila na ukanda, JKT iliimarisha msingi huu na kumjenga kijana Mtanzania, aliyekuwa tayari kwa mabadiliko.
Kuna mifano mingi ya watu waliolitumikia taifa letu kwa uaminifu mkubwa kwa vile walipitia katika mchakato wa "Kitaifa"; mchakato wa kujenga taifa. Inasikitisha kwamba hakuna mwanasiasa aliyetoa ahadi ya kufufua jeshi la kujenga taifa.
Vijana wa enzi zile, walielekeza nguvu zao zote katika kujenga taifa. Hawakukimbilia kujenga majumba yao binafsi, hawakukimbilia kununua magari ya kifahari, hawakuwa na kiburi au majivuno ya vyeo vyao, maana walijua wazi kwamba cheo ni dhamana.
Walikuwa wanyenyekevu katika kulitumikia taifa letu ili kuhakikisha kila Mtanzania anaonja matunda ya uhuru. Wengi wao wamekufa wakiwa masikini na wale walio hai, maisha yao ni ya kawaida; wana mali zile ambazo kila mtu aliyefanya kazi ya mshahara aliweza kumudu.
Vijana wa siku hizi ambao ndio tunaowategemea kusukuma mabadiliko katika taifa letu wanaelekeza nguvu zao, tamaa zao na matumaini yao katika kujenga himaya ya mali na madaraka.
Si dhambi kuwa na mali, lakini kupora wengine ili kujitajirisha binafsi, kutumia rasilimali za taifa na fedha za umma kujitajirisha binafsi ni dhambi kubwa.
Vijana wetu wasomi, wanataka wafanye kazi mwaka mmoja au miwili wawe wamejenga nyumba na kununua magari ya kifahari; wawe na nyumba ndogo kama tano, wawe na fedha ya kunywa na kulewa kila siku ya Mungu, wawe na fedha ya kuwanunua wapiga kura na ikiwezekana wawe na fedha ya kuwaweka juu ya sheria!
Kusema kweli baadhi wamefanikiwa kufanya hivyo; wana fedha na utajiri wa kutisha kuwazidi hata walimu na maprofesa waliowafundisha.
Hali hii haiwezi kuwazuia vijana wetu kujiingiza katika matendo ya rushwa, ufisadi, mikataba mibovu na mkakati mzima wa kuuza rasilimali za nchi yetu ili wajinufaishe na kujenga ufalme wao wanaoutumaini.
Tukizingatia ukweli huu juu ya vijana na matukio tunayoshuhudia sasa hivi ya kuwaondoa viongozi madarakani kwa nguvu ya umma; na ukweli kwamba CHADEMA inashabikiwa na vijana; kuyapuuza maandamano ya CHADEMA kama yale yaliyofanyika Mwanza juzi, ni kujidanganya. Tunakoelekea, vijana ndiyo jibu!
 
Maandamano ya kumwaga damu Libya yabomoa serikali
ban.blank.jpg

Datus Boniface

amka2.gif
UTAWALA wa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi uko chini ya shinikizo kali, kufuatia maandamano makubwa katika mji mkuu wa Libya huku damu ikiendelea kumwagika.
Maandamano hayo makubwa yamesababisha serikali ya Kanali Gaddafi kugawanyika vipande viwili vya Mashariki na Magharibi. Licha ya kuigawanya serikali baadhi ya viongozi wa juu wa serikali na mabalozi wake waliamua kujiuzulu.
Waziri wa sheria Mustapha Abdul Jalil amekuwa wa kwanza kujiuzulu katika uongozi wa serikali ya Gaddaffi.
Mjumbe wa serikali katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Abdel Moneim al-Honi, ametangaza kujiunga na mageuzi hayo na balozi wa nchi hiyo nchini India, Ali al-Essawi, anajiuzulu kutokana na serikali yake kutumia nguvu katika kupambana na waandamanaji.
Hayo yakiendelea naye Mohamed Bayou ambaye alijuzulu kuwa msemaji wa serikali ya nchi hiyo, anasema uongozi wa nchi hiyo umekosea katika kuwatisha waandamanaji kwa kutumia nguvu.
Naye balozi wa Libya nchini Marekani, Ali Aujali, anasema hataendelea kuiwakilisha serikali yake kutokana na kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji jambo ambalo halikubalika.
Aidha, Naibu Balozi wa Libya katika umoja wa mataifa, Ibrahim Dabbashi, anasema wananchi wa Libya lazima walindwe kutokana na kile alichokitaja kama mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na maafisa nchini humo.
Dabbashi anasema hizi ni nyakati za mwisho za Kanali Gaddafi na kwamba ni lazima afunguliwe mashtaka.
Maandamano makubwa yaliyoanza mjini Benghazi hivi karibuni, yameenea sehemu kubwa ya nchi na waandamanaji kufanikiwa kuingia mji mkuu wa nchi, Tripoli.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, waandamanaji hao wamekuwa wakishangilia kwa ushindi huo huku maandamano yakizidi kuenea sehemu kubwa zaidi ya nchi hasa mjini Tripoli.
Waandamanaji hao wameonekana kana kwamba wameshika nchi, kutokana na kufanikiwa kuingia mji mkubwa wa nchi. Magari yamekuwa yakipiga honi kama ishara ya ushindi wa kuteka mji huo.
Inaelezwa kuwa utawala wa Kanali Muammar Gaddafi uko katika wakati mgumu kwa kile kinachoonekana kuwa maandamano ya sasa yamevunja rekodi katika mji mkuu wa nchi. Eneo la magharibi mwa Tripoli inaelezwa kuwa polisi wamekimbia na majengo ya serikali yamechomwa moto na mji uko katika machafuko.
Bado majeshi ya serikali yamekuwa yakitumia mabomu ya machozi katika kuwatawanya waandamanaji hao waliokuwa wamejazana katika mitaa ya Tripoli. Upinzani nao unaahidi kuhakikisha kuwa Rais Muamar Gadaffi anaondoka madarakani.
Taarifa zinasema uwanja wa ndege wa Benghazi umefungwa huku watoto wa Rais Gaddafi wakithibitisha kupitia runinga ya taifa kuwa miji miwili mashariki mwa Libya, Benghazi na Bayda imetawaliwa na upinzani.
Lakini mtoto wa Kanali Gaddafi, Saif al-Islam, ameonya kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe huenda vikazuka. Katika hotuba ndefu kupitia televisheni, anatoa mapendekezo ya mabadiliko ya kisiasa, lakini pia kuahidi kuwa utawala huo ‘utapigana mpaka mwisho' dhidi ya ‘wachochezi'.
‘Baba na majeshi ya nchi yatapigana hadi risasi ya mwisho…,' anakaririwa katika maelezo yake kupitia runinga hiyo.
Anataadhalisha juu ya kutokea zaidi kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe akisema kuwa wafuasi wa babake watampigania kwa hali yoyote.
Licha ya kuanza kuonekana kwa mapinduzi ya wazi kwa kiongozi huyo aliyetawala Libya kwa muda wa miongo minne sasa mabalozi wa Libya katika Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati mzozo huo ili kusimamisha vitendo vya uhalifu vinavyo tekelezwa dhidi ya waandamanaji.
Kanali Muammar Gaddafi anajitokeza kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa maandamano hayo, kupitia runinga ya taifa. Ambapo inadhaniwa huenda angetoa taarifa kamili kuhusu matatizo yanayoendelea, lakini anazungumza kwa chini ya dakika moja tu.
Kiongozi huyo wa Libya anasema alikuwa akizungumza na vijana katika eneo la Green Square mjini Tripoli nyakati za jioni, na kuongeza kuwa anataka kuweka wazi kuwa niko mjini Tripoli wala sio nchini Venezuela.
Licha ya kuendelea kwa maandamano hayo watu 104 wauwawa kufuatia maandamano hayo. Taarifa za shirika la kusimamia haki za binadamu, Human Rights Watch, limekaririwa likisema zaidi ya 104 wamekufa katika siku chache za fujo za Libya.
Awali katika mji wa Benghazi hali ilikuwa ya kutisha, siku moja baada ya bunduki za rashasha na silaha za moto kutumiwa dhidi ya watu waliokuwa kwenye mazishi.
Walioshuhudia matukio hayo wanasema kulikuwa na mtafaruku wakati wanajeshi wa Libya, waliokuwa juu ya mapaa, waliwalenga na kuwafyatulia risasi waombolezaji waliokuwa kwenye maziko ya mwandamanaji aliyeuliwa na askari wa usalama.
Daktari mmoja anakaririwa akisema watu wengine waliuawa mbele ya nyumba zao, na kwamba katika hospitali nyingi kumejaa maiti.
Kambi ya upinzani inasema shambulio lililofanywa halikuwa halali kwani askari hawakuchokozwa lakini kikosi cha usalama kinadai kuwa baadhi ya waandamanaji waliwarushia mabomu.
Libya ni mojawapo ya nchi za kiarabu ambazo zimekumbwa na maandamano ya raia ni pamoja na nchi za Tunisia na Misri kuandamana na kuwalazimisha marais wa nchi hizo kujiuzulu.
Rais wa Tunisia Zine El Abidine Ben Ali aliikimbia nchi yake Januari mwaka huu naye Rais Hosni Mubarak wa Misri alijiuzulu Februari 11. Hata hivyo inadaiwa kuwa nchini Yemen na Morocco bado kunafukuta chini kwa chini.
Hali hiyo inadhihirisha kuwa nchi za kiarabu zimepata mbinu mpya ya kuwaondoa marais ving'ang'anizi madarakani. Hatua hiyo inadhihirisha ni fundisho kwa viongozi wengine wa Afrika ambao wanataka kuendelea kuongoza kwa muda mrefu bila kuleta maendeleo zaidi ya kujilimbikizia mali.
Nchini Marekani marais huanza kuzeeka au kuota mvi baada ya miaka mitano au kumi ya kukaa madarakani., huku wanasaikolojia wakilinganisha Rais Barrack Obama wakati alipoapishwa na sasa anavyoonekana.
Hali ya uzee inatokana hasa kwa kukaa kwa muda mfupi madarakani ni kutokana na kuwa na wajibu mzito wa kuwaletea maendeleo wananchi na nchi kwa ujumla. Lakini jambo kubwa kwa viongozi hao ni kuacha historia yake safi, heshima kwa vizazi baada ya vizazi.
Kwa viongozi wa nchi za kiafrika hali imekuwa tofauti wengi hawachakai bali wanazidi kunawiri na kunenepa.
 
Aliyeiroga Tanzania asipokufa tumekwisha
ban.nasema.jpg

Christopher Nyenyembe

amka2.gif
HII si mara yangu ya kwanza kuyakariri na kuyarudia maneno ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, anayoyatumia mara kadhaa kuhoji umaskini wa Watanzania umetokana na nini huku tukiwa na rasilimali tele lakini hakuna unafuu wowote wa maisha, hali ni ngumu.
Amediriki kutamka wazi kuwa ni nani aliyewaroga Watanzania mpaka tunashindwa kwenda mbele huku tukiishi kwenye nchi ya maziwa na asali, tukiishi kwenye nchi iliyozungukwa na rasilimali nyingi kila kona na hapo ndipo jibu la wapi tunapopopaswa kujilaumu kunakoanzia.
Kiini cha makala hii ya leo hakuna maana ya kutaka kuwasimanga Watanzania wenzangu ambao wote tupo kwenye adha ngumu ya ugumu wa maisha na ambao leo hii kuna watu wanaoshindwa kunywa chai wakishindwa kununua kilo moja ya sukari ambayo hutengeneza kinywaji cha kila rika hasa kwa watoto wadogo na wazee.
Nchi ikiwa imezungukwa na bahari, maziwa, mito mikubwa, mbuga za wanyama wa kila aina, vito vya thamani, madini ya almasi na dhahabu bila kusahau madini adimu hapa duniani ya tanzanite; vitu hivyo vyote vinatufanya tuitwe maskini wa kutupwa ambao tupo kwenye kundi la watu wa dunia ya tatu.
Tanzania ni nchi ya kujivunia ambayo utalii wa ndani unazidi kukua kutokana na uwepo wa vivutio vikubwa vilivyopo bila kusahau kuwa yapo maeneo ambayo kuna dalili za kuwepo kwa mafuta chini ya ardhi lakini watu wanakufa bila kuona hata tone la mafuta likitoka katika nchi hii.
Utajiri wa Tanzania umeifanya iwe nchi yenye mbuga nzuri na za kuvutia, zenye rutuba zinazofaa kwa ajili ya kilimo cha masika na kiangazi lakini hakuna tunachoweza kujivunia kwa hilo kwa kuwa wakulima wengi wanategemea mvua badala ya kuwa na miundombinu ya uhakika ya kilimo cha umwagiliaji kutoka kwenye mito na maziwa yaliyopo.
Hii ndio Tanzania ambayo leo hii imevishwa jina zuri na la kupendeza kuwa ni moja ya nchi masikini duniani, ikikaliwa na watu makini,wanaosifika kwa utulivu na amani waliyonayo ambayo inawazuia kusonga mbele na kuendelea kuzalisha kundi la watu masikini kila siku.
Hapo ndipo zinapojitokeza hoja nyingi na hatimaye hata mtendaji mkuu wa shughuli za Serikali, waziri mkuu anapojiuliza maswali mara kadhaa hivi: "Watanzania tumerogwa, tuna kila kitu, kwa nini hatusongi mbele ni nani anayepaswa kutunasua kutoka hapa tulipo, hivi mchawi wetu ni nani?"
Lazima tujiulize sana na tutafute dawa ya kumjua mtu aliyewaroga Watanzania ilhali wana kila kitu lakini bado wanabaki na sifa ya kuitwa maskini, tatizo ni nini na nani anapaswa kutafuta mwarobaini wa kutibu maradhi haya ya umaskini? Viongozi wakilalamika nani analo jibu muafaka la kumjua aliyeiroga Tanzania.
Wakati tukitafakari na kutaka kujua kiini cha umaskini wetu na matatizo lukuki yanayoikumba jamii lazima ijulikane wazi ni wapi zilipokwama jitihada za kuwasukuma Watanzania hawa ili waweze kuondokana na kadhia mbaya ya umaskini ambayo haipaswi kuonekana au kuwakumba watu hawa.
Watanzania wamelalia mto wa tanzanite, godoro la almasi, shuka la dhahabu, wakinawa maji ya waridi yaliyotulia kwenye bahari na maziwa huku wakiogelea kwenye mito mikubwa na kupumzika chini ya mbuga nzuri za wanyama, kisha hupanda juu ya Mlima Kilimanjaro ili kutukuza utajiri wao waliopewa bure, wanalia kuwa ni maskini.
Wanyama wa kila aina wamekuwa wakiwatukuza Watanzania kwa utajiri walionao, huku wakiimbiwa nyimbo na ndege wa kila aina warukao angani na kulipamba vyema anga la Tanzania, hayo yote yanaonekana ni kitu bure na kuendelea kutangaziwa umaskini mkubwa tulionao.
Tanzania kuwa nchi omba omba kwa mataifa makubwa duniani kunatutia aibu, kunazifanya nchi hizo wahisani zirudishe ukoloni mambo leo na kwa masharti yao nchi huongozwa kwa nguvu zao, kinachobaki mikononi mwetu ni kuwa na bakuli la kuombea msaada huku nchi ina kila kitu.
Lazima ufike wakati tujiangalie hapa tulipofikia, haiwezekani kwa muda wa miaka 50 tangu tulipopata Uhuru, nchi ishindwe kusimama yenyewe ikiongozwa na vichwa vya viongozi wanaoiongoza nchi salama isiyokuwa na majanga makubwa kama yanavyozikumba nchi nyingine, tumekosa nini, kwanini watanzania wawe masikini.
Hivi kweli kwa kipindi cha miaka hiyo 50 ya uhuru nchi imeshindwa kuwa na vyanzo vya uhakika vya kuzalisha umeme na kujikuta nchi ikiingia kwenye mikataba inayoitokea puani, eti leo hii tunapaswa kumlipa bilionea mmoja mabilioni ya fedha za Dowans wakati wasome wengi wa mambo ya umeme na kwa kutumia vyanzo vyetu tusingefika hapo.
Haya matatizo yanayoikumba nchi, kupanda kwa gharama za maisha na kukosekana kwa huduma muhimu hasa maeneo mengi ya vijijini kumesababisha athari kubwa za utunzaji wa maliasili zetu,misitu minene imekatwa na kuyaacha mapori mengi yakigeuka jangwa kwa kukata miti ovyo na kuchoma mkaa kwa kuwa umeme haushikiki.
Kwa kuwa mafuta ya taa yanayotegemewa na Watanzania wengi huko vijijini hayashikiki kwa bei, watu wamerudi enzi za ujima, wanatumia vijinga vya moto kuangazia usiku, vikongwe wataendelea kuuawa hadi lini kwa imani za kishirikiana hasa baada ya macho yao kuonekana kuwa mekundu kwa sababu ya moshi mkali wa kuni.
Ndiyo maana nasema hivi, mtu huyu aliyeiroga Tanzania asipokufa tutakwisha kwa kuwa hakuna njia mbadala inayoleta matumaini mazuri ya kurejesha maisha bora kwa kila Mtanzania, hali inazidi kuwa tete si mijini wala vijijini kila sehemu ni kilio tu.
Ni nani aliyewaroga Watanzania ambao ujasiri wao na uvumilivu wao pengine umegeuka na kuwa fimbo ya mafisadi ya kuwapigia watu masikini ili wasiweze kunyanyuka hapo walipo, wakiliacha kundi la watu wachache wakiitafuna nchi watakavyo wengine wakizidi kulia na kusaga meno kwenye nchi ya asali na maziwa.
Ipo haja na iwe wajibu kwa serikali kutafakari kwa kina ahadi zote zilizokuwa zikitolewa na chama tawala (CCM) wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2010 zimeanza kutekelezwa au hazitekelezeki, mbona hali ya maisha inazidi kuwa ngumu kwa Watanzania hawa ni nani anayeweza kuwaokoa ?
Mbona zile kaulimbiu za maisha bora kwa kila Mtanzania haziimbiki, mbona waliokuwa wakiimba wamenyamaza kimya, kwa ukimya huo ina maana kuwa tayari ahadi zote zilizokuwa zikipambwa kwenye majukwaa zimetekelezwa?
Tukimjua mchawi aliyewaloga Watanzania tunaweza kupata jibu kuwa hata viongozi wetu pengine wanawaogopa wachawi waliozingira uchumi wetu, wanawaogopa mafisadi waliotanda pembeni mwa nyumba zao bila kujali ulinzi salama uliopo, kama ni hivyo tusubiri mtu aliyeiroga Tanzania afe, asipokufa tumekwisha.
 
