Mnatoa wapi ujasiri wa kupiga watu picha wakipata majanga badala ya kuwasaidia?

Loading failed

JF-Expert Member
Sep 14, 2023
1,946
5,852
Ndugu wana Jf , ndugu zangu wa MMU na wasio na upande wowote.

Ni kweli kuna utandawazi ila sio kuondoa utu wetu kama binadamu, ndugu zangu kuna tabia mbaya sana imeibuka miongoni mwa sisi binadamu, inatokea binadamu mwenzako kwa jinsia yake kapata matatizo badala ya kutoa msaada watu wanabaki wakishangaa makundi kwa makundi huku wanapiga picha na kuwarekodi waathiriwa jinsi wanavyoteseka kwenye majanga.

Ndugu inasikitisha sana binadamu mwenzako anapata ajali inaweza ikawa ya gari , treni, ndege, pikipiki, baiskeli au ajali ya kwenda kwa miguu kwa aina zake alafu mtu anatoa simu yake na kuanza kupiga picha na wengine wanarekodi kabisa huku wamewasha flash light.

Inasikitisha sana mtu ana angukiwa na ukuta, mti, gari, au kitu kizito chochote, au ana ungua moto au ana zama kwenye maji alafu watu wanakodoa macho kupiga picha pamoja na kunong'onezana wao kwa wao.

Binadamu utu wetu ume kwenda wapi, ni ujasiri upi unao wenye chuki mbaya ambao unashindwa kutoa msaada bali unaona bora utoe simu yako na kuanza kupiga picha au kuwarekodi waliopata maafa.

Inasikitisha mwenzako kapata tabu au kafariki au anavuja damu alafu badala mumsitiri na kumpatia huduma ya kwanza mnaanza kupiga picha.

Mbaya kabisa mtu mwingine anajiselfia kabisa eneo la tukio ili aonekane na yeye alikuepo je ni sawa ni halali . Ubinadamu wetu upo wapi na wauliza.

Sawa hatukatai upendo wa wengi utapoa wakati huu hatari na katika kizazi hiki cha nyoka ila utu wetu uko wapi. Mwingine unakuta ana gombana na mkewe wanavutana , wanapigana na wakati mwingine mpaka kuvuana nguo na kuachana uchi ila badala ya kuwapatanisha na kuwasitiri watu mnarekodi jinsi walivyo uchi na wanavyopigana ili mkaziposti wapi na wauliza?

Upendo na hofu ya Mungu tunaye mwamini na nyie msio amini ipo wapi, utu wetu kama wanadamu upo wapi na wauliza?

Ndugu haiwezekani mbaya kabisa unakuta mtoto mdogo ana adhibiwa vibaya sana na watu wanao mzunguka katika jamii zetu , anaumia na analia kwa uchungu kuomba msaada ila badala msaidie mnampiga picha na wakati mwingine kumrekodi kabisa. Kwa kweli ina huzunisha sana.

Ndugu zangu huo ujasiri wa kutoa simu zenu na kupiga picha, kuwarekodi na hata kupost mitandaoni mnautoa wapi , kwa nini huo muda wakutoa simu yako na kuanza kurekodi ,kupiga picha usiutumie kutoa msaada kwa aliyeathiriwa na ajali au majanga yaliyo mbele yake.

Najua na ongea na watu , najua wengi wetu mna husika hapa ila badilikeni kuweni na utu sisi ni binadamu na hapa duniani tunapita.

Nyie ambao hamuhusiki kwa namna yeyote tumieni muda huu kuwaeleza hao wanaopiga watu picha na kuwarekodi katika majanga mbali mbali ili hali wapo tuu na hawatoi msaada wowote.

ONYO: MAJANGA MENGINE NI HATARI KWA WASAIDIZI , SIYO LAZIMA UTOE MSAADA KWA KUMSHIKA MUATHIRIWA MENGINE YANAHITAJI UPELELEZI NA UKIJICHANGANYA UTAJIBEBEA KESI/ MAGONJWA . TOA MSAADA HATA KWA NAMNA YA KUPELEKA TAARIFA KATIKA VITUO VYA POLISI AU SERIKALI ZA MITAA NA SIYO UKAE PALE UNAPIGA PICHA NA UMBEA HOVYO HOVYO HUKU MUATHIRIWA AKIENDELEA KUTESEKA /KUDHALILIKA UTU WAKE , KAMA KAFA AU YUPO UCHI MFUNIKENI BILA KUMSHIKA
 
Kizazi hiki kinaitwa kizazi Cha picha na video. Ovyo kweli kweli ,tabia mbaya sana ila hatuna la kufanya tunavumilia tu
 
Kuna wale wenye ujasiri wa kuibia wanaopatwa na matatizo kama Ajali sijui huo ujasiri huwa wanaupata wapi.
 
Wengine wanavyosaidia sisi tunakuwa tunafanya coverage ya matukio
 
Back
Top Bottom