Lunyungu apata ajali

Pole sana ndugu,tuna mshukuru Mungu kwa kukunusuru na ajali mbaya,nakuombea upone majeraha uliyoyapata........Jamani tuwe waangalifu sana kwenye bara bara zetu hizi,ajali zimekuwa nyingi sana wakati huu na watu wengi wamepoteza maisha.
 
Last edited:
Tunamshukuru Mungu kwa kukunusuru. Pole sana Lunyungu. Pamoja na kutokupata majeraha mengi, unahitajika kufanyiwa uchunguzi wa kina.
 
Wishing you speed recovery bro. God is with you. Update us on ur condition
 
Pole sana mkuuu , Mungu atakuafu na kukupunguzia maumivu na hayo majeraha yapone haraka Inshaallah
 
Pole kaka Lunyungu, Mungu atakurehemu upate nafuu na kupona kabisa. mlio karibu muendelee kutupatia maendeleo yake.
 
Pole sana mkuu Lunyngu. Tunashukuru uhai unao na umeweza kutarifu yaliyokusibu kupitia kwa Maxence. Uwe na afya tele with speeeeeedy recovery.
 
Naungana na nyie wadau wote kumpa pole Lunyungu.Nimepata nafasi ya kuteta naye kama alivyo fanya Mzee Jasusi .Lunyungu alikuwa ndani ya mbuga ya Saadan na mwendo wa km 90 kwa saa .Alikuwa na gari aina ya Range Rover Vogue basi ghafla ikafunguka boneti na akapoteza control.Walikuwa ni watu 2 pekee ndani ya gari akitokea Bukoba kupitia Arusha maana alikuwa Biharamulo kuona yanayo tokea huko .

Anasema gari liligonga daraja na kushuka porini katika shimo kubwa likapinduka miguu juu.Ndipo wananchi wa Lugoba wakaanza kupora na kuchukua vitu kama saa , radio ya gari ,na vifaa kadhaa vya gari .

Lunyungu anaumwa bega sasa la kushoto na alipata majeraha kidogo mkono wa kulia na kichwani.Anasema anaikosa sana JF na anawapa shukrani wote sisi kwa kumuombea.anasema namba zake ni

0784 220011 anapatikana hapo .

Tunamuombea kila jambo jema.
 
Pole kaka Lunyungu, Mungu atakurehemu upate nafuu na kupona kabisa. mlio karibu muendelee kutupatia maendeleo yake.

...Mungu amrehemu? mnh, kiswahili hiki 'kinatisha'
 
Back
Top Bottom