Na bado! Tuna mkakati mzito wa kuiongezea nguvu chadema....tutaunganisha makundi yote ya kijamii
 
DK Slaa atibua mambo kwa Wassira Send to a friend Sunday, 27 February 2011 21:04

_dk%20wilbord%20slaa.jpg
Katibu mkuu wa Chadema,Dk Wilbroad Slaa

Anthony Mayunga, Bunda na Frederick Katulanda, Butiama
ALIYEKUWA mgombea ubunge wa ubunge kwa tiketi ya Chadema jimbo la Bunda Elias Maarugu ametimuliwa kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho uliohutubiwa na katibu mkuu Dk Wilbroad Slaa baada ya kukataliwa
na wananchi kwa madai kuwa alihongwa na kumwachia Stephen Wasira.

Dalili za kumkataa Maarugu zilianza mapema mara baada ya kuitwa asalimie wananchi mjini Bunda, umati mkubwa wa wananchi ulipiga kelele na kudai hawataki kumsikiliza kwa kuwa aliwasaliti na kuuza haki zao.

Wananchi hao walipiga kelele wakisema hawako tayari kumsikiliza huku wakimtaka atoke jukwaani kwa kuwa hafai, "hatumtaki huyo mtoeni hapo aliuza kura, alihongwa msaliti hafai mtoeni hatutaki kumsikiliza."

Kelele hizo zilisikika sauti kwa nguvu za wananchi waliojaza uwanja wa stendi ya zamani.

Licha ya Maarugu kujikakamua na kusema Peoples, wananchi walipaza sauti na kumtaka atoke haraka sana," hatutaki kumsikiliza huyo mtoeni huyo hafai msaliti alikuwa wapi kwanini amekuja leo siku zote alikuwa
wapi?"walihoji.

Kutokana na kelele na wananchi kugoma kumsikiliza Dk Slaa alilazimika kuingilia kati na kusema kuwa, "sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, hivyo kama umma wote huu unakukataa ndugu yangu Maalugu kuna kitu naomba utueleze kwa nini watu hawa wanakukataa."

Hata hivyo katibu mkuu huyo kuwataka wananchi wawe na subira wananchi waliendelea kugoma na kusema kuwa hawako tayari kumwona wala kumsikiliza hivyo wakamtaka atoke eneo hilo.

"Maarugu Chadema inapinga ufisadi ndani na nje ya chama kama unatuhumiwa wewe ni mtu mzima na kuheshimu sana nakuomba uamke taratibu uage uende kwako na sisi tunakuchunguza, natamka kuanzia sasa
kuwa nakufutia ugombea wa miaka mitano ijayo kwa kuwa hufai maana nakataliwa na wananchi, nitatoa taarifa kwenye kamati tendaji ya chama,"alisema.

Kutokana na kauli hiyo Maarugu ambaye aliwahi kuwa mkuu wa wilaya ya Magu na Misenyi alilazimika kushuka taratibu huku akizomewa na maelfu ya wananchi waliokuwa wamefurika hapo,huku Dk Slaa akiwasihi wananchi
wasimpige,kumtukana kwa kuwa suala lake bado linachunguzwa na wananchi watapewa majibu.

Aliagiza kamati tendaji ya chama wilaya kuketi haraka kujadili kisha kutoa taarifa kwake ndani ya wiki mbili, na kama wataridhika nayo wataifanyia kazi,vinginevyo watalazimika kuunda kamati maalumya kufuatilia kwa kuwahoji wananchi wa jimbo hilo.

Mapema Mkurugenzi wa mambo ya Bunge na halmashauri wa chama hicho John Mrema alisema kitendo hicho hakipaswi kuvumiliwa hata kwa viongozi wengine wa chama hicho na kuwa chadema mambo yao yako wazi.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amekataa madai ya wakazi wa Tarime kudai kuwa kura zao zilichakachuliwa na CCM kushinda Ubunge katika jimbo hilo.

Akizungumza jana katika uwanja wa mpira wa barabara ya Nyamwaga, mwenyekiti wa Chadema, alisema hakubaliani na hoja za watu kusingizia chama chake kilishindwa uchaguzi kutokana na kuchakachuliwa kura bali mgawanyiko wa ndani.

Alisema katika kipindi cha uchaguzi alifika Tarime na kukaa kikao na viongozi wa chama chake Tarime na kubainisha kuwa katika kikao hicho aliwaeleza wazi kama hawajui kushindwa uchaguzi na kama wamesahau kutawaliwa na CCM basi wajue kuwa watajifunza pale ambapo kiti cha ubunge kitakapo ondoka.

"Niliwaeleza katika kikao cha ndani kama hawajui hathari za ubinafsi basi watajifunza pale watakapopoteza kiti cha Ubunge, niliwaeleza kuwa mtajifunza pale mtakapotawaliwa na CCM. Sasa kuniambia kuwa kura zilichakachuliwa nakataa…sababu naijua," alieleza Mbowe ambaye alionekana kukasirika.

Mwenyekiti huyo ambaye ni kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni, alisema ingawa alitambua mpasuko huo, yeye akiwa kiongozi wa chama mwenye dhamana ya kupitisha majina ya wagombea, walipoletwa waliogombea waliwapima kwa vigezo na kuamua kulirudisha jina la Waitara Chacha.

"Leo nalisema hili ili mjue kuwa pale ubinafsi unapotawala katika harakati za ukombozi ni hatari sana…, Mwera alikuwa anataka kuwa mbunge, Waitara, Heche na Matage, wote hawa waliutaka ubunge lakini hawawezi kuwa wote ni lazima ashinde mmoja," alifafanua.

Alisema kuwa kila mmoja anayo haki ya kugombea ubunge lakini inapofikia kila mmoja anataka kushinda hapo ndipo inapokuwa ngoma.

"Nasema tulirudisha jina la Waitara, hatujutii hilo na wala watitajutia. Mwera anaona ahaa…, nadhani hakuridhika, siwezi kujadili mtu hapa na Mwera namheshimu. Basi hapa ndipo ukatokea mgawanyiko na ninyi mkawashabikia mkasahau tatizo siyo mtu bali ni kushinda ubunge," alisema Mbowe.

Alisema lakini tokea kumalizika kwa uchaguzi huo watu wakawa wanasema kuwa walisalitiwa na wao kwa wao na wengine kwenda nje ya wilaya kusaidia kampeni jambo ambalo alisema siyo kweli na kusema kwa vile uchaguzi umekwisha sasa ni zamu ya kujipanga na kuangalia walipokosea na kujiandaa kwa uchaguzi.

"Sitaki kusikia hili la kuchakachuliwa kura Tarime, kama mnadai kuwa mlichakachuliwa kura mlikuwa wapi? Ukerewe ambao walikuwa wakiambiwa mambo kama tarime wameshinda, mabomu yalipigwa lakini wakerewe walikomaa na matokeo yakatangazwa, Mwanza risasi za moto zilipigwa na mabomu usiku kucha siku tatu lakini wakaona looo watangaze sasa Tarime mlikuwa wapi?" alihoji Mbowe.
 
Madaraka Nyerere aitabiria Chadema ushindi 2015 Send to a friend Sunday, 27 February 2011 20:56

Frederick Katulanda, Butiama
MJANE wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere, jana aliwaombea dua njema kwa Mungu, viongozi wakuu wa Chadema huku mtoto wake, Madaraka Nyerere, akikitabiria chama hicho kupata ushindi wa kura milioni sita dhidi ya kura milioni nne za CCM, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 .

Hatua hiyo inakuja wakati viongozi wa chama hicho cha upinzani, wakiwa katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, kuendesha maandamano ya kuishinikiza serikali, isilipe tuzo ya Sh94 bilioni kwa Kampuni wa Dowans.

Tuzo hiyo imetolewa na Mahakama ya Kimatafa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara, baada ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuvunja mkataba kati yake na Dowans.

Maandamano ya Chadema katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, yamekuwa yakiungwa mkono na maelefu ya wananchi.

Jana maandamano hayo yalifanyika katika Kijijni cha Butiama, Musoma Vijijini alikozaliwa na kuzikwa mwasisi wa taifa la Tanzania Mwalimu Julius Nyerere.Viongozi wa chama hicho na baadhi ya wananchi, walikwenda kwenye kaburi la kiongozi huyo, ili kuomba dunia.

Akizungumza mbele ya kaburi hilo, Mama Maria aliomba akisema "mtumishi wa Mungu, tazama hawa viongozi wanaokuja mbele yako, wanafanya kazi, tunakuomba kila mmoja wao umwezeshe kutambua kuwa yeye ni mtumishi wa watu tu."

Hata hivyo, jukumu la kuzungumza alipewa Madaraka ambaye alisema aliposikia habari kuhusu maandamano, hakuelewa vizuri, lakini sasa ametambua na kuamini kuwa hilo ni jambo jema.

Madaraka alisema kwa muda mrefu amekuwa akikitambua chama tawala na kwamba alikuwa hawajui Makongoro na Mbowe akimaanisha kuwa taifa halikuwa na ubaguzi wa dini wala ukabila.Alisema hata hiyo sasa ameanza kutambua na kuona tofauti.

"Kazi ya upinzani ni kusaka kura. Nilisikia katika uchaguzi uliopita kuwa watu walipiga kura na wengine hawakupiga kura. Sasa nadhahi mwaka 2015 watakaopiga kura watakuwa milioni 12 na CCM watapata kura milioni sita lakini, Chadema wao watapata kura milioni sita. Hizi nyingine milioni mbili zitakuwa za watu ambao hawatapiga kura," alisema Madaraka.

Madaraka pia ni mume wa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chadema, Leticia Nyerere.

Kabla ya kuchaguliwa mbunge wa viti maalumu, Leticia aligombea ubunge katika Jimbo la Kwimba, lakini alibagwa Shanif Mansoor wa CCM.

Mbali na Leticia Nyerere, Chadema ina mbunge mwingine kutoka katika familia ya Baba wa Taifa, anayejulikana kwa jina la Vicent Nyerere. Vicent ni mbunge wa kuchaguliwa katika Jimbo la Musoma Mjini.

Madaraka alisema kwa sasa hana shaka na Chadema kwa sababu chama kinakubalika kwa wananchi na kwamba hiyo inatokana na jinsi viongozi wanavyojipanga.

Alisema kujipanga huko ni pamoja na kupita mikoani wakitetea wananchi na kunadi sera.

Madaraka alisema wakati fulani hakuelewa mantiki ya wabunge wa Chadema, kususia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, lakini sasa anajua.

"Lengo lenu ni zuri, unaweza kuwa na lengo zuri sana lakini likapotoshwa kwa makusudi. Kwa hiyo mkipita kuwapambanulia wananchi, wataelewa tu," alisema Madaraka.

Katika Kijiji cha Butiama, wabunge hao na viongozi wa Chadema, walikaribishwa na mtoto mwingine wa hayati baba wa taifa Makongoro Nyerere, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mara.

Baada ya kupokewa na Madaraka Nyerere, walisalimiana na Mama Maria Nyerere na baadaye Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alimshukuru kwa kuwakaribisha Butiama.

"Tunakutakia mema, tunakuomba utuombea, tunaomba utuunge mkono pale panapotakiwa, taifa letu bado linaitegemea familia yenu," aliomba dua Mbowe.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa sala katika kaburi la Baba wa Taifa, Katibu Mkuu wa chama hicho,Dk Willbroad Slaa, alisema kwa sasa kanisa liko katika mchakato wa kumtangaza Nyerere kuwa Mtakatifu.

Dk Slaa alitilia mkazo mchakato huo akiwataka Watanzania kuombea suala hilo ili likamilishwe kwa wakati uliopangwa.

Leo maandamano hayo yaliyoanza jjini Mwanza juzi, yataelekea katika Mkoa wa Kagera.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments

0 #1 elibariki yerald 2011-02-28 08:07 soneni mbele wanaume dunia na umma wa watanzania upo nyuma yenu kazi inaonekana na Mungu awazidishie mzidi fanikiwa...msilewe na kuungwa mkono mwanzoni na baadaye mkajisahau maana maadui ni wengi wanawatafuta...lakini mkijua ndio mnaanza kazi mtafika mbali Tanzania yenye neema inawezekanaaa
Quote

Uvujaji nyaraka za siri bado waitesa serikali Send to a friend Sunday, 27 February 2011 20:51 0diggsdigg

Ramadhan Semtawa
KUENDELEA kuvuja kwa nyaraka za siri kumezidi kuitesa serikali, baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Hawa Ghasia, kueleza wabunge jinsi tatizo hilo linavyokua, huku taarifa yake ikifichwa kwa kile kilichoitwa ni nyaraka ya siri.

Tayari, Ghasia kwenye Bunge la Tisa aliwahi kuonya watumishi wa umma wanaovujisha nyaraka za siri za serikali, kauli ambayo ilionekana kwa wakati huo kuchukizwa na mabomu aliyokuwa akiyarusha Dk Willibrod Slaa, akiwa Mbunge wa Karatu.

Ghasia alirejea kilio hicho juzi akifafanua mbele ya wabunge wa Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala, na kuweka bayana kuwa serikali inaendelea kupambana na tatizo hilo.

Hata hivyo, akichangia hoja hiyo Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, alihoji jinsi uvujaji huo unavyoendelea na wahusika wakiwamo wabunge hasichukuliwi hatua.

Mtemvu alifafanua kwamba wabunge hawako juu ya sheria, hivyo kama wanakutwa na nyaraka hizo za siri za serikali, ni vema wangechukuliwa hatua za kisheria.

"Waziri umeelezea hili la kuvuja kwa nyaraka za siri za serikali. Mimi nasema kama nyaraka zinavuja na wahusika wanajulikana hata kama ni sisi wabunge sheria ichukue mkondo wake," alisisitiza Mtemvu.
Mtemvu alisema nyaraka za siri wakati mwingine zinasambaa hadi mitaani na kutumika kufungia maandazi.

Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Gosbert Blandes, akichangia taarifa hiyo alisema kitendo cha kutokea matatizo ya mikataba kama Richmond kinaonyesha kuna tatizo kwa watumishi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Blandes alihoji uwezo wa watumishi wa ofisi ya AG na kusisitiza: "Serikali lazima iwaendeleze vijana elimu...kwa sababu haitoshi tu kumchukua mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam halafu akae pale aingie mikataba mikubwa ya kimataifa."

"...hawa lazima wapewe elimu zaidi ili waweze kukabiliana na mahitaji makubwa ya ushindani wa kitaaluma katika kuandaa mikataba mbalimbali mikubwa ya kimataifa."

Kuhusu watumishi hewa, Blandes alishangaa kuona karne hii ya sayansi na teknoloji serikali inaendelee kulia na watumishi hewa wakati kuna mfumo imara wa kuhifadhi taarifa kwa kompyuta.

Kuhusu ongezeko la mishahara ya watumishi, mbunge huyo aliweka bayana kwamba kwa kuangalia ukali wa maisha ikiwamo mfumko wa bei ya vitu, serikali imekuwa ikihadaa watumishi katika kile inachokiita nyongeza ya mshahara.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments

0 #2 elibariki yerald 2011-02-28 08:16 WAZALENDO NA WANAWEMA WA TANZANIA MUENDELEE KUVUJISHA SIRI ZA SERIKALI KWASABABU HAWAPENDI KUONA UNYAMA UNAOFANYWA NA VIONGOZI KUITAFUNA NCHI YETU...SIRI GANI ZA KUHUJUMU NCHI? NA WEWE BLADES SI UMECHAKACHUA MATOKEO KARAGWE? HAUNA JIPYA MTEMVU NA WEWE MIGOGORO YANGA WAHUNI TU NYIE

WANAUCHUNGU NA NCHI NDIO MAANA WANAVUJISHA SIRI,,SIRI NI ILE YENYE MANUFAA KWA WATANZANIA NA SIO UWONGO KWANINI NANI AKYEWAAJIRI SI WANANCHI KWAHIYO TUNA HAKI KUJUA NA WAWAKILISHI WETU NI LAZIMA WATUAMBIE WANATIMIZA WAJIBU WAO...

WACHAWI NI NIYI WENYEWE AMBAO MNAHUJUMU UCHUMI NA KUIBA RASILIMALI ZETU NA SIO WATUMISHI HAO WA AG.SONENI MBELE TUNAKOMBOLEWA SIO MUDA....

HEKO WANAWEMA, HEKO WANANCHI ,HEKO WATANZANIA NA WANAJAMII WOTE WAPENDAO UTU NA HESHIMA KWA KILA MTU.

Quote

+1 #1 Mhifadhi 2011-02-28 04:01 Uvijaji wa nyaraka unatokana na wale walio maofisini kuona uchungu kwa taifa kwa sababu ya madudu yanayotendwa na viongozi wao. Si dhani kama mikataba inayovuja ingekuwa wazi na yenye maslahi kwa umma kungekuwa na haja ya kuizungumzia ila kwa maana inaonekana inaliua taifa ndo maana watu wanaita kwa umma kwa njia zisizofaa. Swala hapa ni kuwa na uwajibikaji na utawala bora. Madudu mengi yanafichwa ktk taasisi za umma kwa kisingizio cha kuwa ni nyaraka za siri. Ni vyema serikali na taasisi zake zikajirekebisha ktk kulipigania taifa kwa ukweli ndipo tuanze kuzungumzia uvujaji wa nyaraka. Swala la mishahara nadhani serikali haijaona matokeo yake. Huoni wanafunzi wanafeli mitihani? hicho ni kiashiria cha kwanza kuwa watu wamechoka, vingine vitakuja taratibu
Quote

Uvujaji nyaraka za siri bado waitesa serikali Send to a friend Sunday, 27 February 2011 20:51 0diggsdigg

Ramadhan Semtawa
KUENDELEA kuvuja kwa nyaraka za siri kumezidi kuitesa serikali, baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi), Hawa Ghasia, kueleza wabunge jinsi tatizo hilo linavyokua, huku taarifa yake ikifichwa kwa kile kilichoitwa ni nyaraka ya siri.

