Lunyungu apata ajali

Naungana na nyie wadau wote kumpa pole Lunyungu.Nimepata nafasi ya kuteta naye kama alivyo fanya Mzee Jasusi .Lunyungu alikuwa ndani ya mbuga ya Saadan na mwendo wa km 90 kwa saa .Alikuwa na gari aina ya Range Rover Vogue basi ghafla ikafunguka boneti na akapoteza control.Walikuwa ni watu 2 pekee ndani ya gari akitokea Bukoba kupitia Arusha maana alikuwa Biharamulo kuona yanayo tokea huko .

Anasema gari liligonga daraja na kushuka porini katika shimo kubwa likapinduka miguu juu.Ndipo wananchi wa Lugoba wakaanza kupora na kuchukua vitu kama saa , radio ya gari ,na vifaa kadhaa vya gari .

Lunyungu anaumwa bega sasa la kushoto na alipata majeraha kidogo mkono wa kulia na kichwani.Anasema anaikosa sana JF na anawapa shukrani wote sisi kwa kumuombea.anasema namba zake ni

0784 220011 anapatikana hapo .

Tunamuombea kila jambo jema.

Shukran kwa taarifa hii Mkuu Mugishangwe.
 
Mkuu tuko pamoja nawe, tunakutakia kheri upone haraka tuendeleze hili libeneke
 
Pole Lunyungu na ugua pole. Ahsante Max. Dua na maombi yetu yatakuwa na ndugu na jamaa wa Linyungu
 
Pole sana Kamanda, tuko wote katika maombi upate nafuu haraka tuendeleze mapambano.
 
Ndugu wana JF
Nimepokea salam zenu za heri kabisa .Jamani nimepona na Mungu ni mwema sana .Niko hai .Najiandaa kurudi Kagera kweney uchaguzi siku chache zijazo .Nimeona makubwa na kweli Mungu mwacheni aitwe Mungu .Ninawashukuru sana sana wana JF .Nina endelea vyema ila nilishikwa na tetemeko kubwa sana moyoni na mwili mzima .
 
Ndugu wana JF
Nina endelea vyema ila nilishikwa na tetemeko kubwa sana moyoni na mwili mzima .

Pole sana mkuu....!

BWT: Madaktari wamekuhakikishia kuwa hilo TETEMEKO halikuacha nyufa sehemu yoyote ya mwili ambazo usipozithibiti kwa sasa zinaweza kukuleta maafa baadaye?
 
Back
Top Bottom