Tayari, Ghasia kwenye Bunge la Tisa aliwahi kuonya watumishi wa umma wanaovujisha nyaraka za siri za serikali, kauli ambayo ilionekana kwa wakati huo kuchukizwa na mabomu aliyokuwa akiyarusha Dk Willibrod Slaa, akiwa Mbunge wa Karatu.

Ghasia alirejea kilio hicho juzi akifafanua mbele ya wabunge wa Kamati ya Bunge ya Sheria, Katiba na Utawala, na kuweka bayana kuwa serikali inaendelea kupambana na tatizo hilo.

Hata hivyo, akichangia hoja hiyo Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, alihoji jinsi uvujaji huo unavyoendelea na wahusika wakiwamo wabunge hasichukuliwi hatua.

Mtemvu alifafanua kwamba wabunge hawako juu ya sheria, hivyo kama wanakutwa na nyaraka hizo za siri za serikali, ni vema wangechukuliwa hatua za kisheria.

“Waziri umeelezea hili la kuvuja kwa nyaraka za siri za serikali. Mimi nasema kama nyaraka zinavuja na wahusika wanajulikana hata kama ni sisi wabunge sheria ichukue mkondo wake,” alisisitiza Mtemvu.
Mtemvu alisema nyaraka za siri wakati mwingine zinasambaa hadi mitaani na kutumika kufungia maandazi.

Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Gosbert Blandes, akichangia taarifa hiyo alisema kitendo cha kutokea matatizo ya mikataba kama Richmond kinaonyesha kuna tatizo kwa watumishi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Blandes alihoji uwezo wa watumishi wa ofisi ya AG na kusisitiza: “Serikali lazima iwaendeleze vijana elimu...kwa sababu haitoshi tu kumchukua mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam halafu akae pale aingie mikataba mikubwa ya kimataifa.”

“...hawa lazima wapewe elimu zaidi ili waweze kukabiliana na mahitaji makubwa ya ushindani wa kitaaluma katika kuandaa mikataba mbalimbali mikubwa ya kimataifa.”

Kuhusu watumishi hewa, Blandes alishangaa kuona karne hii ya sayansi na teknoloji serikali inaendelee kulia na watumishi hewa wakati kuna mfumo imara wa kuhifadhi taarifa kwa kompyuta.

Kuhusu ongezeko la mishahara ya watumishi, mbunge huyo aliweka bayana kwamba kwa kuangalia ukali wa maisha ikiwamo mfumko wa bei ya vitu, serikali imekuwa ikihadaa watumishi katika kile inachokiita nyongeza ya mshahara.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments

0 #2 elibariki yerald 2011-02-28 08:16 WAZALENDO NA WANAWEMA WA TANZANIA MUENDELEE KUVUJISHA SIRI ZA SERIKALI KWASABABU HAWAPENDI KUONA UNYAMA UNAOFANYWA NA VIONGOZI KUITAFUNA NCHI YETU...SIRI GANI ZA KUHUJUMU NCHI? NA WEWE BLADES SI UMECHAKACHUA MATOKEO KARAGWE? HAUNA JIPYA MTEMVU NA WEWE MIGOGORO YANGA WAHUNI TU NYIE

WANAUCHUNGU NA NCHI NDIO MAANA WANAVUJISHA SIRI,,SIRI NI ILE YENYE MANUFAA KWA WATANZANIA NA SIO UWONGO KWANINI NANI AKYEWAAJIRI SI WANANCHI KWAHIYO TUNA HAKI KUJUA NA WAWAKILISHI WETU NI LAZIMA WATUAMBIE WANATIMIZA WAJIBU WAO...

WACHAWI NI NIYI WENYEWE AMBAO MNAHUJUMU UCHUMI NA KUIBA RASILIMALI ZETU NA SIO WATUMISHI HAO WA AG.SONENI MBELE TUNAKOMBOLEWA SIO MUDA....

HEKO WANAWEMA, HEKO WANANCHI ,HEKO WATANZANIA NA WANAJAMII WOTE WAPENDAO UTU NA HESHIMA KWA KILA MTU.

Quote

+1 #1 Mhifadhi 2011-02-28 04:01 Uvijaji wa nyaraka unatokana na wale walio maofisini kuona uchungu kwa taifa kwa sababu ya madudu yanayotendwa na viongozi wao. Si dhani kama mikataba inayovuja ingekuwa wazi na yenye maslahi kwa umma kungekuwa na haja ya kuizungumzia ila kwa maana inaonekana inaliua taifa ndo maana watu wanaita kwa umma kwa njia zisizofaa. Swala hapa ni kuwa na uwajibikaji na utawala bora. Madudu mengi yanafichwa ktk taasisi za umma kwa kisingizio cha kuwa ni nyaraka za siri. Ni vyema serikali na taasisi zake zikajirekebisha ktk kulipigania taifa kwa ukweli ndipo tuanze kuzungumzia uvujaji wa nyaraka. Swala la mishahara nadhani serikali haijaona matokeo yake. Huoni wanafunzi wanafeli mitihani? hicho ni kiashiria cha kwanza kuwa watu wamechoka, vingine vitakuja taratibu
Quote
 
Familia ya Nyerere yawapongeza CHADEMA

Na Suleiman Abeid, Butiama

VIONGOZI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana walitembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambako walipewa
matumaini kuwa wanaweza kuibuka na ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 na kuongoza nchi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 50 ya uhuru.

Ubashiri huo umetolewa jana kijijini Butiama na mmoja wa watoto wa hayati baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Bw. Magige Kambarage alipokuwa akitoa shukrani zake kwa viongozi wa CHADEMA waliokuwa wamekwenda kijijini Butiama kuzuru kaburi la hayati baba wa Taifa na kumjulia hali mjane wake, Mama Maria Nyerere.

Msafara wa viongozi wa CHADEMA ukiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa uliwasili kijijini Butiama saa 6.00 mchana jana na kupokewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mara, Bw. Makongoro Nyerere ambaye pia ni mmoja wa watoto wa hayati baba wa taifa.

Akiukaribisha msafara huo uliojumuisha wabunge mbalimbali wa chama hicho, Bw. Makongoro aliupongeza ujumbe huo kwa kuona umuhimu wa kufika Butihama, na hasa nyumbani kwao, kuwajulia hali na kutembelea kaburi la marehemu baba yao, kwa kuwa siasa si uadui.

Baada ya kutembelea kaburi hilo na kuweka mashada ya maua, Bw. Kambarage aliwapongeza viongozi wa CHADEMA kwa uamuzi wao wa kuendesha maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima ili kuzungumzia mstakabali wa Taifa la Tanzania.

Kugombana ndani ya siasa ni ujinga tu ndiyo unaotusumbua, mimi nasema kitendo hiki cha maandamano mlichokifanya ni kitendo kizuri sana, pamoja na kwamba mimi ni mwanachama wa CCM, lakini nakupongezeni,� alisema.

Hizi safari za kutembea kwa miguu na kushirikiana na wananchi ni kitu muhimu, eleweni kwamba mna dhamana kubwa hivi sasa mbele ya umma wa Tanzania, kwani ninyi ndiyo kambi kuu ya upinzani hapa nchini, fanyeni kazi msije mkapoteza dhamana mliyokabidhiwa na wananchi, umma umeishawakubali,� alieleza Bw. Kambarage.

Alisema katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana, watu wengi hawakujitokeza kupiga kura, lakini wapo zaidi ya milioni 20 wenye haki ya kupiga kura, ambapo aliwataka viongozi hao wa CHADEMA wafanye kazi kubwa ya kuwatafuta waliko ili ifikapo mwaka 2015 waweze kupiga kura.

Mimi nasema hawa ambao hawakupiga kura wapo wengi sana, watafuteni waliko, 2010 CCM tulipata kura milioni tano za urais, lakini naamini mkiwatafuta hawa waliopotea, katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 CHADEMA mtazoa zaidi ya kura milioni sita na CCM tutaambulia kura milioni nne, naamini hivyo,� alieleza Bw. Kambarage.

Alisema moja ya kazi wa vyama vya upinzani nchini ni kuwainua watanzania katika mambo ambayo serikali iliyoko madarakani imeshindwa kuwatekelezea na kwamba hivi sasa Watanzania wameishakikubali chama cha CHADEMA na ndiyo maana wanakiunga mkono badala ya CCM," nakuombeeni Mungu aibariki kazi yenu,� alisema.

Awali, mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe alimweleza mama Maria Nyerere kuwa lengo la ziara yao hiyo ni kumjulia hali yeye na familia yake, kudhuru kaburi la hayati baba wa Taifa na kuomba dua katika kaburi lake ikiwa ni katika kuenzi heshima aliyokuwa nayo katika Taifa la Tanzania.

Nachukua fursa hii kukushukuru kwa heshima kubwa uliyotupatia ya kukubali kuja kukujulia hali pamoja na kutembelea kaburi la hayati baba wa Taifa, tunasema hii ni heshima kubwa kwetu sisi CHADEMA wakati tukiwa katika mkoa wa Mara kuendesha maandamano ya amani na mikutano ya hadhara kuzungumzia mstakabali wa taifa letu,

Tunaomba utuombee kwa Mungu ili tuweze kufanya kazi zetu vizuri na ikibidi kutuunga mkono, basi utuunge katika lolote lile ambalo tutahitaji kuungwa mkono na wewe, lengo letu ni moja tu kuwatumikia Watanzania ili waweze na kufaidi matunda ya uhuru wa nchi yetu,� alieleza Bw. Mbowe.

Kwa upande wake mama Maria Nyerere aliwashukuru viongozi hao wa CHADEMA kwa uamuzi wa kumtembelea ili kumjulia hali ambapo aliwaombea kwa Mungu aweze kuwapa afya njema na waendelee kuwatumikia wananchi kwa haki bila ya upendeleo wowote.

Akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Musoma na vitongoji vyake katika viwanja vya Shule ya Msingi Mukendo juzi, Bw. Mbowe alisema chama hicho hakina mpango wa kumchukulia hatua Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi mkoani Shinyanga, Bw. John Shibuda kwa vile kinaamini hakijawa na mgogoro naye.

Bw. Mbowe alilazimika kutoa ufafanuzi huo wa kuhusiana na Bw. Shibuda baada ya kutakiwa na wananchi aeleze nini hatma ya mbunge huyo ambaye amekuwa akionesha dalili za kupingana na maelekezo ya chama mara kwa mara.

Mwenyekiti huyo alijikuta akiulizwa swali hilo mara baada ya yeye kutoa ufafanuzi wa kitendo cha spika kubadili kanuni za bunge na kutaka kuilazimisha CHADEMA kuungana na vyama vingine kuunda kambi ya upinzani bungeni, wananchi hao walipiga kelele wakisema, na Shibuda, Shibudaaaa.

Kutokana na kelele hizo, Bw. Mbowe alilazimika kuwauliza wananchi hao iwapo walikuwa wakimtaka Bw. Shibuda aongee nao, nao walijibu kwamba wanachohitaji ni yeye kutoa ufafanuzi kuhusiana na madai ya kutaka kupingana na viongozi wake ndani ya CHADEMA.

Bw. Mbowe aliwaeleza wananchi kwamba Bw. Shibuda hana tatizo lolote ndani ya chama na kwama mambo yaliyokuwa yamejitokeza ni mambo madogo madogo ambayo hayawezi kusababisha mbunge huyo kufukuzwa ndani ya Chama.

Ndugu zangu napenda nikufahamisheni wazi kuwa tupo humu ndani ya vyama vya siasa kwa sura na tabia tofauti, inaweza kutokea Bw. Shibuda akashindwa kuelewana lugha na Bw. Wenje, huu huwezi kuuita kuwa ni ugomvi, ni kutofautiana kwa lugha tu ni suala la kibanadamu, ninachowaomba, tuvumiliane, Bw. Shibuda bado ni mwenzetu,� alieleza Bw. Mbowe.

Bw. Mbowe aliwaeleza wananchi hao kuhusiana na suala la msimamo wa CHADEMA kukataa kushirikiana na vyama vingine vya upinzani ndani ya bunge kwa vile baadhi ya vyama hivyo havina msimamo kutokana na vingine kufunga ndoa na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Aidha alieleza kushangazwa kwake na huruma ya machozi ya mamba kwa binadamu iliyooneshwa na Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda ndani ya bunge kwa kuvitaka vyama vya upinzani kushirikiana kwa lengo la kuwa na nguvu imara, kitendo ambacho alisema si huruma ya kweli.

Ndugu zangu haiwezi kutokea hata siku moja, adui yako akakupa ushauri wa jinsi ya kupata nguvu ili uweze kumteketeza kama alivyojaribu kufanya spika wetu wa bunge. Huyo anadai wapinzani tuungane ili tuwe na nguvu bungeni, si kweli maana tukiwa na nguvu zaidi tutakishinda chama chake.

Hizi zilikuwa ni mbinu tu za CCM katika kujaribu kusambaratisha upinzani hapa nchini, lakini sisi CHADEMA tumekataa na kubaki na msimamo wetu, hata mawaziri vivuli wote wanatokana CHADEMA, bado tunawapima hawa wenzetu ili tuone kama kweli wana dhati ya kuwa wapinzani dhidi ya CCM, alieleza Bw. Mbowe.

1 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... lazima mjiulize nyie hapo mnaonekena kama kunguru wa zenji mwenzenu kapiga jezi yake nyie zenu mbona hazifanani nanyi ?mnajidanganya tena poleni sana tu safari ni ndefu sana tu
February 27, 2011 9:21 PM
 
Butiku awaponda viongozi CCM

Imeandikwa na Nashon Kennedy, Mwanza na Mgaya Kingoba, Zanzibar; Tarehe: 28th February 2011 @ 07:33 Imesomwa na watu: 102; Jumla ya maoni: 0

KADA wa siku nyingi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Joseph Butiku amesema chama hicho kimepoteza dira na mwelekeo, amewalaumu viongozi kwa kukifikisha mahali hapo.

"CCM imepoteza dira kwa sababu kubwa mbili, kwanza ni viongozi wetu wa chama wa ngazi zote ambao wako mstari wa mbele kupoteza dira ya chama," alisema Butiku katika mkutano wa waandishi jana.

"Wameshindwa kulinda na kuendeleza maadili, miiko na kanuni za chama," alisema na kufafanua, "chama chenyewe chini ya miongozo yake na Katiba yake hakina matatizo."

Akitoa mfano kada huyo wa CCM alisema: "katika imani ya chama ya rushwa kwangu ni mwiko sitatoa wala kupokea rushwa, leo hii tunawashuhudia na kuwasikia viongozi hao wakisutana namna ambavyo walishiriki kutoa rushwa katika uchaguzi wa ubunge, na hivyo mashahidi wa utoaji wa rushwa wao ni viongozi wa CCM wenyewe."

Wakati Butiku akitoa kauli hiyo jijini Mwanza, huko Zanzibar juzi viongozi na wanachama wa chama hicho waliazimia kujipanga katika uchaguzi wa chama hicho mwakani ili wapate viongozi waadilifu.

Walisema wanataka wapate viongozi waumini wa kweli, wasiopenda kujikweza na waliopo kwa maslahi ya CCM ili kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Butiku alisema baada ya kuona mambo hayaendi vizuri katika chama, ameamua kulisemea hilo na kuahidi kwamba ataendelea kukisoa chama hicho hadharani ili viongozi wasikie na wachukue hatua za kukinusuru.

"Nasema hadharani ili viongozi wetu wa chama wasikie, maana ukiona mtu mzima kama mimi nayasema mambo haya hadharani ujue kuna jambo, ingawa ninapozungumza haya wapo wanaosema mimi ninakisaliti chama lakini mimi nasema ukweli kutoka moyoni mwangu.

"Walioshindwa ni sisi viongozi wa chama, tunahitaji tukae mahali tuzungumze ili tufanye tathimini tujue ni wapi tulipokosea maana hata wana CCM waliojitokeza kupiga kura katika uchaguzi uliopita walikuwa wachache sana, na nimekuwa nikiyasema haya lakini napuuzwa," alisema Butiku.

Kauli hiyo haikutofautiana na ya Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar Rais mstaafu Aman Abeid Karume aliyesema kuwa baadhi ya wanachama wa chama hicho walipiga kura ya hasira.

Butiku alisema katika mambo ya chama yeye atasema ukweli daima na kuwa hawezi kulisemea jambo lolote lenye maslahi ya chama kwa chuki bali dhamira yake ni safi.

"Wapo viongozi wengine katika chama wao hawataki kulisikiliza jambo la mtu yeyote, hali hii sio nzuri hata kidogo maana inalenga kumnyima haki mwanachama ya kuzungumzia mambo ya chama chake," alisema.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Pius Msekwa alipoulizwa kuhusu madai hayo ya Butiku alisema. "Hivi kweli unataka nibishane na Mzee Butiku magazetini..yule ni kada mwenzangu na ndivyo anavyoiona CCM."

Msekwa alisema haipendezi kubishana makada kwa makada kwenye vyombo vya habari na akashauri atafutwe siku nyingine na yeye atoe maoni yake namna anavyoiona CCM.

"Wewe chapisha hayo maoni yake, tutayasoma mimi na viongozi wenzangu halafu na sisi tutatoa maoni yetu baadaye."

Lakini visiwani Zanzibar katika uwanja wa Demokrasia mjini Unguja wakati wa mkutano wa hadhara wa kukipongeza chama hicho kwa kushinda uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana, Karume aliwaponda viongozi wanaong'ang'ania kugombea halafu wakashindwa, akihoji kuna faida gani ya kufanya hivyo?

Kabla ya kutoa kauli hiyo, wanachama wa chama hicho katika risala ya mikoa mitatu ya Mjini Magharibi, Kusini Unguja na Kaskazini Unguja iliyosomwa na Katibu wa Chama Mkoa wa Kusini Unguja, Shija Othman Shija, walieleza kuwa pamoja na ushindi wa asilimia 50.1 mwaka jana, CCM inakabiliwa na changamoto kadhaa kubwa.

"Mojawapo ni kukomboa majimbo tuliyoyapoteza na kuongeza kura za urais na hayo yatawezekana kwa sababu nia tunayo na sababu tunazo za kufanya hivyo.

"Aidha, tujipange vizuri kwa uchaguzi wa mwakani ili kuandaa ushindi wa mwaka 2015 kwa kuchagua viongozi waadilifu, waumini wa kweli, wasiopenda kujikweza, waliopo kwa maslahi ya CCM kwa moyo wao wote na si kulilia madaraka," ilieleza risala hiyo ya wanachama wa CCM.

"Tunaamini viongozi wetu mtatuunga mkono katika hili kwa sababu bila CCM imara nchi itayumba. Tunataka kupata viongozi bora kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa ili kujiweka katika mazingira mazuri ya ushindi kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015."

Karume alipopewa fursa ya kuzungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, aliunga mkono risala hiyo akisema chama hicho kina uwezo wa kushinda uchaguzi wowote ule, lakini lazima kibadilike.

"Tunao uwezo wa kuyakomboa hayo majimbo kama mlivyoeleza na kushinda uchaguzi, lakini lazima tubadilike. Kwani hivi ni lazima mtu ugombee, kuna faida gani ya kugombea halafu ushindwe. Sio kwamba hatupo, tupo wengi, tuwaachie wengine," alisema Karume na kushangiliwa na wana-CCM wenzake.

Alitolea mfano wa Jimbo la Nungwi ambalo katika uchaguzi mkuu uliopita, CCM ilipoteza uwakilishi na ubunge, lakini ikipata kura nyingi za urais, na kusema; "kaeni mfanye hesabu, iko namna nitawambia. Mimi sina tabia ya kuficha mambo. Wale wale wana CCM walitokea huku huku, walipiga kura za hasira."

Aliwaeleza wanachama hao pamoja na viongozi wa CCM kuwa huko waendako ni lazima wawe wakweli, waaminiane, washirikiane na kupendana, kwa sababu wamefanya hivyo huko nyuma na watafanikiwa zaidi wakiwa wamoja.

Kwa upande wake, Dk. Shein ambaye alimshinda mgombea wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad na baadaye wakaunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, alisema dunia inabadilika na watu wanaenda na wakati, hivyo CCM lazima ijiimarishe.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM aliyokuwa akiinadi wakati wa kampeni haikuwa hati ya kuombea kura, bali ataitekeleza kama ilivyoainishwa, kwa nguvu zake zote.
 
Shivji alipu ufisadi kwenye majengo

Na Gladness Mboma

BAADHI ya majengo makubwa nchini yamedaiwa kujengwa kwa kutumia fedha za walanguzi na mafisadi na fedha zinazopatikana kutokana na pango
zinahamishiwa nchi za nje kwa kigezo cha uwekezaji.

Profesa Issa Shivji wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akitoa mada iliyokuwa inahusu ardhi na ulinzi wa rasilimali katika katiba kwenye kongamano liloandaliwa na Asasi ya HakiArdhi.

Prof. Shivji alisisitiza kwamba magorofa makubwa yanayojengwa Tanzania yanajengwa na fedha za walanguzi, wanaiba fedha kutoka Tanzania wanapeleka Dubai na kisha wanarudisha fedha kiduchu na kazi kubwa ya viongozi nchini ni kuyazindua.

Alisema kuwa utakuta matajiri wanatoka Dubai wanakuja kupora ardhi na kuhamishia utajiri wote kwao na kuwa, kilichobaki sasa ni kuanza kupora mito na milima.

"Kumekuwa na uporaji wa ardhi ya kijiji na wawekezaji mafisadi wa ndani na nje kwa visingizio mbalimbali kama kilicho kwa ajili ya kuzalisha nishati, na uzalisha wa mazao ya chakula kwa ajili ya masoko ya kimataifa," alisema.

Alisema kwa miaka 50 baada ya uhuru wananchi wengi hawana haki ya kupata ardhi badala yake wawekezaji ndiyo wameipata na wamekuwa wakitumia kupora utajiri wa nchi.

Prof. Shivji alisema kuwa uporaji huo wa ardhi umesababisha maisha kuwa magumu, bei za vyakula zimepanda kwa sababu ya wananchi kukosa nafasi ya kuzalisha tena.

"Ninashauri wananchi washirikishwe katika kujadili mfumo mpya wa katiba utakaotoa fursa kwa wananchi ili wawe na nguvu ya kumiliki ardhi na rasilimali zao," alisema.

Alisema kwamba katiba ya sasa haisemi lolote kuhusu ardhi badala yake imegusia haki ya wananchi kumiliki ardhi na kusababisha utata kuhusu umilikishaji wa ardhi.

Prof. Shivji alisema madai na matakwa ya wanakijiji na wananchi waliowengi kuhusu ardhi na rasilimali zao yawe mstari wa mbele katika mjadala wa kitaifa kuhusu katiba mpya.

Naye Bw. Odenda Lumumba kutoka Chama cha Watetezi wa Ardhi Kenya alitoa uzoefu wa masuala ya ardhi na jinsi ilivyoingizwa kwenye mabadiliko ya katiba mpya ya nchi yao, alisema kuwa walianza mjadala wa muda mrefu na baadaye walifanikiwa.

Alisema kuwa wao waliandaa mapendekezo yao na kuyapeleka kwenye mchakato wa katiba na asilimia 90 ya mapendekezo yao yamepitishwa na kuwataka Watanzania kutolala usingizi katika hilo.

Bw. Bashiru Ally, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliwataka Watanzania wasisubiri kengele ya mwezi wa nne wakati muswada wa mijadala kuhusu katiba utakapopelekwa bungeni, bali waanze kuijadili sasa.

"Kuna wasiwasi wa wananchi kutoshirikishwa katika mjadala wa katiba na badala yake unaweza ukatekwa nyara," alisema.

1 Maoni:

blank.gif

Anonymous said... Profesa
Nakushukuru kwa mada yako. hiyo haipingwi ila niwakati chini ya ushauri wako utueleze tufanye nini ili kunusuru nchi. Pia waeleze viongozi walioko madarakani kwamba itakuwa aibu kwao pale wananchi watakapoamua kudai hai yao ya ardhi kwa nguvu walizo nazo, kwani itakuwa na madhara makubwa kwao na wagani jambo ambalo litakuwa ni aibu kubwa. najaribu kuangaliya yanayofanyika kwenye nchi za kiarabu na kujiuliza endapo wenye maisha bora zaidi yetu wamechoka na mambo wanayofanyiwa, itakuwaje maskini hohehahe wakiamua????????? oh. hatari iko mbele na tutashindwa kujitetea. labda uwashauri wageni waanze kuondoka kungali mapema na waiogope ardhi yetu.

February 27, 2011 9:16 PM

Post a Comment
 
Familia ya Nyerere yatabiri CHADEMA kushinda 2015
• Mama Maria aongoza sala

na Sitta Tumma na Janeth Josiah, Musoma

amka2.gif
FAMILIA ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, imekitabiria Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ushindi wa kishindo wa kuongoza nchi mwaka 2015.
Familia hiyo ya mwasisi wa taifa imesema ukomo wa serikali ya CCM umefika ambapo inaamini Uchaguzi Mkuu wa urais ujao, CHADEMA itaibuka kidedea.
Kauli hiyo ya familia ya Mwalimu Nyerere, ilitolewa jana na mtoto wa tatu wa Baba wa Taifa, Magige Nyerere, akiwa mbele ya kaburi la Baba wa Taifa wakati viongozi wa CHADEMA Taifa walipozuru nyumbani kwa mwasisi huyo Butiama, Musoma, mkoani Mara, ambapo waliweka mashada katika kaburi hilo na Mama Maria kuongoza sala.
Alisema anaamini wapigakura mwaka 2015 watakuwa milioni 12 na kati ya hao, CHADEMA itapata kura milioni sita na CCM itaambulia kura milioni nne.
Kwa mujibu wa mwanafamilia huyo wa Baba wa Taifa kwa sasa nchi iko katika joto kubwa la kisiasa.
"Lazima tuseme ule ukweli uchaguzi mkuu uliopita CHADEMA haikuweza kuongoza dola, lakini mwaka 2015 wapigakura watakuwa milioni 12 na milioni sita zitaenda CHADEMA na milioni nne CCM.
"Hali ilivyo sasa, joto la kisiasa hapa nchini liko juu na wananchi wameonekana kufanya mageuzi ya kiuongozi," alisema Magige Nyerere mbele ya mke wa Baba wa Taifa, Maria Nyerere.
Huku akimfananisha Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na mdogo wake, Makongoro Nyerere, ambaye naye alikuwapo alisema, "Nakiri kuwa mimi ni CCM, lakini nafurahia kazi na siasa yenu…naomba uendelee hivyo na hata ukiwa bungeni kama kiongozi wa upinzani."
Viongozi hao wa CHADEMA na msafara wao walizuru nyumbani kwa Nyerere majira ya saa 5:55 asubuhi kwa lengo la kumsalimia mjane wa Baba wa Taifa.
Kiongozi wa msafara huo, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, alimuomba Mama Maria kukiunga mkono chama hicho na kukiombea mema.
"Mama tumekuja kukusalimia na familia yako…CHADEMA tunaomba mtuombee na mtuunge mkono," alisema Mbowe kisha Mama Maria kutikisa kichwa kuashiria kukubaliana na maelezo hayo.
Akitoa nasaha zake mbele ya kaburi la Nyerere, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema mchakato wa Nyerere kuwa Mtakatifu mwenye kheri bado haujakamilika, hivyo raia wawe na uvumilivu.
Alisema nchi ya Uganda imepiga hatua juu ya mchakato huo, hivyo hatuna budi kuwa wavumilivu.
Kuhusu maandamano ya CHADEMA nchi nzima, Magige Nyerere alisema," Awali nilipatwa na wasiwasi mkubwa, lakini nimebaini kumbe ni maandamano mazuri; yaendelee."
Hata hivyo, mtoto huyo wa Baba wa Taifa alisema maandamano hayo ni vema yakaendelea kwa amani, ili kufikisha ujumbe husika katika mamlaka husika.
Wakiwa wilayani Tarime jana Mbowe alimtaka Rais Kikwete kuacha mara moja kuwajaza hofu Watanzania juu ya kuwepo mipasuko ya kidini. Mbowe ambaye aliongoza maandamano makubwa kabla ya mkutano, alihoji sababu ya Rais Kikwete kushindwa kuwakamata na kuwasweka ndani wanaoleta chokochoko za kidini.
Viongozi hao wa CHADEMA kesho wataendelea na ziara yao katika mkoa wa Shinyanga kwa kufanya maandamano makubwa ya kuwashukuru wananchi kwa kuwapa kura na kuwataka wananchi wapinge hatua ya serikali ya kutaka kuilipa kampuni ya Dowans.
 
Chibulunje alishutumu Jeshi la Polisi

na Danson Kaijage, Chamwino

amka2.gif
MBUNGE wa Chilonwa, Ezekiel Chibulunje (CCM), amelituhumu Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kwa kuhusika kusababisha fujo na vifo vya watu kadhaa katika Wilaya ya Chamwino mkoani hapana.
Tuhuma hizo alizitoa katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofanyika katika Shule ya Sekondari ya Dodoma, ambapo madiwani na mbunge huyo pamoja na viongozi wa serikali walikuwa wakijadili vurugu zinazoendelea kati ya wafugaji na wakulima katika kitongoji cha Wali, kata ya Izava, Wilaya Chamwino.
Chibulunje ambaye amewahi kuwa Naibu Waziri wa Miundombinu katika serikali ya awamu ya nne, alilazimika kutoa kauli hiyo baada ya kumwomba Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Chamwino, Laulent Hoya, kutoa taarifa ya uvunjifu wa amani katika kitongoji cha Wali.
Alieleza kuwa mgogoro kati ya wakulima na wafugaji wa maeneo hayo, umefikia hatua ya kupoteza maisha ya watu kwa kuwa unakuzwa na viongozi wa mkoa kwa kuwakumbatia wafugaji ambao ni Wasukuma wakati wakulima wa maeneo hayo wakiendelea kunyanyaswa.
"Nashangaa kuona viongozi wa mkoa wakidai kuwa mgogoro huo unatokana na mipaka jambo ambalo si kweli," alihoji Chibulunje.
Mbali na hilo pia aliendelea kueleza kuwa mgogoro huo ulianza kuongelewa enzi ya uongozi wa mkuu wa mkoa wa zamani William Lukuvi lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na badala yake wafugaji wamekuwa wakiendelea kulindwa.
"Jamani hivi Jeshi la Polisi linahusika katika kuweka mipaka ya maeneo yao; kazi kubwa wanayoifanya si kulinda amani ya raia na mali zake sasa maana inakuwaje polisi kutoka Kongwa wanakuja wamejaa kwenye magari kwa ajili ya kuwapiga wakulima wa kitongoji cha Wali," alihoji Chibulunje.
Baada ya mbunge huyo kulituhumu jeshi la polisi pamoja na uongozi wa mkoa kwa madai kuwa ndio wanaokumbatika migogoro hiyo mkuu wa mkoa wa Dodoma James Msekela alidai kuwa ofisi yake inashughulikia tatizo hilo kwa kufuata sheria wala siyo siasa.
 
Chadema wanavuruga nchi- JK Send to a friend Monday, 28 February 2011 21:30 0diggsdigg

akihutubukikwete.jpg
Rais Jakaya KIkwete

Ramadhan Semtawa
RAIS Jakaya Kikwete jana alilihutubia taifa, huku akitumia muda mwingi kujibu mapigo ya kauli za Chadema dhidi yake na kutahadharisha kuwa chama hicho, kina lengo la kuleta machafuko nchini."Kauli na vitendo vya wenzetu hao vyenye dhamira ya kutaka kuleta machafuko makubwa na uvunjifu wa amani nchini." alisema Rais Kikwete ambaye amekuwa kimya bila kulihutubia taifa kwa muda wa miezi miwili.

Onyo la Rais Kikwete limekuja siku chache baada ya Chadema kumpa siku tisa ikitaka mkuu huyo wa nchi atekeleze baadhi ya mambo ikiwamo kutoilipa fidia ya Sh94 bilioni kampuni ya Dowans.

Lakini, jana katika hotuba yake, Rais Kikwete pamoja na kufafanua hoja kadhaa, alisisitiza "Hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa."

Rais Kikwete alifafanua kwamba, hivi karibuni wananchi wengi wameingiwa na hofu kubwa kuhusu usalama wa nchi yao hali ambayo ni ngeni kwa Watanzania.

"Hofu hiyo inatokana na kauli na vitendo vya wenzetu wa Chadema vyenye dhamira ya kutaka kuleta machafuko makubwa na uvunjifu wa amani nchini," alieleza Rais Kikwete.

Mkuu huyo wa nchi ambaye tayari amemaliza siku 100 za ngwe yake ya pili akiwa Ikulu, aliweka bayana kuwa kufanya maandamano na mikutano ni haki ya msingi ya vyama vya siasa na raia, lakini, akaonya kuigeuza fursa hiyo kuwa jukwaa la kuchochea ghasia kwa nia ya kuindoa Serikali iliyoko madarakani kwa mabavu.

Kikwete alisisitiza kuwa hatua hiyo ni matumizi mabaya ya fursa ya kufanya maandamano na isiyostahili kuungwa mkono na Watanzania wazalendo, wapenda amani na nchi yao.

Rais alisema Tanzani ni nchi ya kidemokrasia na kila miaka mitano hufanyika uchaguzi wa kuchagua viongozi na kuweka bayana.

"Uchaguzi wa mwisho tumefanya tarehe 31 Oktoba, 2010. Kabla ya hapo tulikuwa na kampeni zilizochukua karibu miezi mwili na nusu. "

Kwa mujibu wa Rais Kikwete, katika kampeni hizo, kila chama kilielezea jinsi kitakavyokabiliana na matatizo yanayowakabili wananchi ikiwa ni pamoja na hayo yanayoyazungumzwa sasa na Chadema.

"Hatimaye siku ya uchaguzi wananchi walifanya uamuzi wa kuchagua chama walichokiamini, nacho ni Chama cha Mapinduzi.,"alieleza

"Iweje leo, miezi mitatu baadaye kwa mtu au chama cha siasa kufanya maandamano kwa masuala yale yale waliyoyasema kwenye kampeni. Siyo sawa hata kidogo," alisema Rais Kikwete.

"Kuchochea ghasia ati kwa nia ya kuiondoa Serikali madarakani ni kinyume cha Katiba na ni kuiingiza nchi katika mgogoro usiokuwa wa lazima. Tutasababisha umwagaji wa damu, watu kupoteza maisha na mali zao kuharibiwa bila sababu yoyote ya msingi,"alionya Rais Kikwete.

Kikwete alisema katika nchi ya kidemokrasia na kwa wanademokrasia wa kweli, wanapomaliza uchaguzi mmoja, hujiandaa kwa uchaguzi mwingine kwa kujenga upya chama , kuongeza wanachama, kuboresha sera na hoja pamoja na namna ya kuziwasilisha ili watu wawakubali na kuwachagua.

Rais Kikwete aliitaka Chadema kutumia Bunge kuwasilisha hoja zao badala ya mikutano ya hadhara inayotoa kauli za chuki kwa Serikali.

"Na, uwanja muhimu wa kufanya sehemu kubwa ya hayo ni katika Bunge na Halmashauri za Wilaya kupitia wabunge na madiwani wenu,"alieleza Rais Kikwete

Kikwete ambaye mara ya mwisho alitoa hotuba ya mwezi wakati wa mwaka mpya wa 2011, alisema kuacha kufanya hivyo na badala yake kuamua kuzunguka nchi nzima na kuchochea ghasia kwa lengo la kuwaondoa walioshinda ni kinyume na misingi ya demokrasia na kusisitiza

Alisisitiza "Tutajenga misingi ya hovyo na nchi yetu itakosa amani na utulivu daima."

Aliwataka Chadema kukaa chini na kujiuliza wanachokifanya na athari zake kwa wananchi akisema, "kama kila atakayeshindwa uchaguzi anafanya hivyo tutakuwa nchi ya namna gani?"

"Tanzania yetu hii yenye sifa na heshima ya kuwa nchi ya amani na utulivu itapoteza kabisa sifa hiyo na badala yake umwagaji wa damu na mateso kwa watu wasiokuwa na hatia vitageuka kuwa maisha ya kawaida." alisema.

Rais alisema kitendo hicho haikiitendei haki nchi na hata wananchi ambao viongozi wa siasa wamekuwa wakidai kuwapenda na kuwatetea.

"Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu; ndugu zetu wa Chadema wanayajua yote haya, lakini wanalo lao jambo. Wanataka kuipeleka nchi yetu pabaya kwa kukidhi uchu wao wa madaraka. Kwao sasa demokrasia haina maana, inaweza kusubiri," alifafanua Rais.

Aliwataka Watanzania kuwa makini na Chadema akisema "naomba tuyakatae mambo yao. Tusiwafuate. Waambieni mchezo wao ni hatari na ni mauti yetu. Sisi katika Serikali tutajitahidi kutimiza wajibu wetu wa kulinda usalama wa nchi yetu, watu wake na mali zao."

Hali ngumu ya maisha
Rais alikiri, "Ni kweli kuna hali ngumu ya maisha, na kukabiliana nayo ndiyo kazi tunayoendelea nayo kufanya kila siku."

"Tumeelekeza nguvu zetu na rasilimali zetu huko na mafanikio yanaonekana katika nyanja mbalimbali na maeneo mbalimbali, lakini akisisitiza, "hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa."

Alifafanua kwamba, kikwazo siyo upungufu wa sera wala dhamira, bali ni kiwango cha maendeleo madogo ya uchumi wa nchi na hivyo uwezo siyo mkubwa wa kuyakabili na kuyamaliza matatizo yote haraka kama ambavyo ingepaswa iwe.

Kikwete akirejea zama mbali za viongozi mbalimbali tangu uhuru, alisema hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliongoza kwa miaka 23 na hakuyamaliza matatizo ya maendeleo ya nchi hii.

"Na wale wa umri wangu au kunizidi wanakumbuka hali ilivyokuwa wakati anang'atuka. Hakuacha nchi ikiwa tajiri. Mzee Mwinyi kakaa miaka 10 hakuyamaliza, Mzee Mkapa nae kakaa miaka 10 hakuyamaliza. Mie nimekaa miaka mitano hayakwisha na nitamaliza mitano hayataisha yote." alisema

Alisema jambo la muhimu ni kuwa katika kila awamu nchi iweke malengo ya kupiga hatua ya kusonga mbele katika kujiletea maendeleo na kuongeza, hali iliyokuwa wakati ule sivyo ilivyokuwa mwaka 1985, wala 1995 au 2005 na ilivyo sasa.

Kuhusu mafanikio yake alisema, "Katika miaka mitano hii kuna maendeleo yanayoonekana wazi, pamoja na changamoto nyingi tumefanya juhudi kubwa na mafanikio yanaonekana katika nyanja zote za maisha ya Watanzania. Mwenye macho haambiwi tazama.''

Rais alirejea matukio mbalimbali yanayoitikisa dunia, akisema ni muhimu watu kutambua ukweli kwamba uchumi kama wetu ambao haujajenga uwezo wake wa ndani wa kujitosheleza kwa mahitaji yake, huathirika sana na yanayotokea katika uchumi wa dunia.

"Unapoyumba na sisi tunayumba. Bei za mafuta katika soko la dunia zikipanda na kwetu kupitia gharama za uchukuzi na uzalishaji huongezeka na kusababisha bei za bidhaa kupanda," alifafanua Rais akitaka wananchi wafahamu jinsi athari za dunia zinavyoweza kugusa uchumi wa nchi.

Mfumuko wa bei ukipanda China, nguo na bidhaa tunazonunua kutoka China hupanda bei. Hivi sasa mataifa yote makubwa tunakonunua bidhaa mfumuko wa bei umepanda na sisi tunaathirika.

Alihoji, "mvua ikikosekana kunakuwa na uhaba wa chakula, bei za vyakula hupanda na watu wengine hukosa chakula. Lawama kwa Serikali au Rais Kikwete inaanzia wapi?

Hali ya Umeme
Rais alikiri pia hali ya upatikanaji wa umeme nchini kwamba ni mbaya na kuweka bayana, "chanzo cha matatizo ni kupungua sana kwa maji katika bwawa kubwa la Mtera.

"Hadi jana kina cha bwawa hilo kimeshuka hadi kufikia mita 691.25 ambacho ni pungufu kwa mita 7. Kwa sasa zimebaki mita 1.25 tu juu ya kiwango cha chini kinachoruhusiwa kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme,"alisema.

Hata hivyo, alisema 15 Februari, 2011, Baraza la Mawaziri lilijadili na kuidhinisha mpango wa dharura wa Tanesco wa kukodi mitambo ya kuzalisha MW 260 za umeme na kuongeza, baraza limeitaka bodi na menejimenti ya shirika hilo kuhakikisha mchakato huo unakamilika mapema iwezekanavyo ili kupunguza makali na athari za ukosefu mkubwa wa umeme kwa jamii na uchumi wa nchi.

Akionekana kukwepa jinamizi la Richmond aliyowahi kuita kuwa ni 'Phantom,' Rais alisema, ilisisitizwa pamoja na udharura uliokuwepo sheria na taratibu za manunuzi ya umma vizingatiwe kwa kuhakikisha mkataba utakaoingiwa uwe ni wenye maslahi kwa taifa na watoa huduma wawe ni makampuni yanayofahamika na yenye sifa stahiki na kuaminika.

Milipuko ya Gongo la Mboto

Kikwete ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu, alitangaza kwamba Serikali itawalipa fidia waathirika wa mambomu yao na kwamba Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA -JKT) limepewa wajibu wa kujenga upya nyumba zilizobomolewa na mabomu hayo.

Rais alifafanua, "Nimeagiza Jeshi la Kujenga Taifa lifanye kazi hiyo kupitia Shirika lake la Uchumi. Nimeamua hivyo ili kuhakikisha kuwa maisha ya ndugu zetu waliokumbwa na maafa haya yanarejea kuwa ya kawaida mapema iwezekanavyo."

Aliongeza kwamba, ameagiza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ishirikiane na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Kitengo cha Taifa cha Maafa kuhakikisha kuwa utekelezaji unaanza mapema iwezekanavyo.

Hali ya chakula
Akizungumzia tatizo hilo Rais alisema, katika baadhi ya maeneo nchini kumeanza kujitokeza matatizo ya upungufu wa chakula kuanzia mwezi Januari 2011 na kuongeza, mengi ya maeneo hayo ni yale yanayopata mvua za vuli ambazo bahati mbaya hazikuwa nzuri.

" Imetambuliwa katika Halmashauri 36 za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, Mwanza, Shinyanga, Mara, Tabora, Singida, Dodoma, Lindi, Mtwara na Iringa ndiko kwenye maeneo mengi yenye upungufu mkubwa, " alisema Rais.

Hata hivyo, alisema tayari serikali imeidhinisha kutolewa kwa jumla ya tani 13,760 za chakula kutoka Akiba ya Taifa ya Chakula (NFRA) kwa ajili ya kuhudumia watu 423,530 walioathiriwa na upungufu wa chakula katika maeneo hayo huku kazi ya usambazaji ikiendelea.

" Hadi sasa jumla ya tani 4,822 za chakula cha msaada kimekwishatolewa katika mikoa ya Arusha, Iringa, Morogoro na Lindi. Napenda kuwathibitishia kuwa tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kuwa hakuna Mtanzania atakayekufa kwa njaa. Tutawahudumia ipasavyo hawa waliokwishatambulika na wengineo watakaojitokeza siku za usoni, " alifafanua.

Mbowe amjibu

MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amesema chama chake hakitaacha maandamano licha ya kushutumiwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa wanachochea vurugu katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi.

Mbowe ambaye alikuwa akihutubia katika Uwanja wa Josho Mjini Shinyanga, alisema kuwa ameamua kuijibu mapema ili kueleza msimamo wa chama chake kuwa hawataacha maandamano hata wakikamatwa na kuwekwa ndani.

"Kikwete leo atahutubia taifa na kusema maandamano yetu yanachochea vurugu, namjibu kuwa tutaandamana na tutaendelea kuandamana. Tunaandamana kwa sababu hatutaki Dowans ailipe kama ambavyo yeye na Kamati Kuu ya chama chake wameamua kuilipa kwa fedha za walipa kodi," alieleza.

Alisema Rais Kikwete anazungumzia bei ya sukari wakati akijua fika kuwa tatizo ambalo limesababisha kupanda kwa bei ya sukari na kuyafanya maisha ya Watanzania kuwa magumu ni sera mbovu za chama chake na kushindwa kwa utawala wake.

"Kikwete anazungumzia mgao wa umeme, taifa gani limekaa na mgao wa umeme kwa miaka saba na halitatuliwi. Halafu anataka tuheshimu Serikali, tusiandamane, tutaendelea kuandamana na tutaandamana," alisema Mbowe.

Alisema katika hotuba yake ya mwezi amezungumzia juu ya Serikali yake kununua mitambo mingine ya kufua umeme kwa kutumia kiasi cha Sh 400 milioni fedha za walipa kodi wakati la Dowans halijaisha.

"Haki ya Mungu tutaendela kuandamana na kama anatuona sisi ni wachochezi basi anikamate Mbowe na wengine anaowaona wachochezi na akatushitaki, leo tunaandamana Shinyanga na kurudi makwetu kwa amani, lakini kuna siku tutaandamana na hatutarudi ila sijui tutakwenda wapi kama hapa Shinyanga tutaenda kwa mkuu wa mkoa sijui…" alieleza Mbowe.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Last Updated on Tuesday, 01 March 2011 08:36 Comments

12345678

#113 Kamanda 2011-03-01 12:20 Quoting Zinklia:
Chadema siyo chama ila kikundi cha wachochezi mtauona mwisho wake!

Kati ya muuaji na muandamanaji yupi mchochezi? CCM ni wauaji uankumbuka walichokifanya Arusha? Hatuta wasamehe kwa lile milele.

Quote

+1 #112 Omar Ali 2011-03-01 12:19 Quoting U all ask from JK...:
Msisahau kuwa mengi katika maoni yenu hapo juu Rais JK aliyarithi na kuyapokea na kuyabeba kutoka kwa utawala wa Awamu iliyopita. Tusiwe wazulumati tumpe haki yake rais JK na tumchaji (acountability) kwa upungufu hapo tuta elewa ukweli. Tufahamu kuwa kila mmoja anahitaji na kuitaka serikali imfikirie Je wewe na yule mume ifikiria nini nchi yenu?

Hilo ndio tatizo la Kikwete (JK feki) na wana-CCM wenzake ka' wewe.Hakuna anayemchukia Kikwete kama individual bali kundi lote la CCM (zamani TANU/ASP) ambao wametawala tangu Uhuru. Yeye ni focal point ya mashambulizi sababu ndio kinara leo. Kesho mkimpa Lowassa tutamshumbulia Lowasa sio Jakaya! Utawala wa nchi hii haujawahi kubalidika...wanapishana magavana tu. Hivi, kwa mfano,Kikwete hahusiki na IPTL tangu akiwa waziri?

Quote

+2 #111 JBP 2011-03-01 12:18 Kama rais ana hofu ya CHADEMA kusababisha machafuko na hivyo kusababisha vifo na uhalibifu wa nyumba na mali nyingine za raia, mbona hakuwa na hofu hiyo mapema kabla mabomu hayajalipuka na kuua watu na mali zao kuharibiwa? Au huo siyo anaoita uhalibifu usio wa lazima?Kwani sheria inasemaje kuhusu mtu anayekiuka katiba? Kama CHADEMA wanachochea chuki, uhasama na uvunjifu wa amani na katiba kwa nini yeye kama mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu asichukue hatua za kisheria dhidi yao? HIZI PROPAGANDA TU ZA KUJARIBU KUWAHADAHA WANANCHI NA WALA HAZINA MSINGI WOWOTE ZAIDI YA KUTAPATAPA TU. HATUDANGANYIKI KIKWETE!!!!!!!! !!!!!!!
Quote

+2 #110 ak 2011-03-01 12:16 Quoting mamatida:
mie sioni watu wanalolishabiki a hapa vita? kugombana ndugu,hivi vikizuka vita ni rais atakaeumia?hapana ni sisi raia tena ndugu hakuna ccm wala chadema amabae ni raia wa kigeni sote ni watanzania na nddugu wa damu kabisa tofauti za kushabikia vyama zisitupeleke kwenye kusahau udugu wetu,panapotoke a vita marais hukimbilia nchi za jirani na wanapewa hifadhi wao na familya yao jee tunaoshabikia hali itakuaje?
mie sasa napata na wasiwasi sisi chadema tumekuchagueni viongozi wetu kwa nia safi kabisa tulitarajia tumeshindwa na huo ndio ukweli haijalishi tumeshindwa kwa faul or penalty bado ukweli unabaki tumeshindwa tuu face ukweli tujiandae vyema kisera,mnatupa mashaka viongozi wetu kuchochea vurugu kwa sababu tumeshindwa kwa wastaarabu wa chadema hiyo sio njia muafaka

we usiwe [NENO BAYA] mashaka ya chadema uanyo wewe, mapinduzi hayaji kwa kuishia kulalamika lazima matenda ya fanyike kama unajiona chadema inakupa machsha kajiunge na mafisadi CCm, tunamaana ya kuikomboa nchi hii maneno yameisha tosha. na kama wakiiba kura tunawachekea eti tumeshindwa tu tutabaki hivyo hivyokama haukotayari kuona mapinduzi ya kweli na wewe anza kukimbilia nchi ya jirani na familia yako, tumia akili usituchefue

Quote

+4 #109 deograsius mrosso 2011-03-01 12:13 HUYU RAIS NI WA KIKE NINI? MBONA KILA KITU ANALALAMIKA TU BADALA YA KUTEKELEZA MAMBO YA MSINGI MFUMKO WA BEI KWENYE MATAIFA YA NJE NA SISI SI TUONGEZE BEI YA MALIGHAFI ZETU USIFANYA WATANZANIA NI [NENO BAYA] ONGEA POINTI
Quote

#108 Kamanda 2011-03-01 12:12 Ulisomea uchumi wapi wewe? Unajua Uchumi? Sasa kama kikwete anakusanya bilion 400 mbona mkapa aliboresha zaidi yake akikusanya biliona 40 kwa mwezi kamaulivyo sema.

wewe hujui uchumi kabisa, maana tokea mkapa aondoke madarakani yaani miaka mi5 iliyopita ni kipindi ambacho kisingekua na mfumuko wa bei kama uliopo

Kiuchumi na kimahesabu ya fedha miaka mitano isingekua na athari hizi.

Naomba nikwambie, hakuna rais ambaye hana makosa yake, lakini mkapa was the one of the best presidents. nataka nikupe sababu.

1.aliimarisha thamani ya fedha ya tanzania. 1 US$ ilikua ni sama na TZS 567 mkapa alipoingia, baada ya miaka 10 1US$ ikawa ni sawa na 875 TZS sawa na anguko la TZS 308, sasa tukimuaangalia kikwete wako Alikuta 1 US$ ni sawa na TZS 875 na sasa baada ya miaka mitano 1 US$ ni sawa na TZS 1510 ambayo ni anguko la TZS 635 (About mara 2) baada ya miaka kumi kiuchumi fedha yetu itakua about mara 4 itakua ni about (1US$=2710 TZS).
is this a best president?
2. mkapa aliukuta uchumi ulikua ukikua chini ya kiwango (yaani ni aibu) lakini baada ya miaka 10 ulikua ukikua 7% kwa mwaka. tokea kikwete alipoingia tumekua tukipewa false fugure( takwimu za uongo) maana mkapa aliukuza uchumi kutoka asilimia 4% - 6% na kwenye kampeni tuliambiwa kikwete aliukuza kutoka 4%-6% (The same) is this possible? ukweli ni kwamba hajaukuza uchumi kabisa ila ameuangusha na watanzania tunadanganywa kwa false fugure.
3.Mkapa aliakuta soda moja Coke sh 200 akaondoka baada ya miaka 10 1Coke 250 (sawa na ongezeko la sh 50), haha sasa kikwete wako ni hatari maana alikuta 1 coke 250 na leo ni 500 baada ya miaka mitano ya uongozi. Cement mkapa alikuta 5000 miaka kumi baadae akaacha 6000 (ongezeko la 1000) lakini kikwete wako amekuta 6000 leo ni 22000 (ongezeko la 16000) Ndugu hujui uchumi. Haiwezekani kabisa.
4.Mkapa alipunguza matumizi ya serikali na kupelekea watu wakatafuta pesa kwa nguvu, Kikwete je? About asilimia 80 ya mapato ya nchi inakwenda JWTZ na about 97% ya 20% iliyobaki unatumiwa na serikali kuu kuiendesha,kikw ete wako anabakia kuomba msaada. what is all 80% of the income to JWTZ for? and what is 97% of the remained 20% goin to central governemt for? je kwa namna hii kutakua na hospitali?shule?vituo vya polis?mishahara bora? Huyu si rais.
5. Unajua nikwanini kikwete ametengeneza pesa mpya wakati 2012 tutakua na fedha moja afrika mashariki? tuulize wanauchumi? kimahesabu miakamitano haiwezi kuwa na tofauti kubwa hivi.Uliza wanauchumi.

Quoting dogo:
Huyu ndugu yangu anachokiongea hakijui, mkapa alikuwa ankusanya Biliono 40 kwa mwezi lakini JK anakusanya bilioni 400 kwa mwezi hivyo muongelee na mazuri yake pia. inaonekana hhujui kama uchumi wa dunia umeanguka kiasi kikubwa na hujui shilingi 350 ya 1998 ni sawa na shilingi ngapi ya leo. msifuate mkumbo na U. hapa kinachoonekana ni U. tu na si kingine. mkapa ameuza migodi yote tena kwa bei poa, na mingine kajiuzia mwenyewe leo mkapa kawa mzuri, haibu gani? kijana usiwalenganishe hao wawili.kosa la kikwete ni moja tu alitaka kila kitu kiwe bayana wananchi wawajue wahalifu wao alitegemea kuwa angepewa ushirikiano kumbe wapinzani walichukulia kuwa ndio sehemu ya kupata umaharufu. kipindi cha mkapa migodi imebinafsishwa kwa miaka 100 ndugu yangu wewe unapata asilimia 3 na mzungu anapata asilimia 97. JK ipo siku wataelewa hao kama wewe upo upande gani?Quoting mtimbwafs:
Binafsi namuheshimu saaana muheshimiwa aliyehutubia jana lakini naomba japo nitoe ushauri kwake na kwa Watanzania wapenda maendeleo;
1. Kikwete kwa hotuba ya jana anaonekana hana tena jipya la kutufanyia Watanzania ndio maana amebaki kulalama tu pasipo kupima mambo yalivyo. Namshauri atafute timu ya washauri ambao wanauelewa mkubwa wa mambo watete nae juu ya hali halisi ya nchi yetu ilivyo sasa na wapi tunataka kuelekea.
2. Kitendo cha kumkashifu mwalimu Nyerere hadharani wakati sisi Watanzania wazalendo tunamuona kama dira yetu na mzalendo aliyejenga misingi ya kweli ya kizalendo katika taifa letu ni kutukosea adabu watanzania. Nashauri atafute kitu kingine cha kuongea na kama hana neno atulie tu sisi tutaendelea kumvumilia na kumuelewa tu, mbona hata alipotuita Mbayuwayu, Kong'ona na kashifa kibao tulimvumilia?.
3. Mh. Mkapa alipokuwa anaondoka madarakani alituacha hapa; Kilo ya sukari tshs. 650 kwa vijijini, Mkate tshs. 350, Sembe 150 kwa kilo, mafuta ya taa 400 kwa lita, chumvi ya mawe 70 kwa kilo nauli ndani ya Dar tshs. 100/150 na HAZINA kulikuwa na akiba kibao ambazo ulisema mambo ni shwari ili kutupeleka katika nchi ya maziwa na asali. Tafadhali mheshimiwa sana Tafakari hali ile na ya sasa halafu CHUKUA HATUA.
3. Kuilaumu CHADEMA kama ndio mchawi wa Watanzania kwa sasa ni kuinyima haki ya msingi na kutokuitendea haki Demokrasia kwa kuwa WATANZANIA ni waelewa na hali yetu ya maisha tunaijua wenyewe ilivyo hatuhitaji mzungu kutoka ulaya atuambie kwa kuwa CDM wanajua nini wanafanya na ni kwa faida ya nani, hivyo achana nao jipange vizuri ili kutuletea tija WATANZANIA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA!.
Quote

-2 #107 U all ask from JK... 2011-03-01 12:10 Msisahau kuwa mengi katika maoni yenu hapo juu Rais JK aliyarithi na kuyapokea na kuyabeba kutoka kwa utawala wa Awamu iliyopita. Tusiwe wazulumati tumpe haki yake rais JK na tumchaji (acountability) kwa upungufu hapo tuta elewa ukweli. Tufahamu kuwa kila mmoja anahitaji na kuitaka serikali imfikirie Je wewe na yule mume ifikiria nini nchi yenu?
Quote

-1 #106 Kezilahabi 2011-03-01 12:09 Quoting Zinklia:
Chadema siyo chama ila kikundi cha wachochezi mtauona mwisho wake!

Bora ya wachochezi kuliko Chama Cha Majambazi

Quote

+2 #105 mekaki 2011-03-01 12:09 ujue mtoto akililia wemmbe mpe...kama mtu hakushinda kihalalai na akaang'ang'ania madaraka (kwa ajaili ya kutimiza maslahi ya wachache bila kusahau dowans) acha yamkute,,,,haya sasa nchi ndio hii hawezi kuiongoza,hawez i hata kuzungumza ,anajichanganya ,anaonyesha udhaifu.

watanzania wa leo si kama wale wa miaka aya sitini au sabini...sasa lazima kieleweke badala ya kutumia mwavuli wa kusema tanzania nai annchi ya amanai,demokras ia wakati si kweli....nanai anaweza kuwa naa amanai wakati watoto wanalala njaa,wanasomea chini,umeme hakuna ukija hela inalipwa kubwa,uzembe na maafda ya makusudi,,,,,ba do neno amanai hapao lipo? kama n=kiongozi anapita anadhulumiwa bado hiyo demokrasia ipo...kama vyama vya siasa vilivyosajiliwa vinanyimwa haki za mmsingi je? bado demokrasia ipo?

Quote

+2 #104 Ali Akida 2011-03-01 12:09 wapo akina makamba humu ndani, wanajibu kwa nguvu, ukiwambia twende tuongee kwenye open space hawataki. jamani kudanganyana kumeisha. nafrahi anaposema rais wetu ni mpole na anachekacheka, basi kuchekacheka huko ndiko kunako tufikisha pabaya, hajui wapi pakucheka na wapi pakung'ata. namkumbusha bwana Mbade a k a Makamba kuwa Nyerere angekuwepo uchafu uliopo kwenye serikali hii usingekuwepo hata huyo makamba wenu asingekuwepo kwenye system. responce ya wananchi kwenye maandamano ni dalili za kuchoshwa na maisha ya matumaini. siku hizi kama hufahamiki au kuwa mtoto wa kiongozi hupati nafasi babu, angalia watoto wa viongozi ndio wanaoshika nafasi za juu ndio maana tuna kata tamaa, juzi nilikuwa naangalia bunge kuna Vita kawawa Mbunge wa kuchaguliwa, dada yake ni mbunge wa viti maalamu, wewe mwenzangu na mimi unambiwa hubiri amani!!! kama sijashiba nitahubiri vipi amani!!!
Quote

+1 #103 anna 2011-03-01 12:08 mimi kwa upeo wangi nadhani imefika wakati sasa wa kiongozi kuu wa nchi/seriali kuschukua hatua madhubuti kwa watendaji wake wasio wakweli/wasiowaaminifu/wenye kutuhumuiwa na kashfa mbali mbali zinazogusa maslahi ya umma ili kubaki na viongoz waadilifu na wenye kujali maslahi ya wananchi wote hasa walala hoi.wakati hilo likiendelea kiongozi mkuu/serikali ni lazima iseme sasa ni hatua gani wanachukua ili matatizo yanayoikabili nchi kama kupanda kwa bei ya vyakula,mgao wa umeme,ukosekana nji wa maji,elimu duni,kupanda kwa nauli za daladala na mabasi ya mikoani yaweze kutatuliwa kwa haraka kwa sababu kipato cha mtanzania wa sasa hasa wa hali ya chini ni majonzi jamani pia wale waliopo kazini mshahara kupanda ni siasa tupu.sasa kama mtanzania Mungu amemjalia pumzi ya leo kinachofuata anawaza hii leo itapiota vipi kuanzia asubuhi mpaka anapolala yaani utakuta hata mlo mmoja kwa siku ni shida!!!!na hapo hapo ndani ya nchi hiyo hiyo wapo wengine ambao kazi yao ni kuchota au kutumia vibaya pesa za walipa kodi kama wanavyoripo[NEN O BAYA] mara kwa mara lakini hakuna kinachofanyika zaidi ya kulindana.Kiukweli hata kama mtu unawaheshimu sana wazazi wako lakini kama wanafanya ndivyo sivyo na hawasikilizi la mtu huwa inafika hatua waweza kuwachoka!!!ndi po tulipofika sasa yaani ndani ya nchi yetu wenyewe lakini kiukweli TUMECHOKA na siasa za ulaghai za kila siku kwamba Maisha yataboreshwa kivipi????au ndo kupanda gharama za maisha ndo uboreshaji mpya mliokuja nao????jamani jamani cheo ni dhamna ipo siku Mungu atawauliza mlitufanyia nini watanzania.Maana ugumu wa maisha unapelekea hata watanzania kukata tamaa ingwa viongozi wa dini wanajitahidi kutufariji ila kiukweli viongozi wetu acheni maneno ya majibishano kama kweny taarabu/mipasho bali fanyeni mambo ya msingi kutukomboa watanzania na janga hili la ugumu wa maisha.
Mwisho nawasihi watanzania wenzangu pamoja ugumu wa maisha tulionao naomba kwa imani zetu pia tuzidi kumuomba Mungu abadilishe mioyo ya hawa viongozi wetu iwe na hofu ya Mungu ndani yake ili wabadilike na kutenda yale yanayostahili kwa maslahi ya taifa.Kweli tuzidi kuomba Mungu.asanteni sana.

Quote

+2 #102 Mwanaharakati 2011-03-01 12:07 saa ya ukombozi inakaribia, chadema tusongembele. Tumechoka kufanywa [NENO BAYA] na utawala wa kifisadi wa ccm.
Quote

-1 #101 Kezilahabi 2011-03-01 12:06 Namuunga mkono Rahisi Kiwete...CHADEMA wabaya sana. Wameleta DOWANS/Richmond,wanawa linda mafisadi wamependisha ovyo bei ya mafuta na vyakula,walilip ua mabomu G'mboto, hawawalipi wafanyakazi mishahara vizuri, wamefungua sekondari za kufelisha maskini (za kata) na wameunda serikali kuubwa wasiyoweza kuiendesha! CHADEMA hawafai...tuwatoe madarakani. THAT'S WHAT UR FAKE PRESIDENT IS IMPLYING, LOL.
Quote

-4 #100 Zinklia 2011-03-01 12:05 Chadema siyo chama ila kikundi cha wachochezi mtauona mwisho wake!
Quote

+6 #99 Omar Ali 2011-03-01 11:53 Rais gani analalamika kila siku...raia tufanyeje?
Quote

12345678
Refresh comments list
 
Chadema wanavuruga nchi- JK Send to a friend Monday, 28 February 2011 21:30
akihutubukikwete.jpg
Rais Jakaya KIkwete

Ramadhan Semtawa
RAIS Jakaya Kikwete jana alilihutubia taifa, huku akitumia muda mwingi kujibu mapigo ya kauli za Chadema dhidi yake na kutahadharisha kuwa chama hicho, kina lengo la kuleta machafuko nchini."Kauli na vitendo vya wenzetu hao vyenye dhamira ya kutaka kuleta machafuko makubwa na uvunjifu wa amani nchini." alisema Rais Kikwete ambaye amekuwa kimya bila kulihutubia taifa kwa muda wa miezi miwili.

Onyo la Rais Kikwete limekuja siku chache baada ya Chadema kumpa siku tisa ikitaka mkuu huyo wa nchi atekeleze baadhi ya mambo ikiwamo kutoilipa fidia ya Sh94 bilioni kampuni ya Dowans.

Lakini, jana katika hotuba yake, Rais Kikwete pamoja na kufafanua hoja kadhaa, alisisitiza "Hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa."

Rais Kikwete alifafanua kwamba, hivi karibuni wananchi wengi wameingiwa na hofu kubwa kuhusu usalama wa nchi yao hali ambayo ni ngeni kwa Watanzania.

"Hofu hiyo inatokana na kauli na vitendo vya wenzetu wa Chadema vyenye dhamira ya kutaka kuleta machafuko makubwa na uvunjifu wa amani nchini," alieleza Rais Kikwete.

Mkuu huyo wa nchi ambaye tayari amemaliza siku 100 za ngwe yake ya pili akiwa Ikulu, aliweka bayana kuwa kufanya maandamano na mikutano ni haki ya msingi ya vyama vya siasa na raia, lakini, akaonya kuigeuza fursa hiyo kuwa jukwaa la kuchochea ghasia kwa nia ya kuindoa Serikali iliyoko madarakani kwa mabavu.

Kikwete alisisitiza kuwa hatua hiyo ni matumizi mabaya ya fursa ya kufanya maandamano na isiyostahili kuungwa mkono na Watanzania wazalendo, wapenda amani na nchi yao.

Rais alisema Tanzani ni nchi ya kidemokrasia na kila miaka mitano hufanyika uchaguzi wa kuchagua viongozi na kuweka bayana.

"Uchaguzi wa mwisho tumefanya tarehe 31 Oktoba, 2010. Kabla ya hapo tulikuwa na kampeni zilizochukua karibu miezi mwili na nusu. "

Kwa mujibu wa Rais Kikwete, katika kampeni hizo, kila chama kilielezea jinsi kitakavyokabiliana na matatizo yanayowakabili wananchi ikiwa ni pamoja na hayo yanayoyazungumzwa sasa na Chadema.

"Hatimaye siku ya uchaguzi wananchi walifanya uamuzi wa kuchagua chama walichokiamini, nacho ni Chama cha Mapinduzi.,"alieleza

"Iweje leo, miezi mitatu baadaye kwa mtu au chama cha siasa kufanya maandamano kwa masuala yale yale waliyoyasema kwenye kampeni. Siyo sawa hata kidogo," alisema Rais Kikwete.

"Kuchochea ghasia ati kwa nia ya kuiondoa Serikali madarakani ni kinyume cha Katiba na ni kuiingiza nchi katika mgogoro usiokuwa wa lazima. Tutasababisha umwagaji wa damu, watu kupoteza maisha na mali zao kuharibiwa bila sababu yoyote ya msingi,"alionya Rais Kikwete.

Kikwete alisema katika nchi ya kidemokrasia na kwa wanademokrasia wa kweli, wanapomaliza uchaguzi mmoja, hujiandaa kwa uchaguzi mwingine kwa kujenga upya chama , kuongeza wanachama, kuboresha sera na hoja pamoja na namna ya kuziwasilisha ili watu wawakubali na kuwachagua.

Rais Kikwete aliitaka Chadema kutumia Bunge kuwasilisha hoja zao badala ya mikutano ya hadhara inayotoa kauli za chuki kwa Serikali.

"Na, uwanja muhimu wa kufanya sehemu kubwa ya hayo ni katika Bunge na Halmashauri za Wilaya kupitia wabunge na madiwani wenu,"alieleza Rais Kikwete

Kikwete ambaye mara ya mwisho alitoa hotuba ya mwezi wakati wa mwaka mpya wa 2011, alisema kuacha kufanya hivyo na badala yake kuamua kuzunguka nchi nzima na kuchochea ghasia kwa lengo la kuwaondoa walioshinda ni kinyume na misingi ya demokrasia na kusisitiza

Alisisitiza "Tutajenga misingi ya hovyo na nchi yetu itakosa amani na utulivu daima."

Aliwataka Chadema kukaa chini na kujiuliza wanachokifanya na athari zake kwa wananchi akisema, "kama kila atakayeshindwa uchaguzi anafanya hivyo tutakuwa nchi ya namna gani?"

"Tanzania yetu hii yenye sifa na heshima ya kuwa nchi ya amani na utulivu itapoteza kabisa sifa hiyo na badala yake umwagaji wa damu na mateso kwa watu wasiokuwa na hatia vitageuka kuwa maisha ya kawaida." alisema.

Rais alisema kitendo hicho haikiitendei haki nchi na hata wananchi ambao viongozi wa siasa wamekuwa wakidai kuwapenda na kuwatetea.

"Ndugu Zangu, Watanzania Wenzangu; ndugu zetu wa Chadema wanayajua yote haya, lakini wanalo lao jambo. Wanataka kuipeleka nchi yetu pabaya kwa kukidhi uchu wao wa madaraka. Kwao sasa demokrasia haina maana, inaweza kusubiri," alifafanua Rais.

Aliwataka Watanzania kuwa makini na Chadema akisema "naomba tuyakatae mambo yao. Tusiwafuate. Waambieni mchezo wao ni hatari na ni mauti yetu. Sisi katika Serikali tutajitahidi kutimiza wajibu wetu wa kulinda usalama wa nchi yetu, watu wake na mali zao."

Hali ngumu ya maisha
Rais alikiri, "Ni kweli kuna hali ngumu ya maisha, na kukabiliana nayo ndiyo kazi tunayoendelea nayo kufanya kila siku."

"Tumeelekeza nguvu zetu na rasilimali zetu huko na mafanikio yanaonekana katika nyanja mbalimbali na maeneo mbalimbali, lakini akisisitiza, "hayo si matatizo ya kumalizika ndani ya siku tisa."

Alifafanua kwamba, kikwazo siyo upungufu wa sera wala dhamira, bali ni kiwango cha maendeleo madogo ya uchumi wa nchi na hivyo uwezo siyo mkubwa wa kuyakabili na kuyamaliza matatizo yote haraka kama ambavyo ingepaswa iwe.

Kikwete akirejea zama mbali za viongozi mbalimbali tangu uhuru, alisema hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliongoza kwa miaka 23 na hakuyamaliza matatizo ya maendeleo ya nchi hii.

"Na wale wa umri wangu au kunizidi wanakumbuka hali ilivyokuwa wakati anang’atuka. Hakuacha nchi ikiwa tajiri. Mzee Mwinyi kakaa miaka 10 hakuyamaliza, Mzee Mkapa nae kakaa miaka 10 hakuyamaliza. Mie nimekaa miaka mitano hayakwisha na nitamaliza mitano hayataisha yote." alisema

Alisema jambo la muhimu ni kuwa katika kila awamu nchi iweke malengo ya kupiga hatua ya kusonga mbele katika kujiletea maendeleo na kuongeza, hali iliyokuwa wakati ule sivyo ilivyokuwa mwaka 1985, wala 1995 au 2005 na ilivyo sasa.

Kuhusu mafanikio yake alisema, "Katika miaka mitano hii kuna maendeleo yanayoonekana wazi, pamoja na changamoto nyingi tumefanya juhudi kubwa na mafanikio yanaonekana katika nyanja zote za maisha ya Watanzania. Mwenye macho haambiwi tazama.''

Rais alirejea matukio mbalimbali yanayoitikisa dunia, akisema ni muhimu watu kutambua ukweli kwamba uchumi kama wetu ambao haujajenga uwezo wake wa ndani wa kujitosheleza kwa mahitaji yake, huathirika sana na yanayotokea katika uchumi wa dunia.

"Unapoyumba na sisi tunayumba. Bei za mafuta katika soko la dunia zikipanda na kwetu kupitia gharama za uchukuzi na uzalishaji huongezeka na kusababisha bei za bidhaa kupanda," alifafanua Rais akitaka wananchi wafahamu jinsi athari za dunia zinavyoweza kugusa uchumi wa nchi.

Mfumuko wa bei ukipanda China, nguo na bidhaa tunazonunua kutoka China hupanda bei. Hivi sasa mataifa yote makubwa tunakonunua bidhaa mfumuko wa bei umepanda na sisi tunaathirika.

Alihoji, "mvua ikikosekana kunakuwa na uhaba wa chakula, bei za vyakula hupanda na watu wengine hukosa chakula. Lawama kwa Serikali au Rais Kikwete inaanzia wapi?

Hali ya Umeme
Rais alikiri pia hali ya upatikanaji wa umeme nchini kwamba ni mbaya na kuweka bayana, "chanzo cha matatizo ni kupungua sana kwa maji katika bwawa kubwa la Mtera.

"Hadi jana kina cha bwawa hilo kimeshuka hadi kufikia mita 691.25 ambacho ni pungufu kwa mita 7. Kwa sasa zimebaki mita 1.25 tu juu ya kiwango cha chini kinachoruhusiwa kuendesha mitambo ya kuzalisha umeme,"alisema.

Hata hivyo, alisema 15 Februari, 2011, Baraza la Mawaziri lilijadili na kuidhinisha mpango wa dharura wa Tanesco wa kukodi mitambo ya kuzalisha MW 260 za umeme na kuongeza, baraza limeitaka bodi na menejimenti ya shirika hilo kuhakikisha mchakato huo unakamilika mapema iwezekanavyo ili kupunguza makali na athari za ukosefu mkubwa wa umeme kwa jamii na uchumi wa nchi.

Akionekana kukwepa jinamizi la Richmond aliyowahi kuita kuwa ni 'Phantom,' Rais alisema, ilisisitizwa pamoja na udharura uliokuwepo sheria na taratibu za manunuzi ya umma vizingatiwe kwa kuhakikisha mkataba utakaoingiwa uwe ni wenye maslahi kwa taifa na watoa huduma wawe ni makampuni yanayofahamika na yenye sifa stahiki na kuaminika.

Milipuko ya Gongo la Mboto

Kikwete ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu, alitangaza kwamba Serikali itawalipa fidia waathirika wa mambomu yao na kwamba Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA -JKT) limepewa wajibu wa kujenga upya nyumba zilizobomolewa na mabomu hayo.

Rais alifafanua, "Nimeagiza Jeshi la Kujenga Taifa lifanye kazi hiyo kupitia Shirika lake la Uchumi. Nimeamua hivyo ili kuhakikisha kuwa maisha ya ndugu zetu waliokumbwa na maafa haya yanarejea kuwa ya kawaida mapema iwezekanavyo."

Aliongeza kwamba, ameagiza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ishirikiane na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na Kitengo cha Taifa cha Maafa kuhakikisha kuwa utekelezaji unaanza mapema iwezekanavyo.

Hali ya chakula
Akizungumzia tatizo hilo Rais alisema, katika baadhi ya maeneo nchini kumeanza kujitokeza matatizo ya upungufu wa chakula kuanzia mwezi Januari 2011 na kuongeza, mengi ya maeneo hayo ni yale yanayopata mvua za vuli ambazo bahati mbaya hazikuwa nzuri.

" Imetambuliwa katika Halmashauri 36 za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Morogoro, Mwanza, Shinyanga, Mara, Tabora, Singida, Dodoma, Lindi, Mtwara na Iringa ndiko kwenye maeneo mengi yenye upungufu mkubwa, " alisema Rais.

Hata hivyo, alisema tayari serikali imeidhinisha kutolewa kwa jumla ya tani 13,760 za chakula kutoka Akiba ya Taifa ya Chakula (NFRA) kwa ajili ya kuhudumia watu 423,530 walioathiriwa na upungufu wa chakula katika maeneo hayo huku kazi ya usambazaji ikiendelea.

" Hadi sasa jumla ya tani 4,822 za chakula cha msaada kimekwishatolewa katika mikoa ya Arusha, Iringa, Morogoro na Lindi. Napenda kuwathibitishia kuwa tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kuwa hakuna Mtanzania atakayekufa kwa njaa. Tutawahudumia ipasavyo hawa waliokwishatambulika na wengineo watakaojitokeza siku za usoni, " alifafanua.

Mbowe amjibu

MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe amesema chama chake hakitaacha maandamano licha ya kushutumiwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa wanachochea vurugu katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi.

Mbowe ambaye alikuwa akihutubia katika Uwanja wa Josho Mjini Shinyanga, alisema kuwa ameamua kuijibu mapema ili kueleza msimamo wa chama chake kuwa hawataacha maandamano hata wakikamatwa na kuwekwa ndani.

“Kikwete leo atahutubia taifa na kusema maandamano yetu yanachochea vurugu, namjibu kuwa tutaandamana na tutaendelea kuandamana. Tunaandamana kwa sababu hatutaki Dowans ailipe kama ambavyo yeye na Kamati Kuu ya chama chake wameamua kuilipa kwa fedha za walipa kodi,” alieleza.

Alisema Rais Kikwete anazungumzia bei ya sukari wakati akijua fika kuwa tatizo ambalo limesababisha kupanda kwa bei ya sukari na kuyafanya maisha ya Watanzania kuwa magumu ni sera mbovu za chama chake na kushindwa kwa utawala wake.

“Kikwete anazungumzia mgao wa umeme, taifa gani limekaa na mgao wa umeme kwa miaka saba na halitatuliwi. Halafu anataka tuheshimu Serikali, tusiandamane, tutaendelea kuandamana na tutaandamana,” alisema Mbowe.

Alisema katika hotuba yake ya mwezi amezungumzia juu ya Serikali yake kununua mitambo mingine ya kufua umeme kwa kutumia kiasi cha Sh 400 milioni fedha za walipa kodi wakati la Dowans halijaisha.

“Haki ya Mungu tutaendela kuandamana na kama anatuona sisi ni wachochezi basi anikamate Mbowe na wengine anaowaona wachochezi na akatushitaki, leo tunaandamana Shinyanga na kurudi makwetu kwa amani, lakini kuna siku tutaandamana na hatutarudi ila sijui tutakwenda wapi kama hapa Shinyanga tutaenda kwa mkuu wa mkoa sijui…” alieleza Mbowe.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Last Updated on Tuesday, 01 March 2011 08:36 Comments

12345678

#113 Kamanda 2011-03-01 12:20 Quoting Zinklia:
Chadema siyo chama ila kikundi cha wachochezi mtauona mwisho wake!

Kati ya muuaji na muandamanaji yupi mchochezi? CCM ni wauaji uankumbuka walichokifanya Arusha? Hatuta wasamehe kwa lile milele.

Quote

+1 #112 Omar Ali 2011-03-01 12:19 Quoting U all ask from JK...:
Msisahau kuwa mengi katika maoni yenu hapo juu Rais JK aliyarithi na kuyapokea na kuyabeba kutoka kwa utawala wa Awamu iliyopita. Tusiwe wazulumati tumpe haki yake rais JK na tumchaji (acountability) kwa upungufu hapo tuta elewa ukweli. Tufahamu kuwa kila mmoja anahitaji na kuitaka serikali imfikirie Je wewe na yule mume ifikiria nini nchi yenu?

Hilo ndio tatizo la Kikwete (JK feki) na wana-CCM wenzake ka' wewe.Hakuna anayemchukia Kikwete kama individual bali kundi lote la CCM (zamani TANU/ASP) ambao wametawala tangu Uhuru. Yeye ni focal point ya mashambulizi sababu ndio kinara leo. Kesho mkimpa Lowassa tutamshumbulia Lowasa sio Jakaya! Utawala wa nchi hii haujawahi kubalidika...wanapishana magavana tu. Hivi, kwa mfano,Kikwete hahusiki na IPTL tangu akiwa waziri?

Quote

+2 #111 JBP 2011-03-01 12:18 Kama rais ana hofu ya CHADEMA kusababisha machafuko na hivyo kusababisha vifo na uhalibifu wa nyumba na mali nyingine za raia, mbona hakuwa na hofu hiyo mapema kabla mabomu hayajalipuka na kuua watu na mali zao kuharibiwa? Au huo siyo anaoita uhalibifu usio wa lazima?Kwani sheria inasemaje kuhusu mtu anayekiuka katiba? Kama CHADEMA wanachochea chuki, uhasama na uvunjifu wa amani na katiba kwa nini yeye kama mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu asichukue hatua za kisheria dhidi yao? HIZI PROPAGANDA TU ZA KUJARIBU KUWAHADAHA WANANCHI NA WALA HAZINA MSINGI WOWOTE ZAIDI YA KUTAPATAPA TU. HATUDANGANYIKI KIKWETE!!!!!!!! !!!!!!!
Quote

+2 #110 ak 2011-03-01 12:16 Quoting mamatida:
mie sioni watu wanalolishabiki a hapa vita? kugombana ndugu,hivi vikizuka vita ni rais atakaeumia?hapana ni sisi raia tena ndugu hakuna ccm wala chadema amabae ni raia wa kigeni sote ni watanzania na nddugu wa damu kabisa tofauti za kushabikia vyama zisitupeleke kwenye kusahau udugu wetu,panapotoke a vita marais hukimbilia nchi za jirani na wanapewa hifadhi wao na familya yao jee tunaoshabikia hali itakuaje?
mie sasa napata na wasiwasi sisi chadema tumekuchagueni viongozi wetu kwa nia safi kabisa tulitarajia tumeshindwa na huo ndio ukweli haijalishi tumeshindwa kwa faul or penalty bado ukweli unabaki tumeshindwa tuu face ukweli tujiandae vyema kisera,mnatupa mashaka viongozi wetu kuchochea vurugu kwa sababu tumeshindwa kwa wastaarabu wa chadema hiyo sio njia muafaka

we usiwe [NENO BAYA] mashaka ya chadema uanyo wewe, mapinduzi hayaji kwa kuishia kulalamika lazima matenda ya fanyike kama unajiona chadema inakupa machsha kajiunge na mafisadi CCm, tunamaana ya kuikomboa nchi hii maneno yameisha tosha. na kama wakiiba kura tunawachekea eti tumeshindwa tu tutabaki hivyo hivyokama haukotayari kuona mapinduzi ya kweli na wewe anza kukimbilia nchi ya jirani na familia yako, tumia akili usituchefue

Quote

+4 #109 deograsius mrosso 2011-03-01 12:13 HUYU RAIS NI WA KIKE NINI? MBONA KILA KITU ANALALAMIKA TU BADALA YA KUTEKELEZA MAMBO YA MSINGI MFUMKO WA BEI KWENYE MATAIFA YA NJE NA SISI SI TUONGEZE BEI YA MALIGHAFI ZETU USIFANYA WATANZANIA NI [NENO BAYA] ONGEA POINTI
Quote

#108 Kamanda 2011-03-01 12:12 Ulisomea uchumi wapi wewe? Unajua Uchumi? Sasa kama kikwete anakusanya bilion 400 mbona mkapa aliboresha zaidi yake akikusanya biliona 40 kwa mwezi kamaulivyo sema.

wewe hujui uchumi kabisa, maana tokea mkapa aondoke madarakani yaani miaka mi5 iliyopita ni kipindi ambacho kisingekua na mfumuko wa bei kama uliopo

Kiuchumi na kimahesabu ya fedha miaka mitano isingekua na athari hizi.

Naomba nikwambie, hakuna rais ambaye hana makosa yake, lakini mkapa was the one of the best presidents. nataka nikupe sababu.

1.aliimarisha thamani ya fedha ya tanzania. 1 US$ ilikua ni sama na TZS 567 mkapa alipoingia, baada ya miaka 10 1US$ ikawa ni sawa na 875 TZS sawa na anguko la TZS 308, sasa tukimuaangalia kikwete wako Alikuta 1 US$ ni sawa na TZS 875 na sasa baada ya miaka mitano 1 US$ ni sawa na TZS 1510 ambayo ni anguko la TZS 635 (About mara 2) baada ya miaka kumi kiuchumi fedha yetu itakua about mara 4 itakua ni about (1US$=2710 TZS).
is this a best president?
2. mkapa aliukuta uchumi ulikua ukikua chini ya kiwango (yaani ni aibu) lakini baada ya miaka 10 ulikua ukikua 7% kwa mwaka. tokea kikwete alipoingia tumekua tukipewa false fugure( takwimu za uongo) maana mkapa aliukuza uchumi kutoka asilimia 4% - 6% na kwenye kampeni tuliambiwa kikwete aliukuza kutoka 4%-6% (The same) is this possible? ukweli ni kwamba hajaukuza uchumi kabisa ila ameuangusha na watanzania tunadanganywa kwa false fugure.
3.Mkapa aliakuta soda moja Coke sh 200 akaondoka baada ya miaka 10 1Coke 250 (sawa na ongezeko la sh 50), haha sasa kikwete wako ni hatari maana alikuta 1 coke 250 na leo ni 500 baada ya miaka mitano ya uongozi. Cement mkapa alikuta 5000 miaka kumi baadae akaacha 6000 (ongezeko la 1000) lakini kikwete wako amekuta 6000 leo ni 22000 (ongezeko la 16000) Ndugu hujui uchumi. Haiwezekani kabisa.
4.Mkapa alipunguza matumizi ya serikali na kupelekea watu wakatafuta pesa kwa nguvu, Kikwete je? About asilimia 80 ya mapato ya nchi inakwenda JWTZ na about 97% ya 20% iliyobaki unatumiwa na serikali kuu kuiendesha,kikw ete wako anabakia kuomba msaada. what is all 80% of the income to JWTZ for? and what is 97% of the remained 20% goin to central governemt for? je kwa namna hii kutakua na hospitali?shule?vituo vya polis?mishahara bora? Huyu si rais.
5. Unajua nikwanini kikwete ametengeneza pesa mpya wakati 2012 tutakua na fedha moja afrika mashariki? tuulize wanauchumi? kimahesabu miakamitano haiwezi kuwa na tofauti kubwa hivi.Uliza wanauchumi.

Quoting dogo:
Huyu ndugu yangu anachokiongea hakijui, mkapa alikuwa ankusanya Biliono 40 kwa mwezi lakini JK anakusanya bilioni 400 kwa mwezi hivyo muongelee na mazuri yake pia. inaonekana hhujui kama uchumi wa dunia umeanguka kiasi kikubwa na hujui shilingi 350 ya 1998 ni sawa na shilingi ngapi ya leo. msifuate mkumbo na U. hapa kinachoonekana ni U. tu na si kingine. mkapa ameuza migodi yote tena kwa bei poa, na mingine kajiuzia mwenyewe leo mkapa kawa mzuri, haibu gani? kijana usiwalenganishe hao wawili.kosa la kikwete ni moja tu alitaka kila kitu kiwe bayana wananchi wawajue wahalifu wao alitegemea kuwa angepewa ushirikiano kumbe wapinzani walichukulia kuwa ndio sehemu ya kupata umaharufu. kipindi cha mkapa migodi imebinafsishwa kwa miaka 100 ndugu yangu wewe unapata asilimia 3 na mzungu anapata asilimia 97. JK ipo siku wataelewa hao kama wewe upo upande gani?Quoting mtimbwafs:
Binafsi namuheshimu saaana muheshimiwa aliyehutubia jana lakini naomba japo nitoe ushauri kwake na kwa Watanzania wapenda maendeleo;
1. Kikwete kwa hotuba ya jana anaonekana hana tena jipya la kutufanyia Watanzania ndio maana amebaki kulalama tu pasipo kupima mambo yalivyo. Namshauri atafute timu ya washauri ambao wanauelewa mkubwa wa mambo watete nae juu ya hali halisi ya nchi yetu ilivyo sasa na wapi tunataka kuelekea.
2. Kitendo cha kumkashifu mwalimu Nyerere hadharani wakati sisi Watanzania wazalendo tunamuona kama dira yetu na mzalendo aliyejenga misingi ya kweli ya kizalendo katika taifa letu ni kutukosea adabu watanzania. Nashauri atafute kitu kingine cha kuongea na kama hana neno atulie tu sisi tutaendelea kumvumilia na kumuelewa tu, mbona hata alipotuita Mbayuwayu, Kong'ona na kashifa kibao tulimvumilia?.
3. Mh. Mkapa alipokuwa anaondoka madarakani alituacha hapa; Kilo ya sukari tshs. 650 kwa vijijini, Mkate tshs. 350, Sembe 150 kwa kilo, mafuta ya taa 400 kwa lita, chumvi ya mawe 70 kwa kilo nauli ndani ya Dar tshs. 100/150 na HAZINA kulikuwa na akiba kibao ambazo ulisema mambo ni shwari ili kutupeleka katika nchi ya maziwa na asali. Tafadhali mheshimiwa sana Tafakari hali ile na ya sasa halafu CHUKUA HATUA.
3. Kuilaumu CHADEMA kama ndio mchawi wa Watanzania kwa sasa ni kuinyima haki ya msingi na kutokuitendea haki Demokrasia kwa kuwa WATANZANIA ni waelewa na hali yetu ya maisha tunaijua wenyewe ilivyo hatuhitaji mzungu kutoka ulaya atuambie kwa kuwa CDM wanajua nini wanafanya na ni kwa faida ya nani, hivyo achana nao jipange vizuri ili kutuletea tija WATANZANIA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA!.
Quote

-2 #107 U all ask from JK... 2011-03-01 12:10 Msisahau kuwa mengi katika maoni yenu hapo juu Rais JK aliyarithi na kuyapokea na kuyabeba kutoka kwa utawala wa Awamu iliyopita. Tusiwe wazulumati tumpe haki yake rais JK na tumchaji (acountability) kwa upungufu hapo tuta elewa ukweli. Tufahamu kuwa kila mmoja anahitaji na kuitaka serikali imfikirie Je wewe na yule mume ifikiria nini nchi yenu?
Quote

-1 #106 Kezilahabi 2011-03-01 12:09 Quoting Zinklia:
Chadema siyo chama ila kikundi cha wachochezi mtauona mwisho wake!

Bora ya wachochezi kuliko Chama Cha Majambazi

Quote

+2 #105 mekaki 2011-03-01 12:09 ujue mtoto akililia wemmbe mpe...kama mtu hakushinda kihalalai na akaang'ang'ania madaraka (kwa ajaili ya kutimiza maslahi ya wachache bila kusahau dowans) acha yamkute,,,,haya sasa nchi ndio hii hawezi kuiongoza,hawez i hata kuzungumza ,anajichanganya ,anaonyesha udhaifu.

watanzania wa leo si kama wale wa miaka aya sitini au sabini...sasa lazima kieleweke badala ya kutumia mwavuli wa kusema tanzania nai annchi ya amanai,demokras ia wakati si kweli....nanai anaweza kuwa naa amanai wakati watoto wanalala njaa,wanasomea chini,umeme hakuna ukija hela inalipwa kubwa,uzembe na maafda ya makusudi,,,,,ba do neno amanai hapao lipo? kama n=kiongozi anapita anadhulumiwa bado hiyo demokrasia ipo...kama vyama vya siasa vilivyosajiliwa vinanyimwa haki za mmsingi je? bado demokrasia ipo?

Quote

+2 #104 Ali Akida 2011-03-01 12:09 wapo akina makamba humu ndani, wanajibu kwa nguvu, ukiwambia twende tuongee kwenye open space hawataki. jamani kudanganyana kumeisha. nafrahi anaposema rais wetu ni mpole na anachekacheka, basi kuchekacheka huko ndiko kunako tufikisha pabaya, hajui wapi pakucheka na wapi pakung'ata. namkumbusha bwana Mbade a k a Makamba kuwa Nyerere angekuwepo uchafu uliopo kwenye serikali hii usingekuwepo hata huyo makamba wenu asingekuwepo kwenye system. responce ya wananchi kwenye maandamano ni dalili za kuchoshwa na maisha ya matumaini. siku hizi kama hufahamiki au kuwa mtoto wa kiongozi hupati nafasi babu, angalia watoto wa viongozi ndio wanaoshika nafasi za juu ndio maana tuna kata tamaa, juzi nilikuwa naangalia bunge kuna Vita kawawa Mbunge wa kuchaguliwa, dada yake ni mbunge wa viti maalamu, wewe mwenzangu na mimi unambiwa hubiri amani!!! kama sijashiba nitahubiri vipi amani!!!
Quote

+1 #103 anna 2011-03-01 12:08 mimi kwa upeo wangi nadhani imefika wakati sasa wa kiongozi kuu wa nchi/seriali kuschukua hatua madhubuti kwa watendaji wake wasio wakweli/wasiowaaminifu/wenye kutuhumuiwa na kashfa mbali mbali zinazogusa maslahi ya umma ili kubaki na viongoz waadilifu na wenye kujali maslahi ya wananchi wote hasa walala hoi.wakati hilo likiendelea kiongozi mkuu/serikali ni lazima iseme sasa ni hatua gani wanachukua ili matatizo yanayoikabili nchi kama kupanda kwa bei ya vyakula,mgao wa umeme,ukosekana nji wa maji,elimu duni,kupanda kwa nauli za daladala na mabasi ya mikoani yaweze kutatuliwa kwa haraka kwa sababu kipato cha mtanzania wa sasa hasa wa hali ya chini ni majonzi jamani pia wale waliopo kazini mshahara kupanda ni siasa tupu.sasa kama mtanzania Mungu amemjalia pumzi ya leo kinachofuata anawaza hii leo itapiota vipi kuanzia asubuhi mpaka anapolala yaani utakuta hata mlo mmoja kwa siku ni shida!!!!na hapo hapo ndani ya nchi hiyo hiyo wapo wengine ambao kazi yao ni kuchota au kutumia vibaya pesa za walipa kodi kama wanavyoripo[NEN O BAYA] mara kwa mara lakini hakuna kinachofanyika zaidi ya kulindana.Kiukweli hata kama mtu unawaheshimu sana wazazi wako lakini kama wanafanya ndivyo sivyo na hawasikilizi la mtu huwa inafika hatua waweza kuwachoka!!!ndi po tulipofika sasa yaani ndani ya nchi yetu wenyewe lakini kiukweli TUMECHOKA na siasa za ulaghai za kila siku kwamba Maisha yataboreshwa kivipi????au ndo kupanda gharama za maisha ndo uboreshaji mpya mliokuja nao????jamani jamani cheo ni dhamna ipo siku Mungu atawauliza mlitufanyia nini watanzania.Maana ugumu wa maisha unapelekea hata watanzania kukata tamaa ingwa viongozi wa dini wanajitahidi kutufariji ila kiukweli viongozi wetu acheni maneno ya majibishano kama kweny taarabu/mipasho bali fanyeni mambo ya msingi kutukomboa watanzania na janga hili la ugumu wa maisha.
Mwisho nawasihi watanzania wenzangu pamoja ugumu wa maisha tulionao naomba kwa imani zetu pia tuzidi kumuomba Mungu abadilishe mioyo ya hawa viongozi wetu iwe na hofu ya Mungu ndani yake ili wabadilike na kutenda yale yanayostahili kwa maslahi ya taifa.Kweli tuzidi kuomba Mungu.asanteni sana.

Quote

+2 #102 Mwanaharakati 2011-03-01 12:07 saa ya ukombozi inakaribia, chadema tusongembele. Tumechoka kufanywa [NENO BAYA] na utawala wa kifisadi wa ccm.
Quote

-1 #101 Kezilahabi 2011-03-01 12:06 Namuunga mkono Rahisi Kiwete...CHADEMA wabaya sana. Wameleta DOWANS/Richmond,wanawa linda mafisadi wamependisha ovyo bei ya mafuta na vyakula,walilip ua mabomu G'mboto, hawawalipi wafanyakazi mishahara vizuri, wamefungua sekondari za kufelisha maskini (za kata) na wameunda serikali kuubwa wasiyoweza kuiendesha! CHADEMA hawafai...tuwatoe madarakani. THAT'S WHAT UR FAKE PRESIDENT IS IMPLYING, LOL.
Quote

-4 #100 Zinklia 2011-03-01 12:05 Chadema siyo chama ila kikundi cha wachochezi mtauona mwisho wake!
Quote

+6 #99 Omar Ali 2011-03-01 11:53 Rais gani analalamika kila siku...raia tufanyeje?
Quote

12345678
Refresh comments list
 
Lowassa ashauri mishahara ya wafanyakazi ipande Send to a friend Monday, 28 February 2011 21:31 0diggsdigg

lowasakabisa.jpg
Mussa Juma, Arusha

WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, ameishauri Serikali kuunda tume ya kurekebisha mishahara ya watumishi wa umma ili iendane na hali ya maisha ya sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha jana, Lowassa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, alisema uchumi wa dunia sasa umeyumba na hivyo kusababisha vitu vingi kupanda bei.

Kwa mujibu wa Lowaasa, kuendelea kuwalipa wafanyakazi mishahara kwa viwango vya sasa ni kuwapunguzia ari ya kutekeleza wajibu wao kwa umma.

Lowassa alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), akitokea jijini Dar es Salaam.

Lowassa na Uchumi
Jana Lowassa ambaye katika mkutano huo alijikita zaidi kuzungumzia machafuko ya kidini yaliyotokea jimboni kwake Monduli katika mji wa Mto wa Mbu, ni muhimu sasa, wafanyakazi wa umma wakapata mishahara itakayokidhi gharama za maisha.

"Hali ya uchumi duniani sio nzuri na inasababisha vitu vingi kupanda bei kama mafuta na nafaka hali ambayo imetokea nchi zilizoendelea na hivyo kuathiri hadi nchi nyingine ikiwapo Tanzania,"alisema Lowassa.

Alisema machafuko yanayoendelea nchini Libya na kulipuliwa kwa visima nchini Iraq yamesababisha kupanda kwa kiasi kikubwa kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.

Lowassa aliendelea kueleza kuwa kama Serikali ikiunda tume ya kupitia upya mishahara ya wafanyakazi, inapaswa kushirikisha viongozi wa vyama vya wafanyakazi, wataalamu wa uchumi na wadau wengine.

"Licha ya kuunda tume pia Serikali nashauri wataalam wa uchumi kutazama Bajeti ya Serikali ili kuona vitu gani vinaweza kupunguzwa bila kuathiri utendaji wa Serikali,"alisema Lowassa.

Lowassa pia alizungumzia mfumko wa bei wa vitu mbalimbali ikiwamo sukari na kueleza kuwa yote hayo yanasababishwa na kuyumba kwa uchumi wa dunia na sio tatizo la Tanzania pekee.

Vurugu za kidini
Akizungumzia vurugu za kidini zilizoibuka Mto wa Mbu hivi karibuni na kusababisha watu 12 kujeruhiwa na mali kadhaa kuharibiwa, Lowassa aliwataka wakazi wa mji huo kutulia na kuendeleza uhusiano mwema baina yao .

"Pale Mto wa Mbu kuna makabila zaidi ya 120 na muda mrefu wanakaa kwa amani hivyo kwa tukio hili naomba maelewano yaendelee kuwepo,"alisema Lowassa.

Lowassa pia aliviomba vyombo vya habari kuwa makini na migogoro ya kidini ili visije vikachochea hasa kwa kusema dini fulani ni sahihi na nyingine sio sahihi.

Katika siku za hivi karibuni vyama vya wafanyakazi vimekuwa vikiomba Serikali kupandisha mishahara hasa kutokana na kupanda wa gharama za maisha, ikiwepo bei za vyakula, usafiri na mahitaji mengine.

Msimamo wa Tucta
Kauli ya kiongozi huyo, Mbunge wa Monduli (CCM), imekuja wakati kukiwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Tucta), likiendelea kuibana Serikali kuhusu suala la maslahi ya wafanyakazi.

Uhusiano baina ya Tucta na Serikali ya Awamu ya Nne umezorota kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa kutokana na kile kinachodaiwa na wafanyakazi kuwa ni Serikali kutotekeleza ahadi za kuboresha maslahi yao kwa muda mrefu.

Desemba 8, mwaka jana, Tucta baada ya kimya cha muda mrefu, walitangaza rasmi kuanza tena kwa mgogoro baina yao na Serikali wakiishinikiza iongeze mishahara ya wafanyakazi kuanzia Januari mwaka huu.

Ombi la wafanyakazi kupitia Tucta ni kutaka kima cha chini cha mshahara kuongezwa hadi kufikia Sh315,000/- kwa mwezi, kiwango ambacho Rais Jakaya Kikwete alishasema "hakiwezekani" na kwamba Serikali haina uwezo wa kulipa fedha nyingi kiasi hicho.

Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Nocolaus Mgaya, ndiye amekuwa kinara wa wafanyakazi nchini katika kudai maslahi bora zaidi, hali ambayo ilisababisha Rais Kikwete Mei 4, 2010 'kuwatisha', pale walipotaka kuandaa mgomo wa nchi nzima uliokuwa ufanyike Mei 5, mwaka huo.

Mvutano huo ulisababisha wafanyakazi kupitia Tucta kutangaza msimamo kwamba wasingempa kura mgombea yeyote wa kiti cha urais "asiyejali masilahi yao au yule aliyezikataa kura zao".
Hata hivyo, baadaye wakati akizindua kampeini za kitaifa za CCM akiwania kurejea tena Ikulu, Agosti 21, 2010 katika Viwanja vya Jangwani, Kikwete alisema Serikali ilikuwa imepandisha mishahara ingawa si kwa kiwango cha walichotaka Tucta.

Msimamo wa Tucta ni kwamba kima cha chini cha mishahara ya wafanyakazi kilichoongezwa kutoka Sh 104,000 hadi Sh 135,000 kwa mwezi ni kidogo na kwamba hakuna uwiano mzuri baina ya watumishi wa kada za chini na wale wa ngazi za juu kama makatibu wakuu wa wizara na wakurugenzi wa vitengo mbalimbali serikalini.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Comments

12

#22 eric 2011-03-01 12:32 haki ya mungu rudisha kwanza hela zetu alafu ndo uanze kutaka umarufu
Quote

0 #21 mekaki 2011-03-01 12:29 ujue...lowasa anaonyesha mfano mbaya wa viongozui ambao wanajifanya kuona mabaya kwa sabababu wanataka kuwashawishi wananchi .ni sawa na wabunge ambao hurudi majimbonii kwao au kwa wananchi baada ya kujua karibu uchaguzi unakaruibia na hapo hupretend kuwapa vimisaada aua kuongea vizueiii

ng'o?

Quote

0 #20 dibania 2011-03-01 12:25 ila mbona nyie viongozi mnazidi kujilimbikizia mali
Quote

+1 #19 Mzawa 2011-03-01 12:10 Kuongeza mshahara sio sababu hatutaki kufikia hela ya Zimbabwe unakwenda dukani na kiroba cha manote.

Tunataka uchumi na maisha ya mtanzania yaboreshwe. Ungekuwa mshauri mzuri kwa swahiba wako ungemshauri kila wizara inaposikia kitu tofauti na wananchi wafuatilie na kutoa jibu kabla ya kuwa sumu kwa watanzania.

Mfano huko madukani kunakera kabisa. Kwa sasa hivi unajua bei ya gunia la mkaa acha hilo nondo ni bei gani. Kwahio hata akipapandisha mshahara ya bei inapanda.
Mshahara upande lakini vitu vipungue bei kutokana na hali ya maisha ya mtanzania.

Lakini haya mambo ya kuongozwa kama mapimbi tumechoka. Kama mtu hawezi kazi na kutoa majibu ya kuridhisha inamaana kila mtu atajiongozea anavyotaka.

Quote

0 #18 mume mwema 2011-03-01 11:28 naomba papaa sendeka atoe maoni yakesababu anamjua sana lowasa jamani tusije danganywa na lowasa sababu ametufadhaisha sana ametusikitisha na ametufedhehesha sana kama ni gia ya urais melamba dume ana hasira na huenda akaja kujiuzulu tena sendeka umemsoma lowasaaaaaaaaaa aaa
Quote

+2 #17 mtakahaki bahati 2011-03-01 11:14 weeeeeeeeeee! mzee ogopa nguvu ya umma na kauli zako hizo za unafiki wa kutafuta umaruufu wewe ni mchafu sana kwa umma wa tz kama kweli richard monduli (richmond )inakuhusu basi tafuta kioo ujione livyo mchafu kwa tz,tawala pesa ulizo fisadi lakini sio tanzania, na mungu akupe uhai ili siku moja uje urudishe ulichofisadi na kundi lako.mishahara sio ishu.bali kubolesha uchumi na upatikanji wa huduma/vitu muhimu kwa wa tz wote
Quote

-2 #16 ASAK 2011-03-01 10:57 LOWASSA HAPO UMENENA.ILA MSHAURI SWAHIBA WAKO KWANI HAJUI AFANYALO.
Quote

+1 #15 mimi 2011-03-01 10:51 Huna hata aibu haya yote si umeyasababbisha mwenyewe isingekuwa Richmond leo hii TANESCO wangekuwa ICU? Umeme juu maisha juu! kipi kisichojulikana unataka tume ianze kuchunguza sukari imepanda kiasi gani?
Wewe ndio wa kuinyoshea kidole serikali kweli? Wewe ulikuwa WM tumepigika mpaka sole za viatu vikaenda upande

Quote

+1 #14 Mdaho Gwalihenzi 2011-03-01 10:22 Mheshimiwa sana Lowasa,naomba usitumie vyombo vya habari kujitakasa. Nenda kwa swahiba wako mkubwa J.K. atakusikiliza na kutekeleza ushauri wako. Mbona maengine hayakutangazwa na alitekeleza!
Quote

+1 #13 NOMA 2011-03-01 10:16 Asalaleeeeh,

WEWE MZEE WA RICHMOND? siamini, nawaagiza mkimuona popote pigeni mawe angalau gari lake! baada ya kututesa sasa anapandia migongo yetu wafanyakazi tuliochoka na pilikazao za kutafuta pesa, CHADEMA itisha maandamano nchi nzima tumalize kesi na Mafisadi tena sasa watafute pa kwenda maana wakitoka watakuta Gadafi naye kwaheri

Quote

+1 #12 kelvin shitindi 2011-03-01 10:11 Ni kweli unachozungumza ila kwangu naona haina maana kwa sababu ukiongeza mishahara na hali vitu vinazidi kupanda itakua haina maana ni sawa na kumpa mtu shilingi 4000 alafu akatumia shilingi 2000 na kubakia na shilingi 2000 na alafu ukamuongezea na kumpa shilingi 8000 na akaja aakatumia shilingi 6000 je utakua umemsaidia au umemdanganya mtanzania ? cha msingi ni kuwapunguzia tax wafanyakazi au kuwafutia kabisa tax alafu kupunguza vat hilo ndo muhimu acha siasa zako za kutudanganya,
Quote

0 #11 Brigedia General 2011-03-01 09:43 2015*
Quote

+1 #10 Brigedia General 2011-03-01 09:41 Kila mtu anajau mishahara ni midogo inabidi iongezwe. Lakini kinachokuongele sha hapa Lowassa ni kuwania urais 2011. Ni ufisadi na tamaa yako wewe na mafisadi wenzako ndiyo yametufikisha hapa tulipo.
Quote

+1 #9 ahmad suleman 2011-03-01 09:37 Acha kutudanganya. ushauri wako utakuwa wa maana ukiweza kutujibu ulitekeleza vipi maoni ya Tume ya Ntukamazina ya kurekebisha mishahara wakati ukiwa Waziri Mkuu. Unatafuta namna ya utokeje baada ya kuona hukubaliki na wananchi pamoja na CCM yenu.
Quote

+3 #8 Mwanchi Mwadilifu 2011-03-01 09:06 We na timu yako ndio mliotufikisha hapa, kwa ajili ya tamaa ya mali, umetuingiza kwenye Richmond huku ukijilipa mamilioni kwa siku bila hata ya umeme kuzalisha na uchumi ukizidi kudolola, leo unasema mishahara ipande c uongo uo kama mlivyozoa kutunganya kwanza pesa mnayo? au ndio unajiwekea mazingira ya kugombea 2015! hautapata kitu mzee bora upumzike ule pension yako ya kfisadi
Quote

12
 
Back
Top Bottom